Raisi wa klabu Inter Milan Massimo Moratti amekiri kuwa atakuwa na furaha kama kocha wa England Fabio Capello atarudi Italy kuja kuongoza Inter.
Inter ambayo msimu uliopita walishika nafasi ya pili katika Seria A wamempoteza kocha wao Leonardo ambaye amejiunga na Paris Saint German hivyo kupelekea timu hiyo kukosa mwalimu, na sasa Moratti ameanza mchakato wa kutafuta kocha mpya huku majina yakitajwa kuhusishwa na kibarua vha kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Giuseppe Meazza.
Alipoulizwa kuhusu Capello na vyombo vya habari Italia Moratti amesema: "Nani asiyempenda Fabio? ni kocha mzuri na ningependa kufanya nae kazi."
Capello ambaye kwa sasa bado ana mkataba na Three Lions mpaka baada ya kuisha kwa michuano ya EURO 2012 itayofanyika nchini Poland na Ukraine.
Makocha wengine wanaotajwa kuja kumrithi Leonardo ni pamoja mchezaji wa zamani wa Inter Sinisa Mihajlovic anayefundisha Fiorentina, kocha wa Palermo Delio Rossi, kocha wa zamani wa Geneo Giampiero Gasperini, Louis Van Gaal na makocha wa zamani wa Brazil Dunga na Zico.