Search This Blog

Saturday, June 25, 2011

KAGAME CASTLE CUP: MATCH REPORT


MATCH REPORT: SIMBA VS VITAL'O - FIRST HALF

Vital'O waliuanza mchezo vizuri, wakitawala vilivyo mchezo ndani ya kipindi chote cha kwanza na wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini kukosa umakini na umahiri Juma Kaseja walizipoteza nafasi hizo.Kwa upande wa Simba wakiwa wamewaanzisha wachezaji wao wapya mabeki Derrick Walulya na Saidi Nassoro Cholo, Ulimboka Mwakingwe, Haruna Moshi na Salum Machaku walionekana kukosa maelewano na hivyo kupelekea kushindwa kucheza vizuri ndani kipindi hiki ingawa wachezaji kama Ulimboka Mwakingwe, Boban na beki Said Nassoro Cholo walionekana kucheza vizuri.
Ndani ya kipindi kwanza Simba walicheza faulo 14, Mgosi akicheza 5, Boban 3, Cholo 1,Maftaa 3, Santo akacheza 2 na kupata kadi moja ya njano.
Vital'O walicheza faulo 8.
Kona- Simba 5, Vital'O - 1

SECOND HALF
Kipindi cha pili Simba waliuanza mchezo kwa kasi Boban,Machaku na Mwakingwe wakilisakama lango la Vital'O, lakini kutokana na kukosa umakini kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi aliyecheza chini kiwango Msimbazi walishindwa kupata bao.
Vital'O ndani second half walionekana kuchoka na kutokana Simba kuwashambulia sana walianza kucheza rafu zisizo na msingi hasa kwa Boban.
Waburundi hawa baada ya kipindi cha pili kuanza walifanya mabadiliko kwa kumtoa Stanley Minzi na kuingia Mbakiye Beby Miami, pia walimtoa Ndizeye Alain akaingia Garukwishika Jean.
Simba waliwatoa Salum Machaku, Banka, Mgosi na nafasi zao zilichukuliwa na Shija Mkina, Patrick Mafisango na Rajab Isiaka.
Kipindi cha pili Simba walicheza Faulo 4, huku Vital O wakicheza faulo 10 na kupata kadi 1 ya njano.

MAONI YA MAKOCHA
Mosses Bassena-"Timu yangu ilijitahidi kucheza vizuri na kumiliki mchezo kwa zaidi ya asilimia 70, na tumepoteza nafasi nyingi za kufunga hasa ndani ya kipindi cha pili lakini haikuwa siku yetu hasa kwa Mgosi ambaye leo hakuwa ndani ya kiwango chake.Tunajipanga kucheza vizuri katika michezo inayofuatia ili tuweze kufanikisha adhma yetu kubeba kombe hili."

YAOUNDE KANYANKOLE - VITAL'O COACH
"Nashukuru timu imepata sare dhidi ya timu kubwa kama Simba tena ukizingatia tulikuwa tunacheza mbele ya maelfu ya washabiki wa wapinzani wetu lakini vijana wangu wamejitahidi na tumefanikiwa kupata sare.Naamini tutajipanga na kupata ushindi katika mechi zijazo.Simba ni timu nzuri japo wanaonekana hawajazoeana lakini naamini wakikaa muda mrefu watakuwa na timu bora."

BOXING: FRANCIS CHEKA VS DANIEL WANYONYI

Bondia Francis Cheka amefanikiwa kumshinda Daniel Wanyonyi kwa pointi katika pambano ambalo lilikuwa zuri na la kusisimua.



21: 10- Matokeo ni Cheka ameshinda kwa pointi kutoka kwa majaji wawili
21:06 - Raundi ya 10 imeisha na mkenya alianguka tena, tunasubiri matokeo
21: 02 - Raundi ya mambo sio mazuri kwa mkenya, Cheka anashambulia vilivyo
20:59 - Raundi ya 8, wanashambuliana zamu kwa zamu na Cheka amefanikiwa kumwangusha mkenya , lakini anainyka na kuendela na mchezo
20:55 - Raundi ya 7 mkenya anaendeleza mashambulizi lakini cheka anajitahidi
20:50 - Raundi ya 6 mkenya amezinduka Cheka ameelemewa
20:44 - Raundi ya 5 imeisha Cheka ameendelea kufanya vizuri na mkenya anazidi kuvimba jicho
20:40 - Raundi ya 4 imeisha Cheka anaendelea kupafomu vizuri, mkenya amechanika anatokwa na damu.
20:35 - Raundi ya 3 Cheka anendelea na mashambul
20:32 - Raundi pili mkenya anajaribu kurudisha mashambulizi.
20:20 - Raundi kwanza imeisha Cheka amecheza vizuri sana
20:15 - Pambano linaanza
20:13 - Nyimbo za taifa zinapigwa na unaanza wimbo wa Tz.
20:12 - Mabondia wote wanaingia ulingoni, Cheka anashangiliwa sana.

KAGAME CASTLE CUP: LIVE MATCH CENTER


MATCH UPDATE: SIMBA VS VITAL' O
dakika 45 za kwanza zimemalizika matokeo 0:0 huku simba wakionekana kuelemewa kwenye sehemu ya kiungo na kupelekea mpaka wakati huu wa mapumziko wachezaji wake wanaocheza sehemu ya kiungo kucheza jumla ya faulo 14 huku musa mgosi peke yake akiwa amecheza jumla ya faulo 5, Vital'o wamefanikiwa kuingia kwenye eneo la hatari la simba mara 6 huku golikipa juma kaseja akiokoa magoli mawili,
salum machaku wa simba kapewa kadi ya njano.
dakika 45: subs Vital'o, stanley Minzi-out,mbakiye bebi -in
dakika 60: SImba, salum machaku -out,shija mkina-in
dakika 64: nzigamasabosteve-yellow card
dakika 67: simba-subs ,mohamed banka-out,patrick mafisango-in
dakika 69: golikipa wa Vital'o ameumia baada ya kugongana na Ulimboka mwakingwe lakini ananendelea na mchezo
wakati huo huo simba wanaishambulia sana Vital'o
dakika 72: simba ,musa mgosi-out,rajabu ishiaka -in
dakika 74: bado matokeo ni 0:0,ulimboka mwakingwe amecheza vizuri sana kwa upande wa simba mpaka sasa.
huku mshambuliaji aliyeingia kipindi cha pili wa Vital'o ,mbakiye beby akiwasumbua sana mabeki wa simba.
dakika 81: saidi nassor amepiga shuti lake la 3 katika mchezo wa leo lakini linatoka nje
dakika 82: aruna moshi amepiga shuti limetoka juu ya goli.
dakika 86: vital'o wamekosa bao,
dakika 90: dakika mbili zimeongezwa

fulltime: simba 0:0 Vital'o

KAGAME CASTLE CUP: LIVE MATCH CENTER

OCEAN VIEW VS ETINCELLES

MATCH UPDATE: FULLTIME OCEAN VIEW 3-2 ETINCELLES

MATCH UPDATE:DK, 45, OCEAN VIEW2 - 2 ETINCELLES





VIKOSI VYA SIMBA NA YANGA VITAKAVYOSHIRIKI KAGAME-CASTLE CUP 2011


KIKOSI CHA SIMBA KATIKA KAGAME CASTLE CUP NI.
MAKIPA
Juma Kaseja
Will Ochieng

MABEKI
Salum Kanoni
Nassor Said Chollo
Amir Maftah
Patrick Mafisango
Kelvin Yondani
Juma Nyosso
Derrick Walyalu

VIUNGO
Mwinyi Kazimoto
Athuman Idd 'Chuji'
Jerry Santo
Haruna Moshi 'Boban'
Mohamed Banka
Ulimboka Mwakingwe

WASHAMBULIAJI
Shija Mkina
Rajabu Isiaka
Mussa Hassan 'Mgosi'













Kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania kitakachoshiriki michuano Kagame Castle Cup ni :





Yaw Berko, Mohamed Said, Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Nadir Haroub ' Canavaro', Chacha Marwa, Bakari Mbegu, Tonny Ndolo na Juma Seif 'Kijiko'.

Wengine ni Julius Mrope, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari, Jerry Tegete, Kenneth Asamoah, Kigi Makasi, Hamisi Kiza, Oscar Joshua na Davis Mwape.

THE CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP/ CLUB CHAMPIONSHIP BASIC RULES

The purpose of this circular letter is to bring to your notice some of the important rules and regulations, which govern our tournaments. These rules must be observed strictly.

1. PRE-MATCH MEETING

Pre-match meetings will be held at 10.00 a.m. one day before the match at the designated venue. Any changes will be notified to concerned teams.

a) Playing teams must send managers and team captains. It is preferable if coaches can attend also but a captain is a must.
b) All teams must register two sets of uniforms. The second named is the away team. In case of colour clash, the second named team shall be required to change.
c) Reporting time for every match at the Stadium is one hour before kick-off time.
d) On the day of the match, playing teams must confirm their starting line-ups two hours to CECAFA secretariat and sponsors to co-ordinate television programme.
2. FINES

Fines will be imposed as follows: -

a) Lateness for pre-match meeting $50
b) Teams without captain at the pre-match meeting $50
c) Teams reporting for the pre- match meeting without playing uniform $50
d) Teams reporting late at the stadium $50
e) CECAFA officials reporting late at pre-match meeting or stadium $50

f) Teams failing to honour post match interviews will be fined US 100

3. APPEALS

Appeals or protests must be submitted to the CECAFA secretary within three hours after the end of the match together with an appeal fee of 50 dollars. The fee is non- refundable.

4. PLAYERS REGISTRATION

Each team is allowed to register up to 20 players before the start of the tournament. No player will be allowed to use more than one number during the tournament. The list of 20 players cannot be altered. Failure to register players, a fine of $200 dollars and for a player using more than one number; a fine of $50 will be imposed. The $50 dollar rule will also apply to a player who fails to produce passport for National Team’s engagements and playing licence for Clubs competition during inspections. Players MUST produce playing licences aunthenticated by their federations during club cup championship. National teams jersey shall be numbered from 1-20 while clubs can number their jerseys from 1-35. But registration for both competitions is up to 20 players for the whole duration.

5. REPORTS

Referees and Match Commissioners reports must be received within three hours after the end of the match.

6. COMPLIMENTARY

The host association will give six complimentary tickets to the playing teams during the tournament. CECAFA officials will also receive two complimentary tickets per official. The tickets will be given during pre-match meetings.

7. DEPARTURE

Teams eliminated in preliminary rounds will be required to leave within the next available means or 24 hours unless there is absolutely no connection within that period. Any additional stay will be covered by the teams concerned. Acquisition of visas and all travel arrangements will be the responsibility of each team. And travel schedule regarding arrival and visa acquisition if need should be submitted to CECAFA and host nation one month before the start of the competition. CECAFA will not be liable to compensate teams with visa fees.

8. FORCE MAJEURE

Where a match ends prematurely as a result of force majeure or darkness or any other reasons then the organising committee will decide when the match shall be replayed.

9. SIZE OF THE PARTY

Each team is allowed a party of 25 people inclusive of players and officials. Visiting team must meet the cost of extra people, if any. CECAFA and host nation will not entertain extra persons. During your stay, CECAFA and host nation will cover full board accommodation, meaning Bed and breakfast, lunch with one small soft drink, dinner with one small soft drink. All other extras like laundry, water during training, alcohol, extra meals, telephone/fax/internet should be covered by the teams and individual delegates.

10. TROPHIES/MEDALS

The first, second and third teams will receive gold, silver and bronze medals in that order. Each team will be entitled to 25 medals.

11. All delegates to CECAFA tournaments MUST carry their national flags and
Two Cassette of the national anthem.

12 A team causing abandonment of a match for whatever reasons shall be disqualified from the tournament and forfeit all it’s right due to it. The team shall leave for home with the immediate available transport.

13. The host FA will provide you with more information concerning or related to the tournament.

14. All Member Associations MUST pay US$1500 annual fee and every participating team/club MUST pay US$ 400 as participation fee before the start of the tournament.
15. One day before the start of the competition, there will be an orientation for all teams who must send their head of delegation, team manager, doctor and captain.
16. During our competitions starting with Challenge cup 2007, all national teams cannot display any of its sponsors on their kit. Clubs must also inform CECAFA their sponsors two weeks before the start of the event.
17. During our challenge cup and club cup competitions, our sponsors have the following rights: a)To host any team at a place of their choice
b)To be photographed with teams and players
c)Display their promotional materials

18. In order to improve the day to day general administration of CECAFA, it is my sincere hope that all leaders will co-operate. The teams should also display the FIFA FAIR PLAY MOTTO during the tournament.



NOTE. ANY Rule not provided in the above basic regulations, the organizers will refer to CAF and FIFA rules for direction

Nicholas Musonye
GENERAL SECRETARY

Friday, June 24, 2011

LEO KATIKA BABA NA MWANA

IAN WRIGHT AKIMZINGUA MWANAE SHAUN WRIGHT PHILIPS KATIKA MECHI YA KUMUAGA MARTIN KEOWN


Jordi Cruyff akimbusu baba yake Johan Cruyff baada ya kupokea medali ya ushindi wa pili wa kombe UEFA Cup kutoka kwa UEFA President Lennart Johansson.

Wim Bergkamp akimpigia mpira mwanae Dennis katika mchezo wa kumuaga uliofanyika katika uwanja wa Emirates, mwaka 2006.

SAMUEL ETOO AKIPOKEA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA KUTOKA BABA YAKE


Jack Rodwell akisaini mkataba mpya wa Everton akiwa na Baba yake Malcom.

MAJEMBE MAPYA YA AZAM TOKA NCHINI GHANA YAWASILI

MWANASHERIA WA AZAM FC AKISHUHUDIA WINO UKIMWAGWA NA MSHABULIAJI WAHAB YAHAYA

HAPA NI BAADA YA KUFIKA KWENYE KLABU YA AZAM FC

BEKI NAFIU AWUDU AKIMWAGA WINI KWENYE FORM ZA AZAM FC


Beki wa kimataifa wa Ghana ambaye ni nahodha wa kikosi cha King Faisa, na Nahodha wa timu ya Taifa ya Ghana cha wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani Nafiu Awudu (KUSHOTO ) akiwa na mshambuliaji aliyefunga magoli 10 msimu huu ligi kuu ya Ghana Wahab Yahaya. wote wamemwaga wino kuichezea Azam FC leo hii

WAKENYA WAZIDI KUTIKISA USAJILI WA ULAYA


Baada ya juzi mdogo wa Mcdonald Mariga kuripotiwa kuzivutia klabu za Celtic na Aston Villa, sasa ni zamu mkenya mwingine Eric Odhiambo ametingisha soko la uhamisho nchini Scotland.

Odhiambo ambaye msimu uliopita alimaliza mkataba wake na klabu ya Inverness amekuwa akifuatilia na klabu kadhaa nchini baada ya kumalizika kwa ligi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa wakala wa mshambuliaji huyo aliyejiunga na Inverness mwezi January 2009, alifunga mabao 4 katika michezo 18 ya msimu uliopita likiwemo goli la kusawazisha alilofunga dhidi ya Glasgow Rangers, anasema mchezaji huyo wa zamani Leicester amezivutiwa klabu kadhaa nchini Scotland zikiwemo timu kubwa.

"Nafahamu kuna klabu nyingi zinamtaka Eric, kuna timu moja tayari wameshatuma ofa lakini Eric anasubiri kuona kama kuna timu nyingine zitaleta ofa halafu ataangalia ipi bora ya kuichukua."-alisema wakala wa mchezaji huyo Clive Hart.


KAGAME CASTLE CUP PREVIEW

MABINGWA mara sita wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Simba SC ‘Wekundu wa Msimbazi’, Jumamosi hii wanafungua dimba la michuano hiyo inayojulikana Kombe la Kagame tangu mwaka 2002, kwa kumenyana na Vital’O ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba walio chini ya kocha Mganda, Moses Bassena watamenyana na Vital’O timu ambayo pamoja na kuwa na historia ya kucheza soka tamu kwenye michuano hii, lakini hawajawahi kutwaa taji, siku moja kabla ya watani wa wa jadi, Yanga kucheza mechi yao ya kwanza na el Merreikh ya Sudan.
Hadi leo bado haikuwa imejulikana ni wachezaji gani (20) ambao Simba imetuma majina yake CECAFA kwa ajili ya kuwatumia kwenye michuano hiyo, lakini katika wachezaji wapya, shaka ipo kwa beki Shomari Kapombe wa Polisi Moro na kiungo Mwinyi Kazimoto tu iliyemsajili kutoka JKT Ruvu, kutokana timu za za jeshi kuweka ngumu, kwa kudai ni waajiriwa wa taasisi hizo na hawawezin kufanya kazi uraiani.
Wachezaji wengine wapya wa Simba, kipa Mkenya, Willies Ochieng, aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Finland, mabeki Obadia Mungusa ‘Robot’ wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Nassor Masoud ‘Choro’ wa JKT Oljoro, viungo Haruna Moshi ‘Boban’ mchezaji huru, Athumani Iddi ‘Chuji’ wa Yanga na Salum Machaku wa JKT Ruvu.
Bassena ataunganisha wachezaji hao na wale aliowakuta kwenye klabu hiyo akina Juma Kaseja, Salum Kanoni, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Jerry Santo, Mohamed Banka, Amri Kiemba, Emmanuel Okwi, Mussa Mgosi, Shija Mkina, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Nico Nyagawa kupata nyota wa kucheza Kombe la Kagame.
Kwa vyovyote, mechi ya Jumamosi inatarajiwa ngumu kwa Simba, kwani Vital’O ambayo imecheza Robo Fainali tatu za michuano ya klabu Afrika, Ligi ya Mabingwa mwaka 1985 na lililokuwa Kombe la Washindi mara mbili katika miaka ya 1983 na 1990 miaka yote imekuwa ikitoa ushindani na kuonyesha soka safi, ingawa kutwaa taji ndio imekuwa mtihani mgumu kwao
.

Vital'O FC iliyoanzishwa kama Rwanda Sport FC miaka 1960, kabla ya kuwa ALTECO mwaka 1971, baadaye Tout Puissant Bata mwaka 1973, kisha Espoir kabla ya kuanza kutumia jina lake la sasa (Vital'O) mwaka 1975, itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Simba 1-0 zilipokutana mara ya mwisho kwenye michuano hii, Julai 20, mwaka 2008 Dar es Salaam, bao pekee la beki Kelvin Yondan dakika ya 42, mchezo wa Kundi A, ulioihakikishia Simba tiketi ya kuingia Robo Fainali.
Simba, ambao ni mabingwa mara nyingi wa michuano hii, pia ndio timu ya mwisho ya Tanzania kuchukua Kombe la Kagame wa 2002 visiwani Zanzibar, ikiiwafunga 1-0 Prince Louis ya Burundi, bao pekee la Nteze John dakika ya sita, kikiosi cha Wekundu wa Msimbazi kikiundwa na Mohamed Mwameja, Said Sued, Ramadhan Ramadhan aliyetoka na kumpisha Majuto Komu dakika ya 35, Amri Said, Boniface Pawasa, Suleiman Matola, Stephen Mapunda ‘Garrincha’ aliyempisha Joseph Kaniki ‘Golota’ dakika ya 74, Shekhan Rashid, Yusuf Macho, Nteze John aliyempisha Emmanuel Gabriel dakika ya 61 na Mkenya Mark Sirengo
YANGA V EL MERREIKH:
Yanga, wanaorejea kwenye michuano hiyo tangu washiriki kwa mara ya mwisho mwaka 2008 na kukomea Nusu Fainali, watafungua dimba na El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, siku ambayo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro watetezi wa taji, APR watamenyana na Ports.
Unatarajiwa kuwa mchezo mwingine mkali na wa kihistoria, kwani utawakumbusha mashabiki wa Yanga fainali ya michuano hiyo, mwaka 1986 Abubakar Salum ‘Sure Boy’ akiwa bado mbichi anaingia kutokea kwenye benchi na kufanya mambo makubwa, lakini mwishowe yeye mwenyewe anaharibu.
Sure Boy alitokea benchi Yanga ikiwa nyuma kwa mabao 2-0 na kusawazisha yote, lakini mchezo ulipohamia kwenye mikwaju ya penalti winga huyo matata wa zamani pamoja na kiungo Muhiddin Cheupe walikosa penalti zao, Yanga ikilala 4-2 na kukosa Kombe nyumbani.
Lakini ubabe wa Merreikh kwa Yanga uliendelea tena mwaka 2007 katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika walipowatoa mabingwa hao wa Bara kwa jumla ya mabao 2-0, wakianza na sare ya bila kufungana Uwanja wa Kirumba mwanza, mechi ambayo aliyekuwa mfadhili wa Yanga, Yussuf Manji aliinunua kwa Sh. Milioni 100 na mashabiki wakaingia bure.
Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ wakati huo, ilitoka kutolewa na Esperance ya Tunisia katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa kwa kichapo cha mabao 3-0.
Yanga ipo Kundi B na El Merreikh ya Sudan, Bunamwaya ya Uganda na Elman ya Somalia, wakati Simba SC ipo Kundi A na Vital’O ya Burundi, Etincelles ya Rwanda na Ocean View ya Zanzibar na mabingwa watetezi, APR wamepangwa kundi C pamoja na St George ya Ethiopia, Ulinzi ya Kenya na Ports ya Djibouti.
Timu mbili za juu katika kila kundi, zitafuzu moja kwa moja kuingia Robo Fainali, wakati washindi wa tatu wa makundi yote watalinganishwa kwa wastani wa pointi ili kupata timu nyingine mbili za kutinga Robo Fainali, zitakazochezwa Julai 4 na 5 na kuonyeshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya Supersport ya Afrika Kusini.
Nusu Fainali zitachezwa Julai 6 na 7 na mechi ya kusaka mshindi wa tatu pamoja na fainali zitachezwa Julai 9, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Michuano ya Kagame ilianza kama Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, mwaka 1974 kabla ya kuwa Kombe la Kagame mwaka 2002, kufuatia Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuamua kudhamini michuano hiyo.
Simba inaongoza kuchukua taji hilo mara nyingi, mara sita, ikifuatiwa na AFC Leopards mara tano sawa na Tusker FC zote za Kenya, Yanga mara tatu sawa na APR FC, Gor Mahia ya Kenya na SC Villa ya Uganda, wakati Luo Union na El-Merreikh zimetwaa taji hilo mara mbili na ATRACO ya Rwanda, KCC, Police FC za Uganda na Rayon Sports zimetwaa mara moja kila moja.
Timu ya mwisho ya Tanzania kutwaa taji hilo ni Simba SC mwaka 2002 visiwani Zanzibar, wakati miaka miwili mfululizo iliyopita taji liliweka maskani Rwanda, 2009 kwa ATRACO na 2010 kwa APR.

GASPERINI KOCHA MPYA WA INTER MILAN


INTER MILAN wamemthibitisha Gian Gasperini kuwa kocha wao mpya.
Gasperini, 53, bado hajamaliza hatua za mwisho za kukamilisha mkataba wa miaka miwili lakini Inter wamethibitisha kuwa ndiye mrithi wa Leonardo.
Akiongea na vyombo vya habari Raisi wa Inter Massimo Moratti alisema: "Nimeridhika na uteuz wa Gasperini, namtakia kazi njema katika kuiwezesha Inter kuwa mabingwa wa dunia."
Gasperini ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Genoa, aliiwezesha timu hiyo kurudi katika Seria A na kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya katika EUROPA Cup kabla hajafukuzwa November mwaka jana.

LIGI KUU YA ENGLAND - USAJILI ULIOKAMILIKA MPAKA LEO



Arsenal
Ins:
Carl Jenkinson (from Charlton Athletic for undisclosed)

Aston Villa
Outs:
Brad Friedel (to Tottenham for free)

Blackburn Rovers
Outs:
Phil Jones (to Manchester United for £16.5m), Zurab Khizanishvili (to Kayserispor, TUR for undisclosed), Frank Fielding (to Derby County for undisclosed)

Bolton
Outs:
Johan Elmander (to Galatasaray, TUR for free)

Chelsea
Ins:
Lucas Piazon (from Sao Paulo, BRA for undisclosed)

Outs:
Michael Mancienne (to Hamburg, GER for undisclosed), Jacopo Sala (to Hamburg, GER for undisclosed), Gokhan Tore (to Hamburg, GER for undisclosed)

Everton
Outs:
James Vaughan (to Norwich City for undisclosed), Hope Akpan (to Crawley Town for free)

Fulham
Ins:
Dan Burn (from Darlington for undisclosed)

Liverpool
Ins:
Jordan Henderson (from Sunderland for £16m)

Manchester United
Ins:
Phil Jones (from Blackburn Rovers for £16.5m), Ashley Young from Aston Villa

Outs:
Bebe (to Besiktas, TUR on loan), Ritchie de Laet (to Norwich City on loan)

QPR
Outs:
Mikele Leigertwood (to Reading for undisclosed)

Newcastle United
Ins:
Yohan Cabaye (from Lille, FRA for £4.3m), Demba Ba (from West Ham United for free), Sylvain Marveaux (from Rennes, FRA for free*), Mehdi Abeid (from Lens, FRA for undisclosed)

Outs:
Kevin Nolan (to West Ham United for £4m)

Norwich City
Ins:
James Vaughan (from Everton for undisclosed), Steve Morison (from Millwall for £2.1m), Elliott Bennett (from Brighton for £1.2m), Ritchie de Laet (to Manchester United on loan)

Stoke City
Outs:
Abdoulaye Faye (to West Ham United for free)

Sunderland
Ins:
Ahmed Elmohamady (from ENPPI, EGY for £2m), Sebastian Larsson (from Birmingham Cityfor free*), Keiren Westwood (from Coventry City for free*)

Outs:
Jordan Henderson (to Liverpool for £16m)

Swansea City
Ins:
Danny Graham (from Watford for £3.5m)

Outs:
Dorus de Vries (to Wolves for free)

Tottenham
Ins:
Brad Friedel (from Aston Villa for free)

Outs:
Jamie O’Hara (to Wolves for undisclosed*)

West Bromwich Albion
Ins:
Billy Jones (from Preston North End for undisclosed), Gareth McAuley (from Ipswich Town for free)

Wolves
Ins:
Jamie O’Hara (from Tottenham for £5m*), Dorus de Vries (from Swansea City for free*)

USAJILI WAZIDI KUPAMBA MOTO BARANI ULAYA.


Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa paundi million 26.5 kwa ajili ya mshambuliaji wa F.C Porto Radamel Falcao, baada ya mkorombia huyo kukubali deal la kuvuna paundi million 5 kwa mwaka na matajiri hao London.

Falcao ambaye alifunga mabao 39 katika msimu uliopita anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea tarehe 1 Julai.

Usajili huu wa Falcao umezua maswali mengi kuwa ni nani kati ya Fernando Torres, Didier Drogba na Nicolas Anelka atafunguliwa milango ya kuondoka Stamford Brdige.


ARSENAL WAKATAA OFA YA PAUNDI MILLION 27 KWA FABREGAS


Klabu ya Arsenal imekataa ofa paundi million 27 kutoka Barcelona kwa ajili ya kiungo Cesc Fabregas.

Barca ambao wamekuwa katika harakati za kumrudisha Catulunya kwa zaidi ya miaka 3 lakini Gunners siku zote wamekuwa wagumu kumuachia Mhospania huyo.

Ripoti zinasema kuwa CEO wa Arsenal Ivan Gazidis aliikataa ofa rasmi ya Barca iliyowasilishwa na makamu wa raisi wa mabingwa hao Ulaya Maria Bartomeu ambaye alikuwa London wiki iliyopita.Hata hivyo taarifa kutoka vyanzo vya habari kutoka Nou Camp zinasema Barca wanajipanga kupeleka tena ofa nyingine kwa Arsenal ndani siku chache zijazo.


Wakati huo huo manager wa klabu ya Barcelona Pop Guardiola amesema kuwa usajili wa Fabregas kipaumbele cha kwanza katika mipango ya kukimarisha kikosi chake.

Akiongea na vyombo vya habari vya Spain Gurdiola alisema: "Kumsajili Cesc ndio kipaumbele cha kwanza katika usajili wa msimu huu kwa sababu ndiye mchezaji ambaye yupo katika mipango ya muda mrefu ya klabu hii."


MAN CITY WAMGEUKIA MATA


Baada ya kutoswa na Alexis Sanchez sasa matajiri wa EPL Manchester City wanajipanga kumsajili winga wa Valencia ya Hispania Juan Mata.

Mabingwa hao FA Cup wanajipanga kukiongezea ubora kikosi cha Roberto Mancin ambacho kimepata nafasi ya kushiriki katika ligi wa mabingwa wa ulaya msimu ujao.

City ambao juzi ripoti kutoka Chile zinasema baada ya klabu hiyo kuizidi mbio Barca za kumsajili Sanchez, walipewa nafasi ya kuongea na mchezaji mwenyewe lakini Sanchez aligoma kuongea na timu hiyo, lakini katika hali nyingine jana mmiliki wa Udinese Gianpaolo Pozzo alisema mchezaji huyo anauzwa kwa paundi million 44, kiasi ambacho kimeongeza ugumu katika suala la mchile huyo hivyo kuwafanya City kumgeukia Juan Mata kama mbadala.

Juan Mata kwa sasa yupo katika kikosi Spain under 21 katika michuano ya EURO under 21.


LIVERPOOL KUTOA OFA YA PAUNDI MILLIONI 10 KWA CHARLIE ADAM



Majogoo wa jiji Liverpool wanategemea kuwasilisha rasmi ofa paundi million 10 kwa ajili ya kupata huduma za kiungo Charlie Adam katika mazungumzo yao na klabu ya Blackpool yaliyopangwa kufanyika weekend hii.

Kiungo mwenye umri wa miaka 25 pia amekuwa katika rada za Sir Alex Ferguson lakini Liverpool wanaonekana kuwa nafasi zaidi ya kupata saini ya kiungo huyo ambaye walitoa ofa ya paundi million 8 mwezi January lakini Blackpool wakachomoa.

Liverpool wanatarajiwa kukutana na mwenyekiti wa Blakcpool Karl Oyston.


Ashley Young - First Interview - MUTV

Cavaliers make Irving No. 1 pick & Top 10 drafts of all time.

Bila kificho mimi ni mpenzi mkubwa wa mchezo wa soka kwa kuucheza na kuangalia,lakini pia naipenda michezo mingine kwa kuicheza na kuiangalia,michezo ninayoipenda ni KIKAPU,MPIRA WA MEZA NAVOLLEYBALL,nakumbuka mwaka 2000 nikiwa pale Azania Secondary kwenye michezo ya UMISETA nilichaguliwa kwenye timu nne za Wilaya ya Ilala kwenye hiyo michezo,baadae nikachaguliwa timu tatu za mkoa wa Dar Es Salaam kwenye michezo ya SOKA,KIKAPU NA MEZA.
Kwa upande wa Kikapu nimekua mpenzi mkubwa sana wa ligi ya NBA,usiku wa kuamkia leo Draft za NBA zimefanyika, kwa mtazamo wangu nimetengeneza top 10 drafts of all time.

1.Ervin ‘magic’ Johnson, LA LAKERS .1979. Magic anaaminika kuwa mtu aliyeubadilisha mchezo wa kikapu kwa upande wa biashara . Hii ni kutokana na upinzani wake na nyota mwingine Larry Bird , upinzani ambao ulikuwa sawa na upinzani wa kanda ya mashariki na kanda ya magharibi . Upinzani huu uliipa ligi ya NBA umaarufu mkubwa kama kampuni ya kibiashara .

2.Bill Russell,Boston Celtics,1956.Bill Russell ni moja kati ya draft bora za miaka yote kwenye NBA . Sababu kubwa ni jinsi alivyoweza kuunganisha juhudi ,kipaji na uwezo binafsi sambamba na majukumu ya uongozi kwenye timu yake ya Boston Celtics . Chini ya Russell Celtics waliweza kutwaa taji la NBA mara 11 kwenye misimu 13 .
3.Michael ‘mj’ Jordan ,CHICAGO BULLS ,1984. Hakuna anayejua kwanini timu ya Portland Trail Blazers ambayo ilikuwa na nafasi ya kumchagua Jordan iliamua kuachana naye na kumchagua mtu mwingine Sam Bowie kwenye nafasi ya pili waliyokuwa nayo ya kuchagua mchezaji mwaka 84,Houston Rockets walimchagua Hakeem Olajuwon mwaka huo huo kwenye nafasi ya kwanza . Kimsingi walichokosa Blazers kilikuwa faida ya bulls kwani chini ya Jordan Bulls waliweza kutengeneza historian a Jordan mwenyewe alijiwekea historia yake binafsi si tu kama mchezaji wa NBA bali mwanamichezo maarufu kuliko wote ulimwenguni.
4. David Cowens,Boston Celtics ,1970. Huyu ni mmoja wa wachezaji waliojishindia tuzo lukuki wakati wake kwenye NBA , Cowens aliweza kurithi vyema nafasi ya Bill Russell kwenye timu ya Boston Celtics akiwaongoza kutwaa mataji mawili ya NBA .
5. Kevin Garnett,MINESOTTA TIMBERWOLVES ,1995. Minesotta walionekana kama wanafanya mchezo wa hatari kumsajili mtu ambaye hana uzoefu wa mashindano ya vyuo NCAA , lakini mwishowe haikuwa hivyo kwani Garnett au KG kama mashabiki wa kikapu wanavyomuita aliiishia kuwa mmoja wa wachezaji bora wa nafasi yake , Garnett alikuja kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya kwanza akiwa na Boston Celtics mwaka 2008.
6.Larry Bird,1978.BOSTON CELTICS Huyu ni mtu ambaye alichaguliwa kabla ya msimu wa mashindano ya vyuo kumalizika akiwa na chuo chake cha Indiana State . Bird ni mmoja kati ya wachezaji bora wa muda wote kwenye ligi ya NBA .
7.Dirk Nowitzki,Milwaukee Bucks , 1998. Dirk Nowitzki alichaguliwa na timu ya Milwaukee Bucks lakini kwenye siku hiyo hiyo ya Draft Dallas walimbadili na Robert Taylor waliyemchagua kwenye nafasi ya Sita na kumchukua Nowitzki . Uwezo mkubwa alio nao Dirk wa kutupa mitupo ya point tatu ulibadili kabisa mtazamo wa NBA na mchezo wa kikapu kwa ujumla kwa nafasi ya power forward . Dirk aliiongoza Dallas kufika fainali ya NBA mwaka 2006 ambapo alichaguliwa kuwa MVP kwa mwaka uliofuata na mwaka huu kwa msimu ulioisha aliiongoza Dallas Mavericks kutwaa ubingwa wa NBA huku akichaguliwa tena kuwa MVP .

8.Paul Pierce,BOSTON CELTICS ,1998.Mwanzoni Pierce alitazamwa kama mtu ambaye angewemo kwenye lajawapo kati ya nafasi tatu za juu kwenye orodha ya wachezaji ambao walikuwa wanachaguliwa kwenye draft ya mwaka 98 , lakini laiishia kuchaguliwa katika nafasi ya 10. Almanusura aombe uhamisho lakini ujio wa Ray Allen na Kevin Garnett ulimsaidia kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa NBA na sasa akaribia rekodi ya kuwa mfungaji wa pili kwa ubora wa miaka yote kwenye timu ya Boston Celtics .
9.Reggie Miller,INDIANA PACERS ,1987.Reggie Miller ni mmoja kati ya watupa 3 pointers bora wa miaka yote na alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya marekani Dream Team kwa miaka mingi na alikuwa anachezeshwa kwa jukumu la kufunga 3 pointers tu .
10.Jullius ‘dr J’ Erving , Milwaukee Bucks ,1972.Dr J angeweza kuwa timu moja na gwiji Kareem Abdul Jabar lakini mwishowe aliishia kuwa Philadelphia 76ers ambako aliweza kutwaa ubingwa wa NBA pamoja na tuzo ya MVP.


Kyrie Irving mwenye Mpira amekua Drafted Namba 1 na kunyakuliwa na CLEVELAND CAVALIERS.



tupo pamoja!! -MARCIO MAXIMO



Thursday, June 23, 2011

LUNYAMILA ANATOKA UJERUMANI KUJA KUMUUA SIMBA!

Winga hatari wa zamani klabu ya Dar es salaam Young Africans Edibily Jonas Lunyamila, akimtoka beki wa zamani wa Simba Mathias Mulumba, katika mchezo wa fainali ya kombe la Hedex kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika miaka ya tisini, na hii ilikuwa ni muda mfupi baada ya Lunyamila kutua nchini toka nchini Ujerumani alikokuwa amekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, na siku hii akiwapiga Simba moja kati ya mabao mawili na lingine likifungwa na Bakari Malima kufuatia kona ya Lunyamila.

EXCLUSIVE INTERVIEW:NIMEKUJA KUFANYA KAZI-NIYONZIMA

Aliyekuwa mchezaji wa kutumainiwa wa Klabu ya APR ya Rwanda HARUNA NIYONZIMA amewasili rasmi nchini akitokea nchini humo ili kujiunga na Young Sports Club ya Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Shaffih Dauda Blogspot, NIYONZIMA amesema amewasili nchini ili kuitumikia klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuiwezesha kupata mataji mbalimbali ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo aliyepokelewa na viongozi mbalimbali wa Klabu ya Yanga, alikuwa akitajwa mara kwa mara na mashabiki wa timu hiyo kwamba atajiunga na vijana wa jangwani ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.

“Nimekuja nchini kufanya kazi na si vinginevyo, soka linachezwa popote ninachoomba ni ushirikiano kutoka kwa mashabiki, wachezaji na viongozi wa timu kwani bila ushirikiano siwezi kufanya lolote Jangwani,” alisema NIYONZIMA.

Akifafanua mchezaji huyo wa kimataifa amesema, yeye sio Mungu na anayeweza kufanya maajabu akiwa klabuni hapo.
Kutokana na hilo alisisitiza kutumia uwezo wake kwa ushirikiano na wachezaji wenzake ili kupata mafanikio.

Kuhusiana na Michuano ya Kombe la Kagame Castle Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni katika viwanja mbalimbali ikiwemo Taifa na Jamuhuri mkoani Morogoro, NIYONZIMA amesema hilo liko chini ya viongozi wa klabu ya Yanga.

“Siwezi kusema kama nitashiriki kwenye michuano ya Kombe la Kagame, mimi ni mwajiriwa wa Jangwani kwa sasa hivyo wao ndio watakaoamua nani wa kucheza au lah,” alibainisha mchezaji huyo.

Wakati huo huo alizungumzia mustakabali wake wa baadae kuhusiana na soka na kusema anaiheshimu kazi hiyo kwa kuwa ndio inayompa fedha za kujikimu kimaisha ikiwemo kuhudumia familia yake.

Hivyo amejiunga na Yanga baada ya kupata ushauri kwa marafiki zake ikiwemo wachezaji wenzake wanaocheza soka nchini ambao wamempa moyo kwamba atafanya vizuri akiwa na timu hiyo.

Kuhusiana na kama atarudi APR ya Rwanda mara baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika NIYONZIMA amesema hatarajii kufanya hivyo kwani kitendo cha kuondoka hakikuwafurahisha viongozi wa timu hiyo.

“Ni vigumu kuzungumzia hali ya baadae kimpira, ila kwa kuwa ni mchezo lolote linaweza kutokea. Nimeondoka APR huku viongozi wangu wakiwa na kinyongo,” alimalizia.

ANDY COLE KUTEMBELEA TANZANIA WIKI IJAYO

UNAMFAHAMU ANDREW ALEXANDER COLE,AU KWA KIFUPI ANDY COLE , ANDY COLE NI MFUNGAJI BORA WA PILI WA MUDA WOTE KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND AKIFUNGA MABAO 187,

REKODI AMBAYO NI ALAN SHEARER PEKEE AMEIPITA KWA MABAO YAKE 260.COLE ANA HESHIMA YA KIPEKEE AMBAYO NI ILE YA KUWA MCHEZAJI ALIYETUNUKIWA TUZO KARIBU ZOTE NCHINI ENGLAND , COLE AMEWAHI KUTWAA TUZO YA PFA YOUNG PLAYER OF THE YEAR, PAMOJA NA TAJI LA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA.

KWENYE TAREHE 29 YA MWEZI HUU ANDREW ALEXANDER COLE ATAZURU NCHINI TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA PROJECT YA AIRTEL RISING STARS.

TFF WANANIZINGUA SANA KUHUSU ITC YANGU-SHEKHAN RASHID

shekhan rashid (kushoto ) akiwa mazoezini nchini Sweden.




Muda mchache uliopita nifanya mahojiano na kiungo Shekhan Rashid ambaye kwasasa anacheza soka la kulipwa nchini Sweden.

Shaffih K Dauda

mambo vipi kaka,unaendeleaje huko?

Shekhan Rashid
nipo kaka tff wananizingua sana kuhusu itc yangu,maombi yametumwa wiki ya 4 sasa kimya kujibu hawataki..
Shaffih K Dauda
duu ebu nipe details za kutosha nilifanyie kazi­ ­..
Shekhan Rashid
walitumiwa maombi na SFF (Swedish Football Federation ) wiki nne zilizopita, juzi wakatumiwa reminder na tukapiga simu kwa Angetile ambaye alikubali kuwa ameipata hiyo Email akasema ameijibu kwa fax na email, lakini chama cha mpira huku wakasema hawajapata jana tukampigia simu tena Angetile akasema ana-sign na kuituma wakati kasahau kua aliniambia kaituma. leo asubuhi tukampigia tena simu akasema nimetuma tumeenda chama cha mpira hapa kumbe bado hawajatuma. sielewi ugumu uko wapi wakati mimi sina mkataba na timu yoyote toka mwaka 2009 sioni ugumu uko wapi kutuma hiyo ITC. unaona viongozi wanavyoua soka huko tz ? sisi tunao malizia soka inakuwa hivyo jee vipi Vijana wanaochipukia itakuwaje?..
Shekhan Rashid
SFF imenionyesha mpaka fax na delivery report kuwa imefika..ila TFF hawataki kunitumia ITC
,

Shaffih K Dauda

pole sana kaka,ngoja niifuatilie ishu yako.








VIINGILIO KAGAME CASTLE CUP 2011

Michuano ya Kagame Castle Cup 2011 inaanza keshokutwa (Juni 25 mwaka huu) ambapo
viingilio kwa kituo cha Dar es Salaam vitakuwa VIP A sh. 15,000, VIP B sh.
10,000, VIP C sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 5,000, viti vya bluu sh.
3,000 na sh. 2,000 kwa viti vya kijani. Kwa siku ambazo timu za Yanga au Simba
hazitacheza kiingilio cha chini kitakuwa sh. 1,000.

Kwa kituo cha Morogoro ambapo mechi zitachezwa Uwanja wa Jamhuri kiingilio
kitakuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 1,000 mzunguko.

Pia kumefanyika mabadiliko katika mechi za kwanza za timu za Simba na Yanga.
Mechi ya Simba na Vitalo ya Burundi iliyokuwa ichezwe siku ya ufunguzi Juni 25
mwaka huu sasa itachezwa Juni 26 mwaka huu.


Nayo mechi kati ya Yanga na El Mereikh ya Sudan iliyokuwa ichezwe Juni 26 mwaka
huu sasa itachezwa Juni 25 mwaka huu. Mechi zote hizo zitaanza saa 10 kamili
jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu ambayo imeshawasili mpaka sasa ni Vitalo wakati Elman ya Somalia, Ocean
View ya Zanzibar na El Merreikh zinatarajiwa kuwasili leo kuanzia mchana.

Vilevile mtihani wa utimamu wa viungo (physical fitness test) kwa waamuzi
watakaochezesha michuano hiyo utafanyika kesho (Juni 24 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.


Waamuzi ni Gebremichael Lulesghed –Eritrea, Dilicho Sherefa- Ethiopia, Sylvester
Kirwa-Kenya, Wiish Yabarow –Somalia, Hussein El Fadil –Sudan, Israel Mujuni –
Tanzania, Ronnie Kalema –Uganda na Ibada Kombo –Zanzibar.

Waamuzi wasaidizi ni Charles Nizigiyimana –Burundi, Egue Yassen Hassan –
Djibouti, Mussie Kinde –Ethiopia, Brasan Mamati –Kenya, Simba Honore –Rwanda,
Ahmed Waleed –Sudan, Samwel Mpenzu –Tanzania na Mark Ssonko –Uganda.

MAFUNZO KWA MAKATIBU WAKUU


Mafunzo kwa ajili ya mfumo wa uhamisho wa wachezaji (Transfer Matching System-
TMS) na usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom yatafanyika kwa
siku tatu kuanzia Juni 27 hadi 29 mwaka huu.

Washiriki wa mafunzo hayo yatakayofanyika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ni makatibu wakuu na mameneja wa TMS (TMS Managers) wa
klabu hizo.

HATUA YA 16 BORA COPA COCA COLA

Hatua ya 16 bora ya michuano ya Copa Coca Cola 2011 itafanyika Juni 24 na 25
mwaka huu kwenye viwanja vya Kumbukumbu ya Karume na Tanganyika Packers ulioko
Kawe.

Mechi hiyo zitachezwa saa 2.30 asubuhi na saa 10 kamili jioni. Juni 24 mwaka huu
itakuwa ni Kinondoni na Pwani (Karume- asubuhi), Kilimanjaro na Rukwa (Kawe-
asubuhi), Temeke na Mara (Karume- jioni), Shinyanga na Arusha (Kawe- jioni).

Juni 25 mwaka huu ni Kigoma na Dodoma (Karume- asubuhi), Tanga na Mbeya (Kawe-
asubuhi), Mjini Magharibi na Ruvuma (Karume- jioni) na Morogoro na Ilala (Kawe-
jioni). Robo fainali itachezwa Juni 26 na 27 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.

UCHAGUZI WA COASTAL UNION

Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake kilichofanyika Juni 22 mwaka huu
kilipitia fomu za wagombea uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga. Kamati
ilibaini wagombea Yakubu Nuru Athumani, Titus Munthali Bandawe na Steven Mnguto
kutotimiza masharti ya uombaji wa uongozi wa klabu hiyo, hivyo kuwaondoa katika
orodha ya wagombea.


Uchaguzi wa Coastal Union utafanyika Julai 2 mwaka huu kwa nafasi ya Mwenyekiti
na wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti haina mgombea na
itajazwa baadaye kwa mujibu wa Katiba ya Coastal Union Ibara ya 29(3).


Boniface Wambura
Ofisa Habari