Search This Blog

Saturday, June 11, 2011

MAANDALIZI YA HAYE DHIDI YA KLITSCHEKO


KAMA RAMBO KWENYE ROCK

HILLARY ECHESSA AONDOKA SIMBA


Kiungo wa Simba raia wa Kenya Hillary Echessa ameondoka kwenye kambi ya klabu hiyo leo asubuhi na kurudi kwao Nairobi.
Chanzo cha kuondoka kwa kiungo huyo ni kwamba alitoa masharti ya kuongezewa mkataba wake unaoishia mwezi wa saba kabla ya mechi ya DC Motema kitu ambacho uongozi wa Simba umeshindwa kukifanikisha hivyo kupelekea kiungo huyo kuondoka Msimbazi huku timu hiyo ikiwa inakabiriwa na mechi kubwa hapo kesho.

TUNAMUUZA LUKAKU - ANDERLECHT


Anderlecht wamekiri kuwa watamuuza Romelu Lukaku kipindi hiki cha kiangazi.

Anderlecht’s general manager Herman van Holsbeeck anaamini kuwa Lukaku atauzwa.

"Hakika ataondoka na kuondoka kwake ni muhimu sana kwetu hasa kwenye uhamisho," Van Holsbeeck aliliambia Gazet van Antwerpen.

“Sijui kama atananuliwa na Chelsea, kuna timu kubwa nyingi wanavutiwa nae na tunaongea nao, ila kitu kimoja ambacho najua ni kwamba hatakuwepo hapa msimu ujao."

FERGIE AMPIGIA SIMU SANCHEZ NA KUMWAMBIA JIUNGE NASI


Manchester United boss Sir Alex Ferguson ameingilia kati suala uhamisho wa Udinese superstar Alexis Sanchez.

Gazeti la Uingereza la Daily Mail linasema kuwa United Boss alichukua maamuzi ya kumpigia simu binafsi Alexis Sanchez na kumwambia ajiunge na Manchester United.

The Chile forward anapenda kwenda kucheza Spain lakini Barca wanaonekana kutokuwa na bajeti ya kutosha kumsaini winga huyo ingawa kuna taarifa kuwa miamba hiyo ya soka ya ulaya wanatarajia kutoa kiasi cha pesa pamoja na kumtoa Bojan Krkic ili kuweza kuwalainisha Udinese ambao wanataka paundi millioni 30 kwa ajili ya Sanchez.

Kwa sasa inaaminikia Ferguson yupo karibu sana na agent wa Sanchez kitu ambacho kinaleta matumaini kuwa atafanikiwa kumshawishi Sanchez ahamie Theatre Of Dreams.

WACHEZAJI WA KIINGEREZA WANAPENDA SANA STAREHE


ROBIN VAN PERSIE amewaponda wachezaji wa kiingereza kuwa wanapenda sana starehe kuliko kucheza soka.

Van Persie anasema anashangazwa sana na tabia za baadhi ya wachezaji hao, "Ninapoona baadhi ya wachezaji wa kiingereza wanakesha nje mpaka saa 9 usiku huwa napata jibu moja tu kuwa watakuwa hawana thamani watakapofikisha umri wa miaka 33.Kwangu mimi ni muhimu sana kuwa napata kifungua kinywa na wanangu wawili asubuhi,na hiyo haitawezekana kama utakuwa unahangaika kwenye madisko usiku mzima.Nikifanya uamuzi mwingine basi itakuwa ni kufanya kitu ninachokipenda kucheza soka." alimaliza Van Persie.


Friday, June 10, 2011

VITU ALIVYOFANYA XAVI HERNANDEZ MSIMU MZIMA

KALI YA LEO

TFF YAKANUSHA KULA PESA ZA ZAWADI ZA WASHINDI WA LIGI KUU YA VODACOM

Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF limekanusha taarifa za kwamba , TFF imetafuna fedha za ubingwa wa Tanzania Bara zinazotakiwa kupewa mabingwa wapya Dar es salaam Young Africans.

Akikanusha taarifa hizo katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema kwamba TFF walifanya makubaliano na Uongozi wa klabu ya Yanga juu ya namna ya kupewa fedha hizo na hadi sasa tayari wameshamaliza kulipa kiasi cha fedha walizokuwa wanadaiwa na club ya Yanga. Pia amekiri kutokulipwa kwa muamuzi bora ,na cheki ya mchezaji bora amesaini hivi karibuni .

KING ERIC KUREJEA OLD TRAFFORD


ERIC CANTONA atarudi Theatre Of Dream mwezi August kwa ajili ya kucheza mechi ya kumuaga Paul Scholes.

Scholes ambaye alitundika daluga mwishoni mwa msimu uliopita, anategemea kuagwa na mashabiki wengi katika mechi dhidi ya New York Cosmos.

Uwepo wa Cantona kama kocha unaonekana utazidi kuongeza mahitaji ya tiketi.

King Eric mwenye umri wa miaka 45 alisema: "Nataka kumpongeza Paul kwa kuwa na na kipindi kizuri na Unite, naangalia mbele kurudi OT katika jukumu langu kama kocha wa New York Cosmos.Huu utakuwa usiku mkubwa kwangu na familia yangu hivyo najipanga kufurahia kila kitu siku hiyo."


Liverpool sasa yahamishia majeshi kwa Gael Clichy

Liverpool wametoa ofa ya kushtukiza ya paundi 5m kwa ajili ya beki wa kushoto wa Arsenal Gael Clichy.

Arsenal's Cesc Fabregas 'set to seal Barcelona transfer on Monday'

wakala wa kiungo Cesc Fabregas, Darren Dein hapo kesho anaelekea Catalonia kukamilisha dili.

Taarifa kutoka gazeti la Marca la nchini Hispania zinasema Arsene Wenger ameshamkubalia Fabregas kuhama,

MICHUANO YA COPA COCA COLA 2011





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 10, 2011

MICHUANO YA COPA COCA COLA 2011
Msimu wa Tano wa michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 unaanza kesho (Juni 11 mwaka huu) katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika viwanja vinne tofauti.

Uzinduzi rasmi wa michuano hiyo utafanywa saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi. Mikoa yote 28 ya Tanzania Bara na Visiwani inashiriki katika michuano ya mwaka huu.

Mechi maalumu ya uzinduzi itakuwa kati ya bingwa mtetezi Kinondoni na Dodoma na itaanza saa 10 jioni. Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Tamco na Nyumbu vya Mkoa wa Pwani, na Karume na Tanganyika Packers (Kawe) vya Mkoa wa Dar es Salaam.

Siku hiyo ya uzinduzi pia kutakuwa na mechi kati ya Temeke na Ilala itakayofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers, Kigoma itapambana na Pwani kwenye Uwanja wa Nyumbu wakati Mjini Magharibi itaoneshana kazi na Morogoro katika Uwanja wa Tamco. Mechi hizo zitachezwa saa 2.30 asubuhi.

Ukiondoa mechi hizo rasmi za ufunguzi, kila siku kutakuwa na mechi mbili kwenye viwanja vyote. Mechi ya kwanza itaanza saa 2.30 asubuhi wakati ya pili itachezwa saa 10 jioni.

Hatua ya awali inachezwa katika makundi manne ya timu saba saba ambapo nne za kwanza katika kila kundi ndizo zitakazoingia hatua ya 16 bora.

Fainali itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati waamuzi 20 ambao wana umri chini ya miaka 17 wakiwemo wasichana wawili ndiyo watakaochezesha michuano hiyo.

Boniface Wambura

USAIN BOLT AWANYAMAZISHA WANAOMSEMA VIBAYA.

Usain Bolt ( KATIKATI ) AMEWAONYESHA WALIOKUA NA MASHAKA JUU YA UWEZO WAKE BAADA YA KUSHINDA MBIO ZA MITA 200 HUKO KTK MJI WA OSLO NCHINI NORWAY,
ALITUMIA MUDA WA SEKUNDE 9.86.

DONE DEAL - FERGIE AMNYAKUA ASHLEY YOUNG KWA £20 MILLION


ALEX FERGUSON amemalizana na Aston Villa baada ya kumnyakua Ashley Young kwa ada ya £20 mIL. jana usiku.

Baada ya usajili huuMan United sasa watakuwa wametumia kiasi cha £55m wakiacha mbali wapinzani kwenye kivuli chao.

Kuwasili kwa Young kumekamilisha usajili wa Fergie kufikia £55m akiwa bado anaendelea kukiimarisha kikosi chake.

Ashley Young alifaulu vipimo vya afya katika kliniki iliyopo katika uwanja wa mazoezi wa United Carrington halafu akatia saini mkataba wa kuichezea Man U kwa miaka minne, na sasa anaungana na Phil Jones ambaye alijiunga na United kwa £16m jumatano, na pia dili lingine la kumsaini David de Gea lenye thamani ya £18M linasubiri saini tu.

Ujio wa Ashley mwenye uwezo wa kucheza kama winga au mshambuliaji wa pili atakuwa nyongeza tosha katika kuifanya United kuwa na safu kali ya ushambuliaji, ingawa pia uwepo wake Old Trafford unaweka shakani nafasi ya Luis Nani .



ARSENAL WAKARIBIA KUMNYAKUA CHAMBERLAIN NA MAN UNITED WATOA OFFER KWA AJILI YA NASRI


Inaaminika kuwa Arsene Wenger anakaribia kumnasa kwa £ 12 million Alex Oxlade Chamberlain kutoka Southamton .

Winga huyo mwenye kipaji anatarajia kutimiza umri wa miaka 18 mwezi wa nane mwaka huuyupo kwenye mapumziko akiwa anafahamu fika kuwa atathibitishwa kuwa mchezaji wa Arsenal Julai 1.

The deal for the Southampton academy graduate - ambaye anaonekana kama Theo Walcott mpya amekuwa akifuatilia na timu za Liverpool na Manchester United lakini Wenger anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsaini kinda huyo wa kiingereza.

Wakati huo huo DailyMail wanaripoti kuwa Manchester United wanapanga kuwasilisha ofa ya paundi millioni 10 kwa ajili ya kumsajili Arsenal's midfielder Samir Nasri.

Wakala wa Nasri Jean Pierre Bernes bado hajahusishwa na jambo lolote kuhusu dili mpaka United watakapowasilisha ofa yao rasmi .


GIGGS ANAWEZA KUSTAAFU - FAMILIA


Familia ya mwanasoka na mchezaji wa Man United Ryan Giggs imesema inahofia kuwa winga huyo wa United anaweza akatundiga daluga mufuatia skendo yake ya kumsaliti mkewe na kaka yake.

Rafiki wa karibu wa familia hiyo anasema. "Tunahofia kuwa Ryan ataamua kuacha soka ili kuepuka kuzungumzia na vyombo vya habari.Kuendelea kucheza soka kutamleletea usumbufu mkubwa, watu wengi waliokuwa wanamsapoti wamepoteza imani nae na Ryan hawezi kuvumilia kupambana na maneno kutoka kwa fans.”

A club source saidXhanzo cha habri kutoka United kinasema: “Hili jambo linakuwa na linatia watu wasiwasi ndio maana Ferguson yupo tayari kumpa mapumziko marefu ili Giggs atumie muda kuweka mambo vizuri.”

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Giggs amekuwa akiandamwa na skendo ya kumsaliti mkewe baada ya kuwa na mahusiano na mke wa kaka yake.

Thursday, June 9, 2011

AZAM FC YAANZA RASMI MAANDALIZI YA MSIMU UJAO

Azam FC itaanza mazoezi Jumatatu tarehe 13 june 2011, wachezaji 16 wanatarajiwa kuanza mazoezi baadaye wachezaji sita waliokuwa na timu ya Taifa na waghana watajiunga na wenzao tarehe 27 kabla ya wachezaji wa timu ya taifa ya vijana U-23 kumalizia kujiunga na wenzao tarehe 29 June 2011.
Source: group page ya azam fc on facebook.

NIPE NAMBA AU NAONDOKA - KUSZCZAK AMWAMBIA FERGIE


Tomasz Kuszczak ametishia kuhama Manchester United ikiwa hatakuwa golikipa namba moja Old Trafford.

The 29-year old Polish goalkeeper amekuwa akikaa benchi kwa zaidi ya miaka minne na sasa Van Der Sar amestaafu Kuszczack anaona ndio muda muafaka wa kupata nafasi.

Lakini kutokana na taarifa za ujio wa kipa David De Gea kutoka Atletico Madrid, Kuszczack amesema wazi kuwa anataka kucheza au aondoke.

"Kwangu mimi ipo wazi kabisa nicheze kwenye goli la United au niondoke hapa", aliiambia France Football.

“Sir Alex Ferguson hajaniambia chochote kuhusu mkataba mpya.Hajaniambia chochote ,sijui nifikirie nini.Nina mawazo fulani hivyo nitajua cha kufanya.Nafikiri nitaendelea kubaki England nimekuwa pale kwa miaka saba, na uwezo wangu unafahamika pale.".

Arsenal yajiandaa kumpoteza Fabregas

nasikitika sana kuondoka ila sina jinsi.....


Imelipotiwa kuwa Arsenal imeshindwa kumshawishi nahodha Cesc Fabregas kubaki,na badala yake anaonekana siku zake zimewadia kurudi klabu yake ya zamani Fc Barcelona.
Meneja wa washika bunduki Arsene Wenger amemruhusu kuondoka lakini haruhusiwi kujiunga na vilabu vya England.

Real Madrid inaweza kumsajili Sergio Aguero kwa ada ya uhamisho ya €45m – mkurugenzi wa IMG

SIJUI KUN AGUERO ANAWAAGA MASHABIKI WA ATLETICO
MADRID ?


Bruno Satin, mkurugenzi wa kampuni IMG, kampuni inayomiliki haki za mshambuliaji wa Atletico Madrid ,Sergio Aguero, amedhibitisha upinzani wa jadi hauwezi kumzuia kun aguero kujiunga na Real Madrid.

mshambuliaji huyo nyota wa argentina ametangaza anataka kuhama baada ya kuitumikia klabu ya atletico madrid kwa kipindi cha misimu mitano.

Wesley Sneijder: sina sababu ya kuihama Inter

SNEIJDER AKIWA NA MKEWE


Kiungo wa Inter Wesley Sneijder amesema hana mpango wa kuihama klabu yake ingawa anatafutwa kwa udi na uvumba na vilabu vya Manchester United na Chelsea.

lakini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema kwenye klabu ya inter kuna kila kitu kizuri anachokihitaji.

PHOTO: GIGGS NA MAKOMBE YOTE ALIYOSHINDA NA MAN UNITED

MFUKO WA BARCA HAUTOSHI KWA FABREGAS


Mpango wa Barcelona kumchukua Cesc Fabregas kutoka Arsenal unaonekana upo mashakani baada ya Catalunya club kutangaza bujeti yao ya uhamisho kuwa ni £40, kiasi ambacho ni pungufu ya £10 ya gharama ya kumsajili kiungo huyo kutoka Emirates.

Barca wamechukua hatua isiyo ya kawaida kutangaza bajeti ya uhamisho baada kuthibitisha kuwa wanachukua hatua za kupunguza deni la klabu.

Makamu wa Raisi wa kitengo cha masuala ya pesa wa mabingwa hao wa ulaya Javier Faus alisema, "Pep Guardiola atapata £40million kwa ajili ya kusajili kwa pamoja na pesa itakayopatikana kupitia mauzo ya wachezaji

Kiasi hiki ni kidogo tofauti na Arsenal wanavyotaka kwa ajili ya Fabregas ingawa kinaweza kupanda ikiwa Barca watawauza Bojan Krkic, Jeffren na Maxwell.


TURKEY FA - TUTAWASHTAKI FIFA CHELSEA


Shirikisho la soka la Uturuki limewaonyaChelsea kuwa watatshatakiwa kwa FIFA ikiwa watajaribu kumshawishi isivyo halali Guus Hiddink kujiunga nao.

Inaeleweka kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anajiandaa kumrudisha kocha huyo wa kiholanzi Stamford Bridge sehemu ambayo Hiddink alifanya kazi kama kocha wa muda wa klabu hiyo mwaka 2009.

Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ana mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Uturuki mpaka mwakani na sasa shirikisho la soka la Uturuki limeionya klabu hiyo kuwa litawashtaki kwa FIFA ikiwa watajaribu kupitia mlango wa nyuma na kumshawishi Guus kujiunga nao akiwa bado na mkataba na TFF.


"Chelsea wana tabia ya kuwasajili wachezaji walio ndani ya mikataba, kama kitu kama hichi kikitokea kwa Hiddink tutawashtaki kwa FIFA.Waheshimu mkataba ambao Guus na FA." alisema Raisi wa TFF Mahmut Ozgener alipoongea na gazeti la Uturuki la HURRIYET..



Ada ya paundi milioni 30 kumpeleka alexis Sanchez Old Trafford.

Manchester United ipo mbioni kutumia kiasi paundi milioni 30 ( £30million) kwa ajili ya kupata saini ya winga Alexis Sanchez kutoka Udinese.
United walikua wanafikilia kumpata winga huyo raia wa Chile mwenye umri wa miaka 22, kwa kiasi cha paundi milioni 25 – lakini klabu yake imegoma kutoa apunguzo la ada yake ya uhamisho.
Sanchez mwenyewe anataka kujiunga na vijana wa Alex Ferguson kuliko Barcelona, akijua fika atatumia muda mrefu kuchoma mahindi pale Nou Camp.wakala wake, Fernando Felicevich, amedhibitisha kukutana na na mabosi wa barcelona lakini akadhibitisha pia hakuna dili lolote lililofanyika. Pia akasema ana matumaini makubwa iwapo udinese na Manchester Utd watakubaliana ada ya uhamisho basi Sanchez atajiunga na Man utd muda wowote.

DREAM TEAM YA ANDRIY SHEVCHENKO


Baada ya David Villa kuchagua kikosi chake bora leo tunawaletea kikosi bomba cha mchezaji wa zamani AC Milan Andriy Shevchenko.

Goalkeeper
Gianluigi Buffon

Kipa bora mwenye matukio ya kusisimua.Nilimfunga penati kwenye Champions League final mwaka 2003 lakini Buffon ameokoa michomo yangu mingi kuliko niliyomfunga.

Right-back
Cafu

Mpambanaji kiwanjani, yupo madhubuti na nguvu.Krosi zako kutokea nyuma ziliniletea magoli mengi nikiwa nae AC Milan na utani ulinisaidia kupunguza pressure ya mchezo kwenye mazoezi na mechi.

Centre-back
John Terry

Mlinzi imara na kiongozi asilia, anaweza kutuliza tabia za wachezaji kupaniki.Ana maamuzi mazuri na pia ni hatari sana katika mashambulizi ya kona..

Centre-back
Alessandro Nesta

Sijawahi kuona mtu anayeweza kusoma mchezo, mwenye akili na mzuiaji imara kama Nesta.Alitoa mchango mkubwa sana katika kuisadia AC Milan kuwatuliza Juventus in 2003 Champions League.

Left-back
Paolo Maldini

Mchezaji aliyebarikiwa na mwenye kujituma.Kiongozi mzuri mwenye kipaji cha kuzuia na anajua kubuni mashambulizi .Kwa kifupi ni moja ya mabeki bora niliowahi kuwashuhudia maishani mwangu.

Right midfield
Kaka

Mwalimu mbunifu anayelazimisha kasi ya mchezo.Nilikuwa nafuraha sana kuwa ndani ya timu na yeye, alikuwa ananipa pasi nzuri za mwisho na nilifunga magoli mengi shukrani kwa pasi zake za akili.

Centre-midfield
Steven Gerrard

Kiungo wa daraja juu, Gerrard anapenda kuongoza kwa mfano, ni maarufu kwa tabia yake ya kutokukata tamaa.Amebarikiwa nguvu, na uwezo kupiga pasi na mashuti yenye macho.

Centre-midfield
Zinedine Zidane

Alikuwa anafanya maajabu na miujiza kupitia kipaji chake.Kwenye mechi ulikuwa unashindwa kutabiri ataufanyia nini mpira, nje ya uwanja ni mtu alikuwa ni mtu mwema sana.Mwana miujiza Zidane.

Left-midfield
Lionel Messi

Ni vigumu kumpata mchezaji ambaye anaweza ku-dribble na kufunga kama Messi, ndio mshambuliaji wa karne 21.Sina maneno mazuri ya kuzungumzia zaidi, lakini Lionel yupo kila sehemu uwanja akiwafanya mabeki kuonekana wajinga.

Centre-forward
Ronaldo

Mwenye ujuzi, nguvu yupo kama mashine.Uwezo wake alionyesha katika kila timu aliyochezea unazungumza kila kitu.Nawaza angefanya mambo makubwa kiasi gani kama asingekumbwa na balaa la majeruhi.

Centre-forward
Wayne Rooney

Hakuna mchezaji katika soka la kisasa anayeweza kufikia ufanisi na kazi yake uwanjani, na tabia yake kama walivyo watu wengi wa aina yake.Ni mchezaji aliyekamilika ambaye kila kocha angependa kuwa nae katika kikosi chake cha kwanza.

Substitutes:

Petr Cech
Nina heshima kubwa sana kwa Cech, ameweza kuendelea kucheza soka kwenye kiwango kikubwa hata baada ya kupata majeraha makubwa.

Carles Puyol
Ni beki mzuri ambaye yuko tayari kujitolea kila kitu kwaajili ya timu yake.

Michael Ballack
Ana kipaji kikubwa na mtu uwezo wa kulitawala dimba.

Frank Lampard
Mchezai mwenzangu wa kipindi nipo Chelsea anaweza kuanzisha na kumaliza mashambulizi ya timu.

Andrea Pirlo
Kiungo mwenye akili na uwezo wa kutoa pasi mahali popote uwanjani.

Ryan Giggs
Mr Gentleman of modern football: ana hekima na mbunifu pamoja ujuzi mzuri wa kucheza soka.

Cristiano Ronaldo
Ujanja wake wa kuchezea mpira, anaweza kuutawala mpira na kazi zake anayoifanya uwanjani inaongea kila kitu.

Kiko wapi kikosi cha Stars kilichonyakuwa Kombe la Chalenji mwaka 1974:

OMARI MAHADHI AKIOKOA MCHOMO GOLINI KWAKE.




“Kikosi cha Taifa Stars kilichotwaa Kombe la Chalenji kwa mwaka huo 1974 kilikuwa ni, golini alikuwa ni Omari Mahadhi (marehemu), beki wa kulia alicheza Zaharani Makame, beki wa kushoto alicheza Mohamed Chuma (marehemu), namba nne alicheza Salim Amir, wakati sentahafu alisimama Mohamed Bakari ‘Tall’ na namba sita alicheza Jella Mtagwa.
“Namba saba alicheza Godfrey Nguruko ambaye baadaye kipindi cha pili alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Shiwa Lyambiko, namba nane alicheza Sunday Manara ‘Computer’, wakati sentafowadi alisimama Mwinda Ramadhani, namba kumi alicheza Gibson Sembuli na kumi na moja alicheza Lucas Nkondola.
KIKOSI CHA TAIFA STARS KILICHOTWAA KOMBE LA
CHALENJI MWAKA 1974:
1.Omari Mahadhi
2.Zaharani Makame
3.Mohamed Chuma
4.Salim Amir
5.Mohamed Bakari ‘Tall’
6.Jella Mtagwa
7.Godfrey Nguruko/Shiwa Lyambiko
8.Sunday Manara
9.Mwinda Ramadhani
10.Gibson Sembuli
11.Lucas Nkondola.
1.OMARI MAHADHI:
Alikuwa ni kipa mahiri na wakutumainiwa wa timu ya Taifa Stars katika miaka ya 1970 katikati mpaka miaka ya 1980 mwanzoni. Licha ya kuwa na umbo la kawaida, lakini alikuwa hodari mno awapo golini na kutokana na umahiri aliokuwanao ilikuwa sio rahisi kufungwa bao kirahisi.
Mahadhi alichaguliwa kuchezea Taifa Stars akitokea klabu ya African Sports ya Tanga. Pamoja na kuichezea klabu ya African Sports, pia ameichezea kwa mafanikio makubwa klabu ya Simba SC na alikuwa langoni katika kikosi cha Simba cha mwaka 1977 kilichoifunga Yanga mabao 6-0.
Baada ya kustaafu kucheza soka la ushindani miaka ya themanini alijishughulisha na kazi ya ukocha akifundisha baadhi ya timu zikiwemo Simba SC na Waziri mkuu FC ya Dodoma. Kwa hivi sasa hatunaye tena, kwani amefariki dunia katika miaka ya 1980 mwishoni.
2. ZAHARANI MAKAME:
Makame alikuwa beki mahiri aliyemudu kucheza vyema nafasi ya ulinzi namba mbili. Alichaguliwa kujiunga na timu ya Taifa Stars mwaka 1974 akitokea klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo ilikuwa daraja la kwanza wakati huo.
Pamoja na kuichezea timu ya Taifa Stars na Coastal Union kwa mafanikio makubwa, pia ameichezea timu ya mkoa wa Tanga. Kwa hivi sasa inasemekana Makame anaishi Tanga.
3. MOHAMED CHUMA:
Unapotaja mabeki mahiri waliowahi kuichezea timu ya Taifa Stars sio rahisi kusahau kulitaja jina la beki mahiri na shupavu Mohamed Chuma, kwani mlinzi huyo ameichezea timu ya Taifa Stars kwa kipindi kirefu kuliko walinzi wengine wote.
Umahiri wa mlinzi huyu ambaye alikuwa anamudu kucheza vyema nafasi ya ulinzi wa namba tatu ulitokana na aina ya uchezaji wake, kwanialikuwa anacheza kwa kujituma, asiyekata tamaa na ilkuwa sio rahisi kwa washambuliaji kumpita kirahisi.
Chuma alichaguliwa kujiunga na timu ya Taifa Stars akitokea klabu ya Nyota FC ya Mtwara. Pamoja na kichezea timu ya Taifa Stars kwa kipindi kirefu, Chuma alimudu kuichezea klabu yake ya Nyota Afrika FC ya Mtwara mpaka alipostaafu soka la ushindani katika miaka ya 1980 mwanzoni. Kwa hivi sasa hatunaye tena Chuma, kwani amefariki dunia mwaka 1984.
4. SALIM AMIR:
Amir naye kama alivyokuwa Chuma alikuwa ni beki mahiri wa timu ya Taifa Stars miaka ya 1970 katikati aliyemudu kucheza vyema nafasi ya ulinzi namba nne.
Amir alichaguliwa kuichezea timu ya Taifa Stars akitokea klabu ya Coastal Union ya Tanga. Amir alikuwa anatumia akili sana awapo uwanjani hali iliyowafanya washambuliaji wa timu pinzani aliokuwa akikabiliana nao kupata wakati mgumu kumpita. Kwa hivi sasa Salim Amir inasemekana anaishi Tanga akijishughulisha na shughuli zake binafsi.
5. MOHAMED BAKARI `TALL`:
Bakari alikuwa ni mmoja wa mabeki wa kati wa kutegemewa wa timu ya Taifa Stars katika miaka hiyo ya 1970 katikati. Bakari alichaguliwa kuchezea timu ya Taifa Stars akitokea klabu ya Cosmopolitan FC ya Jijini Dar es Salaam iliyokuwa moja ya klabu kubwa Jijini Dar es Salaam wakati huo ukiondoa klabu za Simba na Yanga.
Pamoja na kuvuma akiwa na timu ya Taifa Stars na Cosmopolitan FC, pia katika vipindi tofauti vya nyuma ameichezea klabu ya Simba SC, timu ya mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama Mzizima United na timu ya Taifa ya Vijana.Kutokana na umbo lake la urefu alilokuwa nalo na kumudu kucheza vyema nafasi ya ulinzi wa kati na kuwa kikwazo kikubwa kwa washambuliaji wa timu pinzani alizokuwa akikabiliana nazo wapenzi wa soka nchini walimbatiza jina la ‘Tall’.Kwa hivi sasa Bakari ni mkufunzi wa michezo na ni mkuu wa kitengo cha michezo katika shule ya Yamen English Midium Primary School iliyopo Chang`ombe Jijini Dar es Salaam.
6. JELLA MTAGWA:
Kama alivyokuwa Bakari, Mtagwa naye alikuwa ni mlinzi wa kati na kiungo mahiri wa kutegemewa wa timu ya Taifa Stars katika miaka ya 1970 katikati mpaka 1980 katikati. Mtagwa ameichezea timu ya Taifa Stars miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1974 mpaka 1984.Licha ya kuichezea kwa mafanikio makubwa timu ya Taifa Stars, pia katika vipindi tofauti vya nyuma ameichezea klabu ya Nyota Afrika ya Morogoro, Yanga, Pan African na timu ya Taifa Vijana. Mtagwa anakumbukwa na wapenzi wa soka nchini kuwa ni mchezaji pekee picha yake iliyowahi kuwekwa katika Stempu za Posta. Kwa hivi sasa Mtagwa anaishi Friends Corner Magomeni Jijini Dar es Salaam.

7. GODFREY NGURUKO:
Nguruko alikuwa ni mashambuliaji mahiri na wa kutegemewa wa timu ya Taifa Stars aliyemudu kucheza vyema nafasi ya winga ya kulia namba saba katika katika miaka hiyo ya 1970 katikati.Nguruko alichaguliwa kuchezea timu ya Taifa Stars akitokea klabu ya Coastal Union ya Tanga moja ya klabu iliyokuwa na wachezaji mahiri wakati huo. Katika mechi hiyo ya fainali ya michuano ya Chalenji baina ya Taifa Stars na Uganda Cranes, Nguruko kipindi cha pili alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Shiwa Lyambiko. Kwa hivi sasa inasemekana Nguruko anaishi Mkoani Tanga akijishughulisha na shughuli zake binafsi.

8. SHIWA LYAMBIKO:
Huyu Lyambiko alikuwa ni mshambuliaji wa timu yaTaifa Stars katika kipindi hicho cha miaka ya 1970 katikati. Lyambiko alikuwa akipokezana kucheza nafasi ya winga ya kulia namba saba na Godfrey Nguruko.Katika fainali hiyo ya mashindano ya Chalenji baina ya Taifa Stars na Uganda Cranes, Lyambiko aliingia kipindi cha pili, lakini alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliofunga penalti kati ya zile tano ambazo Taifa Stars walizipata siku hiyo.Lyambiko alichaguliwa kuchezea timu ya Taifa Stars akitokea klabu ya Mseto FC ya Morogoro moja ya klabu kubwa nchini wakati huo iliyokuwa inatandaza soka safi. Kwa hivi sasa Lyambiko anaishi Mkoani Morogoro.

9. SUNDAY MANARA:
Unapozungumzia wachezaji waliowahi kuvuma na kutamba hapa nchini kwa kucheza kandanda safi na la uhakika huwezi kuacha kulitaja jina la Sunday Manara.Kutokana na kucheza soka safi na la kimahesabu katika miaka hiyo ya 1970 pamojana ‘Computer’ kutotumiwa nchini Tanzania kwa wakati huo,lakini yeye wapenzi wa soka walimbatiza jina la ‘Computer’, wakimaanisha kuwa ana uwezo mkubwa wa kucheza soka vizuri na kwa uhakika kama ‘Computer’.Pamoja na kucheza soka kwa mafanikio makubwa hapa nchini Tanzania, Sunday inasemekana alikuwa mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza soka la kulipwa Ulaya.Sunday pamoja na kung’ara akiwa na timu ya Taifa Stars,pia katika vipindi tofauti vya nyuma ameichezea klabu ya Yanga, Nyota Afrika ya Morogoro na Pan African. Sunday ni ndugu ya wachezaji wengine mahiri wawili waliowahi kutamba hapa nchini Kitwana Manara na Kassim Manara ambao wote walichezea kwa mafanikio makubwa klabu za Yanga na Pan African. Kwa hivi sasa Sunday anaishi Jijini Dar es Salaam akijishughulisha na shughuli za biashara.

10. MWINDA RAMADHANI:
Mwinda alikuwa ni mmoja wa washambuliaji wa kutegemewa sana na timu ya Taifa Stars katika miaka hiyo ya 1970 katikati. Mwinda alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya Taifa Stars mwaka 1974 akitokea klabu ya Pamba FC ya Mwanza.Pamoja na kuichezea kwa mafanikio makubwa timu ya Taifa Stars na timu ya Pamba FC ya Mwanza, pia ameichezea timu ya Taifa ya vijana na klabu ya Yanga SC na alikuwa katika kile kikosi cha timu ya Yanga ha mwaka 1977 kilichofungwa mabao 6-0 na Simba.Kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa akiuonyesha akicheza nafasi ya ya ushambuliaji wa kati sentafowadi na kufunga mabao, wapenzi wa soka nchini walimbatiza jina la ‘Maajabu’ wakimaanisha kuwa alikuwa akifunga mabao kimaajabu mno. Kwa hivi sasa inasemekana Mwinda anaishi nchini Uingereza.

11. GIBSON SEMBULI:
Kati ya washambuliaji wachache mahiri waliowahi kutokea nchini kwa upigaji mashuti makali ni huyu Gibson Sembuli, kwani katika miaka ya 1970 kulikuwa hakuna mpigaji mashuti makali kama yeye.Sembuli alichaguliwa kuchezea timu ya Taifa Stars mwaka 1974 akitokea klabu ya Jogoo FC iliyokuwa na maskani yake makuu Mjini Morogoro.Pamoja na kuichezea timu ya Taifa Stars na Jogoo FC ya Morogoro kwa mafanikio makubwa, pia katika vipindi tofauti ameichezea klabu ya Yanga SC, Nyota Afrika FC ya Morogoro na Pan African. Kwa hivi sasa hatunaye tena Sembuli, kawani amefariki dunia mwaka 1979.

12. LUCAS NKONDOLA:
Kati ya wachezaji wachache waliokuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi wawapo uwanjani ni huyu Lucas Nkondola,kwani alimudu kucheza vyema nafasi ya ulinzi wa kushoto namba tatu, kiungo namba sita na nane na nafasi ya ushambuliaji wa kushoto namba kumi na moja.Pamoja na kutamba akiwa na timu ya Taifa Stars katika miaka hiyo ya 1970, pia kutokana na umahiri wake wa kusakata soka ameweza kuichezea klabu ya Pamba FC ya Mwanza, Sungura FC ya Tabora, Simba SC, timu ya Mkoa wa Mwanza, timu ya Mkoa wa Shinyanga, timu ya Mkoa wa Dar es Salaam na timu ya Taifa ya Vijana.Katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya Chalenji mwaka1974, Nkondola ndiye aliyefunga bao pekee kwa upande wa Taifa Stars katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza, kabla ya Uganda Cranes kusawazisha bao katika dakika ya 85.Pia katika upigaji wa penalti Nkondola alifunga penalti moja kati ya tano zilizopatikana kwa upande wa Taifa Stars siku hiyo. Kwa hivi sasa Nkondola anaishi Magomeni Jijini Dar es Salaam akijishughulisha na shughuli zake binafsi

YANGA NA AFRICAN LYON ZAKATAZWA KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA




VILABU VYA YANGA NA AFRICAN LYON VIMEPIGWA STOP KUENDELEA KUFANYA USAJILI WA WACHEZAJI WAPYA KWA AJILI YA MSIMU UJAO MPAKA PALE WATAKAPOMALIZA KULIPA MAFAO YA WACHEZAJI WALIWAVUNJIA MIKATABA.


HAYO YAMESEMWA NA AFISA HABARI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA, TFF,BWANA BONIFACE WAMBURA.


VIINGILIO VYA SIMBA VS DC MOTEMA PEMBE VYATAJWA!

MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA GEOFREY NYANGE AKIWATAJIA VIINGILIO WAANDISHI WA HABARI.


VIINGILIO MCHEZO KATI YA SIMBA DHIDI YA DC MOTEMA PEMBE HAPO SIKU YA JUMAPILI VITAKUA KAMA IFUATAVYO.

VIP A = 20,000
VIP B= 10,000
VIP C= 10,000
ORANGE STRAIGHT ,CURVE = 8,000
BLUE NA GREEN = 5,000

AZIM DEWJI ATIMIZA AHADI NA KUTOA AHADI NYINGINE.

MDAU WA SOKA NCHINI TANZANIA, AZIM DEWJI(KULIA ) HII LEO AMETIMIZA AHADI YAKE YA KUNUNUA KILA GOLI AMBALO LINGEFUNGWA NA TIMU YA VIJANA U-23 KWA SHILINGI MILIONI 5 KWENYE MCHEZO DHIDI YA TIMU YA VIJANA YA NIGERIA, TIMU YA VIJANA YA TANZANIA ILISHINDA BAO 1-0,
MDAU HUYO HAKUISHIA HAPO KWANI ALITOA AHADI NYINGINE KWA TIMU HIYO YA SHILINGI MILIONI 15 KAMA WATAFANIKIWA KUIONDOSHA MASHINDANONI NIGERIA.

MKATABA KATI YA PUMA NA SAFA UWE CHANGAMOTO KWA TFF YETU.

HII NI JEZI YA TAIFA STARS IKIWA BILA YA NEMBO YA.
MDHAMINI


JEZI HII INA NEMBO YA KAMPUNI YA UHLSPORT JE,KUNA CHOCHOTE
TFF WANANUFAIKA KWA KUITANGAZA HII BRAND?






HUU NI MFANO WA TSHIRT AMBAZO TFF WANGEWEZA KUZIUZA




NA KUTENGENEZA PESA YA KUMWAGA.








HII NDIYO JEZI MPYA YA BAFANA BAFANA BAADA YA SAFA




KUINGIA MKATABA WA MIAKA 7 NA KAMPUNI YA PUMA WENYE THAMANI YA




DOLA MILIONI 2 KWA MWAKA.

Na SHAFFIH DAUDA
CHAMA CHA SOKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI KIMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA VIFAA VYA MICHEZO YA PUMA KWA AJILI YA KUSAMBAZA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA TAIFA ZA AFRIKA YA KUSINI. NI MKATABA WA MIAKA SABA WENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI MBILI KWA MWAKA ($2M) ZAIDI YA TSH BILIONI 3 ZA KITANZANIA KWA MWAKA.


BAADA YA KUPATA TAARIFA HII IMENIFANYA NIKIFIKIRIE CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU NCHINI TANZANIA TFF, KWA JINSI AMBAVYO KIMEKUWA KIKISHINDWA KUTAMBUA KWAMBA TIMU YA TAIFA NI BIDHAA. LAITI KAMA KINGEKUA NA MIPANGO MATHUBUTI JUU YA MAENDELEO YA SOKA, KINGEWEZA KUPATA PESA AMBAZO ZINGEKIPUNGUZIA GHARAMA NYINGI ZA UENDESHAJI WA TIMU ZA TAIFA, NA MATOKEO YAKE KWA VIPINDI TOFAUTI, TIMU ZA TAIFA ZIMEKUWA ZIKIVAA JEZI ZENYE NEMBO ZA MAKAMPUNI MBALIMBALI YANAYOTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO PASIPO NA KUWA NA MIKATABA NAYO, NA HIVYO KUTONUFAIKA KABISA KWA KUVAA NA KUZITANGAZA NEMBO HIZO.


HIVI KARIBUNI KATIKA KILE KILICHOONEKANA KANA KWAMBA NI KUJIVUA GAMBA KWA TAASISI HIYO NGURI YA USIMAMIZI WA MCHEZO WA SOKA NCHINI, IKIWAAMINISHA WADAU WA SOKA KWAMBA IMEAZIMIA KULETA MAGEUZI NA MABORESHO YA KIUTENDAJI NA TIJA NDANI YA TAASISI, TFF ILIANZISHA KITENGO KIPYA CHA MASOKO KWA ZINGATIO LA KUZIUZA BIDHAA ZINAZOHODHIWA NA TAASISI HIYO.

LAKINI PAMOJA NA KITENGO HICHO KUANZISHWA CHINI YA MKURUGENZI WA KITENGO HICHO JIMMY KABWE, BADO HAKUNA MABADILIKO YA AINA YOYOTE YA KIUTENDAJI HUSUSANI KATIKA IDARA HIYO YA MASOKO YALIYOKWISHAONEKANA HADI SASA.

LENGO LANGU KUBWA HASA LA KUANDIKA WALAKA HUU NI KUTAKA KUELEZEA NAMNA AMBAVYO VYAMA VYA SOKA VYA NCHI MBALI MBALI ULIMWENGUNI VINAVYONUFAIKA KWA KUINGIA MIKATABA MINONO NA HAYA MAKAMPUNI YA KUTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO ,

NI KWELI MAKAMPUNI HAYA HUPENDA KUJIHUSISHA NA VYAMA VYA SOKA VYA NCHI HUSIKA AMBAZO TIMU ZAKE ZA TAIFA ZINAFANYA VIZURI.
KWA MFANO KIASI CHA PESA AMBACHO KAMPUNI YA NIKE INALIPA KWA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL KUVAA VIFAA VYENYE NEMBO YAKE NI TOFAUTI KABISA NA KIASI WANACHOLIPWA NIGERIA KWA KUVAA VIFAA HIVYO HIVYO VYA NIKE.

KUTOKANA NA HALI YA USHINDANI MKUBWA WA KIBIASHARA ILIVYO DUNIANI HIVI SASA, KAMPUNI YA KUTENGENEZA VIFAA VYA MICHEZO YA PUMA IMEAMUA KUVAMIA SOKO LA AFRIKA AMBAPO AFRIKA YA KUSINI IMEKUA NCHI YA 11 KUINGIA MKATABA NA KAMPUNI HIYO BARANI AFRIKA, ZIKIWEMO PIA BAADHI YA NCHI KAMA IVORY COAST, CAMEROON, MISRI NA MALAWI.
UKISIKIA PUMA INAKILIPA SAFA KIASI HICHO CHA DOLA MILIONI 2 KWA MWAKA UNAWEZA KUDHANI WANALIPA PESA TASLIMU.
HILO PIA LINAWEZEKANA MAANA HATUJUI VIPENGELE VILIVYOMO NDANI YA MKATABA WAO.

LAKINI PIA KUNA UWEZEKANO NDANI YA HUO MKATABA WA KIASI HICHO CHA DOLA MILIONI 2 KUNA PIA GHARAMA ZA VIFAA AMBAVYO SAFA ITAVITUMIA KWA TIMU ZAKE ZA TAIFA (VIJANA, BANYANA BANYANA NA BAFANA BAFANA).
PIA SAFA INAWEZA KUTENGENEZEWA JEZI Z A MASHABIKI (REPLICA) KWA BEI YA JUMLA NA KUZIUZA KWA FAIDA.

KAMA NINGEKUA MKURUGENZI WA MASOKO WA TFF NINGEIONA FURSA HIYO YA KAMPUNI YA PUMA KUTAKA KUJITANGAZA HASWA KUPITIA MATAIFA YA AFRIKA, NA NINGEWATAFUTA WAHUSIKA AU WAWAKILISHI WA KAMPUNI HIYO BARANI AFRIKA, NA KUWAPA MCHANGANUO KAMA SI MAPENDEKEZO ( PROPOSAL ) YA KUINGIA MKATABA NA TFF WALAU KWA KUANZIA BILA HATA MKATABA MNONO, LAKINI KWENYE MKATABA KUWEPO VIPENGELE KADHAA VYENYE KUIFADISHA TFF.
KWA MFANO, MOJA KATI YA VIPENGELE HIVYO KATIKA MKATABA NI KUTENGENEZEWA JEZI ZA MASHABIKI (REPRICA ) AMBAZO CHAMA CHA SOKA KITAUZIWA KWA BEI YA JUMLA. MATHALANI TFF IKIUZIWA JEZI MOJA YENYE UBORA KWA TSH 5,000/=, HALAFU WENYEWE WAKAUZA KWA TSH 20,000/= KILA JEZI, HEBU PIGA HESABU KWA NCHI YETU YENYE WATU ZAIDI YA MILIONI 40 ANGALAU WAUZE NAKALA 10,000 TU ZA JEZI, NI FAIDA KIASI GANI WANGETENGENEZA? NI KARIBU MILIONI 150 HIVI.

NADHANI WANGEKUA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA NAMNA HIYO VIKOSI VYA TIMU ZA VIJANA WA KIKE NA KIUME AMBAVYO KILA SIKU TUNAAMBIWA HAVINA WADHAMINI, VINGEPATA MATUNZO MAZURI LAKINI PIA BENDERA YA TAIFA INGEWEZA KUPEPERUSHWA VYEMA.
ILI KUWEZA KUFANIKISHA HILI, SIYO LAZIMA TFF WAUZE WENYEWE HIZO JEZI, WANAWEZA KUTANGAZA ZABUNI NA WAKAPATA KAMPUNI NA KUINGIA NAYO MKATABA WA KUSAMBAZA JEZI HIZO, HALAFU KAMPUNI HIYO IKAPATA GAWIO KUTOKA KWENYE FAIDA YA THS 15,000 KATIKA KILA JEZI KUTOKANA NA MAKUBALIANO.

HUU MKATABA MNONO BAINA YA CHAMA CHA SOKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI ( SAFA ) NA KAMPUNI YA PUMA UWE CHANGAMOTO KWA SHIRIKISHO LETU LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ( TFF ), UKIZINGATIA HIVI KARIBUNI TULIWEZA KUCHEZA NAO MCHEZO WA KIRAFIKI.
TUSIISHIE HAPO PIA TUJIFUNZE NAMNA WANAVYOENDESHA MAMBO YAO KITAALAMU NA KISAYANSI KATIKA KUENDESHA MCHEZO WA SOKA.

WACHEZAJI WA KIINGEREZA WAKIWA MAPUMZIKONI UARABUNI

ROONEY, McALLISTER NA ANDY CARROL

WAYNE ROONEY, COLEEN NA MTOTO WAO KAI

LAMPARD AKIJIACHIA NA DEMU WAKE


JOHN TERRY NA MKEWE WAKIWA ABU DHABI


MAGOLI YOTE WALIYOFUNGA MESSI NA RONALDO MSIMU HUU

PHOTO: XAVI AKIWA NA MAKOMBE YOTE ALIYOWAHI KUSHINDA NA BARCA

Last Moments of Ronaldo in Football Brazil vs Romania ( Honoring )

PHIL JONES AKIONDOKA HOSPITAL BAADA YA KUMALIZA KUFANYA VIPIMO VYA KUJIUNGA NA MAN UNITED

Mlinzi wa Blackburn Phil Jones akiondoka katika hospitali ya Bridgewater jijini Manchester leo jioni baada ya kumaliza kuchukua vipimo kwa ajili ya kujiunga na Manchester United.

Wednesday, June 8, 2011

BAADA YA MIEZI MITANO NAREJEA UWANJANI-JOSEPH OWINO




BEKI WA KIMATAIFA WA UGANDA JOSEPH OWINO AMESEMA MATIBABU ALIYOFANYIWA NCHINI INDIA YALIKUA YA MAFANIKIO SANA, ''NILIKATIKA LIGAMENT LAKINI BAADA YA UPASUAJI NIMEFANIKIWA KUTIBIWA NA HIVI NINAVYOONGEA NAWEWE 'JEMBE' NIPO FITI SANA TU'' HAYO YALIKUA MANENO YA OWINO NILIPOKUA NAFANYA NAE MAHOJIANO KWA NJIA YA SIMU KUTOKA NCHINI UGANDA.

KUANZIA LEO KILA JUMATANO BLOG YAKO ITAKUA INAVIVUMBUA VIPAJI VYA KITANZANIA VINAVYOTESA BARANI ULAYA!!

KIJANA ABUBAKARI YAHYA AKIWA MAZOEZINI NA TIMU YAKE YA
HALMIA
.








ALIKUA ANAISHI NA JABIR AZIZI KIUNGO WA AZAM FC MAENEO YA


MAGOMENI.






KWASASA AMEDILI URAIA WA TANZANIA NA KUWA RAIA WA SWEDEN


BAADA YA KUBADILI URAIA ANATUMIA ABUBACAR ERRIKSON.
















BRYAN ROBSON AACHIA NGAZI UKOCHA THAILAND


Former England captain Bryan Robson ameachia ngazi kama kocha wa timu ya taifa ya Thailand.

The 54-year-old aliambia FA ya Thailand kuwa angependa kuondoka na mabosi wake wakubali kumwachia.

"Bryan aliomba kujiuzulu na mkataba wake umekatishwa lakini siwezi kuzungumzia zaidi ili swala." alisema Raisi wa Thailand FA Worawi Makudi.

Robson ameendelea kuwa balozi rasmi wa timu yake ya zamani ya Manchester United na amesema ataendelea na jukumu hilo.

United leo wamesema katika mtandao wao kuwa maamuzi ya Robson hayahusiani kabisa na tishio la kuugua ugonjwa wa kansa.

The former United captain alifanyiwa upasuaji wa koo kwa ajili ya kansa mwezi 3 mwaka huu na madaktari walimwambia atapona kabisa.

DREAM TEAM YA ANDRIY SHEVCHENKO


Baada ya David Villa kuchagua kikosi chake bora leo tunawaletea kikosi bomba cha mchezaji wa zamani AC Milan Andriy Shevchenko.

Goalkeeper
Gianluigi Buffon

Kipa bora mwenye matukio ya kusisimua.Nilimfunga penati kwenye Champions League final mwaka 2003 lakini Buffon ameokoa michomo yangu mingi kuliko niliyomfunga.

Right-back
Cafu

Mpambanaji kiwanjani, yupo madhubuti na nguvu.Krosi zako kutokea nyuma ziliniletea magoli mengi nikiwa nae AC Milan na utani ulinisaidia kupunguza pressure ya mchezo kwenye mazoezi na mechi.

Centre-back
John Terry

Mlinzi imara na kiongozi asilia, anaweza kutuliza tabia za wachezaji kupaniki.Ana maamuzi mazuri na pia ni hatari sana katika mashambulizi ya kona..

Centre-back
Alessandro Nesta

Sijawahi kuona mtu anayeweza kusoma mchezo, mwenye akili na mzuiaji imara kama Nesta.Alitoa mchango mkubwa sana katika kuisadia AC Milan kuwatuliza Juventus in 2003 Champions League.

Left-back
Paolo Maldini

Mchezaji aliyebarikiwa na mwenye kujituma.Kiongozi mzuri mwenye kipaji cha kuzuia na anajua kubuni mashambulizi .Kwa kifupi ni moja ya mabeki bora niliowahi kuwashuhudia maishani mwangu.

Right midfield
Kaka

Mwalimu mbunifu anayelazimisha kasi ya mchezo.Nilikuwa nafuraha sana kuwa ndani ya timu na yeye, alikuwa ananipa pasi nzuri za mwisho na nilifunga magoli mengi shukrani kwa pasi zake za akili.

Centre-midfield
Steven Gerrard

Kiungo wa daraja juu, Gerrard anapenda kuongoza kwa mfano, ni maarufu kwa tabia yake ya kutokukata tamaa.Amebarikiwa nguvu, na uwezo kupiga pasi na mashuti yenye macho.

Centre-midfield
Zinedine Zidane

Alikuwa anafanya maajabu na miujiza kupitia kipaji chake.Kwenye mechi ulikuwa unashindwa kutabiri ataufanyia nini mpira, nje ya uwanja ni mtu alikuwa ni mtu mwema sana.Mwana miujiza Zidane.

Left-midfield
Lionel Messi

Ni vigumu kumpata mchezaji ambaye anaweza ku-dribble na kufunga kama Messi, ndio mshambuliaji wa karne 21.Sina maneno mazuri ya kuzungumzia zaidi, lakini Lionel yupo kila sehemu uwanja akiwafanya mabeki kuonekana wajinga.

Centre-forward
Ronaldo

Mwenye ujuzi, nguvu yupo kama mashine.Uwezo wake alionyesha katika kila timu aliyochezea unazungumza kila kitu.Nawaza angefanya mambo makubwa kiasi gani kama asingekumbwa na balaa la majeruhi.

Centre-forward
Wayne Rooney

Hakuna mchezaji katika soka la kisasa anayeweza kufikia ufanisi na kazi yake uwanjani, na tabia yake kama walivyo watu wengi wa aina yake.Ni mchezaji aliyekamilika ambaye kila kocha angependa kuwa nae katika kikosi chake cha kwanza.

Substitutes:

Petr Cech
Nina heshima kubwa sana kwa Cech, ameweza kuendelea kucheza soka kwenye kiwango kikubwa hata baada ya kupata majeraha makubwa.

Carles Puyol
Ni beki mzuri ambaye yuko tayari kujitolea kila kitu kwaajili ya timu yake.

Michael Ballack
Ana kipaji kikubwa na mtu uwezo wa kulitawala dimba.

Frank Lampard
Mchezai mwenzangu wa kipindi nipo Chelsea anaweza kuanzisha na kumaliza mashambulizi ya timu.

Andrea Pirlo
Kiungo mwenye akili na uwezo wa kutoa pasi mahali popote uwanjani.

Ryan Giggs
Mr Gentleman of modern football: ana hekima na mbunifu pamoja ujuzi mzuri wa kucheza soka.

Cristiano Ronaldo
Ujanja wake wa kuchezea mpira, anaweza kuutawala mpira na kazi zake anayoifanya uwanjani inaongea kila kitu.

VIWANGO VYA UBORA WA WACHEZA TENNIS ULIMWENGUNI BAADA YA KUMALIZIKA MASHINDANO YA WAZI YA UFARANSA.

MWANADADA CAROLINE WOZNIACK MCHEZAJI NAMBARI MOJA
KWA UPANDE WA KINA DADA.

Women's rankings

WTA singles rankings as of Monday 6 June 2011:

1. Caroline Wozniacki (Den)
2. Kim Clijsters (Bel)
3. Vera Zvonareva (Rus)
4. Na Li (Chn)
5. Victoria Azarenka (Blr)
6. Maria Sharapova (Rus)
7. Francesca Schiavone (Ita)
8. Petra Kvitova (Cze)
9. Marion Bartoli (Fra)
10. Samantha Stosur (Aus)


WACHEZAJI BORA WA MCHEZO WA TENNIS ULIMWENGUNI. ROGER FEDERER
KUSHOTO NA RAFAEL NADAL- KULIA


Men's rankings
ATP singles rankings as of Monday 6 June 2011:

1. Rafael Nadal (Spa)
2. Novak Djokovic (Ser)
3. Roger Federer (Swi)
4. Andy Murray (GB)
5. Robin Soderling (Swe)
6. David Ferrer (Spa)
7. Tomas Berdych (Cze)
8. Gael Monfils (Fra)
9. Mardy Fish (US)
10. Andy Roddick (US)


BREAKING NEWS - PHIL JONES KUFANYIWA VIPIMO LEO NA KUJIUNGA NA MAN UTD


Blackburn Rovers defender Phil Jones ameonekana jijini Manchester na kwa mujibu wa Skysports leo baadae atafanyiwa vipimo vya afya na Manchester United.

Inaaminika Man United wamemchukua Jones kwa paundi millioni 16 na wameshakubaliana na Rovers.

Jones ambaye amepewa na United mkataba wa miaka 5 alitakiwa kuondoka na timu ya vijana ya England U21 kuelekea Denmark jana lakini aliharisha ili aweze kukamilisha uhamisho na United na anategemewa kuondoka leo usiku kuelekea Denmark kujiunga na wanzake.

Kwa usajili huu United wamewapiga bao mahasimu wao wakubwa Liverpool ambao nao walikuwa karibu mno kufanikisha kumsajili Jones.