Search This Blog
Saturday, July 14, 2012
LIVE MATCH CENTRE: YANGA 0-2 ATLETICO - FULL TIME
DK. 5 - Mpira ndio unaanza na timu zote zinaonekana kumiliki mpira kwa zamu.
DK 10 - Mchezo bado umetulia timu zinaonekana kusomana, ubaoni kunasomeka Yanga 0-0 Atletico
DK. 15 - Yanga 0-0 Atletico
DK 30 - Yanga 0-0 Atletico
Mpira ni mapumziko na timu zimetoka sare tasa mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamzilizika.
Kipindi kinaanza ndani ya dimba la taifa, Yanga 0-0 Atletico.
dk. 62 - Jerry Tegete ambaye hakuwa na mchezo mzuri leo anatoka na anaingia Said Bahanuzi ambaye ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga, matokeo bado ni tasa - milango ya timu zote bado ni migumu.
DK. 68 - Nizar Khalfani anaingia na Rashid Gumbo anatoka.
DK. 70 - Zikiwa zimebaki dakika 20 kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi, timu zote bado hazijaweza kuweka mpira kwenye nyavu. Mechi inaelekea kuisha sare hii kama mambo yataendelea kuwa hivi yalivyo.
DK 81 - Goaaaaaaaaaaaaaaaaaal - Atletico ya Burundi inapata bao la kuongoza hapa zikiwa zimebaki dakika takribani tisa mchezo kuisha.
DK. 89 - Atletico wanapata bao la pili hapa - beki za Yanga zinakatika kabisa hapa uwanjani.
DK. 90 - Mpira unamalizika hapa uwanja wa taifa. Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wanaanza vibaya michuano hii kwa kufungwa mabao mawili kwa bila. Kwa mchezo mzima Atletico walionekana kumiliki sana mpira kuliko Yanga, na nafasi kadhaa walizotengeneza wamefanikiwa kuzitumia vizuri mbili na kupeleka kupata ushindi huu.
KELVIN YONDANI KUANZA KWENYE KIKOSI CHA YANGA KITACHOANZA LEO KWENYE MECHI YA UFUNGUZI WA KAGAME CUP
1.Yaw Berko - 19,
2.Juma Abdul - 14,
3.David Luhende - 29
4.Nadir Haroub Cannavaro (C) - 23
5.Kelvin Yondani - 5
6.Athuman Idd Chuji - 24
7.Shamte Ally - 7
8.Rashid Gumbo - 16
9.Jeryson Tegete - 10
10.Haruna Niyonzima - 8
11.Hamis Kiiza - 20
Subs;
1.Ally Mustapaha 'Barthez' - 1
2.Godfrey Taita - 17
3.Oscar Joshua - 4
4.Stephano Mwasika - 3
5.Ladislaus Mbogo - 29
6.Juma Seif Kijiko - 13
7.Idrisa Rashid - 12
8.Nizar Khalfan - 7
9.Said Bahanunzi - 11
Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro,
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Physician: Dr Sufian Juma
Massagist: Jacob Onyango
Kit Manager: Mahmoud Omary (Mpogolo)
SERENGETI DANCE LA FIESTA YATISHA NDANI YA JIJI LA MAHABA TANGA
Mmoja wa waratibu na jaji, Issa Qwisa Thomson akikabidhi kitita cha
shilingi milioni moja kwa kundi kinara la Questions Crew kati ya saba
yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta
2012,lililofanyika jioni ya leo ndani ya kiota cha mangoma cha
Lakasachika mkoani Tanga.
Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akiwa na kitita cha fedha taslim sh milioni moja,kwa ajili ya kukabidhi kwa kundi la Questions Crew lililoibuka
mshindi wa kwanza kati ya makundi saba yaliyojitokeza kushiriki
shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo
kwenye ukumbi wa Lakasachika mkoani Tanga.
Baadhi ya wacheza shoo wa kundi la Questions Crew wakizungumza machache mara baada ya kukabidhiwa kitita chao cha shilingi milioni moja
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti-Tanga wakikabidhi
Kreti moja ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa kundi la Questions Crew mara baada ya kuibuka washindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012 mkoani Tanga.
Watu mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Kundi la Sweet Girls likionesha umahiri wake kucheza kwenye shindano la
kulisaka kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta 2012
Kundi la la Street Colour likionesha umahiri wa kucheza mbele ya sehemu
ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza jioni ya leo kushuhudia
shindano la Serengeti dance la Fiesta lililofanyika ndani ya ukumbi wa
Lakasachika
Kundi la Questions Crew likicheza
kouwania kitita cha milioni moja kilichotolewa na kampuni ya bia ya
Serengeti sambamba na kreti moja ya bia.
Mdau Thomson akikata kiu yake safi kabisaa.
Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ukumbi wa Lacasa chika.
Pichani juu na chini Sehemu ya wakazi
mbalimbali wa jiji la Tanga waliojitokeza kushuhudia shindano hilo
lilovuta hisia za vijana wengi
Mmoja wa majaji wa shindano hilo B Dozen akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.
Mmoja wa majaji wa shindano hilo
Isakwisa Thomson akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano
hayo kwa mkoa wa Tanga.
Majaji wa shindano la Serengeti dance la fiesta 2012 wakijadiliana jambo
wakati shindano likiendelea ndani ya ukumbi wa Lakasachika jioni ya
leo,ambapo wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kwa wingi na
kujionea vipaji
Friday, July 13, 2012
VICENTE DEL BOSQUE, CARLO ANCELOTTI NA TOP 5 YA MAKOCHA WALIOTIMULIWA KWENYE TIMU ZAO PAMOJA NA KUFANYA KAZI NZURI
1: VICENTE DEL BOSQUE
Real Madrid wana historia ya kubadilisha makocha wao kuliko wanavyobadilisha vitambaa vya meza za kulia msosi kwenye canteen, lakini kocha wa sasa wa Spain Del Bosque anaweza kuwa ndio aliyefukuzwa kwa kuonewa kuliko wengine. Akiwa ameshinda makombe mawili ya La Liga, mawili ya champions league, Spanish Supercup, UEFA Supercup na Intercontinental cup wakati akiwa kiongozi wa benchi la ufundi la Los Blancos, aliiongoza klabu kupata mafanikio makubwa katika historia ya klabu hiyo.
Mara magalatico wakaanza kuja kwenye klabu bila ruhusa ya kocha, klabu ikafanya uamuzi wa kushtusha zaidi ulipoamua kutomuongeza mkataba mpya Del Bosque mwaka 2003. Matokeo yake akaondoka na klabu ikashindwa kufanya vizuri hata kufikia kukaa misimu minne bila kombe la maana mpaka mwaka 2007 (chini ya Fabio Capello) pamoja na kutumia mipesa mingi katika kununua wachezaji wakubwa.
Ilikuwa kama wamepigwa laana na Vicente Del Bosque ambaye baada ya kukaa kwa muda bila kazi, mnamo mwaka 2008 baada ya Luis Aragones kujiuzulu kuifundisha Spain - Bosque akatwaa majukumu ya ukocha na kuifanya Spain kuwa moja mataifa ya kuogopwa kwa soka duniani hivi sasa.
2: HARRY REDKNAPP -TOTTENHAM HOTSPUR
Harry Redknapp aliiokoa Spurs kutoka kwenye hali mbaya iliyokuwa ikitishia uwepo wao kwenye ligi kuu baada ya kocha Juande Ramos alipoiacha klabu ikiwa imepata pointi mbili kwenye mechi nane. Redknapp akaingia White Hart Lane na kuiwezesha timu kumaliza kati kati mwa msimamo wa ligi, kabla ya kuiongoza Spurs kucheza champions league mwaka mmoja baadae ambapo walifanya vizuri kiasi cha kufika kwenye robo fainali.
Ingawa Spurs walianza vizuri msimu uliopita kiasi cha kuonekana kutishia utawala wa vilabu vya Manchester - lakini mwisho wa siku walimaliza kwenye nafasi ya nne, ambayo walistahili kucheza Champions league kama isingekuwa walioshika nafasi ya sita kutwaa kombe la ulaya mwaka huu. Hili halikumfurahisha Daniel Levy ambaye uhusiano wake na Harry ulianza kuyumba mara baada ya kocha huyo kuanza kuhusishwa na kuchukua nafasi ya ukocha kwenye timu ya taifa ya England, na matokeo yake akamtimua kabisa mwishoni mwa msimu. Andre Villas Boas ndio mwanaume aliyepewa jukumu la kuinoa Spurs - huku akiwa na kivuli cha kuyapita mafanikio ya Harry.
3: SAM ALLARDYCE - BLACKBURN
Akiwa amefanya maajabu pale Bolton kwa miaka kadhaa iliyopita, Alladyce akapewa jukumu la kuinoa Blackburn. Sam aliweza kujiwekea misingi imara pale Ewood Park, akiiongoza klabu kutoka kwenye matatizo waliyoyapata chini ya Paul Ince , na akafanikiwa kuiweka Blackburn kuwa moja ya vilabu 10 vya juu vya England.
Matajiri wa kihindi "The Venkys' walikuwa na mawazo tofauti, wakamtimua Big Sam mara baada ya kuinunua klabu hiyo na kumpa kazi Steve Keane - mwanaume ambaye bado yupo kibaruani pale Ewood pamoja na kwamba kuteuliwa kwake kumeshadhihirisha kuwa ni moja ya uamuzi mbovu zaidi kwenye historia ya klabu hiyo kwenye Premier league.
4: CARLO ANCELOTTI - CHELSEA
Baada ya kushindwa kumvutia Guus Hiddink kwa dili la moja kwa moja pale Stamford Bridge, Roman Abramovich akaenda na kumpa mkataba wa muda mrefu Carlo Ancelotti kutoka AC Milan. Alimsaini muitaliano huyu mwaka 2009 na akaiongoza vizuri Chelsea kushinda EPL na kombe la ligi mwaka 2010.
Ingawa msimu uliofuatiwa alishinda kombe la FA, lakini alitolewa na Manchester United kwenye Champions league hatua ya robo fainali na kupoteza ubingwa wa ligi kwa United tena. Ancelotti akatimuliwa na kijana mdogo Anfre Villas Boas akapewa nafasi yake lakini nae hakudumu kwa muda mrefu akatimuliwa.
NEIL WARNOCK - QPR
Warnock alifanya kila kitu na kila mbinu na kufanikiwa kuiwezesha timu ya tajiri Tony Fernandes kupanda mpaka ligi kuu ya England msimu uliopita, na kukata kiu ya washabiki wa klabu hiyo kongwe ya kucheza ligi kuu baada ya kushindwa kwa miaka mingi. Ingawa mpaka kufikia kipindi cha Christmas timu ilikuwa hina matokeo mazuri kwenye ligi mmiliki wa timu Tony Fernandes akaamua Warnock aliyewapandisha daraja hakuwa mtu sahihi wa kuendelea kubaki kwenye benchi la ufundi na hatimaye akamtimua na kumpa kibarua Mark Hughes - badala ya kumpa Warnock fedha za kutosha za kununua wachezaji wenye hadhi na ubora wa kucheza ligi.
Warnock kiukweli hakupaswa kuendewa alivyotendewa na QPR, ukiangalia hakupewa fedha za kutosha kufanyia usajili - ambazo Hughes alipata lakini mwisho wa siku kwa bahati timu ikabakia kwenye ligi siku ya mwisho pamoja na kufungwa na City.
MILOVAN WA SIMBA: ASEMA HARIDHISHWI NA VIWANGO VYA BOBAN, KAZIMOTO NA NYOSSO
KOCHA
Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema kuwa kikosi chake hakipo imara katika
kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame.
Hayo
aliyasema muda mchache baada ya mechi ya fainali kati ya timu yake na Azam FC,
mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na badaye kupiga penati na
Simba kushinda mabao 3-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa.
Milovan
alisema, Kagame ni michuano mikubwa yenye upinzani mkubwa kutokana na kila timu
kujiandaa kwa kuchukua ubingwa.
Kocha
huyo aliwataja wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha bado Haruna Moshi
‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar .
Alitaja
sababu ya kutokuwa fiti ni mapumziko ya wiki mbili yamesababisha wachezaji hao
kuwa imara katika viwango vyao vilivyozoeleka uwanjani, hivyo amepanga kuwapa
mazoezi ili kurejesha hali yao
ya mwanzo.
Simba
inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo dhidi ya URA ya Uganda saa
10:00 jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00
mchana Uwanja wa Taifa.
mwisho
KOCHA WA YANGA: NINA KIKOSI BORA CHA KUTETEA UBINGWA WA KAGAME
WAKATI
akijiandaa kuvaana na wapinzani wake Atletico ya Burundi, Kocha Mkuu wa Yanga, Tom
Saintfiet ametamba kuwa kikosi kipo fiti.
Yanga
ambao Mabingwa wa watetezi wa Kombe la Kagame wanatarajiwa kucheza na Atletico
kesho jioni saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha
huyo ambaye raia wa Ubeligiji amesema maandalizi ya siku chache tangu afike
akae pamoja na kikosi zinatosha kutetea taji hilo la ubingwa.
Mbeligiji
huyo amesema, atajitupa uwanjani kesho huku akiwa na hofu kubwa dhidi ya
wapinzani wake kutokana na ukubwa wa michuano hiyo .
Katika
hatua nyingine, Kocha huyo amesikitika kuwakosa wachezaji makinda, Frank
Domayo, Simon Msuva na Omega waliopo kwenye kambi ya Timu ya taifa ya vijana ya
U-20 inajiandaa kucheza na Nigeria
katika mashindano ya vijana ya Afrika ya umri wao .
Yanga
ipo kundi C na timu ya APR, Wau Salaam watakaocheza nao kesho, mechi
itakayoanza kuchezwa majira ya saa ya 8:00 mchana Uwanja wa Taifa.
KALI YA LEO: MARADONA AKATAA KUTAMBUA UAMUZI WA AL WASL KUMFUKUZA
Makocha wengi wanapokuwa wamefukuzwa, wanapaki mabegi yao, wanaaga wachezaji wao na benchi la ufundi, na kutoa taarifa kwa media kuelezea namna ambavyo maisha yao yalivyokuwa ndani ya klabu na kistaarabu watawatakia mema mabosi wao katika kuiendeleza klabu. Diego Maradona hayupo hivyo, siku moja baada ya kufukuzwa na klabu ya Al Wasl, muargentina huyo ametangaza kwamba bado anataka kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
"Napenda kusema kwamba siku imekuwa ni nia yangu kuendelea kubaki kwenye nchi hii nzuri ambayo siku zote imekuwa ikinipokea vizuri, ninawashukuru sana kwa hili hasa Sheik kwa kunipokea na kunipa nafasi ya kufundisha klabu ya Emirate," taarifa iliyotolewa na Maradona inasomeka.
"Ukweli ni kwamba katika siku za mwisho, tumekuwa tukiongea kujaribu kukubaliana kuhusu ununuzi wa wachezaji wapya, ni hitaji ambalo nililihitaji kwa ajili kuweza kutimiza mipango yangu ya kushinda ligi kwa matokeo mazuri.
"Siku zote nitakuwa mwingi wa shukrani kwa mwajiri wangu na ningependa kuweka hili wazi kwamba nilikuwa na furaha siku zote nikiwa klabuni na jinsi walivyonipa sapoti. Lakini kwa bahati mbaya, klabu imetoa taarifa ambayo siisapoti kwa sababu bado nataka kuendelea kuifundisha Al Wasl.
"Kama haiwezekani klabu kununua wachezaji wapya kwa sababu hawana fedha za kufanya hivyo, basi kuna uwezekano mkubwa tukakaa na kulijadili hili pamoja na bodi kujaribu kupata suluhisho. Natumaini kutakuwa na kikao chetu hivi karibuni tujadili hili suala. Nina uhakika wapo tayari kujadili hili na tutafikia makubaliano mazuri tu."

KISA CHA MWL J.K NYERERE KUTOINGIA KWENYE VIWANJA VYA SOKA.
Na Adam Fungamwango
NAHODHA wa Taifa Stars Abdurahman Juma akimtambulisha rais wa Sudan wakati huo Nimeir kwa mchezaji Omary Zimbwe, huku Mohamed Chuma kushoto, Kitwana Manara mrefu na Abdallah Kibadeni anayeonekana kichwa wakishuhudia kwenye mechi ya kimataifa kati ya Stars na Sudan! Kwenye mechi hiyo Stars ilicheza tumbo wazi kwa uzembe wa viongozi wa FAT! Nyerere ambaye alikuwa rais wakati huo kwa tukio hilo alisusa kwenda mpirani hadi anafariki! Hii ilikuwa miaka ya 1970 hivi
MBWANA SAMATTA IS ON FIRE!
Mshambuliaji Mbwana Samatta ameendelea na rekodi yake nzuri ya kupasia nyavu pale alipoiongoza TP Mazembe kuifunga OC MUUNGANO mabao 5-0,
Samatta peke yake alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo wa ligi kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Samatta peke yake alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo wa ligi kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WAO KWA KUIFUNGA AZAM KWA PENATI
Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar
Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya
Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya
Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka
suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri
na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo
kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na
kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo
kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano
ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Urafiki.
Wachezaji wa timu ya Azam FC nao wakisalimiana na viongozi mpira wa miguu kutoka Zanzibar pamoja na mgeni rasmi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki. |
Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba
kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya
Azam FC katika mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao. |
Salum Kinje akimpongeza Felix Sunzu kwa kufutupia bao la kwanza la Simba |
Thursday, July 12, 2012
MSAADA TUTANI: HII KIBOKO HUYU NI NANI - MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ITALIA.
Tip - Huyu ni mchezaji wa timu ya taifa ya Italia na leo ametimiza umri wa miaka 30. Chemsha Bongo utaje jina la mchezaji huyu. |
LIVE MATCH CENTRE: SIMBA YATWAA UBINGWA WA URAFIKI CUP - YAIFUNGA AZAM KWA PENATI
Felix Sunzu anaipatia Simba bao la kuongoza hapa uwanja wa Taifa kwenye dakika za mwanzo kabisa za mchezo.
Dk ya 45 Azam wanasawazisha goli hapa na mpira unaenda mapumziko matokeo yakiwa sare. Mcha Viali ndio mfungaji wa goli.
Kipindi cha pili kinaanza hapa timu zinashambuliana kwa zamu.
Azam wanapata bao la pili John Bocco anaweka mpira kimiani.
Simba wanapata penati na Mwinyi Kazimoto anaenda kupiga penati hiyo.
Ni goli - Mwinyi Kazimoto aka Failasufu anafunga bao la pili kwa upande wa Simba.
Mpira umeisha na timu zimeanza kwenda kwenye hatua ya penati.
Penati zinamalizika kupigwa na Simba wanatoka na ushindi wa penati 3-1 na matokeo ya jumla yakawa 5-3.
UCHAGUZI YANGA: HIZI NDIO SERA ZA MGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI CLEMENT SANGA
Leo tunaendelea na utaratibu wetu wa kuwafanyia mahojiano wagombea nafasi ya uongozi wa klabu ya Yanga kwenye uchaguzi utakaofanyika siku chache zijazo.
Leo tunaye mgombea nafasi ya umakamu mwenyekiti bwana Clement Sanga. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo.
Ni kitu gani kilichokusukuma kugombea uongozi wa Yanga?
Nimejitosa kuwania nafasi hii nikiamini nina uwezo na sababu ya kuiongoza Yanga, ili niweze kutoa mchango wangu kwa klabu ninayoipenda tangu utotoni.
Ili ndoto za yale ninayofikiri ni muhimu katika vipaumbele vyangu, kwa kushirikiana na viongozi wenzangu sanjari na wanachama, kwanza kabisa kutengeneza mfumo ambao mipango yake inatekelezeka.
Mfumo huo wa awamu tatu tofauti, tukianzia mipango ya muda mfupi, muda wa kati na mipango ya muda mrefu, ambao hata kama muda wetu wa kukaa madarakani utamalizika, itawawia rahisi viongozi wajao kuongoza kwa kufuata mfumo zaidi ambao utarahisiha utekelezaji wa majukumu yao.
Kama wanachama wa Yanga watakuamini na kukupa nafasi utaifanyia nini klabu?
Kama nikipata ridhaa ya kuiongoza Yanga kuna mambo ambayo nitayapa kipaumbele ikiwemo suala la marekebisho ya Katiba.
Kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, lakini kwa kuwashirikisha zaidi wanachama tutaipitia upya Katiba na kuifanyia marekebisho, ili tuwe na Katiba imara, yenye nguvu itakayoletea tija.
Kwa sasa Yanga haina dira wala mwelekeo. Tunahitaji kuwa na dira na mwelekeo, bila hivyo hatutafika popote, hivyo nikiingia madarakani kwa kushirikiana na viongozi wenzangu mtazamo wangu utakuwa katika kujenga mfumo wa kudumu katika masuala yafuatayo.
A. Umoja: Kusimamia suala la umoja na mshikamano ndani ya klabu na kuondoa makundi na kuhakikisha Yanga inakuwa moja kwani haiwezekani mwana- Yanga adui yake, awe mwana Yanga, hivyo umefika wakati mambo hayo yaondolewe.
Ili kuimarisha uhusiano na kujenga umoja ndani ya Yanga, tutahakikisha vikundi vyote vilivyomo ndani ya klabu vinatambuliwa kikatiba ili viweze kuendelea kuisaidia klabu kwa utaratibu ulio rasmi.
Hii nikimaanisha viongozi wa matawi Tanzania nzima, Wazee, vijana na hata vikundi vya ushangiliaji vinavyoleta hamasa katika michezo yetu mbalimbali.
B. Soka la vijana: Nitahakikisha natilia mkazo kuendeleza soka la vijana na kuibua vipaji vipya kama ilivyokuwa miaka ya zamani.
Mpira si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu, soka inaanza chini hivyo ni vyema watu wakatambua hilo, ili mchezo huu upige hatua kama zilivyo nchi zilizoendelea duniani, ni lazima utengenezwe msingi kwanza kwa kuchagua vijana wadogo, ambao baadaye watakuwa hazina kwa Yanga.
C. SACCOS- Kuwafanya wana Yanga wajivunie zaidi klabu yao, tutapanua wigo wa taasisi yetu, kwa kuanzisha Mfuko wa Akiba na Mikopo kwa wanachama (SACCOS), ambao utakuwa ukitoa mikopo kwa wanachama wake, kupitia matawi jambo ambalo litaondoa utegemezi katika klabu na hata miongoni mwa wanachama.
D. KUJITEGEMEA: Tutabadili mfumo wa uendeshaji klabu uendane na hali ilivyo ya soka la sasa, ambapo klabu inatakiwa kujiendesha kibiashara, kwani Yanga ni taasisi kubwa yenye fedha nyingi, ambazo zikitumika ipasavyo, zitaisaidia timu kiuchumi na kujiendesha kisasa na jambo hilo litawezekana iwapo tutakuwa na Katiba bora ambayo itawezesha jambo hilo kutekelezeka kiurahisi.
Ni aibu klabu kubwa kama Yanga kuwa maskini, wakati ina raslimali za kutosha ambazo haziinufaishi, hivyo kubadili mfumo wa uendeshaji kutaifanya iweze kujiendesha kwa kujitegemea.
Nia sio kurudi nyuma bali kwenda mbele na kuondoa umaskini uliokithiri katika klabu yetu na kuifanya ijiendeshe kisasa na kuwa klabu ya kulipwa ambayo inaweza kukabiliana na klabu nyingi kubwa za Afrika.
Kwa kushirikiana na viongozi wenzangu nitaweka mawazo ya kuifanya Yanga iweze kujiendesha kibiashara na ikiwezekana kubadili katiba kwa kutilia mkazo suala la kampuni ili tuweze kuuza hisa za klabu, jambo ambalo litasaidia kuongeza mapato pamoja na kuwajibika kwa wanachama ambao sasa watakuwa sehemu ya klabu kwa karibu zaidi.
E. UENDESHAJI WA KLABU: Pia katika kuboresha mfumo huu wa uendeshaji, tutaunda idara kadhaa kwa ajili ya kurahisisha suala hilo, ambapo kutakuwa na Idara za Uhasibu, Masoko, Sheria pamoja na ile ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano.
Pia shughuli zote zinazohusu klabu zitafanyika makao makuu ya klabu yetu Jangwani, hivyo mawasiliano yoyote ya kikazi baina ya wachezaji, viongozi, wanachama na wadau wa Yanga yatafanyika klabuni lengo ni kuongeza heshima na uadilifu kwa Yanga.
Ili kulipa nguvu suala hilo tutalifanyia ukarabati jengo la makao makuu ya klabu liwe na hadhi ya Yanga na kwa ujumla uongozi wangu kwa kushirikiana na wenzangu utakuwa ule unaozingatia zaidi Katiba.
F. MATAWI: Nitahahakikisha uongozi wangu unaimarisha matawi ya klabu na kufanya wanachama kufahamu na kuchangia shughuli za klabu na kwa kuanzia itakuwa busara kila wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam kuwa na ofisi na vitendea kazi muhimu na mpango huo utaendelea nchi nzima.
Lakini pia lazima niwe muwazi tangu sasa, kuwa si kila jambo litahusisha wanachama wote, mfano mipango ya timu kwa maana ya usajili, ushiriki wa ligi na michuano ya Kimataifa, hilo likishikwa na watu wengi nafasi yake ya mafanikio huwa ndogo, tutazipa nguvu kamati za ufundi na mashindano kufanya kazi kwa wepesi na ushirikiano mkubwa.
Unawaambia nini wanayanga?
Naomba wanichague mimi wajenge imani kwangu kwani nitahakikisha kwa kushirikiana na wenzangu tunajenga timu imara ya ushindani, itakayokuwa tishio katika michuano ya ndani na ya kimataifa. Wamchague Sanga kwa Yanga inayoeleweka.

EXCLUSIVE: EMMANUEL OKWI SASA KWENDA AUSTRIA JUMAPILI HII - PARMA MMMMH!??? AIOMBEA SIMBA USHINDI DHIDI YA AZAM LEO
Dakika chache zilizopita nimetoka kufanya mazungumzo ya simu na mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda the 'Cranes' Emmanuel Okwi kuhusu sakata la uhamisho wake kwenda barani ulaya kufanya majaribio ya kujiunga na moja ya vilabu vikubwa kwenye bara hilo.
Kwenye mazungumzo yetu yapatayo dakika tatu, Okwi kwanza alinitaka niwaambie mashabiki wa Simba kwamba anaiombea kheri klabu yake kwenye mchezo wa fainali ya leo usiku dhidi ya Azam FC ili kuweza kuanza msimu mpya vizuri, pili ndio akanipa taarifa juu ya sakata lake la kutafuta timu ya kucheza ulaya, "Shaffih nashukuru mungu leo nimepata viza ya kwenda nchini Austria kwenda kufanya majaribio na klabu Redbull Salsburg inayoshiriki ligi kuu ya Austria. Jumapili ya wiki hii ndio nategemea kuondoka rasmi Uganda na kwenda huko kufanya majaribio. Taarifa nyingine nitaendelea kukupa nikiwa huko."
Okwi ambaye wiki iliyopita ilisemekana alikuwa akitafuta viza ya kwenda nchini Italia kwenda kufanya majaribio na klabu ya Parma baada ya kukataa kujiunga na vilabu vikubwa vya South Africa Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns - amesema mpango huo lakini kwa sababu tofauti zilizo nje ya uwezo kwa sasa zimembidi aende Austria kwanza."
Redbull Salsburg ni klabu inayomilikiwa na kampuni ya utengenezaji vinywaji ya Redbull. Ni bingwa wa mara saba wa Austria Bundesiliga pia ni moja ya vilabu vikubwa barani ulaya vyenye academy za soka barani Afrika - ikiwa yenyewe imejenga shule yake ya kukuza vipaji vya soka nchini Ghana.
Yanga yatangaza kikosi cha Kagame
ZIKIWA zimesalia siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Kagame kuanza, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji, Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaocheza huku akimtema nahodha wake, Shadrack Nsajigwa .
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi, keshokutwa Jumamosi na siku hiyo itafungua kwa kuanza kucheza na Atletico ya Burundi.
Akitangaza kikosi hicho, Tom alisema haikuwa kazi rahisi kwake kupata kikosi hicho kutokana na viwango vya wachezaji wake kwenye tim hiyo.
Saintdiet alisema, wachezaji ambao amewaacha wasisikitike akiwemo Nsajigwa anatambua umuhimu kwenye timu na badala yake waendelee na mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mbelgiji huyo amekitaja kikosi hicho kuwa ni makipa ni Yaw Berko na Ally Mustapha ‘Bartherz’, Mabeki ni Juma Abdul, Godfrey Taita, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani ‘Vidic’, Ladislaus Mbogo.
Viungo ni Athumani Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Rashidi Gumbo, Nizar Khalfani, Shamte Ally na Idrisa Rashidi
Washambuliaji ni Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi na wachezaji aliowaacha ni Stephene Mwasyika, Ibrahim Job, Said Mohamed, Nsajigwa Omega Seme, Frank Domayo na Simon Msuva waliopo Timu ya taifa ya vijana ya U-20, Nurdin Bakari mwenye majeraha ya paja.
Subscribe to:
Posts (Atom)