MVUA
kali inayonyesha hivi sasa Bagamoyo, imesababisha klabu ya Yanga
iliyoweka kambi Bagamoyo mkoani Pwani kujiandaa na mechi dhidi ya watani
wa jadi, Simba SC Jumamosi kusitishwa jioni hii.
Mvua hiyo inavuruga programu za mazoezi magumu ya kocha Freddy Felix Minziro, ambaye anawafua haswa wachezaji wa timu hiyo mjini hapa wanalala hoi.
Ukisikia watu wanalala viatu- yaani inamaanisha kwani baada ya mazoezi ya asubuhi yaliyoanza saa 2:30 hadi sa 6:00 mchana, wachezaji wote walikuwa hoi na waliingia vyumbani kwao kupumzika tu hadi muda wa chakula cha mchana.
Wakati timu inajiandaa kutoka kwa mazoezi ya jioni, mvua ilizidi kuchanganya na ikakubaliwa jioni maeozi yasifanyike tena.
Wachezaji wa Yanga wanaonekana kupania haswa kushinda mechi ya Jumamosi, kwani hawfaanyi mzaha hata kidogo kwenye mazoezi na wanahimizana wenyewe kwa wenyewe.
Watani wao wa jadi, Simba SC wao wameweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi hiyo, ambayo wao wanahitaji sare tu kutangaza ubingwa- wakati kwa Yanga inataka heshima tu, kwani matokeo yoyote hayawezi kubadilisha chochote kwao.
Wamekwishajihakikishia nafasi ya tatu- na hawawezi kupanda zaidi ya hapo, maana yake wanapigania heshima ya utani wa jadi na kupoza machungu ya kuvuliwa ubingwa kabla ya mechi ya mwisho ya ligi.

acha utani yanga wanapendezaaaaaaaaa ndani ya uzi huu
ReplyDeleteWANAJANGWANI TUNAFANYA KUFURU MSIMBAZI MAZEE
ReplyDelete