Search This Blog

Saturday, October 29, 2011

USHINDI WA YANGA DHIDI YA SIMBA KTK PICHA....

ALAMBAA! ALAMBAAA ! HUYU NI MZEE YUSUF MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA





FADHILA LEMBA




Athuman Idd Chuji ( shoto ), Jackson Chove na Said Mohamed


Mohamed Hussein ' Mmachinga ' ( shoto ), Steve Nyerere na Edibily Lunyamila ( kulia )







































BREAKING NEWS: BOBAN AMPIGA VICHWA OKWI BAADA YA KUFUNGWA NA YANGA


Kufuatia matokeo ya kufungwa na watani wao wa jadi 1-0 dakika chache zilizopita, taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya dressing room ya Simba SC ni kwamba Haruna Moshi Boban amempiga vichwa mchezaji mwenzie Mganda Emmanuel Okwi kwa madai ya kuikosesha ushindi timu kwa kukosa mabao mengi ya wazi.

“Haruna amempiga Okwi baada ya mechi kuisha huku akimtuhumu kuikosesha timu ushindi kwa kukosa kufunga katika nafasi za wazi.Baada ya kumpiga Okwi, Haruna ameondoka hapa uwanjani peke yake bila kuongozana na wachezaji wenzie,” kilisema chanzo cha habari.

Mpaka sasa haijajulikana Okwi ameumia kwa kiasi gani kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Boban.

MATCH LIVE CENTER : YANGA VS SIMBA

DAVIS MWAPE ALIYEMCHINJA MNYAMA LEO TAIFA AKISHANGILIA GOLI LAKE.


LINE UPS

YANGA:

1. YAW BERKO

2. GODFREY TAITA

3. OSCAR JOSHUA

4. CHACHA MARWA

5. NADIR HAROUB

6. JUMA SEIF ' KIJIKO '

7. NURDIN BAKARI

8. HARUNA NIYONZIMA

9. DAVIS MWAPE

10. KENETH ASAMOAH

11. HAMIS KIIZA

RESERVES




SHABANI KADO

IBRAHIM JOB

BAKARI MBEGU

RASHID GUMBO

IDRISA RASHID

JERRY TEGETE

PIUS KISAMBALE.



SIMBA

1. JUMA KASEJA

2. SAIDI NASSOR CHOLLO
3. JUMA JABU

4. JUMA NYOSO

5. VICTOR COSTA

6. JERRY SANTO

7. AMRI KIEMBA

8. SHOMARI KAPOMBE

9. FELIX SUNZU

10. EMANUEL OKWI

11. ULIMBOKA MWAKINGWE


RESERVES

MWINYI KAZIMOTO

OBADIA MUNGUSA

PATRICK MAFISANGO

HARUNA MOSHI

SALUM MACHAKU

MWETA

UHURU SELEMANI

KICK OFF: Mpira unaanza.Timu zote zinakosa nafasi za mabao.

DK 30: Simba 0-0 Yanga

dk 40: Sunzu anakosa bao la wazi hapa

DK 45: Half time Simba 0 -0 Yanga.

Second half: Simba inamtoa Amri Kiemba anaingia Haruna Moshi Boban.

DK 55: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Hamis Kiiza anaingia Idrisa Rashid.

dk 70: Simba wanamtoa Ulimboka mwakingwe anaingia Mwinyi Kazimoto.

GOAL: YANGA 1-0 SIMBA - DAVIS MWAPE ANAIPA UONGOZI YANGA.

DK75: MABADILIKO - ANATOKA MWAPE ANAINGIA JERRY TEGETE.

DK 80: YANGA 1-0 SIMBA

DK85 : YANGA 1-0 SIMBA

DK 90 + 4

FULL TIME: YANGA 1-0 SIMBA

MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA ZA WATANI WA JADI;

P W D L
Yanga SC 86 32 28 23
Simba SC 86 23 28 32

JUNI 7, 1965
Yanga v Sunderland (Simba)
1-0
MFUNGAJI: Mawazo Shomvi dk. 15).

JUNI 3, 1966
Yanga v Sunderland (Simba)
3-2
WAFUNGAJI:
Yanga: Abdulrahman Lukongo dk. 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk. 83. Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk. 86.

NOVEMBA 26, 1966
Sunderland v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Mustafa Choteka dk. 44.

MACHI 30, 1968
Yanga v Sunderland
1-0
MFUNGAJI: Kitwana Manara dk. 28.

JUNI 1, 1968
Yanga v Sunderland
5-0
WAFUNGAJI:
Maulid Dilunga dk. 18 (penalti), Dilunga dk. 43, Salehe Zimbwe dk. 54, Zimbwe dk. 89, Kitwana Manara dk. 86.

MACHI 3, 1969
Yanga v Sunderland
(Yanga ilipewa pointi za chee na ushindi wa mabao 2-0, baada ya Sunderland kugoma kuingia uwanjani).

JUNI 4, 1972
Yanga v Sunderland
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Kitwana Manara dk. 19,
Sunderland: Willy Mwaijibe dk. 11.

JUNI 18, 1972
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Leonard Chitete.

JUNI 23, 1973
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Haidari Abeid 'Muchacho' dk. 68.

AGOSTI 10, 1974
Yanga v Simba
2-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Gibson Sembuli dk. 87, Sunday Manara dk. 97.
Simba: Adam Sabu dk. 16.
(Mechi ya kihistoria iliyochezwa Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza).

JULAI 19, 1977
Simba v Yanga
6-0
WAFUNGAJI:
Abdallah Kibadeni dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20.

OKTOBA 7, 1979
Simba v Yanga
3-1
WAFUNGAJI:
Simba: Nico Njohole dk. 3, Mohammed Bakari 'Tall' dk. 38, Abbas Dilunga dk.72. Yanga: Rashidi Hanzuruni dk. 4.

OKTOBA 4, 1980
Simba v Yanga
3-0
WAFUNGAJI: Abdallah Mwinyimkuu dk. 29, Thuwein Ally dk. 82, Nico Njohole dk. 83.

SEPTEMBA 5, 1981
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Juma Hassan Mkambi dk. 42

APRILI 29, 1982
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Rashid Hanzuruni dk 2.

SEPTEMBA 18, 1982
Yanga 3-0 Simba
WAFUNGAJI:
Omar Hussein dk. 2 na 85, Makumbi Juma dk. 62.

FEBRUARI 10, 1983
Yanga v Simba.
0-0

APRILI 16, 1983
Yanga v Simba
3-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Charles Mkwasa dk. 21, Makumbi Juma dk. 38, Omar Hussein dk. 84, Simba; Kihwelu Mussa dk. 14.

SEPTEMBA 10, 1983,
Yanga v Simba
2-0
WAFUNGAJI: Lila Shomari alijifunga dk. 72, Ahmed Amasha dk. 89.

SEPTEMBA 25, 1983
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Makumbi Juma dk. 75,
Simba: Sunday Juma dk. 72.

MACHI 10, 1984
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Omar Hussein dk. 72.
Simba: Idd Pazi kwa penalti dk 20.

JULAI 14, 1984
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Abeid Mziba dk. 39.
Simba: Zamoyoni Mogella dk. 17

MEI 19, 1985
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Omar Hussein dk. 6
Simba: Mohammed Bob Chopa dk. 30.

AGOSTI 10, 1985
Yanga v Simba
2-0

MACHI 15, 1986
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Abeid Mziba dk. 44
Simba: John Hassan Douglas dk. 20.

AGOSTI 23, 1986
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Edward Chumila dk. 9, Malota Soma dk. 51
Yanga: Omar Hussein dk. 5.

JUNI 27, 1987
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Edgar 'Fongo' Mwafongo dk. 36.

AGOSTI 15, 1987
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Abeid Mziba dk. 14.

APRILI 30, 1988
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Justin Mtekere dk. 28
Simba: Edward Chumila dk. 25.

JULAI 23, 1988
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Edward Chumila 21, John Makelele dk. 58
Yanga: Issa Athumani dk. 36.

JANUARI 28, 1989
Yanga v Simba
2-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Issa Athumani dk. 4, Abeid Mziba dk. 85
Simba: Malota Soma dk. 30.

MEI 21, 1989
Yanga v Simba
0-0

MEI 26, 1990
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Mavumbi Omari dk 6.

OKTOBA 20, 1990
Yanga v Simba
3-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Makumbi Juma dk 33, Thomas Kipese dk. 82, Sanifu Lazaro dk. 89
Simba: Edward Chumila dk. 58.

MEI 18, 1991
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Said Sued 'Scud' dk. 7.

AGOSTI 31, 1991
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Said Sued Scud.

OKTOBA 9, 1991
Yanga v Simba
2-0
WAFUNGAJI: Athumani China dk. 3, Abubakar Salum 'Sure Boy' dk. 54.

NOVEMBA 13, 1991
Yanga v Simba
2-0

APRILI 12, 1992
Yanga 1-0 Simba
MFUNGAJI: Kenneth Mkapa dk. 10.

SEPTEMBA 26, 1992
Simba v Yanga
2-0

OKTOBA 27, 1992
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Damian Morisho Kimti.

MACHI 27, 1993
Yanga v Simba
2-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Said Mwamba Kizota dk. 47 na 57
Simba: Edward Chumila dk. 75.

JULAI 17, 1993
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Dua Said dk. 69.

SEPTEMBA 26, 1993
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Dua Said dk. 13.

NOVEMBA 6, 1993
Simba v Yanga
0-0

FEBRUARI 26, 1994
Yanga v Simba
2-0
MFUNGAJI: Mohammed Hussein 'Mmachinga' na James Tungaraza 'Boli Zozo'.

JULAI 2, 1994
Simba v Yanga
4-1
WAFUNGAJI:
Simba: George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani, Dua Saidi Yanga; Constantine Kimanda.

NOVEMBA 2, 1994
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Madaraka Selemani dk. 71

NOVEMBA 21, 1994
Simba v Yanga
2-0
WAFUNGAJI: George Lucas dk. 18, Madaraka Selemani dk. 42.

MACHI 18, 1995
Simba v Yanga
0-0

OKTOBA 4, 1995
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Said Mwamba 'Kizota' dk. 70, Mchunga Bakari dk. 79,
Yanga: Mohamed Hussein ÔMmachingaŐ dk. 40.

FEBRUARI 25, 1996
Yanga v Simba
2-0

SEPTEMBA 21, 1996
Yanga v Simba
0-0

OKTOBA 23, 1996
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Mohamed Hussein 'Mmachinga' dk. 46

NOVEMBA 9, 1996
Yanga v Simba
4-4
WAFUNGAJI:
Yanga: Edibilly Lunyamila (penalti) dk. 28, Mustafa Hozza alijifunga dk 64, Said Mwamba 'Kizota' dk. 70, Sanifu Lazaro dk. 75.
Simba: Thomas Kipese dk. 7, Ahmed Mwinyimkuu dk. 43, Dua Saidi dk. 60 na 90.
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)

APRILI 26, 1997
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Idelfonce Amlima dk. 16
Simba: Abdallah Msamba sekunde ya. 56

AGOSTI 31, 1997
Yanga v Simba
0-0

OKTOBA 11, 1997
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Sekilojo Chambua dk. 52
Simba: George Masatu dk. 89
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya)

NOVEMBA 8, 1997
Yanga v Simba
1-0
MFUNGAJI: Sekilojo Chambua dk. 85
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma)

FEBRUARI 21, 1998
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Akida Makunda dk. 46
Simba: Athumani Machepe dk. 88

JUNI 7, 1998
Yanga v Simba
1-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Idelfonce Amlima dk. 28
Simba: Abuu Juma (penalti) dk. 32

MEI 1, 1999
Yanga v Simba
3-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Idd Moshi dk. 59, Kalimangonga Ongala dk. 64, Salvatory Edward dk. 70, Simba: Juma Amir dk. 12.

AGOSTI 29, 1999
Yanga v Simba
2-0
WAFUNGAJI: Bakari Malima dk. 49, Mohamed Hussein 'Mmachinga' dk 71

JUNI 25, 2000
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Steven Mapunda dk. 59 na 72
Yanga: Idd Moshi dk. 4.

AGOSTI 5, 2000
Yanga v Simba
2-0
MFUNGAJI: Iddi Moshi 37 na 47. (Alifunga mabao hayo, akitoka kwenye fungate ya ndoa yake)

SEPTEMBA 1, 2001
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Joseph Kaniki dk. 76

SEPTEMBA 30, 2001
Simba v Yanga
1-1
WAFUNGAJI:
Simba: Joseph Kaniki dk. 65,
Yanga: Sekilojo Chambua dk. 86
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza)

AGOSTI 18, 2002
Simba v Yanga
1-1
WAFUNGAJI:
Simba: Madaraka Selemani 65
Yanga: Sekilojo Chambua (penalti). dk. 89

NOVEMBA 10, 2002
Simba v Yanga
0-0

SEPTEMBA 28, 2003

Simba v Yanga
2-2
WAFUNGAJI:
Simba: Emmanuel Gabriel dk. 27 na 36
Yanga: Kudra Omary dk. 42, Heri Morris dk. 55

NOVEMBA 2, 2003
Simba v Yanga
0-0

AGOSTI 7, 2004
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Shaaban Kisiga dk. 64, Ulimboka Mwakingwe dk. 76
Yanga: Pitchou Kongo dk. 48

SEPTEMBA 18, 2004
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk. 82

APRILI 17, 2005
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Nurdin Msiga dk. 44, Athumani Machupa dk. 64,
Yanga: Aaron Nyanda dk. 39
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

AGOSTI 21, 2005
Simba v Yanga
2-0
MFUNGAJI: Nico Nyagawa dk. 22 na 56
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)

MACHI 26, 2006
Simba v Yanga.
0-0

OKTOBA 29, 2006
Simba v Yanga
0-0

JULAI 8, 2007
Simba v Yanga
1-1 (dakika 120)
WAFUNGAJI:
Simba: Moses Odhiambo (penalti dk. 2)
Yanga: Said Maulid (dk. 55).
(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo).
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

OKTOBA 24, 2007:
Simba Vs Yanga
1-0
Mfungaji: Ulimboka Mwakingwe
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

APRILI 27, 2008:
Simba Vs Yanga
0-0

OKT 26, 2008
Yanga Vs Simba
1-0
MFUNGAJI: Ben Mwalala dk15.
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

APRILI 19, 2009
Simba Vs Yanga
2-2
WAFUNGAJI:
SIMBA: Ramadhan Chombo dk 23, Haruna Moshi dk 62
YANGA: Ben Mwalala dk48, Jerry Tegete dk90
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)
(Matokeo haya yanahusu mechi za Ligi ya Bara na iliyokuwa Ligi ya Muungano pekee)

OKTOBA 31, 2009
Simba Vs Yanga
1-0
MFUNGAJI: Mussa Hassan Mgosi dk 26
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

APRILI 18, 2010
Simba Vs Yanga
4-3
WAFUNGAJI:
SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+
YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89

OKTOBA 16, 2010:
Yanga Vs Simba
1-0
MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70

MACHI 5, 2011
Simba Vs Yanga
1-1
WAFUNGAJI:
YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.
SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.
(Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja)




Simba, Yanga nje ya Ligi Kuu

P W D L
Yanga SC 18 8 2 8
Simba SC 18 8 2 8

NJE ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na Yanga zimekuwa zikikutana katika mechi zenye msisimko wakati mwingine za kuwania mataji, tena yenye thamani ya mamilioni na mvuto wake umebaki kuwa kama kawaida.
Kwa wenye kuikumbuka mechi ya fainali ya Ligi, Uwanja wa Nyamagana, mjini Mwanza mwaka 1974, hawawezi kuisahau mechi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, kwa sasa maarufu kama Kombe la Kagame.
Kwa nini? Kwa sababu wafungaji wa mabao ya Yanga kwenye Uwanja wa Nyamagana ndio wafungaji wa mabao wa timu hiyo katika ushindi wa 2-0 visiwani Zanzibar kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kubwa kuzikutanisha Simba na Yanga nje ya Ligi Kuu na Watoto wa Jangwani, chini ya kocha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati huo wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutwaa Kombe.
Tangu wakati huo hadi Januari 12 , mwaka 2011, watani hao wa jadi katika soka ya Tanzania wamekutana kwenye mechi ambazo si za Ligi mara 18 na katika hizo, Yanga imeshinda mechi nane, Simba mechi nane na zimetoka sare mbili.
Ni mechi gani, za mashindano gani, endelea;

KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:
JULAI 10, 2011
Yanga 1-0 Simbam, Fainali
MFUNGAJI : Kenneth Asamoah dk 108

JANUARI 1975
Yanga Vs Simba; Fainali, 2-0
WAFUNGAJI: Gibson Sembuli na Sunday Manara

JANUARI 1992
Simba Vs Yanga; Fainali
1-1, Simba ilishinda kwa penalti 5-4

JULAI 27, 2008
Simba Vs Yanga; Mshindi wa Tatu
(Yanga haikutokea uwanjani, Simba ikapewa ushindi wa chee)

KOMBE LA HEDEX:
JUNI 30, 1996
Yanga Vs Simba 2-0
CCM Kirumba, Mwanza
WAFUNGAJI: Bakari Malima na Edibily Lunyamila

KOMBE LA HEDEX:
JULAI 13, 1996
Simba Vs Yanga 1-1, Taifa, Dsm
WAFUNGAJI:
SIMBA: Hussein Amaan Marsha kwa penalti
YANGA: Bakari Juma Malima

KOMBE LA TUSKER:
FEBRUARI 10, 2001
Yanga Vs Simba (fainali) 0-0
(Simba ilishinda kwa penalti 5-4, Uwanja wa Taifa)

MACHI 31, 2002.
Simba Vs Yanga 4-1
WAFUNGAJI:
SIMBA: Mark Sirengo dk. 3 na 76, Madaraka Selemani dk. 32 na Emanuel Gabriel dk. 83.
YANGA: Sekilojo Chambua dk 16.
(Mechi hii ya fainali iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, FAT).

JULAI 2, 2005
CCM Kirumba, Mwanza. Fainali
Simba Vs Yanga, 2-0
WAFUNGAJI: Emmanuel Gabriel dk. 60, Mussa Hassan Mgosi dk. 72

AGOSTI 15, 2006
Simba Vs Yanga; Nusu Fainali, 1-1
WAFUNGAJI:
SIMBA: Emanuel Gabriel dk. 69
YANGA: Credo Mwaipopo 90
(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 7-6)

DESEMBA 25, 2009
Yanga Vs Simba; Nusu Fainali, 2-1
WAFUNGAJI:
YANGA: Jerry Tegete dk 67, Shamte Ally dk 120
SIMBA: Hillary Echesa dk 78 (penalti)
(Uwanja wa mpya wa Taifa)

KOMBE LA MAPINDUZI:
JANUARI 12, 2011
Simba Vs Yanga; Fainali 2-0
WAFUNGAJI: Mussa Mgosi dk 33, Shijja Mkinna dk 71
(Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

KOMBE LA AICC:
JUNI 1989
Yanga Vs Simba SC 1-0
MFUNGAJI: Joseph Machella

APRILI 20, 2003,
CCM Kirumba, Mwanza
Yanga Vs Simba 3-0
WAFUNGAJI:
Kudra Omary dk. 30, Heri Morris dk 32 na Salum Athumani dk. 47

JANUARI 19, 2003, Kombe la CCM
Simba Vs Yanga 1-1, Dsm
WAFUNGAJI:
SIMBA: Jumanne Tondolo dk. 10
YANGA: Mwinyi Rajabu dk. 20

NGAO YA JAMII:
FEBRUARI 17, 2001
Yangs Vs Simba 2-1, Dsm
WAFUNGAJI:
YANGA: Edibilly Lunyamila dk. 47, AllyYussuf 'Tigana' dk 80.
SIMBA: Steven Mapunda 'Garrincha' dk.43

AGOSTI 18, 2010
Yanga vs Simba 0-0
(Yanga ilishinda kwa penalti 3-1)
WAFUNGAJI: Geoffrey Bonny, Stefano Mwasyika na Isaac Boakye kwa upande wa Yanga na Mohamed Banka kwa Simba.
WALIOKOSA: Ernest Boakye kwa Yanga na Emanuel Okwi, Uhuru Suleiman na Juma Nyosso kwa Simba.

AGOSTI 17, 2011
Simba 2-0 Yanga
WAFUNGAJI:
Haruna Moshi ‘Boban’ dk 15 na Felix Sunzu dk 38 (penalti)


NOVEMBA 15, 2000
KOMBE LA FAT
Yanga Vs Simba 2-1
Sheikh Amri Abeid, Arusha.
WAFUNGAJI:
YANGA: Aziz Hunter 40 na Vincent Tendwa
SIMBA: Ally Yussuf 'Tigana' dk.37

NOVEMBA 12, 2000
MARUDIANO KOMBE LA FAT
Simba Vs Yanga 1-0, Dsm
MFUNGAJI:
SIMBA: Ben Luoga dk.44
(Matokeo ya jumla yakawa 2-2 na Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penalti 5-4)

UKWELI KUHUSU LUIS NANI: KUTOKA KATIKA DIMBWI LA UMASKINI MPAKA KUWA TAJIRI NA SHUJAA WA MANCHESTER UNITED.


May 2007. Aurelio Pereira alipokea simu kutoka kwa Carlos Queiroz, rafiki wake wa zamani na msaidizi wa Sir Alex Ferguson @ Manchester United.

Kuna kitu kinamsumbua Queiroz.

Amewasili Ureno na bosi wake David Gill kufanya mazungumzo ya uhamisho wa winga mpya kutoka kituo cha kukuza vipaji cha Sporting Lisbon, hivyo Queiroz alikuwa anataka kuhakikishiwa kuwa United wanafanya uamuzi mzuri kwa kulipa £17million kwa Luis Carlos Almeida da Cunha aka Nani.

“Carlos alikuwa hotelini in Lisbon,” anakumbuka Pereira, mwenye umri wa miaka 64 na kiongozi wa jopo la maskauti wa kuibua vipaji katika klabu ya Sporting ambaye ana heshima kubwa nchini Ureno kwa kuvumbua vipaji vya nyota kama Luis Figo, Cristiano Ronaldo, Paul Futre na Ricardo Quaresma.

Anaendelea Pereira, “Quieroz alikuwa anataka kujua kuhusu mentality ya Nani na kama angeweza kuhimili presha ya kuichezea United.

“Hakutaka kujua kama alikuwa na miguu mizuri.Alijua kila kitu kuhusu hilo.Alitaka kufahamu kuhusu tabia yake, vipi angeweza kukabiliana na mazingira ya nchi mpya na timu mpya.

“Yalikuwa majukumu mazito kwa Quieroz kwa sababu ulikuwa ni uhamisho wa Euro million 25 na alitaka kuwa uhakika kwa 100%.Nilimtuliza na kumuhakikishia alikuwa anamnunua mchezaji aliyekamilika.”

Masaa kadhaa baadae United walikamilisha uhamisho wa kumsajili kijana wa miaka 20 kwenda Old Trafford, na ukurasa mpya wa maisha ya Luis Nani ukawa umefunguliwa.

< MJI WA SANTA FILOMENA ALIPOKULIA LUIS NANI>

Nani alikulia katika mji wa Santa Filomena, mji mdogo uliojengwa katika mteremko wa vilima vya Amadora kaskazini magharibi mwa jiji la Lisbon.

Asilimia 30 ya watu kwenye sehemu hiyo wenye umri kati ya miaka 15 na 30 wote wana rekodi mbaya za uhalifu.Haishauriwi kwenda kutembelea eneo hilo kama hauna uhusiano na watukama Alcides Mendes, mwanzilishi na Raisi wa Espaco Jovem, taasisi ya vijana ambayo ilimsaidia Nani kuwa mbali na uhalifu baada ya kutenganishwa na wazazi wake ambao alitoka nao katika Visiwa vya Carpe Verde vilivyopo barani Afrika akiwa na umri mdogo kabisa.

Baba yake Domingos alirudi Santa Filomena on holiday wakati Nani ana miaka 7 na tangu wakati huo hakuwahi kurudi.Mama yake Maria do Ceu aliondoka Ureno na kwenda Uholanzi Nani alipokuwa na miaka 12, na kumuacha Nani akiishi na Aunty yake Antonia pamoja na familia yake, wakiwa wanalala watu sita katika chumba kimoja.

Kupitia madirisha ya nondo unapata nafasi ya kuona vizuri njia ya reli ambayo Nani angetembea kwa miguu kwa umbali wa maili 6 kwenda mazoezini na klabu yake ya kwanza Real Massama.Muda mwingine, kama alikuwa amechelewa, basi alidandia treni na kumkwempa kondakta.On the other hand, umbali wa mwendo wa dakika 2 kutoka nymbani kwao kulikuwa na uwanja mdogo wa kuweza kuhimili wachezaji watano uwanjani - uwanja ambao alijifunza soka la mtaani.

“Hilo soko kubwa kwetu,” anasema Pereira. “Watoto wa kiafrika kama Nani.Hata unaweza kuona anavyochanganya high level performance na tricks kutoka mtaani.”

Hapa ndipo Nani alipojifunzia namna ya kutumia miguu miwili, ubora anaoutumia kuonyesha kipaji chake katika wing ya kulia @ Manchester United.

“Nilikuwa natumia masaa kulenga sehemu ya duara kwa kutumia miguu yangu miwili,nilikuwa nataka sana kujua kucheza vizuri kwa kutumia miguu yangu yote,” anasema Nani.

Kati ya takribani watoto maskini 80 in Santa Filomena, Alcides Mendes anakumbuka Nani ndiye alikuwa mtoto pekee ambaye hakuacha kuzimbikiza ndoto zake.

“Nani alikuwa na mtindo wa kuchagua wachezaji dhaifu kwa upande wa timu yake ili muda wote aweze kumiliki mpira yeye,’ anasema Mendes. “Kwenye pitch walikuwa wanacheza wachezaji watano watano(mtoano), na mshindi anabaki uwanjani kucheza na watano wengine, na muda mwingine timu yake ilipofungwa alikuwa anakasirika sana. Akili yake ilikuwa katika kushinda tu. Muda wote alikuwa anataka kushinda na kuendelea kucheza tu, nothing else.

“Ilikuwa ni vigumu sana kwa watoto kujua ulimwengu nje hapa. Tatizo ni kwamba hapa watu wengi waishio hapa sio wahamiaji lakini pia sio Wareno pia.

“Wamezaliwa hapa lakini wazazi wao wanatokea katika makoloni ya zamani ya Ureno kama Cape Verde, hivyo wanakuwa wanatengwa na jamii (Nani hakupata uraia wa Ureno mpaka alipofikisha miaka 18).Hata mashuleni kuna madarasa maalum kwa ajili yao.

“Nyumba aliyokuwa anaishi Nani ilikuwa ndogo lakinifamilia yao ilikuwa ina umoja sana na walikuwa na mahusiano mazuri katika yao. Kaka yake mkubwa alikuwa mtu muhimu sana kwake. Alikuwa anafanya kazi katika ujenzi na muda mwingine Nani alikuwa naenda kumsaidia kazi.”

Pamoja na ugumu wa maisha, Nani ana kumbukumbu nzuri kuhusu makuzi yake. Mchezo mwingine aliokuwa anaupenda akiwa na taasisi ya Espaco Jovem, ulikuwa ni Capoeira, muunganiko wa Brazilian martial art na music.Hata tabia yake ya kuruka someraults (sarakasi) ambayo ndio huifanya kila anapofunga ni kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mitaa ya Santa Filomena.

“Rafiki zangu walisema nilikuwa kichaa lakini nilikuwa nataka kupata kitu Fulani kutoka capoeira na ndio maana siku zote nashangilia kwa kuruka sarakasi,” alisema Nani katika mahojiano ya TV in Portugal wiki nne zilizopita. “Watu siku zote walikuwa wanazungumza kuhusu Nani(jina alilopewa na dada zake), yule mtoto mwenye nywele za curly.

“Maisha yalikuwa magumu lakini ya furaha. Tatizo pekee lilikuwa njaa. Tulikuwa na hali mbaya sana nyumbani, hukukuwa na chakula, alikuwa kaka yangu Paulo ambaye alileta chakula kidogo nyumbani.

“Tulifikia hatua ya kuiba matunda na vitu vingine vya kula. Nilienda katika tabia zisizo nzuri lakini siku zote nilifanikiwa kurudi katika mstari ulionyooka.

“Hauwezi kubadilisha wala kuuficha ukweli huu ya maisha yako ya zamani, na sioni aibu juu ya sehemu nilipozaliwa au maisha magumu niliyopitia. Kama nimefika hapa nilipo ilikuwa kwa sababu ya juhudi zangu na moyo wangu wa kujituma.”

Nani anakataa kwamba baba yake alimtekeleza, anasisitiza sheria na kanuni za Ureno zilizomzuia kurudi kwa familia yake.Wanaume hawa wawili walikutana tena mwaka 2006 na Nani anakumbuka: “Alijaribu kunielezea kwamba hakunitekeleza, lakini nilimzuia asiendelee na mazungumzo yale na nilimwambia: “Hauhitaji kujieleza, nipo poa.Nina furaha, nafahamu kilichotokea, hivyo hahitaji kunielezea chochote.”

“Sikuwa namkumbuka sasa kwa sababu kaka Zangu alikuwa katika nafasi yake. Walinipa kila aina ya sapoti na mapenzi. Nilikuwa mdogo, nalindwa na hakuna aliweza kunigusa.”

Nani hajasahau kipindi alipokuwa anategemea timu yake yake ya Real Massama kwa ajili ya chakula na rafiki zake kwa ajili ya nguo.

Nilikuwa na marafiki wengi waliokuwa wananisaidia sana na kunisapoti kwa sababu nilikuwa na maisha magumu. Nilikuwa sina uwezo wa kununua nguo nzuri hivyo rafiki zangu walinipa zile ambazo walikuwa hawazivai tena. Sometimes walikuwa wananialika kwenda kukaa kwao hata wiki.

“Nilikuwa mtoto wa Real Massama.Walinipa kila kitu-viatu na chakula.Nilikuwa Napata huduma kuliko mtu yeyote katika klabu ile.”


Mshauri wa Nani katika klabu hiyo ya daraja la pili, Luis Dias, anakiri Nani angeweza kujiunga na Benfica badla ya Sporting Lisbon na Manchester United.Dias, sasa ni kocha wa timu ya vijana ya Sporting, na alikuwa kocha wa Nani katika timu ya under 11 kipindi Massama walipoalikwa kucheza @ Stadium of Light (Estadio de Luz) na kocha wa zamani wa Benfica Graeme Souness.

“Ni kweli alifanya mazoezi na Benfica na Sporting,” anasema Dias. “Benfica waliwapeleka Massama kucheza katika uwanja mkubwa mbele ya mashabiki wote kabla ya mchezo wao na Boavista.

“Lakini mvua ilikuwa inanyesha sana siku hiyo na Souness alisema watoto hawatocheza kwa sababu wangeharibu majani.Unapotoa ahadi kwa mchezaji wa umri wa namna ile, unatakiwa kuitimiza, lakini Benfica walishindwa.

“Baada ya muda kidogo, walimfuata Nani kwa ajili ya kumsajili lakini Nani alifikiri hawakuwa na heshima kwake .Hakutaka kuwa bidhaa kwa Benfica. Ingawa alikuwa maskini lakini Nani na kiburi sana.”

Katika kutambua machungu ya Nani ya kubeba viatu vyake katika mfuko wa plastiki (Rambo), Dias aliandaa mchango kutoka kwa wachezaji wakubwa kumchangia Nani pesa ananunue mfuko mzuri.Ilikuwa ni moja ya sehemu ya special attention aliyokuwa akipewa Nani.

“Nilikuwa zaidi ya kocha, nilikuwa saikologisti, daktari, na dereva sometimes. Nilijua kazi yangu haikuwa kumfundisha tu. Pia nilitakiwa kuwa mwalimu wake, ku-control chakula anachokula, wapi alikuwa analala, kwenda shule na kuhakikisha alikuwa anaudhuria darasani. Hivi ni vitu ambavyo wazazi wanafanya.

“@ Massama, alikuwa anakula chakula cha mchana kabla ya mazoezi na kula dinner baada ya hapo. Kilikuwa ni kitu ambacho watoto wengine hawapati. Kama alikuwa hajakula akiwa klabuni basi asingekuwa amekula kabisa.”

Ni mwendo wa nusu saa kutoka Lisbon, kusini maili 11 kutoka katika daraja la Vasco da Gama na mdomo wa mto Tagus, kabla hujafika vijijini around Alcochete, ndipo mahali Nani alipong’arisha kipaji chake.

Hapa ndio kilipo chuo cha Academica do Sporting Clube de Portugal.

Ni takribani miaka 10 tangu Sporting walipojenga hii complex, ikiwa na viwanja saba vilivyokamilika na hotel ya watoto 50 kati ya 130 ambao wanajifunza mahala pale. Inagharimu zaidi ya £4m kuiendesha academy hiyo, lakini Diogo Matos, mkurugenzi wa academy, anakisia academy hiyo tayari imeshaipa klabu ya Sporting faida ya £150 million kupitia mauzo ya mastaa kama Cristiano Ronaldo na Nani.

“Tuna kitu Fulani maalum kinachoendelea hapa,” anasema Matos ambaye matunda yake ya sasa ya wachezaji under 19 wameibuka kuwa moja ya timu bora barani ulaya katika michuano ya NextGen Series(champions league for under19).

Ingawa iliamuliwa kumbakisha Nani at Massama kwa sababu ya hali ya nyumbani kwao, lakini alikuwa akifanya mazoezi na Sporting kabla ya kujiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 16. Nani alivuna mshahara wa £900 kwa mwezi akiwa kama mchezaji wa academy, lakini aliibuka kupata £10,000 aliposaini kama professional.

Pesa hiyo ilitumika kumuhamisha aunt yake Antonia nje ya Santa Filomena, na ameendelea kuisapoti familia yake kiuchumi hadi sasa anapopata mshahara mkubwa akiwa na United.Ni mzigo ambao Nani anapenda kuubeba lakini anakiri, hali hii imekuwa ikiingilana na career in premier league.

“Namshukuru Mungu kwa hali yangu ya sasa na mimi ni nguzo katika familia yangu.Kila linapotokea tatizo wanakuja kwangu mimi na sijawahi kusema hapana.Nafahamu wapi nilipitia kipindi nilipokuwa mdogo.Sipendi kuona mtu yeyote katika familia yetu akiwa na shida.

“Lakini matatizo binafsi yananifanya nipoteze umakini. Muda mwingine kiakili nachoka kabisa. Inaweza kuwa hata kabla ya mechi kubwa au derby, lakini nitapokea simu na kumpigia yeyote anayehusika kutatua tatizo lolote linaloikumba familia yangu.

“Napata pesa nyingi lakini hazikushuka tu kutoka mbinguni. Lazima nijitume. Nisipocheza vizuri, watu watanifukuza.”

Maisha nchini England hayakuwa mapesi kwa Nani. Ilichukua muda kupata imani kutoka kwa mashabiki na kuibuka kutoka kwenye kivuli cha Ronaldo at United. Kulikuwa na kipindi ambapo wasiwasi wa Queiroz juu ya Nani kuweza kumudu kucheza Old Trafford ilianza kuchukua nafasi.

Hata baada ya kuongoza kwa kutoa asisists nyingi msimu uliopita, alijikuta akiwa kwenye benchi katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Barcelona, na kuwasili kwa winga wa kiingereza Ashley Young kipindi cha kiangazi kulizusha speculations kwamba mreno huyo angeweza kuondoka Old Trafford.

In fact, Nani amethibitisha ubora wake akiwa na United msimu huu. Ana furaha nje ya uwanja na hata nyumbani kwake – Cheshire ambapo anakaa na mpenzi wake Daniela na mbwa wao wawili.

“Sikuwa na bahati nzuri kuzoea maisha ya England, tena ilikuwa vigumu sana kuishi peke yangu, huku nikiwa sijui kuongea lugha ya pale. Ilifikia kipindi nilikuwa naishi kwa Cristiano na nilijisikia vizuri sana Kulikuwa kuna watu poa sana na tulikuwa na kila kitu – swimming pool, Jacuzzi, tennis, kiukweli kipindi nakaa kwa Ronaldo sikuwahi kui-miss familia yangu.

“Lakini baadae ilibidi niondoke kwa Ronaldo kwa sababu ilibidi niwe na maisha yangu. Ilikuwa vigumu sana kwa sababu ilikuwa nyumba kubwa na usiku ilikuwa kama nyumba ya mchawi.

“Nilikuwa naogopa hata kuwa nyumbani. Sometimes sikuwa natoka hata chumbani. Nilienda kulala mapema bila kula vizuri kwa sababu sikutaka kula dinner peke yangu.”

Hata sasa, Nani anakiri, hawezi kuangalia movie za kutisha kwa sababu zilikuwa zinamfanya asilale kwa woga. Anapenda kukaa na Daniela na kuangalia tamthilia na kupig piano.


October 2011. Katika uwanja wa Porto Estadio Do Dragao. Nani alifunga mabao mawili ya mwanzo katika ushindi wa Ureno wa 5-1 dhidi ya Iceland, na kumfunika mchezaji mwenzie Ronaldo. Siku iliyofuata katika kurasa za mbele za gazeti la Correio da Manha na A Bola walieka picha zake akiwa anashangilia.

Mtoto kutoka Santa Filomena ametoka mbali sana.

Friday, October 28, 2011

DSM DERBY COUNTDOWN: MAELEKEZO


MECHI- YANGA vs SIMBA
-Milango itafunguliwa saa 7 mchana.
-Hakuna kitu chochote kitakachoruhusiwa kuuzwa uwanjani
-Mashabiki wakae maeneo kulingana na tiketi zao. Eneo la VVIP ni maalumu kwa wageni waalikwa na si kwa ajili ya watu wenye tiketi za VIP A.
-Msalaba Mwekundu (Red Cross): Tunawakumbusha Red Cross wataendelea kukaa katika maeneo yao husika, kwa sababu rangi zao zinatumika duniani kote na hazina uhusiano na klabu/timu yoyote.

BRIAN ROBSON ATUA NCHINI TANZANIA KWA AJILI YA CLINIC YA AIRTEL RISING STARS

BRIAN ROBSON AKIWA NA MANEJA UHUSIANO WA AIRTEL JACKSON MBANDO ( KULIA )

HAPA AKITETA JAMBO NA AFISA MAENDELEO WA TFF SALUM MADADI



NILIPATA FURSA YA KUPIGA STORY KADHAA NA BRIAN ROBSON..














TIMBE: YANGA WANILIPE MISHAHARA YANGU NA FEDHA ZA KUVUNJA MKATABA


Kocha Sam Timbe ambaye alifungashiwa virago na ‘Wanajangwani’ baada ya kurejeshwa kwa kocha aliyemtangulia, Mserbia Kostadin Papic, ameutaka uongozi wa klabu hiyo umlipe fedha zake ili aondoke zake nchini.

Akizungumza jana na kwenye hoteli ya Markham, Timbe alisema kuwa anasikitishwa na kile anachofanyiwa sasa na uongozi wa Yanga kwani aliamini kuwa watatanguliza uungwana na kumlipa stahili zake mara tu walipoamua kuvunja mkataba wake wa ajira.

"Ni wao ndio walioamua kuvunja mkataba… wanapaswa kunilipa haki yangu ili na mimi nifanye mambo mengine. Hadi sasa sijui ni lini watanilipa fedha zangu," alisema Timbe.

Alisema kuwa mbali na kuidai Yanga gharama ya kuvunja mkataba wake, pia anaidai klabu hiyo fedha za kuingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo pamoja na mshahara wake wa mwezi uliopita hadi sasa.

"Niliposaini mkataba mwezi Mei mwaka huu walinilipa sehemu tu ya fedha tulizokubaliana na nyingine waliahidi kunilipa baadaye… lakini hadi walipovunja mkataba Oktoba 23, hawakuwa wamenilipa fedha zilizobakia na zote naamini kwamba watanilipa mara moja ili niondoke zangu,” alisema Timbe, ambaye aliongeza kuwa hajui ni kwanini ametimuliwa ghafla wakati timu aliyokuwa akiifundisha ilikuwa na mwelekeo mzuri na kukamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Bara.

"Baada ya mechi yetu dhidi ya Oljoro, nilipewa barua ya kunijulisha kikao na uongozi wa Yanga ili kujadili maboresho ya benchi la ufundi. Katika barua hiyo niliambiwa kwamba kikao kitakuwa cha watu wanne ambao ni mimi na viongozi watatu ambao wangefika hapa hotelini ninakoishi," alisema.

Hata hivyo, Timbe anasema kuwa alishangaa kuona kuwa kesho yake anafuatwa na kiongozi mmoja na kupewa barua ya kuvunja mkataba, bila kupewa maelezo zaidi.

"Mimi sikuwa na jinsi isipokuwa ni kudai haki yangu. Ila iliniuma moyoni nilipokuja kufahamu kuwa tayari walishamleta kocha mwingine wa kutwaa nafasi yangu. Jambo hili limenisikitisha sana," alisema Timbe.

TIMBE ASHIKILIWA HOTELINI, ADAIWA FEDHA ZA MALAZI.


Kocha aliyefungashiwa virago na klabu ya Yanga, Mganda Sam Timbe, amejikuta katika hali ngumu baada ya kung’ang’aniwa na uongozi wa hoteli aliyokuwa akiishi jijini Dar es Salaam kutokana na deni linalozidi Sh. milioni 19.5.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa hoteli ya Markham iliyopo Mikocheni zinaeleza kuwa Timbe ameshikiliwa ili kuishinikiza Yanga iliyompangia hotelini kulipa deni hilo linalotokana na malazi ya dola za Marekani 75 kwa siku (Sh. 128,576) pamoja na huduma nyingine ambazo zimelimbikizwa na Yanga tangu katikati ya Juni.

Meneja wa hoteli hiyo aliiambia blog hii jana kuwa uongozi wa Yanga ulimlipia Timbe kwa mwezi mmoja tu na tangu hapo hawajalipa tena na kuacha deni hilo liongezeke kila uchao.

"Tunajua si Timbe ambaye anatakiwa kutulipa fedha hizi, lakini tumeamua kushikilia hati yake ya kusafiria na tutaendelea kumdhibiti ili Yanga ambao ndio waliompangia watulipe fedha zetu," alisema meneja huyo.

Uongozi wa Yanga ulikiri jana kuwa ni kweli unadaiwa na hoteli waliyompangia Timbe na kudai kuwa wapo katika mchakato wa kuwalipa fedha hizo.

"Sisi (Yanga) tumefanya biashara na makampuni mbalimbali na hakuna iliyowahi kukimbilia kwenye vyombo vya habari kama hawa wenzetu. Tunawasiliana nao kila wakati na kuwaahidi kuwalipa fedha hizo, lakini tunawashangaa kwa hatua yao hii… ni kweli wanatudai na tupo kwenye mchakato wa kuwalipa," Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.



WAMBURA: NAENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YANGU


Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara(FAM) kabla ya kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho, Michael Wambura amesema amemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Alfred Tibaigana ili kumweleza kile alichodai kutopokelewa kwa rufaa yake aliyowasilisha kwenye ofisi za shirikisho hilo.

Wambura anaishutumu TFF kukataa rufaa yake kwao juzi akipinga kuondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM na kamati ya uchaguzi ya TFF iliyokutana jijini Dar es Salam wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Wambura alisema kuwa amefikia uamuzi wa kumuandikia barua Tibaigana kujua kama kamati yake ina uwezo wa kusikiliza rufaa yake au haina kabla ya kuamua kuchukua hatua nyingine anazofikiri zinamfaa.

Alisema kuwa,hilo limekuja baada ya jana TFF kwa mara nyingine kukataa kupokea kiasi cha Sh 300,000 kama ada ya rufani.Wambura alisema kuwa endapo Tibaigana atamjibu kwamba hana uwezo wa kusikiliza sakata lake, anatarajia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa lengo la kupata haki yake.

"Jana nimepeleka tena Sh,300,000 kama ada ya rufani pia wamekataa, baada ya hapo niliamua ni kwenda kutumia kwa njia ya benki na kisha nikawapelekea risiti ambayo pia wamekataa na nimeamua kuwatumia kwa Fax.

"Sasa hivi nimemwandikia barua Tibaigana kumweleza kuhusu kilichotokea ni matumaini yangu atanijibu haraka na kama ataniambia hata uwezo wa kusikiliza rufaa yangu Jumatatu nitakwenda kutafuta haki mahakamani," alisema Wambura.

Kamati ya uchaguzi ya TFF ilimwondoa Wambura kwa madai ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA)inayozuia masuala ya soka kupeleka mahakamani ikidai aliwahi kwenda mahakani kuishtaki Simba.

VITA KUBWA YANUKIA KATI YA T.F.F NA VILABU VYA LIGI KUU


Mgogoro mkubwa unakaribia kuikumba Ligi Kuu ya Tanzania baada ya viongozi wa vilabu kusema hawatoitambua kamati itakayoteuliwa na Rais wa Shirikisho Soka nchini TFF, Leodegar Tenga na kutishia kugomea kushiriki mzunguko wa pili iwapo TFF hawatawalipa fedha zao.

Makamu mwenyekiti wa Simba na Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu mchakato wa Kampuni ya Ligi, Geofrey Nyange 'Kaburu' ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kusisitiza kwamba wao wanatambua kamati ya ligi ikiwa ni utekeleza makubaliano ya mkutano mkuu na si vinginevyo.

Katika kushikilia msimamo huo, Osiah aliweka wazi kuwa Rais Tenga anatarajiwa kuwasilisha majina ya watu ambao amewateua kuunda kamati huru ya kusimamia Ligi Oktoba 27, jana kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya TFF.

Lakini jana Kaburu alisema wameshawasilisha barua TFF ya kuwataka kusitisha uteuzi wa kamati hiyo na kwamba kama TFF itaendelea kung'ang'ania kuundwa kwa kamati hiyo klabu kama wadau wakuu wa soka hawataitambua na wanaendelea na mchakato wao wa kuanzisha kampuni.

Kaburu alisema pia wameitadharisha TFF isithubutu kufanya mazungumzo yoyote na mdhamini wa Ligi msimu wa 2012/2013 kwa kuwa ule wa Vodacom unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo mikataba yote itasimamiwa na kampuni ambayo itakuwa tayari imeshaanzishwa.

"Klabu nyingi za Ligi Kuu zinaidai TFF fedha nyingi ambazo tayari zilikwishatolewa na wadhamini wa Ligi Kuu na madeni haya yanatokana na utoaji wa hundi hewa na TFF kutumia fedha za klabu kwa matumizi tofauti yaliyodhamiriwa.

"Klabu 13 za Ligi ambavyo ziliudhuria kikao chetu kilichofanyika JB del-monte ukiondoa Kagera Sugar ambayo ilikosa mwakilishi tuliazimia kutocheza mzunguko wa pili wa ligi hii inayoendelea hadi hapo TFF itakapolipa madeni hayo."

"Tumefanya utafiti wa kile kilichoelezwa na rais Tenga kwamba Bundesliga ya Ujerumani inaendeshwa na kamati, kitu ambacho hakina ukweli, Bundesliga ipo katika mfumo wa kampuni," alisema Kaburu.

"Suala la uendeshwaji wa Ligi huru ni maelekezo ya FIFA ambayo yameshatekelezwa na nchi nyingi duniani na mfumo bora wa uendesaji wa ligi yenye tija..."Tanzania suala hili lilishajadiliwa kwenye azimio la Bagamoyo mwaka 2007, lakini cha kusikitisha hadi FIFA wanarudi tena mwaka 2011 kupitia azimio hilo hakuna lolote lililofanyika.

"Viongozi wa klabu tulitarajia mara baada ya kikao chetu cha Aprili mwaka huu na Rais Tenga alitakiwa kuunda kamati mara moja na kuanza kazi kabla ya msimu huu wa ligi kuanza, cha kusikitisha mpaka leo hii kamati haijaundwa na hakuna taarifa rasmi kwa klabu.

Katibu wa TFF, Osiah akijibu madai hayo alisema jana usiku kamati itakaa na kujadili majina ya wajumbe ambao wataunda kamati ya kusimamia ligi.

"Klabu zote za Ligi Kuu ni wajumbe wa mkutano mkuu na tulishakubalia kwenye mkutano mkuu kuwa tuwe na kamati ya mpito itakayokuwa ikisimamia ligi kwa muda wa miaka miwili baada ya hapo kutakuwa na uchaguzi."
Osiah aliongeza kuwa klabu kutishia kugomea kucheza ligi kwa sababu kutolipwa madeni yao na kukataliwa kwa kampuni huko ni kuchanganya ajenda.

Thursday, October 27, 2011

BRYAN ROBSON - NAHODHA WA MAN UNITED ALIYECHEZA MICHEZO MINGI KULIKO WOTE


UNAPOZUNGUMZIA MANAHODHA WALIOWAHI KULITEKA SOKA LA NCHINI ENGLAND HUWEZI KUEPUKA KULITAJA JINA LA BRIAN ROBSON.

BOBSON ALIKUWA MOJA YA WACHEZAJI WALIOWIKA SANA AKIWA NA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND NA VILABU KADHAA NCHINI HUMO HUSUSANI MANCHESTER UNITED AMBAKO HADI ANASTAAFU ALIKUWA NA REKODI KAMA NAHODHA ALIYECHEZA MICHEZO MINGI KULIKO WOTE.

BRIAN ROBSON ALIZALIWA HUKO CHESTER LE STREET TAREHE 11 MWEZI JANUARI MWAKA 1957 AKIWA MTOTO WA PILI KATI YA WATOTO WANNE . BABA YAKE MZAZI AMBAYE ALIFAHAMIKA KWA JINA KAMA HILO BRIAN ROBSON ALIKUWA DEREVA WA MALORI YA KUBEBA MIZIGO. AKIWA NA UMRI MDOGO WA MIAKA 6 , ROBSON ALIKUWA SHABIKI MKUBWA WA KLABU YA NEWCASTLE UNITED HUKU SHUJAA WAKE KWENYE MCHEZO HUU AKIWA MSHAMBULIAJI NYOTA WA TIMU HIYO WYN DAVIES.

KIPAJI CHA ROBSON KWENYE MICHEZO KILIANZA KUONEKANA MAPEMA TANGU SHULENI AMBAKO ALISHIRIKI KWENYE RIADHA NA SOKA KWA NYAKATI TOFAUTI .

SIFA YA UONGOZI KWA ROBBO KAMA MASHABIKI WENGI WANAVYOPENDA KUMUITA ILIANZA KUONEKANA WAKATI HUU AMBAKO KWENYE UMRI MDOGO ALIWEZA KUWA NAHODHA WA TIMU YAKE YA SHULE NA ILE YA WILAYA .

WAKATI ALIPOMALIZA SHULE BRIAN ROBSON ALIJIUNGA NA KLABU YA WEST BROMWICH ALBION BAADA YA KUFANYA MAJARIBIO KWENYE TIMU ZA COVENTRY , BURNLEY NA SHEFFIELD WEDNESDAY.

BAADA YA MUDA BRIAN ROBSON ALIHAMIA MANCHESTER UNITED MNAMO MWAKA 1981 AKINUNULIWA KWA ADA YA UHAMISHO ILIYOWEKA REKODI KWA KIPINDI HICHO YA PAUNDI MILIONI 1.5. REKODI HII ILIDUMU KWA MUDA WA MIAKA 6 HUKU IKIVUNJWA NA PETER BEARDSLEY ALIYEUZWA NA NEWCASTLE KWENDA LIVERPOOL.

ROBSON ALIPOJIUNGA UNITED ALIPEWA JEZI NAMBA 7 NA ALIIMILIKI JEZI HII KWA MUDA WOTE ALIPOKUWA KWENYE TIMU HII.

ROBBO NDIYE ALIYEKUWA NAHODHA WA KWANZA KUTWAA TAJI CHINI YA KOCHA SIR ALEX FERGUSSON AKIFANYA HIVYO MWAKA 1991 AMBAPO UNITED WALITWAA KOMBE LA FA BAADA YA KUWAFUNGA CRYSTAL PALACE KWA BAO 1-0 BAADA YA SARE YA MABAO 3-3. TAJI HILI LILIMPA ROBSON REKODI YA KUWA NAHODHA WA KWANZA KUTWAA KOMBE FA MARA TATU KWA MAN UNITED .

HUO ULIKUWA MWENDELEZO WA MAISHA MAZURI AKIWA NA TIMU HII CHINI YA KOCHA MPYA ALEX FEGUSSON AMBAKO UNITED ILIENDELEA KUTWAA MATAJI BAADA YA KUFANIKIWA KUTWAA TAJI LA KWANZA LA ENGLISH PREMIER LEAGUE MWAKA 92/93.

BRIAN ROBSON ALICHEZA MECHI YAKE YA MWISHO AKIWA NA UNITED MWEZI MEI TAREHE 8 MWAKA 1994 KWENYE MCHEZO AMBAO UNITED ILITOKA SARE YA BILA KUFUNGANA NA COVENTRY CITY.

HADI HAPA BRIAN ROBSON ALIKUWA AMEIWAKILISHA UNITED MARA ZISIZOPUNGUA 461 HUKU AKIFUNGA MABAO 99 AMBAPO ALIFANIKIWA KUTWAA MATAJI MATATU YA KOMBE LA FA , MATAJI MATATU YA UBINGWA WA LIGI KUU YA ENGLAND NA KOMBE LA WASHINDI BARANI ULAYA.

KATIKA KIPINDI CHOTE HICHO ROBSON PIA ALIIWAKILISHA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND MARA 90 KATIKA MIAKA YA 81 NA 90 HUKU AKIFUNGA MABAO 26.

BAADA YA UCHEZAJI BRIAN ROBSON ALIHAMIA KWENYE UKOCHA AMBAKO ALIANZIA MIDDLESBOROUGH KAMA KOCHA MCHEZAJI HUKU AKIWA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND CHINI YA TERRY VENABLES. BAADA YA HAPO BRIAN ROBSON ALIZIFUNDISHA BRADFORD CITY , WEST BROMWICH ALBION , SHEFFEILD UNITED NA TIMU YA TAIFA YA THAILAND .

MWAKA 2008 BRIAN ROBSON ALIREJEA UNITED KAMA BALOZI WA KIMATAIFA WA KLABU HIYO , JUKUMU AMBALO LIMEMLETA NCHINI TANZANIA AMBAKO ATASHIRIKI KWENYE UZINDUZI WA MRADI WA AIRTEL NA MANCHESTER UNITED WA AIRTEL RISING STARS .