Ni fainali ambayo inatawaliwa na hadithi ya timu zote mbili kuwakosa wachezaji muhimu, Chelsea ikiwakosa wanne na Munich ikiwakosa watatu.
Ni fainali inayofanyika kwenye uwanja wa nyumbani wa timu inayoshiriki mchezo wa fainali jambo ambalo linatokea kwa mara ya kwanza kwneye kizazi hiki .
Bayern Munich moja kwa moja wanaingia kwenye mchezo kama timu yenye nafasi kubwa ya kushinda . Ukiangalia baadhi ya factor nyingi za ushindi ziko upande wao. Ukiangalia wachezaji watakaowakosa ni tofauti na wale watakaokosekana na Chelsea. Munich itawakosa Luis Gustavo, David Alaba na Olger Badstubber.
Moja ya matatizo makubwa ya Bayern Munich ni kwenye defense na hii ni kwa sababu tofauti na ilivyo Chelsea na timu nyingine toka England ambazo huanza kujengwa tangu nyuma kwenye defense, Bayern Munich ni timu ambayo imeanza kujengwa kwenye safu ya ushambuliaji ambako ndio hasa ilipo nguvu yake kuu.
Mario Gomez akisaidiwa na kina Toni Kroos,Thomas Mueller, Arjen Robben , Franck Ribery na Bastian Schweisteiger wote wamekuwa msaada mkubwa kwa Bayern wakati ikiwa inashambulia na ndio maana wakati mwingine mapungufu ya Bayern kwenye defense yanashindwa kuonekana.
Hata hivyo defense ya Bayern Munich ambayo imekuwa kwenye wakati mgumu mara nyingi imekuwa ikisaidiwa na wachezaji watakaokosekana leo ambao ni Alaba, Badstubber na Gustavo .
Kukosekana kwa wachezaji hawa kutailazimu Bayern pengine kuwatumia Anatoly Tymoschuk ambaye ni midfielder mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kati , Philip Lahm huenda atatumika kwenye mojawapo kati ya pande mbili za safu ya ulinzi kwa maana ya kushoto au kulia huku Bastian Schweinsteiger akilazimika kushuka chini kucheza kama kiungo mkabaji .
Bayern ni timu ambayo ina mabao mengi ndani yake huku Mario Gomez akiwa katikati ya mipango yote ya ufungaji . Ukitazama takwimu za msimu huu a ligi ya mabingwa zinaonyesha kuwa Bayern Munich ni moja ya timu tatu zilizofunga mabao mengi tangu hatua ya makundi hadi kufika fainali .
Ukiitazama Chelsea ambayo itacheza leo ndio unapata taswira halisi ya jinsi walivyo kwenye wakati mgumu wakicheza na Bayern. Pengo la Ramires ni kubwa pengine kuliko mapengo ya wachezaji wote watakaokosekana kwenye line up ya Chelsea leo. Ukitazama kazi aliyoifanya ya kupunguza threat ya Dani Alves kwenye mchezo wa nusu fainali halafu jiulize umuhimu gani angekuwa nao kwa kumzuia mmojawapo kati ya Arjen Robben na Franck Ribery.
Ukiachilia mbali kazi ya kukaba Ramires ametokea kurekebisha sehemu muhimu ya mchezo wake ambayo ni ufungaji wa mabao muhimu kama alivyofanya kwenye nusu fainali dhidi ya Barca na hata kwenye fainali ya kombe la FA .
Branislav Ivanovic naye atakuwa pengo kubwa sana kwa Chelsea. Ivanovic ni beki mwenye umuhimu wa aina yake kwa Chelsea hasa ukizingatia kuwa Terry hatakuwepo na Gary Cahill na David Luiz hawana match fitnesss . Bahati mbaya naye ni mchezaji mwingine anayeingia kwenye orodha ya watu watakaokosekana hii leo . Ukabaji wake wenye nidhamu ya ufundi hali wa jukumu la beki pamoja na mabao yake muhimu ambayo hufunga akipanda ni jambo ambalo linafanya kukosekana kwake kuwe mazingira magumu kwa Chelsea .
Raul Meireles ni jina lingine ambalo Chelsea italikosa, Meireles ni kiungo ambaye hutimiza jukumu analopangiwa na kocha na hulifanya kwa asilimia mia moja hamsini . Work Rate yake ni kubwa, na ana uwezo wa ziada ambao kocha yoyote huhitaji kwenye timu .
Wachezaji hawa watatu wanaifanya kazi ya Chelsea kuwa ngumu kwa kuwa wametokea kuwa misingi muhimu ya kikosi cha Chelsea chini ya Roberto Di Matteo ambapo timu hii imekuwa ikishinda mechi nyingi kwa kufanya kazi na kutumia nafasi chache ambazo zinapatikana .
Moja ya mambo ambayo yataamua mchezo wa fainali kwa Chelsea ni mfumo watakaotumia. Endapo wataamua kupaki basi kwa staili waliyoifanya dhidi ya Barca watadhurika kwa hakika kwa kuwa Bayern Munich ni timu ambayo haina matatizo ya kiufundi ambayo yanaonekana kuidhuru Barca . Bayern tofauti na Barca ina mpango mbadala pale mpango wake wa msingi unaposhindikana . Ukipaki basi Bayern wanao wachezaji ambao watawatumia kwa kupiga mashuti ya mbali kama Schweisteiger, Kroos, Lahm na Thomas Mueller . Ukiamua kuwaelekeza mabeki au viungo wawili dhidi kucheza kwa kumkaba mmojawapo kati ya Robben na Ribbery Bayern watatumia shimo litakalobaki katikati ya uwanja kukudhuru na kama Chelsea watakuwa wakiokoa kwa kuwapa Bayern Umiliki wa mpira kwenye set pieces pia watadhurika kwa kuwa Bayern wanafunga kupitia ste pieces kwa kuwa wanae aina ya mshambuliaji ambaye Barcelona walimkosa ambaye ni Mario Gomez na hata Chelsea wakiridhika na kutafuta sare ili wajaribu bahati ya kwenye penati historia inaonyesha kuwa timu za ujerumani ni hatari sana kwenye penati kama walivyotambua Real Madrid kwenye nusu fainali.
Hata hivyo Chelsea wamekuwa wakicheza vizuri wakiwa under pressure hasa kutokana na kuridhika kuwa under dog kwenye michezo kadhaa msimu huu.
Rudi kwenye mechi ya Barcelona na utagundua hilo. Haya yote hayamaanishi kuwa Chelsea hawana nafasi kwani bado wanae Didier Drogba ambaye ni mshambuliaji wa mechi kubwa . Wanaye Fernando Torres ambaye anabaki kuwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuziona nyavu .
Itakuwa fainali ngumu na isiyoamulika kirahisi , dakika 90 zitaamua bingwa wa ulaya msimu .