Search This Blog

Saturday, March 1, 2014

LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 1 - 0 NACIONAL AL ALHLY FULL TIME


Mpira umekwisha Yanga wanaondoka na ushindi

90' Yanga wanaongoza bado

82' Canavaro anaipatia Yanga bao la kwanza - Yanga 1 - 0 Al Ahly

70' Zikiwa zimebaki dk 20 mchezo kumalizika milango bado migumu - Yanga 0 - 0 Al Ahly

60' Yanga 0 - 0 Al Ahly

 49' Yanga wameshapata kona tisa na zote tasa

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 0 - 0 Al Ahly
Mpira ni mapumziko, Young Africans 0 - 0 Al Ahly - Yanga wametengeneza nafasi tatu za wazi wameshindwa kuzitumia.43' Yanga 0 Al Ahly 0.

40' Milango ya timu zote bado migumu

37’ Yanga 0 Al Ahly 0.

Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Al Ahly

26' Hamis Kiiza anakosa bao la wazi hapa

24' Yanga 0 - 0 Al Ahly

18' Emmanuel Okwi anapiga shuti kali kipa anaucheza na kupata majeraha

14' Yanga 0 - 0 Al Ahly

11’ Yanga wanapata kona ya pili inaokolewa na wachezaji wa Ahly. (0-0)

10’ Penaltyyyyyy hapana Refa anakataa kwa madai mshambuliaji wa Al Ahly alijidondosha. (0-0)

09’ Msuva anacheza fyongo pale. (0-0)

07’ Yanga wametawala kati, Msuva na Niyonzima wanaonana vizuri. (0-0)

5' Yanga wanapata kona na inaokolewa na Al Ahly

3' Al Ahly wanalishambulia lango la Yanga lakini Dida anaokoa hatari

1' Young Africans 0 - 0 Al Ahly

Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Young Africans Vs Al AhlyKIKOSI CHA NACIONAL AL AHLY 

Ekramy, Moawad, Nagiub, Wael Gomaa, Fathy, Rabea, Ashaur, Mousa Edan, Gedo, na Amri GamalKIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA LEO
1. Deogratias Munish "Dida" - 30
2. Mbuyu Twite - 6
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23 (C)
5. Kelvin Yondani "Cotton" - 6
6. Frank Domayo "Chumvi" - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Emmanuel Okwi - 25
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20

Subs:
1. Juma Kaseja - 1
2. Juma Abdul - 12
3. David Luhende - 3
4. Athuman idd "Chuji" - 24
5. Hassan Dilunga - 26
6. Said Bahanuzi - 11
7. Didier Kavumbagu - 7

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AL AHLY - OKWI NDANI, KASEJA AANZIA BENCHI

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA LEO
1. Deogratias Munish "Dida" - 30
2. Mbuyu Twite - 6
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23 (C)
5. Kelvin Yondani "Cotton" - 6
6. Frank Domayo "Chumvi" - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Emmanuel Okwi - 25
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20

Subs:
1. Juma Kaseja - 1
2. Juma Abdul - 12
3. David Luhende - 3
4. Athuman idd "Chuji" - 24
5. Hassan Dilunga - 26
6. Said Bahanuzi - 11
7. Didier Kavumbagu - 7

MANUEL PELLEGRINI KUKAA JUKWAANI MECHI YA MARUDIANO DHIDI YA BARCELONA


Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amefungiwa mechi mbili na UEFA asisogelee eneo la kiufundi la uwanja kwa kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake kufungwa na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.

Pellegrini alisema baada ya timu yake kushindwa 2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson "hakuwa mwaadilifu kwa timu zote mbili".

Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na amepewa adhabu ya kukaa jukwaani pamoja na mashabiki katika mchezo wa pili wa michuano hiyo na Barcelona mnamo Machi 12, pamoja na mechi nyingine za ziada.

Friday, February 28, 2014

HUYU NDIO ALEN HALILOVIC - MRITHI WA MESSI NDANI YA FC BARCELONA - AZITOSA SPURS NA MAN UNITED AENDA CAM NOU


Baada ya miezi kadhaa ya tetesi juu ya atma yake itakuwa wai, kinda la klabu ya Dinamo Zagreb mwenye miaka 17 Alen Halilovic hatimaye ameamua timu ya kujiunga na kucheza soka na uamuzi aliochukua ni habari mbaya kwa vilabu vya Arsenal, Man United na Tottenham.

Badala ya kuchagua kujiunga na vilabu hivyo kutoka EPL, usiku wa jana kiungo huyo kinda wa timu ya taifa ya Croatia aliandika kupitia akaunti ya instagram na kuthibitisha kwamba anajiunga na klabu bingwa ya Spain FC Barcelona.

Halilovic, ambaye ni kiungo mshambuliaji amekuwa akifuatiliwa na vilabu vingi vya bara la ulaya kutokana na kipaji kikubwa alichokionyesha kiasi cha kuitwa 'New Messi'

Kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika: Thanks Dinamo Zagreb for everything!!My first club and biggest love!!Now is time to move on to Barcelona ❤️

Halilovic anategemewa kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu huu na ataanza kuitumikia Barcelona B.

ANGALIA UWEZO WA KINDA HUYU KISHA TOA MAONI YAKO ANASTAHILI KUITWA MESSI MPYA

YANGA V AL AHLY: JE, YANGA WANAWEZA KUWADUWAZA WAMISRI?

                                 
    
Hatimaye muda umefika. Al Ahly tayari wapo jijini. Kwa mashabiki wa Yanga, ni wakati wa hisia mchanganyiko. Furaha iliyojichovya kwenye woga wa kukutana na timu kubwa. Kwa upande mmoja wasingependa kukutana na wababe wao katika raundi ya kwanza. Kwa upande wa pili, timu kubwa kama Alhly hupandisha mzuka kwa mashabiki.
Ni fursa nyingine tena kwa Yanga, aidha kufungua ukurasa mpya kwa kuwafunga wamisri kwa mara ya kwanza au kuendeleza uteja kwa waarabu.
Mechi sita, vipigo vinne, kapu la magoli 14 huku wakijitutumua kwa kufunga bao moja ni historia ambayo kila Mwanajangwani asingependa iendelee hio Jumamosi.
Mara ya mwisho, timu hizi zilipokutana, Al Ahly walimaliza biashara kwenye mechi ya kwanza tu kwa ushindi wa 3-0 huko Cairo. Kipigo cha ‘tatu bila’ kilipelekea kocha wa Yanga wa wakati huo, Dusan Kondic kuinua mikono na kukiri ‘kiroho safi’ tu kuwa Al Ahly wapo anga zingine na Yanga hawawezi kushinda hata mechi ya marudiano nyumbani.
Mechi ya marudiano hapa Dar, ilishuhudia, udhaifu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga ukirahisha pambano kwa Al Ahly na kuondoka na ushindi wa 1-0. Si tu bao la Flavio Amado liliowaumiza Yanga, kitendo cha mashabiki wa Simba kuishangilia Al Ahly kwa mtindo wa kuhesabu pasi kiliwafanya Yanga wawe wanyonge Zaidi.
Kwa mara nyingine tena, hata kabla ya pambano kuchezwa, hukumu ya kihistoria inafanya ulimwengu wa kandanda wa bara la Afrika usiwape uzito Yanga kuitoa Al Ahly. Hata hivyo Jangwani, tofauti na miaka ya nyuma, wana imani kubwa kuwa maandalizi waliyoyafanya yanawapa nafasi nzuri ya kuwaduwaza wamisri.
Baada ya kuwashuhudia Al Ahly wakiwafunga CS Sfaxien kwenye Super Cup, kocha msaidizi, Boniface Mkwasa, alisema jamaa wanafungika. Sababu kuu mbili zinaweza kuwa zilimpa Mkwasa ujasiri wa kutamka Al Ahly wanafungika kinyume na alivyofanya Profesa Dusan Kondic mwaka 2009.
Moja, kikosi cha Yanga kimeboreka kulinganisha na kikosi cha mwaka 2009. Pili, kikosi cha Al Ahly cha mwaka huu ni dhaifu kiasi ukilinganisha na kikosi chao cha mwaka 2009. Machafuko ya kisiasa yaliyotokea mwaka 2011 na kusababisha kusimamishwa kwa ligi yamewadhoofisha ndani ndan je ya uwanja.
Kwa Yanga, usajili wa Emmanuel Okwi kumeiongezea nguvu safu ya ushambuliaji. Mwaka 2011, Yanga walitolewa na Zamalek kwa sababu ya udhaifu wa safu yao na hata mwaka 2009, wangeweza angalau kupata sare au kuondoka na ushindi hapa Dar.
Pili tofauti na miaka ya nyuma, matumaini ya Yanga yanabebwa na safu ya ushanbuliaji hasa ukizingatia udhaifu wa idara za kiungo na ulinzi.
Kasi ya Okwi na Ngassa wakichagizwa na uwepo wa Hamisi Kiiza ndani kumi nane ndio silaha kuu ya Yanga katika kulitia misukosuko lango la Al Ahly. Hata hivyo, makali ya ushambuliaji wa Yanga yatategemea Ngassa atapangwa wapi, kati au pembeni.
Ingawa alipangwa kati kama kuingo mchezeshaji dhidi ya Ruvu Shooting na kuonekana kung’aa, Ngassa anahitaji eneo kubwa Zaidi linalopatikana pembeni kutumia vizuri Zaidi kasi yake. Dhidi ya Al Ahly, tofauti na Ruvu Shooting, Ngassa atapewa  nafasi ndogo kukimbiza mpira na muda mchache sana kufanya maamuzi ya wapi aupeleke mpira. Ni vigumu kwa Ngassa kukupa ubora wake wote akipangwa katikati. Labda Pluijm anaweza kumrudisha Ngassa pembeni na kumuacha Niyonzima kucheza kati.
Golini, kuna kasheshe la Kaseja na Munishi. Nani atapangwa? Kocha Pluijm ataamua aidha kuchagua uzoefu wa Kaseja katika michuano ya kimataifa au kiwango cha juu cha sasa cha Munishi? Uzoefu au Kiwango?
Tatizo ni kuwa Kaseja kwa sasa hajapata mechi za kiushindani za kutosha kurudisha kiwango chake. Pili, Kaseja ana tatizo la kuchelewa kuruka licha ya kuwa ana uwezo mkubwa wa kuchupaa na kuelekea upande sahihi wa uelekeo wa mpira (Timing weakness, excellent reflex).
Safu ya ulinzi ya Yanga ina leta wasiwasi Zaidi. Nadir Haroub na Kelvin Yondani, licha ya ukakamavu wao wanapata shida wanapokutana na washambuliaji wanaopendelea kukokota mpira miguuni. Alichowafanyia Ramadhani Singano kwenye mtani Jembe, waarabu wanaweza kukifanya maradufu Zaidi. Pia safu ya ulinzi inabidi kutuliza vichwa hasa wanapokutana na mashambulizi mfululizo. Nadir Haroub anatakiwa ajaribu kutulia na kujua ni wapi aupeleke mpira.
Utulivu, umakini na uangalifu wa Mbuyu Twite utahitajika sana kwenye pambano hili. Tofauti na walinzi wenzake, Twite anajua ni wapi afanye tackling na tackling ya aina gani kwa wakati upi. Kwenye kiungo, msalaba wa Yanga utabebwa na uwezo wa kukimbia na pia umakini wa kuwa katika sehemu sahihi kwa wakati sahihi wa kiungo Frank Domayo. Tofauti na viungo wengi nchini, Domayo si tu anazidi kuimarika, bali anajua kucheza bila mpira. Anajua kukaba nafasi kwa kuwahi kufika katika eneo hatari inapoelekea. Ataibeba roho ya Yanga katikati.
Kwa upande wa Al Ahly, kikosi chao ni dhaifu ukilinganisha na vikosi vyao vya zamani. Hata hivyo, Al Ahly wanajua kuwa ni dhaifu, wanajua kuwa maadui wanalijua hili hivyo wanajiandaa kwa mashambulizi ya adui anayekuja na matumaini ya ‘kuiua Al Ahly dhaifu’. Wengi wameangamia kwa kutaka kutumia udhaifu wa Al Ahly ndio maana Al Ahly dhaifu imeweza kutetea ubingwa wao wa Afrika. Orlando Pirates waliingia mkenge na kujikuta wakiambulia kipigo kwenye fainali.
Kwa sasa Al Ahly ni kama Simba mzee, anafahamu udhaifu wake na kuutumia udhaifu huo kama silaha yake. Wanaweza kukuachia utambe na mpira na kuwasumbua huku wenyewe wakihitaji nafasi chache sana kuuweka mpira kimiani. Kama alivyo Simba aliyezeeka, pigo lao kubwa ni timing na kutumia nafasi chache kutoa pigo takatifu.
Kustaafu kwa Aboutreika ambaye amekuwa nguzo yao kwa takriban muongo mzima, kunaacha pengo Fulani. Hata hivyo, bado wana kikosi kilichosheheni mchanganyiko wa vipaji vya kutosha kuisumbua klabu kigogo chochote cha soka barani Afrika, sembuse na Yanga.
Kwa wacheza Kamari na mashabiki wanaliangalia pambano bila utumwa hisia za unazi, ushabiki na uzalendo, ni dhahiri kuwa Al Ahly wana nafasi kubwa ya kusonga mbele. Hata hivyo, maandalizi ya kuridhisha, safu ya ushambuliaji na nguvu ya mashabiki vinaipa nafasi nzuri na uwezo Yanga wa kuwaduwaza wamisri na kufungua ukurasa mpya.
Je,Yanga watakomesha ubabe wa Wamisri kwa timu za ukanda wa Afrika Mashariki unawaofanya miaka nenda rudi waanzie huku?  Mwaka jana walianza kampeni yao na Tusker ya Kenya na kuchukua ubingwa, mwaka huu wamesogea kwetu dhidi ya Yanga. Au, je, Yanga watakubali kufanywa ngazi ya waarabu kuelekea hatua ya makundi?

On paper, Al Ahly are still heavy favorites to progress to the next round. They are the defending Champions, have a winning squad of players who can do the job anywhere. But in Ngassa, Okwi and Hamisi Kiiza Yanga have the necessary offensive power to upset the Egyptian giants.


Thursday, February 27, 2014

OFFICIAL: KIM POULSEN ATEMESHWA KIBARUA TAIFA STARS - SALUM MADADI NA HAFIDH BADRU KUONGOZA JAHAZI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.

Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.

Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.

Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.

Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.

Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).

Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.


NIONAVYO MIMI: AZAM FC HAIWAPENDI WATANZANIA.


Na Oscar Oscar Jr.
0789-784858

Siwezi kushangaa siku moja nikiamka asubuhi na kusikia taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa, wamiliki wa timu ya Azam wameamua kununua Ndege yao kwa lengo la kurahisisha Usafiri wa kwenda mikoani kucheza michezo yao ya ligi kuu na ile ya barani Afrika ambayo timu hiyo imekuwa ikishiriki kwa msimu wa pili sasa mfululizo. Kila nchi duniani ina tamaduni zake na moja ya tamaduni za kitanzania ni kushirikiana kwenye matukio muhimu ya kijamii.
Watanzania pamoja na tofauti zao za dini, kabila, kipato daima wamekuwa pamoja kwenye mambo ya kijamii kama vile misiba.harusi n.k Hata kama utakuwa na pesa kiasi gani, kama huna tabia ya kushiriki na wenzako kwenye mambo ya kijamii, siku yakikukuta utaona cha mtema kuni! Hii inatuonyesha kuwa ushiriki na mahusiano mazuri kwenye jamii yako ni muhimu kuliko vikapu vya pesa ulizonazo.

Klabu ya Azam ilianzishwa mwaka 2007 na kufanikiwa kucheza ligi kuu msimu wa 2008/2009 kwa mara ya kwanza na kumaliza kwenye nafasi ya 8. Msimu wa 2009/2010 ilifanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya 3 huku wakiweka histori ya kumnunua mshambuluaji wa klabu ya Yanga Mrisho Ngassa kwa mamilioni ya pesa za Kitanzania. Azam waliweza kumsajili kiungo wa Rwanda marehemu Patrick Mafisango, Kally Ongala, Jabir Azizi, Ramadhani Chombo Redondo na mastaa kibao na hapa ndipo walipoanza kuteka taratibu hisia za watanzania kama timu itakayoleta mapinduzi ya soka nchini.

Watanzania baada ya kuona timu ya Azam inakuja na mbinu ambazo zinaendana na soka la kisasa, wengi wakaamini kuwa hii ndiyo timu ya kuishabikia. Azam wamejenga uwanja wao, wana timu bora ya vijana, wana hosteli za wachezaji wao na mambo mengi mazuri lakini, hawana mashabiki! Hata wale wachache ambao huwa wanaonekana timu hiyo ikicheza wanapiga piga ngoma ni kama mashabiki bandia tu.Tayari Azam wamefanikiwa mara 2 mfululizo kucheza mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika, kwa timu iliyoanzishwa mwaka 2007 haya ni mafanikio.

Watanzania wengi sana wanaipenda timu ya Azam lakini, wanashindwa kujiweka wazi kutokana na namna timu hiyo inavyoendeshwa.Uendeshwaji wa Azam fc haujampa nafasi mwananchi kushiriki na hii inatokana na timu hiyo kujiweza kifedha. Azam wanasahau kuwa timu tajiri kama Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester United na nyingine kibao, mafanikio yao yamechangiwa zaidi na mashabiki lukuki wanaonunua bidhaa za timu hizo na kuingia uwanjani kila mwishoni mwa wiki.

Shabiki duniani kote ni mchezaji wa 12 na ndiyo maana klabu kama ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani hairuhusu mchezaji wake yoyote kuitumia jezi namba 12 kwa sababu wanaamini jezi hiyo inavaliwa na washabiki wao wanaokuja kuitazama timu kwenye kila mechi wanayocheza. Azam FC ni lazima wawape nafasi mashabiki ya kuwa sehemu ya timu yao, kuna uwezekano wakafanya kila kitu ila kukosa mashabiki, itaendelea kuwagharimu kila siku. Kwa kutumia kigezo cha mapato ya mlangoni tu, unaweza kugundua kuwa huenda klabu Yanga ndiyo inaongoza kwa idadi kubwa ya mashabiki huku ikifuatiwa na klabu ya Simba kwa karibu sana. Mbeya city wanaweza kuwa nafasi ya 3 na Coastal Union kushika nafasi ya 4. Azam fc hamjifunzi tu?

Klabu za Simba na Yanga hapa nchini,zinamashabiki wengi sana na hali hii inatokana na sababu nyingi,chache kati ya hizo ni ukongwe wa vilabu hivyo na mafanikio makubwa waliyoyapata kwenye ligi kuu nchini na mashindano mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati.Ingawa timu za Coastal Union toka jiji la Tanga,Tukuyu Stars toka jiji la Mbeya na Mtibwa sugar toka Morogoro nazo kwa nyakati tofauti zimewahi kutwaa Ubingwa wa ligi kuu lakini ni wazi kuwa,Simba na Yanga ndo watawala wa ligi hiyo.

Ni ukweli uliowazi kuwa vilabu vya simba na yanga ukichunguza namna vinavyoendeshwa utagundua kuwa ni kama miradi ya watu binafsi ambao wanatumia wafuasi lukuki wa timu hizo kujiongezea kipato.Wachezaji wengi wanaonunuliwa kwa bei kubwa hasa wale wanaotoka nje ya nchi,wanaletwa kwa pesa za watu binafsi,wanapewa magari,nyumba na mishahara yao kutoka mifukoni mwa watu wanaoziongoza klabu hizo.

Watanzania wa leo si sawa na wale wa mwaka 47,siku klabu ya Pamba ya Mwanza au Ujenzi ya Rukwa zitakapopanda daraja na kushiriki ligi kuu,itakuwa ni sawa na ujio mpya wa Mbeya City. Kutokana na Propaganda za kila siku ndani ya klabu za Simba na Yanga, watu wamechoka na wanachosubiri ni kuja kwa timu ambayo wataamini imekuja kuleta mabadiliko ya kweli kama unavyoona watu wa Mbeya na timu yao. Azam Fc wanatakiwa kujifunza faida ya mashabiki na kubadilisha mwelekeo wao na kama wataendelea na tabia yao ya kuamini kuwa pesa ndo kila kitu, kuna uwezekano watakuja kuzidiwa mashabiki hata na timu ya Lipuli fc kutoka Iringa.

Kuna timu nyingi tu duniani zinazomilikiwa na watu binafsi kama ilivyo kwa Azam FC, Chelsea inamilikiwa na Roman Abramovic, Manchester City inamilikiwa na Sheikh Mansour, AC Millan inamilikiwa na Silvio Berlusconi na nyingine kibao.Sio Azam FC tu inayotumia watoto wa mmiliki kuwa sehemu ya bodi ya timu hiyo hata AC Millan pia inamtumia Barbara Berlusconi binti wa mmiliki wa klabu hiyo kama sehemu ya wakurugenzi wake lakini, bado mashabiki wamepewa kipaumbele cha juu achilia fedha walizonazo wamiliki wa klabu hiyo.

Kitu kikubwa kinachowasumbua Azam FC ni kutaka kupambana na klabu za Simba na Yanga ndani ya jiji la Dar es Salaam na kusahau kuwa,Tanzania ina mikoa zaidi ya 25 kwa sasa.Azam FC ni wageni kwenye viwanja vyote vya ligi kuu Tanzania hadi kwenye uwanja wao wenyewe wa Azam Complex pale Chamazi jiji Dar es Salaam na hili lilijidhihirisha kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara ambapo karibu maelfu ya wakazi wa Mbeya walivamia kiwanja cha Azam Complex.

Timu ya Mbeya City imejenga tabia ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini wakiwa mbeya na nje ya mkoa huu kwenda kuwajulia hali na kuwapa mkono wa pole.Hii kitu unaweza usiielewe kwa haraka lakini,inatengeneza mahusiano mazuri sana kati ya timu na wananchi.Azam FC mnaweza kufanya kitu kingine hata kujichanganya na watoto wa shule mikoani.Hii inaweza kuondoa taswila iliyopo sasa kuwa Azam haijichanganyi,wamejitosheleza n.k Watanzania wanawahitaji,wapeni nafasi kwenye timu yenu.

HATIMAYE CHELSEA YAWA TIMU YA KWANZA YA EPL KUFUNGA BAO KATIKA 16 BORA - IKITOKA SARE NA GALATASARY UGENINI

VIDEO: HATIMAYE RONALDO, BALE, BENZEMA WAIWEZESHA MADRID KUSHINDA UJERUMANI BAADA YA MIAKA 14

MAKALA: TOFAUTI KATI YA YANGA NA SIMBA (unakumbuka 5-0?)


May 6, 2012 ilikua ni tarehe ya madiliko makubwa katika klabu hizi mbili kongwe hapa Tanzania. Hii ndio tarehe ambayo Simba iliifunga Yanga mabao matano kwa sifuri, kipigo kilichochangiwa na Mgogoro wa Yanga kwa wakati huo pia.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo mashabiki wa Simba walikua na furaha kubwa, wakati ilikuwa kinyume kwa mashabiki wa Dar-es-salaam Young Africans ambao waliondoka na huzuni.
Ni takriban miaka miwili tangu mechi hiyo ilipochezwa, hii leo mambo yamekuwa tofauti, ambapo Yanga wanaendelea kutawala ligi kuu wakati Simba imekua ikijaribu kuziba nafasi liyoachwa kati yake na mtani wake wa jadi.
 Na hizi ni tofauti 4 kubwa ambazo kati ya Simba na Yanga kwa sasa.
1.     UONGOZI
Baada ya kufungwa kwa mabao 5-0,Yanga walibadilisha uongozi kutoka kwa Loyd Nchunga na kwenda kwa Yusuph Manji,ni wazi kwamba tokea Manji aingie madarakani Yanga imekua imara kufuatia uongozi huo kushikamana kwenye kila jambo ili kuhakikisha klabu inaenda mbele kwenye nyakati zote,bila kutengeneza makundi hata kwenye nyakati ngumu.

Katika kuhakikisha klabu hiyo inasonga mbele kwa mafanikio makubwa,hivi karibuni Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji alikemea kitendo cha wazee kuzungumza maswala yanayohusu klabu kwa waandishi wa habari kwa kuwa yupo mtu maalum wa kuzungumzia mambo hayo,Kitendo ambacho kilikuwa kikijitokeza pia kabla ya Uongozi wa Manji bila kukemewa.

Wakati upande wa simba viongozi wanamakundi na haijulikani nani mwenye uamuzi wa mwisho katika klabu,kitendio kilichopelekea timu hiyo kuonekana kuwa na mgawanyiko kiasi jambo ambalo linaloaathiri hadi wachezaji kwenye ligi kuu Tanzania Bara.

2.     VIKOSI
Ukilingisha vikosi vilivyocheza katika mchezo wa 5-0 na hivi vya sasa ni rahisi kuona kwanini simba ipo nyuma zaidi ya Dar –es-salaam Young Africans,ambayo kwa sasa ina kikosi imara kinachofahamu vyema nini cha kufanya uwanjani,huku wachezaji wa hakiba wenye uwezo pia.

“Star players” wa yanga : okwi, yondani, ngassa, niyonzima,kiiza, kavumbagu,domayo,dida,Msuva

Ukiangalia upande wa simba, wachezaji ambao walicheza katika mchezo wa 5 – 0, wengi wao hawapo simba. Ukiachia Merehemu General Patrick Mafisango, wachezaji watatu waliokua muhimu kwenye mechi hiyo wote wapo jangwani, “ okwi,yondani na kaseja”.

 “Star Players”  Singano na Tambwe

NB: star player ni mchezaji ambae ana uwezo wa kubadilisha matokeo ya mchezo either kwa kudominate mchezo au kufunga mabao.

3.     DAR ES SALAAM DERBY
Hii ni mechi ambayo kwa kipindi cha karibuni yanga imekua ikifungwa na simba. Kuna mambo mengi yanayosababisha yanga kufungwa ila kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinachosababisha matokeo mabaya kwa yanga ni

Pressure Ya Mechi
Ni kitu ambacho kinaweza kukufanya ushinde au ushindwe kwenye mechi. Hii ndio mechi kubwa Tanzania ambayo inakuja na pressure nyingi kutoka kwa mashabiki. Kwa miaka ya karibuni yanga uingia kwenye hii mechi akiwa katika form nzuri kitu kinachowafanya wawe relaxed na wasijiandae vyema. Wanaichukulia hii mechi kama ya kawaida, ni kitu kizuri ila ni ukweli kwamba hii mechi sio ya kawaida.

Wanakutana na simba ambayo inapania kushinda  hii mechi na kuipa uzito mkubwa sana. Hii inatokana na pressure kubwa kutoka kwa mashabiki. Wanatumia resources zote walizokua na nazo ili mradi washinde, hii ni kwasababu kwa miaka ya karibuni ushindi katika mechi ya watani ndio kitu peke ambacho simba inaweza kujivunia.

Viongozi na wachezaji wa yanga inabidi wabadilike,  mechi hii bado ina umuhimu sana hasa kwa mashabiki.  Ila kuna baadhi ya mashabiki ambao wameshaanza kuona mechi kati yanga na Azam ndio kubwa kuliko na simba.

4.     USAJILI
Hapa ndipo kwenye utofauti mkubwa,

a)     Uongozi wa Yanga unasera ya kusajili wachezaji bora tuu, watu wengi wanasema yanga inaua vipaji, mimi sioni kwa mtazamo huo,Timu nyingi kubwa duniani zinazotawala ligi zao kama Bayern Munich,Chelsea,Celtics ya Scotland,Barcelona,Juventus na nyinginezo zinafalsafa kama ya yanga
b)     Kua na Ushindani kwenye kikosi, yanga ina wastani wa wachezaji wawili katika kila namba, kitendo kinachomsaidia mwalimu kua na chaguo kubwa na bora la wachezaji huku wachezaji wenyewe kutobweteka pia ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.




c)     Kwa upande wa simba usajili wao wa safari hii umekuwa kama wakujaza wachezaji tuu kwa kiasi Fulani,kwenye Dirisha dogo wamewasajili magolikipa wawili,Huku nafasi kama beki wa kushoto ikiwa ni tatizo,kitu ambacho kinamfanya mwalimu amchezeshe henry joseph kwenye nafasi hiyo,Simba imekubali dirisha dogo kupita bila kusajili mshambuliaji,wakionekana kuridhika na washambuliaji waliowapa matokeo kwenye mechi ya mtani Jembe akiwemo Tambwe.
        Hata ni mawazo Yangu,si msimamo wa kituo,na wewe unaruhusiwa kua na yako


Wednesday, February 26, 2014

MJADALA: NANI MCHEZAJI BORA KABISA KATI YA DIDIER DROGBA NA SAMUEL ETO'O.


SIUNGI MKONO UTEUZI WA CHUJI, ERASTO TAIFA STARS


Na Baraka Mbolembole

 Jana timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ilitajwa na shirikisho la
soka nchini, TFF. Shirikisho hilo lipo katika hatua za mwisho za
kuvunja mkataba na wa kocha Kim Poulsen ambao bado umebakiza miezi miwili, hivyo kutokana na kocha huyo kushindwa kuifikisha Tanzania katika michuano ya AFCON, katika mwaka 2013, kushindwa kuwa na matokeo mazuri  katika harakati za kufuzu kwa michuano ijayo ya kombe la dunia, kushindwa kuifikisha walau fainali za CECAFA, na matokeo mabaya
katika harakati zilizofeli za michuano ya CHAN iliyomalizika mwezi uliopita nchini Afrika ya kusini.
Ni sababu za muhimu ambazo TFF, wameona na wakati huu timu ikijiandaa na harakati za kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015, nchini Morocco ni lazima wawe na kocha mwenye mkakati wa kuifikisha Tanzania katika fainali hizo ambazo mara ya mwisho, Taifa Stars ilishiriki mwaka 1980, nchini Nigeria.

Katika orodha hiyo wapo wachezaji waliostahili kuwemo ila wapo pia ambao hawakuwa na sifa za kuwemo kikosini kwa sasa. Stars itacheza na timu ya Taifa ya `Zimbabwe, mwanzoni mwa mwezi ujao katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Shirikisho la soka Ulimwenguni.

 Sipingani na uamuzi wa kiungo Athumani Iddi ' Chuji', lakini je mchezaji huyo alikuwa na sifa za kuwepo Stars kwa wakati huu akiwa hajapata muda wa kutosha wa kucheza katika klabu yake
tangu tarehe 20, Disemba? Haya ni makosa ambayo wakati mwingine yanaleta ugumu wa timu kufanikiwa. 
Timu ya Taifa ni mkusanyiko bora wa wachezaji wa nchi husika katika wakati husika. Ndiyo, Chuji atakuwa akiwasaidia wachezaji vijana kupata uzoefu

Hivi, huyu kijana wa Academy ya Allience, Athanas  Mdamu, imekuwaje akaachwa wakati kuna wachezaji vijana kama Elius Maguli, Juma Luizio wanaocheza katika klabu zao na kufanya vizuri wasipewe nafasi. Ndiyo hata kama ni mchezaji mzuri, huko ni kuikosea heshima ligi kuu yetu.
Ni kuwakosea heshima wachezaji wengine. Nafikiri vijana kama hawa wanatakiwa kucheza katika timu za Taifa za vijana, na si moja kwa moja Stars. Hamis Mcha, Erasto Nyoni, ni maingizo ambayo yanathibitisha kuwa bado hakuna usawa wakati wa uteuzi wa wachezaji muhimu wa timu ya Taifa. Wateuaji wanaendeshwa kwa hisia za kukariri.

Michael Aidan, Hassan Mwasipili, Edward Charles ni wachezaji ambao wametoka nje ya Dar es Salaam, katika vilabu vya Ruvu Shooting, JKT Ruvu, na Mbeya City, ila kukosekana kwa wachezaji kama Himid Mao na Said Mourad, Luizio, Maguli, ni maamuzi mabaya na yanayoonesha kuwa timu imara ya Taifa ya Tanzania itakuwa ni ngumu kupatikana kwa kuwa uteuzi huu wa siku ya jana unaonesha wazi kuwa ndani ya TFF, kuna ukiritimba mkubwa. 
Uwepo wa Chuji,Erasto, Mdamu, ni sawa ila wapo wachezaji ambao wanasifa zaidi yao kwa sasa . Mara zote tumekuwa
tukikosoa kuhusu uteuzi mbaya wa timu ya Taifa na huu uliofanywa na watu wa mpira ni mbovu zaidi.