Search This Blog
Saturday, July 28, 2012
LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 2 - 0 AZAM FC - YANGA MABINGWA WA KAGAME CUP
90+2: Said Bahanuzi anafunga bao la pili na refa anamaliza mpia hapa. Yanga wanafanikiwa kuutetea ubingwa wao wa Kagame Cup.
87: Said Bahanunzi ananyeshwa kadi ya njano dakika ya 87
85: Dakika tano zimebakia mpira kumalizka, na Azam hawaonyeshi dalili yoyote ya ziada kutafuta bao la kusawazisha huku ukuta wa Yanga ukisimama imara vilivyo.
78: Azam wanamiliki zaidi mpira huku Yanga wakiwa wamerudi nyuma kupaki basi. George Blackberry Odhiambo anapiga shuti kali linalotoka nje sentimita kidogo kutoka langoni.
75: Yanga wanafanya mabadiliko anatoka Gumbo anaingia Juma Seif Kijiko. Mpira unaonekana kupooza na timu zote zikionekana kuchoka.
67: Azam wanafanya mabadiliko, anaingia Mrisho Ngassa anatoka Kipre Tchetche.
56: Yanga nao wanafanikiwa kufika ndani ya sita ya Azam nao wanafuata mkondo wa Azam na wanapoteza. Kwa kifupi timu zote zinatengeneza nafasi ya kufunga lakini safu zao za ushambuliaji zinakosa umakini na wanshindwa kuzitumia.
55: Azam wanaendelea kupoteza nafasi za wazi kuweza kufunga mabao.
DK 46: Kipindi cha pili kinaanza hapa.
45: Mpira ni mapumziko. Azam watajuitia nafasi walizopoteza, Yanga wanacheza wakiwa wanaonyesha hali ya kuutaka ushindi kwa hali na mali, tofauti na Azam wanaocheza wakiwa wame-relax kama tayari wameshinda.
DK 44: Azam wanafanya makosa ya kizembe hapa na Ibrahimu Shikanda anarudisha mpira mfupi nyuma unaomfikia Hamis Kiiza na anweka kimiani goli la kuongoza la Yanga.
DK 40: Rashid Gumbo analeta uhai sana kwenye safu ya mashambulizi ya Yanga - Azam wanacheza mpira zaidi katikati ya uwanja na wanalisogelea sana lango la Yanga lakini wanakosa umakini.
DK 35: Yanga wanalishambulia lango la Yanga na wanajaribu kwa kila kila hali kuweza kupata bao. Azam wenyewe wanacheza zaidi pasi huku wakipoteza nafasi nzuri za kufunga.
DK 30: Azam wanalisogelea sana lango la Yanga lakini wanashindwa kuzitumia nafasi wanazopata - Yanga wanaonekana tishio sana wanapofika kwenye lango la Azam na lolote linaweza kutokea hapa.
DK 20: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, japo Azam wanaendelea kutawala sana safu ya kiungo. Yanga 0 - 0 Azam.
DK 15: Yanga 0 - 0 Azam
DK 10: Azam wanaonekana kumiliki mpira zaidi katika dakika hizi 10 za mwanzo, huku Yanga wakicheza vizuri nyuma na wakishambulia kwa counter attack.
DK 02: Azam wanalishambulia lango la Yanga na John Bocco anakosa goli baada shuti alilopiga kupaa juu ya lango.
DK 01: Mechi ndio inaanza hapa - Azam 0 - 0
Timu ndio zinaingia uwanjani na zinajipanga kukaguliwa. Yanga kama kawaida wamevaa jezi za njano na Azam wamevaa nyeupe.
KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA DHIDI YA AZAM FC KWENYE FAINALI YA KAGAME CUP 2012
1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1
2.Stephano Mwasika - 3
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Rashid Gumbo - 16
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza 'Diego' - 20
11.David Luhende - 29
Subs:
1.Yaw Berko - 19
2.Ladislaus Mbogo - 28
3.Juma Seif 'Kijiko' - 13
4.Idrisa Rashid - 12
5.Shamte Ally - 15
6.Nizar Khalfan - 7
7.Jeryson Tegete - 10
Head Coach: Tom Saintfiet
Ass Coach : Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athuman
Team Doctor : Dr Suphian Juma
Kit Manager : Mahmoud Omary (Mpogolo)
Massagist : Jacob Onyango
Team Manager : Hafidh Saleh
2.Stephano Mwasika - 3
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Rashid Gumbo - 16
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza 'Diego' - 20
11.David Luhende - 29
Subs:
1.Yaw Berko - 19
2.Ladislaus Mbogo - 28
3.Juma Seif 'Kijiko' - 13
4.Idrisa Rashid - 12
5.Shamte Ally - 15
6.Nizar Khalfan - 7
7.Jeryson Tegete - 10
Head Coach: Tom Saintfiet
Ass Coach : Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athuman
Team Doctor : Dr Suphian Juma
Kit Manager : Mahmoud Omary (Mpogolo)
Massagist : Jacob Onyango
Team Manager : Hafidh Saleh
LIVE MATCH CENTRE: AS VITA 2 - 1 APR - KAGAME CUP MSHINDI WA TATU
DK 45: Imebaki daika moja kumaliza dakika 45 za kipindi cha pili.
DK 44: APR wanapata bao moja hapa na kugeuza matokeo kuwa 2-1
DK 35: Vita 2 - APR.
DK 22: AS Vita wanafunga bao la pili.
DK 14: AS VITA 1 - 0 APR
BAADA YA KUSHUKA KIWANGO - RYAN BABEL ASHUSHWA HADI KIKOSI CHA PILI CHA TSG HOFFENHEIM
Baada ya kuonyesha kiwango kisichoridhisha kwa takribani miezi kadhaa iliyopita, mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uholanzi Ryan Babel ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya TSG 1899 Hoffenheim inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Bundesiliga ya Ujerumani - ameshushwa kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha klabu hiyo ilipanda daraja mwaka 2008 na kushika nafasi ya pili kwenye bundesiliga.
Kwa taarifa nilizozipata leo kutoka kwa kocha msaidizi wa TSG Hoffenheim, Rainer Widmayer ni kwamba baada ya manager wa klabu hiyo Markus Babbel kuona kiwango cha mchezaji huyo kikizidi kushuka amemshusha kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha timu hiyo, huku akiwekwa sokoni kwa kuuzwa kwa €5 million, lakini amekuwa hana soko.
HII NDIO INTERVIEW NILIYOFANYA NA KOCHA TSG HOFFENHEIM

KLABU YA TSG HOFFENHEIM YAIALIKA TSC MWANZA KUFANYA NAO MAZOEZI - WALA CHAKULA CHA USIKU PAMOJA
Dauda nilikuwepo |
Nikiwa na wachezaji wa TSG Hoffenheim na TSC Mwanza baada ya mazoezi |
Mazoezi ya pamoja |
Kocha wa TSC Mwanza Bwana Kaijage alipewa zawadi ya jezi ya klabu ya TSG Hoffenheim |
BAADA YA MAZOEZI NAHODHA WA TIMU TSG HOFFENHEIM ALITOA RISALA YA KUWASHUKURU TSC MWANZA MENGINE YAKAENDELEA KATIKA PITA PITA YANGU KWENYE JENGO LA TSG HOFFENHEIM - NIKAINGIA KWENYE LAUNDRY HAPA NI GYM YA ACADEMY YA TSG HOFFENHEIM WABONGO TUIGE HII KITU - PROGRAM NZIMA YA MAZOEZI NDANI YA MWEZI BAADA YA YOTE - HATIMAYE VIJANA WAKAKARIBISHWA DINNER
Friday, July 27, 2012
CRISTIANO RONALDO, DROGBA, ETO'O NA WACHEZAJI WENGINE SITA AMBAO ILIBAKI KIDOGO WASAJILIWE NA ARSENAL
Huku taarifa za kusajiliwa kwa Yann M'Villa zilipokuwa zimepamba moto siku chache kabla ya Euro 2012, kila aliamini kinda hilo la kifaransa litakuwa ndio usajili wa pili Arsene Wenger baada ya Lukas Podolski. Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti Arsenal hawana mpango wa kumsajili tena M'Vila. Hili sio jambo geni kwenye soka na sio geni kwenye klabu ya Arsenal hasa kwenye kipindi hiki cha uongozi wa Arsene Wenger.
Hawa hapa ni wachezaji wengine ambao Wenger alikaribia kuwasaini akiwa Arsenal.
ZLATAN IBRAHIMOVIC
Akiwa na miaka 19, Zlatan alikuwa amekaribia kabisa kujiunga na Arsenal kutoka Malmo kwa ada ya uhamisho wa £3million mwaka 2000, hapo ilikuwa hivyo mpaka Wenger alimpotaka mchezaji afanye trial-majaribio kabla ya kusajiliwa rasmi. Lakini kwa Zlatan hiyo akaona ni dharau akaamua kuachana na Arsenal ambao tayari walishampa jezi.
JUAN MATA
Wakati wa kiangazi mwaka 2011, ambapo mtoto wa Catalunya Cesc Fabregas alipokuwa akililia kurudi nyumbani Nou Camp - na ikaonekana na dhahiri anaondoka Arsenal walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Juan Mta kusaidia kuziba pengo la Cesc. Huku wakiwa na fungu la kutosha walilolipwa na Barca wakaanza kujichelewesha ili kuishinikiza Valencia imuuze kwa bei chee mchezaji wao, Chelsea wakaingilia kati na kutoa kisu kilichohitajika na wakafanikiwa kumsajili kwa ada ya £24 million
PETR CECH
Baada ya kumtongoza kwa muda mrefu, ilionekana kama Cech alikuwa anajiunga na Arsenal akitokea Sparta Prague mwaka 2002. Timu zote zilishakubalina bei na mahitaji binafsi ya mchezaji lakini kibali cha kufanyia kazi kikawa kikwazo kikaleta shida na Arsenal wakaona waachane na mpango wa kumsajili, badala yake akajiunga na timu ya Ufaransa Rennes kabla ya baadae kwenda kujiunga na klabu ambayo imemfanya kuwa moja ya magolikipa bora duniani. Chelsea.
DIDIER DROGBA
Wenger aliwahi kufunguka kwamba alikuwa na nafasi ya kumsajili Drogba kwa pesa ndogo isiyozidi hata mshahara wa wiki wa mchezaji wa Chelsea (£100,00)
" Tulikuwa tunamuangalia vizuri Drogba lakini tulihisi hakuwa tayari kucheza England," Wenger alisema, "Lilikuwa ni kosa kumkosa Didier lakini unapokuwa kwenye soka, kila mtu anaweza kuelewa. Hata hivyo tayari tulikuwa na Thierry Henry."
SAMUEL ETO'O
Akiwa ndio anaondoka Real Mallorca kama mfungaji wao bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya La Liga akiwa amecheza misimu mitatu tu, Eto'o alipewa ofa kujiunga na Arsenal in 2004 na Wenger, ingawa mshambuliaji huyo na tabia yake ya kujisikia ilimfanya kocha wa Arsenal ajiulize mara mbili mbili amsajili au la mchezaji ambaye hivi karibuni alisema kumtandka wakala wake ilikuwa ni idea nzuri. Arsenal hatimaye wakajitoa kwenye mbio za kumsajili mcameroon ambaye nae alsema chaguo lake lilikuwa ni Barcelona.
CLAUDIO MAKELELE
Mwaka 1996 Wenger alikamilisha usajili wa kiungo Patrick Vieira kuja Arsenal. Wiki moja baadae akapokea simu kutoka Nantes ikimuuliza kama Wenger atakuwa tayari kumsajili kiungo Makelele.
Mazungumzo yakafanyika na dili la Makelele kuelekea London lilikuwa karibu (kwa mujibu wa mahojiano ya Wenger aliyoyafanya 2006) ingawa Wenger akajitoa kwenye bio za kumsajili kiungo huyo, akimtegemea Vieira.
YAYA TOURE
Huku kaka yake mkubwa Kolo akiwa ameshasajiliwa tayari, Arsenal walionekana kama wanataka kuuteka ukoo wote wa Toure, walimpotaka kumsajili Yaya. Alienda london na hata kufanikiwa kuichezea Arsenal ya vijana kwa mchezo mmoja kabla ya suala la vibali vya kazi kuleta tena utata na Toure akaenda kujiunga na Olympiakos kalba ya kuja kuwa mmoja ya viungo bora kabisa wa kati duniani akiwa na Barcelona na Man City.
CRISTIANO RONALDO
Stori ilikuwa hivi...... akiwa mdogo Ronaldo alionyeshwa jiji la London lilivyo na kupelekwa mpaka uwanja wa Arsenal na kupewa jezi la Gunners ikiwa na jina lake nyuma na Arsene Wenger mwenyewe.
Arsenal hawakuishia hapo walifiikia mpaka hatua ya kukubaliana ada ya uhamisho ya £4million na Sporting Lisbon.
Then, kwa bahati mbaya, Lisbon wakacheza na Machester United in 2003 kufungua uwanja wao mpya. Ronaldo akacheza mchezo huo na kuwapeleka puta sana United, na mwishowe Sporting wakashinda kwa 3-1. Wakiwa kwenye ndege kurudi England wachezaji wa Man U wakamshawishi Fergie amsajili CR7, na babu nae akatuma ofa ya £12million kisha kocha msaidizi wa United wakati huo, Carlos Queiroz akaenda kuongea na Ronaldo na wakala wake na akafanikisha dili hilo ambalo limeigharimu sana Arsenal.
BARUA YA WAZI KWA ROBIN VAN PERSIE
Mpendwa RVP
Ningependa kukupongeza kwa kuwa msimu mzuri uliokuwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Ulimaliza msimu bila kupata majeruhi, ukishinda tuzo nyingi, na kuvunja rekodi za klabu na ligi kuu; kitu ambacho kitaenda katika vitabu vya historia ya Arsenal.
Ulileta utulivu, amani na heshima kwenye kikosi ndani na nje ya uwanja.
Mtu mkubwa, mwenye majukumu mazito; Ulitekeleza majukumu yako vizuri, tena vizuri zaidi ya vile nilivyotegemea.
Kama mshabiki wa Arsenal, Nimeshuhudia vipaji vingi na ninakiri, umebarikiwa sana na ninadiriki kukuita "genius".
Lakini, tarehe 4 ya mwezi July 2012, ulishusha bomu ambalo limeigeuza Arsenal kuwa sehemu iliyochafuka, ulipotoa taarifa iliyoelezea nia yako ya kutosaini mkataba mpya ambao klabu ilikuwa imekupa.
Mimi ni nani kukuambia cha kufanya? Lakini najua kitu kimoja kwa hakika, Arsenal ilikuwa Arsenal, Arsenal ni Arsenal, na itaendelea kuwa Arsenal.
Watu wengi wamekuwa wakitushambulia kwa kukosa tamaa ya mafanikio, jambo ambalo silipingi, lakini kwa kipindi hiki cha usajili tumekuwa wepesi sana katika kusajili, tayari tumemsajili Lukas Podolski na Olivier Giroud.
Nimekuwa nikiamini ilikuwa step iliyokuwa na mweleko mzuri, kuwasajili wachezaji ambao tayari wameshathibitisha kuwa ni daraja la juu ili kuweza kukupunguzia mzigo wewe uliokuwa nao msimu uliopita.
Pamoja na kuwa nyuma kwenye nafasi ya tatu, lakini tuliweza kufuzu kushiriki kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya msimu, huku tukivishinda vilabu vilivyotumia fedha nyingi kwenye usajili kama Liverpool, Tottenham na Chelsea ambao wamefuzu kwa sababu tu walikuwa mabingwa wa ulaya.
Umekuwa kwenye klabu hii kwa miaka nane sasa, naweza kusema nimekushuhudia dimbani kwa misimu miwili tu. Katika misimu hii miwili ulikuwa unacheza vizuri kabisa, ukifunga magoli muhimu na mazuri.
Misimu sita iliyobaki ilikuwa imejaa na kuandamwa na majeruhi, majeruhi na majeruhi zaidi ambayo mwishowe yalikupa jina ya "The Man of Glass".
Wakati ukiwa kwenye nyakati ngumu za maisha yako ya soka, kipindi ambacho baadhi ya mashabiki walitaka uondoke, unadhani nani alikusimamia pale? Arsene Wenger! Sasa fikiri angekubalina na matakwa ya mashabiki waliotaka uondoke, ungekuwa kama alivyo Alberto Aquilani sasa hivi.
Kama ninavyopenda kukupongeza juu ya kiwango chako msimu uliopita, pia naamini kulikuwa na kitu kilichoitwa "teamwork".
Haikuwa tu teamwork, kilikuwa ni kikosi chote cha Arsenal kikicheza kama familia. Umoja ndani ya kikosi ulikuwa na nguvu, wachezaji wenzio walikuwa tayri kufanya lolote kwa ajili yako.
Kama unakumbuka mchezo dhidi ya Wigan katika uwanja wa DW stadium ambapo tulitoka na ushindi wa 4-0, Theo Walcott alikuwa na nafasi ya kufunga, lakini alichagua kuchelewesha mpira, kabla ya kukupa wewe assists na ukafunga huku ukizidi kujiongezea wastani mkubwa wa magoli ya kufunga.
Kila mtu alitaka ufanikiwe.
Namuangalia Wayne Rooney na Antonio Valencia, najiuliza ni mara ngapi nimeshuhudia wanavyosadiana dimbani, ushirikiano na umoja wa wachezaji ni kitu ambacho fedha haiwezi kununua.
Mfano mzuri tumehushudia hivi karibuni kwenye michuano ya Euro 2012 iliyomalizika hivi karibuni, alikuwa wapi yule Van Persie wa msimu uliopita wa Arsenal?
Sasa tamaa yako ya mafanikio imekuwa sana kuliko ya klabu ndani ya msimu mmoja mzuri?
Wapi ilipokuwepo tamaa yako ya mafanikio mwezi uliopita mlipotolewa kwa aibu kwenye Euro 2012, ilikuwa wapi tamaa yako ya mafanikio kipindi Arsenal wanakutibia majeraha yako kwa miaka, ilikuwa wapi tamaa yako ya mafanikio ulipokuwa ukipokea pesa nyingi kwa kazi usioifanya?
Muda wa kuilipa fadhila Arsenal kwa imani waliyoinyesha kwako, tamaa yako ya mafanikio ghafla imekuwa kubwa?
Sikulaumu sana wewe, Namlaumu Arsene Wenger.
Imani yake isiyokufa na mapenzi yake kwa wachezaji kama Matheieu Flamini, Samir Nasri, Gael Clichy, Cesc Fabregas na wengine, ndio inayomponza.
Gianfranco Zola alikuwa moja ya wachezaji waliobarikiwa vipaji vikubwa ambao wamewahi kuonekana kwenye premier league. Alipata mafanikio gani na Chelsea? Lakini jina lake litaendelea kubaki kule juu kama gwiji kila aina ya maneno unayoweza kuyatumia.
Mwisho, ningependa kukushukuru kwa muda mzuri uliotuletea hapa, magoli mazuri uliyofunga(sina idadi kamili).
Nakutakia mafanikio mema kwenye maisha yako ya soka, nakutakia mafaniko kwenye klabu yako mpya. Nenda kashinde makombe ndugu.
Pindi utakapoondoka nakuomba unifanyie jambo moja, sahau kila kitu kuhusu Arsenal na tafadhali usijaribu kutuzungumzia.
Badge iliyopo kwenye jezi pembeni mwa kifua siku zote itakuwa kubwa na thamani kuliko jina lililopo nyuma.
Kwaheri RVP

Imeandikwa na shabiki wa Arsenal.
BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KUSHUTUSHWA NA KUONDOKA KWA MILOVAN - MSEMAJI WA KLABU ATOA MAJIBU
Salaam...Jamani, Milovan Cirkovic ana udhuru na safari yake ilikuwa imepangwa regardless matokeo ya Azam....Kama tungeingia fainali, angecheza kwanza mechi na kuondoka kesho yake....Tatizo kitu kidogo tu Simba watu wanaongeza chumvi na kwa bahati mbaya, sisi washabiki wa Wekundu tuna mioyo myepesi sana...Kitu kidogo tu tukiambiwa tunalegea kabisa...Wenzetu waliambiwa wanaletewa Maximo hapa, chenga....Wapo tu.....Wamepigwa tano hapa.....Wapo tu....Wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu...Wapo tu....Sisi ikiandikwa Okwi yuko Dar watu wanakuja na visu ofisini.....Yaani nashindwa hata kuelewa....Inaumiza lakini, WHY tuko hivi? Tuko on the back foot utadhani sisi ndiyo the worst team in the country!
· · · 2 hours ago- 6 people like this.
- Fred Mtakikiukweli Kamwaga ameuka kama mtunga taarabu tu. sasa wewe mtu kama ni msemaji wa club wapi na wapi uanze kuzungumzia mambo ya Maximo wakati wewe unayakuzungumzia ya club yako. Toa taarifa ya club yako watu wakuelewe! Yaani umetoka kabisa kw...See Moreabout an hour ago · · 2
- Salim Bongoland Jamani simba timu ya maendeleo imeendelea kimpira. Walisema hayoabout an hour ago via mobile ·
- Fred Mtaki tatizo mnawaendea kina Kamwaga na mavisu ofisini!
- Kazukamwe Bahanuz Yanga Hana lolote huyo55 minutes ago via mobile ·
- Anthony Siame kamwaga hao ndiyo mashabiki wa timu zetu hasa simba na yanga kwani we mgeni nao33 minutes ago · · 1
- Lusekelo Hudson duu kwa viongozi hawa mpira bongo una safari ndefu sana18 minutes ago · · 1
- Hassan Abbas Pole kaka@Kamwaga...
- Mpeli Jr NgonywikeNdugu yangu Ezekiel Kamwaga pole sana!!! Najua upo ktk kipindi cha majaribu ya kibarua chako na migogoro klabuni. Laiti usemaji wa klabu ungekuwa ndo hivi basi ajira Tanzania zingekuwa nje nje . . . . . Maximo, goli tano na nafasi ya 3!!! H...See More5 minutes ago · · 1
- Epafraditto Frank kaka leo umejitoa muhanga kusema kweli, ni vizuri lakini angalia kauli hii isije kukugeuka kaka clifford ndimbo, simba nawajua, hawataki kuambiwa ukweli na hivi wana machungu ya kichapo......take care..all in all big for good comments and clearance of "poor mindset among simbas fans
- Ayoub Jay kawaida simba ni mnyama mkali sana na hatari porini. Hasira za mashabiki wenu ni sawa na hasira za ukali wa simba.....usiwashangae, jina la timu linachangia washabiki kufanana na mnyama halisi..... Iko siku watakutafuna kabisa,....ohoo...shauri yako wee.....
Subscribe to:
Posts (Atom)