Search This Blog

Sunday, March 9, 2014

LIVE SCORE: AL AHLY 1 - 0 YANGA (Penati 4-3) AL AHLY WANAPITA - YANGA WANATOKA



Al Ahly wanapata penati 4 - 3 Young Africans
Waliopata Yanga Didier, Canavaro, Okwi huku waliokosa ni Oscar, Bahanuzi na Twite.
Al Ahly wanafuzu hatua ya 16 bora
MIKWAJU YA PENATI

Al Ahly Wamepata penati 4 - Waarab wanapita 

YANGA Yanga wamepata penati 3  

Mpira umemalizika, Al Ahly 1 - 0 Young Africans
Aggrigate 1-1
Kinafuata penati

Dk 90 zimekamilika na refa anaongeza dakika 5 za nyongeza

Domayo alikuwa na nafasi nzuri ya kuisawazishia Yanga lakini anakosa - dk 89

Dk 85 Al Ahly 1 - 0 Yanga

Goli limewaamsha zaidi Al Ahly sasa wanalishambulia zaidi lango la Yanga ambao wapo nyuma wakilinda goli.  Dakika 78

Dakika ya 70, Al Ahly wanapata bao la kwanza

Dk 67 Al Ahly wanapata kona lakini Yanga wanaokoa

Chuji anaiingia kuchukua nafasi ya Ngasa,

Dk 54 Yanga wanakosa bao la wazi, Simon Msuva anakosa umakini katika lango la maadui

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Al Ahly 0 - 0 Young Africans

Mpira ni mapumziko Yanga 0-0 Al Ahly

Ddk 40: Waarab wapo golini kwa Yana kwa muda mwingi, huku Yanga wakifanya mashambulizi ya kushtukiza, mpira bado bila bila

k 35 Cannavaro amepewa kadi ya njano, faulo inapigwa nje ya eneo la hatari la Yanga lakini golikipa Dida anadaka.

8 comments:

  1. watu wanaweza kuiangalia live hiyo mechi hapa www.nilesports.tv

    ReplyDelete
  2. Safi sana kaka kazi nzuri

    ReplyDelete
  3. Mtoto halali na pesa

    ReplyDelete
  4. KWELI YANGA NI YEBOYEBO JUICE!!! SASA TULIVYOSEMA KAMOJA HAKATOSHI WAKASEMA KINATOSHA TUTAWASHAMBULIA SANA WAARABU MATOKEO YAKE WAMEKWENDA KUPAKI GARI NA KUWAKARIBISHA WAARABU KUWEKA KAMBI KWENYE GOLI LAO! MATOKEO NDO HAYO WAMEKUFA HALAFU WASWAHILI UTASIKIA "YAMGA YAFA KIUME"
    KUFA KUFA TU HAKUNA KUFA KIUME WALA KUFA VIZURI. HAYA NJOONI TUENDELEE KUGOMBEA MILIONI AROBAINI ZA VODA!! NA TIMU TUMEANDAA KWA MILIONI MIA NNE!! HII NDO BONGO BWANA.!! ILA KIDOGO TU MNGEKUWA KAMA SIMBA!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi simba ilipocheza kwa Mara ya mwisho na timu chovu zaidi toka misri(Harras al Hadood) tena kwenye uwanja huo huo aliochezea yanga juzi matokeo yalikuwaje vile filipo?

      Delete
  5. MUHIMU KUISOMA NA KUELEWA BROO SHAFII NA WATANZANIA WOTE

    Nikiwa kama shabiki mkubwa wa soka ila mwenye upeo mdogo kuliko walio ibeza Yanga
    Napenda kuipongeza Yanga na kuipa pole kwa kutopewa sapoti na taifa lao
    Maana nimefananisha hii na mtoto afanyae mazuri shuleni lakini apewi hata mkono wa hongera na mzazi wake
    Ukweli inauma sana
    Sijasomea uchambuzi wa soka ila nachambua kutokana ninavyo uelewa

    Ushabiki upo
    Fitna zipo
    Ila hivyo vyote vinatokea kutokana na mambo yafuatayo

    Ushabiki- ni pale timu A inafanya vizuri katika nchi alafu timu B ambayo inafanya vizuri pia. Wanachuana kuchukua ubingwa, basi suala la ushabiki linatokea hata, mbinu za tofauti na ndani ya uwanja zina ibuka
    Kwani mpira ni suala lihitajio mafanikio tu-.
    Hakuna club isiotaka mafanikio ndiyo maan hata mchezaji huwa anahitaji kupewa amasa tu na si vinginevyo.
    Hapo juu nimesema mpira ni suala la mafanikio tu kwa sababu ambayo ntaiweka katika ficho
    Tunasema mpira una matokeo 3
    1:kushinda
    2;kudroo
    3:kufungwa

    Shabiki gani anapenda kufungwa au droo???

    Swali
    Watanzania wengi ni wana kupenda michezo au wana michezo!!

    Muhimu::: kama unawakilishwa wewe shabiki unawakilishwa taifa lako
    Linawakilishwa ligi
    Wanawakilishwa wachezaji wa timu yako
    unachukia nini timu sasa ikiwa hili jambo la manufaa kwako
    Swali;;
    Je ulibeza yanga ili muicheke!!!!
    Je umeibeza Yanga ili ligi letu lisiwe maharufu!!!!
    Je umeibeza Yanga ili tuwe sawa tusizidiane!!
    (Tuwe kama darasa lenye kutoa kumi mbovu tu)
    Au ulibeza Yanga ili itoke timu yako ipite??
    (Maana kocha wa newcastle aliombea chelsea mabaya ili yeye ashiriki uefa maana alikuwa nafasi ya nne na chelsea alikuwa anaelekea kutwaa taji sasa angeingingia kama bingwa, na hii ndiyo ikamfanya kocha wa newcastl aombe mabaya japo hakufanikiwa.)

    Fitina- fitina ni sehem ya mchezo
    Ila fitina tuakikishe tunajua kuitumia
    Tukicheza wenyew kwa wenyew tuwekeane fitina
    Ila tukicheza gem za kitaifa tuwawekee wao wageni fitina
    Kwanini tuseme ukimfuata hutoki!!
    Badala ya waharabu kusema ukimfuata mtanzania hutoki!!

    Waharabu wana umoja wanapeana mbinu ili wawakilishe mataifa yao
    Di Mateo kamuangusha Barca kwa mbinu za Mourinho nan asiye jua hilo!!!!
    Hivyo ndiyo soka lilivyo

    VIONGOZI TUAMKE TUELIMISHE MASHABIKI WA TIMU ZETU.

    Utajiuliza mimi ni shabiki wa timu gani
    Mimi naipenda
    Yanga
    Simba
    Azam

    Namshabikia
    Niyonzima na Ngassa
    Tambwe na Baba Ubaya
    Kipre na Mwaikimba

    Ila mimi ni shabiki wa
    Abajalo
    African sports
    Mwanalugali

    Hery Inocent
    88.5 kibaha

    TUBAKI NJIA KUU

    ReplyDelete
  6. Maandalizi ya Yanga sio kwa ajili ya milioni 40 za VPL,haya ni maandalizi kwa ajili ya msimu mzima ukijumuisha mechi za ligi na za kimataifa,ndio maana unaona timu kama Chelsea,Real Madrid na Man City zinatumia fedha nyingi kuimarisha vikosi vyao hata kama hazichukui ubingwa.Nafikiri aliyeponda gharama za maandalizi ya Yanga hana tofauti na wale wanaong'oa viti pale uwanja wa Taifa na inawezekana ni mmoja wao

    ReplyDelete
  7. Hivi ile timu ya Tanzania ambayo washabiki wake wamezoea kung'oa viti uwanja wa taifa lini na yenyewe itashiriki mechi za kimataifa ili wawaone wenzao walivyo wastaarabu?wao kila mwaka wanasubiri mtani jembe ndio mechi zao za kimataifa ambapo wanaweka kambi Zanzibar kwa ajili ya mechi moja tu ya Bonnza

    ReplyDelete