Michezo ya iliyochezwa weekend hii katika ligi mbalimbali barani ulaya.Kuanzia kwenye Bundesliga, La Liga, mpaka kwenye Barclays premier league tumeshuhudia nyota kama Wayne Rooney, Edin Dzeko, Cristiano Ronaldo, Roberto Soldado na Maria Gomez wakifunga zaidi ya mabao 15 ndani ya wikiendi hii.
CRISTIANO RONALDO – REAL MADRID (LA LIGA)
Akicheza mechi yake ya kwanza ya La Liga, winga wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo alifanikiwa kufikisha idadi ya magoli 102 tangu ajiunge na Real Madrid miaka 2 iliyopita.
Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick katika mchezo huo dhidi Zaragoza, na kufikisha jumla ya hat tricks 9 tangu atue Santiago Bernebeu.
EDIN DZEKO (MAN CITY – EPL)
Baada ya kuhangaika kutafuta fomu yake msimu uliopita, mshambuliaji kutoka Bosnia Edin Dzeko amezidi kuwakata mdomo wote waliokuwa wana mashaka na uwezo baada ya jana kufunga mabao manne katika ushindi wa mbao 5-1 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Dzeko ambaye alianza msimu kwa kufunga moja ya mabao katika mechi ya ngao ya hisani dhdi ya Manchester, kwa sasa ndio anaongoza kwa ufungaji katika premier league akiwa na magoli 6.
ROBERTO SOLDADO – VALENCIA (LA LIGA)
Mshambuliaji wa zamani Real Madrid nae alifuata nyayo za Cristiano Ronaldo baada ya kuisaidia Valencia kuitandika Racing Santander kwa mabao 4-3 kwenye mchezo wa ufunguzi wa La Liga.
Soldado ambaye alilewa kwenye academy ya Real Madrid kabla kufanikiwa kuichezea Real Madrid B, baadae akafanikiwa kupanda mpaka kikosi cha wakubwa na alicheza kwa mechi takribani 11, na kufunga mabao mawili kwenye La Liga pekee, baadae akapitia kwenye timu kama Osasuna, Getafe na sasa yupo Valencia.
Mpaka sasa Soldado ameshafunga jumla ya mabao 63 katika michezo 141.
MARIO GOMEZ – BAYERN MUNICH (BUNDESLIGA)
Bayern Munich walienda kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani baada ya ushindi wa 3-0 dhidi Kaiserslautern, shukrani kwa mtoto wa nyumbani Mario Gomez aliyefunga mabao yote.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani ambaye alifunga goli pekee katika mchezo dhidi ya FC Zurich alianza kwa kufunga kwa penati dk ya 37 na baadae akafunga mengine mawili kipindi cha pili.
Gomez ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi kwenye Bundesliga, alikuwa mfungaji bora katika msimu uliopita wa ligi hiyo kwa kufunga mabao 28.
WAYNE ROONEY – MANCHESTER UNITED
Siku ya jana itakuwa ni siku ya kukumbukwa kwa Wayne Rooney baada ya kufunga mabao 3 katika ushindi wa 8-2 wa Man United dhidi ya Arsenal.
Hat-tricks ya jana ilikuwa ya 6 tangu ajiunge na United, akifikisha jumla ya mabao 152 akiwa Old Trafford na kumfanya aweze kuingia katika vitabu vya historia ndani ya United kwa kuwemo kwenye orodha ya wafungaji bora 10 wa muda wote wa klabu hiyo.
Pia jana Rooney aliendeleza historia yake ya kuifunga Arsenal, Rooney alifunga bao la kwanza kabisa akiwa na Everton dhidi ya Gunners in 2002, na pia Baba Kai alifunga bao la kwanza la EPL na goli 100 akiwa na United katika mechi dhidi ya Arsenal.