Search This Blog
Saturday, February 1, 2014
BARCELONA WAKANUSHA KUJARIBU KUMPA MKATABA MPYA VICTOR VALDES ANAYETAKA KUONDOKA CAMP NOU
Barcelona wamekanusha madai kwamba wamempa mkataba mpya golikipa Victor Valdes.
Msimu uliopita golikipa huyo wa kihispania alitangaza uamuzi wake wa kuondoka Camp Nou wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.
Lakini Radio Marca ilisema kwamba mabingwa watetezi wa la liga wamejaribu kubadili uamuzi wa kipa huyo mwenye miaka 32 kwa mara ya mwisho.
Taarifa kutoka Barca ilisema: "FC Barcelona inakanusha taarifa iliyotolewa jioni(jana) na radio Marca kuhusu ofa ya mkataba mpya wa Victor Valdes.
“Klabu inaheshimu uamuzi wa mchezaji. Tungependa kuonyesha shukrani, ueledi kwenye suala hili."
Barcelona bado wamekuwa wakihusishwa na magolikipa kadhaa kama wabadala wa Valdes, akiwemo golikipa wa Borussia Monchengladbach Marc Andre ter Stegen.
KOCHA ALIYEIPA SPAIN UBINGWA WA ULAYA AFARIKI DUNIA LEO HII
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Luis Aragones amefariki dunia, akiwa na miaka 75, jumamosi ya leo katika clinic moja jijini Madrid, daktari Pedro Guillen amethibitisha.
Kocha huyu atakumbukwa kwa kuiongoza Hispania katika awamu mpya ya mafanikio mnamo mwaka 2008, alipoiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la EURO na baada ya hapo alistaafu na kumpisha Del Bosque. Aliifundisha Spain kuanzia mwaka 2004 - 2008.
WASIFU WA ARAGONES

REAL MADRID KUUFANYIA MATENGENEZO MAKUBWA UWANJA WA SANTIAGO BERNABEU - KUINGIZA WATU 90,000 UKIKAMILIKA
Friday, January 31, 2014
DAKIKA ZA MWISHO ZA DIRISHA LA USAJILI: TETESI NA USAJILI ULIOKAMILIKA - MASAA MATANO YAMEBAKIA
Uhamisho wa beki Eliaqum Mangala na mwenzie Fernando kutoka umekwamba na wachezaji hao wameonekana kwenye ndege wakielekea jijini Madeira kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Ureno kesho.
Papiss Cisse amekataa kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor lakini msenegal huyo bado anaweza kuuzwa usiku huu ikipatikana ofa ambayo Newcastle wanaitaka.
Borussia Monchengladbach bado wanamhitaji mshambuliaji wa Newcastle.
Wilfred Zaha amejiunga rasmi na Cardiff City kwa mkopo akitokea Manchester United |
Chelsea wamethibitisha kumsajili Kurt Zouma kutoka St Etienne, lakini mlinzi huyo ataendelea kubakia kwenye timu hiyo ya Ufaransa mpaka mwisho mwa msimu.
Kinda hilo lenye miaka 19 amejiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.
Emmanuel Frimpong amejiunga na Barnsley akitokea Arsenal |
Kocha wa Manchester United amethibitisha rasmi kwamba wapenzi wa klabu hiyo wasitegemee kusajiliwa kwa mchezaji yoyote leo hii zaidi baadhi ya wachezaji wataondoka kwa mkopo.
Adel Taarabt amekamilisha usajili wake wa kujiunga na AC Milan akitokea QPR |
Lewis Holtby amekamilisha uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Fulham kwa mkopo |
"BAYERN WANAFANYA KILA NJIA KUTUDHOOFISHA ILI TUSIWE TISHIO KWAO" - ASEMA CEO WA DORTMUND
Borussia Dortmund CEO Hans-Joachim Watzke ametoa tuhuma kwamba mahasimu wao Bayern Munich wana lengo la kuidhoofisha timu yake kwa kuwasajili wachezaji wao muhimu.
Bayern tayari imeshamsajili Mario Gotze kutoka BVB na hivi karibuni wametangaza kwamba Robert Lewandowski atajiunga na timu yao akitokea Dortmund mwezi June mwaka huu.
Watzke anaamini kwamba utawala wa Bayern umeifanya Bundesliga kuwa michuano ya timu moja na kusisitiza kwamba kikosi cha Pep Guardiola kina nia ya kuzuia timu kama Dortmund kukua na kuwa tishio kwao baadae.
"Hakuna ligi yoyote sasa hivi inayotawaliwa na klabu moja kama ilivyo hapa kwa Bayern ndani ya Bundesliga. Hali ya hapa sio kama ya ligi ya Hispania, au Uskochi," Watzke aliwaambia wandishi wa habari.
"Bayern sasa wanafanya kisasi baada ya Dortmund kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo. Wantaka kutuharibia timu ili kuhakikisha hatuji kuwa tishio tena.
"Na wanafanya hivyo kwa kuwasajili wachezaji wetu.
"Hatuwezi kufanya lolote kuwazuia wachezaji wetu kwenda mahala ambapo wanaahaidiwa mishahara mara mbili tunayowalipa. Pamoja na yote haya, hatutobadili mbinu zetu."
Watzke aliendelea na kusema kwamba Dortmund haitosita kusajili vizuri mwishoni mwa msimu ili kuwa tayari kushindania ubingwa wa Bundesliga msimu ujao.
"Tutawekeza kwa kiasi kikubwa wakati wa kiangazi na hatuzungumzii fedha kidogo, tutasajili kwa fedha nyingi tu wakati wa kiangazi. Tutafanya hivyo kwa kuzingatia bajeti yetu."
Bayern mpaka sasa wanaongoza kwa pengo la pointi 13 mbele ya Bayer Leverkusen katika Bundesliga, huku Dortmund wakiwa nyuma kwa pointi 17 katika nafasi ya 3.

SIKU YA MWISHO YA USAJILI: MAN UNITED NA CITY ZAPIGANA VIKUMBO KUSAINI MABEKI WA PORTO
Manchester United wametuma ofa ya kiasi cha €15 million kwa ajili ya kumsaini beki wa kati wa klabu ya Porto Nicolas Otamendi.
Wakati Porto wakiwa radhi kumuuza beki huyo wa kiargentina kuliko kumuuza beki mwingine wa kati Eliquiam Mangala, bado hawajaamua rasmi kuuza au wasiuze mchezaji huyo.
Otamendi amekuwa kwenye kikosi cha Porto tangu msimu wa 2010/11 wakati timu ilipokuwa chini ya Andre Villas-Boas' wakati walipotwaa makombe matatu, ukiwa msimu wa kwanza kwa beki huyo.
Beki huyo mwenye miaka 25 tayari ameshaichezea timu yake ya taifa ya Argentina mechi 16, lakini amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa tangu alipowasili kocha Alejandro Sabella.
Hata hivyo, ofa ya United inaweza ikafeli kutokana na wapinzani wao Manchester City kumtaka Mangala, hivyo Porto hawawezi kukubali kuwauza mabeki wao tegemezi wa kati kwa pamoja.

WENGER: KUNA ASILIMIA 80 TUTASAJILI MCHEZAJI LEO", - RAMSEY NJE WIKI SITA
Arsene Wenger amesisitiza pamoja na kwamba Julian Draxler hatoweza kusajiliwa Arsenal leo katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya, lakini na ana uhakika wa asilimia "80" kwamba klabu yake itatangaza usajili mpya leo hii.
Kumekuwepo na taarifa kwamba kcha huyo yupo sokoni akiwinda saini za wachezaji kama Miroslav Klose au Alvaro Morata baada ya uhamisho wa kumleta Julian Draxler kuonekana kuwa mgumu, lakini inaaminika kocha huyo anaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Southmpton Morgan Schneiderlin.
Kocha huyo mfaransa alikuwa akiongea na waandishi wa habari hivi punde amesema kwamba klabu yake itamkosa kiungo wao tegemezi Aaron Ramsey kwa wiki sita baada ya kupata maumivu mwezi uliopita.
"Ramsey atakuwa nje kwa wiki nne mpaka sita, nahesabu sita," aliwaambia waandishi wa habari. "Tupo kwenye jitihada za kusajili mchezaji mwingine kutokana kutokuwepo kwa Ramsey na Flamini ambaye kasimamishwa.
"Nina uhakika tutasajili mchezaji mmoja leo. Kuna asilimia 80 za kukamilika kwa suala hilo."
SIKU YA MWISHO YA USAJILI - WENGER AKANUSHA KUTAKA KUMSAJILI DRAXLER
………………………………………………………………………………...
Wakati yakiwa yamebakia masaa machache mpaka muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya kufungwa, kocha wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha rasmi kwamba klabu yake haitomsaini kiungo wa klabu ya Schalke Julian Draxler
"Usajili wa Draxler umetengenezwa na magazeti, na sio mimi. Ataendelea kuwepo Schalke," Wenger amewaambia maripota muda mchache uliopita.
RONALDO: SOKA INAMHITAJI FALCAO KWENYE KOMBE LA DUNIA 2014, NAMUOMBEA APONE HARAKA"
Cristiano Ronaldo amemtakia kheri mpinzani wake wa zamani Radamel Falcao apone haraka na kusema "soka inamhitaji Falcao" katika fainali zijazo za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Monaco, hatocheza msimu mzima baada ya kupata maumivu makubwa ya goti mapema mwezi huu, na mpaka sasa hakuna uhakika wa kwenda kushiriki kwenye michuano ya dunia mwezi 6 mwaka huu.
Hata hivyo daktari ambaye amemfanyia opasuaji mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico amesema anaweza kupona mapema na kushiriki World Cup na Cristiano Ronaldo ana matumaini Falcao atapona na kurejea dimbani mapema.
"Ujumbe pekee ninaoweza kumpa ni kwamba ninajua ana nguvu sana na mjasiri mno, ninatumaini atapona haraka na arudi dimbani kwa sababu soka inamhitaji Falcao.
"Kombe la dunia na timu ya Colombia inamsubiri. Naomba apone haraka na kurudi kucheza. Ni kitu ambacho wote tunataka kama familia ya soka."
Falcaoalikuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa La Liga kabla hajajiunga na Monaco wakati wa kipindi cha kiangazi kilichopita na alikuwa na upinzani na Ronaldo mara kwa mara ukizingatia timu zao ni pinzani pia.
Thursday, January 30, 2014
JE,MWAMUZI ALIKUWA SAHIHI KUIPA PENATI MAN CITY PAMOJA NA KUMPA KADI NYEKUNDU BEKI DANNY ROSE?
Mwamuzi msaidizi Scott Ledger jana
usiku alikuwa na mchango mkubwa kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu
nchini England baada ya kutoa maamuzi tata yaliyoisaidia Manchester City
kuifunga Totenham mabao 5-1.
Kwenye mchezo huo mwamuzi huyo
aliipa Man City penati ambayo haikustahili kutokana na beki wa Spurs Danny Rose
kuucheza mpira kwanza kabla ya mshambuliaji Edin Dzeko hajaanguka chini.
Maamuzi hayo yalipelekea beki huyo
kupewa kadi nyekundu ikiwa ni pamoja na adhabu ya penati ilikwamishwa wavuni na
Yaya Toure.
Subscribe to:
Posts (Atom)