Dk 90+5 FULL TIME! Taifa Stars 0-1 Uganda
Dk 90 mpira umeongezwa dakika 5. Taifa Stars 0-1 Uganda
Dk 87 Kiungo wa Uganda Kalanda anaumia na wakati huohuo Uganda inapata kona.
Dk 84 Iguma Dennis anamchezea faulo Mrisho Ngassa. Aggrey Morris anapiga faulo juu ya lango la Uganda. Taifa Stars 0-1 Uganda
Dk 81 YELLOW CARD! Majegwa Brian wa Uganda anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kubishana na mwamuzi akipinga filimbi ya kumchezea faulo Bocco.
Dakika 79: Amri Kiemba anapoteza nafasi ya wazi ya kusawazisha akiwa amebaki yeye na mlinda lango
Dk 79 Kelvin Yondani wa Taifa Stars anaokoa mpira wa hatari uliokuwa unaelekea katika lango la timu yale na mpira unakuwa kona ambayo inapigwa kisha inaokolewa na mabeki wa Taifa Stars.
Dk 76 Mchezo unaendelea na tayari wachezaji wawili wa Taifa Stars ambao ni Athuman Idd Chuji na Khamis Mcha wanapasha misuli moto.
Dk 75 Kabugo Savio wa Uganda anagalagala chini baada ya kuumia na mwamuzi anasimamisha mchezo ili Kabugo atibiwe.
Dk 74. SUB; Uganda inafanya mabadiliko anatoka Edema Patrick anaingia Ntege Ivan
Dk 71 Ngassa anaisumbua ngome ya Uganda lakini David Luhende anashindwa kuuwahi mpira anaopigiwa na Ngassa.
Dk 63 SUB; Taifa Stars inafanya mabadiliko ametoka Mwinyi Kazimoto ameingia Haruna Chanongo.
Dk 56 Mpira unapasuka baada ya Bocco kupiga mpira na beki wa Uganda akataka kuuzuia.
Dk 54 timu zinashambuliana kwa zamu. Kiungo cha Taifa Stars kinazidi kupwaya.
Dk 46 GOOOOOO....! Iguma Dennis anaipatia Uganda bao la kwanza! Taifa Stars 0-1 Uganda
Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA
Dk 45 + 2 HALF TIME! Taifa Stars 0-0 Uganda.
Dk 43 Uganda wanakosa bao la wazi baada ya kuichambua ngome ya Taifa Stars lakini kipa Juma Kaseja anaudaka mpira uliopigwa na Kalanda.
Dk 41 Aggrey Morris anamchezea rafu Kalanda Frank.
Dk 38 Taifa Stars inapata kona. Kona inapigwa na inaokolewa na mabeki wa Uganda lakini kipa wa Uganda Muwonge Hamza anaumia na mpira unasimama kwa muda.
Dk 37 Mpande Joseph wa Uganda anakosa bao la wazi akishindwa kuunga pasi ya Kalanda Frank.
Dk 36 Uganda inapata kona! Inapigwa lakini Taifa Stars wanaokoa.
Dk 33 Aggrey Morris anapiga faulo safi inayotoka nje kidogo ya lango la Uganda.
Dk 32 Said Kyeyune wa Uganda amemchezea rafu Mwinyi Kazimoto.
Dk 31 YELLOW CARD! Wadada Nico wa Uganda anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Ngassa.
Dk 27 Bocco anachezewa faulo na Kabugo Savio.
Dk 24 Kiungo wa Taifa Stars Amri Kiemba anaonekana amechoka sana na anashindwa kucheza katika kiwango chake cha siku zote.Swaumu inaweza ikawa sababu.
Dk 22 Mrisho Ngassa anaiwahi pasi nzuri ya Mwinyi Kazimoto na kupiga shuti kali langoni kwa Uganda lakini mpira unatoka nje.
Dk 20 Bocco anakosa mabao mawili ya wazi katika lango la Uganda baada ya kukosa umakini. Taifa Stars 0-0 Uganda
Dk 19 Aggrey Morris wa Taifa Stars anafanyiwa madhambi na Edema Patrick
.Dk 16 SUB: Uganda wanafanya mabadiliko ametoka Odur Tonny ameingia Kalanda Frank.
Dk 15 Viungo wa Taifa Stars wanakosa umakini mbele ya wenzao wa Uganda huku wakipoteza pasi nyingi.
Dk 13 Uganda wanatawala mpira hasa katika kiungo.
Dk 11: Odur Tonny wa Uganda ameumia na mpira unasimama kwa muda ili atibiwe. Odur ameumia nyonga na anaomba kutoka nje.
DK 5: Timu bado zinaendelea kushambuliana zamu kwa zamu.
DK 1: Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa na timu zikicheza mchezo wa kusomana taratibu kiasi.
VIKOSI VINAVYOANZA LEO
Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakari 'Sure Boy', John Bocco, Mrisho Ngassa na Amri Kiemba.
DK 1: Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa na timu zikicheza mchezo wa kusomana taratibu kiasi.
VIKOSI VINAVYOANZA LEO
Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakari 'Sure Boy', John Bocco, Mrisho Ngassa na Amri Kiemba.
Uganda; Muwonge Hamza, Waswa Hassan, Wadada Nico, Majegwa Brian, Kabugo Savio, Kasaga Richard, Iguma Dennis, Said Kyeyune, Mpande Joseph, Edema Patrick na Odur Tonny