Baada ya David Villa kuchagua kikosi chake bora leo tunawaletea kikosi bomba cha mchezaji wa zamani AC Milan Andriy Shevchenko.
Goalkeeper
Gianluigi Buffon
Kipa bora mwenye matukio ya kusisimua.Nilimfunga penati kwenye Champions League final mwaka 2003 lakini Buffon ameokoa michomo yangu mingi kuliko niliyomfunga.
Right-back
Cafu
Mpambanaji kiwanjani, yupo madhubuti na nguvu.Krosi zako kutokea nyuma ziliniletea magoli mengi nikiwa nae AC Milan na utani ulinisaidia kupunguza pressure ya mchezo kwenye mazoezi na mechi.
Centre-back
John Terry
Mlinzi imara na kiongozi asilia, anaweza kutuliza tabia za wachezaji kupaniki.Ana maamuzi mazuri na pia ni hatari sana katika mashambulizi ya kona..
Centre-back
Alessandro Nesta
Sijawahi kuona mtu anayeweza kusoma mchezo, mwenye akili na mzuiaji imara kama Nesta.Alitoa mchango mkubwa sana katika kuisadia AC Milan kuwatuliza Juventus in 2003 Champions League.
Left-back
Paolo Maldini
Mchezaji aliyebarikiwa na mwenye kujituma.Kiongozi mzuri mwenye kipaji cha kuzuia na anajua kubuni mashambulizi .Kwa kifupi ni moja ya mabeki bora niliowahi kuwashuhudia maishani mwangu.
Right midfield
Kaka
Mwalimu mbunifu anayelazimisha kasi ya mchezo.Nilikuwa nafuraha sana kuwa ndani ya timu na yeye, alikuwa ananipa pasi nzuri za mwisho na nilifunga magoli mengi shukrani kwa pasi zake za akili.
Centre-midfield
Steven Gerrard
Kiungo wa daraja juu, Gerrard anapenda kuongoza kwa mfano, ni maarufu kwa tabia yake ya kutokukata tamaa.Amebarikiwa nguvu, na uwezo kupiga pasi na mashuti yenye macho.
Centre-midfield
Zinedine Zidane
Alikuwa anafanya maajabu na miujiza kupitia kipaji chake.Kwenye mechi ulikuwa unashindwa kutabiri ataufanyia nini mpira, nje ya uwanja ni mtu alikuwa ni mtu mwema sana.Mwana miujiza Zidane.
Left-midfield
Lionel Messi
Ni vigumu kumpata mchezaji ambaye anaweza ku-dribble na kufunga kama Messi, ndio mshambuliaji wa karne 21.Sina maneno mazuri ya kuzungumzia zaidi, lakini Lionel yupo kila sehemu uwanja akiwafanya mabeki kuonekana wajinga.
Centre-forward
Ronaldo
Mwenye ujuzi, nguvu yupo kama mashine.Uwezo wake alionyesha katika kila timu aliyochezea unazungumza kila kitu.Nawaza angefanya mambo makubwa kiasi gani kama asingekumbwa na balaa la majeruhi.
Centre-forward
Wayne Rooney
Hakuna mchezaji katika soka la kisasa anayeweza kufikia ufanisi na kazi yake uwanjani, na tabia yake kama walivyo watu wengi wa aina yake.Ni mchezaji aliyekamilika ambaye kila kocha angependa kuwa nae katika kikosi chake cha kwanza.
Substitutes:
Petr Cech
Nina heshima kubwa sana kwa Cech, ameweza kuendelea kucheza soka kwenye kiwango kikubwa hata baada ya kupata majeraha makubwa.
Carles Puyol
Ni beki mzuri ambaye yuko tayari kujitolea kila kitu kwaajili ya timu yake.
Michael Ballack
Ana kipaji kikubwa na mtu uwezo wa kulitawala dimba.
Frank Lampard
Mchezai mwenzangu wa kipindi nipo Chelsea anaweza kuanzisha na kumaliza mashambulizi ya timu.
Andrea Pirlo
Kiungo mwenye akili na uwezo wa kutoa pasi mahali popote uwanjani.
Ryan Giggs
Mr Gentleman of modern football: ana hekima na mbunifu pamoja ujuzi mzuri wa kucheza soka.
Cristiano Ronaldo
Ujanja wake wa kuchezea mpira, anaweza kuutawala mpira na kazi zake anayoifanya uwanjani inaongea kila kitu.
Its okay for others but for Rooney No.
ReplyDelete