Search This Blog

Saturday, December 28, 2013

ASHANTI UNITED YATOA KADI ZA UANACHAMA, WAPENZI WA KANDANDA WAOMBWA KUJIUNGA !!

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAPENZI wa soka nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kuomba kadi za uanachama katika klabu ya Ashanti United yenye makazi yake maeneo ya Ilala, jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa Ashanti, Marijani Rajab ameuambia mtandao huu kuwa mwenye nia ya kujiunga na timu hiyo ya wananchi au ya kijamii afike ofisi zao zilizopo maeneo ya Ilala.

“Tupo Ilala, ofisi zetu zinatazamana na jengo la Mwalimu House, ni jengo dogo na chini yake kuna ofisi za DAWASCO au fika Ilala sokoni kwa wauza mitumba, muulize mtu yeyote ofisi za Ashanti, bila shaka atakuonesha, ni rahisi sana”. Alisema Marijan.
Marijan aliongeza kuwa katika kadi zao wanatumia picha za kidijitali ambazo wanapiga wao na gharama ya picha hizo  ikiwa ni pamoja na ada ya awali ya kadi hiyo ni shilingi za Kitanzania elfu kumi na moja  tu (11,000/=) na baada ya dakika kumi  kadi yenye ubora wa juu inatolewa.
“Kadi zetu ni za kisasa zaidi, karibuni wote wanaotaka mapinduzi ya soka la Tanzania. Njoo uungane na watanzania wenzako wenye mapenzi na Ashanti Unted. Timu hii ni ya Kihistoria, ina malengo makubwa ya kufuta ufalme wa Simba na Yanga”. Alisema Marijan.
Afisa habari huyo alifafanua kuwa kama kuna mtu anataka kujiunga na matawi, Ashanti wana tawi kubwa linaloitwa Napoli na mtu yeyote anaweza kwenda hapo  kumuuliza katibu kuhusu taratibu zao ambazo ni rahisi sana.
Marijan aliwatoa hofu watu kuwa vigezo na masharti ni vilevile kwa mujibu wa sheria, mtu awe na umri wa miaka 18, awe na akili timamu na vingine ambavyo sheria na katiba inaruhusu.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa watanzania kujiunga na timu hii ya kijamii ili kutoa `Ubepari` wa Simba na Yanga.
“Timu zinazoonekana kuwa na mwelekeo wa kuondoa ufalme wa Simba na Yanga ni zile za makampuni binafsi. Lakini Ashanti ni timu ya kijamii, ina uhusiano mkubwa na wananchi. Ina malengo ya kuuondoa Ukurwa na Udoto wa Simba na Yanga”. 

MORROCO: NAWARUDISHA WACHEZAJI WA OLJORO MCHEZONI, NI CHANGAMOTO KUBWA, LAKINI NITAFANIKIWA!!


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

KUPOTEZA muelekeo kwa klabu ya Jeshi ya JKT Oljoro ya jijini Arusha kumemfanya kocha wake mpya, Hemed Morroco kuwa na kazi nzito ya kurudisha morali ya wachezaji wake ili warudi mchezoni katika mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara unaorajia kuanza januari 25 mwakani.

Akizungumza leo hii, kocha Morroco amesema  kuwa ameipokea timu ikiwa nafasi ya 11 ikijikusanyia pointi 10 tu, hivyo kazi yake kubwa ni kuandaa kikosi cha mapambano na kuinusuru timu isishuke daraja.

“Nina changamoto kubwa sana, lakini ndio maana nipo hapa kuhakikisha timu inarudi nafasi nzuri. Kwasasa najaribu kubadili mfumo wa uchezaji na kurekebisha makosa yaliyokuwepo katika kikosi”. Alisema Morroco.

Kocha huyo aliyekuwa anaifundisha Coastal Union Mzunguko wa kwanza aliongeza kuwa usajili alioufanya dirisha dogo utamsaidia kurudisha makali ya JKT Oljoro na mpaka sasa wachezaji wote wapo kambini kujiwinda na ngwe ya lala salama.
Morroco aliwataja wachezaji aliowaongeza katika kikosi chake kuwa ni Jacob Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed Ali, Mussa Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar na Shaweji Yusuf.

“Ligi imekuwa ngumu sana, ushindani ni mkubwa. Nilikuwa na Coastal Union mzunguko wa kwanza, nilishuhudia namna timu zinavyoshindana. Nafikiri changamoto ni kubwa, lakini mimi ni Kocha, naikubali kazi hii na lazima niisaidie timu”. Alisema Morroco.

Aidha,  Morocco alisema wachezaji wa Oljoro wanaonekana kuwa na ari kubwa licha ya kupoteza muelekeo katika mzunguko wa kwanza.

“Najaribu kuwarudisha mchezoni ili wafanye kazi kama walivyokuwa wanafanya awali. Hii inawezekana na ndio maana tupo kambini mapema kutafuta nguvu za kuanza nazo januari 25 mwakani”. Alisema Morocco.

Katika mzunguko wa kwanza, JKT Oljoro ilimaliza katika nafasi ya 11 ikijikusanyia pointi zake 10 kibindoni, sawa na Ashanti United waliopo nafasi ya 12, lakini tofauti yao ni wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Oljoro ilishinda mechi  mbili tu (2), ikitoa sare nne (4), na kupoteza michezo saba(7), hivyo Morroco ana kazi kubwa ya kusaka ushindi zaidi ngwe .

Nafasi waliyopo Oljoro ni hatari tupu, kwani wakizembea watajikuta katika dhahama ya kushuka daraja, ingawa michezo 13 iliyosalia wanaweza kurekebisha mambo na kujiweka katika mikono salama.

KOMBE LA MAPINDUZI: KOCHA WA ITALIA PRANDELLI MGENI RASMI SIMBA VS AFC LEOPARDS


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MAANDALIZI ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu.

Msemaji wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc, AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati ya maandalizi imeshakamilisha  taratibu za kuzipokea.

SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.

Karim amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia,  Cesare Prandelli.

Pambano la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.

“Ninavyozungumza na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar”. Alisema Karim.

Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.

“Uwanja wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia. Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao”. Alisema Karim.
Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya milangoni kufanikisha mipango.

“Michuano hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo, tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao  kwa wingi ndio mafanikio yetu”. Aliomba Karim.

Aidha ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea michuano hiyo.

Michuano iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City ambazo hazikushiriki.

Mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.

Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.

MGAMBO YAGOMA KUSHUKA DARAJA, YAJIVUNIA USAJILI WA DIRISHA DOGO!!



Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

VIBONDE wa ligi kuu soka Tanzania bara, Mgambo Shooting ya mkoani Tanga imeanza mazoezi ya kujiandaa na mikikimikiki ya kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu  wa 2013/2014.

Akizungumza leo baada ya mazoezi ya timu hiyo, kocha msaidizi , Moka Shaban Dihimba amesema wameongeza wachezaji wanne katika dirisha dogo la usajili, hivyo watakuwa na nguvu mpya.

“Tulikuwa na mapungufu mengi, wachezaji walikuwa na hofu kubwa,  ndio maana tulifanya vibaya na kushika mkia. Tumewasajili Suleiman Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali ambao watatusaidia kupambana kufa na kupona”. Alisema Dihimba.

Dihimba alisema mazoezi yanakwenda vizuri chini ya kocha mkuu, Ramadhan Kampira na kikubwa wanachofanya kwa sasa ni kutafuta kasi na kumiliki mpira ili kuzikabili timu pinzani kwa umahiri.

“Timu za ligi kuu si kwamba zina mpira mkubwa sana, zote zinacheza soka la kawaida na sisi tunaweza kuwamuda kabisa. Nakuhakikishia kuwa kwa mechi 13 zilizobaki, tutabaki ligi kuu”. Aliongeza Dihimba.

Kocha huyo alikiri kufanya vibaya zaidi mzunguko wa kwanza kwasababu walishinda mchezo mmoja tu, wakatoa sare tatu na kufungwa mechi tisa, hivyo kujikusanyia pointi 6 tu katika nafasi ya mwisho.

Alipoulizwa kwanini timu imekuwa na matokeo mabaya hata msimu wa mwaka jana, Dihimba alieleza kuwa wachezaji wao wanakosa uzoefu na wanatawaliwa na hofu hasa wanapokutana timu kubwa.

“Tunakaa na wachezaji kwa muda mwingi na kuwaelekeza nini cha kufanya, lakini wamekuwa wakifanya makosa makubwa yanayoigharimu timu. Wana makosa ya kiufundi na tumeyaona, lakini kwa sasa tumejipanga vizuri kushindana”. Alitamba Dihimba.

KAGERA SUGAR KUANZA MAZOEZI RASMI JANUARI 2, THEM FELIX ATAMBA KUPASIA NYAVU ZAIDI!!


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam.

KLABU ya Kagera Sugar inaingia kambini desemba 31 mwaka huu, lakini mazoezi yataanza rasmi januari pili mwakani kujiwinda na mzunguko wa pili  ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi januari 25, 2014.

Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange ameuambia mtandao huu kuwa nia yao ni kurejesha makali yao kama msimu uliopita.

“Mipango ya kambi imekamilika, mimi na kocha mkuu Jackson Mayanja tunajiandaa kukisuka kikosi chetu upya. Kuna makosa yaliyokuwepo mzunguko wa kwanza, tuliyagundua mapema na sasa kazi ni kurekebisha tu”. Alisema Kabange..

Kabange aliongeza kuwa katika dirisha dogo la usajili wamemuongeza  Andrew Mathew kazembe kutoka Abajalo FC  ili kukamilisha idadi ya wachezaji 25.

“Tulitumia muda mrefu kumchunguza mchezaji huyo, tumezingatia nidhamu na uwezo wake, kwa kiasi kikubwa atatusaidia ngwe ya pili  ya ligi kuu bara”. Aliongeza Kabange.

Aidha kocha huyo alisema tatizo la safu ya ulinzi limepata dawa baada ya beki wao wa kati, Amandus Nestar kurejea uwanjani  kufuatia  kupoma tatizo lake la mguu.

“Karibu mzunguko mzima, Nestar amekuwa akisumbuliwa na mguu, madaktari wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha anarejea uwanjani. Hivi ninavyozungumza na wewe, beki huyo yuko tayari kuanza mazoezi na hali hii itaimarisha safu yetu ya ulinzi”. Alisema Kabange.

Kwa upande wake mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Them Felix alisema kuwa anajiandaa vikali kuhakikisha anaisadia klabu yake kufanya vizuri na hatimaye kuingia tatu bora msimu huu.

Them aliongeza kuwa mchezaji wa mpira wa miguu hana mapumziko, pale timu inapopewa mapumziko, yeye anatakiwa kutafuta njia mbadala ya kufanya mazoezi binafsi ili kulinda uwezo wake na kasi yake.

“Binafsi nimekuwa nikifanya mazoezi na Bukoba Veteran, nimejijanga vizuri na nina uhakika wa kufanya vizuri. Kikubwa Mwenyezi Mungu atupe afya njema”. Alisema Them.

Msimu wa mwaka jana, Kagera Sugar ikiwa chini ya kocha Mkongwe, Alhaji Abdallah Athuman Seif `King Kibadeni Mputa` ilishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Simba, ya pili Azam fc na mabingwa walikuwa Dar Young Africans.

Msimu wa mwaka huu, klabu hii haijawa na matokeo mazuri sana kwani mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika, tayari imeshajikusanyia pointi 20 katika nafasi ya sita.

Friday, December 27, 2013

CLOUDS KUPAMBANA NA MAKIPA WA LIGI KUU KESHO

 Nahodha midifield kisheti,MBWIGA MBWIGUKE...Amerejea baada ya kuwakosa YANGA kwenye mchezo uliopita.
   Winga hatari Nuno Kabezi bado anasumbuliwa na goti lakini matumaini ya kucheza bado yapo
Mshambuliaji hatari Alex Luambano yupo tayari kuwafunga makipa.



TIMU ya soka la Clouds Media Group Limited inayomiliki vituo vya redio vya Clouds FM na Choice FM pamoja na Clouds TV, kesho Jumamosi jioni itajitupa kwenye Uwanja wa Kinesi kucheza na timu ya magolikipa wa timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Timu ya Clouds Media Group Limited itajumuhisha wafanyakazi wa redio za Clouds FM na Choice FM pamoja na Clouds TV,
 
ambapo miongoni mwao wapo Shaffih Dauda, Alex Luambano, Mbwiga wa Mbwiguke, James Tupatupa, Chriss Kahongo, Ezra Kaaya, James Tupatupa, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na wengineo.
Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, Dauda amesema timu yao imejiandaa vilivyo kuzima ngebe za makipa hao wanaoongozwa na nahodha wao Shaaban Kado wa Coastal Union.
 
“Tumejiandaa vizuri kushinda mchezo huu na ni matumaini yetu kwamba tutaibuka na ushindi mnono, wachezaji wetu wote wako vizuri kupambana,” alisema Dauda ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji.
Kwa upande wa timu ya makipa, Kado amesifu uwezo wa makipa hao na kusema wamejipanga kuionyesha kazi Clouds Media Group.
“Kuna wachezaji wengi makipa ambao tuna uhakika watafanya vizuri na naomba watazamaji waje wengi kutazamamechi hii,” alisema Kado.
 
Miongoni mwa makipa watakaocheza mechi hiyo ni Kado, Hussein Sharrif ‘Casillas’, Juma Kaseja, Deo Munishi, Ali Mustapha ‘Barthez’, Amani Simba na wengineo wanaotamba ligi kuu. 

BAADA YA KATIBU MKUU - MSEMAJI WA SIMBA NAE AACHIA NGAZI MSIMBAZI



MJADALA: JE KWELI RAHEEM STERLING ALIKUWA OFFSIDE ?



WENGI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA

 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, (kushoto) akijadiliana jambo na Benny Kisaka  mdogo wa marehemu wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 
Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
 
Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 
Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
  
Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
 
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.

KALAMA NYILAWILA KUMVAA IBRAHIMU MAOKOLA DESEMBA 31 MSASANI KLABU


Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini, Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekezai bondia Kalama Nyilawila jinsi ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam Nyilawila anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu Picha nawww.superdboxing coach.blogspot.com
Kalama Nyilawila akijifua
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola siku ya Desemba 31  mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini

Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi

na mapambano mengine ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya raundi sita sita 

siku hiyo itasindikizwa na burudani za kila aina akiwemo mwana hi pop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia ya burudani
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Thursday, December 26, 2013

LUNYAMILA AENDELEA KUPATA NAFUU....

Viongozi wa Young Africans Sports Club pamoja na wachezaji wa zamani walipomtembelea kumjulia hali mchezaji Edibily Lunyamila katika hospitali Mwananyamala Disemba 24 mwaka huu.
Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la mapafu, hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.

Young Africans Sports Club tunamuombea Lunyamila apate nafuu ya haraka na kupona kabisa aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Abdallah Bin Kleb, Mohamed Bhinda, Juma Kaseja, Dr Nassoro Ally Matuzya, Kaise Edwin wakiwa nje ya wodi aliyolazwa mchezaji Edibily Lunyamila siku moja kabla ya Xmass wallipokwenda kumjulia hali
Wachezaji wa zamani wa Young Africans Sports Club wakiwa pamoja na viongozi walipokwenda kumjulia hali Lunyamila.

MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI KWA POINT NA KUIBUKA NA PIKIPIKI



Bondia Mohamed Matumla kushoto akimwadhibu Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mohamed Matumla kushoto akipambana na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao  uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


lulu akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda


l
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Hamis Ajari kushoto akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uriofanyika wakati wa sikukuu ya krismas cheka alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Sadiq Abdulazizi kushoto akipambana na Juma Fundi wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya krismas juma fundi alishinda kwa point mpambano uho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliouhulia mpambano huo uliokuwa mkali na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki nchini

Wednesday, December 25, 2013

MISS TANZANIA 2013 ASHEREHEKEA SIKUKUU YA X - MASS PAMOJA NA WATOTO YATIMA MOROGORO



 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa Maria Sista Flora Chuma..
 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Leo amejumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole  kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss Kanda ya Mashariki Missa Clara Pamoja  Sabra Islam Miss Morogoro 2013 . Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.Aliongozana na Wazazi wake pamoja na Ndugu jamaa na marafiki zake  
 Mkurugenzi wa  kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega Akiwa na  Katibu wa Miss Tanzania Bosco Majaliwa leo awlipoongozana na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria  Cha Mkoani morogoro
 Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika Picha ya Pamoja leo walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss tanzania Happiness Watimanywa Aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss tanzania Pamoja na Wazazi wake ndugu na jamaa wake wa Karibu.
 Ndugu na Marafiki wa  Miss tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa  Alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro..

JAMES KISAKA AFARIKI DUNIA, MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMINA.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.

Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.

Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.

Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, December 24, 2013

MOHAMED MATUMLA NASIBU RAMADHANI KUMARIZA UBISHA CHRXMAS


Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao leo katika

ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam leo katikati ni promota wa mpambano huo kaike siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Promota kaike Siraju akiwainua juu mikono Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani kwa ajili ya mpambano wao wa kugombea pikipiki siku ya sikukuu ya Xmasi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MTAWALA NA MWESIGA WAPATA MASHAVU TFF.