KOCHA
Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema kuwa kikosi chake hakipo imara katika
kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame.
Hayo
aliyasema muda mchache baada ya mechi ya fainali kati ya timu yake na Azam FC,
mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na badaye kupiga penati na
Simba kushinda mabao 3-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa.
Milovan
alisema, Kagame ni michuano mikubwa yenye upinzani mkubwa kutokana na kila timu
kujiandaa kwa kuchukua ubingwa.
Kocha
huyo aliwataja wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha bado Haruna Moshi
‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar .
Alitaja
sababu ya kutokuwa fiti ni mapumziko ya wiki mbili yamesababisha wachezaji hao
kuwa imara katika viwango vyao vilivyozoeleka uwanjani, hivyo amepanga kuwapa
mazoezi ili kurejesha hali yao
ya mwanzo.
Simba
inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo dhidi ya URA ya Uganda saa
10:00 jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00
mchana Uwanja wa Taifa.
mwisho
No comments:
Post a Comment