Search This Blog

Saturday, November 23, 2013

RAGE AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA NDANI YA SIKU 14


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.

 

Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

 

TFF itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.

 

JAMAL MALINZI ATANGAZA KAMATI NDOGONDOGO MPYA ZA TFF


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.

 

Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.

 

Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.

 

Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.

 

Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.

 

Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.

 

Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.

 

Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.

 

Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.

 

Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.

 

Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.

 


RIBERY: CRISTIANO ANASTAHILI TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA -

Nyota wa Bayern Munich Franck Ribery amesema kwamba yeye pamoja na  Cristiano Ronaldo wote wanastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia -  2013 Ballon d'Or.

Wawili hao ndio wanapewa sana nafasi ya kutwaa tuzo hiyo mbele ya Lionel Messi, ambaye ameshinda mara nne mfululizo tuzo hiyo. 

Ribery amezungumza namna anavyoheshimu kipaji cha Ronaldo, lakini anahisi mafanikio yake ya msimu uliopita na klabu yake ya Bayern yanaweza kumfanya amfunike mreno huyo.

"Wote tunajua kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri sana. Kiuhalisia kabisa anastahili kutwaa tuzo hii," mfaransa huyo aliiambia Kicker.

"Japokuwa, kura zinaangalia ulichokifanya ndani ya mwaka mzima na mie nimefanya vizuri. Watu wataangalia chaguo sahihi, sina wasiwasi kabisa."

ADEN RAGE AHIRISHA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI MPAKA KESHO

Baada ya kurejea kwa mbwembwe jana na kusisitiza yeye bado ndio mwenyekiti halali wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage leo aliitisha mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo Kariakoo msimbazi, lakini katika hali ya kushangaza Rage ameiharisha mkutano huo.

Waandishi wa habari wakiwa tayari wanawasili msimbazi ikatoka taarifa kwamba mwenyekiti huyo aliyesimamishwa na kamati ya utendaji mapema wiki hii hatoweza kukutana leo kwa kuwa anaenda kukutana na uongozi wa TFF na kwahiyo mkutano wake na waandishi wa habari atafanya kesho Jumapili.

Msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kimwaga muda mfupi uliopita kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook alitoa taarifa rasmi juu ya kuhairishwa kwa mkutano huo mpaka kesho.

PICHA YA SIKU: JASIRI HAACHI ASILI.


LEO TP MAZEMBE DHIDI YA SFAXIEN KWENYE FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO.









Friday, November 22, 2013

BAYERN MUNICH VS DORTMUND: KLASSIKER YA KWANZA YA MSIMU HUU WA BUNDESLIGA - DORTMUND WAKIWA NA HALI MBAYA YA MAJERUHI


Inaweza kuwa haina ukubwa wa El Clasico ya Spain, lakini katika miaka ya hivi karibuni Borussia Dortmund na Bayern Munich wamejenga upinzani mkubwa unaoifanya mechi baina yao iwe miongoni mwa mechi 'classics'. Hivi sasa mechi hiyo imepewa jina  Bundesliga Klassiker, na jumamosi hii itakuwa ndio klassiker ya kwanza itakapochukua nafasi.

Japokuwa ni bado kabisa mwanzoni mwa msimu mpya, lakini matokeo ya mechi hii yatatokea muelekeo wa ubingwa utaelekea wapi msimu huu, ubingwa ambao Bayern waliuchukua kutoka kwa Dortmund msimu uliopita. 

Baada ya Jupp Heynckes kuiongoza Bayern kushinda makombe matatu msimu uliopita, Pep Guardiola tayari ameanza vizuri.  The Bavarians wamedondosha pointi 4 tu kutoka katika michezo yao 12 na tayari wanaongoza ligi kwa pointi nne mbele ya Dortmund na  Bayer Leverkusen.

Bayern chini Guardiola pia wana rekodi nzuri. Chini ya filosofia za Pep ina maana sasa Bayern wana uwezo wa kumiliki mpira zaidi huku wakifanya 'pressing' kama msimu uliopita, mbinu ambayo Dortmund wanaimudu pia.

Kitu kingine cha kuvutia kuhusu kuanza vizuri kwa Guardiola ni kwamba amekuwa akiandamwa na majeruhi katika kikosi chake , hasa kwenye kiungo. Thiago Alcantara, Bastian Schweinsteiger, Javi Martinez na Mario Gotze wote wamekuwa wakikosekana kwenye mechi za msimu huu, lakini Guardiola aliweza kuimudu hali hiyo vizuri sana. Uamuzi wa kumhamisha kutoka beki wa kulia Philipp Lahm mpaka kwenye kiungo umeonyesha kuwa na mafanikio jambo ambalo lilipelekea hata kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low kumtumia kwenye eneo hilo wiki iliyopita. 


Wakati Thiago, Martinez na Gotze wakiwa wamerudi kwenye uzima, Schweinsteiger kwa mara nyingine atakosekana kwenye mechi ya kesho na ataungana na majeruhi wengine kama Frank Ribery aliyeumia kwenye mechi ya kugombea kufuzu michuano ya kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa. Kutokuwepo kwake kunaongeza nafasi ya kuanza kwenye mechi itakayochezwa kwenye dimba la timu ambayo imemtambulisha vizuri kwenye ulimwengu wa soka.

Kuondoka kwa Gotze Dortmund kunaonyesha wazi pengo la rasimali baina ya vilabu hivi vikubwa viwili, jambo ambalo linaonyesha wazi ukubwa wa mafanikio ya timu hiyo nyumbani na ulaya katika miaka ya hivi karibuni.  Jurgen Klopp anakutana na changamoto kubwa ya kuendelea kuiongoza kwa mafanikio klabu hiyo kama msimu uliopita. Kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri, mpaka katika michezo miwili iliyopita walipofungwa na Arsenal nyumbani na kuweka hatma yao katika Champions league kuwa shakani kabla ya kufungwa na Wolfsburg jambo ambalo linamaanisha itabidi waepuke kufungwa jumamosi ikiwa wantaka kubakia kuwa washindani wa ubingwa wa Bundesliga.

Kama ilivyo kwa Bayern, Dortmund wamekuwa wakiandamwa na matatizo ya majeruhi msimu huu, lakini tofauti na wapinzani wao, wenyewe wanakosa kikosi imara bila kuwa na wachezaji wanaowategemea. Kiungo wao tegemezi Ilkay Gundogan amecheza mechi moja tu msimu huu kutokana na majeruhi, pia kwa bahati mbaya zaidi katika mechi dhidi ya Bayern Jurgen Klopp itabidi apange kikosi ambacho kitakuwa hakina mchezaji hata mmoja wa kikosi cha kwanza katika safu ya ulinzi.

Lukasz Piszczek bado hajacheza kabisa msimu huu, wakati beki wa kati Neven Subotic amepata tatizo la goti katika mchezo dhidi ya Wolfsburg. Kama hilo halitoshi, wote wawili Mats Hummels na Marcel Schmelzer wakaumia katika mechi za kimataifa wiki hii mwanzoni. Beki mkongwe wa kijerumani Manuel Friedrich amechukuliwa kwa mkopo wa muda mfupi na anaweza kuanza kwenye mechi ya kesho.

Dhidi ya safu kali na bora ya ushambuliaji ya Bayern, itawahitaji kuwepo kwa juhudi kubwa zaidi kutoka kwenye safu ya ulinzi ya  Dortmund ili kutoka japo na sare kwenye mchezo huo. Dortmund walishinda kwenye mechi yao ya kwanza waliyokutana msimu huu katika  German Super Cup, lakini hiyo ilikuwa wakati Guardiola alipokuwa akitafuta baance ya timu. Ni vigumu kuona matokeo yanayofanan jumamosi ya kesho na Bayern wanaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kwenye ubingwa wa Bundesliga.

BAADA YA SOKA GIGGS NA GARY NEVILLE WAFUNGUA MGAHAWA WA VYAKULA


Fry-up: Gary Neville and Ryan Giggs cooked off with chefs Brendan Fyldes (left) and Martin Wignall (right)

Katika kuelekea ufunguzi wa mgahawa wao magwiji wa soka wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs na Gary Neville jana waliingia kwenye mashindano ya kupika misosi.

Giggs na Neville kwa pamoja jana walishiriki kwenye mashindano hayo yaliyofanyika maeneo ya Westfield Stratford City shopping centre jijini London ikiwa ni moja ya shamrashamra ya ufunguzi wa mgawaha wao wa Cafe Football.

Wawili hao walishindana na mpishi mkuu wa mgahawa huo, Brendan Fyldes pamoja na mpishi wa Michelin chef Michael Wignall.


Giggs na mwenzie walipika vyakula vikuu vitatu ambavyo vitakavyokuwa vikipatikana hapo vikiwemo Nev's Noodle Pot, Wignall's Halftime Orange na Chocolate Pistachio Turf.
Neville alisema: 'Shindano hili lilikuwa nafasi nzuri kwa wanunuzi Westfield Stratford City kuona nini tumewaandalia kwenye Cafe Football.
'Mapishi matatu tuliyopika ni mfano tu uzuri wa vyakula ambavyo vitakuwa vikipatikana Cafe Football.
Re-United: Giggs (right) and Neville say the cafe is focused on quality food with a nod to sport

Having a laugh: The restaurant will open its doors to the public next month


Mgahawa huo utafunguliwa rasmi mwezi ujao. 
Partnership: Giggs and Neville were team-mates at United from 1992 until Neville's retirement in 2011


RONALDO: NATAKA KUMALIZIA SOKA LANGU BERNABEU - SINA UHAKIKA KAMA NITAHUDHURIA SHEREHE ZA BALLON d'OR"

Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba hana nia ya kuondoka Real Madrid, akikiri kwamba anafikiria kumaliza maisha yake ya soka ndani ya Santiago Bernabeu.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ambaye alihusishwa sana na kurudi Manchester United mapema mwaka huu, baada ya kusema kwamba hana furaha ndani ya mji mkuu wa Spain, lakini mwishowe akaamua kusaini mkataba mpya utakaomfanya abaki na  Los Blancos mpaka June 2018.

Ronaldo hajutii uamuzi wa kusaini mkataba mpya, akielezea hana mpango kabisa wa kuondoka Madrid.

"Hivi sasa, nahisi nahitaji kumalizia maisha yangu ya soka hapa kwa sababu nina furaha sana," alisema nahodha wa Ureno.

"Napenda kuishi jijini Madrid, kuichezea klabu bora ulimwenguni na sina lingine nilitakalo. Mambo yanapokuwa mazuri, unapokuwa umetulia na kupewa hamasa ya kufanya vizuri zaidi, unakuwa hauna wasiwasi na kitakachotokea mbele.
"Nathaminiwa na kupendwa hapa. Huu ni msimu wangu wa tano hapa. Mwanzoni nilijiona kama sikuwa na nafasi kubwa mioyoni mwa mashabiki, lakini nikagundua kwamba inawezekana ilikuwa mimi ndio ambaye sikuwa sawa. 

"Sasa hivi nina furaha kwa asilimia 100. Ni kama vile ndoto kwenda Bernabeu kila siku, watu wananipenda sana. Nataka kuwa hapa kwa miaka mingi ijayo na kuumaliza mkataba wangu, hakuna klabu nyingine kama Madrid."

Ronaldo ameichezea Madrid katika mechi rasmi 200 tangu alipojiunga nayo akitokea United mwaka  2009.

Wakati huo huo mshambuliaji huyo amesema kwamba haipi sana kipaumbele tuzo ya Ballon d'Or na hajaamua kama atahudhuria sherehe za utoaji tuzo hizo.

"Sikirii sana kuhusu Ballon d'Or. Sijajua kama nitahudhuria sherehe za utoaji tuzo hiyo - sina wazimu juu ya jambo hilo."

ZIDAN APIGWA NYUNDO YA MIAKA SITA JELA


Mahakama moja nchini Misri imemuadhibu mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya taifa hilo Mohamed Zidan kwenda jela kwa miaka sita baada ya kumkuta na hatia ya kutoa cheki tatu mbovu kwenye kampuni ya real estate.

Kampuni ya hiyo (Arab Company for Projects and Urban Development) ilifungua mashtaka dhidi ya Zidan, mapema mwaka huu.

Mwanasoka huyo, 31, amekuwa nje ya dimba tangu alipoondoka katika klabu ya Baniyas iliyopo huko UAE mwezi January mwaka huu. Zidan ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi katika TV ya Al-Jazeera Sports kama mchambuzi, ingawa bado hajatangaza kustaafu kabisa soka.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Dortmund na Werde Bremen hakuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo ikitolewa.

Thursday, November 21, 2013

RONALDO'S INCREDIBLE NUMBERS...


KUTANA NA KIJANA CLAUDIO GABRIEL

MTANGAZAJI ATIMIZA AHADI YAKE YA KUTANGAZA HABARI UCHI.



Mwanadada Doria Tillier ametekeleza ahadi yake ya kutangaza taarifa ya habari ya hali ya hewa kwenye kituo kimoja cha Televisheni akiwa uchi.
Mwanadada huyo alitoa ahadi kama Ufaransa itafanikiwa kurudisha mabao 2 waliyokuwa wamefungwa na Ukraine kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za kombe la Dunia basi angetangaza taarifa ya habari akiwa kwenye hali ya utupu.
Kwenye mchezo wa marudiano Ufaransa ilifanikiwa kuitandika Ukraine mabao 3-0 na kufanikiwa kukata tiketi ya kwenda Brazil mwakani.

MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUCHUANA NANI MTANI JEMBE DODOMA, MUSOMA NA SINGIDA

Na Mwandishi Wetu

Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe itaendelea kuunguruma tena Jumapili wiki hii na kuwapa nafasi mashabiki wa Simba na Yanga walioko Dodoma, Musoma na Singida na kuchuana vikali katika michezo mbalimbali huku wakihakikisha timu zao zinaibuka na kitita cha shilingi milioni mia moja zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya Watani wa Jadi kupitia kampeni hiyo.

Mratibu wa mabonanza hayo, Lawrence Andrew amesema jijini Dar es salaam jana kwamba mashabiki watapata fursa ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama vile foosball, kuvutana kamba, soka la wachezaji saba kila upande maarufu kama “Seven aside” na kuongeza kuwa ili kuhakikisha mashabiki hao wanafurahia ipasavyo burudani mbalimbali za muziki zitakuwepo pamoja na Nyama choma.
Andrew alisema kuwa katika mji wa mji wa Dodoma bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika uwanja wa shule ya Dodoma Sekondari ambapo bendi maarufu ya The TNC Band itatumbuiza. Na huko Musoma bonanza litafanyika katika uwanja wa Mukonde na kupambwa na bendi ya Musoma Stars huku mkoani Singida likifanyika katika Uwanja wa Namfua na burudani kabambe ikishushwa na Wana Pamba Music Band aka Watoto wa Mujini bendi ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mkoani humo.

Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia Nani Mtani Jembe. Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.

Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.

Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.

Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.

Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu siku ambayo watani wa jadi Simba na Yanga watacheza mechi ya kuhitimisha kampeni hiyo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

KASEJA APIGWA CHINI KIKOSI CHA STARS CHALLENJI: IVO, DILUNGA, KIMWAGA, SAMATA NA ULIMWENGU NDANI

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.

Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.   

MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.


FIFA YABADILISHA TAREHE YA KUPIGA KURA ZA KUMCHAGUA MCHEZAJI BORA WA DUNIA - RONALDO SASA ANA NAFASI KUBWA MBELE YA RIBERY NA MESSI

Cristiano Ronaldo sasa yupo katka nafasi nzuri ya kutwaa tuzo yake ya pili ya Ballon d’Or baada ya kufunga mabao matatu yaliyoipeleka Ureno kombe la dunia 2014.

Kwa mujibu wa Sporting Life, Ronaldo amemuondoa  Franck Ribery katika kilele cha listi ya wachezaji waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo.

Pia imeripotiwa kwamba shirikisho la soka duniani FIFA limeongeza muda wa kupiga kura za kumchagua mshindi wa 2013 Ballon d’Or. 
Uamuzi wa FIFA kuruhusu makocha na manahodha pamoja na waandishi kuwasilisha majina matatu ya Top 3 kabla ya Nov. 29 tofauti na mwanzo ilivyokuwa Nov. 15, limeleta maswali mengi kutoka kwa wadau wa soka kama ilivyoripotiwa na ESPN FC

Kwa mujibu wa makala moja  iliyoandikwa kwenye ESPN FC ,  Francesc Aguilar aliandika kwenye mtandao wa:
Sina maneno tena. FIFA na wameongeza muda wa kupiga kura mpaka Nov. 29 2013. Mara ya kwanza viwango vya wachezaji katika michezo ya pili ya kufuzu kombe la dunia 2014 havikuwemo katika katika mchakato. Hilo halikuwa sawa kama nilivyo na mashaka juu ya uamuzi wa sasa. 
FIFA inaharibu mchakato wa kura za Ballon d'Or kwa maamuzi ya namna hii. Huhitaji kuwa na akili nyingi sana kuona kwamba uamuzi wa kuongeza siku za kupiga kura unamnufaisha zaidi CR7." alisema mwandishi huyo wa kihispania.

Listi ya wachezaji 23 wanaowania Ballon d’Or itakatwa mpaka kufikia wachezaji watatu tu Dec. 9, kabla ya mshindi hajatangazwa mwakani huko Zurich.
Imekuwa ikifahamika wazi kwamba Ronaldo, Ribery na Lionel Messi wataunda top 3, lakini Ribery alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na mchango wake aliotoa katika mafanikio ya kutwaa makombe matatu ya Bayern msimu uliopita.

Winga huyo wa kifaransa mpaka sasa hajapoteza mechi akiwa na klabu yake msimu huu, na alikuwa na mchango mkubwa kuisaidia Ufaransa kupata nafasi ya kwenda 2014 World Cup. 

NI WAKATI MWAFAKA WA ADEN RAGE KUONDOKA SIMBA


Na Baraka Mbolembole

Kuelekea mwisho wa utawala wa Hassan Dalali kama mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, timu hiyo ya ' Msimbazi' ilikuwa katika wakati mgumu kiutawala. Dalali, alikua aishi kuvurugana na aliyekuwa katibu wake mkuu, Mwina Kaduguda. 

Kwa mtazamo wa haraka, Dalali ndiye ' Mwanachama- kiongozi' anayekubalika zaidi na ' Wana- Simba', ila katika utendaji wake wa mambo muhimu katika makaratasi ilikuwa ni tatizo kubwa. Kumalizika kwa muda wa utawala wake, klabu ikaingia
katika uchaguzi huru na wa haki na hapo, Julai, 2010, Ismail Aden Rage akaingia madarakani.
Nchi yetu bwanaaa, kila mahali migomo tu, hadi wenye maduka wameingia katika hali hiyo ili kutetea usawa wao. Je, haki ni nini? Bila shaka haki ni kitu ambacho kinajiendesha chenyewe bila choyo, Mtu mwenye hekima na Busara hutembea na kitu hiki huku kikimuongoza katika harakati zake za maisha. Harakati ni nini? Harakati ni njia ya maisha tu. Ni lazima tuitende haki na kuisadiki. Yule mwenye kufanya dhuluma, atalipwa dhuluma, na malipo ya dhuluma hiyo huwa ni kubwa kuliko dhuluma yenyewe.

 'MTU MKUBWA NI MWANAFUZI'
Kwa, Rage bila shaka Simba, ilifikiriwa ingesogea hatua fulani mbele, ila matokeo yake ni watu kukosa imani zaidi kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Moro United, na katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Nchini, FAT, ( Sasa, TFF).. Mimi kwa upande wangu nilikuwa mara zote nikiangukia katika upande wa hoja za Mh. Rage, si kutokana na ' Siasa' zake bali kutokana na aina ya mtazamo wake wakati akiwa anazungumzia mipango ya maendeleo.
Wakati akiingia klabuni Simba, kama Mwenyekiti wa klabu nilifikiri labda sasa Simba itakuwa katika hali fulani nafuu, kiuchumi, kiutawala, na kiuendeshaji. Matokeo yake imekuwa ni fedhea kubwa. Wakati huu, ' Wasomi' kama Rage wakitawala soka la Tanzania, ni wazi mawazo yao mapya yanaweza kupingwa na upande mwingine, hasa upande ule ambao wanaamini kuwa soka linaweza kuendeshwa na mwanasoka wa zamani. Hapana, kuondoka kwa Dalali, hakukuja kwa bahati mbaya, alikuwa kiongozi mzuri lakini elimu yake ikamuondoa huku kundi kubwa la wanachama likitaka aorodheshwe katika orodha ya mwisho ya wagombea kinyume na katiba.
Funzo la kuondoka madarakani kwa Dalali, huku wanachama wengi wakimpigania lilipita nje ya fikra za Rage ambaye alikuja kushinda kwa kishindo katika uchaguzi. Ahadi zake zilikuwa ni nzuri, zilimvutia kila mmoja na ndiyo maana alishinda. ' Mtu mkubwa ni Mwanafunzi, kwani hutamani vitu zaidi kuliko watu wengine', na kwa Rage jambo moja kubwa lililomuingiza madaraki ni kuhiimariasha klabu kutoka katika utegemezi wa pesa za watu binafsi. Alisema kuwa ndani ya utawala wake Simba itakuwa na uwanja wake binafsi. Muda umekwenda sasa, na suala la Mwenyekiti huyo aliyesimamishwa na kamati ya utendaji kutoitisha mkutano wa katiba mpya ya klabu limewakera wengi na kumuona ni mtu mbinafsi, hasiye shahurika na mwenye maamuzi mabaya kwa klabu.

' PESA NI MTEGO'.
 Palipo na pesa ndipo pajaapo watu, lakini mafanikio yoyote huletwa na mawazo na mikakati mizuri ambayo inatekelezeka kwa maslahi ya pande zote. Katika mambo haya, Falsafa na Saikolojia, ni vitu muhimu vya kuzingatiwa, ipi iwe mwanzo, Saikolojia na falsafa?. Tusisahau kuwa ndani ya mambo haya pia kuna wenye kupenda vya bure, kikawaida hao ndiyo ' wenye mradi halisi', na wapo wenye uzalendo na wanaojua na kupenda ukweli wa mambo utendeke, Kundi hili la mwisho namaanisha, ' Ni lazima uwape wazalendo watakalo, ili nao wakupe utakacho'. Sababu ya yote hayo ni pesa.

 Kwa Aden Rage, pesa imekuwa ikimvuruga kwa kila namna, ameshindwa kuifanya Simba kujiendesha bila kutegemea mifuko ya watu. Na wakati klabu ikiwa imeuza wachezaji kama Herry Joseph, Mbwana Samatta, Danny Mrwanda, Patric Ochan, Mwinyi Kazimoto, Emmanuel Okwi, ni zaidi ya billioni moja wachezaji hawa wameingiza. Kama si kweli, Je, hawakuuzwa au walikopeshwa, na Simba ilinufaika vipi na biashara hiyo?

Klabu ya soka ya Simba iliwahi kumaliza msimu wa 2009 / 10 pasipo kupoteza mchezo wowote na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Baada ya mafanikio yale Simba imepitia vipindi vya kupanda na kushuka ndani ya uwanja, huku sehemu kubwa ya wachezaji wa kikosi kile ikiwa imepungua. Kuanzia katika benchi la ufundi mabadiliko yamekuwa ya mara kwa mara, Patrick Phiri ambaye alikuwa kocha wa kikosi kilichomaliza msimu bila kufungwa, aliondoka na tangu, majira ya kiangazi, mwaka 2010, makocha, Moses Basena, Milovan Curkovick na Patrick Liewig , Abdallah Kibadei  walishikiria nafasi hiyo .

 Sio tu mabadiliko katika benchi la ufundi bali hata waliokuwa wachezaji wa kikosi kile wamekuwa wakipungua kwa kiasi kikubwa msimu hadi msimu. Wapo wachezaji ambao wameuzwa, wapo ambao wameamua kuachana na timu hiyo kwa sababu za kimaslahi mara baada ya kumalizika kwa mikataba yao, wapo ambao wameondolewa kwa sababu za kinidhamu, na pia wapo wachezaji ambao wameondolewa kwa sababu za nje ya klabu ama za uwanjani mara baada ya kutofautiana na baadhi ya viongozi au wanachama matajri wenye pesa na ushawishi mkubwa kuliko Rage.

Mimi ni mtu ambaye napenda kupigania ukweli. Jukumu langu ni kutafuta na kuwaelekeza ' wazalendo' katika njia nzuri kama ipasavyo kuwa. Majira yanaendelea kugeuka, na umefika wakati wa watu kukataa kuchezwa ' shere' kwa ahadi za uongo. Huu ni wakati wa kutoa ahadi zilizoimarika na zitakazojidhihirisha baadaye. Ni wakati wa kuwaeleza watu kuwa ahadi hewa au zisizotekelezeka si garantii ya uongozi bora. " Kijana, hata serikali ilitumia miaka 50 kujenga uwanja" aliwahi kuniambia Rage wakati fulani nilipoandika makala kuhusu utendaji wake wa ' Kisiasa' ndani ya Simba. Ahadi ni deni na bila shaka wakati akiahidi kuwa atahakikisha klabu inakuwa na uwanja wake kabla ya kumalizika kwa utawala wake alimaanisha nini? Huu ni wakati mwafaka kwa Rage kuondoka Simba, alitakiwa ajiuzulu kwa hiari yake mwenyewe kwa kuwa ameshindwa kuwa mtendaji mzuri wa klabu, hukui ndani ya uwanja matokeo yakiwa ni mabaya kwa miezi 16 sasa.
   MASHABIKI, MWANACHAMA, KIONGOZI
Kwenye mchezo wa soka kuna mashabiki. Shabiki ni mtu anayependa sana mambo au kitu fulani, Pia kuna wanachama, ' Mwanachama' ni mtu aliyejiunga na wenzake na kushiriki nao katika shughuli za umoja huo. Achana na hao, pia kuna uongozi, Kiongozi ni mtangulizi wa jambo fulani, ' mtu mkubwa' anayesimamia shughuli maalumu kwa kueleza au kuelekeza. Haya ni makundi makubwa matatu yenye nguvu na uwiano tofauti lakini jukumu kubwa hapa ni kuhakikisha kila upande unakuwa sehemu ya malengo na mafanikio yanayotarajiwa. Simba pia ni timu ambayo imezungukwa na makundi haya matatu japo kuna kundi lingine ambalo ni la wachezaji. Hawa ni watendaji wa ndani ya uwanja, na pia kuna kundi la  mwisho la benchi la ufundi hapa kocha ndiye ' bosi mkubwa'.

 Makundi yote haya ndiyo ambao ujenga timu, na umoja unaokuwepo ndiyo hutoa timu bora inayotoa zawadi ya ushindi kwa mashabiki, wanachama, viongozi, wachezaji na atimaye furaha hiyo huwa kubwa zaidi kwa benchi la ufundi. FALSAFA na SAIKOLOJIA, Falsafa ni mwendo wa maisha ya binadamu, Saikolojia ni ufahamu na utendaji kazi wa nafsi au akili ya mwanadamu. Hivyo basi
 Simba kama timu inayoendeshwa na kuzungukwa na makundi ya watu inaweza kuwa timu kama tu makundi hayo yatakuwa na umoja wenye nia moja.

 MAMBO HAYA NI MUHIMU PIA KUTAZAMWA
MASHABIKI' Hili ni kundi ambalo lipo mbali sana na klabu, ni kundi kubwa la watu ambalo mara zote hupata hisia za ukweli za uchungu kipindi timu inapokuwa inatoa matokeo mabaya uwanjani. Kundi hili huwa halipati taarifa muhimu za klabu, kuingia katika mikutano muhimu ya klabu, kwa sababu katiba ya Simba inaonesha, ' Simba ni timu ya Wanachama hai'. Mashabiki wana nguvu sana kuliko makundi yote yaliyomo ndani ya klabu na mara nyingi huwa tatizo kubwa, hasa pale wanapokuja juu na kushinikiza jambo fulani. Na, kwa Aden Rage naye amekutana na hasira za mashibi wa klabu hiyo ambao wamekuchikizwa na hali ya mambo inavyoendeshwa.
 Ila, nao wanatakiwa kufahamu kuwa katika soka kuna matokeo ya aina tatu za matokeo: Sare, Kushinda, ama Kufungwa. '

  WANACHAMA'.
 Simba ni klabu ya wanachama hai. Na ndani ya kundi hili ndipo hupatikana viongozi wa juu wa klabu. Wanapatikanaje?. Yule mwenye sera na mtazamo mzuri kwa klabu ndiye anaweza kupata kura ambazo zitamuwezesha kuongoza klabu katika mwendo unaotakiwa. Lakini chaguzi nyingi za klabu huwaingiza madarakani watu wenye mtazamo tofauti na mitazamo inayokusudiwa na klabu. Kama kila mwanachama atazingatia na kufikiria sana anapopata nafasi ya kupiga kura. Itamlazimu achague viongozi ambao watawakilisha katika njia ya manufaa. Lakini sivyo inavyokuwa. Si wapembuzi wa fikra, hawafikirii kuhusu baade, zaidi ya wakati uliopo. Ni wao ndiyo waliomuingiza madarakani Rage
   HIVI NDIVYO NILIVYOVUNJA IMANI YANGU KWA RAGE
Ilikuwa ni wakati ambao kiongozi huyo aliponipigia simu na kuniambia kuwa 'Usiandike tena kuhusu mimi', alifikia hatua ya kusema hivyo baada tu ya kumfananisha na ' mwanasiasa mahiri'. Aliniuliza kuhusu makala yangu na kila swali lake nilimpatia majibu, ila nilipokuwa nikitaka kumuuliza mimi alikuwa akinijibu majibu yaliyonikera.
Ilikuwa ni baada ya kuwaadaa wanachama katika mkutano wa mwaka wa klabu, agosti, 2012. Katika mkutano ule ambao hofu ya kupinduliwa kwake ilikuwa kubwa, wanachama walikwenda na hoja moja muhimu kuhusu ahadi yake ya uwanja na namna mradi huo unavyoendelea hadi sasa.  Rage, akawajibu kuwa kila kitu kinashindikana kutokana na klabu kukosa millioni 30 ili waongezee katika millioni 50 walizokuwa nazo ili kulipia hati ya kiwanja serikalini. Wakachangishana, bwanaaa. Ikapatikana millioni 32 hivi, wanachama wakafurahi sana na kushangilia.
Vyombo vingi vya habari vikaripoti, ' Wanachama Simba wachanga zaidi ya millioni 30', lakini hao wanachama wenyewe waliochanga, Zacharia Hans Pope alitoa kiasi cha millioni 10 , Rage akatoa millioni tano sawa na aliyekuwa makamu wake mwenyekiti, Geofrey Nyange Kaburu ambaye pia alitoa millioni tano. Nikafikiria nikaandika '; Simba, katikati ya wanasiasa, ila itavuka'.
 Katika makala hiyo niliwalaumu sana wanachama wa klabu kwa kudanganywa kila siku. Eti, klabu ilikuwa imekosa millioni 30 ili wapate hati ya uwanja, wakati ndani ya siku mbili walitumia zaidi ya millioni 50 kuwasajili Mrisho Ngassa na Ramadhan Chombo. Nikagusia pia kuhusu hilo na kusema kuwa waliwatafuta wachezaji wa kuvunja nguvu ya mapinduzi baada ya timu kuwa dhaifu katika michuano ya Kagame Cup.
Niligusia vitu vingi kiukweli na pengine niliviweka wazi tu. Vilimkera sana  Rage. Aliniambia ' Kuna watu wamekuwa wakiniuliza huyo kijana una matatizo naye' hawa ni watu wake ambao walikuwa wakimpigia simu na kumuuliza kama amesoma makala hiyo. Aliongea mengi sana, Ila nikamuomba anisomee mahali ambapo anafikiri kuna makosa, ' Hakuna makosa, ila nilishakwambia usiandike kuhusu mimi'. Kweli, sijawahi kumuandika tena Aden Rage, na wala sitaandika makala kuhusu yeye, ila kwa jambo kama hili naweza kusema. ' Mtu mkubwa ni mwanafunzi', Ila hata awe na akili nyingi kiasi gani, hawezi kubadili mwendo wa historia, anachoweza kufanya ni kubadilisha baadhi ya mambo na kuyafanya yawe safi. Labda, Rage atakumbukwa kutokana na Siasa zake ndani ya Simba, ila angeacha heshima kubwa kama angeweza kuisadia klabu kuwa na uwanja wake wa mazoezi.
Ni wakati sahihi wa Rage kuondoka? Acha tu aondoke, angefanya kwa hiari yake mwenyewe kung'atuka.  ' MAADILI' Ni tawi la falsafa ambalo hutafakari masuala ya mwendo wa jamii ili kubaini tabia nzuri na mbaya, tabia zisizo sahihi na potofu. Ethiki
, hutathimini mwendo wa jamii ili kuhakikisha kuwa maisha yanakuwa ya haki, amani na usawa. Masuala ya maadili  hayalingani katika jamii zote, ila kwa Aden Rage, Simba ilikuwa katika mwendo mbaya
0714 08 43 08

NSA JOB SASA YUPO CHINA

 Nsa Job kulia akiwa na mchezaji mwenzake,
 Kikosi cha timu ya Watanzania kinachoshiriki mashindano huko nchini China.

Wednesday, November 20, 2013

HAT TRICK HERO CRISTIANO RONALDOOOOOO!






Mabao matatu aliyoyafunga jana Ronaldo kwenye mchezo dhidi ya Sweden yamemfanya kufikisha jumla ya mabao 47 na kumfikia mshambuliaji Pedro Pauleta,Pauleta ndiye alikuwa anashikilia rekodi ya timu ya Taifa ya Ureno ya kufunga mabao mengi. Kama Ronaldo akifanikiwa kufunga tena basi atakuwa anaweka rekodi ya kuifungia Ureno mabao mengi.

SHOMARI KAPOMBE IN ACTION!