Shirikisho la soka nchini jana limetangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi viongozi wa shirikisho hilo na bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara ambapo tarehe 20 na 18 ndio siku ambazo chaguzi hizo zinafanyika. Uchaguzi wa TFF tarehe 20 Oktoba na bodi ya ligi tarehe 18.
Lakini pia ikumbukwe ratiba ya ligi kuu msimu ujao inaonyesha kwamba mechi ya watani wa jadi ya Simba na Yanga ya raundi ya kwanza itakuwa tarehe 20 Oktoba pia siku moja na uchaguzi wa TFF.
Kwa ukubwa wa matukio haya mawili kufanyika nadani ya siku moja kunahitajika kujipanga ukizingatia yanaingiliana. Tayari baadhi ya wadai wameshaanza kuonyesha wasiwasi wao kuhusu matukio haya kufanyika siku moja - mmojawapo ni aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Bwana Fredrick Mwakalekebela, je wew kama mdau una maoni gani??????????????
Huo ni uhuni wa viongozi wa TFF tu..mechi ya taifa na uganda ilikuwa hivihivi na matokeo yake tukapigwa nyumbani
ReplyDeleteMimi naona ilituweze kufuatilia vizuri nini kinaendelea kwenye matukio hayo mawili yaani Uchaguzi na Mchezo wa WaMkuu wa TFF halafu Pambano la Watani Simba na Yanga lipigwe hii itatupa fursa ya kuona safu yetu mpya ya uongozi wa Shirikisho letu.Nina imani na Uongozi wa Rais Tenga atachukua ushauri huu na kufanya mabadiliko kwa manufaa ya mpira wetu. Mimi Lungo Abdallah wa Lushoto, Tanga.
ReplyDeleteInawezekana yote kufanyika kwa siku moja ila kwa gharama kubwa sana kwa mantiki kwamba inabidi mtu kama mimi ambaye ninapenda vyote viwili ni sacrifice kimojawapo. kwakuwa vitu vyote vinapangwa na watu/TFF busara inaweza ikatumika kuvitenganisha (kila kimoja siku yake)
ReplyDeletealafu japo sina ushahidi ila ninahisi kuna kitu hapa ebu angalia inaonekana kuna trend ya siku yanapofanyika maamuzi muhimu ya TFF basi kutakuwa kuna mechi muhimu inachezwa siku hiyo kama c timu ya Taifa basi Timu kubwa hapa nchini. alafu siku kunapokuwa na mkutano wa kujadili mambo muhimu ya Simba basi mkutano utapangwa siku Simba ikiwa inacheza mechi..cjui kuna nini hapo ....?????????????!!!!!!!!!!!
Uchaguzi uanze halafu lichezwe pambano la watani wajadi simba na yanga.
ReplyDelete