Search This Blog

Saturday, May 26, 2012

TAIFA STARS YATOKA SARE NA MALAWI - YAJIWINDA KUWAKABILI AKINA DROGBA

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania - Taifa Stars leo imetoka sare tasa dhidi ya Msumbiji kwenye mchezo kirafiki kuelekea kwenye mechi ya kugombea nafasi ya kucheza KWENYE KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014 dhidi ya Ivory Coast.
Mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars Mbwana Samata ambaye anacheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe nchini DRC Congo akijaribu kumtoka beki wa malawi Foster Namwela wakati timu hizo zikimenyana kwenye uwanja wa Taifa jioni hii
 Wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars wakiingia uwanjani jioni hii kwa ajili ya kupasha mwili kabla ya mpambano wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Malawi The Flames
 Wachezaji wa timu ya Malawi wakipasha mwili kabla ya kuingia uwanjani kukwaana na Taifa Stars jioni hii kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa Stars wakijifua kabla ya mpambano huo jioni hii.

HIZI NDIO NJIA WATAKAZOPITA SIMBA KULITEMBEZA KOMBE LAO - KUTOKA MSIMBAZI MPAKA DAR LIVE

NAHODHA WA NIGERIA: KIFO CHA YEKINI KINA UTATA - UFANYIKE UCHUNGUZI - HAKUWA NA KICHAA.

Nahodha wa zamani wa Nigeria Segun Odegbami ameomba kufanyika kwa uchunguzi wa kina dhidi ya kifo cha RashidI Yekini.

Yekini aliripotiwa kutekwa muda mfupi kabla ya kifo chake, lakini chanzo halisi cha kifo chake bado hakijawa wazi.

"Walimchukua na kumteka kwa takribani wiki 3 na walipomrudisha, tayari alikuwa maiti - je kuna kitu gani kilitokea kipindi chote hicho walichokuwa kuwa nae?" -alisema Odegbami.

"Hakuna anayesema kwamba aliuwawa lakini chochote walichomfanya - katika jitahada za kumtibu kwa ugonjwa usio mkubwa ambao hakuwa nao - ndio kunaweza kuwa kumepelekea kuisha kwa uhai wake.

"Ndio maana tunasema uchunguzi inabidi ufanyike, ili atleast tujue nini kilisababisha kifo chake. Wapi alipokufa? Walimpeleka wapi? Nani alimtibu tena kwa ugonjwa gani?

"Huyu ni gwiji wa soka la Afrika - nyota na mtu ambaye amefanya watu wengi kupenda soka."

Polisi wa Nigeria wa Oyo State, mahali ambapo Yekini alikuwa akiishikabla ya kifo chake, wameliambia shirika la habari la Uingereza kwamba hakuna uchunguzi wowote uliofunguliwa juu ya kifo cha mchezaji huyo.

Odegbami ambaye pia alicheza na Yekini, anasema watu walikosea kuamini kwamba Yekini , ambaye aliishi kwa kujitenga katika miaka ya hivi karibuni, kwamba alikuwa akiandamwa na msongo wa mawazo.

"Watu wana mtazamo kwamba alikuwa ni chizi," alisema Odegbami, ambaye alikuwa na mawasiliano na Yekini mapema mwaka mwaka huu.

"Rahidi alikuwa sawa kiakili, alikuwa na afya, na fiti na hakuwa na tatizo lolote. Mtu wa namna hiyo hawezi kufa kiajabu ajabu na hakuna mtu anayejua amekufa vipi - wapi alifia na nini kilichomuua."

PEP GUARDIOLA AAGWA BARCELONA NA TAJI LA 14 -BARCELONA WAKIICHAPA BILABO 3-0


Barcelona vs Athletic Bilbao 3:0 GOALS HIGHLIGHTS by maidb7abc

ETOO KUTUMIA MAMILIONI YA WARUSI KUFUNGUA KITUO CHA SOKA KENYA


MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya taifa yCameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Samuel Eto'o, amekiri kuipenda Kenya hasa maeneo ya Pwani.

Eto'o amesema hayo baada ya kutangaza kuanzisha Chuo cha Soka katika eneo la Laikipia na kununua majumba kadhaa mjini Mombasa.


Mwanasoka huyo pia amezuru Laikipia kutazama mechi ya fainali ya Kombe la Laikipia Unity ambalo linafadhiliwa na Wakfu wa Zeitz.


Etoo alitangaza azimio la kuanzisha chuo hicho baada ya kuwaona wanasoka chipukizi walivyo na vipaji vya soka.
Kenya ina vipaji chungu nzima katika soka na chuo chetu kitasaidia kuwakuza na kuwapa vijana nafasi ya kujipatia riziki, kitaifa na kimataifa pia.

Etoo pia alisema anavutiwa mno na mandhari ya Mkoa wa Pwani akidokeza kuwa na nia ya kutafuta mali katika eneo hilo.

Ninaipenda Kenya na kila ninapokuja ninahisi kuwa nyumbani. Ninatamani kujenga au kununua nyumba mjini Mombasa lakini Laikipia pia ni kuzuri, alisema mwanasoka huyo.

EXCLUSIVE: HII NDIO SIRI YA MAISHA YA WACHEZAJI WA KIBONGO NJE YA TANZANIA.


Kwa miaka ya hivi karibuni Watanzania tumekuwa tukijivunia sana juu wachezaji wetu wa kibongo kujaribu kucheza soka la kulipwa katika nchi mbalimbali barani ulaya. Lakini je umeshawahi kujiuliza ni wachezaji wetu wa kitanzania wanaishi vipi kwenye nchi hizo. Kupitia www.shaffihdauda.com utapata kujua mambo mengi yaliyo nyuma ya maisha ya Wachezaji hawa wa kibongo waliopo barani ulaya kwa madai ya kucheza soka la kulipwa.

STAY TUNEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEED

Friday, May 25, 2012

EDEN HAZARD: MBELGIJI AMBAYE SIKU 8 ZIJAZO ATAAMUA KUJIUNGA NA MAN UNITED, CHELSEA AU MAN CITY.





SHINJI KAGAWA: KUTOKA LIGI YA DARAJA LA PILI YA JAPAN MPAKA DORTMUND - SHINJI KAGAWA SUPERSTAR ANAYEFUATIA NDANI YA MAN UNITED?S

Wakati taarifa za usajili wake kwenda Manchester United zikizidi kukaribia kuwa ukweli, ebu leo tuangalie uchambuzi wa kisoka kuhusu Shinji Kagawa.

Misimu miwil iliyopita, Shinji Kagawa alikuwa hajulikani kabisa nje ya Japan, lakini watu wale wenye macho yanayoona mbali waliona kiungo aliyebarikiwa uwezo wa kucheza soka huku akiisadia klabu yake ya Cerezo Osaka kupanda daraja la juu kwenye soka la Japan ndani ya misimu mitatu tu. Sasa yupo karibuni kujiunga na mabingwa kihistoria wa Barclays Premier league pale Theatre of Dreams - baada ya Red Devils kutuma ofa ya £13miilion kwa Dortmund.

Kagawa alikuwa ndio mjapan wa kwanza kuisaini mkataba wa level ya proffessional kabla ya kumaliza kutoka kwenye elimu ya juu ya sekondari. Akiwa na miaka 18 aliweza kupata nafasi ya kwenye kikosi cha kwanza cha Cerezo, na kujiamini kwake kukapanda sana baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kufunga. Kagawa alifunga mabao 27 katika mechi 44 kwenye msimu wa 2009 na kuwasaidia Cerezo kurudi kwenye ligi kuu ya Japan baada ya kushuka kwa miaka 3. Lakini hakuweza kucheza sana kwenye ligi kuu ya Japan, baada ya wakala wa kijerumani Thomas Kroth kushughulikia uhamisho  ambao ulimuamisha kinda hilo kwenda Borussia Dortmnund - wakati timu hilipokuwa ikijipanga upya baada ya kumaliza ligi kwenye nafasi ya 5.

Performance yake pale Dortmund inajieleza yenyewe; kwenye msimu wa kwanza barani ulaya, Kagawa alikuwemo kikosi bora ya Bundesiliga japokuwa alitumia nusu ya msimu kuwa nje ya dimba kutokana  na majeruhi. Mwaka huu, ameweka rekodi mpya kwa Wajapan waliowahi kucheza Ulaya kwa kufunga mabao 13 kwenye mechi 32. Shinji ni hatari kila anapogusa mpira, ana uwezo wa kutengeneza nafasi kwa kutoa pasi za mwisho huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali.


Nchini kwao Japan, Kagawa ni moja ya wanasoka wenye majina makubwa sana na mara nyingi amekuwa akitumika kwenye matangazo akitangaza vinywaji pamoja video games.

Jezi yake ndio inaongozwa kwa kuuzwa, kwenye msururu wa maduka ya kuuza vifaa vya soka KAMO, huku ikitegemewa mauzo kupanda ikiwa tu atajiunga na klabu yenye umaarufu mkubwa kuliko zote duniani huko ASIA - Manchester United. Umaarufu wa Kagawa ambao kwa sasa upo sawa na wachezaji kama Yuto Nagamoto wa Inter pamoja na mshambuliaji wa CSKA Moscow Keisuke Honda.

Lakini tofauti na wenzake Nagamoto na Honda ambao wanapenda sana kutokea kwenye vyombo vya habari, Kagawa yeye ni kama Paul Scholes hapendi mambo ya kuwa karibu sana na media kwa aibu aliyonayo.

Pamoja na kuwa na miaka miwili Ujerumani, bado anaongea aidha kupitia mtafsiri wake au vyombo vya habari vya Japan ambavyo vimekuwa vikimfuata.

Ikiwa atahamia England itabidi ajipange sana ama aendelee kuufuata mfano wa Paul Scholes ili aweze kuepukana na vyombo vya habari vya nchi hiyo ambavyo vingine vimeanza kusema United wanamsajili Mjapan huyo kwa sababu za kibiashara - kuongeza mauzo ya bidhaa zao barani Asia hasa nchini Japan. Lakini  ama kwa hakika huyu ni aina ya kiungo mshambuliaji ambaye United wanamhitaji ili kuweza kukirudishia kikosi uwezo wa kutawala tena soka la England.

Ndani ya misimu miwili aliyokaa na Dortmund - amesaidia klabu hiyo kuupora utawala wa soka la Ujerumani kutoka kwa Bayern Munich kwa mara mbili mfululizo.

SEPP BLATTER: MIKWAJU YA PENATI INAPOTEZA MAANA SOKA

Sepp Blatter - Raisi wa FIFA.
No wonder Waingereza hampendi Sepp Blatter.

Wiki moja baada ya timu ya Chelsea ya England kuifunga FC Bayern Munich kwa mikwaju ya penati na kufanikiwa kuchukua kombe la Mabingwa wa Ulaya - jana Bosi wa FIFA Sepp Blatter amesema anaona ni bora itafutwe njia mbadala wa kuamua mshindi wa mechi badala ya mikwaju hiyo ya penati.
Drogbaa akifunga penati iliyoipa Ubingwa wa Chelsea.

Blatter alisema: "Soka inakuwa inapoteza maana kabisa linapokuja suala la penati. Huu ni mchezo wa timu ya watu 11 kila upande, kwa maana hiyo linapokuja suala one against one - mchezo huo unapoteza maana yake.

"Labda Franz Becknbauer na wenzie kwenye kamati yao, wanaweza kutuonyesha suluhisho, inawezekana isiwe sasa labda baadae."

FAMILIA YA MAFISANGO YAOMBA MSAADA SIMBA NA AZAM


FAMILIA ya aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Simba na timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Patrick Mutesa Mafisango, imeomba msaada kutoka kwa klabu ambazo marehemu alizitumikia miaka ya hivi karibuni.


Marehemu Mafisango, kabla ya kutua Simba na hivi karibuni kurejeshwa Amavubi ambako pia aliwahi kuwa nahodha, alikipiga kwa wana Lambalamba, Azam FC.

Akizungumza katika mahojiano nA Clouds TV hivi karibuni, nyota wa zamani wa Simba, ambaye anakipiga timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Mussa Hassan Mgosi, alisema kifo cha mchezaji huyo ni pigo kwa familia yake na hasa watoto wake watatu aliowaacha.

Mgosi alisema kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu nchini Congo na jinsi ambavyo familia hiyo ilikuwa ikimtegemea marehemu kwa kuwatumia fedha ili waweze kujikimu na hali ngumu ya maisha, huu ni muda muafaka kwa Simba, Azam na Amavubi kutoa sapoti, walau familia hiyo iweze kujikimu.

Aidha mbali na timu hizo, Mgosi aliwaomba wachezaji kutoka Simba, Azam na wadau mbalimbali, kujichanga na kila mtu kutoa kile alichonacho ili waweze kuliokoa jahazi ambalo mpiganaji mwenzao ameliacha.

Marehemu Mafisango, alifariki usiku wa kuamkia Mei 17 kwa ajali ya gari katika eneo la Veta Chang’ombe jijini Dar es Salaam na kuzikwa mwishoni mwa wiki iliyopita, katika makaburi ya Kinkole nje kidogo ya jiji la Kinshasa. Marehemu ameacha wake watatu na watoto watatu.

TFF: HATUTOMLIPA HATA SENTI MOJA JAN POULSEN


SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limeweka wazi kwamba aliyekuwa kocha wa timu ya taifa(Taifa Stars)Mdenmark Jan Poulsen hatalipwa mishahara yake ya miezi mitatu iliyosalia katika mkataba wake.

Msimamo huo wa TFF umekuja baada ya  gazeti la Mwananchi wiki iliyopita kumkariri Poulsen akililalamikia shirikisho hilo lwa kutolipwa mshahara wake wa mwezi mmoja,sambamba na fidia inayotokana na kuvunjwa kwa mkataba wake.
Hivi karibuni TFF ilisitisha huduma ya Poulsen kwa Taifa Stars na badala yake ikamtangaza aliyekuwa kocha wa timu za taifa za vijana, Kim Poulsen kuchukua jukumu hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa hatua ya kutomlipa Poulsen mishahara ya miezi mitatu inatokana ukweli kwamba kocha huyo hatakuwa na kazi ya kufanya katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya mkataba wake kilichosalia hadi Julai 30.

"Kwanza kabisa ieweweke kwamba serikali ndiyo iliyokuwa inamlipa  Poulsen mshahara baada ya kuingia naye mkataba na sio TFF."Katika utaratibu wa kawaida wa serikali tunaoufahamu awezi kulipwa mshahara wa bure wakati hajafanya kazi yoyote,huo ndio ukwli wenyewe,"alisema Wambura

Akifafanua zaidi, Wambura alisema TFF iliamua kusitisha huduma za Poulsen licha ya kwamba mkataba wake unaendelea kuwa hai kwa lengo la kuta nafasi kwa kocha mpya kupanga mipango ya muda mrefu.

"Kila baada ya muda fulani kocha anatakiwa awasilishe ripoti ya timu yake,sasa utapataje ripoti sahihi wakati kesho kutwa mkataba wake unamalizika.

"Pia niweke vizuri hapo,TFF haikuvunja mkataba wa Poulsen bado upo na utamalizika Julai 30 tulichokifanya ni kuzungumza nae na kukubaliana kwamba hakutaongeza mkataba hivyo tunatafuta kocha mwingine,"alisema.

Wambura aliongeza kuwa,licha ya kibarua cha kocha huyo cha kuinoa Taifa Stars kusitishwa,bado TFF itaendelea kuwa nae katika mkataba mwingine unaohusiana na ukufunzi wa makocha nchini.

"Poulsen pia alikuwa na kazi nyingine ya ukufunzi wa makocha hata hapa ametuaga anakwenda kwao kuhudhuria harusi ya mtoto wake akirudi ataendelea,"alisema Wambura

Kwa  upande mwingine kusitishwa kwa kibarua cha Poulsen kunahusishwa  na shinikizo la wadau wa soka waliotaka mabadiliko katika benchi la ufundi kufuatia Taifa Stars  kuporomoka mfululizo kwa takribani miezi saba kwenye viwango vya ubora vya Shiriki

BOBAN NA SAMATTA KUONGOZA MASHAMBULIZI YA TAIFA STARS


KOCHA wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Kim Poulsen amewapa majukumu ya ufungaji mabao kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi 'Boban' na mshambuliaji Mbwana Samata katika kikosi chake kilicho kambini hivi sasa.

Katika mazoezi ya kikosi hicho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Kim amekuwa akiwachezesha pamoja Boban anayeichezea Simba na Samata anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuonyesha maelewano makubwa na wakupachika mabao mengi ya kiufundi.

Kim amekuwa akikigawa kikosi chake katika timu mbili na kuwachezesha pamoja, Samata anayetumika kama mshambuliaji namba tisa na Boban anayetumika kama mshambuliaji namba 10.

Kitendo cha Kim, kumtumia Boban kama mshambuliaji badala ya kiungo kama asili yake, kimeonekana kuwa na faida, kwani kimetoa fursa kwa chipukizi wa JKT Ruvu,  Frank Domayo kutumika kama mpishi namba nane.

Naye Mrisho Ngasa ambaye amekuwa akimtumia kama winga wa kushoto kama ilivyo kwa Mwinyi Kazimoto anayecheza winga wa kulia, mara kadhaa amekwaruzana na Kim kutokana na tabia yake ya kung'ang'ania kukaa pembeni badala ya kuingia ndani kuwasaidia viungo Domayo na Shaabani Nditi hasa pale mashambulizi yanapoelekezwa kwao.

Katika safu ya ulinzi, kocha huyo Mdenmark amekuwa akimpanga Aggrey Morris kama mlinzi wa kati akisaidiana na Kelvin Yondan anayecheza namba nne huku Shomari Kapombe akiimarisha ulinzi wa kulia kama ilivyo kwa Waziri Salum anayedhibiti nafasi ya beki wa kushoto.

Picha halisi ya kikosi cha kwanza cha Kim kutokana na mazoezi hayo ni kipa Juma Kaseja, Shomari Kapombe,Wazir Salum, Kelvin Yondan, Aggrey Morris, Shaaban Nditi, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Haruna Moshi'Boban', Mbwana Samata na Mrisho Ngasa.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kutua leo saa 10 jioni kwa ndege ya Air Malawi tayari kwa kuivaa Taifa Stars kesho katika pambano la kimataifa la kirafiki litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars itaikabili The Flames ikiwa ni maandalizi ya mechi yake ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan, huku pia Malawi ikitumia mechi hiyo kujiandaa kupambana na Kenya.

Viingilio katika mtanange wa Taifa Stars na Malawi  vitakuwa Sh 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, Sh 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, Sh 15,000 kwa jukwaa la viti maalumu B na C na Sh 20,000 kwa jukwaa la viti maalumu A.

HISTORIA - FC BAYERN MUNICH NI TIMU YA WAGENI WALIOZAMIA MUNICH - TSV 1860 MUNICH NDIO WAKONGWE NA WAZAWA WA MUNICH




Katika kipindi hiki chote ambacho nimekaa hapa jijini Munich Ujerumani, nimepata kugundua vitu kadhaa vinavyozihusu klabu pinzani za jiji hili FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen.
Hizi ni klabu mbili ambazo zote zipo katika jiji moja na zinafanana kidogo na timu zetu pinzani za Simba na Yanga - Bayern Munich na 1860 Munich na zenyewe zina upinzani mkubwa sana na zote zinatumia kiwanja cha Allianz Arena kuchezea mechi za nyumbani lakini pia klabu hizi mbili zipo katika eneo moja ndani ya jiji la Munich - Umbali wa kutoka makao makuu ya Bayern mpaka 1860 Munich ni dakika 5 kwa kutembea.

Kihistoria TSV 1860 Munich ndio klabu ya kwanza kuanzishwa, ilianzishwa na mabavaria wenyewe miaka 152 iliyopita. Ilikuwa ndio klabu ya kwanza jijini Munich kupata mafanikio ya kucheza ligi kuu ya Ujerumani. Miaka ikasonga baada ya mbele mpaka ilipofika mwaka 1900, baadhi ya wageni kutoka nje ya jiji la Munich wakaamua kujiondoa kutoka kwenye klabu ile kutokana na kuona kwamba Mabavariani ambao ndio wenye timu kiasili hawawapi nafasi ya kutosha hivyo wakaamua kuunda klabu ya FC Bayern Munich.

Baasi wageni wakachanganyikana na wazawa kiasi na kuanza kuisimamisha FC Bayern Munich ambayo ilikuja na kuwazidi wapinzani wao 1860 Munich na kuwa klabu ya kwanza kutoka Munich kubeba kombe la ligi kuu ya Ujerumani.

Lakini pamoja na kwamba Bayern ndio timu yenye mafanikio makubwa kiuchumi na kisoka lakini bado TSV 1860 Munich wanachuana kwa kuwa na mashabiki wengi na Bayern ndani ya jiji hili la Mabavariani.

Hii ndio historia fupi na utofauti wa vilabu hivi viwili.

GOLI LA SIKU: IRAQ VS SIERRA LIONE

Thursday, May 24, 2012

OFFICIAL: LLOYD NCHUNGA ABWAGA MANYANGA YANGA

LLOYD NCHUNGA BIHARAGU
C/O LLOYD ADVOCATES,
Morogoro/Bibi TIti  Mohamed Rd,7th Floor, J.K. Nyerere Pension towers
P.BOX 75111, Dar-Es- Salaam,Tanzania.


                                                                   

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUJIUZULU NAFASI YA UENYEKITI WA KLAB YA YANGA.
Ndugu wana Habari, najua kwamba taarifa hii itawafedhehesha wajumbe na wanayanga wanaotuunga mkono,hasa ukizingatia maamuzi ya pamoja ya vikao vyetu vya kamati ya utendaji vilivyopita kwamba hakuna wa kujiuzulu kati yetu mpaka tujue hatma ya mkutano mkuu ambao tulipanga ufanyike tarehe 15 Julai 2012, ukiachia mbali shinikizo la kujiuzulu linalotolewa na baadhi ya wazee na wanaojiita vijana wa klab, kwa wajumbe wa kamati ya utendaji, na hasa mimi kama mwenyekiti.
Nawashukuru wajumbe kwamba tulifanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano mzuri, na hata pale tulipotofautiana tulifanya hivyo kwa hoja na kufikia maazimio ambayo wote tulikuwa tunawajibika nayo.
Tangu tumeingia madarakani tumeweza kushirikiana na kupata mataji matatu katika kipindi cha mwaka mmoja, yaani; Ngao ya Hisani 2010, Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011, na Ubingwa wa  Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), 2011. Zaidi ni kwamba tuliuwa uteja kwa watani wetu wa jadi kila tulipokutana katika ligi ukiachia mbali mechi ya tarehe 6 Mei 2012, ambayo tulifungwa goli 5 bila, na kuleta mtafaruku mkubwa katika klab yetu.
Hali kadhalika tumeshirikiana  mpaka tumeweza kuboresha mkataba kati yetu na TBL kupitia Kilimanjaro Premium Lager, tumeingia mkataba na  kampuni ya NEDCO  kuendeleza mali zetu katika mtaa wa mafia na uwanja wetu wa KAUNDA baada ya kufikia hatua nzuri katika kupata hati miliki za maeneo yote mawili. Nafahamu kwamba kampuni hiyo iko katika hatua za mwisho za kumalizia michoro.
Hali kadhalika tuliingia mkataba wa kuzalisha na kuuza bidhaa zenye nembo yetu na hasa baada ya kufanya marekebisho yatokanayo na matakwa ya sheria kule BRELA na pia mkataba na kampuni ya NEXUS LTD, ambayo itakuwa inatutafutia wadhamini wa nje na ndani, kufanya promosheni zetu na kampeni kwa njia ya electronic kupitia mitandao mbalimbali na kukusanya data za wanachama na kusajili  wapya tukiwa na malengo ya kukusanya shilingi 300,000,000/= hadi 800,000,000/= kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu. Haya yote tuliyafanya tukilenga kujitegemea kujazia mapengo yaliyokuwa yakitokana na kutegemea ufadhili wa mtu mmoja mmoja.
Kwa ridhaa yenu tumekua tukiendelea na mazungumzo na makampuni mbali mbali kwa ajili ya udhamini na kwa sababu maalum, nitazitaja katika hati ya makabidhiano kwa kiongozi ajaye.
Aidha, tumeshirikiana katika kufanya mambo mbali mbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na sikukuu ya kuadhimisha miaka 77 ya Yanga, sikukuu za pasaka, kuchangia jamii na waliokumbwa na maafa, na kongamano la vijana lililolenga kuwaamsha vijana kuitambua nafasi yao katika Yanga ikiwa ni pamoja na kupata azimio la kuanzisha SACCOSS ya Yanga, ambapo maombi yapo kwa msajili Manispaa ya Ilala.
Haya yote nayataja ikiwa ni kuwashukuru kwa ushirikiano na ikiwezekana muweze kuyakamilisha yaliyobaki ambayo mtaona yalikuwa mazuri.
Lakini pia tulipopata matatizo tulikuwa pamoja.  Nichelee kusema tu kwamba tulisimama pamoja baada ya kujiuzulu Makamu Mwenyekiti wetu Ndugu Davis Mosha na mjumbe wetu  ndugu Seif A. Seif, Ali Mayayi, na wengineo, kwani tulifungwa na katiba.Tulisimama pamoja pia katika suala la kujiuzulu ndugu Yusuf M. Manji, aliyekuwa mdhamini mteule na mfadhili mkuu ambaye sasa ameonyesha nia ya kurudi nanyi mkaridhia mkutane naye. Awali, tulitumia kila jitihada za kumrejesha lakini ikashindikana.
Hata hivyo doa limetupata baada ya kufungwa na watani wetu goli 5 bila, ambapo kuna wanachama wanaoelewa na wasioelewa kabisa.
Ninachokiona mimi ni usaliti wa hali ya juu uliombatana na matukio mbalimbali yaliyopita na yanayoendelea hadi kujaribu kupindua uongozi wa halali wa kidemokrasia. SIWATUHUMU WACHEZAJI MOJA KWA MOJA, isipokuwa  mfululizo wa matukio wiki tatu kabla ya mchezo ule na sasa, inaonyesha kwamba kulikuwa na usaliti mkubwa ambao sisi hatukuweza kuubaini mapema.
Sioni mantiki katika hoja kwamba wachezaji walikuwa wakidai mishahara, posho n.k.  Au ati mtendaji wetu alishikiliwa Arusha kwa deni la hoteli, ndiyo  tuvune bao 5!
Kwa wanaoijua Yanga, imewahi kuwa na madeni makubwa katika Hoteli mbali mbali, mawakala wa ndege n.k, na baadhi tumeyakuta na sisi tumekuja tukayalipa. Hii imewahi kutokea kabla na wakati akiwepo mfadhili, sembuse sisi tulioachwa baki, na bado wachezaji walicheza kwa morali.
Hata hivyo, utamaduni wa kutimuana baada ya matokeo mabaya ni dhambi ambayo itatula kama hatutaiacha, kwani wenye hila na uchu wa madaraka wataendelea kutumia mbinu hiyo ili kuuondoa uongozi wa kidemokrasia.
Baada ya mapinduzi kushindikana na TFF kuonya kuhusu mapinduzi hayo, wazee kupitia msemaji wao , Mzee Akilimali wamesikika katika kipindi cha Michezo  cha Redio moja maarufu hapa nchini wakidai kwamba ni bora Yanga ishushwe daraja au kufungiwa kuliko mimi kuendelea kuongoza!
Hii imenikumbusha HEKMA ZA MFALME SELEMANI akiamulia ugomvi wa wanawake wawili waliokuwa wakigombea mtoto naye akaamuru wamgawane nusu kwa nusu. Yule mwenye mtoto kweli alimuomba Mfalme amuachie mwenzie kuliko kumkata nusu.
Kwa hekma hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu katika Uenyekiti  wa Yanga kwani ni klab ninayoipenda hata kama sio kiongozi kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba yetu.
Vile vile siko tayari kuona klab yangu ikisalitiwa au kuhujumiwa eti kwa sababu tu mimi ni kiongozi.
Natumaini kamati ya utendaji kwa pamoja na wale tuliowateua chini ya ibara ya 29(3) ya katiba ya Yanga pamoja na bodi ya wadhamini, itawaongoza wanachama mpaka kufikia mkutano mkuu kwa  mafanikio zaidi.
 Nitaendelea kuwa mwanachama mwadilifu na nitatoa mchango wangu wa hali na mali pale nitakapo hitajika na nikiwa  na uwezo wa kufanya hivyo.
YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
Wasalaam,


LLOYD NCHUNGA BIHARAGU.

Nakala kwa:-
Mama Fatma Karume,Mdhamini
Francis Kifukwe, Mdhamini
Bwana Yusuf Manji – Kwa taarifa

NI MUDA WA KULA BATA TU - CESC FABREGAS NA DEMU WAKE UFUKWENI




TANGAZO LA AROBAINI YA MOHAMED ABDALLAH BACHECHE


Familia ya marehemu MZEE ABDALLAH MOHAMMED ( MACHECHE) ,wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa mchango wenu mkubwa mlio uonyesha wakati maazishi katika shughuli nzima za kumpumnzisha mtoto wetu mpendwa"MOHAMMED ABDALLAH (BACHECHE)"
Tunapenda kuwaarifu kwenye shughuli ya AROBAINI ya mtoto wetu itakayofanyika nyumbani kwao kwa Marehemu MZEE ABDALLAH MOHAMMED (MACHECHE) Makumbusho / kijitonyama,karibu na shule ya msingi makumbusho. Tarehe 26/05/2012, Kuanzia saa saba mchana baada ya sala ya adhuhuri

Mudy Bacheche(kulia) akiwa na nduguye Mkamba Ali Othman ambaye walikuwa wakielewana sana na ndio kila mmoja bestman wa mwenzie katika harusi zao.MKAMBA alifariki wiki moja baada ya kifo cha mudy kwa kuuguliwa na mafindofindo makali ya kooni..Mudy Bacheche ambaye amewahi kuwa bingwa wa pool na Mkamba ni wapwa wa IBRAHIM KAMWE”BigRight” wenyewe wanamwita anko T.“MUNGUAZILAZE ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI” ‘ameen’

MALAWI WATUA LEO - KUWAONA DHIDI YA STARS NI BUKU 3 TU

Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kuwasili nchini leo saa 10 jioni kwa ndege ya Air Malawi kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Mechi hiyo ni kwa ajili ya kuipima nguvu Taifa Stars kabla ya mechi yake mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen.
 
Malawi itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu ambapo Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
 
Malawi ambayo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu baada ya mechi hiyo itakwenda Zanzibar ambapo Mei 28 mwaka huu itacheza na Zanzibar Heroes.
 
Makocha wa timu zote mbili Taifa Stars na The Flames kesho (Mei 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF.

ARJEN ROBBEN ALIVYOZOMEWA NA MASHABIKI WA BAYERN MUNICH

Katika mechi dhidi ya Uholanzi na Bayern Munich mchezaji wa Bayern Arjen Robben ambaye ni raia wa Uholanzi alipata utata kidogo wa kuchagua timu gani aichezee. Akiwa asubuhi amefanya mazoezi na wachezaji wenzie wa Bavarians watu wengi wakawa wanategemea jioni yake angeichezea klabu yake, lakini tulipofika uwanjani Robben alionekana kavaa jezi za timu yake ya taifa - na mashabiki wa Bayern kuona hivyo wakaanza kumzomea mchezaji huyo wakimuita mjinga kila alipogusa mpira. 

SHAFFIH DAUDA NILIPOFUATA NYAYO ZA KAKA YANGU CHARLES HILLARY

SAFARI YANGU YA KWENDA KUANGALIA MECHI YA BAYERN MUNICH NA UHOLANZI

Usiku wa kuamkia jana nikiwa na mwenyeji wangu wa hapa Ujerumani - DJ Max tulienda kuangalia mechi ya kirafiki kati ya Bayern Munich na Uholanzi. HAPA TUKIWA TUNAELEKEA UWANJA WA ALLIANZ ARENA


ALLIANZ ARENA IKIWA IMEBADILIKA BAADA YA MECHI YA CHAMPIONS LEAGUE

BAADA KUONGEZWA MKATABA - MILOVAN KUWATAJA WATAKAOACHWA NA SIMBA LEO


WAKATI mabingwa wa Soka Tanzania bara, Simba SC wakimuongezea mkataba kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Circovic  wachezaji wa timu hiyo watakaoachwa kwenye usajili msimu huu watajulikana kuanzia leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga pazia hilo la usajili litafunguliwa na kocha Milovan ambaye atapendekeza majina ya wachezaji watakaotemwa msimu huu.

Kamwaga alisema Simba ilikuwa inahitaji kukamilisha kwanza suala la mkataba mpya wa kocha Milovan aliyeiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania bara msimu huu ndipo waanze zoezi la usajili.

"Kocha wetu alikuwa na mkataba wa miezi sita ambao umemalizika hivi karibuni, leo hii (jana) mchana Kamati ya Utendaji tupo kwenye  mchakato wa kumsainisha kocha Milovan mkataba mpya.

"Baada ya kusaini mkataba huo kocha atapendekeza majina ya wachezaji watakaobaki zoezi litakaloanza kesho 'leo' alisema Kamwaga na kuongeza kwamba kocha huyo atashirikiana na benchi zima la ufundi la timu hiyo.

Kimwaga alisema wapenzi na mashabiki wa timu hiyo watarajie usajili mzuri msimu huu ambao utaiwezesha timu yao kufanya vizuri  ndani na nje ya nchi kama walivyofanya msimu huu.

NCHUNGA ASISITIZA HATOJIUZULU - AMPONDA BHINDA, AMUITA KIGEUGEU

Chairman wa Yanga anayeandamwa na shinikizo la kutakiwa kujiuzulu, Lloyd Nchunga amewaponda baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliojiondoa na kusema uamuzi wao siyo dawa ya suluhu ya mgogoro uliopo, na kwamba katiba ya klabu hiyo inampa mamlaka ya kuteua wengine kuziba nafasi hizo.

Nchunga ambaye amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari kutokana kung'ang'ania kwenye mstari wa kukataa kuachia ngazi, amesema katiba ya Yanga inatoa mamlaka ya kuchagua watu wengine kuziba nafasi za wajumbe wa kuchaguliwa waliojiuzulu, na tayari amefanya hivyo.

"Kipengele cha 29, ibara ya (3) ya Katiba ya Yanga, kinaruhusu kuteuliwa kwa watu wa kuziba nafasi za wajumbe wa kuchaguliwa wa Kamati ya Utendaji waliojiuzulu," alisema kwa kujiamini Nchunga.

Aliongeza: "Kutokana na uteuzi huo wa watu wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wajumbe wa kuchaguliwa waliojiuzulu, hakutafanyika uchaguzi mdogo. Wateule wapya tumeshawaandikia barua za kuwafahamisha.

Nchunga alisema kamati ya utendaji itawatangaza wajumbe wapya mwishoni mwa wiki hii na kuongeza: "Waliodhani kwamba kujiuzulu kwao kamati ya utendaji kungeweza kuwa kiini cha mimi pia kujiuzulu, watakuwa wameingia mlango siyo sahihi."

Alisema amegundua baadhi ya wajumbe kwenye kamati hiyo hawana msimamo na ndiyo hao ambao wamekuwa wakimshinikiza yeye kujiuzulu bila kufahamu kwamba uamuzi huo hauwezi kuwa suluhu ya mgogoro.

Amemtaja mjumbe aliyejiuzulu hivi karibuni, Mohamed Bhinda kuwa ni mmoja ya watu vigeugeu na waliokosa msimamo kutokana na kutoa kauli zisizo sahihi na zenye lengo la kupotosha ukweli.

Juzi, Bhinda alikaririwa na chombo kimoja cha habari akisema kikao cha kamati ya utendaji cha Yanga kilichokutana hoteli ya Protea ilimtaka Nchunga ajiuzulu kwa faida ya Yanga kwa vile mzani unaonyesha ndiye chanzo cha mgogoro wa Yanga.

Bhina alikwenda mbali zaidi na kusema, mwenyekiti wake baada ya kubanwa alikubali kujiuzulu muda wowote, lakini Nchunga alipinga kauli hiyo na kusema hakuna kikao kilichoitiswa akakubali kuachia ngazi.

"Bhinda ni dhaifu, kwanza aliyoyasema siyo tuliyoyazungumza, anatumika tu lakini ajue kutumika kwake anajidhalilisha, kamati ya utendaji tunakaa tena hivi karibuni tutamjadili na kumchukulia hatua kali za kinidhamu," alisema Nchunga.

Bosi Nchunga alitumia fursa ya kuzungumzia hali ilivyo Yanga kwa kuwaonya wazee wa klabu hiyo kwa kusema, angependa kuona mgogoro wa uliopo unaisha katika njia ya amani tofauti na hali inavyoonekana sasa.

"Hao wazee kama wameshindwa kunipindua kikatiba watulie, wasinione nimekaa kimya wakaniona mjinga, nawaheshimu ndiyo maana nimekaa kimya. Kama wanataka tuchafuane, mimi pia naweza kufanya hivyo.

"Ninawaheshimu wazee hawa, nisingependa kuingia nao kwenye matatizo, nawafahamu wote na kila mmoja anavyoishi. Nawaomba wapokee heshima yangu, wasinilazimishe kuivunja," alisema.

Kuhusu kuimarika shinikizo la kutakiwa kujiuzulu, Nchunga alisema: "Msimamo wangu uko wazi, nilishasema na narudia tena, haipo sababu ya kujiuzulu kwa shinikizo la wachache, lakini kama binadamu nitaeleza kila kitu Ijumaa."

THOMAS ULIMWENGU AUMIA KIFUNDO CHA MGUU KAMBINI NA STARS

Ulimwengu katika uzi wa Brazil

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu naye kuumia kifundo cha mguu.
Kuumia kwa Ulimwengu anayekipga katika klabu ya TP Mazembe ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunafa timu hiyo kufikisha majeruhi wawili ambapo jana, kiungo wake Nurdin Bakari alichanika nyama za paja hali itakayomlazimu kukaa nje ya dimba kwa siku saba.
Daktari wa Stars, Mwanandi Mwankemwa alisema Ulimwengu alipata maumivu hayo wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na maumivu hayo, Ulimwengu naye ataukjosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen akisaidiwa na Mzalendo Sylvestre Marsh imepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma jijini  Dar es Salaam ikijiandaa mechi yake  ya mchujo kufuzu Kombe la Dunia  hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa  Abidjan  Juni 2 mwaka huu. 

SOURCE: DINA ISMAIL (http/mamapipiro.blogspot.com)

JUMA KASEJA NAHODHA MPYA TAIFA STARS



NDOTO za mlinda mlango namba moja Tanzania, Juma Kaseja kuwa Nahodha wa timu ya taifa, zimetimia baada ya benchi la ufundi la Taifa Stars, kumteua kipa huyo wa Simba SC kushika wadhifa huo.
Maofisa wa benchi la ufundi la Stars, chini ya kocha Kim Poulsen, Wasaidizi wake, Sylvester Marsh na Juma Pondamali kwa pamoja na Meneja Leopold Mukebezi, baada ya kikao chao wamemteua rasmi Kaseja kuwa Nahodha wa timu hiyo, akirithi mikoba ya beki wa kulia, Nsajigwa Shadrack ambaye ameachwa kwenye kikosi hicho.
Hata hivyo, haijafahamika kama Kaseja atakuwa Nahodha wa kudumu wau muda wa Stars, kwa sababu chini ya Jan Poulsen, aliyekuwa kocha wa Taifa Stars kabla ya Kim, Shaaban Nditi ndiye aliyekuwa anapewa mikoba ya Unahodha Nsajigwa anapokuwa nje ya kikosi.
SOURCE:http://bongostaz.blogspot.com/

MISS KIGAMBONI NI HATARI MWAKA HUU - KUFANYIKA JUNI 15


MAZOEZI kwa ajili ya kushiriki shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' yameshaanza mapema wiki hii imefahamika. Shindano hilo limepangwa kufanyika ifikapo Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam. Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo tayari wameshaanza mazoezi kwenye ukumbi wa Break Point ulioko Posta jirani na Club Billicanas. Alisema kuwa bado milango iko wazi kwa warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanakaribishwa kushiriki kuwania taji hilo. Aliongeza kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu. "Kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa katika kufanya mchakato wa kupata warembo wenye sifa ili waweze kwenda kuiwakilisha vyema Kigamboni katika mashindano ya Kanda," alisema Somoe. Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen Kweka. Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003. "Bado tunakaribisha wadau wa sanaa ya urembo kutudhamini shindano hili, tunaamini uwepo wao ndio utafanikisha ubora na hadhi ya shindano letu mwaka huu kama tulivyodhamiria," aliongeza. Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF. Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.

Wednesday, May 23, 2012

SIMBA KUIPA FAMILIA YA MAFISANGO FEDHA NYINGI - KWA MARA YA KWANZA - KUWEKA HISTORIA YA KUTEMBEZA KOMBE MITAANI

 
Baada ya kutoka taarifa za kwamba wiki hi klabu ya Simba itafanya sherehe za kushangilia ushindi wa kombe la VPL baadhi ya mashabiki tofauti wamekuwa wakitoa maoni hasi juu ya uamuzi wa klabu hiyo kufanya hivyo wakati ikiwa imefiwa na mchezaji wao Patrick Mafisango wiki iliyopia tu. Hivyo leo kupitia mtandao wa Facebook msemaji wa simba alijibu maoni haoa kama ifuatavyo.

Ezekiel Kamwaga - Msemaji wa Simba
Nimesoma sana maoni ya watu kuhusu show ya Simba DarLive.... Nakubaliana na karibu wote waliotoa haki yao. Kwanza mimi ni nani au Simba ni nani hadi isikubaliane na maoni ya watu? Lakini ningependa kusema machache kuhusu maoni ya watu.... Mosi, watu wa mpira wanajua kwamba kuna kitu kinaitwa logical reason na footballing reasons. Kwamba kuna mahali inabidi soka ifanywe soka na logic ibaki kuwa logic. Ndiyo maana kuna msemo kwamba Common Sense Is Not Always Common. Nitafafanua....Alipokufa uwanjani Marc Vivien Foe miaka kumi iliyopita, pambano liliendelea kama kawaida.... It was not logical reason, it was footballing reason.... Mara baada ya kifo cha mchezaji Antonio Puerta wa Celta Vigo mwaka 2007, siku tatu baadaye Celta ilicheza na AC Milan, na ikatangazwa kuwa ni kwa heshima ya Puerta, hata kama kuna wachezajiu walishindwa kucheza.... Footballing reason... Maisha si mali ya binadamu.... Hebu tuseme hivi, Kama Simba itasubiri hadi arobaini ya Mafisango ipite ndipo ifanye sherehe na kwa bahati tukapata msiba mwingine siku ya 35, je, itabidi tuahirishe tena kwa siku nyingine 40? Au Taifa likapata tukio ambalo litasababisha tuingie kwenye maombolezo, au Mungu apishilie mbali, itokee kitu kinaitwa Force Majeure kwa lugha ya kisheria (an act of God) kama vile tsunami au tetemeko la ardhi, tutafanyaje? Tutaahirisha tena? Kwa wanaomjua vema Mafisango, kama angeulizwa huko aliko (Mungu amweke mahali pema peponi) yeye angekuwa wa kwanza kuturuhusu tufanye sherehe yetu ya ubingwa.

Nimebaini kwamba wako watu ambao wanataka kuonyesha kwamba Simba haina huruma au haijaguswa kabisa na msiba wa Mafisango kuliko wao. Baadhi yetu tumeishi na Mafisango, tumelala naye, tumefanya naye mazoezi na tunamjua kuliko baadhi ya watu ambao wametoa comments... Sasa najiuliza, hivi mwenye uchungu na Mafisango ni nani haswa? Yule ambaye aliamka saa kumi alfajiri na kwenda Muhimbili kuhakikisha amehifadhiwa vizuri na kumuandalia msiba na mazishi ya kitaifa au yule ambaye analalamika tu kila kukicha? Simba ina uchungu sana na Mafisango lakini It is a football club na lazima maamuzi yake yana base kwenye football na si common sense au mila za kiafrika.

Kufanya sherehe kwenye mazingira haya ni kumuenzi pia Mafisango. Timu inachukuaje ubingwa na kukaa tu kana kwamba hakuna kilichofanyika? Tusisahau kwamba kinachofanyika mwaka huu ni kitu kipya... Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 75 ya Simba kufanyika Bus Tour.

Hii ni kama Pilot Project.... We can only get better....Mwakani, tutachukua on board yale mapungufu ya mwaka huu na kufanya kitu kizuri zaidi.... Lakini, mnaupondaje uongozi kwa kujaribu kufanya kitu kizuri... Mbona mwaka juzi hakuna miongoni mwenu aliyetoa wazo la Bus Tour? Kwanini Watanzania tumekuwa na tabia ya kutaka kuponda tu kila kitu badala ya kutoa maoni ya kurekebisha ili twende vizuri.

Kuna mtu hapa anaitwa Mohamed Mashango, naona yeye anajua kuponda tu....Anafikia hatua ya kulinganisha Simba na timu ya mtaani kwake ya Kitintale.... Haya ni matusi kwa Simba, lakini ndiyo aina ya washabiki wa Simba tulionao !

Simba haijui kufanya sherehe? Nani anafanyaga Simba Day kila mwaka? Ni klabu gani nyingine ina utaratibu wa kufanya kitu kama Simba Day katika ukanda huu wa Afrika Mashariki? Kuna klabu gani imewahi kufanya party ya kiwango cha juu hapa Tanzania kama wakati tunazindua Simba TV? Mashango anapata wapi ujasiri wa kuilinganisha Simba na Kitintale? Glorie namuonaga uwanjani na hata mazoezini wakati mwingine lakini sijui kama huyu Mashango anakuja hata mpirani.... Au anaangaliaga ya Kitintale?

Niwafahamishe pia kwamba mpango wa kusaidia familia ya Mafisango upo...Iwe kwa kuandaa mechi au namna nyingine yeyote.... Muhimu zaidi ni kwamba Simba itafiwa tena na tena. Na imewahi kufiwa huko nyuma pia.... Cha msingi ni kwa klabu kuweka utaratibu wa kusaidia familia za wachezaji wake wote katika siku zijazo... Hili ndilo klabu inalolipanga kwa sasa.... Lakini naomba niwaambie kitu kimoja, familia ya Mafisango itapewa fedha nyingi na Simba.... Kiasi ambacho hakuna klabu yoyote ya Tanzania au Afrika Mashariki imewahi kukitoa kwa familia ya mchezaji aliyefariki.

You can take my word on that..... Niseme mwishoni kwamba inawezekana ukumbi wa DarLive si mzuri, yes, we can take that on board.... Inawezekana washabiki hawajapenda kuweka viingilio, we can take that on board..... Pengine watu wangependa sherehe hizo ziandane na utoaji tuzo kwa wachezaji, hilo pia ni wazo zuri. Ninalichukua.

Ningetaraji michango ya namna hiyo kwa Wana Simba.... Si kusema hatujui kupanga sherehe, hatuna uchungu na Mafisango au tuna tamaa ya fedha.....

Ningeomba tushiriki kwenye sherehe za mwaka huu na tujiandae kwa sherehe nzuri zaidi, za kiwango zaidi na zenye ubora zaidi msimu ujao.... Hiyo ndiyo Simba.

HIVI NI BAADHI YA BIASHARA ZINAZOIFANYA BAYERN MUNICH KUWA KLABU YA PILI KWA THAMANI KUBWA DUNIANI

NAMNA FC BAYERN MUNICH WANAVYOTENGENEZA FEDHA KUPITIA BRAND YAO - SIMBA, YANGA, AZAM JIFUNZENI


Kama nilivyoripoti jana kwamba nilifanikiwa kupata nafasi ya kufanya ziara kwenye makao makuu ya klabu ya Bayern Munich. Pamoja na kufanikiwa kutembelea sehemu mbalimbali zilizo ndani ya jengo la makao makuu ya timu hiyo, ikiwemo uwanja wa mazoezi, sehemu ya kuifadhia makombe waliyotwaa pamoja na kutembelea kwenye duka kubwa ambalo linauza vifaa tofauti vinavyotengenezwa kwa kutumia brand ya Bayern Munich.


Pamoja na kujifunza vitu vingi kwenye ziara yangu ya jana, lakini kubwa zaidi ni jinsi FC Bayern Munich inavyoweza kujiendesha kibiashara na kuweza kutengeneza pesa nyingi kupitia bidhaa tofauti wanazotengeneza na kuziuza.


FC Bayern kupitia brand yao wanatengeneza aina zote za mavazi kuanzia Kofia, mashati, soksi, fulana, skafu, vitambaa vya jasho, suruali za aina zote, viatu vya aina zote kuanzia vya michezo mpaka vya kawaida yaani kifupi kila aina mavazi wanatengeneza. Pia wanatengeneza vitu kama vifaa vya shule madaftari, pen za wino na penseli, wanatengeneza vifaa vya kuchezea kwa watoto kama vile midoli pamoja magari  ya kuchezea.


Jamaa pia hawajaawatupa masista duu - wamewatengenezea handbags, vitopu, nguo na viatu vikali vya kisasa maalum kwa wadada. Pia wamama wa nyumbani nao wametengenezewa vifaa vya kupikia kama vile majiko ya gesi, sufuria mpaka glass na vikombe tofauti vyote vikiwa na nembo ya FC Bayern Munich.


Kwa utafiti nilioufanya nimegundua klabu hii inategemea kwa kiasi kikubwa mapato yatokanayo na bidhaa wanazotengeneza kuweza kujiendesha hata kabla hawajayagusa mapato mengine yatokanayo na biashara nyingine wanazojihusisha nazo. Mamilioni ya EURO yanaingia kwenye accounts za klabu hii  kupitia biashara hii kwa sababu mamailioni ya washabiki wa Bayern Munich hapa Ujerumani na duniani kote wanaisapoti timu yao kwa kununua bidha mbalimbali zinatengenzwa na timu yao. Kwa mfano shabiki ambaye ni baba atamnunulia mwanae kuanzia vifaa vya shule mpaka midoli ya kuchezea yenye nembo ya Bayern katika kuhakikisha anaichangia timu yake kwa kununua bidhaa zao. Hii pia inaenda hivyo hivyo kwa watu wa rika na jinsia tofauti ambao ni wapenzi wa Bayern  mwisho wa siku timu yao inakuwa na uwezo mkubwa wa kifedha ambao unawapa mabavu ya kusajili mchezaji yoyote wanayemtaka kwa kuwa wanakuwa na fungu la maana la kununua na kuwalipa wachezaji. Hivyo kwa namna hiyo timu inapata maendeleo.

Hili ni somo kubwa kwa vilabu vyetu vikongwe Simba na Yanga, ambavyo kwa utaifiti mdogo nilioufanya ni moja kati ya vilabu vichache vyenye washabiki wengi barani Afrika, lakini vinaoongoza kwa umaskini na migogoro. Havina mipango endelevu na ndio maana kila siku vinazidi kuwa omba omba kwa matajiri ambao ni washabiki wa vilabu hivyo. 
Kwa mfano klabu ya Yanga ambayo kwa miaka kwa karibuni imekuwa katika mikono ya tajiri Yusuph MANJI / ebu jiulize kama wangekuwa wamemtumia Manji kuwatafutia mikopo ambayo wangeitumia kutengeneza vitu au bidhaa kama za Bayern Munich na kuviuza kwa mamilioni ya washabiki wao leo hii klabu hii ingekuwa tajiri kiasi gani? Hii pia hata kwa Simba inawezekana na kuweza kujipnga na kuwa na seriousness kwenye mipango yao. Naomba viongozi wa vilabu hivi waangalie mafanikio ya Bayern yaliyotokana na mipango thabiti na wachukue kama Challenge ili kuweza kutoka mfumo wa kimaskini walionao sasa na kuweza kwenda mbele kwa mfumo wa kisasa kama wenzetu huku nje. Endapo vilabu hivi vitaondokana na mfumo wa kizamani na kuiga vitu wanavyofanya wenzetu kwa hakika vilabu vitatengeneza fedha nyingi sana ambazo kama zikitumika vizuri zitaisadia kuziletea maendeleo vilabu hivi pamoja na kuendeleza soka la Tanzania kiujumla. 


Kutoka Munich Ujerumani Nwasilisha.

AZAM KWENYE MICHUANO YA KAGAME KWA MARA YA KWANZA MWAKA HUU

WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na timu tatu, nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo, yanaendelea vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na watatangazwa katika Mkutano maalum hivi karibuni.

BAADA YA BOBAN KUANGUKA NA KUZIMIA - DAKTARI ASHAURI WACHEZAJI WA SIMBA KUPEWA TIBA YA SAIKOLOJIA

Baada ya Haruna Moshi kuzimia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinshasa juzi,  Daktari wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars', Mwanandi Mwankemwa amesema wanawapa ushauri wa karibu wachezaji wa Simba waliopo katika timu hiyo ili warejee katika hali zao za kawaida.

Haruna 'Boban' presha yake ilishuka ghafla Jumatatu asubuhi alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kinshasa na kulazimika kupatiwa huduma  haraka na daktari wa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa 1:30.

Daktari aliyemtibu, alimpa kahawa na chumvi na alimshauri asifikirie mambo mengi wala kufanya kazi ngumu kwa vile presha yake itashuka na kugharimu maisha yake.

Dk Mwankemwa alisema tukio la kifo cha ghafla cha Patrick Mafisango haliwezi kusahaulika mapema kwa wachezaji wenzake, na kwa sababu hiyo wanahitaji uangalizi wa karibu kiushauri ili kuhakikisha wanarejea kwenye hali yao ya kawaida.

Alisema kuna athari kubwa kwa mchezaji kucheza uwanjani huku akikosa utulivu wa akili kichwani kutokana na msongo wa mawazo juu ya tukio lolote la kusikitisha linaloweza kumgusa kwa karibu.

"Ni rahisi hata mchezaji kuumia anapocheza uwanjani, huku akili yake ikijaa kumbukumbu ya tukio baya kama ajali iliyosababisha kifo cha Mafisango," alisema Mwankemwa.

Daktari huyo alisema zaidi kuwa, ili mchezaji aweze kushiriki vizuri kwenye mchezo ni lazima aingie uwanjani akili yake ikiwa imetulia bila kuwa na msongo wa mawazo kwa jambo lolote lile.

"Kwa maana hiyo, tunachofanya kwa sasa ni kuwapa ushauri kila wakati ili kuwaondoa katika hali, tunatarajia hali itakuwa nzuri baada ya siku kadhaa, ingawa mwisho wa siku mwalimu wao (Kocha Kim Poulsen) ataamua ni wachezaji gani anaweza kuwatumia," alisema Mwankemwa ambaye pia ni daktari wa timu ya Azam FC.

Kauli ya kocha huyo imekuja siku chache tangu kiungo wa Simba, Moshi 'Boban' aliyeonekana kuguswa zaidi na kifo cha Mafisango kupata matatizo ya kiafya muda mfupi baada ya kushiriki mazishi Jumapili iliyopita.

Mchezaji huyo wa Simba tangu alipopokea taarifa ya kifo cha Mafisango alikuwa hawezi kuzungumza lolote zaidi ya kububujikwa na machozi ya uchungu, jambo ambalo linaweza pia kumwathiri kiuchezaji.

Boban ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kocha Kim Poulsen kuunda kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa ugenini dhidi ya Ivory Coast kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

SIMBA NA APR WAAMUA KUICHANGIA FAMILIA YA MAREHEMU PATRICK MAFISANGO


KLABU ya APR FC na Shirikisho la Soka la Rwanda(Ferwafa), wameandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba kwa lengo la kupata fedha za kuchangia watoto na familia ya Marehemu Patrick Mafisango.

Mafisango aliyezikwa Jumapili eneo la Kinkole, nje ya Jiji la Kinshasa baada ya kufariki kwa ajali ya gari Dar es Salaam, ameacha watoto wadogo watatu, wanaume wawili Crespo na David pamoja na binti Patrina.

Hali ya familia mchezaji huyo ambae hana wazazi na alilelewa na shemeji yake Papaa Pierre tangu akiwa mdogo, si nzuri kiuchumi ingawa waligharamia sehemu kubwa ya mazishi ya ndugu yao.

Makamu Mwenyekiti wa Ferwafa, Raoul Gisanura na Katibu Mkuu wa APR, Adolphe Kalisa wameiambia Mwananchi msibani jijini Kinshasa kwamba wako tayari kucheza mechi hiyo muda wowote kabla ya kuanza kwa kombe la Kagame mwezi ujao.

Gisanura alisema; "Ni jambo zuri sana kuichangia hii familia ili hawa watoto wafaidi matunda ya baba yao na waende shule, kwavile hali halisi inaonyesha kwamba ni mzigo mkubwa kwa familia iliyoachwa pamoja na mama zao."

Kalisa alisema; "Simba na APR zimefaidika sana na Mafisango kuliko watu wa Kinshasa hivyo ni wajibu wetu kufanya kitu kama fadhila kusaidia hii familia, sisi tuko tayari kucheza na Simba lakini ingekuwa vizuri zaidi hiyo mechi ikaandaliwa na kampuni huyu ambayo si klabu hizo mbili wala Shirikisho."

Mwakilishi wa Simba aliyekuwa jijini hapa, Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi'  alipoambiwa na Mwananchi kuhusiana na hilo alisema halina matatizo kwani ni kiasi cha kujadiliana tu na kuweka mambo kwenye mpango na akaahidi kufikisha kwa uongozi wa juu. 

source: www.mwananchi.co.tz

NIMETOKA KUSHUHUDIA BAYERN MUNICH WAKIIFUNGA UHOLANZI 3-2

Usiku wa kuamkia leo nilienda uwanja wa Allianz Arena kuangalia mechi ya kirafiki kati ya FC Bayern Munich na timu ya taifa ya Uholanzi - mechi imeisha kwa Bayern kuibuka na ushindi wa 3-2.


Hii ndio ilikuwa tiketi yangu ya kuingia uwanjani kuangalia mechi hiyo.


Bayern Munich 3 - 2 Netherlands footyroom.com by Futbol2101

PHOTOS: ZIARA YANGU KWENYE MAKAO MAKUU YA BAYERN MUNICH

Leo nimefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya klabu ya Bayern Munich hapa Ujerumani. Ni ziara ambayo ilikuwa na lengo la kuweza kupata kujifunza vitu zaidi jinsi kalbu hii inavyoendeshwa pamoja na kuweza kuona namna mazingira ya klabu hii kubwa duniani yalivyo. Kiukweli wenzetu wameendelea sana, kwa sababu wameweka umakini mkubwa katika kuziendesha klabu zao tofauti na nyumbani. Bayern Munich kupitia brand yao ya klabu yao wanatengeneza kila aina ya merchandise kuanzia mavazi mpaka vifaa vya michezo na vya majumbani kupitia logo ya klabu hiyo, na kupitia biashara hiyo hizo ndio maana haishangazi kuiona klabu hii ikiwa ndio tajiri zaidi hapa Ujerumani na pia ikiwa imetajwa kama klabu ya pili kwa thamani kubwa dunaiani baada ya Manchester United. Kwa mengi zaidi endelea kutembelea hapa,
Klabu hii pia ina mkataba wa kampuni ya magari ya AUDI - na kupitia mkataba huo wachezaji ana watumishi pamoja na watendaji wa klabu hii wote wanatumia magari ya kampuni hii. Hili hapa juu ni gari la mchezaji David Alaba ambaye hapa alikuwa akiondoka baada ya kuisha kwa mazoezi ya timu hiyo.

Hili ni gari la nahodha Philip Lahm.
Huu ndio mchuma wa Mario Gomez ukiwa umepaki nje ya jengo la makao makuu ya Bayern Munich.
Nikiwa nimesimama nje ya jengo la FC Bayern Munich pamoja baadhi ya mashabiki wa timu hiyo na walinzi wa makao makuu ya The Bavarians.
Dauda nikiutazama mchuma wa Striker Mario Gomez
Bwana Frank Ribery akiondoka kwenye gari lake.
Bidhaa zinazotengenezwa kwa nembo ya Bayern Munich na kuingizia klabu hii fedha nyingi sana. Haya ni majiko ya gesi.

Hizi ni glassi za kunywea pombe ambazo zote zimetengenezwa kwa nembo ya FC Bayern Munich.

Hapa nikiwa kwenye chumba cha kuifadhia makombe ya FC Bayern Munich.