Search This Blog

Wednesday, May 23, 2012

AZAM KWENYE MICHUANO YA KAGAME KWA MARA YA KWANZA MWAKA HUU

WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na timu tatu, nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo, yanaendelea vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na watatangazwa katika Mkutano maalum hivi karibuni.

1 comment:

  1. Kushiriki kwa Azam Fc mashindano haya ni muhimu sana kwa soka letu nchini kwani Yanga na simba zinatakiwa zipate changamoto kila eneo kuanzia uwanjani hata nje ya uwanja. Kwa jicho jema ninawaona Azam kama ujio mzuri kwa soka letu kwani Hawa wawili hawa(Yanga na Simba) hawalitendei haki soka letu....
    Umetoa makala hapo toka Munich jinsi inavyotengeneza pesa Hata sie tunaweza sasa nini tatizo kwa vilabu hivi viwili wakati vina viongozi tena wanaijiita wasomi wazuri ? Karibu sana Azam Tunakuhitaji zaidi ya wewe unavyotuhitaji Hebu onyesha ujio wako sio wa kubahatisha Cheza mpira

    ReplyDelete