Search This Blog

Friday, April 5, 2013

BAADA YA ODEMWINGIE NA EMENIKE - SASA YOBO NAE ADAI KUTOHESHIMIWA NA KOCHA STEPHEN KESHI


Nahodha wa Nigeria Joseph Yobo amesema kunahitajika kuwepo kwa kwa njia nzuri ya mawasiliano baina ya benchi la ufundi la Super Eagles na wachezaji wakongwe wa timu hiyo. 

Yobo ni mchezaji wa mwingine kuongezelea masuala ya mawasiliano mabovu hadharani huku akimlaumu kocha Stephen Keshi kwa kutomtaarifu juu ya kuachwa kwake kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichotoka sare ya 1-1 na Kenya katika mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia 2014.
Yobo anamfuatia mshambuliaji wa West Brom Peter Odemwingie na Emmanuel Emenike, ambao wote kwa pamoja wamesema kwamba kocha huyo amekuwa akiwatendea ndivyo sivyo. 

Mlinzi wa Fenerbahce Yobo anaamini kutokuelewana baina ya kocha na wachezaji kunaweza kuondoshwa na ikiwa kutakuwa namna bora ya kuwasiliana na baina ya kocha na wachezaji, hasa wakongwe.

Mlinzi huyo mwenye miaka 32, ambaye ndiye mchezaji wa Nigeria aliyecheza mechi nyingi kuliko wote(95), amesema anahisi kutoheshimiwa na Keshi baada ya kocha huyo kushindwa kumtaarifu kwamba asingemwita kwenye mechi iliyopita dhidi ya Kenya.

"Nimekuwa na timu ya taifa kwa takribani miaka 10, sitegemei kucheza kila mchezo sasa ikiwa nashindwa kujitoa kwa yote," Yobo alikiambia kituo cha BBC Sport.

"Lakini tabia ya Keshi inakatisha sana tamaa. Sijawahi kutaka kutendea tofauti na wengine, ninachohitaji ni heshima tu ninayostahili ambayo mie nimekuwa nikiitoa kwa taifa langu na makocha wote waliopita.
"Sitokuwepo kuitumikia Nigeria milele, lakini inabidi wachezaji wasiwe wanastaafu kuichezea Super Eagles wakiwa na huzuni au kutokuwa na furaha kama inavyotokea siku za hivi karibuni.Unapowafanyia dharau wachezaji wakongwe wale chipukizi wanaona mfano huo mbaya ndani ya timu." 

Yobo aliisadia Nigeria kubeba ubingwa wa AFCON 2013 nchini South Africa mwezi February lakini ameshasema kwamba michuano hiyo ndio ilikuwa ya mwisho kwake.

Na akasisitiza kwamba yeye si mmoja ya wachezaji wakongwe wanaotaka kuziba nafasi kwa chipukizi na angependa kuwaona wakikua na kuwa wachezaji wazuri watakaoiletea mafanikio Super Eagles.

"Nafahamu sitoweza tena kushiriki kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika. Wachezaji wachanga wanastahili kupata nafasi wakiwa wanachipukia kama mimi nilivyopata huko nyuma wakati nakua."
Japokuwa, Yobo anaamini bado anaweza kutoa mchango kwa timu yake ya taifa na ataendelea kuichezea Super Eagles japo kwa muda fulani mfupi.
"Sina tofauti na yoyote - napenda kuitumikia nchi yangu na sitoweza kuyapa mgongo majukumu yangu kwa nchi yangu," alisema
"Kwa michuano ya kombe la Mabara na Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil, japokuwa kwa sasa inaonekana sina nafasi kwa sababu kocha hajaniita, lakini nitaitwa ningependa kwanza kuongea na Keshi vitu kadhaa, then nitapaki mabegi yangu na kujiunga na kambi. Ikiwa sitochaguliwa then nitaendelea kuitumikia klabu yangu ya Fenerbahce."

Keshi, kwa upande wake amesema hafurahishwi kuona baadhi ya wachezaji wamekuwa wakinung'unika hadharani.
"Sipendi kujiingiza kwenye mambo ya wachezaji na vyombo vya habari, ningependelea waje kuzungumza na mimi mwenyewe juu ya madai yoyte waliyonayo dhidi yangu,"Keshi alikiambia kituo cha BBC.

No comments:

Post a Comment