Search This Blog

Saturday, August 17, 2013

LIVE MATCH CENTRE: NGAO YA HISANI - YANGA SC 1 - 0 AZAM FC FULL TIME


Mpira umemalizika, Young Africans 1 - 0 Azam FC
Salum Telela dkk 2
Young Africans wanatwaa Ngao ya Jamii 

Dakika ya 80 Yanga bado wanaongoza.

Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Dakika ya 68, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Hussein Javu kuchukua nafasi ya Jerson Tegete

Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Azam FC 
Salum Telela dkk 2

Dakika ya 42 mwamuzi wa pembeni Hamis Chang'alu anatoa maamuzi yanayoonyesha kuwachukiza mashabiki wa Yanga na wanamzomea sana.

Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Dakika ya 24, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Deogratius Munishi 'Dida' kuchukua nafasi ya Ally Mustapha 'Barthez' aliyeumia

Dakika ya 16 anaingia Mbuyu Twite kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani aliyeshindwa kurejea kufuatia kupata maumivu

Dakika ya 16 anaingia Mbuyu Twite kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani aliyeshindwa kurejea kufuatia kupata maumivu

Dakika ya ya 15, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Dakika  ya 10 ya mchezo Kelvin Yondani anapata majeraha, anatolewa nje kupatiwa matibabu

Dakika ya pili ya mchezo, Salum Telela anaipatia Young Africans bao la kwanza

Mpira ndio umeanza hapa uwanja wa Taifa kati ya Young Africans Vs Azam FC

VIKOSI VYA LEO

YANGA 
1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1
2.Juma Abdul - 12
3.David Luhende - 3
4.Kelvin Yondani - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Saimon Msuva - 27
8.Salum Telela - 2
9.Jerson Tegete - 10
10.Didier Kavumbagu - 7
11.Haruna Niyonzima - 8

Subs:
1.Deogratius Munishi 'Dida' - 30
2.Mbuyu Twite - 6
3.Rajab Zahir - 14
4.Frank Domayo - 18
5.Nizar Khalfani - 16
6.Said Bahanuzi - 11
7.Hussein Javu - 21

INAWEZEKANA HUYU NDIO BINADAMU ANAYEICHUKIA MANCHESTER UNITED KULIKO YOYOTE YULE....ASEMA NI BORA KUWA KABURINI KULIKO KUWA NDANI YA OLD TRAFFORD

 united-grave Manchester United kwa hakika ndio klabu ambayo inashabikiwa zaidi kwenye soka ulimwenguni, lakini pia inawezekana ndio klabu inayochukiwa zaidi pia. 
Hili linaweza kutihibitishwa na mtu mmoja aitwaye George Atkinson, ambaye alihakikisha kupitia mfuniko wa kaburi lake kwamba dunia inatambua namna anvyoichukia klabu bingwa ya England. 
 Bwana huyu alifariki dunia mnamo mwaka 2005 na tayari alishatoa kauli ya (Ni bora niwe chini ya hapa kuliko kuwepo Old Trafford) ambayo aliagiza iwekwe kwenye mfuniko wa kaburi ikitokea amefariki dunia. Atkinson inasemekana alikuwa ni shabiki wa Liverpool na hakuwa anaipenda United hata chembe.

Friday, August 16, 2013

KALI YA LEO: RONALDINHO ATOBOA SIRI: WAKATI NIKIWA BARCA KABLA YA MECHI NILIKUWA NAFANYA MAPENZI


dinhoteeth Ronaldinho has had an operation to fix his teeth, talks to Playboy about losing virginity at 13 

















Mwanasoka bora wa zamani wa dunia, mbrazil Ronaldinho Gaucho amezungumza na jarida la picha za kiutuzima PLAYBOY na kutoboa siri kwamba wakati akiwa anaichezea klabu ya FC Barcelona mara nyingi kabla ya mechi hasa za nyumbani alikuwa akifanya ngono kabla ya kwenda kuungana na wenzie kwenda uwanjani.

Akizungumza na PLAYBOY BRAZIL, Ronaldinho ambaye hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha fizi zake alisema: "Wakati nikiwa Barcelona mara nyingi nilikuwa nafanya mapenzi kabla ya mechi, na kwangu halikuwa tatizo bali faida kwa kiwango changu uwanjani, ilinisaidia kuwa katika hali ya furaha kabla ya mchezo na hvyo kunifanya nicheze vizuri.
 Ronaldinho pia aliliambia jarida hilo kwamba sasa ameacha ukicheche na ametulia na mwanamke mmoja ampendae kwa dhati, "Nimezama penzini sasa, Nina mchumba na maisha yangu naishi kwa utulivu zaidi. Huko nyuma nilikuwa sio muaminifu kwenye mapenzi, lakini sasa sina mpango wa kuwa namna hiyo. Mara ya kwanza nimeshiriki tendo la ndoa nilikuwa na miaka 13 na jirani yangu, hakikuwa kitendo kizuri kwa sababu bado tulikuwa watoto." 

WAYNE ROONEY NA LUIS SUAREZ WARUDI KUFANYA MAZOEZI NA VIKOSI VYA KWANZA VYA TIMU ZAO


Luis Suarez amerudi kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza Liverpool baada ya kuwaomba radhi wachezaji wenzie na timu kwa ujumla baada ya kutoa maneno yaliyowachukiza wenzake na klabu kwa ujumla kuhusu ysakata la uhamisho wake.

Wiki iliyopita kocha Brendan Rodgers alisema kwamba Suarez hatoruhusiwa kufanya mazoezi na wenzake wa kikosi cha kwanza mpaka atakapoomba radhi.
Rooney akiwasili mazoezini leo asubuhi

Pia leo mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney abaada ya kufanya mazoezi na timu ya pili ya United wiki iliyopita, leo hii amerudi kujiunga na wenzake wa kikosi cha kwanza wakijiandaa na mechi ya kesho dhidi ya Swansea.

PHOTOS: SERENGETI SOKA BONANZA NYUMBANI KWA AKINA KASEJA

Mkuu wa vipindi Clouds FM Sebastian Maganga akiwa na mshabiki mwenzie wa Chelsea wakijiandaa kwa ajili ya Serengeti Soka Bonanza


Shaffih Dauda akiwa na mashabiki wa Arsenal

HATIMAYE UCHAGUZI WA TFF WAIPISHA MECHI YA SIMBA NA YANGA - SASA KUFANYIKA OKTOBA 26-27

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.

Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.

Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.

Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

BREAKING NEWS: MRISHO NGASSA AIDHINISHWA KUICHEZEA YANGA - KWA SHARTI LA KUILIPA SIMBA MILLIONI 45

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).

Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

BAADA YA TAREHE ZA UCHAGUZI WA TFF NA MECHI YA SIMBA NA YANGA KUINGILIANA: KAMATI YA UCHAGUZI YAITISHA KIKAO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ili kufanya uamuzi wenye manufaa kwa washabiki wa mpira wa miguu baada ya tarehe ya uchaguzi aliyotangaza kuingilia na mechi ya watani wa jadi (Simba na Yanga) ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Sekretarieti ya TFF imepokea maoni kutoka kwa wapenzi mbalimbali wa mpira wa miguu wakiomba matukio hayo mawili (Uchaguzi wa TFF na mechi ya Simba na Yanga) yafanyike katika siku tofauti.

Wakati Kamati ya Uchaguzi inatangaza uchaguzi kufanyika Oktoba 20 mwaka huu tayari ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa imeshatoka, na ikionesha kuwa timu ambazo zina historia ya kipekee katika mpira wa miguu zitacheza siku hiyo.

Sekretarieti imelazimika kumwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kwa vile yeye na kamati yake ndiye wenye mamlaka ya kuitisha Mkutano wa Uchaguzi. Huko nyuma TFF imeshafanya mikutano huku kukiwa na mechi za timu ya Taifa (Taifa Stars), jambo ambalo liliwezekana kutokana na mikutano hiyo kuwa na ajenda moja tu.

Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni ameitisha kikao cha kamati yake kujadili barua hiyo ya sekretarieti.

COCA COLA YATOA MIPIRA 100, FULANA 800
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa shukrani kwa kampuni ya Coca Cola kwa kukabidhi fulana 800 na mipira 100 kwa ajili ya ngazi ya mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ngazi ya mikoa yanayoanza Septemba Mosi mwaka huu.

Coca Cola ndiyo inayodhamini mashindano hayo yaliyoanzia ngazi ya wilaya ambapo mwaka huu yatachezwa kwa kanda na baadaye fainali itakayochezwa kuanzia Septemba 7-14 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikishirikisha mikoa 16 itakayokuwa imefanya vizuri katika ngazi ya kanda.
Kila mkoa utapata fulana 25 na mipira mitatu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu zao kwa ajili ya michuano hiyo ngazi ya kanda itakayomazika Septemba 6 mwaka huu.

Kanda hizo ni Mwanza itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida inaunda Kanda ya Arusha.

Zanzibar itakuwa na Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja wakati Kanda ya Dar es Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke na mkoa mmoja wa Unguja.

Kanda ya Mbeya inaundwa na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma wakati Dodoma, Morogoro, Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.

Mwanza itatoa timu nne kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za Arusha timu mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza timu mbili.

Wakati huo huo, semina ya makocha 32 wa timu za mikoa zitakazoshiriki michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola iliyokuwa ikiendeshwa na mkufunzi Govinder Thondoo kutoka Mauritius inafungwa leo (Agosti 16 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MWANDISHI GRACEMO BAMBAZA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo wa Radio ABM ya Dodoma, Gracemo Bambaza kilichotokea Agosti 14 mwaka huu katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani Bambaza kwa kipindi chote akiwa mwandishi alikuwa akifanya kazi nasi, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.

Bambaza aliyezaliwa mwaka 1973 na ambaye pia aliwahi kufanya kazi katika vituo vya redio vya Wapo cha Dar es Salaam na Pride cha Mtwara amesafirishwa jana (Agosti 15 mwaka huu) kwenda Karagwe mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bambaza, ABM Radio na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Bambaza mahali pema peponi. Amina

TIKETI MECHI YA YANGA, AZAM KUUZWA ASUBUHI
Tiketi kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam itakayochezwa kesho (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitaanza kuuzwa saa 3 asubuhi.

Vituo vitakavyouza tiketi hizo Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Barber Shop iliyoko Sinza Madukani.

Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari yote yanayouza tiketi yatahamia uwanjani saa 7 kamili mchana.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.

BREAKING NEWS: YANGA YAHAIRISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA KUIJADILI AZAM TV

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni , uongozi wa Yanga uliitisha mkutano Mkuu wa dharura uliokuwa  ufanyike  tarehe 18 Agost 2013 viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la kujadiliana na suala la Azam Television kurusha mechi za Yanga. Mkutano huo kwa sasa umeahirishwa kutokana na sababu  ifuatayo
Tarehe 14.8.2014 Naibu Waziri wa Habari, Utamadun,Vijanai  na Michezo Mheshimiwa Amosi Makala aliitisha kikao cha pamoja ,kilichojumuisha pande zote husika wakimwemo  wasaidizi wake, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi wa Yanga sc na uongozi wa Azam Media.
Baada ya kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa
(a)Klabu ya Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia katika utengenezaji wa mkataba  wa udhamini wa haki za matangazo na televisheni  wa Azam Media ili kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba kwa namna yoyote haviathiri klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam Media wanaotarajiwa kupewa haki hizo na Timu ya Mpira  Azam FC moja ya timu pinzani ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom
(b)Kuwepo na utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na uongozi wa Yanga kuzungumzia mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande zote mbili.
Hivyo basi baada ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa taarifa kwa wanachama wake kuwa mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti 2013, viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa hadi mtakapotangaziwa vinginevyo, lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa uongozi kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo juu
Pia uongozi unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga kwa kuonyesha ukomavu na kusimamia maendeleo  ya klabu yetu kwa Hali na mali, na uongozi Utaendelea kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi pia unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yetu wakati wa mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa michuano ya kutetea ubingwa tunaoushikiria  wa Ligi Kuu ya vodacom
Clement Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young Africans Sports Club
16.08.2013

MJADALA: WENGER KAUZA/KATOA MKOPO WACHEZAJI 17 KWENYE DIRISHA LA USAJILI - ARTETA NJE WIKI 6 - ABAKIA NA WACHEZAJI 10 TU WA KIKOSI CHA WALIO FITI KUCHEZA. NINI ANAWAZA KOCHA HUYU?

 Ligi kuu ya England inaanza wikiendi hii - huku timu kubwa baadhi zikiwa zimejipanga vizuri hasa Chelsea. Man City, Liverpool na Spurs, lakini Manchester United na Arsenal hawajawa active kwenye dirisha la usajili hili. Man United wana afadhali kwa sababu wana kikosi chao kile kile walichoshinda nacho ubingwa msimu uliopita. Lakini upande wa Arsenal hali sio nzuri. Mpaka kufikia leo Ijumaa kocha wa timu hiyo Arsene Wenger amesajili mchezaji mmoja tu tena alikuwa huru - Sanogo, huku akiwa tayari ameuza au kutoa kwa mkopo wachezaji 17 wakiwemo mastaa kama Gervinho, Arshavin, Santos, Djorou na wengineo. 

Arsenal mpaka sasa ilikuwa imebakiwa na wachezaji 11 wale wazoefu wa kikosi cha kwanza lakini ghafla usiku wa jana ikatoka taarifa kwamba Kiungo tegemezi Mikael Arteta amepata majeruhi ambayo yatamuweka nje kwa wiki sita za mwanzo mwa msimu wa ligi, hivyo kuiacha Arsenal ikiwa na imebakia na wazoefu 10 tu ambao wanaweza wakaanza kwenye wa kwanza wa ligi dhidi ya Aston Villa.
Wenger amekuwa mtu wa kuzungumza zaidi kuliko utendaji kwenye soko la usajili na siku za dirisha la usajili zinakaribia kuisha.

Kwa hali ilivyo kama Wenger hatokuwa mjanja Arsenal wanaweza wakaanza vibaya ligi. Wenger anawaza nini? Jadili................................


WACHEZAJI WA ARSENAL WALIOBAKI WA KIKOSI CHA KWANZA

Goalkeepers: Szczesny, Fabianski.
Defenders: Mertesacker, Koscielny, Jenkinson, Gibbs, Vermaelen (majeruhi), Monreal (majeruhi), Sagna (majeruhi).
Midfielders: Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Ramsey (hayupo fiti), Cazorla (ametoka kusafiri kutoka ECUADOR jana), Arteta (majeruhi), Diaby (majeruhi), Frimpong*, Miyaichi (majeruhi).
Forwards: Podolski, Giroud, Walcott, Sanogo (majeruhi), Park*, Bendtner*.

MAKALA: SABABU KWANINI FRANK RIBERY NDIO MCHEZAJI ANAYESTAHILI KUTWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA ULAYA



Tuzo ya mchezaji bora wa ulaya ni nafasi nyingine ya ulimwengu wa soka kumtunza mchezaji bora kwenye mchezo wa soka barani ulaya. Tuzo hii haipaswi kufuata matakwa na mapenzi ya vyombo vya habari na kwa sababu hiyo tuzo hii safari haipaswi kwenda nchini Spain bali Ujerumani.



Listi ya waliostahili na kusahaulika
Tuzo za namna hii hukufanya ujiulize ubora wa mchezo huu hivi sasa. Listi ya wanasoka wanaoitwa bora haipo sawa. Kupuuzwa kwa wachezaji wanaocheza mchezo wa kuzuia unaonyesha kuna tatizo kwenye mchezo wa soka la kisasa. Kipaji binafsi, marudio ya vipande vya mechi na magoli ndivyo vitu ambavyo ulimwengu wa soka la kisasa na hizi tuzo za namna hii zinachoangalia katika kutoa ushindi wa mchezaji fulani. Labda hii ni kwa sababu ulimwengu wa sasa hutazami kiundani mchezo mzima.

Labda kwa sababu hii ndio maana mabeki na wachezaji kama  Carrick na Busquets mara nyingi wamekuwa wakichukulia poa bila kupewa heshima wanayostahili na mashabiki ambao wametekwa na vipande vya mtandao wa YouTube. Katika zama hizi za ukuaji wa teknolojia na mitandao ya kijamii inaonekana wazi kuna ukuaji mkubwa wa idadi ya mashabiki waitwao 'highlight fans'.


Hizi tuzo pia zimeanza kuwa tuzo za ushindani wa umaarufu. Kwa maana hiyo ndio maana wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ni  Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na mwanzoni alikuwepo pia Gareth Bale! Wote watatu walicheza vizuri msimu uliopita lakini ni Messi peke yake aliyeshinda japo kombe moja, La Liga. 
Kuna wachezaji wengi wazuri ambao inawezekana waliotoa mchango mkubwa kustahili kuwemo kwenye Top 10 ya wachezaji bora wa ulaya - ambao walimzidi hata Bale; wachezaji kama Marco Reus, alifanya vitu vikubwa kwenye michezo yenye ushindani kumzidi Bale. Juan Mata pia, alikuwa ndio mchezaji bora wa Chelsea msimu uliopita, kwangu mie inawezekana kumzidi hata Van Persie katika premier league.
Na pia vipi kuhusu wachezaji kama Javi Martinez, Arturo Vidal na Ilkay Gundogan? Watatu hawa kwa pamoja na Bastian Schweinsteiger walikuwa ni baadhi ya viungo wangu bora wa ulaya msimu uliopita. Vipi kwa sababu hawana mpira wa madoido kiasi cha kushindwa kuingia mchuano wa kupigiwa kura kwa ajili ya tuzo hii? Listi iliyotolewa ni listi ya washambuliaji tu na wafungaji na matokeo yake tuzo hizi zimeonekana kuangalia vilivyovutiwa zaidi. 
 
Lakini haipaswi kuwa namna hii. Mshindi wa tuzo anabidi kuwa mchezaji ambaye amesaidia kuipeleka timu yake hatua nyingine ya ubora na mafanikio kwa maana ya vikombe.  Kwa maana hiyo inabdi mchezaji huyo atoke Bayern Munich. 

Bayern walikuwa bora na walitawala msimu uliopita na hii tuzo inabidi kuwa zawadi ya mafsnikio yao. Dortmund pia walikuwa bora lakini Bayern walikuwa zaidi. Heynckes inabidi awe kocha bora wa msimu na mchezaji wa Bayern atwae tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ulaya na dunia. Lakini nani anastahili tuzo hizo? 
 
Kuna vipaji vingi sana katika kikosi cha Bayern; Lahm, Schweinsteiger na Javier Martinez wanastahili japo kutajwa kwa pamoja na Mandzukic. Klabu ilishinda makombe matatu - ni mafanikio ya timu kwa ujumla. Japokuwa, ikiwa utataka kumpa tuzo ni mchezaji mmoja binafsi katika wachezaji wa Bayern - basi  Frank Ribery anastahili tuzo hiyo mbele ya wengine na hizi ndio sababu kwanini anastahili.
 
Kutothaminiwa kwa Kipaji cha Ribery


Kutothaminiwa au kukubalika kwa mchango wa baadhi ya wachezaji bora kabisa linanikera sana. Sijui ni kovu lilo kwenye uso wake ambalo inawezekana ndilo linalowatisha au kesi yake inayomkabili kutembea kahaba aliye na umri mdogo, au mashabiki na vyombo vya habari hawaoni tu ubora alionao Ribery. Lakini kwa hakika kutokana kiwango chake msimu uliopita lazima watakuwa wameona ubora wa mfaransa huyu. 
 
Ribery alijiunga na Bayern mwaka 2007 akitokea Marseille kwa ada iliyoweka rekodi ya uhamisho wakati kwa klabu hiyo €25m. Hii ilikuja baada ya Zinedine Zidane kumpachika Ribery ‘mgodi wa madini wa soka’. Mambo mazuri zaidi yalitegemewa kutoka mfaransa huyu ambaye maisha yake ya soka yalitawaliwa na vizingiti vingi. 
 
Alifukuzwa kwenye academy ya Lille akiwa na miaka 16 kwa kushindwa kufanya kazi za shule kitu ambacho kwa mujibu wa wanafunzi wenzie kilikuwa bora kwao kwa sababu walichoshwa na tabia yake ya ubabe. Aliendelea kujifunza soka na kucheza kwenye vilabu vidogo vidogo kabla ya kuhamia Metz. Kutokea hapo nyota yake ikaanza kupata mwangaza na kuvivutia vilabu kadhaa vikiwemo Galatasary na Marseille lakini mwishowe alibaki Ufaransa. Hapa ndipo aliporudi kwenye mstari - labda mafundisho aliyoyapata baada ya kusilimu na kuwa muislamu yalimtuliza mnamo mwaka 2006. 
 
Katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Bayern Ribery alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ufaransa mwaka 2007 na 2008 na pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ujerumani  2008. Lakini kwa bahati mbaya majeruhi yakamharibia safari yake ya kwenda kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.
 
Lakini misimu miwili iliyopita, akiwa chini ya uangalizi wa Jupp Heynckes, ubora wa Ribery umeonekana dhahiri na muhimu zaidi kwa Bayern na mafanikio ya timu hiyo. Kwa kifupi kuibuka kwa Bayern na kuwa bora barani ulaya kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Ribery ambaye hana mpinzani katika kikosi chake.
 
Hivi karibuni Joachim Low, kocha mkuu wa Ujerumani alikaririwa akisema kwamba Ribery ndio mchezaji bora wa soka la Ujerumani, akisisitiza kwamba uwezo wake wa kukaba na kushambulia hakuna mfano wake. 
 
Ubora wake katika kuzuia na kushambulia.
 
Ni vigumu kupingana na maoni ya Low kuhusu mfaransa huyu. Ribery amekuwa winga/mchezaji bora wa upande wa kushoto duniani kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya kila kitu katika upande huo wa uwanja; akiwa anamiliki mpira anaweza kukimbiza ndani na nje na kutafuta nafasi ya kutoa krosi au kupiga mkwaju golini. Anaweza kuingia ndani na kucheza kwenye mstari na kuwa mchezeshaji pamoja na kufunga mabao pia. Japo hana uwezo wa kuchezea mpira kumzidi Ronaldo lakini kwa namna anavyoshambulia ni wachache sana wanaweza kucheza vizuri dhid yake. Na hapa akiwa anashambulia. 
 
Akicheza kama mlinzi basi labda hakuna mshambuliaji anayeweza kuzuia kuliko Ribery. Na hii inatokana utayari na kujituma kwake kufanya kazi ya kuzuia - kitu kinachomfanya kuwa bora zaidi kwa wakati huu. Nguvu na akili anayotumia inamfanya awe mchezaji sana kumtazama. Sio mbinafsi na utayari wake wa kufanya kazi kwa ajili ya timu unampa ubor ambao wengi wanaukosa.
 
Kiufundi anaofa vitu vingi kwenye mchezo wake lakini bado ana ndihamu ya mchezo, huku akiwa na maamuzi mepesi na sahihi kwenye mechi - kwa namna ya wapi na muda gani anatakiwa kuwa eneo lipi dimbani. Uwezo wake umetoa mchango mkubwa katika kuifanya Bayern iwe hapa ilipo sasa.

  Uwezo wa Frank Ribery ndio unawakilisha mchezaji wa kisasa anayehitajika kwenye soka la kileo. Hakuna nafasi ya kubaki nyuma au mbele pekee. Jukumu la mchezaji wa kisasa ni kuwa vizuri kwenye kushambulia na kuzuia. Ribery anaifanya yote haya kwa ubora wa hali ya juu na anastahili kutunzwa - UEFA na FIFA watakosa cha kujitetea safari hii kama tuzo zitaenda kwa mtu mwingine tofauti na Ribery. 
 BY AIDAN SEIF CHARLIE

Thursday, August 15, 2013

PICHA YA SIKU: MAROUNE FELLAINE NA MATHIEU VALBUENA

Maroune Fellaine wa Belgium akipambana na kiungo wa Ufaransa Mathieu Valbuena katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana.

JOSE MOURINHO VS CRISTIANO RONALDO: NAMNA MAHUSIANO YALIVYOHARIBIKA WAKIWA MADRID


Ilikuwa taswira ya kusisimua sana. Cristiano Ronaldo anakimbia kuelekea kwenye benchi la ufundi la Madrid, anatanua mikono yake na anaenda kumkumbatia Jose Mournho. Mwanga wa Cameras ulitawala na mashabiki walishangilia baada ya kuona kitendo hicho cha staa wa timu hiyo kukumbatiana na kocha wake katika kuonyesha mshikamano na upendo uliopo baina yao. Lakini je tukio hili lilikuwa lina ukweli ndani yake?

Cristiano alifunga mabao yote matatu wakati Madrid ilipoifunga  Levante 3-1 mnamo February mwaka 2012 na nahodha huyo wa Ureno aliahidi kushangilia na kocha wa viungo Rui Faria ikiwa angeweza kufunga hat-trick. Hivyo wakati alipofunga goli la tatu, akataka kutimiza ahadi yake na akakimbia kwa takribani 50 yards kuelekea bechi la ufundi la Madrid, wakati Faria alipoinuka kutoka kwenye siti yake akimsubiri. Lakini Mourinho akamuwahi na kukaa mbele yake, kwa kushindwa kumfikia aliyempanga, mshambuliaji huyo ikabidi amkumbatia Special One.
 

Hapa wakizozana mazoezini


Picha ya tukio hilo lilionyesha taswira ya chanya. Lakini ukweli nyuma ya pazia, wareno hawa hawakuwa na mahusiano mazuri, huku Mourinho akisema mchezaji huyo anajiamini sana na hafurahishwi na tabia yake ya kupinga maelekezo yake ya uwanjani.


Kugombana baina ya wawili hawa kilikuwa kitu cha kawaida kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hata katika msimu wa kwanza wa Mourinho ndani ya Bernabeu. Siku chache baada ya kushinda Copa del Rey shukrani kwa goli la Ronaldo katika dimba la Mestalla dhidi ya Barcelona, lakini wiki kadhaa nyuma ilikuwa imefungwa 2-0 na FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu. Akiwa amechukizwa na kufungwa kwa timu yake, Cristiano aliwahimiza wachezaji wenzie waachane na mbinu chafu za Mourinho na kucheza mchezo wa kushambulia zaidi. Baada ya mchezo, Mourinho alimsema sana Ronaldo kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Ronaldo alifunguka kwa waandishi wa habari baada ya mchezo kwamba hakuwa anapenda aina ya mchezo Mourinho anaowafundisha. Matokeo yake? Aliachwa kwenye mchezo uliofuatia ambapo Madrid walifungwa 3-2 nyumbani dhidi ya Zaragoza.

Kutokea hapo Mourinho alikuwa anatumia zaidi wasaidizi wake kumpa maelekezo Ronaldo, lakini baadae ikabidi wasuluhishwe na wakala wao Jorge Mendes - rafiki yao na patna wao katika biashara. Akiona mteja wake akipigwa benchi wakati akiwa katika mbio za kuwania tuzo ya Pichichi kwenye La Liga, Mendes ikabidi aingilie kati ugomvi huo.

Ugomvi ukapotea . Wote wawili Mourinho na Ronaldo walikuwa wakitengeneza fedha nyingi na kampuni ya Mendes Gestifute na ukiachana na masuala yao ya timu ya Real Madrid - kulikuwa na biashara iliyotakiwa kukua. "Hawakuwa na mahusiano ya karibu sana, waliongea mara chache sana katika kipindi cha miaka mitatu ya Mourinho ndani ya Madrid, ni Mendes aliyepooza ugomvi wao." Mtu mmoja wa karibu na Madrid alisema.

Na Mendes angeendelea kuingilia kati kwa mara nyingine. Mwezi  January mwaka huu, Mourinho alikuwa kwenye kitimoto baada ya kuanza kumeweka benchi Iker Casillas kitu kilichoplekea mgawanyiko mkubwa ndani ya Madrid. Alikosa sapoti, vyombo vya habari vya Spain pia mashabiki wote walimgeuka, hivyo alihitaji kusaidiwa. Na nani hasa angeweza kumpa msaada huo zaidi ya nyota mkubwa wa klabu hiyo? Hivyo Ronaldo akaamua kutoa goli lake kwa Mourinho katika ushindi wa
4-3 dhidi ya Real Sociedad (kwa ombi la Mendes), lakini pia aliongea hadharani kumtetea bosi wake. Wakala Mendes alimuomba Cristiano kuviambia vyombo vya habari kwamba Mourinho alikuwa anafanya kazi yake kwa mafanikio ya timu. Mourinho akaanza kuhema vizuri sasa.


Lakini siku tisa baadae, mahusiano yao yakaharibika tena. Mourinho alikipongeza kikosi chake katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Valencia katika Copa del Rey, lakini alitoa kauli za kumsema Cristiano kwenye vyombo vya habari na baadae kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwa kumwambia "Shut up and run!" mbele ya wachezaji wenzie. Jambo ambalo lilimshangaza raisi wa Real Florentino Perez lakini aliishia kuambia kwamba suala hilo ni la kawaida kwenye chumba hicho.

Ronaldo alihisi kutotendewa haki na Mourinho ukizingatia alikuwa upande wake pale wote walipomgeuka 0 pia amekuwa ndio msaada mkubwa wa timu uwanjani.

"Naamini hapo ndipo mahusiano yaoyalipofikia hatua mbaya zaidi," kipa wa zamani wa Madrid Paco Buyo alisema. "Ronaldo hakuwa na furaha na ukosoaji kutoka kwa Mourinho - kwa sababu alikuwa naafanya kazi kubwa kwa ajili ya manufaa ya klabu - akifunga mabao meng zaidi."

Mourinho baadae alikaririwa akisema mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 hapendi kupokea ushauri wake wa kiufundi. "Wakati nilimpokosoa kiufundi kwa sababu nilihisi angeweza kuongeza ubora zaidi, hakutaka kukubaliana na nilichokisema. Hilo linawezekana kwa sababu tayari anajua sana na kocha hawezi kumwambia chochote cha kumuongezea ubora zaidi...." aliwaambia waandishi wa habari.


Lakini Ronaldo alishindwa kutaja sababu ya kutokuelewana kwao na Ronaldo, chanzo ambacho kilikuwa ni binafsi zaidi kuliko masuala ya kiufundi.

Ronaldo alichukizwa sana namna Mourinho alivymfanyia - siku kadhaa tu baada ya kumtetea kwa nguvu zote. Kwa mujibu wa watu wa karibu wa mshambuliaji huyo waliongea na vyombo vya habari.

Wiki iliyopita huko nchini Marekani kwenye michuano ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi - Mournho ambaye kwa sasa yupo Chelsea alimtupia kijembe kingine Ronaldo kwa kumwambia yeye sio Ronaldo wa ukweli, akimlinganisha na Ronaldo mbrazil.


Lakini mpaka sasa mshambuliaji huyo amegoma kujibu mapigo akisisitiza, "Kuna vitu kwenye maisha havina thamani ya kuviongelea. Mie napenda kufanya mazungumzo yangu zaidi kupitia uwanjani."

Hii ilikuwa siku moja kabla ya mchezo kati ya Real Madrid vs Chelsea - Ronaldo alimjibu Mourinho kupitia mabao yake mawili aliyoifunga Chelsea na kuisadia Madrid kushinda 3-1. s

RAISI JAKAYA KIKWETE ALIVYOKABIDHIWA JEZI YA LIONEL MESSI ILIYOSAINIWA NA WACHEZAJI WOTE WA

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es salaam jana ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza soka na ikiwa ishara ya kutambua ushirikiano wa kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions washauri wa mahusiano wa TBL. (Picha ya Ikulu)



YANGA SC VS AZAM FC JUMAMOSI HII - VIINGILIO HIVI HAPA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA SEPT 14
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu.

Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.

Mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).

Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani.

MJADALA: NI SAHIHI UCHAGUZI WA TFF KUFANYIKA SIKU MOJA NA MECHI YA SIMBA VS YANGA? TOA MAONI YAKO


Shirikisho la soka nchini jana limetangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi viongozi wa shirikisho hilo na bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara ambapo tarehe 20 na 18 ndio siku ambazo chaguzi hizo zinafanyika. Uchaguzi wa TFF tarehe 20 Oktoba na bodi ya ligi tarehe 18.

Lakini pia ikumbukwe ratiba ya ligi kuu msimu ujao inaonyesha kwamba mechi ya watani wa jadi ya Simba na Yanga ya raundi ya kwanza itakuwa tarehe 20 Oktoba pia siku moja na uchaguzi wa TFF.

Kwa ukubwa wa matukio haya mawili kufanyika nadani ya siku moja kunahitajika kujipanga ukizingatia yanaingiliana. Tayari baadhi ya wadai wameshaanza kuonyesha wasiwasi wao kuhusu matukio haya kufanyika siku moja - mmojawapo ni aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Bwana Fredrick Mwakalekebela, je wew kama mdau una maoni gani?????????????? 

Wednesday, August 14, 2013

SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA - AZAM MEDIA NA YANGA KUFANYA MKUTANO WA KUJADILI MASLAHI YA WANA JANGWANI

Hatimaye mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media. 

Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe. 

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media. 

KOCHA WA EVERTON ATHIBITISHA MAN UNITED WALITUMA OFA MOJA TU KWA AJILI YA LEIGHTON BAINES LAKINI WALIIKATAA

Kocha wa klabu ya Everton Roberto Martinez amesisitiza is kwamba Leighton Baines hatojiunga na Manchester United kwenye dirisha hili la usajili. 


David Moyes amekuwa akihusishwa na usajili wa beki huyo wa kushoto wa Everton lakini Martinez amesisitiza ofa ya £12million iliyotumwa mwezi June ilikuwa ni ya mwisho kutoka United. 


Mchezaji mwenzie Marouane Fellaini pia amekuwa akihusishwa na kumfuata Moyes Old Trafford lakini kocha wa Toffees amesisitiza hatouzwa wakati huu.

'Kabla hatujaenda Austria klabu moja iliwasiliana nasi rasmi wakiwa na ofa ambayo kwao ilikuwa ya mwisho kwa ajili ya Leighton,' alisema Martinez.


'Walitoa ofa ya kiasi cha fedha ambacho hakikuwa karibu na thamani halisi ya ubora alionao Leighton Baines.
'Huo ndio ulikuwa mwisho wao na tangu wakati huo kumekuwepo tu na tetesi kuhusu suala hili.

'Tangu wakati huo hakujawahi kuwa na ofa rasmi kwa Leighton. Tumeachana na hilo suala na tunajiandaa na msimu mpya.' 

Baines anatimiza miaka 29 mwaka huu na ofa yoyote zaidi ya  £12million itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuikataa.  


United ilikuwa ikitegemewa kutuma ofa ya £35million kwa ajili ya Baines na Fellaini lakini sasa dili hilo linaonekana kuwa na uwezekano mdogo kufanyika. 

YANGA WATANGAZA MECHI YA SIMBA VS 3 PILLARS YA NIGERIA IMEFUTWA


Muda mfupi uliopita klabu ya Yanga kupitia akaunti rasmi ya mtandao wa Twitter imesema kwamba mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya 3 Pillars ya Nigeria iliyokuwa ichezwe leo imefutwa baada makamu mwenyekiti wa Simba Mzee Kinesi kusema haitambui mechi kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao huu

HATIMAYE UCHAGUZI WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF KUFANYIKA OKTOBA 18 - FOMU KUANZA KUTOLEWA IJUMAA HII

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.

Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.

KAMATI YA SHERIA SASA KUPITIA USAJILI IJUMAA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.

MSHAMBULIAJI MPYA WA SIMBA BETRAM MWOMBEKI AWEKEWA PINGAMIZI NA PAMBA YA MWANZA

Mshambuliaji aliyetokea kukonga mioyo ya mashabiki wa Simba kwa kufumania nyavu, Betram Mwombeki amekwaa kisiki katika usajili wake kuichezea timu hiyo baada ya kuwekewa pingamizi na klabu yake aliyoichezea msimu uliopita, Pamba ya Mwanza.
Awali iliripotiwa kuwa Mwombeki amesajiliwa na timu hiyo akitokea nchini Marekani, hata hivyo Pamba wamepinga taarifa hizo na kusema kuwa mchezaji huyo aliichezea timu yao Ligi Daraja la Kwanza na kufunga mabao mawili msimu uliopita.
Mwenyekiti wa Pamba, Kazimoto Miraj Muzo aliiambia Mwananchi kuwa Mwombeki alikuwa Marekani miaka ya nyuma na mwaka jana alijiunga na Pamba wakati wa dirisha dogo la usajili na kucheza mechi kadhaa tofauti na taarifa kuwa ametokea Marekani.
Muzo alisema kuwa hakuweza kucheza mechi nyingi kutokana na kukabiliwa na maumivu ya goti. “Si kweli kuwa ametokea Marekani, tupo hapa na aliichezea timu yetu. Tuliwaambia Simba, wakabisha na sasa tutakutana mbele ya sheria,” alisema Muzo.
Alifafanua kuwa walizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo, lakini hakuonyesha kujali taarifa hiyo.
“Tumewasilisha vielelezo vyetu TFF, tunasubiri matokeo ya kikao cha Kamati ya Alex Mgongolwa kutoa uamuzi wake, tumedhamiria kupigania haki yetu mpaka mwisho” alisema.
Alisema kuwa kiasi gani cha fedha watakachoidai Simba iwalipe ni siri, kwani daima wao huwa hawapendi kuweka hadharani masuala ya fedha, hasa za kumuuza mchezaji.
Itang’are alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alithibitisha kuongea na Pamba na kuahidi kulifanyia kazi. “Pamba ni ndugu zetu, miaka ya nyuma walitupa wachezaji wengi kama Hussein Marsha, John Makelele, George Masatu, Juma Amir na wengine, na kwa hili sidhani kama tutashindwana,” alisema Itang’are.
Wakati Simba inakabliwa na kikwazo kuhusiana na Mwombeki, Yanga inaelekea kupeta kwa mchezaji, Mrisho Ngassa kutokana na ukweli kuwa Simba hajawasilisha taarifa nyingine zaidi ya mkataba tu.
SOURCE: MWANANCHI