Search This Blog

Friday, October 11, 2013

LIGI KUU YA VODACOM: SIMBA YAIVAA PRISONS, YANGA MGENI BUKOBA VPL


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha raundi ya nane kesho (Oktoba 12 mwaka huu) kwa mechi tatu zitakazochezwa Dar es Salaam na Bukoba mkoani Kagera.

Simba ina fursa ya kuendelea kukamata usukani wa ligi hiyo iwapo itaishinda Tanzania Prisons ya Mbeya katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale inashika nafasi ya kumi na moja katika msimamo wa ligi hiyo.

Ili iendelee kupanda katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo iliyoanza Agosti 24 mwaka huu, Tanzania Prisons ambayo katika mechi yake iliyopita ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Shooting inalazimika kuifunga Simba.

Licha ya sare ya bao 1-1 katika mechi yake iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting, Simba inayoongoza kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Azam na Mbeya City matokeo mazuri katika mchezo huo ni muhimu kwao kama ilivyo kwa wapinzani wao Tanzania Prisons.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 ambapo tiketi zitauzwa uwanjani kwenye magari maalumu kuanzia saa 4 kamili asubuhi.

Mabingwa watetezi Yanga wao watakuwa mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba kuwakabili wenyeji Kagera Sugar wanaofundishwa na Mganda Jackson Mayanja akisaidiwa na Mrage Kabage.

Kagera ambayo inapishana na Yanga kwa tofauti ya pointi moja ilipoteza mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu baada ya kulala kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex. Wakati Yanga ikiwa katika nafasi ya nne kwa pointi 12, Kagera Sugar ni ya sita kwa pointi kumi na moja.

Iwapo Kocha Ernst Brandts atawaongoza vijana wake wa Yanga kuibuka na ushindi katika mechi hiyo na Simba kufanya vibaya kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons huenda akakamata uongozi wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14.

Mwamuzi Zakaria Jacob wa Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya Ashanti United na Coastal Union itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Raundi ya tisa ya ligi hiyo inaanza keshokutwa Jumapili (Oktoba 13 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers (Mabatini, Mlandizi), Mgambo Shooting na Mbeya City (Mkwakwani, Tanga), Azam na JKT Ruvu (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Oljoro JKT (Manungu, Turiani).

Mechi zitakazooneshwa moja kwa moja (live) na Azam TV kupitia TBC1 wikiendi hii ni kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ile kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex.

WE NI MWANDISHI WA HABARI NA UNGEPENDA KWENDA BRAZIL KURIPOTI KOMBE LA DUNIA - MAOMBI YATAANZA KUPOKELEWA DESEMBA 7


VITAMBULISHO KURIPOTI KOMBE LA DUNIA
Maombi ya vitambulisho kwa waandishi wa habari (Accreditation) wanaotaka kuripoti Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) yataanza kupokelewa kwa mtandao Desemba 7 mwaka huu kupitia akaunti ya FIFA Media Channel.

Mwisho wa kupokea maombi hayo itakuwa Januari 31 mwakani, hivyo kwa waandishi wanaotaka kupata vitambulisho hivyo ni lazima wawe na akaunti ya FIFA Media Channel pamoja na utambulisho wa mtumiaji wa akaunti hiyo (user ID).

Kwa mujibu wa FIFA, kila nchi itapewa idadi maalumu ya nafasi kwa waandishi (waandishi wa kawaida pamoja na wapiga picha) baada ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia kumalizika ambapo vigezo mbalimbali vitazingatiwa ikiwemo nchi kufuzu kwa fainali hizo.

Hivyo, nchi ambayo itakuwa imefuzu itakuwa na nafasi zaidi kulinganisha na zile ambazo hazitakuwa na timu katika fainali hizo za Brazil.

Mgawanyo wa nafasi zitakazotolewa kwa Tanzania utapangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kulingana na maombi yatakayokuwa yamewasilishwa FIFA kupitia FIFA Media Channel.



NYALLA, NYAULINGO, NYENZI WASHINDA RUFANI
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewarejesha warufani wote watatu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Samwel Nyalla, Ayubu Nyaulingo na Ayoub Nyenzi walikata rufani mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaondoa katika uchaguzi huo ambapo wote wanagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali.

Akisoma uamuzi wao leo (Oktoba 11 mwaka huu) mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF, Jaji Luanda amesema baada ya kusikiliza hoja za Mrufani Nyalla walipitia Kanuni za Uchaguzi za TFF na kugundua yafuatayo;

Ibara ya 10(3) imeweka masharti makuu mawili ya ujazaji wa fomu za kugombea uongozi. Fomu hiyo ni lazima iwe na saini ya mgombea na ni lazima ithibitishwe na viongozi wa shirikisho.

Kamati imepitia Kanuni za Uchaguzi haijaona sehemu fomu hiyo ya uongozi imeambatanishwa ili kuifanya kuwa Kanuni ya Uchaguzi. Ni maoni ya Kamati kuwa ni vizuri fomu za kugombea zikawa ni sehemu ya Kanuni za Uchaguzi.

Kwa vile Kanuni za Uchaguzi za TFF za 2013 pia hazijaainisha nini adhabu kwa mgombea aliyekosea kujaza Fomu namba 1 ya kugombea uongozi, Kamati inaona itakuwa si haki kumnyima mgombea nafasi ya kushiriki katika uchaguzi kwa vile tu fomu yake haijajazwa vipengele vyote.

Nyalla aliondolewa kwenye uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa maelezo kuwa si mtu makini anayeweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu baada ya kushindwa kujaza Fomu namba 1 kipengele cha 15 kinachohusu malengo ya mgombea uongozi.
Kwa upande wa Nyaulingo ambaye aliondolewa kwa kukosa uzoefu uliothibitika kulingana na Ibara ya 29(3) ya Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya Rufani imeamua ifuatavyo;

Kamati ya Rufani ya Uchaguzi imepokea sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza hoja na maelezo kutoka kwa Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi.

Mrufani alifafanua historia yake katika masuala ya michezo kuanzia alipokuwa anasema Chuo Kikuu kuanzia 2005-2009 na pia ushiriki wake kama mchezaji wa Rukwa United iliyowahi kushiriki Ligi ya Mkoa wa Rukwa na ligi nyingine za kitaifa.

Kwa kusoma maana ya ‘Familia ya TFF’ iliyoko kwenye utangulizi wa Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 29(3) na 29(6) ya Katiba hiyo, Kamati imejiridhisha kuwa Mrufani ana sifa za kugombea uongozi wa Shirikisho na amekidhi kigezo cha sifa za ugombea.

Ameshiriki kwenye mchezo wa mpira wa miguu kama mchezaji na mtawala, hivyo kutimiza kigezo kilichohitajika cha ushiriki katika uongozi na utawala wa mchezo wa mpira wa miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.

Kwa kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani. Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani anapewa nafasi ya kushiriki katika uchaguzi.

Kuhusu Ayubu Nyenzi aliyeondolewa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, na pia kushindwa kuthibitisha uraia wake mbele ya Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani katika uamuzi wake imesema;

Imepokea sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza hoja na maelezo kutoka kwa Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi.

Baada ya uchambuzi wa kina, Kamati imeona kuwa kulingana na maelezo yaliyotolewa na Mrufani na viambatanisho vilivyowasilishwa, Kamati haina shaka kuhusu uraia wake. Uthibitisho wa uraia unapaswa kufanywa kwa umakini na taasisi yenye mamlaka ya kiserikali kufanya hivyo.

Kamati pia imejiridhisha kupitia Fomu namba 1 iliyojazwa na kusainiwa na Mrufani kuwa kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010, Nyenzi ameshika nyadhifa za utawala wa mpira wa miguu na hasa katika klabu ya Yanga, uzoefu unaomfanya kuwa na sifa ya kugombea nafasi ya uongozi katika TFF kulingana na Ibara ya 29(3) ikisomwa pamoja na Ibara ya 29(6).
Kwa kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani. Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani atashiriki katika uchaguzi wa TFF kwa nafasi anayogombea.

Wakati huo huo, Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF inakutana keshokutwa (Oktoba 13 mwaka huu), kufanyia mapitio (revision) ya uamuzi wa Kamati ya Maadili kwa waombaji uongozi wanane kama ilivyoombwa na Sekretarieti ili kutoa mwongozo wa utekelezaji wa uamuzi huo.


VODACOM PREMIER LEAGUE HIGHLITES: AZAM Vs YANGA ( 3:2 )

SD TV: GOLI LA SIKU : RUVU SHOOTING Vs JKT RUVU

MJADALA: NINI MTAZAMO WAKO JUU YA KAULI YA JOEY BARTON DHIDI YA SIR ALEX FERGUSON ?



BARTON : FERGUSON ALIKUWA HANA UWEZO WA KUPANGA HATA KONI...



Kiungo mtukutu  wa Queens Park Rangers Joey Barton ameibuka tena kwenye vichwa vya vyombo vya habari baada ya kudai kocha wa zamani wa Manchester Utd Sir Alex Ferguso hakuwa na uwezo wa kufundisha,
Barton alidai nchini England mameneja wanathaminiwa sana kuliko makocha.

'Sina maana ya kutomuheshimu Sir Alex Ferguson - alikuwa meneja mkubwa lakini hakuwa na uwezo wa kufundisha,

sidhani kama alikuwa na uwezo wa kupanga hata koni. Kuna tofauti kubwa kati ya kocha na meneja'.

Barton pia amesema hakubaliani na wazo la kuundwa kwa tume ya kutafuta njia bora ya kuendeleza soka nchini England.
Akizungumza katika kilele cha mkutano wa Viongozi wa vilabu (Leaders in Sports ) uliofanyika kwenye uwanja wa Stamford Bridge , alisema: 'Timu ya taifa ya England ni mbovu na haiwezi kufanya vizuri hata kama itafuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.

HATIMAE WAYNE ROONEY AVUNJA UKIMWA JUU YA SIR ALEX FERGUSON, MANCHESTER UNITED

Wakati mashabiki wa Manchester United wakionyhesha kukata tamaa juu ya uwezo wa meneja wao mpya David Moyes baada ya michezo saba ya ligi kuu ya England,nyota wa klabu hiyo Wayne Rooney bado ana imani kocha huyo atafanya vizuri kama akipewa muda wa kutosha.

Rooney amesema hakufurahishwa na majukumu aliyopewa na Ferguson msimu uliopita,amekili sasa kuwa na furaha pale Old Trafford sababu kubwa ni Moyes kumchezesha kwenye nafasi anayoipenda ya ushambuliaji  tofauti na msimu uliopita ambapo alichezeshwa kwenye nafasi ya kiungo.

‘Kila mtu klabuni alikuwa anajua nafasi niliyokuwa naipenda kucheza,sababu ya mimi kukata tamaa ilikuwa ni kulazimishwa kucheza kwenye nafasi ya kiungo,binafsi sikufurahishwa ila ilinilazimu kucheza kwa ajili ya manufaa ya timu,na ilinibidi wakati furani kuwa mbinafsi ili kunusuru maisha yangu'.

Baada ya mwanzo  mzuri sasa nina furaha na nadhani sasa naweza kukaa meza moja na uongozi wa man utd kwa ajili ya kujadili mambo yangu ya baadae.

Thursday, October 10, 2013

JE UNATAKA KUTENGENEZEWA KIWANJA CHA SOKA,TENNIS NA MICHEZO MINGINE KWA BEI NAFUU KABISA ? TUWASILIANE.






Kwa yeyote anayetaka huduma mojawapo kati ya hizo hapo juu fanya hima tuwasiliane:

TAASISI ZA KISERIKALI NA ZISIZO ZA KISERIKALI,SHULE,VYUO,Vilabu vya soka kama vile COASTAL UNION, AZAM FC, MBEYA CITY,YANGA,MAJIMAJI,SIMBA pamoja na timu zingine zote

Kwa taarifa zaidi tuma email

info@shaffihdauda.com

Wote mnakaribishwa:

NINI MAONI YAKO JUU YA HII TWEET YA TB JOSHUA.


ANGALIA ZOEZI HILI LA SPAIN U-21.

 
Timu ya taifa ya Hispania imeshinda karibia mataji yote makubwa kuanzia mwaka 2008, timu yao ya vijana chini ya U-21 hivi karibuni ilichukua ubingwa wa mataifa ya ulaya ya umri chini ya miaka 21. 

 Kutokana na hayo mafanikio basi ungedhania wanafanya mazoezi makali sana,ukiangalia hiyo Video hapo juu utaona kumbe siyo muda wote wanatoa macho. Wakati wakiwa mazoezini waliamua kucheza mchezo kati ya magolikipa wote watatu dhidi ya wachezaji 18 wa ndani.
Pamoja na mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kuifungia timu yake bao la ushindi lakini cha moto walikiona kutokanana umahili wa magolikipa kutokubali kufungwa kirahisi

WACHEZAJI WA YANGA WATUA SALAMA MJINI BUKOBA, TAYARI KWA MPAMBAO NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI HII.

Mapema Asubuhi hii Ndege ya Precision Air ikiingia kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuwaleta wachezaji wa Yanga ambao wanatarajia kucheza mchezo wao na Wenyeji Kagera Sugar kesho kutwa Jumamosi.
Wachezaji wa Yanga wakishuka, mbele ni Mbuyu Twite wakishuka uwanja wa Ndege Bukoba
Nizar Khalfani nae yupo kwenye kikosi
Wachezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege
Tayari wamekanyaga Ardhi ya Bukoba
Kama kawaida: kushoto ni Khalfan Ngassa kulia ni Niyonzima
Picha ya Pamoja Viongozi na wachezaji
Dida kushoto akipata picha ya pamoja na wenzake
Kocha mkuu wa timu ya Yanga
Asante tumefika salama kazi ni moja ...ushindi ni muhimu Kaitaba
Niyonzima akiwa na Mdau wake wa bukobasports.com
Kelvin Yondani akifurahia baada ya kutua Bukoba asubuhi hii.
Bw. Jamal kalumuna kushoto akiwa na kiongozi wa Yanga
Smart Hotel
Wachezaji wakiingia Smart Hotel


PICHA KWA HISANI YA  MDAU FAUSTINE RUTA (Mc Baraka ) WA .BUKOBAWADAU.

TANZIA! ROBERT IKEREGE AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI




Meneja wa zamani wa Yanga Robert Ikerege ambaye sasa ni mwenyekiti wa tawi la Yanga la Mwananyamala Msisiri,amefiwa na mama yake mzazi Stella Magesa Mkoani Tabora hii leo.


Bwana Ikelege pamoja na familia ya marehemu,wanatoka Dar Es Salaam na kuelekea Tabora kuupitia mwili marehemu,kisha kuusafirisha kwenda kijiji cha Bwima wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza,kwa ajili ya mazishi yakayofanyika siku ya jumamosi.


Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi amina.

CHEMSHA BONGO! TAJA MAJINA YA HAWA JAMAA KWENYE PICHA.


Azam FC yaipoteza Mgambo, yairarua 2-0 Chamazi

Timu ya Azam FC imesogea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) baada ya kuifunga Mgambo JKT 2-0, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
 
Azam FC imepata ushindi huo na kufikisha jumla ya pointi 14 ikiwa nyuma ya Simba SC inayoongoza ligi kwa kuwa na pointi 15, Mgambo wao wanabaki nafasi ya pili kutoka chini wakiwa na pointi zao 5.
 
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza timu zote zilitoshana nguvu kwa kutokufungana huku kila timu ikifanya mashambulizi, dk 26 John Bocco aliyekuwa nahodha wa Azam FC alikosa goli la wazi baada ya kupiga nje mpira akiwa yeye na lango la Mgambo.
 
Azam FC walizidi kulisakama lango la Mgambo, dk 31 na 45 Kipre Tchetche alijaribu kwa kupiga mashuti lakini yakaokolewa na kipa Tony Kavishe wa Mgambo, Mgambo nao hawakuwa nyuma dk 32 Salum Gilla alipiga mpira wa mbali ikadakwa vizuri na kipa Mwadini Ally wa Azam FC.
 
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Azam FC ambao walianza kwa kufanya mabadiliko dakika 45 alitoka Brian Umony nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji chipukizi Farid Mussa Maliki aliyeongeza kasi ya mashambulizi upande wa Azam FC.
 
Mabadiliko hayo yalizaa matunda katika dk 67 ya mchezo Maliki aliandika bao la kwanza  kwa Azam FC akitumia vema kupotezana kwa mabeki wa Mgambo na kumalizia krosi ya mbali iliyopigwa na beki Erasto Nyoni na kufanya matokeo kuwa Azam FC 1-0 Mgambo.
 
Kasi ya Azam FC haikuishia hapo, walifanya mabadiliko mengine kuimarisha sehemu ya kiungo aliingia Hamis Mcha kuchukua nafasi ya Humprey Mieno, baada ya mabadiliko hayo Azam FC ikacheza katika kiwango kinachotakiwa na kuwapa kibarua mabeki wa Mgambo.
 
Dk ya 86 Azam FC walipata goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na mshambuliaji Kipre Tchetche, baada ya beki wa Mgambo Ramadhan Kambwili kumwangusha Maliki akiwa katika harakati za kufunga, Maliki kabla kabla ya kuangushwa alitaka kumpita beki wa Mgambo kwa staili ya Zinadine Zidane ndipo peki huyo alipoamua kumkwatua. bao hilo la Kipre lilihitimisha mchezo huo Azam FC ikitoka na ushindi wa 2-0.
 
Ushindi huo unakuwa wa tatu kwa Azam FC tangu kuanza kwa msimu huu wa 2013/2014, iliifunga Rhino Rangers 2-0 na kuifunga Yanga SC 3-1, imetoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Ashanti United na Tanzania Prisons, imetoka suluhu na Coastal Union.
 
Azam FC itashuka tena katika Uwanja wa Azam Complex siku ya Jumamosi kucheza mechi nyingine ya ligi kuu dhidi ya  JKT Ruvu.
 
Azam FC. Mwadini Ally,  Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Morad, Agrey Moris, Michael Bolou, Brian Umony/Farid Mussa Maliki 45’, Salum Abubakar, John Bocco (cpt), Humphrey Mieno/Khamis Mcha na Kipre Tchetche.
 
Mgambo: Tony Kavishe, Daud Salum/Ramadhan Kambwili, Salum Mlima, Bakari Mtama, Bashiru Chanacha, Novat Lufunga, Nassor Gumbo, Mohamed Samata, Mohamed Netto/Malima Busungu, Salum Gilla/Fully Mganga na Peter Mwalyanzi.

SOURCE: www.azamfc.co.tz

Wednesday, October 9, 2013

KAULI YA JACK WILSHERE KUHUSU URAIA YAZUA UTATA NCHINI ENGLAND.


Leo mapema kiungo wa Arsenal alitoa kauli ifuatayo :

''The only people who should play for England are English people. If you live in England for five years it doesn’t make you English. If I went to Spain and lived there for five years I’m not going to play for Spain''.

 Baada ya kauli hiyo ya Wilshere nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England ya mchezo wa kriketi Kevin Pietersen alimjibu Wilshere kwenye Twitter.

naye mshambuliaji wa zamani wa Wimbledon na timu ya taifa ya England naye aliandika maneno 
yafuatayo kwenye twitter.



PICHA ZA JEZI YA BRAZIL MAALUM KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA ZAVUJA.



Gazeti la Globo Esporte la nchini Brazil limelikisha picha za jezi zinazotaraji kutumika kwenye fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwakani. 
Picha za jezi hiyo ambayo itatengenezwa na Nike zilitaraji kuzinduliwa mwezi Novemba mwaka huu.