Kufuatia kipigo cha cha 6-1 kutoka kwa United States katika mechi yao ya kwanza ya makundi kwenye michuano ya Gold Cup, wachezaji wengi wa kikosi kilichoanza cha timu ya taifa ya Belize wamesema kwamba walifuatwa kwa ajili ya kupewa rushwa ili kupanga matokeo ya mchezo huo. Belize, ambao wapo katika mpango wa kukusanya kiasi cha $25,000 zinazotakiwa kwa ajili ya kuhudumia safari zao ndani ya USA wakati wa michuano hiyo, walifunga bao lao la kwanza kwenye dakika ya 40 ya mchezo baada ya Chris Wondolowski kuwafungia wenyeji mabao mawili ya kuongoza katika dakika ya 12 na 37.
Wondolowski baadae akaongeza bao la 3 kabla ya mapumziko na wachezaji wenzie wakaongeza mengine matatu katika kipindi cha pili, bao moja likifungwa na Landon Donovan kwa penati katika dakika ya 76.
Wondolowski baadae akaongeza bao la 3 kabla ya mapumziko na wachezaji wenzie wakaongeza mengine matatu katika kipindi cha pili, bao moja likifungwa na Landon Donovan kwa penati katika dakika ya 76.
Wachezaji wa Belize wamesema kwamba walikataa hongo ya kiasi cha €10,000($13,074) kwa kila mchezaji — wakitaka kulinda heshima ya nchi yao.
"(Mtoa rushwa) alianza kutuambia kwamba hatuna nafasi ya kuwafunga Marekani hivyo alitaka atupe kiasi cha pesa ili tubadilishe maisha yetu huko nyumbani Belize lakini tufanye atakavyo yeye kwenye mchezo dhidi ya Marekani," Mlinzi wa Belize Ian Gaynair aliiambia 7 News Belize.Wachezaji hao wanasema walifuatwa kwa mara ya kwanza wakati wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Guatemala kabla ya kukutana tena na mtu huyo kwenye shopping mall ya Portland."Nilimuelewesha kwamba hatukuhitaji fedha zake kutoka kwake, na tulikuwa US kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi yetu na sio vinginevyo," alisema golikipa wa Belize Woodrow West.
No comments:
Post a Comment