Search This Blog

Saturday, February 22, 2014

LIVE SCORE: YANGA SC 7 - 0 RUVU SHOOTING - MBEYA CITY 0 - 2 COASTAL UNION



Goli la pili Mohamed Mtindi amefunga tena Dakika ya 92

Coastal Union 2 - 0 Mbeya City 
Na mpira umekwishaa ….

Kutoka Tanga Dakika ya 83 Mohamed Mtindi anaipatia Coastal bao la kuongoza dhid ya Mbeya City

Kadi ya njano kwa Said Madega wa Ruvu Shooting Dk ya 83

Kocha wa Ruvu Shooting Tom Olaba aondoka uwanjani - Dakika ni ya 81

Dakika ya 80, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao saba

Dakika ya 75, Ruvu Shooting 0 - 6 Young Africans

Dakika ya 70, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la sita

Dakika ya 69, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite

Uwanja wa Mkwakwani Tanga ni dakika ya 72 bado ni 0-0

Dakika ya 60, Ruvu Shooting 0 - 5 Young Africans
Anaingia Hassan Dilunga kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa

Dakika ya 54, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la tano

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Ruvu Shooting 0 - 4 Young Africans
Mpira ni mapumziko: 

Yanga 4 - 0 Ruvu Shooting

Mbeya City 0 - 0 Coastal Union


Mbeya City 0 - 0 Coastal Union
Dakika ni ya 33

Dakika ya 30, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la nnE

Dakika ya 27, Emmanuel Okwi anaipatia Young Africans bao la tatu
Dakika ya 20: Yanga 2 - 0 Ruvu 


Dakika ya 15, Ruvu Shooting 0 - 2 Young Africans

Dakika ya 2, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la pili

Sekunde ya 40, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la kwanza

Mpira ndo umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Ruvu Shooting Vs Young Africans

MSHAHARA WA WAYNE ROONEY KWENYE NAMBA - FEDHA ANAYOINGIZA KWA WIKI INAZIDI MSHAHARA WA MWAKA MZIMA WA BARACK OBAMA


Tuuchambue mshahara wa Wayne Rooney kwenye namba maalum:

£160,000 - Hii ndio fedha ambayo itabaki kwenye akaunti ya Rooney kwa wiki - baada ya kulipia kila kitu, kodi na bima. 
£30,000 - Wastani wa mshahara wa wiki kwa mchezaji wa ligi kuu ya England, hii ni kwa mujibu wa  Deloitte's sports business group.
£517 - Huu ni wastani wa mshahara wa wiki wa mtu anayefanya kazi ndani ya UK.  Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anapata £2,740 kila wiki. 
65 - Itamchukua wiki 65 kwa Barack Obama, raisi wa taifa kubwa duniani Marekani, kuweza kutengeneza kiasi anacholipwa Rooney ndani ya siku saba tu  - Obama analipwa £240,000 kwa mwaka.

1885 - Huu ulikuwa mwaka wa kwanza kwa mwanasoka kuweza kulipwa kutokana na kucheza soka. 

£4 - Hiki ndio kilikuwa kiwango cha juu kabisa cha malipo katika Football League mwaka 1901. 
60 - Namba ya miaka iliyotumika mpaka kufikia mwisho wa sheria ya kulipwa kiasi kisichozidi paundi 4 kwa mwanasoka. Sheria hii ilikufa mwaka 1961. Muda mfupi baada ya kufutwa kwa sheria hii, mchezaji wa Fulham na Engand  Johnny Haynes alikuwa mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha  £100 kwa wiki.
£1,200 - Kiasi ambacho golikipa Peter Shilton alitengeneza kila wiki mwaka 1979 wakati alipoweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Uingereza kwa kusaini mkataba mpya na Nottingham Forest.
£10,000 - Mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha tarakimu 5 alikuwa Chris Sutton, wakati mshambuliaji huyo alipojiunga na  Blackburn Rovers akitokea Norwich City mnamo 1994.
£100,000 - Sol Campbell aliondoka Tottenham na kujiunga na Arsenal mnamo mwaka 2001, akasaini mkataba ambao ulimfanya kuwa muingereza wa kwanza kulipwa mshahara wenye tarakimu 6 kila wiki. 

CARLO ANCELOTTI AKARIBIA KUVUNJA REKODI YA KUIWEZESHA REAL MADRID KUCHEZA MECHI NYINGI MFULULIZO BILA KUFUNGWA


Kocha wa kiitaliano Carlo Ancelotti anaweza kuandika historia mpya wikiendi hii endapo ataweza kuingoza Real Madrid kupata matokeo chanya katika mchezo wa wikiendi wa La Liga dhidi ya Elche.

Mpaka kufikia sasa Carlo Ancelotti ameshaiongoza Real kucheza jumla ya mechi 25 mfululizo bila kupoteza mechi hata moja.

Tangu walipofungwa na na Atletico Madrid 1-0 Santiago Bernabeu mwishoni mwa mwezi September, kisha
REAL MADRID: REKODI YA KUCHEZA MECHI NYINGI MFULULIZO BILA KUFUNGWA
 1988-89: 34 MECHI (25 USHINDI, 9 SARE)
Kikosi cha Leo Beenhakker kilicheza mechi 34 mfululizo bila kufungwa wakati waliposhinda La Liga na Copa del Rey msimu wa1988-89.
2013-14: 25 MECHI (21 USHINDI, 4 SARE)
Carlo Ancelotti ameiongoza Madrid kucheza mechi 25 mfululizo bila kufungwa katika msimu wake wa kwanza na anaweza kufikisha 26 endapo atapata matokeo chanya dhidi ya Elche wikiendi hii.
1996-97: 25 MECHI (17 USHINDI, 8 SARE)
Msimu wa kwanza wa Fabio Capello pale Bernabeu ulihusisha mechi 25 bila kufungwa wakati Madrid walipochukua ubingwa wa La Liga baada ya kumaliza nafasi ya 6 msimu wa 1995-96.
mwezi mmoja uliofuatia kufungwa na 1-0 na Barcelona pale Nou Camp, kikosi cha Ancelotti mpaka sasa kimeshacheza mechi 25 bila kupoteza tangu Oktoba 2013.

Wameshinda mechi 21, na wametoa sare mechi 4 na hawajafungwa. Wameshinda dhidi ya Sevilla, Rayo Vallecano, Real Sociedad, Almeria, Galatasaray, Valladolid, Olimpic Xativa, FC Copenhagen, Valencia, Osasuna (mechi 2 Copa del Rey), Celta Vigo, Espanyol ( La Liga na mara 2 kwenye Copa) Betis, Granada, Atletico (mechi 2 copa), Villarreal na Getafe, walitoka suluhu na Juventus, Osasuna na Athletic Bilbao.

Rekodi hii tayari ni nzuri kuliko ya kikosi cha Fabio Capello cha Madrid cha msimu wa 1996-97, ambacho kiliweza kucheza mechi 25 bila kufungwa, lakini walitoa sare mechi 8 - hii ilikuwa katika msimu wa kwanza wa mtaliano huyo.

HATIMAYE WAYNE ROONEY AWA MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI - TAZAMA MCHANGANUO WA MALIPO YAKE


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney jana usiku hatimaye alimaliza tetesi za kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya utakaomuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2019.

Rooney ambaye alisajiliwa na United akitokea Everton mwaka 2004, amesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya £300,000 kwa wiki.

Rooney sasa analipwa jumla ya £15.6m kwa mwaka - kwa maana 

MCHANGANUO WA MSHAHARA MPYA WA ROONEY

£15,600,000 kwa mwaka
£300,000 wiki
£43,000 kwa siku
£1,800 kwa saa
£30 kwa dakika
50p kwa sekunde
 hiyo Rooney sasa amemfunika Cristiano Ronaldo aliyekuwa akishika nafasi ya kwanza kwa kulipwa fedha nyingi za mshahara - Ronaldo mkataba wake mpya na Real Madrid analipwa kiasi cha £288,000 kwa wiki. Pia amemfunika Leo Messi ambaye analipwa kiasi cha £12.08m kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa 2013 Forbes rich list.

Friday, February 21, 2014

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ENGLAND KATIKATI YA URUGUAY NA ITALIA, KUNDI D


Na BARAKA MBOLEMBOLE

WIKI ILIYOPITA tulitazama kundi la pili la michuano ijayo ya kombe la dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake nchini Brazil Juni mwaka huu.   Mabingwa watetezi Hispania, Uholanzi, Australia na Chile ndiyo wanaounda kundi hilo. Leo tunalitazama kundi la nne ( kundi la tatu utalitazama kesho katika mtandao huu) Kundi la D, Lina nchi za  England, Uruguay, Italia na Costa Rica/

NI mataifa machache sana yenye historia ya soka kama Uruguay ' The Sky Blue One'. IKiwa ni nchi yenye wakazi wasizidi millioni nne Uruguay inajivunia kuwa moja ya mataifa yenye mataji mengi ya kimataifa duniani.  Imetwaa ubingwa wa kombe la dunia mara mbili, 1930, na 1950, pia wanaongoza kwa kutwaa ubingwa wa Amerika ya Kusini mara nyingi zaidi, mara 15, huku ubingwa wao wa mwisho wakitwaa mwaka 2011 nchini Argentina.

Mabingwa hao wa kwanza wa dunia,  tayari wamecheza michezo 47 ya fainali za kombe  la dunia, wakiwa wamepata ushindi mara 18, kutoa sare mara 12 na kupoteza michezo 17, wamefunga mabao 76 na kuruhu nyavu zao mara 65. Walimaliza katika nafasi ya nne katika fainali zilizopita, WOZA 2010, na sasa wamefuzu kwa fainali zao za 12 kati ya 20.

Kiwango cha sasa cha nchi ya Costa Rica  kinaweza kufanya kundi hilo kuhesabika kama ni moja ya makundi magumu zaidi, kwani wawakilishi wa Ulaya, England na Italia walifanya vibaya katika fainali zilizopita. England iliishia hatua ya 16 bora na Italia ilishindwa hata kuvuka hatua ya makundi.

Mabingwa hao mara nne, ' Azzurri' ni moja ya mataifa mawili ambayo yanashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo sambamba na Brazil, Italia ilitwaa katika miaka ya 1934 na 1938, wakarudia tena katika miaka ya 1982 na 2006.Wamefuzu kwa mara ya 13 mfululizo  kati ya mara 17 walizowahi kufuzu. Hii ni timu ya kombe la dunia. WAmefuzu mbele ya mataifa ya Denmark, Czech Republic, Bulgaria, Armenia na Malta,  wakishinda michezo sita na sare nne kati ya michezo 10 waliyocheza.

Kikosi hicho kiliifunga England katika robo fainali ya michuano ya Euro 2012 na hatimaye kufika fainali wakati huo. Imeshacheza jumla ya michezo b3,  wakishinda michezo 45, sare katika michezo 21, na wamepoteza mara 17, wamefunga mabao 130 na wameruhusu mabao 78. Italia na Uruguay zinaweza kuvuka kundi hili na kuziacha nje England na Costa Rica.

England ' The Three lions' wamefuzu tena kwa fainali za kombe la dunia. NI moja ya timu maarufu sana katika michuano hiyo japo huwa haifanyi vizuri. Mafanikio yao ya mwisho ni katika fainali za mwaka 1990 walipofanikiwa kufika hadi hatua ya nusu fainali, walishindwa kufuzu kwa fainali za mwaka 1994 na wakaondolewa katika hatua ya robo fainali katika fainali za miaka ya 2002, 2006, na wakaishia hatua ya mtoano mwaka 2010.

Wamewahi kucheza michezo 59 katika fainali 13 walizopita miaka ya nyuma, wameshinda mara 26 tu, sare wametoa mara 19 na wamefungwa michezo 14. Ni moja ya timu zenye uhaba wa mabao katika michuano hiyo, wakiwa wamefunga mabao  77 na kuruhusu mabao 52 ni wastani wa chini katika ufungaji na uzuiaji katika kombe la dunia. Costa Rica wanatajwa kama vibonde katika kundi hili wamefuzu kwa fainali zao za nne. Wamewahi kuishia hatua ya 16 bora katika fainali za mwaka 1990 na wamewahi kuishia hatua ya makundi katika miaka ya 2002 na 2006. WAmecheza michezo 10 ya fainali za kombe la dunia, wameshinda michezo mitatu, wametoa sare mchezo mmoja na wamepoteza michezo sita. Hii ni ratiba ya mechi za kundi hili.
June 14 Fortaleza, 2000:

Uruguay v Costa Rica

June 15 Manaus, 0200:

England v Italy

June 19 Sao Paulo, 2000:

Uruguay v England

June 20 Recife, 1700:
Italy v Costa Rica

June 24 Natal, 1700:
Italy v Uruguay

June 24 B. Horiz, 1700:

NIONAVYO MIMI: BARCELONA NA KADI NYEKUNDU KWA WAPINZANI NI KULWA NA DOTO.


Na Oscar Oscar Jr.
0789-784858
Baada ya klabu ya Fc Barcelona kutolewa kwenye nusu fainali ya UCL msimu uliopita na klabu ya Bayern Munich kwa jumla ya mabao 7-0 ambapo Barcelona ililala kwa mabao 4-0 ugenini kwenye dimba la Arianze Ujerumani na kuja kumaliziwa nyumbani Camp Nou kwa mabao 3-0, watu wengi waliibeza na kuidharau klabu hiyo yenye maskani yake kwenye kitongoji cha Katalunya huko nchini Hispania.

Katika ulimwengu wa soka, hakuna timu ambayo itacheza mechi zake zote bila kufungwa na, kufungwa au kushinda mechi moja au mbili,sio kipimo sahihi cha kujua kama timu imepanda au imeshuka kiwango.Real Madrid mwaka 2011 ilifungwa bao 5-0 mbele ya Barcelona,Arsenal alifungwa bao 8-2 dhidi ya Man united pale Old Trafford,Bayern Munich msimu huu imefungwa bao 3-2 dhidi ya Man city tena pale pale Arianze Arena kwa hiyo,hakuna timu ambayo haifungwi.

Moja kati ya mijadala mikubwa wiki hii kwenye medani ya soka,ilikuwa ni kuhusu kadi nyekundu na penati ambazo zilitolewa kwenye michezo ya UCL kati Man city vs Barcelona na ule wa Arsenal vs Bayern Munich.Mchezo wa Arsenal ulimfanya golikipa Wojciech Szczesny kupewa kadi nyekundu na Bayern kuzawadiwa penati wakati ule wa Man city,ulimfanya pia Martin Demichelis kupewa kadi nyekundu na Barcelona kuzawadiwa penati.

Kabla ya kuanza kulalamikia kadi nyekundu na penati ambazo zinatolewa,nataka tujikumbushe kidogo baadhi ya sheria ambazo zinazungumzia mazingira ya kutokea kwa penati na mchezaji kupewa kadi nyekundu.Kadi nyekundu inaweza kutolewa endapo mchezaji atafanya moja kati ya makosa yafuatayo;
1.Mchezaji kumtemea mate mchezaji mwingine 2.Kushika mpira kwa makusudi(kasoro golikipa na awe kwenye eneo lake) 3.kutumia lugha ya matusi 4.Kucheza madhambi makubwa na kumnyima mchezaji wa timu pinzani nafasi ya kuweza kufunga goli.Hapa nimetaja kwa uchache tu.

Kupitia sheria 17 za mchezo wa soka,mwamuzi wa mchezo anaweza kuipa timu penati endapo moja ya yafuatayo yanaweza kutokea mpira ukiwa mchezoni ndani ya eneo la penati; 1.Kumshika mchezaji wa timu pinzani 2.kuushika mpira kwa makusudi 3.Kusukuma 4.kumzuia mchezaji pinzani nafasi ya kufunga ukiwa kama mlinzi wa pili wa mwisho na mengine mengi,hayo ni kwa uchache tu.Mara ngapi umeona yakitokea haya kwenye soka na mwamuzi asifanye chochote?

Sasa tukirudi kwa kipa wa Arsenal Szczesny,utaona kuwa amefanya makosa yote mawili.Moja ni kumzuia nafasi ya kufunga Arjen Roben kwa rafu aliyomchezea ambayo ni kadi nyekundu na pili,kosa hilo limetokea ndani ya eneo la penati ambapo kwa mujibu wa sheria ni penati ya bila utata.Demichelis naye alimzuia Messi nafasi ya kufunga na pili,tukio hilo lilifanyika ndani ya eneo la penati hivyo,adhabu zote mbili ni sahihi.Dante alipewa kadi ya njano na arsenal kupewa penati kwa sababu hakucheza madhambi makubwa dhidi ya Ozil lakini,kwa sababu kosa hilo lilifanyika ndani ya penati,mwamuzi aliamuru kupigwa kwa penati hiyo.

Tangu mwaka 2008 timu ya Barcelona ilipochukuliwa na kocha Pep Gaudiola,imesumbua timu nyingi sana kutokana na aina ya uchezaji wake na ingawa kocha Gaudiola ameondoka klabuni hapo,makocha wote waliomfuatia kama Tito Vilanova,Jordi Raula(alikuwa msaidizi) na kwa sasa timu ipo chini ya kocha Gerrardo Martino wameendelea kutumia mfumo ule ule wa awali.Ni kweli kuna uwezekano timu hii ikawa imepungua ubora ukilinganisha na mwaka 2009 na 2011 walipotwaa ubingwa wa UCL lakini,ni makosa makubwa kudhani kwamba Barcelona ndiyo imekwisha kisoka.Barcelona bado ni timu bora Duniani na inastahili kuheshimiwa.

Lakini kwa nini kila siku wachezaji wa timu pinzani wapewe kadi nyekundu wanapocheza dhidi ya Barcelona na timu hiyo kupewa penati nyingi? Katika kutafakari kwangu,nimepata majibu yafuatayo;

Jambo la kwanza nililogundua ni staili wanayotumia Barcelona.Barcelona wanatumia "Tiki -Taka style" ambapo wanamiliki mpira kwa muda mrefu huku wakipiga pasi fupi fupi na pindi wanapopoteza mpira,wanaondoka kama nyuki kwenda kuutafuta kwa adui na ndani ya muda mfupi,unarudi tena kwenye himaya yao.Aina hii ya uchezaji ni kama "Sumbua bwege" ambapo timu pinzani wanazunguka dakika nyingi sana uwanjani bila kuupata mpira na kwa sababu hiyo ni rahisi sana kupandwa na jazba na kujikuta wakicheza rafu na kuambulia kadi nyekundu.

Barcelona pia inaundwa na wachezaji ambao ni wadanganyifu na mfano mzuri ni Sergio Busquets,Alex Sanchez bila kumsahau Pedro Rodriguez.Wachezaji hawa ni waongo sana na endapo mwamuzi hatokuwa makini,wanaweza kusababisha penati na kadi nyingi nyekundu.Mfano mzuri ni nusu fainali ya UCL kati ya Barcelona vs Inter Millan 2010 ambapo Thiago Motta alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu ya kawaida tu kiungo Sergio Busquets.Busquets alichezewa rafu mguuni lakini alipodondoka chini,alikuwa akishika kichwa utadhani umechomwa na mkuki!

Kuna muda naona kabisa mapenzi ya waamuzi nayo yanapelekea uwepo wa kadi nyingi nyekundu na penati pengine ambazo hazistahili.Robben Van Persie akiwa na arsenal mwaka 2011 aliwahi kupewa kadi nyekundu kwa kosa ambalo huenda hakustahili.Kama hiyo haitoshi,tumewahi kushuhudia Barcelona akipewa penati mbili kwenye mechi moja dhidi ya Ac Millan.Kutoa penati mbili sio tatizo,lakini ni lazima ziwe zinastahili kutolewa.Timu inayofanya vizuri daima inapendwa na hapa,naona kabisa hili jambo linawatia upofu baadhi ya waamuzi.

Kutokana na ubora wa Barcelona,timu nyingi sana zimekuwa zikikamia pindi wanapokutana.Jose Mourinho akiwa na Real Madrid alifikia kipindi anamuingiza kiungo na mlinzi Pepe kwa ajali ya kucheza tu vurugu uwanjani dhidi ya Xaiv,Iniesta na mtaalamu Messi.Unadhani kwa hali kama hii utaacha kweli kupewa kadi nyekundu? Takwimu zinaonyesha ni mara chache sana kwa timu hasa za Uingereza kucheza UCL na wasipate kadi nyekundu.Ligi ya Uingereza inatumia zaidi nguvu na hata ukirejea kwenye mechi ya man city na Barcelona ya wiki hii,hilo limejidhihirisha.

Na mwisho niseme tu,uwepo wa Messi uwanjani kuna muda inakuwa kero kwa sisi watazamaji kwa sababu analindwa na waamuzi kupita kiasi.Hata ikitokea kaguswa kidogo tu,filimbi inapulizwa na ikiwezekana kadi inatolewa kwa mchezaji aliyemfanyia madhambi hayo.Hakuna namana watu wanaweza wasigusane kwenye mchezo wa soka na kama hawataki Messi aguswe,ni bora wangempeleka akacheze mchezo wa Tennis ambako mchezaji mmoja yuko Magharibi na mwingine yuko Mashariki.

MANUEL NEUER APINGA NA SHERIA YA PENATI, KADI NYEKUNDU NA KUSIMAMISHWA MECHI MOJA KWA PAMOJA

Golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer amewaambia FIFA waachane na adhabu ya mara tatu - penati, kadi nyekundu, na kusimamishwa mechi moja kwa mchezaji ambaye atamzuia mwenzie nafasi ya kwenda kufunga kwa kucheza rafu ndani ya penalty box.

Wakati wa mchezo wa raundi ya 16 bora kati ya  Arsenal na Bayern pale Emirates Stadium, Wojciech Szczesny alimchezea rafu Arjen Robben, na akatolewa nje kwa kadi nyekundu. 
Ingawa David Alaba alikosa penati, Bayern walifanikiwa kushinda 2-0 Szczesny sasa ataukosa mchezo ujao pale Allianz Arena utakaochezwa March 11.
Hata hivyo Neuer anaamini kwamba kusababisha penati ni adhabu tosha - kutoa kadi nyekundu zaidi inakuwa ni adhabu kubwa. 
“Inabidi hili suala waliangalie vizuri, timu inakuwa ishapewa penati, kuongezea kadi nyekundu inazidisha makali makubwa kwa adhabu hiyo. FIFA waliangalie tena hili suala." 

KIUFUNDI ZAIDI: KWANINI MOYES HAPATI MATUNDA MAZURI KUTOKA KWA JUAN MATA KATIKA MFUMO WA 4-4-2?


David Moyes alimsaini Juan Mata kutoka akiwa na matumaini na mategemeo makubwa. Juan Mata alionekana kama mtu atakayekuja kuleta mageuzi ya kuisadia timu hiyo kuingia hata kwenye Top 4. Hata hivyo hali imekuwa tofauti na matarajio, Manchester United ikishinda mchezo mmoja tu kati ya minne Mata aliyocheza. Moja ya vitu vinavyoachangia matatizo haya ni mbinu za kiufundi, hivyo je inafaa kwa Moyes kuangalia upya mbinu zake ili kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji wake wa gharama zaidi - Juan Mata?

Mahala aambapo amekuwa akichezeshwa Mata. 
Baadhi ya watu walihisi Moyes angebadili mfumo kwenda kutumia 4-2-3-1 ili kuweza kupata matokeo mazuri kutoka kwa Wayne Rooney, Mata na Adnan Januzaj nyuma ya mshambuliaji wa mbele Robin van Persie, ingawa hilo halijawezekana mpaka sasa. Mata amekuwa akichezeshwa kama kiungo wa kulia au kushoto. Dhidi ya Arsenal alichezeshwa kama kiungo wa kushoto, ingawa alijaribu kuingia ndani ili kuwa karibu na washambuliaji wawili wa mbele 
matttt

Kama mchoro wa picha unavyoonesha hapo juu, United walikuwa wanacheza na Arsenal inayogombea ubingwa ugenini, lakini hapo juu tunaona Mata alitumia muda mwingi katika maeneo ya ulinzi, akikaa sana nyuma katika eneo la kulinda zaidi lango la timu yake (kutokea kushoto pia). Huu mfumo kwa hakika huwezi kukupa matunda mazuri kutoka Mata ambaye anakuwa bora zaidi anapokuwa na mpira miguuni mwake. Ndio maana haishangazi kuona Mata hakuwa na mchezo mzuri siku hiyo, akitengeneza nafasi mbili tu kwa Van Persie.

Dhidi ya Fulham alicheza vizuri kiasi na kuwa na mpira muda mwingi, ingawa alifanya hivi akicheza kwenye winga ya kulia katika mchezo ambao ulitawaliwa na krosi kutoka kwa wachezaji wa kikosi cha Moyes. Man United ilijaribu kupiga krosi 82, staili ambayo sio tu imepitwa na wakati lakini pia ni staili ambayo ndani yake huwezi kuona ubora wa Juan Mata, ambaye hufanya vizuri kazi yake anapocheza katikati ya mistari ya safu ya ulinzi na kiungo, na sio pembeni.

Mahala kwa kubadilisha
Mata hakufanya vibaya dhidi ya Fulham, alitengeneza nafasi tano za kufunga kwa wachezaji wenzie na katika mechi nne alizocheza ametengeneza jumla ya nafasi 13 (namba ya nafasi alizotengeneza Ashley Young msimu mzima). Lakini angeweza kufanya vizuri zaidi. Dhidi ya Fulham alikuwa na mpira kwa muda mwingi na alikamilisha 96% ya pasi zake zote.
mattttaaaa

Lakini tatizo pekee la hizo pasi zilikuwa katika maeneo ya pembeni, hasa upande wa kulia. Haya sio maeneo ya kupata ubora wa Mata. Mata anahitaji kuchezeshwa kati kati ya safu ya ulinzi ya wapinzania na kiungo, mahala ambapo anaweza kutumia jicho lake la pasi nzuri kwenda kwa washambuliaji. Kama tunavyoona kwenye picha hapo juu, hakuwa na mamalka ya mchezo kwenye eneo hilo.

Wazo la kwanza mbadala na kumuondoa mshambuliaji mmoja na kumchezesha Mata namba 10, jambo litakalomfanya awe na mpira muda mrefu na kuutumia katika maeneo ambayo anataka, sio kurudi nyuma kama ambavyo alivyokuwa akifanya dhidi ya Arsenal. Alicheza kwenye eneo hili katika mchezo pekee wa ushindi wa United katika mechi nne zilizopita - mechi dhdi ya Cardiff, ambapo alitengeneza nafasi nne.

Moyes anaonekana hataki au anasita kuwatumia Januzaj, Mata na Rooney katika kikosi kimoja na Van Persie. Hii inawezakana inatokana kwamba wachezaji wake wote watatu wa zamani wana uwezo wa kuingia ndani nyuma ya mshambuliaji wa kati. Njia pekee ya kufanya mfumo huu kufanya kazi ni kuachana na mfumo wa krosi na kuachia mpira wa pasi zaidi kuelekea ndani utumike zaidi.

Hitimisho
Hivi sasa David Moyes hapati matunda bora ya Juan Mata. Mfumo wa kutumia krosi ambayo Mata anatumika katika winga sio mzuri katika kutaka kupata matunda ya Juan Mata. Mata anahitaji uhuru wa kufanya kazi yake katika maeneo yake ya kati ya uwanja, hasa kwenye eneo la nyuma ya mshambuliaji. Ikiwa Moyes atabadili mfumo kwenda 4-2-3-1 ambao unamfiti Mata, Januzaj na Rooney wakicheza nyuma ya Van Persie. Jambo pekee la kuzingatia ni kuhakikisha mabeki wa pembeni wanakuwa na uwezo wa kutoa msaada mkubwa wakati timu inaposhambuliwa. Moyes hana cha kupoteza hivi sasa - hasa baada ya mfumo wa sasa wa 4-4-2 kutokuwa na matunda kwa timu na kupelekea matokeo mabaya. 

RASMI: FC BARCELONA YASHTAKIWA KWA UDANGANYIFU KATIKA UHAMISHO WA NEYMAR

Mahakama nchini Spain imeishtaki rasmi klabu bingwa ya nchi hiyo FC Barcelona kwa kufanya udanganyifu wa fedha zaidi ya $12.5 million zilizotumika katika uhamisho wa mshambuliaji wa kibrazil Neymar. 
Judge Pablo Ruz alisema maamuzi yake yamekuja kutokana kuwepo kwa ushahidi wa kutosha juu ya mashtaka hayo yanayohusiana na uhamisho wa Neymar uliogharimu kiasi cha 57 million euro kutoka Santos msimu uliopita.
Ruz pia ametoa amri ya kuchunguzwa kwa Raisi aliyejiuzulu wa klabu ya FC Barcelona Sandro Rosell juu ya uhamisho huo. 
Rosell alijiuzulu haraka baada ya kugundulika kiasi cha 40 million euros ($55 million) za uhamisho zililipwa kwa kampuni ya baba yake Neymar, ambaye ameitwa kuja kutoa ushahidi mahakamani hapo. 
Barcelona imeyakataa mashataka hayo. 

Thursday, February 20, 2014

MCHEZO WA ARSENAL VS BAYERN MUNICH KWENYE NAMBA - KIWANGO CHA CHINI ZAIDI KWA ARSENAL MSIMU HUU

Usiku wa jana ulikuwa mrefu sana kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya timu yao kupigiwa soka la hatari na kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi wa klabu bingwa ya ulaya FC Bayern Munchen. 
Usiku wa jana tulishuhudia Bayern Munich wakiweka rekodi mpya ya Champions League baada ya kukamilisha asilimia 95% ya pasi walizopiga. 
Tuangalie ushindi huo wa Bayern kupitia mfumo wa namba. 

863

Hii ni namba ya pasi walizojaribu kupiga Bayern, 95% ya pasi hizi zilifika kwa wenzao. Hii ni rekodi mpya katika champions league tangu utaratibu wa takwimu kwenye mechi uanze msimu wa 2003-04 season..

222

Namba ya pasi walizojaribu kupiga Arsenal. Walikamilisha 71% ya pasi hizo. Namba ya chini kabisa kwa Arsenal katika takwimu za pasi, kabla ya jana namba ya chini kabisa ilikuwa 394, hii ilikuwa kwenye EPL dhidi ya Tottenham mwezi September mwaka jana. 

147

Hii namba ya pasi alizopiga kiungo wa Bayern Toni Kroos.  

127

Namba ya pasi alizopiga Toni Kroos katika nusu ya uwanja golini mwa Arsenal - alikamilisha 96.1% ya pasi hizo. 

100

Goli la Toni Kroos jana usiku lilikuwa goli la 100 kwa Bayern Munich katika mashindano yote msimu huu. Kadi nyekundu ya golikipa Wojciech Szczesny ilimfanya kuwa mchezaji wa 100 kupewa kadi nyekundu tangu Wenger aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 1995. 

78.8

Asilimia ya umiliki wa mpira waliyokuwa nayo Bayern Munich ndani ya dakika 90. 

30

Mchezaji aliyejaribu kupiga pasi nyingi zaidi kwa upande wa Arsenal alikuwa Jack Wilshare ambaye alikamilisha 66% ya majaribio 30.

26

Majaribio ya kufunga yaliyofanywa na Bayern katika goli la Arsenal, Arsenal walijaribu mara 8 tu - mara 1 tu katika kipindi cha kwanza. 

12

Arsenal waliweza kuwa na jumla ya 12% ya kumiliki mpira katika kipindi cha pili.

3

Winga wa Bayern Munich Arjen Robben ndio mchezaji pekee kuwahi kupewa penati 3 katika msimu huu wa Champions league. Mesut Ozil ndio mchezaji pekee aliyekosa mara mbili.  

PROMOTER JAY MSANGI AKAMILISHA MASHARTI YA BMT NA KUKABIDHI NYARAKA ZOTE KWA BMT

 Bondia Phil Williams akisaini mkataba wa malipo ya deni lake
huu ndio mkataba wa malipo ya bondia Phil Williams

meseji ya Ustaadh aliyomtumia Jay Msangi akimwambia hamdai.

MJADALA: NI KWELI MESUT OZIL HANA MSAADA KWA ARSENAL KWENYE MECHI KUBWA ?







 Pamoja na shutuma lukuki kumwandama kiungo Mesut Ozil alikuwa miongozi mwa wachezaji watatu waliotembea sana kiwanjani.
Hii ni orodha ya wachezaji waliojituma sana kwenye mchezo baina ya Arsenal na Bayern Munich

Mathieu Flamini = 13.53km
Jack Wilshere = 11.80km
Mesut Ozil = 11.69km
Mario Gotze = 11.68km
Yaya Sanogo = 11.50km

FABREGAS AOMBA RADHI KWA NIABA YA BARCELONA KUIFUNGA MANCHESTER CITY.

 Kiungo wa FC Barcelona Cesc Fabregas ilimbidi awaombe radhi mashabiki waliohudhuria tuzo za Uingereza kwa niaba ya klabu yake ya Fc Barcelona.
Fabregas ilimbidi aombe radhi baada ya mashabiki hao kuanza kumzomea pale alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya kikundi bora cha kimataifa,akiwa jukwaani na mwanamuziki Nicole Scherzinger ndipo kelele za kumzomea zilipoanza kusikika ukumbini hapo na yeye bila kuchelea aliwajibu '' samahani sana kwa yaliyotokea jana,nimekuja hapa kwa amani kabisa'' alizungumza Fabregas kabla ya kuwatunuku tuzu hiyo wasanii wa kikundi cha Daft Pun.
 Tuzo hizo zilifanyika jijini London kwenye ukumbi wa O2 Arena.
   Fabregas akiwa na mwanamuziki Nicole Scherzinger....
 Fabregas akitoka Hotelini jijini Manchester na wachezaji wenzake mara baada ya mchezo dhidi ya  Man City kurejea nchini Hispania,lakini yeye alimbidi aende jijini London kuhudhuria tuzo hizo.
Fabregas kushoto akishangilia na wachezaji wenzake bao la kwanza la Mesii kwenye mchezo dhidi ya Man City.

TENGA AMTEUA LAWRENCE MULINDWA KUWA MAKAMU WAKE CECAFA


VIDEO: BAYERN MUNICH YAENDELEA KUIONEA ARSENAL EMIRATES


Arsenal vs Bayern Munchen 0-2 by FootyLight0

VIDEO: AC MILAN YAPIGWA NYUMBANI NA ATLETICO MADRID

PICHA YA SIKU:


YALIYOJILI NA TAKWIMU MBALI MBALI ZA MCHEZO KATI YA AC MILAN NA ATLETICO MADRID.




YALIYOJILI NA TAKWIMU MBALI MBALI ZA MCHEZO BAINA YA ARSENAL NA FC BAYERN MUNCHEN.