Kipre Tchetche |
Search This Blog
Saturday, April 6, 2013
MANCHESTER UNITED KUELEKEA UBINGWA WA 20 WA EPL NA NDEGE INAYOPAA BILA MABAWA
Inakuaje Manchester United inapaa kwenye EPL bila mawinga wao kuwa kwenye kiwango bora?
Kama mshabiki wa United, ninafurahishwa sana na uongozi wa pointi 15 kwenye premier league mbele ya mahasimu wetu wa karibu Manchester City. Ni kweli pia sijafurahishwa na kutofanya vizuri kwenye michuano mingine kama vile FA Cup, Caital One na Champions League. Msimu huu ungeweza kuwa mzuri sana kama wachezaji ambao wana jukumu kubwa katika kuifanya United icheze vizuri - mawinga wangekuwa kwenye kiwango bora - lakini kwa bahati mbaya tangu nimekuwa mshabiki wa timu hii sijawahi kuona mawinga wakicheza ovyo kama msimu huu.
Ukimtoa Giggs, Kagawa na muda mwingine Cleverley, tuna mawinga wa asili watatu tu ambao wapo kwenye kikosi cha kwanza. Wote watatu hawajakuwa kwenye kiwango kizuri. Valencia na udhaifu wake wa kutumia mguu mmoja umewafanya mabeki kumzoea, Ashley Young ndio kawa kama Stewart Downing wetu, wakati Nani akiwa bado na ujuzi mkubwa lakini bado hajakomaa kiakili ya soka kama ilivyo kwa mreno mwenzie Cristiano Ronaldo.
Kitu cha kusikitisha ni kwamba United imekuwa ikicheza kwa mfumo wa kutegemea sana mawinga kwa miaka mingi sasa. Toka enzi za akina George Best mpaka wakati wa Cristiano Ronaldo, wachezaji bora wa timu hii hasa wakati wa Fergie wamekuwa ni wanaocheza pembeni.
Nafahamu United wapo kwenye kilele cha EPL na wanaweza kushinda ubingwa kabla ya kuisha kwa msimu, lakini mie kama mshabiki wa timu hii sijafurahishwa na kiwango chetu, hasa kwa upande wa mawinga. Nashindwa hata kuwafananisha na alivyo flop mwenye thamani ya £20 million wa Liverpool Stewart Downing, msimu huu. Left Wing Jesus mpaka sasa afadhali amefunga mabao matatu akiwa na Liverpool kwenye ligi. Je kuna yoyote ambaye anaweza kuotea ni mabao mangapi yamefungwa na Young, Valencia na Nani mpaka kufikia hapa? Bao 1 tu, limefungwa na Nani. Naamini washabiki wa Liverpool wanatucheka sasa ukifikiria namna tulivyowasakama na flop wao Downing.
Ni vipi Sir Alex ameweza kuisadia kuiweka Manchester United katika nafasi ya kwanza bila kuwa na msaada muhimu kutoka kwa wachezaji wa pembeni - ni jambo la kushangaza. Au badilisha jina la "Sir Alex" weka "Robin van Persie" katika sentensi iliyopita, labda unaweza ukapata jibu. Lakini kiuhalisia sidhani kama msimu ujao kwa kiwango cha hawa mawinga wetu waliopo tutaweza kushindania ubingwa wa EPL - SAHAU KUHUSU BARANI ULAYA.
Mpaka sasa, Fergie ameweza kuwatumia wachezaji wengine kwenye nafasi za pembeni pale inapohitajika. Ryan Giggs alikuwa ndio winga bora nchini England kwa muda fulani, lakini sasa umri umeanza kumtupa japokuwa muda mwingine amekuwa akipewa majukumu mazito na anayamudu. Shinji Kagawa amefanya kazi nzuri upande wa kushoto, lakini sio winga. Danny Welbeck ni mchezaji mwingine ambaye kwa msimu huu amekuwa akichezeshwa kwenye winga, lakini tangu aanze kutumika hivyo hajafunga goli hata moja. Hawa wachezaji wanahitaji kucheza kwenye nafasi zao ili kucheza kwenye kiwango kizuri, aihitaji kuwatemea wao wakati mawinga wapo.
Nangalia kwa wivu mkubwa kwa mawinga wa City, Chelsea, Arsenal, Spurs na hata Liverpool wanapokuwa na wachezaji wa pembeni wanaocheza kwa viwango vya juu kwa muda mrefu kama vile akina Silva, Mata, Hazard, Walcott, Podolski, Bale, hata kinda Sterling, hawa ni wachezaji ambao wanaweza kuingia kwenye kikosi cha United na kutulia vizuri kabisa.
Tumaini langu ni kwamba msimu ujao Wilfried Zaha atakuwa mzuri na kuimarika kwa ubora kuzidi hata Walcott.

HUKU MJI WA MANCHESTER UKIGAWANYIKA KWA RANGI 2 - HOTELI MOJA YAFANYA MAKUBWA YAANDA VYUMBA VYENYE KUMBUKUMBU, VITU NA MAJINA YA KIHISTORIA YA UNITED NA CITY
Huku muda ukizidi kusogea kuelekea mchezo wa mahasimu wa jiji la Manchester siku ya Jumatatu, mji wenyewe umekuwa katika hali ya kujigawanya kwenye rangi mbili bluu na nyekundu kama inavyokuwa kila mchezo huu unapokaribia. Ingawa safari hii mbio za ubingwa zikiwa zimekaribia kuisha na kufikia tamati.
Na wale washabiki wa timu hizi ambao watakuwa wanatoka sehemu nyingine tofauti na Manchester wametaarishiwa Hotel ya Piccadilly's Premier Inn ambao itakuwa imegawanyika kwa floors mbili tofauti zenye rangi nyekundu na bluu.
Wakati baa za katikati ya mji zikiwa tayari zina himaya aidha ya United au City, hotel hiyo iliyopo maili kadhaa kutoka uwanja wa Old Trafford imechukua njia tofauti kuwapa hali washabiki watakaofikia hotelini kwa ajili ya mchezo husika.
Wameandaa vyumba vilivyopewa kumbukumbu na watu muhimu wa vilabu hivyo viwili vya mji wa Manchester.
Hii sehemu ya vyumba vya washabiki wa Man City
Mashabiki wa United wametaarishiwa vyumba vyenye majina kama vile fans Room 99 - 'The Treble Room' - and Room 19 - 'The Champions Suite' - ili kuwapa hali ya kwenda kuipa nguvu timu yao waweze kujihakikishia ubingwa mwingine wa 20 wa kihistoria katika Premier League .
Kwa upande wa japokuwa baadhi wameanza kukata tamaa ya ubingwa msimu huu wametaarishia chumba cha kujikumbusha ubingwa wao kwa kukumbuka muda wa goli la Aguero lilowapa ubingwa kwa chumba kimojawapo kupewa jina la "The Aguero Suite' in room '93:20'.
Wakati mashabiki ambao hawashabikii upande wowote baina ya timu hizo mbili wamepewa chumba kilichopewa jina la watu waliozitumikia timu zote mbili 'Dennis Law Suite' na 'The Sparky Mark Hughes Suite',

Chumba hiki ni maalum kwa washabiki wa Man City kujikumbusha muda ambao Aguero alipofunga goli la ushindi ya QPR na kuipa City ubingwa msimu uliopita.
Mashabiki wa United wametaarishiwa vyumba vyenye majina kama vile fans Room 99 - 'The Treble Room' - and Room 19 - 'The Champions Suite' - ili kuwapa hali ya kwenda kuipa nguvu timu yao waweze kujihakikishia ubingwa mwingine wa 20 wa kihistoria katika Premier League .
Kwa upande wa japokuwa baadhi wameanza kukata tamaa ya ubingwa msimu huu wametaarishia chumba cha kujikumbusha ubingwa wao kwa kukumbuka muda wa goli la Aguero lilowapa ubingwa kwa chumba kimojawapo kupewa jina la "The Aguero Suite' in room '93:20'.
Wakati mashabiki ambao hawashabikii upande wowote baina ya timu hizo mbili wamepewa chumba kilichopewa jina la watu waliozitumikia timu zote mbili 'Dennis Law Suite' na 'The Sparky Mark Hughes Suite',
Friday, April 5, 2013
MAREFA WAFUNGIWA KWA KUPEWA RUSHWA YA NGONO ILI WASAIDIE TIMU KUSHINDA
Kutoka Reuters:
Refa Ali Sabbagh na wasaidizi wake Ali Eid na Abdallah Taleb waliondolewa kwenye kusimamia mechi na nafasi zao kujazwa na waamuzi wengine kutoka Thailand na Malaysia katika mchezo kati ya Tampines Rovers vs East Bengal ya India mchezo ulioisha kwa wahindi kushinda 4-2 siku ya jumatano.
Waamuzi hao wa Kilabanoni walichukuliwa na kupelekwa katika taasisi ya kuzuia rushwa ya Singapore na baadae mahakamani." Ilisema taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo ya kupambana na rushwa Singapore.
BLOGERS FC YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO KUNG'ARISHA MEDIA DAY KESHO
Mkurugenzi wa Hoteli ya Sapphire Court ya Jijini Dar es Salaam, Abdulfatah Salim (kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Nahodha wa timu ya wamiliki wa Magazeti 'Tando' Blogers Fc, Muhidin Sufiani, ambaye ni mmiliki wa mtanda wa www.sufianimafoto.com, kwa ajili ya kushiriki katika Bonanza maalum la waandishi Medi Day linalofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni kesho. Katikati ni Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki Mroki. Timu hiyo ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika michezo na bonanza kama hilo, inatarajia kushiriki katika michezo yote itakayo chezwa hiyo kesho, ikiwa ni pamoja na Soka, Netiboli, Kukimbiza Kuku, Kukimbia na Magunia, Kuvuta Kamba, Kucheza Pool, Kuimba na Kudansi 'Sebene' na mingineyo.
Makabidhiano yakiendelea, hii ni Jezi ya Kipa.
Nahodha wa timu hiyo Sufianimafoto (kushoto) akiwa na Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki Mroki, wakiwa na Vifaa vilivyokabidhiwa.
***************************************
HOTELI ya Sapphire Court iliyopo makutano ya mitaa ya Swahili na Lindi, Dar es Salaam leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya wamiliki wa magazeti tando (Blogers FC) kwa ajili ya Bonanza la Media Day, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Sapphire, hoteli iliyojizolea umaarufu mkubwa kwa sasa nchini, Abdulfatah Salim Saleh amesema ameamua kukabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono timu hiyo mpya inayoanzishwa katika tasniya ya michezo nchini.
“Nilipopata ombi lenu, sikutaka hata kujifikiria, nilisema nitawasadia, na huu ni mwanzo tu. Naahidi kushirikiana nanyi zaidi na zaidi na ninawakaribisheni wakati wowote, mimi ni shabiki wa timu yenu kuanzia sasa,”alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Muda wa Blogers FC, Mroky Mroky alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo na wanaahidi kudumisha uhusiano mzuri na Sapphire.
“Wazo hili la kuanzisha timu ni la muda mrefu, lakini lilikuwa likisuasua, ila tukaamua kwa vyovyote lazima tutokee kwenye Media Day ya mwaka huu.
Tulipofikiria suala la wapi tutapata vifaa vya michezo, vichwa vilituuma kidogo, lakini tunashukuru Sapphier wametuliza maumivu hayo,”alisema Mroky.
Naye Nahodha wa Blogers FC, Muhiddin Sufiani amesema kwamba baada ya kupata vifaa hicyo kesho wanatarajia kuanza kuonyesha cheche zao kesho katika Bonanza la Media Day, lengo likiwa ni kubeba ubingwa upande wa soka na kutwaa pia mataji mengine madogo madogo.
Miongoni mwa wachezaji nyota wanaotarajiwa kuichezea Blogers FC kesho ni Issa Michizi, Majjid Mjengwa, Sufiani mwenyewe, Majuto Omary, Joseph Lukaza, Shaffih Dauda, Saleh Ally, Mahmoud Zubeiry, Millard Ayo na John Bukuku.
Bonanza la wanahabari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), litafanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders, chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pamoja na wanahabari kuchuana katika michezo mbalimbali, lakini Bonanza hilo pia litapambwa na burudani ya bendi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern.
Kutakuwa pia na mechi maalum baina ya wanahabari ambao wameoa na wale ambao hawajaoa utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida baina ya vyombo vya habari kumalizika.
Bonanza litaanza saa tatu asubuhi kwa washiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, wavu, kuruka kichura, aina mbalimbali za riadha, kuvuta kamba na kucheza muziki. Bonanza litamalizika saa moja usiku.
Source: http://www.sufianimafoto.com/
DRFA YATANGAZA KUANZA KWA LIGI DARAJA LA PILI
Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),kimetangaza kuanza kwa ligi daraja la pili mkoa wa Dar es Salaam,hatua ya sita bora Aprili 9 mwaka huu ktk viwanja vya shule ya Benjamin William Mkapa,Kinesi na Airwing.Mechi za ufunguzi siku hiyo,Boom FC vs Shariff Star(airwing),Day Break vs Friends Rangers(makurumla),Red Coast vs Abajalo(kinesi).Mohamed Mharizo,Ofisa Habari DRFA.
CLINT DEMPSEY: MAANDALIZI YA KIAKILI KABLA YA KUCHEZA MECHI
Ni namna gani unajiandaa kiakili kabla ya mchezo?
Najaribu sana kutokuwa na wasiwasi kuhusu mechi husika, msongo wa mawazo ya namna yoyote unaweza ukawa kikwazo kwenye uwezo wako uwanjani. Asubuhi ya siku ya mchezo napendelea kuangalia katuni na mtoto wangu wa kike, then tunahamia kidogo kwenye Dora The Explorer au Mickey Mouse club. Nadhani klabu ina wanasaikolojia wa michezo ambao wanaweza kukusaidia, lakini mie huwa siwatumii, nina familia yangu ambao wananisaidia kwenye vitu vya namna hiyo.
Je kuna mbinu za kiakili unzotumia kama vile kujenga taswira kichwani mwako?
Muda mwingine huwa najaribu kufikiria kuhusu kufunga goli, lakini huwa sifikirii sana kuhusu hilo kwa sababu vitu kama hivyo vinaweza vikakuletea msongo wa mawazo ambayo sio mzuri. Na ikiwa inatokea hali hiyo basi labda sio siku kadhaa kabla ya mechi, labda kwenye basi kuelekea dimbani, mara nyingi wakati wa kwenda uwanjani huwa nasikiliza muziki na kujenga taswira ya mchezo utakavyokuwa. Napendelea kusikiliza muziki wa rap ili niweze kupata hali ya kucheza mechi, nawasikiliza watu kama Lil Wayne na Slim Thug.
Unapoamka siku ya mechi huwa unajiandaa vipi kabla ya mchezo husika?
Watalaamu huwa wanashauri kupata mlo wa asubuhi na mchana, lakini mie ninapendelea kula kiasi kidogo sana, na kulala sana kadri inavyowezekana. Huwa nachelewa sana kuamka siku ya mechi, labda saa 5 mpaka 6, na baada ya hapo napata naenda kupata msosi kiasi. Kwa kawaida tunatakiwa kuwa uwanjani kuanzia saa saba 7 na robo ili kuangalia baadhi ya mikanda ya wapinzani, ili kuhakikisha kila mchezaji na benchi la ufundi wanatambua nini cha kukitegemea uwanjani.
Nini unapendelea kufanya kabla ya kipenga kupulizwa?
Wakati ninapotoka kupasha misuli kawaida huwa napata japo keki, pia napendelea kupata Lucozade na kabla ya ya kwenda dimbani kwa ajili ya kuanza kipute nakunywa maji na nusu ya kinywaji cha kuongeza, then baada ya hapo nakuwa tayari.

BAADA YA ODEMWINGIE NA EMENIKE - SASA YOBO NAE ADAI KUTOHESHIMIWA NA KOCHA STEPHEN KESHI
Yobo anamfuatia mshambuliaji wa West Brom Peter Odemwingie na Emmanuel Emenike, ambao wote kwa pamoja wamesema kwamba kocha huyo amekuwa akiwatendea ndivyo sivyo.
Mlinzi wa Fenerbahce Yobo anaamini kutokuelewana baina ya kocha na wachezaji kunaweza kuondoshwa na ikiwa kutakuwa namna bora ya kuwasiliana na baina ya kocha na wachezaji, hasa wakongwe.
Mlinzi huyo mwenye miaka 32, ambaye ndiye mchezaji wa Nigeria aliyecheza mechi nyingi kuliko wote(95), amesema anahisi kutoheshimiwa na Keshi baada ya kocha huyo kushindwa kumtaarifu kwamba asingemwita kwenye mechi iliyopita dhidi ya Kenya.
"Nimekuwa na timu ya taifa kwa takribani miaka 10, sitegemei kucheza kila mchezo sasa ikiwa nashindwa kujitoa kwa yote," Yobo alikiambia kituo cha BBC Sport.
"Lakini tabia ya Keshi inakatisha sana tamaa. Sijawahi kutaka kutendea tofauti na wengine, ninachohitaji ni heshima tu ninayostahili ambayo mie nimekuwa nikiitoa kwa taifa langu na makocha wote waliopita.
"Sitokuwepo kuitumikia Nigeria milele, lakini inabidi wachezaji wasiwe wanastaafu kuichezea Super Eagles wakiwa na huzuni au kutokuwa na furaha kama inavyotokea siku za hivi karibuni.Unapowafanyia dharau wachezaji wakongwe wale chipukizi wanaona mfano huo mbaya ndani ya timu."
Yobo aliisadia Nigeria kubeba ubingwa wa AFCON 2013 nchini South Africa mwezi February lakini ameshasema kwamba michuano hiyo ndio ilikuwa ya mwisho kwake.
Na akasisitiza kwamba yeye si mmoja ya wachezaji wakongwe wanaotaka kuziba nafasi kwa chipukizi na angependa kuwaona wakikua na kuwa wachezaji wazuri watakaoiletea mafanikio Super Eagles.
"Nafahamu sitoweza tena kushiriki kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika. Wachezaji wachanga wanastahili kupata nafasi wakiwa wanachipukia kama mimi nilivyopata huko nyuma wakati nakua."
Japokuwa, Yobo anaamini bado anaweza kutoa mchango kwa timu yake ya taifa na ataendelea kuichezea Super Eagles japo kwa muda fulani mfupi.
"Sina tofauti na yoyote - napenda kuitumikia nchi yangu na sitoweza kuyapa mgongo majukumu yangu kwa nchi yangu," alisema
"Kwa michuano ya kombe la Mabara na Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil, japokuwa kwa sasa inaonekana sina nafasi kwa sababu kocha hajaniita, lakini nitaitwa ningependa kwanza kuongea na Keshi vitu kadhaa, then nitapaki mabegi yangu na kujiunga na kambi. Ikiwa sitochaguliwa then nitaendelea kuitumikia klabu yangu ya Fenerbahce."
Keshi, kwa upande wake amesema hafurahishwi kuona baadhi ya wachezaji wamekuwa wakinung'unika hadharani.
"Sipendi kujiingiza kwenye mambo ya wachezaji na vyombo vya habari, ningependelea waje kuzungumza na mimi mwenyewe juu ya madai yoyte waliyonayo dhidi yangu,"Keshi alikiambia kituo cha BBC.
BAADA YA KUWACHINJA WABOTSWANA KWAO - SAMATTA SASA KUIVUSHA MAZEMBE JUMAPILI MABINGWA WA AFRIKA?
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania ameuanza vizuri mwaka 2013 katika klabu na timu ya taifa baada ya kufunga mabao matatu katika michezo miwili aliyocheza hivi karibuni.
Samata amereja Mazembe akiwa na hali kubwa baada ya kufunga mabao mawili kwa Taifa Stars iliyoshinda 3-1 nyumbani dhidi ya Morocco jijini Dar-es-Salaam katika mchezo wa kusaka kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Kiwango chake kimekuwa ni habari njema kwa kocha wa Mazembe, Lamine Ndiaye mwenye matumaini ya kuiongoza timu hiyo ya DR Congo kuibwaga Mochudi katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe kwa sasa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Mochudi ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 16 jijini Gaborone, ambapo goli hilo pekee lilifungwa na Samata.
Pamoja na ukweli kwamba ubora wa Mazembe unamtegemea Samata, kocha wa Mochudi, Madinda Ndlovu bado anaamini kuwa kikosi chake kitafanya maajabu Lubumbashi hapo Jumapili.
"Bado hatujakata tamaa pamoja na kuwa tumefunga bao moja nyumbani kwetu,” alisema Ndlovu.
Wakati huo huo; hakuna timu iliyowahi kuifunga Mazembe jijini Lubumbashi kwa zaidi ya miaka kumi sasa katika mashindano haya ya Afrika.
EXCLUSIVE: KABURU AKANUSHA KUIHUJUMU SIMBA - ASEMA KUTOZIBWA KWA PENGO LA OKWI, MAFISANGO NA YONDANI NDIO CHANZO WA KUFANYA VIBAYA
ALIYEKUWA makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema
anawashangaa watu wanaomuhusisha na vitendo vya kuihujumu timu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu inayoendelea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaburu aliyejiuzulu wadhifa wake katika klabu ya Simba hivi karibuni alisema watu wanaomshutumu kuihujumu Simba wana nia ya kumchafua na kumgombanisha na Wanasimba wenzake bila ya sababu za msingi.
"Wachezaji wote waliosajiliwa na Simba ni mali ya klabu ya Simba na wanalipwa mishahara na klabu hiyo na sio mtu binafsi.
"Watu wanashindwa kujiuliza baada ya kuchukua ubingwa msimu uliopita Simba imewapoteza nyota wake Kelvin Yondani, marehemu Patrick Mafisango na Emmanuel Okwi, Je? nafasi zao zimezibwa na nani?, wanatakiwa kujiuliza hivyo na siyo kuchafua watu wengine.
"Tatizo la Simba lilikuwa katika safu ya ulinzi, lakini halikuzibwa, wamemuuza Okwi, nafasi yake haikuzibwa sasa leo watu watasema wachezaji wanatumika kuhujumu timu hiyo siyo kweli, sababu ni mapengo ya baadhi ya wachezaji hayakuzibwa,"alisema Kaburu.
Alisema yeye bado ni mwanachama halali wa Simba na ataendelea kutoa michango yake kama mwanachama na endapo atachaguliwa katika kamati yoyote yupo tayari kwa sharti la kumalizika kwa matatizo yaliyopo katika klabu hiyo kwa sasa.

DEMBA BA: HAYA NDIO MAANDALIZI YANGU YA SIKU NZIMA KABLA YA MECHI KUBWA
Alfajiri
“Nikiwa kama muislamu najaribu kuwa nasali mara tano kwa siku. Sala ya alfajiri huwa ndio ya kwanza - hivyo mara nyingi naamka mpaema na kusali, kusali ni moja ya sehemu kubwa ya maisha yangu”Saa 4 Asubuhi
“Siku zote huwa nalala kabla ya 11.30pm, lakini silali sana. Ikiwa tunacheza mechi 3pm siku ya Saturday kawaida naamka mida ya saa 4-5 asubuhi.Saa 4.30 asubuhi
“Pindi niamkapo napendelea kula mayai. Mayai ni mazuri na pia kuna chakula fulani cha kisenegal kinaitwa thiakry. Ni mchanganyiko wa yoghurt na aina fulani ya ngano, pamoja na sukari ndani yake.”Saa 5 asubuhi
“Ikiwa tunacheza nyumbani napendelea kukaa nyumbani na familia yangu na kupumzika. Ni jambo zuri kuwa nao karibu kwa sababu wanaiondoa akili kwenye kuifikiria mechi.”Saa 5.30 asubuhi
“Napendelea kuruka kamba asubuhi. Ni zoezi zuri kwa moyo wangu, linatengeneza vizuri mapigo yangu ya moyo hali ambayo inaniandaa vizuri kwa mchezo.”Saa 7 mchana
“Huwa naenda uwanjani masaa mawili kabla ya mchezo. Pindi ninapofika uwanjani naanza kuweka akili yangu kwenye mchezo, wakati huo huo nakuwa nimeweka headphones kwenye masikio yangu na kusikiliza Quran –kitu hichi kinakuwa kizuri sana kwa akili yangu.”Saa 7.30 mchana
“Pindi niingiapo kwenye chumba cha kubadilishia nguo naongea na wachezaji wenzangu, navaa jezi zangu na baada ya hapo naruka kamba kwa dakika 10 maka 15 mpaka tunapoanza kwenda uwanjani kupasha, huwa kwa kawaida dakika 40 kabla ya mechi kuanza.”Saa 9
“Huwa sina mazingaombwe yoyote kabla ya mchezo - kwangu mimi kitendo hicho ni udhaifu wa akili. Huwa nakuwa nimeipumzisha akili na kuweka umakini uwanjani tu. Soka ni kama gofu - inabidi uweke umakini lakini akili yako iwe huru, vinginevyo huwezi kucheza vizuri.”Thursday, April 4, 2013
BARCELONA YAWATUMIA LIONEL MESSI NA MESCHARANO KUMUALIKA PAPA KWENDA NOU CAMP
Papa wa kanisa katoliki duniani amealikwa rasmi na klabu ya FC Barcelona kupitia Raisi wa timu hiyo Sandro Rosell kwenda kutembelea na kuangalia mechi kwenye dimba la Nou Camp.
Mkuu huyo wa kanisa katoliki, Papa Francis, ni shabiki wa klabu ya nyumbani kwao San Lorenzo na amekuwa akizivutia timu nyingi tangu alipochaguliwa kuwa Papa mwezi uliopita.
Mastaa wa Argentina kama mshindi wa mara nne wa Ballon d’Or Lionel Messi na mchezaji wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano kwa sasa wapo kwenye kikosi cha Blaugrana, na Rosell anasema litakuwa jambo la maana ikiwa mkuu huyo wa Wakatoliki kuweza kuhudhuria mechi mojawapo ya Barca.
Alisema kwenye barua iliyochapishwa na gazeti la El Mundo Deportivo: "Kama Raisi wa Barcelona na itakuwa jambo la heshima kubwa kushea na wewe kitu ambacho wote tunakipenda nacho ni mchezo wa soka.
"Ningependa kukaribisha kuangalia mechi kwenye dimba la uwanja wa Camp Nou na kufurahia mchezo wa soka kutoka kwa wachezaji wetu, hasa waargentina wenzio Messi na Mascherano, ambao wamesapoti mualiko huu kwa kuweka saini zao kwenye barua hii.”

WANANDINGA JKT RUVU SASA HAKUNA KULALA, WAHITAJI KUBAKIA LIGI KUU!
Na Baraka Mpenja Dar
es Salaam
Mlinzi wa kushoto wa klabu ya
maafande wa jeshi la kujenga taifa wa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani, Stanley
Nkomola, amesema ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu ni ngumu sana kwao na
wanahitaji kupigana kufa na kupona ili kukwepa panga la kushuka daraja.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
na mtandao huu, Nkomola amesema timu ikiwa na pointi 31 kwenda juu inaweza
kujinusuru na mkasi wa kushuka daraja, lakini chini ya pointi hizo inaweza
kuporomoka daraja.
“kwa sasa tuna pointi 22 na aprili 10
tunakutana na wagosi wa kaya Coastal union uwanja wa mkwakwani Tanga,
tunahitaji ushindi ili angalau tufikishe pointi 25 na kuendeleza harakati za
kubakia ligi kuu msimu ujao”. Alisema Nkomola.
Mchezaji huyo aliongeza kuwa kila
mchezaji sasa ametambua kuwa anatakiwa kuwajibika kwa nafasi yake, kwani klabu
hiyo ikishuka daraja itakuwa balaa mkoani Pwani na jeshi kwa ujumla.
Pia Nkomola alisisitiza kuwa kubwaga
manyanja kwa kocha wao mkuu Charles Kilinda kumewaathiri sana kiuchezaji kwani
wamekosa mambo mengi ya kiufundi kutoka kwa kocha huyo.
“Unajua kuondoka kwa Kilinda ni sawa
na kuondoka kwa mzazi, lakini tumejipanga ipasavyo kuibakisha timu ligi kuu na
yeye atakaposikia atafurahi sana”. Aliongeza Nkomola.
Akiongelea suala la mashabiki wa
klabu hiyo kukosa imani na timu hiyo, mchezaji huyo alisema klabu hiyo haiwezi kushuka
daraja kutokana na mipango yao ya sasa.
Maafande wa JKT Ruvu wapo nafasi ya
10 katika msimamo wa ligi kuu, nyuma yao kuna timu za Tanzania Prisons wenye pointi 20 nafasi ya
kumi na moja, nafasi ya 12 wapo Africa Lyon wenye pointi 19, nafasi ya 12 wapo
maafande wa Polisi morogoro wakiwa na poniti 18 na mkia unashikiliwa na Toto
Africans wenye pointi 18.
AZAM: TUNAPANGA MAJESHI YA KUWAANGAMIZA BARRACK YC UWANJA WA TAIFA!
Na Baraka Mpenja Dar
es Salaam
Wawakilshi pekee wa Tanzania michuano
ya kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Azam fc maarufu kama wana
lambalamba wanaendelea kupanga majeshi ya kuwashambulia wapinzani wao Barrack
YC ya Liberia mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho utakaopigwa kesho
kutwa dimba maridhawa la Taifa jijini Dar es Samaam.
Afisa habari wa klabu hiyo ,Jafar Idd
Maganga, amesema wanaendelea na maandalizi huku wachezaji wote wakiwa barabara
kuwakabili wapinzani wao.
Idd alisema kuwa mshambuliaji wao nyota
kutoka nchini Uganda, Brayn Umony, umejiunga na wenzake baada ya kukaa nje ya
uwanja akisumbuliwa na majeraha.
“Jioni ya leo tumefanya mazoezi
uwanja wa taifa ili kuuzoe kabla ya mchezo wetu wa jumamosi, hapo kesho
tutafanya mazoezi ya mwisho Chamazi kama sehemu ya kuwapisha ndugu zetu kutoka
Liberia kufanya mazoezi yao ya mwisho uwanja wa taifa”. Alisema Idd.
Pia aliongeza kuwa hapo jana na leo
wapinzani wao wamefanya mazoezi katika uwanja wa Chamazi na kufurahia mandhari
ya uwanja huo.
“Barrack Yc hawajaamini kama sisi
tunamiliki uwanja bora kama ule, wametupongeza sana na kukutakia kila la heri”.
Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliwataka
watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa taifa siku ya jumamosi ili kuwaunga
mkono kama walivyofanya mechi za nyuma.
Alisema katika michezo ya kimataifa,
kinachotakiwa kwa kila mdau wa soka ni kuvaa uzalendo na kuishangilia timu ya
nyumbani bila kujali unazi wa timu.
“Timu imeaandaliwa muda mrefu,
kilichobaki ni kuwapanga wachezaji kisaikolojia kwa ajili ya mechi hiyo,
Watanzania waje kutuunga mkono kwani tutawapa zawadi ya ushindi mnono nyumbani
kwetu”. Alisisitiza Idd.
Azam fc imefikia hatua hiyo baada ya
kuwatungua wasudani kusini, Al Nasri Juba mabao 3-0 uwanja wa taifa na mechi ya
marudiano ugenini, wakaishushia dhahama ya mabao 5-0 na kusonga hatua
inayofuata kwa wastani wa mabao 8-1.
Ilipoenda nchini Liberia klabu hiyo iliwafunga
wapinzania wao Barrack YC mabao 2-1 na sasa inahitaji sare yoyote au ushindi
kuwatupa nje waliberia hao.
Barrack Yc wanahitaji ushindi wa
mabao mawili kwa nunge ili waitoe klabu ya Azam Fc.
Mungu ibarike Azam fc, mungu ibariki
Tanzania.
TFF YAZINDUA MPANGO WA MAENDELEO 2013-2016
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezindua rasmi Mpango wa Maendeleo wa Mpira wa Miguu (Technical Development Plan- TDP) wa 2013-2016 ambao pamoja na mambo mengine unahusisha kutazama upya mfumo wa mashindano na kuunda kanda kwa ajili ya kusimamia maendeleo.
Uzinduzi huo umefanywa leo (Aprili 4 mwaka huu) na Rais wa TFF, Leodegar Tenga katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washirika mbalimbali wakiwemo wachezaji, viongozi wa mpira wa miguu, Serikali, klabu na Wahariri wa Michezo.
Rais Tenga amesema mpango huo unafuatia ule wa 2004-2007, na 2008-2012 ambayo ilitengenezwa kwa msaada wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Mpango wa sasa umetengenezwa na TFF kwa kufuata mpango mfano (standard plan) wa FIFA.
Amesema mpango wa sasa ni wa kiufundi zaidi kwa vile umelenga kuendeleza mpira wa miguu, kwani iliyotangulia ilihusisha zaidi kutengeneza muundo wa TFF, kazi ambayo imekamilika kwani sasa shirikisho lina vyombo mbalimbali vya kusimamia mchezo huo.
“Wakati ule tulikuwa na Ligi Kuu tu, lakini tumeongeza mashindano ya aina mbalimbali kama U17, U20, Kombe la Taifa na sasa michuano ya Copa Coca-Cola itakuwa ya U15. Pia tukatengeneza Kanuni za Fedha, kilichomo katika mpango wa sasa ni kujenga mpira. Chombo (TFF) tayari kipo,” amesema.
Rais Tenga amesema TFF imefika hapa kutokana na watu kujitolea ambapo ametaka moyo huo uendelezwe, lakini akasisitiza washirika wote kuwa na mpango huo na kuusoma kwani umetokana na maoni yao ambapo kila mmoja ana kazi ya kufanya katika mpango huo.
“Naomba washirika wote wasome mpango huu. Kama mtu una mawazo zaidi baada ya kusoma, toa maoni yako. Mpango huu si Msahafu, utabadilika kutokana na maoni ya watu. Kama una mawazo zaidi, toa maoni yako kwa lengo la kujenga, isiwe kazi ya kulaumu tu kuwa mpango una upungufu. Mabadiliko yanafanyika kutokana na mawazo mapya,” amesema.
Amesema maendeleo ya mpira wa miguu ni mchakato mrefu, kwa hiyo unahitaji ushiriki wa watu kutokana na ukweli kuwa uongozi wa mpira wa miguu Tanzania bado ni wa kujitolea.
Rais Tenga amesema ahadi ya TFF ni kushirikiana na washirika mbalimbali kuhakikisha kuna maendeleo kwa faida ya mpira wa miguu wenyewe na nchi kwa ujumla.
Amewashukuru wote waliotoa maoni kwa ajili ya mpango huo wenye kurasa 76. Mpango huo ulioandaliwa na Mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni na Ofisa Maendeleo wa TFF, Salum Madadi unapatikana kwenye CD na nakala laini (soft copy).
PICHA ZA RAMANI YA UJENZI WA UWANJA WA YANGA - UPEMBEZU YAKINIFU WAKAMILIKA
Kampuni ya Beinjing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.
Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.
Katika uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi akinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
Kifukwe alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda.
Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja wa mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.
Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maaalumu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.
SOURCE:http://www.youngafricans.co.tz
PAPISS CISSE: KUTOKA KUWA DEREVA WA GARI LA KUBEBA WAGONJWA MPAKA KINARA WA MABAO NEWCASTLE
Aliwahi kuwa dereva wa gari la kubebea wagonjwa kwenye dharula nchini kwao Senegal.
Lakini sasa Newcastle inamhitaji na kumtegemea Papiss Cisse kuwasaidia kuiokoa timu hiyo msimu huu.Mshambuliaji huyo leo atakuwa anaiongoza Newcastle kwenye dimba la Estadio da Luz kwenye robo fainali ya kombe la UEFA.
Ushindi dhidi ya Benfica kwenye robo fainali itamfanya Alan Perdew na vijana wake kuzidi kuusogelea ubingwa wao wa kwanza tangu walipobeba ubingwa wa Fairs Cup in 1969 ukiutoa wa Intertoto Cup 2006.
Lakini pia itawapa ahueni na matumaini ya kuepeuka kushuka daraja kutoka kwenye Premier League.
Newcastle wana pointi 3 zaidi kutoka kwenye ukanda wa timu zitakazoshuka daraja baada ya kubamizwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Manchester City.
Na ving'ora vya hatari vimeanza kulia pale ST. James Park.
Lakini Cisse si mgeni wa ving'ora kwa sababu tayari alishakuwa mfanyakazi wa gari la kubebea wagonjwa kwa dharula tangu akiwa na umri wa miaka 15.
Kwa sasa anamiliki kituo cha hisani na ameweza kukusanya fedha za kutosha kununua ambulance mpya, X-ray machine na vifaa vingine vya matibabu kwa ajili ya Hosptali yake huko kwao Senegal.
Muda mchache kabla ya kwenda Lisbon, SunSport ilimfanyia surprised Cisse kwa kumpelekea gari la analolijua kiundani - linalomilikiwa na North East Ambulance Service Foundation Trust.
Na mshambuliaji huyo mwenye thamani ya £10million anakiri kumbukumbu za kazi yake ya zamani zilimrudia kwa kasi sana mara baada ya kukaa kwenye usukani mwa gari hilo.
Anakumbuka: “Wakati nakua kule Sedhiou hospitali haikuwa na vifaa vya ubora.
“Hivyo nilikuwa nawachukua watu kutoka kijijini kwetu kwenda mji mwingine, Dakar, ambapo kulikuwa na Hosptali bora zaidi.
“Nilikuwa nawaendesha wagonjwa kwa umbali wa masaa matatu mpaka manne kwenye ambulance.
“Na kwa bahati mbaya niliweza kushuhudia vifo vingi njiani kwa sababu hawakuweza kuhimili mpaka kufika hosptali.
“Kulikuwa na kesi nyingi za wanawake ambaye walipata kupoteza watoto kutokana na mimba zao kuharibika na wengine wakipoteza maisha safarini.
“Hilo ni jambo ambalo linaloniumiza sana kila nikikumbuka.
“Ikiwa na nina jukumu binafsi kwenye maisha yangu ni kusaidia hosptitali kwenye mji wangu.
“Nataka watu wengi wawe na vitendea kazi vyote ili waweze kuwashughulikia wagonjwa mahala pale pale wanapoishi."
Cisse, 27, anaendesha taasisi ya Friends of Sedhiou kutoka nyumbani kwao kusini mashariki mwa Senegal - na pia kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Miss Newcastle 2012, Rachelle Graham.
Ni miezi 15 tangu alipowasili kutoka Freiburg na akaenda kufunga mabao 13 kwenye mechi 14 kuisadia Newcastle kushika nafasi ya 5.
Ingawa msimu huu amekuwa na ukame kiasi, goli lake la umbali wa 20-yard dhidi ya Southampton na kufuatia na mabao ya ushindi ya Stoke City na Anzhi Makhachkala iliwakumbusha mashabiki uwezo wake wa kuwafanyia ugaidi mabeki wa timu pinzani.
Cisse anapenda maisha ya kaskazini mashariki mwa Uingereza. Alikiri: "Najihisi nipo nyumbani. Nimekaribishwa vizuri tangu nilipofika hapa.
“Mashabiki wa hapa ni maalum sana na watu wa aina yake sana.
“Muda mwingine unaweza ukakutana nao mitaani na ni vizuri kuwa ninaongea nao - hainigharimu chochote kufanya hivyo na jambo hilo linanifurahisha sana.
“Miezi yangu sita ya kwanza hapa nimekuwa na furaha sana uwanjani na maisha yanguya nyumbani. Kila ninachokigusa kinageuka dhahabu.
“Sasa hivi nimekuwa na ukame kiasi kwa sababu mabeki wameshaanza kunikamia lakini najitahidi kufanya sana mazoezi ili niwe fiti zaidi niweze kurudi kwenye form niliyokuwa nayo msimu uliopita."
Cisse kwa sasa ndio mshambuliaji tegemeo wa toon tangu Demba Ba ajiunge na Chelsea mwezi January.
Takwimu zinaonyesha wasengali hawa hawakung'ara kwa pamoja kwenye dimba la St. James Park kitu ambacho kiliwafanya mashabiki wa Newcastle kukosa amani.
Wote walifunga kwenye mechi ya kwanza Cisse dhidi ya Aston Villa mwezi February 2012.
Lakini hilo ndio likawa goli la mwisho la Ba kwenye msimu huo — japokuwa alikuwa na msimu mzuri mwanzoni alipofungamabao 15 kwenye ligi mara tu baada ya kuhamia kutoka West Ham United.
Mara nyingine wawili hao kufunga kwa pamoja ilikuwa kwenye mechi ya ushindi wa Magpies dhidi ya Chelsea kabla ya Ba hajahamia Stamford Bridge.
XAVI HERNANDEZ: GOLI ALILOFUNGA DHIDI YA PSG NDIO PENATI YAKE YA KWANZA AKIWA NA BARCA - NI GOLI MAALUM KWA MTOTO MGONJWA WA KANSA
Wiki kadhaa zilizopita katika siku ya Kansa Duniani, kituo cha radio kimoja huko Catalunya kilitengeneza kipindi kuhusu watoto wanaopambana na ugonjwa wa kansa na kuongea na baadhi yao katika Hospital Sant Joan de Déu na Casa dels Xuklis. Miquel alikuwa mmoja ya watoto hao - amekuwa akiugua kansa ya damu tangu lipokuwa na miaka mitatu na moja ya matamanio yake siku zote ilikuwa ni kukutana na Xavi. Akiwa amemsikia mtoto huyo kwenye radio, Xavi baadae akatembelea hospitali na kwenda kumuona mtoto huyo na kumpa zawadi ya jezi aliyoisaini na kumpa ahadi mbili: 'Moja ni kwamba akipona atamchukua na kumpeleka kwenye mazoezi na Barca na ikiwa angefunga basi goli basi lingekuwa maalum kwa ajili ya mtoto hukuakishangilia kwa kushika kichwa chake. Jana kwa bahati nzuri akafunga penati dhidi ya PSG na akashangilia kwa kushika kichwa chake kumaanisha kutimiza ahdi yake kwa mtoto Miquel.
Mechi 150 za michuano ya ulaya
Xavi alicheza mechi yake ya 150 katika michuano ya ulaya dhidi ya PSG, huku mechi 134 zikiwa za Champions league - 10 pungufu kufikia rekodi ya inayoshikiliwa na Raul na Ryan Giggs - mechi 13 zikiwa za UEFA Cup na 3 za European Super Cup. Hii ilikuwa ni rekodi ningine kwa mchezaji anayeongoza kucheza mechi nyingi katika historia ya Barcelona.
Goli lake la kwanza la penati akiwa na Barca
Goli alilofunga dhidi ya PSG ndio lilikuwa la kwanza kuifungia Barcelona kwa mkwaju wa penati tangu alipoanza kuichezea timu hiyo mwaka 1998.
LEO MESSI KUIKOSA MECHI YA MALLORCA: APATA JERAHA LILOMUWEKA NJE WIKI TANO MIAKA 5 ILIYOPITA
Jeraha kama hili alilipata miaka mitano iliyopita
Mara ya mwisho Messi amepata majeraha ya misuli ya paja ilikuwa ni March 4th 2008 dhidi ya Glasgow Celtic katika mechi ya pili ya robo fainali ya Champions League na baada ya hapo alikaa nje kwa wiki tano.
Mara ya mwisho kuumia jeraha la misuli ilikuwa November 2009 kwenye mchezo dhidi ya Athletic Bilbao alipoumia msuli wa paja lake ya kushoto ambapo ilimbidi kukosa mchezo uliofuatia wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Inter - ingawa Barca wakashinda 2-0 mwishoni. Pia alikuja kuumia tena wakati akiwa na timu ya taifa lakini hakuweza kukosa mchezo wowote wa Barca.
Miaka saba bila kutolewa wakati wa mapumziko
Messi alitolewa wakati wa mapumziko kwenye mechi dhidi ya PSG - ikiwa ni mara ya kwanza yeye kutolewa wakati wa mapumziko tangu February 5th 2006 katika mechi dhidi ya Atletico Madrid pale Camp Nou, wakati kocha wa wakati huo Frank Rijkaard alipomuingiza Giuly na Ezquerro akiwatoa Messi na Van Bommel, wakati Barca wakiwa nyuma ya goli moja lilowekwa kimiani na Fernando Torres.
Leo Messi alipost hii picha na kuwaambia mashabiki wake wa mtandao wa Facebook kwamba hajaumia sana |
TARIBO WEST NA TUHUMA ZA KUDANGANYA UMRI: ALIIDANGANYA TIMU ANA MIAKA 28 VIPIMO VIKAONESHA ANA 40
Mchezaji wa zamani wa Nigeria ambaye alivichezea vilabu vya Derby County, Plymouth na Inter Milan Taribo West ametuhumiwa kudanganya ukweli kuhusu umri wake.
Mchezaji huyo aliyestaafu kwa sasa alijiunga na timu ya Serbia Partizan Belgrade mwaka 2002 baada ya kuondoka Derby County aliwaambia mabosi wa klabu yake mpya kwamba ana miaka 28.
Lakini sasa raisi wa zamani wa Partizan Belgrade, Zarko Zecevic, amemtuhumu mnigeria huyo, akisema wakati huo tayari alikuwa na umri wa miaka 40.
'Alijiunga nasi akisema ana miaka 28. Baadae tukagundua ana miaka 40, lakini bado alikuwa anacheza soka vizuri hivyo sijutii kuwa nae kwenye timu yangu,' alisema Zecevic.
Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Croatia, mlinzi huyo ambaye alikuwa maarufu kwa nywele zake zilizojaa rangi pia alidanganya umri wakati anajiunga na timu ya Croatia Rijeka.
Akiwa na miaka 44, wanasema West alimwambia daktari wa timu ana miaka 32.
Ilikuwa ni baada ya vipimo vya afya, madaktari wakagundua kwamba magoti yake yalionyesha ni mtu mzima sana tofauti na alivyokuwa akisema mwenyewe.
Hivyo hakuweza kusajiliwa na timu hiyo lakini baadae akaenda kujiunga na Plymouth na baadae akaenda kujiunga na timu ya Iran Paykan FC mahala ambapo alimalizia soka lake akiwa na umri wa miaka 46 mwaka 2008.
Lakini leo hii ukifungua mtandao wa Wikipedia anajieleza kuwa na miaka 39.

Taribo West wakati akiichezea Derby

Wednesday, April 3, 2013
EXCLUSIVE: NDOLANGA AAPA KUANIKA UCHAFU WOTE WA TFF KWA FIFA
WAKATI ujumbe kutoka Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) utatua nchini
Aprili 16 kwa ajili ya kufanya tathmini ya mchakato wa uchaguzi,
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), Muhidin Ndolanga
amesema atahakikisha anaanika madudu yote yaliyofanywa na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
Ndolanga aliyasema hayo jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa sio yeye peke yake ambaye atakuwa mstari wa mbele kueleza madudu ya shirikisho hilo kwani wapo wengi.
"Mimi najua wapo watu wengi tu ambao wataenda kueleza yaliyotokea mpaka tukafika hapa tulipo, FIFA hawana wanachokijua watataka kujua ukweli kutoka kwetu, sisi kama wadau tutasema yetu na TFF nao watasema yao."alisema Ndolanga ambaye ni mjumbe wa heshima wa shirikisho hilo.
“Haiwezekani TFF ifanye madudu katika utendaji wake na bado itegemee watu wakae kimya. Yaani dhambi na dhuluma ziachwe hivihivi, ukiuliza Fifa, mara Fifa watatufungia, mara fifa hivi, ...,” alisema Ndolanga ambaye enzi ya utawala wake kilichokuwa Chama cha Soka (FAT), Tanzania kiliwahi kufungiwa kwa sababu ya serikali kuingilia kati utendaji wake.
Wakati Ndolanga akisema hayo kuna habari kutoka kwa kiongozi mmoja mwenye wadhifa mkubwa TFF amebainisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi ana nafasi finyu ya kurejeshwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kile walichoeleza kuwa amefanyiwa hujuma na klabu yake ya Yanga ambayo ilimuandikia barua ya kielelezo kuwa ameongoza Yanga kwa miaka miwili.
"Ni kweli kabla ajawa katibu wa Yanga alikuwa seneta na baadae katibu, lakini hakuna na kielelezo chochote ambacho kilionyesha zaidi ya barua ya katibu wa Yanga Laurance Mwalusako ambayo ilitanabaisha aliongoza Yanga miaka miwili.
"Alafu hata mkoa wa Pwani hakupeleka kielelezo kuwa anaongoza kamati ya mashindano wala mkoa wa Dar es Salaam vidhibitisho hiyo havikuwepo sasa kama Malinzi anaweza hakikishe anapata vielelezo hivyo vyote itakapokuja FIFA awe navyo." alisisitiza.

SIMBA YAJIVUA RASMI UBINGWA WA LIGI KUU - YENYEWE YASEMA INATAKA NAFASI YA PILI
UONGOZI wa Simba umeamua kujivua rasmi ubingwa wao na sasa wameamua
kuelekeza nguvu zao katika nafasi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara
ambayo inaelekea ukingoni.
Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi jana umetamka rasmi kushindwa kutetea taji hilo na kuziachia Yanga na Azam ambazo zinafukuzana kuwania ubingwa huo.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha hilo na kudai kuwa kwa sasa uongozi wa klabu hiyo wanajitaidi kuakikisha Simba inamaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mashindano ya Kombe la Shirikisho (CAF) mwakani.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na mwenendo wa timu yao kwa hivi karibuni na kupelekea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.
''Ni kweli kwa sasa hatuwezi tena kutetea ubingwa wetu. Kilichobaki ni kupigana kumaliza katika nafasi ya pili kucheza Kombe la Shirikisho mwakani."
Kamwaga alisema kwa sasa uongozi wa timu hiyo una changamoto nyingi ikiwemo usajili ya mambo mengine mengi.

BAADA YA KUSHINDWA KUNG'ARA NYUMBANI - HUMUD ATISHA SAUZI AFUZU MAJARIBIO JOMO COSMOS
Kiungo wa Azam FC,
Abdulhalim Humoud amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Azam Patrick Kahemele alisema kuwa, Humoud amefuzu majaribio hayo baada ya kufanya mazoezi na klabu hiyo mara moja na kucheza mechi moja.
"Ni kweli Humud amefuzu majaribio na timu ya Jomo Cosmos, yalikuwa ya wiki mbili."
"Kijana wetu amefuzu majaribio hayo baada ya kufanya mazoezi mara moja na kucheza mechi moja."
Kahemele alisema kuwa baada ya kufuzu kwake wanasubiri maafikiano baina ya Azam FC na Jomo Cosmo kuhusu ada ya uamisho ambayo alidai ana uhakika Wataafanikiwa.
"Kama unavyojua kulikuwa na mapumziko ya sikuu ya pasaka,lakini baada ya kwisha tunatarajia Azam na Jomo Cosmo zitazungumza na kuafikiana kuhusu uhamisho wa Humoud," alisema Kahemele.
Iwapo Humoud atafanikiwa kujiunga na timu hiyo atakuwa Mtanzania wa pili kuichezea, baada ya Yusuf Macho 'Musso'

KOCHA WA MTIBWA SUGAR ATIMULIWA KAZI NA AFC LEOPARDS
AFC Leopards ya Kenya imemfukuza Kocha wake Tom Olaba aliyekuwa akiifundisha Mtibwa Sugar msimu uliopita.
Olaba ametimuliwa kwenye kibarua hicho baada ya miezi mitatu kupita tangu ilipompa dhamana ya kuifundisha timu hiyo.
Kutupiwa virago kwa kocha huyo kumekuja baada ya saa chache kabla ya Leopard (Paka Wakubwa) kucheza na Homeboyz FC kwenye Uwanja wa Mumias Complex jana.
Katika mahojiano na vyombo vya habari nchini Kenya, Makamu Mwenyekiti wa Leopards, Walter Onyino, amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo uli kulinda usalama wa Olaba dhidi ya mashabiki wa klabu waliotishia uhai wake kama angekuwa uwanjani hapo.
“Tumemwita arudi Nairobi kwa sababu mashabiki wametishia kumletea vurugu. Kocha wa makipa, John Busolo na Meneja wa timu, Nicholas Muyoti ndiyo waliopewa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa sasa.

Subscribe to:
Posts (Atom)