Search This Blog

Saturday, May 5, 2012

ARSENAL KUWAPISHA SPURS AU NEWCASTLE NAFASI YA TATU - YATOKA SARE YA 3-3 NA NORWICH


Arsenal vs Norwich 3:3 GOALS HIGHLIGHTS by maidb7abc

KIKOSI NGONGORO HEROES LEO

Ngorongoro Heroes starting XI

 Aishi Manula, Ramadhan Khamis, Issa Rashid, Samir Ruhava, Dizana
Ramadhan, Frank Damayo, Frank Sekule, Omega Seme, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva na Ramadhan
Singano.
Reserve:

Saleh Malande, Hassan Dilunga, Jamal Mroki, Said Zege, Jerome Lambele,
Emily Mugeta na Atupele Green.

Uwanja: Khartoum Stadium
Watazamaji: 35,000Muda: Saa 2 kamili usiku
Refa: Aden Abdi Djamal - Djibouti
Waamuzi wasaidizi: Egueh Yacin Hassan, Bogoreh Salime Fahan na Aden Ali Farah- Djibouti.
Kamishna: Patrick Naggi- Kenya

RAMBIRAMBI MSIBA WA AMIR ROSHAN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Amir Roshan akiwa jijini Dar es Salaam.

Alikuwa akiwakilisha mikoa ya Kagera na Shinyanga na alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu tangu afanyiwe operesheni ya kichwa mwishoni mwa mwaka 2010.

Roshan ambaye alianza kuingia kwenye uongozi wa TFF wakati huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) katika uchaguzi uliofanyika mjini Kibaha mwaka 1993, amezikwa jana mchana kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwa vipindi vitano mfululizo. Alichaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 1993, jijini Dar es Salaam (1996), jijini Arusha (2001), jijini Dar es Salaam (2004) na jijini Dar es Salaam (2008).

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameelezea masikitiko yake na mshtuko mkubwa kutokana na kifo cha kiongozi huyo wa muda mrefu kwenye mpira wa miguu, hasa Kanda ya Ziwa akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA).

Osiah amesema TFF inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia ya mpira wa miguu kwa kumpoteza ndugu yao kipenzi, na Shirikisho litamkumbuka kwa mchango wake kwenye mpira wa miguu na dhamana aliyoibeba kwa muda mrefu akiongoza mpira wa miguu katika ngazi ya mkoa na Taifa.

Msiba huu ni pigo kwa familia ya Roshan, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Mungu aiweke roho ya marehemu Amir Roshan mahali pema peponi. Amina


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Powered by Sorecson : Creation de site internet

DIDA AGOMA KURUDI SIMBA KWA KUMUHOFIA JUMA KASEJA


LICHA ya kwamba Simba haikuwahi kuonyesha nia ya kumrejesha kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Deogratius Munishi 'Dida', kipa huyo ametamka kwamba hawezi kurejea Msimbazi kama Juma Kaseja atakuwapo klabuni hapo.

Dida, ambaye aliwahi kuichezea Simba na kukalia benchi kwa kipindi kirefu kabla ya kutemwa, alisema: "Hata kama Simba ikinihitaji sasa, kama Kaseja yupo sitakubali kuichezea. Ni kwa sababu ninajua nitaenda kukaa benchi.

"Najua siwezi kupata nafasi ya kucheza kutokana na uwezo wa Kaseja kwa sasa, lakini pia kwa jinsi anavyoaminiwa na Simba.

"Hakuna anayeweza kumwondoa Kaseja pale kwa sasa, kwanza yeye ni nahodha lazima acheze, kipa mwingine hatapata nafasi hadi Kaseja awe ameumia au awe amechoka kiuwezo, jambo ambalo kwa sasa si rahisi.

"Hivyo ndivyo ilivyo hata Ulaya, si umeona klabu kama Chelsea, Petr Cech au Iker Casillas wa Real Madrid, hao wakipata matatizo ndiyo wengine wataonekana."

Dida naye amecheza mechi zote za ligi isipokuwa mbili za mzunguko wa kwanza, alizosaidiwa na Hussein Sharif 'Casillas'.

Katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Kaseja ndiye amedaka mechi zote, lakini pia ndiye amesimama katika lango katika mechi za kimataifa.
Hali iliyomfanya msaidizi wake, Ally Mustapha 'Barthez' kukalia benchi msimu mzima wa ligi.
  
www.mwanaspoti.co.tz

FLOYD MAYWEATHER VS MIGUEL COTTO NANI KUIBUKA KIDUME

STEWART DOWNING: NAMCHUKIA DI MATTEO NA LEO NITALIPIZA KISASI DHIDI YAKE.

Roberto Di Matteo akifunga goli dhidi ya Middlesbrough.
Roberto Di Matteo  tayari alishamuumiza moyo Stewart Downing - lakini sasa winga huyo wa Liverpool yupo tayari kulipiza kisasi leo hii.

Mwaka 1997, Downing akiwa na miaka 12, akiwa mmoja ya wanafunzi wa shule ya soka ya Middlesbrough alienda Wembley akiwa na matumaini kibao kwamba klabu yake ya nyumbani itatwaa taji la FA Cup.

Lakini ya sekunde 42 Chelsea walikuwa mbele shukrani kwa goli la mita 25 la Roberto Di Matteo.

Liverpool star Downing alisema: “Wote tunakumbuka goli la mapema la Di Matteo likiingia nyavuni. Nimemchukia tangu wakati huo!Majina niliyomuita siwezi hata kuyarudia, lakini alikuwa mchezaji mzuri na anafanya vizuri kama manager akiwa na Chelsea. Leo nataka ayasikie machungu ambayo yameniandama kwa zaidi ya miaka 15."

REST IN PEACE LEGEND OF THE SUPER EAGLES RASHID YEKINI

Shujaa wa soka Nigeria Yekini afariki

Rashid Yekini afariki dunia
Rashid Yekini

Mcheza kandanda bora mara mbili barani Afrika, Rashidi Yekini amefariki dunia.
Yekini alizaliwa katika jimbo la Kaduna mwaka 1963. Baada ya kuanza kucheza kandanda ya kulipwa kwenye ligi nchini Nigeria, alikwenda Ivory Coast kuichezea klabu ya Africa Sports. Baada ya hapo alitimkia Ureno ambako alikuwa mfungaji mabao hodari katika ligi ya daraja la kwanza ya Ureno ambapo msimu wa 1993–94 alikuwa amepachika mabao 34 katika mechi 32 alizocheza.
Kupanda kwa kiwango chake cha usakataji kabumbu akiichezea timu ya taifa ya Nigeria msimu huo ambapo Nigeria ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la Dunia na baadae kufuatiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1993, akiwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kupata tuzo hiyo.
Rashid Yekini, ambaye alikuwa ametalikiana na mkewe tangu mwaka 1994 alikuwa akiishi maisha ya tabu na wapangaji wengine wachahe katika nyumba yake mjini Ibadan, jimbo la Oyo ambapo iliarifiwa mara chache sana alikuwa akitembelewa na wageni.
Yekini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49. Ameacha watoto wawili. Anazikwa siku ya Jumamosi kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huko Irah, jimbo la Kwara.

PAPISS DEMBA CISSE: KLABU TANO KUBWA BARANI ULAYA AMBAZO ZINAJUTA KUTOMSAJILI MSENEGALI HUYU

Kipindi cha kiangazi mwaka 2011 wakati Papiss Cisse akiwa anaichezea SC Freiburg - akiwa amefunga magoli 22 katika mechi 32 za Bundesliga - hakuna klabu iliyokuwa tayari kumsajili.

Hiyo ni kwasababu alikuwa anauzwa kwa £14 million, ada ambayo hakuna kocha au bodi ya wakurugenzi ilikuwa ipo radhi kulipa, especially kwa mchezaji ambaye hakuwa na hata na uzoefu mkubwa katika mechi ya level ya juu - pamoja na kuwa mchezaji wa kulipwa kwa takribani miaka 7.

Timu nyingi zilisemekana kuvutiwa nae - na chache zikatuma maskauti -lakini hakuna klabu iliweza kutuma ofa, na dirisha la usajili la kiangazi likafungwa huku kukiwa hakuna dili yoyote iliwasili Ujerumani kwa ajili yake.

Mwezi January dirisha la usajili likafunguliwa - na klabu zikaendelea kumtamani, japokuwa term hii alikuwa kafunga mabao 9 tu katika michezo 17.

Ada ikashuka mpaka £10million, na timu chachezikaonyesha kuvutika lakini ilikuwa ni Newcastle United ambao waliinyakua almasi toka mchangani.

Kocha Alan Pardew akiweka imani kubwa kwa Cisse na kumsaini kwa mkataba wa miaka mitano na nusu..

Toon walikwa ndio klabu pekee ambayo walitumia naasi na kumsaini mshambuliaji huyo na kumpa nafasi ya kucheza kwenye ligi ya level ya juu.

Michezo 12 ya Premier league baada ya kusajiliwa kijana wa miaka 26 kutoka Senegal kiukweli ameanza kulipa  fadhila, akifunga magoli muhimu 13 - likiwemo moja ya magoli bora kabisa kuwahi kutkea kwenye soka dhidi ya Chelsea.

Hizi ni klabu tano  - ambao ukizingalia kwa sasa - kwa hakika watajuta kutolipa £10million na kumsaini Papiss Cisse walipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo.


BLACKBURN ROVERS
Ndio, Blackburn Rovers wangeweza kumsaini Papiss Cisse. Hivi ndivyo wakala wa mchezaji huyo alivyosema mwezi June 2011: "Blackburn waliamuangalia karibia mara 10 msimu uliopita na nilionana na skauti wao. Lakini hatukusikia chochote kutoka kwao."

Taarifa zinasema walituma ofa iliyokataliwa ya £6 million kwa Cisse, na walitakiwa kuongeza mpaka £12 million, lakini hawakuwahi kufanya hivyo.

Yukubu Aiyegbeni ndio ni mshambuliaji mzuri kwa Blackburn - ukifikiria amefunga mabao 16 katika mechi 29 msimu huu - lakini ikiwa Rovers wangekuwa na world class striker kama Cisse,  katika timu yao, then nafikiri nafasi ya 19 waliopo katika premier league isingekuwa mahala walipo sasa.


SUNDERLAND
Mashabiki wa Newcastle watachukia kufikiri, lakini Papiss Cisse angeweza kujiunga Sunderland mwezi January.

Aliripotiwa kuwa amevutiwa na interest ya Sunderland, huku ripoti nyingine zikisema kwamba manager Martin O'Neill angejaribu kumsaini mshambuliaji huyo.

Lakini chelewa chelewa ikawagharimu Sunderland, baada ya Newcastle ambao ni mahasimu wao wakubwa wakathibitisha kumsaini Cisse.

Ni kitu ambacho kinaweza kuwaandama Black Cats kwa misimu mingi ijayo ikitazamwa impact aliyonayo Cisse kwa wapinzani wao.


TOTTENHAM HOTSPUR
Spurs nao walikuwa wametajwa katika mbio za kutaka saini ya Cisse, na ilikuwa ikifikiriwa kwamba wangetuma ofa yao mwezi January 2012.

Lakini Spurs walisubiri kwa muda mrefu, wakampoteza kwa Newcastle, na wakafanikiwa kumsaini Louis Saha kutoka Everton.

Walifuata uafadhali badala ya ubora - wakagoma kutoa hela na kumsaini Sha bure - na hili linaweza likawa limewagharimu kuchukua ubingwa - na hata inaweza ikawa nafasi ya kushiriki UEFA Chmpions league.


FULHAM
Fulham ilikuwa ni klabu nyingine ya premier league ambayo ilipoteza nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa daraja la juu na mtambo wa magoli Papiss Cisse.

Mwezi wa nane 2011, baada ya Cisse kusema njooni mnisajili kwa timu yoyote yenye pesa nchini England kumnunua, oliripotiwa kwamba the Cottagers walikuwa wapo tayari kutoa £14 million zilizokuwa zikitakiwa na Freiburg.

Kama ilivyo kwa wengine West Londoners nao wakazubaa zubaa na walkapoteza nafasi ya kumsajili msenegal huyo ambaye sasa ni sumu ya mabeki nchini Uingereza.

Bryan Ruiz alisajiliwa kutoka FC Twente kwa £10.6 million - ambazo zilikuwa nyingi zaidi ya Newcastle walizolipa kwa ajili ya Cisse.

Katika michezo 27 na Fulahm, Ruiz amefunga mabao mawili tu. Kwa pesa kidogo wangeweza kumsaini mtambo wa magoli. Watajuta.


JUVENTUS
Wanaweza wakawa kwenye nafasi nzuri ya kuchuku a ubingwa ambao pia wanaweza wakaupoteza kwa AC Milan, lakini kwa timu ambayo inahitaji sana mshambuliaji,  ni kesi ya je ingekuwaje kama Juve wangemsajili Papiss Cisse.

Kibibi Kizee cha Turin waliripotiwa na vyombo vya habari vya Italia kwamba walikuwa radhi kulipa pesa waliyotaka Freiburg. Lakini badala ya Cisse wakaamua mwishowe kumsaini Alessandro Matri, ambaye katika mechi 30 amafunga mabao 10 - na kama kwa hesabu za haraka haraka na kufikirika Cisse angeweza kuwa ametupia magoli mabao 33 katika idadi hiyo ya mechi.

Cisse amegeuka na kuwa investmen nzuri, na kama Juventus wangemsajili na angekuwa kwenye kiwango hiki ama kwa hakika sasa hivi wangekuwa wameshatangaza ubingwa mbele ya AC Milan.

Friday, May 4, 2012

WACHEZAJI WA BARCELONA NDIO WANAOLIPWA MISHAHARA MIKUBWA KULIKO WACHEZAJI WA MCHEZO WOWOTE DUNIANI.

Barcelona wanaweza kuwa hawajawa na msimu mzuri kwa standard yao, lakini kuna vitu fulani bado vinawaweka juu baada ya The Catalans kutetea nafasi ya kwanza kama timu inayolipa mishahara mikubwa wachezaji wake.
Barca wanalipa mshahara wa wastani wa £101,600, ambao ndio mkubwa zaidi kulipwa kwa wachezaji katikamichezo yote duniani.
 Pia soka imetawala katika listi ya vilabu vya michezo 12 duniani vinavyolipa mishahara mikubwa wachezaji wake - huku wapinzani wao Real Madrid wakifuatia nafasi ya pili, Manchester City wakitoka nafasi 10 mwaka jana - mwaka huu wameshika nafasi ya 3, Chelsea wamekamata nafasi ya nne na Bayern Munich, na timu mbili kubwa za Milan na Manchester United wote wakiwemo katika Top 12.

HII NDIO LISTI KAMILI

NELFI IBANEZ: KOCHA WA KWANZA KIKE KUFUNDISHA SOKA WANAUME DUNIANI





"Changamkeni, onyesheni nguvu! Msisimame, zidisheni presha!" Sauti ya kike kutoka kiwanja kimoja pale Lima, ikiwasisitiza wachezaji wa kiume kuongeza bidii na kufanya mazoezi zaidi.

Nelfi Ibanez ni kocha wa kike nchini Peru akiifundisha klabu ya Hijos of Acosvinchos inayocheza kwenye level ya semi-proffessional.

Timu hii chini ya Ibanez imekuwa na rekodi nzuri ambayo imekuwa ikiwashangaza baadhi ya wadau wa soka duniani.

Ibanez, mwanamke wa kibolivia mwenye miaka 43, sio mgeni katika michezo. Kocha huyu mwenye nywele ndefu alianza kufundisha soka nyumbani kwao Bolivia na Spain - na amekuwa akitoa mafunzo kwa timu za vijana na klabu moja nchini Bolivia ambayo alishinda nayo mataji kadhaa katika ligi isiyokuwa ya kulipwa.

Anasema ndoto yake kubwa kawa sasa ni kuiwezesha klabu anayoifundisha ya Hijos of Acosvinchos kupanda mpaka kwenye ligi kuu ya Peru - ingawa anasemabado anajihisi mpweke katika soka.


"Ningependa kuwe na makocha wengi wa kike katika soka," Ibanez aliambia shirika la habari la AFP. "Nafikiri naweza nikawa peke yangu katika dunia. Katika nchi ambazo nimetembelea nilijikuta ni mwanamke pekee ninayefundisha soka wanaume. Hata timu za wanawake katika nchi kama Ujerumani, Marekani na Japan zinaongozwa na wanaume."

Kwa wakurugenzi wa Hijos, klabu iliundwa miaka 66 iliyopita katika mji mkuu na wahamiaji kutoka kijiji cha Andean huko Ayacuncho, Ibanez alikuwa ndio chaguo sahihi.

"Kulikuwa na makocha zaidi ya 20 wa kiperu wakitakata nafasi ya kuikochi timu hii, lakini baada ya kuangalia CV ya huyu mwanamke  - akiwa amesoma Bolivia, Paraguay, akifanya kazi FIFA na pia FC Barcelona - hatukufikiria mara mbili kabla ya kuwasiliana na wakala wake." alisema raisi wa klabu hiyo Jaime Gonzalez.

Ibanez anapenda kutumia mfumo wa kushambulia wa 4-3-3 au 4-4-2, akiwa na mipango ya kuweka presha kubwa katika nafasi zote za wapinzani.

"Kupaki basi nyuma kunaondoa ladha yote ya soka. Siamini katika mifumo hii," alisema  Ibanez.

Ibanez ni maarufu sana katika nchi ambayo wanawake bado wanatafuta uhuru wa kutoa sauti zao zisikike.
Lakini hajioni yeye kama mpiganaji sana. Alikuwa tu anapenda soka tangu akiwa mdogo.

"Sijui kama nimekuwa mpiganaji au shujaa sana. Imetokea tu kwangu," alisema.

Ndoto yake kubwa ni kuifundisha timu ya taifa ya Bolivia na siku moja awawezeshe kushiriki katika kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu World Cup ya 1994.

Anasema japokuwa amekuwa akitukunwa sana na kusikia maneno mengi machafu ndani ya uwanja lakini hajali.

"Wanaweza kusema chochote watakacho. Ni haki yao. Binafsi siku zote nimekuwa nikijiheshimu sana, kama wachezaji."


Wachezaji wa timu yake siku zote wamekuwa wakifanya mazoezi chini ya uangalizi wa mwanamke huyu bila kumuonyesha dalili zozote za ubaguzi.

"Huyu mwanamke anajua soka kiundani sana," alisema Yetro Garcia, kijana wa miaka 21 anayecheza kama mshambuliaji. "Kocha wetu ni shujaa sana na anapenda sana kushinda. Anajua kabisa nini anataka na jinsi ya kutuongoza."

"Sioni tofauti yoyote na kocha wa kiume," anazungumza Diego Moron. "Sina tatizo na yeye kuwa kocha. Kiukweli nafikiria ni jambo zuri sana."

Ibanez anasema amekuwa akipatwa na aibu kwa muda mrefu wakati wachezaji wa kiume wakiwa wanabadilisha nguo vyumbani.
"Hilo ndio tatizo lakini mara zote nimekuwa nikijishughulisha na speech yangu ya kiufundi na maelekezo mbele ya mechi," alisema.

Msaidizi wake Cesar Vidal, 56, alimuongelea pia bosi wake.
"Tunaongea lugha moja. filosofi moja ya kushambulia na kuufanya mpira uwe na ladha, tunaenda kuchukua ubingwa na kuipandisha timu yetu ligi kuu." 

MH AMOS MAKALA AWA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO

Nahodha wa timu ya Bunge Fc Mh Amos Makala ( kushoto ) akisalimiana na Saleh Ally ,nahodha wa Global Publisher
 
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.
 
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

BREAKING NEWS: AZAM YAPIGWA 2-1 NA MTIBWA - SIMBAAAAAA MABINGWA WAPYA WA VPL


Wekundu wa msimbazi Simba SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011/2012,
Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya hii leo Mtibwa Sugar kuifunga Azam Fc mabao 2-1 kwenye mchezo ulioamuliwa kurudiwa hivi karibuni.
kufungwa huko kwa AZAM kunamaanisha hata wakishinda mchezo mmoja uliobakiwa hawataweza kuzifikia pointi 59 za SIMBA,kwasasa Azam wana pointi 53 ambazo zinawahahakishia kumaliza nafasi ya pili na kujipatia nafasi ya msimu ujao kushiriki kwenye kombe la shirikisho barani Afrika. 

HILI NDIO GOLI BORA KATIKA MISIMU 20 YA PREMIERLEAGUE - ROONEY AFUNIKA



 Goli la Wayne Rooney la tik taka dhidi ya Manchester City msimu uliopita limeshinda kama goli bora kabisa tangu kuanza kwa Barclays Premier League - kwa maana ya msimu 20 iliyopita.

Bao hilo lilitangazwa jana alhamisi jioni na chama cha waandishi wa habari wa soka katika chakula cha usiku jijini London.

Wayne Rooney akiwa na tuzo yake.


Mshambuliaji huyo wa Manchester United  alifunga bao hilo katika uwanja wa  Old Trafford mwezi wa pili mwaka jana limeyashinda magoli mengi yaliyofunga katika miongo miwili iliyopita.



Maelfu ya wapenzi wa soka duniani walihusika katika kupiga kura - huku Rooney akipata asilimia 26 ya kura zote, goli la Dennis Bergkamp dhidi ya Newcastle akiwa na Arsenal mwaka 2002 lilishika nafasi ya pili, huku goli la Thierry Henry dhidi ya Manchster United mwaka 2000 likishika nafasi ya tatu.

DSM DERBY COUNTDOWN: PAPIC SIMBA WATATUFUNGA - KUISHTAKI YANGA FIFA

KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic amesema mazingira ya sasa ndani ya klabu yake hiyo yanatoa fursa kubwa kwa Simba kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Jumapili.

Simba na Yanga zitavaana keshokutwa kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali mechi hiyo ilipangwa kupigwa kesho, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliamua kusogeza mbele kwa siku moja baada ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kutoa agizo la kurudiwa kwa mchezo kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar.

Akizungumza jana, Papic aliyeacha kuifundisha timu hiyo tangu Aprili 24 baada ya kibali chake cha kufanya kazi kuisha muda wake alisema Simba ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika pambano dhidi ya Yanga kutokana na wachezaji wa Simba kuwa katika hali nzuri kisaikolojia.

"Nitakwenda uwanjani kuangalia pambano hilo kama mpenzi tu wa soka, lakini kimsingi Simba ina nafasi kubwa ya kushinda pambano hilo tofauti na Yanga, hii ni kutokana na hali halisi ya mazingira ya timu hizi kwa sasa.

"Sifahamu vizuri kinachoendelea huko wakati huu, lakini ukweli Yanga haijatulia, sina sababu ya kukuelezea zaidi nadhani unafahamu hilo hasa kwa kutumia kigezo cha kujiamini, Simba ina nafasi kubwa ,"alisema Papic bila kufafanua zaidi.

Katika hatua nyingine, Papic alisema yupo katika hatua za mwisho kabla ya kuwasilisha malalamiko Shirikisho la soka la Dunia Fifa baada ya uongozi wa Yanga kupuuza madai yake ya kutaka alipwe takribani sh 24 milioni malimbikizo ya mishahara yake ya miezi miwili.

"Kila kitu nimekiandaa, nafikiri Jumapili niwatawasilisha Fifa malalamiko yangu, sikupenda kuchukua uamuzi wa kuishtaki Yanga, lakini sasa nitalazimika kuchukua hatua zaidi baada ya madai yangu kupuuzwa,"alisema Papic.

Alisema licha ya mara kadhaa kufanya jitihada za  kuwasiliana na uongozi wa Yanga kupitia simu ya mkononi bado amekuwa hapati ushirikiano kitendo kinachomfanya aone ni kama dharau kwake.

"Ninavyokuambia mara ya mwisho kuwasiliana na Mwenyekiti wa Yanga ni Aprili 25, tangu hapo nikimpigia hapokei simu yangu, sasa nielewe vipi kama sio dharau?," alihoji Papic.

NGORONGORO UWANJANI KESHO

Ngorongoro Heroes inaikabili Sudan kesho (Jumamosi) kwa staili ya kushambulia ili kuhakikisha inapata
tiketi ya kusonga mbele katika michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 20. Mechi hiyo ya
marudiano itachezwa Uwanja wa Khartoum, jijini hapa kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.

Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo leo (Mei 4 mwaka huu), Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Kim
Poulsen amesema kikosi chake ambacho jana usiku (Mei 3 mwaka huu) kilifanya mazoezi kwenye Uwanja
wa Omdurman kiko katika hali nzuri na kitatumia mfumo wa 4-4-2.

"Nia yetu ni kushambulia toka mwanzo ili kuwafanya Sudan wawe pia na kazi ya kuzuia badala ya kufikiria
kushambulia tu. Nyumbani tuliwafunga mabao 3-1, hivyo hapa watacheza kwa kushambulia tu. Sisi
tutazuia mashambulizi yao kwa kushambulia pia.

"Angalia mechi ya Manchester United na Manchester City pale Etihad. Manchester United walikwenda pale
kujilinda zaidi kuliko kushambulia, hali iliyowafanya wasitengeneze nafasi yoyote ya maana ya kufunga.
Staili hiyo iliwapa mwanya City ambao hatimaye walishinda. Hivyo sisi hatuwezi kucheza kama United kwa
tunataka Sudan wawe na kazi mbili, kushambulia na kuzuia pia.

"Hiyo ndiyo njia ya kuwafanya wasifikirie kutushambulia kwa muda wote, na tukipata bao mapema bila
shaka tutakuwa tumemaliza mechi. Wachezaji wangu tayari nimewafahamisha hili," amesema Poulsen
ambaye timu yake itafanya mazoezi ya mwisho leo usiku (Mei 4 mwaka huu) kwenye uwanja utakaotumika
kwa mechi kesho (Mei 5 mwaka huu).

Ingawa atajua hali kamili ya wachezaji wake baada ya mazoezi ya mwisho leo usiku, lakini kocha Poulsen
amesema anatarajia kutumia kikosi kile kile kilichoifunga Sudan katika mechi ya kwanza iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinaundwa na; Aishi Manula, Jamal Mroki, Issa Rashid, Samir Ruhava, Dizana Ramadhan,
Frank Damayo, Frank Sekule, Omega Seme, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva na Ramadhan Singano.
Wachezaji wa akiba ni Saleh Malande, Hassan Dilunga, Ramadhan Khamis, Said Zege, Jerome Lambele,
Emily Mugeta na Atupele Green.

Mechi hiyo ambayo haitakuwa na kiingilio kwa watazamaji itachezezwa na Aden Abdi Djamal wa Djibouti,
na atasaidiwa na Wadjibouti wenzake Egueh Yacin Hassan, Bogoreh Salime Fahan na Aden Ali Farah.
Kamishna ni Patrick Naggi kutoka Kenya.

Ngorongoro Heroes itaanza safari ya kurejea nyumbani mara baada ya mechi hiyo. Itaondoka hapa saa 9
alfajiri kupitia Nairobi, Kenya na inatarajia kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumapili saa 3.20 asubuhi.

OMBI LA MDAU KUTOKA NCHINI FINLAND

Dear kaka Dauda,
Thanks kwa kipndi chako na Blog yako nzuri..yes inatufanya tuwe updated hata tulio nje ya nchi ya Tanzania na ukweli najua jinsi gani ulivy frutrsted na aina ya uusanii wa soka letu la bongo.
Nipo na wa Tz kibao hapa tunabisha kuhusu maamuzi ya kamati ya Tigaigana na jinsi shereia ya TFF no 22 km sikosei..je inasema refa alitakiwa kusubir dk ZISIZOZIDI 15 AU ZISIZOPUNGUA 15?
Km nilisikia vibaya kutoka kwenye vipindi vya clouds ni kwamba dk zisizozidi 15..
Please unaweza kunifowardia hiyo document?km ipo for public use anyway, au nijibu tu email hii km inawezekana pia kaka...
Thanks..
Mtebe
Tampere, Finland

JULIO: TOTO WASUBIRI KIPIGO TU


KLABU ya Coastal Union iko katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mechi yao ya kumalizia msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Toto Africa inayotarajiwa kupigwa dimba la Mkwakwani jijini hapa.
Akizungumza jijini hapa juzi, Kocha Mkuu wa Wagosi wa Kaya, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, alisema wameamua kuanza maandalizi ili kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu muhimu kwenye mechi hiyo.
Kihwelu alisema kutokana na uimara wa kikosi chake ambacho kimekuwa tishio kwa baadhi ya timu kongwe zinazoshiriki ligi hiyo, wana imani kubwa ya kuibuka na ushindi wa kishindo wakiwa nyumbani.
“Ninachoweza kusema ni kuwa mechi hiyo haitusumbui akili, kwani tuna imani kubwa na kikosi chetu kuweza kushinda siku hiyo,” alisema Julio.
Kocha huyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo, ili kuwapa hamasa wachezaji kufanya vizuri.

HUYU NDIO KIBOKO YA AKINA MESSI NA MULLER - HAYATI GODFREY CHITALU KIBOKO YA MAKIPA WA AFRIKA

Chitalu enzi zake dimbani


Je unadhani Lionel Messi ndio mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ndani ya msimu katika historia ya soka la ushindani duniani?

Hapana - kuna jembe kutoka hapo kwa majirani zetu tunaoshea nao reli moja na mabingwa wa Afrika Zambia - ambaye alifunga mabao 107 katika mashindano yote aliyocheza ndani ya mwaka 1972.

Godfrey 'UCAR' Chitalu, ndio mchezaji aliyefanya shughuli hii. Alizaliwa mwaka 1947 na anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote nchini Zambia akiwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Makazi ya Milele ya Chitalu


Chitalu ambaye ni mmoja ya watu waliokufa katika ajali ya ndege ya timu ya Zambia iliyotokea mwaka 1993 - aliwahi kuzitumikia klabu za Roan United, Kitwe United, Kabwe Warriors. Pia baada ya kustaafu aliamua kuwa kocha wa timu Kabwe Warriors kuanzia mwaka 1984-1991 kabla ya kupewa majukumu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Zambia ambayo ndio alikuwa akiiongoza mpaka timu ilipopata ajali ya ndege mwaka 1993 na kufariki dunia.

Pamoja na kuweka rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja - Chitalu ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi ndani ya uzi wa Chipolopolo akiwa na magoli 76 - manne kati ya hayo alifunga kwenye michuano ya kugombea kufuzu katika Olympic 1980 na mechi za michuano yenyewe - ambapo Zambia ilishiriki.

Pia Chitalu ameweka rekodi ya kufunga mabao 11 katika mashindano ya CECAFA - mabao haya aliyafunga katika michuano ya mwaka 1978

Hizi ni baadhi ya rekodi zake nyingine za utunguaji makipa

    •    81 goals  katika mashindano yote mwaka 1968 - in all competitions in 1968(yakiwemo 11  akiwa Zambia)
    •    45 goals in katika mashindano yote mwaka 1969.
    •    51 goals in all competitions in 1971
    •    107 goals in all competitions in 1972
    •    11 goals at CECAFA ’78 which is a CECAFA record

Godfrey Chitalu 
Personal information
Full name Godfrey Chitalu
Date of birth 22 October 1947
Place of birth Luanshya, Northern Rhodesia
Date of death 27 April 1993 (aged 45)
Place of death Gabon
Playing position Forward
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
–1967 Roan United

1967–1970 Kitwe United

1970–1982 Kabwe Warriors

National team
1980 Zambia U23

1968–1980 Zambia
(76)
Teams managed
1984–1991 Kabwe Warriors
1993 Zambia

Thursday, May 3, 2012

Eti bao hili na Papiss Demba Cisse lipi kali ?

MABAO 1281 YA PELE, HAT-TRICK YA NDANI YA DAKIKA 5 YA VILLA, MABAO 71 YA CHAMPIONS LEAGUE YA RAUL : REKODI NYINGINE AMBAZO LIONEL 'MESSIAH' MESSI BADO HAJAZIVUNJA

Je atakuwa au hatokuwa mchezaji bora wa muda wote?

Lionel Messi jana alivunja rekodi ya Gerd Muller ya kufunga mabao 67 ndani ya msimu mmoja wa ligi za ulaya - kwa kufunga goli lake la 68 ndani ya msimu huu na kuzidi kuongeza kasi katika kufikia kuwa mchezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya mchezo huu.

Wakati majadiliano na mabishano yakiendelea aidha anastahili au hastahili kuwa mchezaji bora wa muda wote, baadhi ya wachezaji wenzie wa Barca wameshampitisha, hakuna shaka kwamba Messi ni bora sana katika kizazi hiki cha soka cha sasa - amekuwa akivunja rekodi kila kukicha na kuacha matendo yake ya uwanjani yaongee badala ya sauti yake.

Msimu alikuwa mchezaji wa tatu kushinda Ballon d'Or kwa mara ya tatu; kwa sasa pia ni ni mmoja kati ya wachezaji wawili waliofunga mabao mengi katika msimu mmoja wa champions league, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano katika mechi moja ya UCL, ndio mchezaji mdogo kiumri kuweza kufikisha mabao 150 ya La Liga, ni mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Barcelona katika mechi rasmi na jana akavunja rekodi ya Muller kwa kufunga bao la 68 na kumpita mjerumani huyo aliyefunga mabao 67 ndani ya msimu mmoja. Haya yote ameyafanya ndani ya miezi mitano ya 2012.

Lakini pamoja na kuvunja rekodi hizo zote, bado kuna njia ndefu mpaka kufikia kilele cha mafanikio ambayo yatawafunga wabshi wake midomo, kijana huyu mwenye miaka 24 bado ana kazi ya kuvunja rekodi hizi




BARCELONA & LA LIGA
ALL-TIME RECORD MESSI'S TOTAL
Barca all-time appearance record: Xavi - 626 326
Mfungaji bora wa Barca in La Liga: Cesar Rodriguez - 192 165
Mfungaji bora wa Barca wa muda wote (including friendlies): Paulino Alcantara - 369 259
Mchezaji wa Barca aliyefunga magoli mengi zaidi kwenye mechi 1: Joan Gamper - 9 5
Kushinda mataji mengi zaidi ndani ya Barca: Xavi, Pep Guardiola, Josep Samitier - 6 5
Mechi nyingi zaidi kwenye La Liga: Andoni Zubizarreta - 622 212
Mataji mengi ya La Liga: Francisco Gento - 12 5
Mfungaji bora wa muda wote wa La Liga: Telmo Zarra - 252 165
Most goals scored in a single Liga game: Laszlo Kubala, Bata  - 7 4
 Hat-trick ya haraka zaidi kwenye La Liga (in minutes): David Villa - 5 12




BARCELONA & CHAMPIONS LEAGUE/EUROPE
ALL-TIME RECORD MESSI'S TOTAL
Makombe mengi ya Champions League na Barca: Andres Iniesta, Carles Puyol, Xavi, Victor Valdes - 3 3
Mechi nyingi zaidi za Most Champions League: Raul - 144 68
Makombe mengi zaidi ya European Cup/Champions League trophies: Francisco Gento - 6 3
Mfungaji bora wa muda wote wa Champions League: Raul - 71 51
All-time top scorer in European competition: Raul - 73 52
Most top-scorer awards in Champions League: Gerd Muller - 4 3
Most goals in a single European Cup season: Jose Altafini - 14 14
Most scoring final appearances in European Cup/Champions League: Alfredo Di Stefano - 5 2
Most goals in European Cup/Champions League finals: Alfredo Di Stefano, Ferenc Puskas - 7 2
Most hat-tricks in the Champions League: Filippo Inzaghi, Mario Gomez, Michael Owen - 3 3







ARGENTINA & INTERNATIONALS
ALL-TIME RECORD MESSI'S TOTAL
All-time appearance record for Argentina: Javier Zanetti - 145 67
All-time top scorer for Argentina: Gabriel Batistuta - 56 22
All-time appearance record in World Cup finals: Lothar Matthaus - 25 8
All-time World Cup top scorer: Ronaldo - 15 1
Most World Cup wins: Pele - 3 0
Most goals in a single World Cup tournament: Just Fontaine - 13 1
Most World Cup tournaments: Antonio Carbajal, Lothar Matthaus - 5 2
All-time Copa America top scorer: Norberto Mendez, Zizinho - 17
2
Most Ballon d'Or wins: Johan Cruyff, Michel Platini, Marco van Basten - 3 3


Pia bado ana msala wa kuifikia rekodi ya kufunga mabao 1,281 ya Pele pamaoja na kufanikiwa kupata mafanikio katika kombe la dunia.

KALI YA LEO - KOCHA AMTANDIKA MAKONDE MCHEZAJI - ATIMULIWA KAZI

MESSI MFUNGAJI BORA WA MAGOLI MENGI KWA MSIMU WA MUDA WOTE NDANI BARA LA ULAYA - ANGALIA WANAOMFUATIA

EUROPE'S  TOP 10 GREATEST GOALSCORING SEASONS
PLAYER CLUB GOALS   SEASON
Lionel Messi (Argentina) Barcelona   68+ 2011-12
Gerd Muller (West Germany)
Bayern Munich
67
1972-73
Ferenc Deak (Hungary)
Szentlorinc
66
1945-46
Gyula Zsengeller (Hungary)
Ujpest
65
1938-39
Dixie Dean (England)
Everton
63
1927-28
Jimmy McGrory (Scotland)
Celtic
62
1927-28
Refik Resmja (Albania)
Partizani Tirana
59
1950-51
Jimmy McGrory (Scotland)
Celtic
59
1926-27
Fred Roberts (Ireland)
Glentoran
59
1930-31
Ferenc Deak (Hungary)
Ferencvarosi
59
1948-49

DSM DEBY COUNTDOWN: TUTAWAFUNGA YANGA NA KUCHUKUA UBINGWA ASEMA MILOVAN

KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic ametamba kikosi chake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayofikia tamati keshokutwa.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Zanzibar ambapo timu yake imeweka kambi, Cirkovic alisema kutokana na hali ilivyo, kikosi chake kinampa moyo kwamba kinaweza kushindana katika michuano yoyote.


“Kikosi changu kiko vizuri na kina uwezo wa kushinda mechi yoyote inayokuja mbele yake hata ya marudiano dhidi ya Al Ahly Shandy itakayofanyika Sudan,” alisema.


Simba inakabiliwa na mechi ya marudiano ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu hiyo inayotarajiwa kufanyika Sudan katikati ya mwezi huu ambapo timu hiyo imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya kushinda mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


"Nina imani na kikosi changu kutokana na hali iliyokuwa nayo...nina uhakika kitafanya vizuri dhidi ya Yanga na hata katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho," alisema Cirkovic.


Simba itacheza na Yanga mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara ambapo ili kutwaa ubingwa,

inahitaji pointi moja, kinyume na hapo inabidi izidishe maombi ili Azam ipoteze mechi ya
mwisho dhidi ya Kagera Sugar, kwa vile nayo ikishinda na Simba ikifungwa zitakuwa
zinalingana pointi na hivyo bingwa atalazimika kuamuliwa kwa tofauti ya mabao.

Cirkovic alisema katika mchezo huu anaomba sapoti ya mashabiki wa Simba akiwataka wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwashangilia ili kuzidisha nguvu ya kutwaa ubingwa ambao msimu uliopita waliukosa kwa tofauti ya bao moja.


“Nawathamini sana mashabiki, na kushinda kwetu hata katika mechi zilizopita ilitokana na kuja kwao kwa wingi uwanjani kutushangilia na wengine waliopata nafasi walithubutu hata kusafiri mikoani kuhakikisha wanashuhudia timu ikicheza, nafarijika sana na mashabiki wangu,” alisema.


Simba inatarajiwa kurejea siku hiyohiyo ya mechi ambapo itafikia moja kwa moja uwanjani ikitokea Zanzibar.

DAR ES SALAAM DERBY COUNTDOWN: MVUA YATIBUA MAZOEZI YA YANGA BAGAMOYO

MVUA kali inayonyesha hivi sasa Bagamoyo, imesababisha klabu ya Yanga iliyoweka kambi Bagamoyo mkoani Pwani kujiandaa na mechi dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Jumamosi kusitishwa jioni hii.
Mvua hiyo inavuruga programu za mazoezi magumu ya kocha Freddy Felix Minziro, ambaye anawafua haswa wachezaji wa timu hiyo mjini hapa wanalala hoi.

Ukisikia watu wanalala viatu- yaani inamaanisha kwani baada ya mazoezi ya asubuhi yaliyoanza saa 2:30 hadi sa 6:00 mchana, wachezaji wote walikuwa hoi na waliingia vyumbani kwao kupumzika tu hadi muda wa chakula cha mchana.

Wakati timu inajiandaa kutoka kwa mazoezi ya jioni, mvua ilizidi kuchanganya na ikakubaliwa jioni maeozi yasifanyike tena.

Wachezaji wa Yanga wanaonekana kupania haswa kushinda mechi ya Jumamosi, kwani hawfaanyi mzaha hata kidogo kwenye mazoezi na wanahimizana wenyewe kwa wenyewe.

Watani wao wa jadi, Simba SC wao wameweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi hiyo, ambayo wao wanahitaji sare tu kutangaza ubingwa- wakati kwa Yanga inataka heshima tu, kwani matokeo yoyote hayawezi kubadilisha chochote kwao.

Wamekwishajihakikishia nafasi ya tatu- na hawawezi kupanda zaidi ya hapo, maana yake wanapigania heshima ya utani wa jadi na kupoza machungu ya kuvuliwa ubingwa kabla ya mechi ya mwisho ya ligi.

SIMBA NDIO KIDUME WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI - NDIO WAWAKILISHI PEKEE KUTOKA UKANDA HUU .

SASA ni rasmi kwamba Simba SC ndiyo fahari ya nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki ambayo imebaki katika michuano ya makombe yanayosimamiwa na Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, hakuna timu kutoka katika jumuiya hiyo ambayo bado ipo katika michuano hiyo ukiondoa Simba SC. Nchi tano zinaunda Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Orodha hiyo inaonyesha kwamba nchi ya Sudan ndiyo kinara kwa ngazi ya vilabu barani Afrika kufikia sasa baada ya kuingiza timu nne katika michuano ya Ligi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la CAF.
Timu ambazo Sudan imeingiza katika michuano hiyo ni El Merreikh na Al Hilal ambazo zimesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa na Al Ahly Shandy na El Amal ambazo zimesonga mbele katika Kombe la Shirikisho (CAF).
Simba iliifunga 3-0 Al Ahly Shandy 3-0 katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Jumapili na sasa inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 2-0 wiki ijayo ili kusonga mbele.
TOVUTI YA SIMBA

NGORONGORO HEROES YAWASILI SALAMA NCHINI SUDAN!


Na Boniface Wambura
Ngorongoro Heroes imewasili salama hapa Khartoum jana saa 4 usiku kwa ajili ya mechi ya michuano ya
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa Jumamosi kuanzia
saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Khartoum ambao ni wa nyasi bandia, na hakutakuwa na kiingilio kwa
watazamaji.

Awali Ngorongoro Heroes ilitarajiwa kuwasili saa 2.10 usiku, lakini ndege iliyokuwa ipande Nairobi kuja
hapa ilichelewa kuondoka kwa saa moja na nusu kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kulikosababishwa na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha
uwanjani hapo.

Mara baada ya kuwasili Taka Hotel ambapo imefikia, Ngorongoro Heroes ilifanya mazoezi ya saa moja
kuanzia saa 4.30 usiku kwenye Uwanja wa Khartoum ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi dhidi ya
Sudan. Ngorongoro Heroes ilishinda mchezo wa kwanza mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.

Hoteli ya Taka ndipo pia timu ya El Merreikh ya hapa Sudan imeweka kambi yake kujiandaa kwa mechi ya
marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
El Merreikh ililala mabao 2-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Lubumbashi.

Kwa mujibu wa kocha Kim Poulsen, wachezaji wote wako katika hali nzuri na kikosi kitakachoanza kwenye
mechi hiyo kitajulikana kesho (Ijumaa) baada ya mazoezi ya mwisho yatakayofanyika saa 2 usiku kwenye
Uwanja wa Khartoum.

Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Ngorongoro Heroes ni Aishi Manula, Ramadhan Singano, Hassan
Dilunga, Frank Damayo, Frank Sekule, Issa Rashid, Hassan Ramadhan, Saleh Malande, Said Zege, Emily
Mugeta, Jerome Lambele, Samir Ruhava, Simon Msuva, Thomas Ulimwengu, Atupele Green, Dizana
Yarouk, Jamal Mroki na nahodha Omega Seme.

Mwamuzi Aden Abdi Djamal wa Djibouti ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Djamal atasaidiwa na
Wadjibouti wenzake Egueh Yacin Hassan, Bogoreh Salime Fahan na Aden Ali Farah. Waamuzi hao
watawasili kesho (Ijumaa) saa 8 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakati Kamishna wa mechi hiyo
Patrick Naggi kutoka Kenya atawasili leo (Alhamisi) saa 2.10 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.

Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Sudan itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Nigeria. Mechi
ya kwanza itchezwa Julai 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itakuwa kati ya Agosti 10
na 12 mwaka huu.

Ikifanikiwa kuitoa Nigeria, Ngorongoro Heroes itacheza mechi ya raundi ya tatu na mshindi kati ya Afrika
Kusini na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itakuwa ugenini kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu
wakati ya marudiano itakuwa nyumbani Oktoba 6 mwaka huu

papiss demba cisse is on FIRE!

FABRICE MUAMBA AWASHUKURU MASHABIKI

GEORGE ' Blackberry ' ODHIAMBO ATUA AZAM FC

                 HAPA NIKIWA NA Blackberry
       Mzigo mzima ndani ya Sports Bar ya Clouds TV
siku ya jumatatu....

Mshambuliaji raia wa Kenya, George Odhiambo maarufu kama Blackberry leo hii ameanza mazoezi na kikosi cha timu ya Azam.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia alikua mwanansoka bora chipukizi nchini kenya mnamo mwaka 2008 na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mwanansoka bora wa mwaka wa Kenya,
Kabla ya kujiunga na Azam kwa majaribio,Odhiambo alikua anaichezea timu ya RANDERS ya nchini Denmark ,
wakati nikizungumza nae hii leo amesema kwasasa yupo huru kujiunga na timu yoyote baada ya kukatisha mkataba na timu ya Randers.


Personal information
Full name
George Odhiambo Ogutu
Date of birth
(1992-12-31) December 31, 1992 (age 19)
Place of birth
Height
1.75 m (5 ft 9 in)
Playing position
Winger, Forward
Club information
Current club
Number
18
Senior career*
Years
Team
Apps
(Gls)
2009-2011
46
(18)
2011-
2
(0)
National team
2011-
16
(4)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 18 May 2011.
† Appearances (Goals).
‡ National team caps and goals correct as of 4 March 2011