Search This Blog

Saturday, September 8, 2012

MAMBO MANNE MUHIMU KUMUHUSU CRISTIANO RONALDO

> Pamoja na utajiri mkubwa alionao akiwa ndio mcheza soka anayelipwa vizuri zaidi duniani nyuma ya David Beckham kwa mujibu wa jarida la Forbes. Cristiano Ronaldo ni tofauti na vijana wengine wenye mafanikio kama yake - yeye hanywi pombe kabisa. Unajua kwanini?
Baba yake alifariki kutokana na matatizo yaliyosababishwa na unywaji wa pombe. Hivyo Ronaldo hanywi pombe kwa kuwa inamkumbusha kifo cha baba yake.

> Wakati baba yake alipokuwa hai, ndoto yake kubwa ilikuwa ilikuwa ni kumuona mwanae akishinda tuzo ya uchezaji bora wa dunia, na mwaka 2008 akiwa na Manchester United aliitimiza ndoto hiyo ya marehemu baba yake. 

>Tumeshuhudia watu wengi maarufu wenye fedha kama Cristiano Ronaldo wamekuwa wakitumia fedha zao nyingi katika kujichora tatoo, lakini pamoja na ubishoo wote alionao Cristiano Ronaldo anasema hajachora tattoo kwa sababu ana changia damu mara nyingi.

> Ronaldo alitoa kiasi cha €3 Million ambazo ni sawa na fedha za madafu zaidi ya Billion 7 kwa nchi za kiafrika zilizokuwa zinakabiliwa na balaa la njaa.

LIONEL MESSI NA DI MARIA WAIZAMISHA PARAGUAY

FALCAO AWAADHIBU AKINA SUAREZ - COLOMBIA IKIIFUNGA 4-0 URUGUAY

CRISTIANO RONALDO NA POSTIGA WAIPA URENO USHINDI WA TAABU DHIDI YA LUXEMBOURG

ENGLAND WAIFANYIA MALDOVA WALICHOIFANYIA UJERUMANI MIAKA 11 ILIYOPITA

SERENGETI FIESTA 2012 YAVINJA REKODI MKOANI TABORA

Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
Anaitwa Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki. 
 Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangwaka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo.



 Pichani kulia ni Shaffih Dauda Dauda anbaye abaemamai ghetto
 Wakazi wa mji wa Tabora wakiwa ndani ya uwannja wa Ally Hassan Mwinyi wakati tamasha la Serengeti Fiesa lilipokuwa linaondoka
 Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua mashine,na kulia kwake ni Hamza Balla,
 Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012,Supa Nyota Ney Lee akitumbuiza jukwaani.
Msanii mahri wa muziki wa kizazi kipya,Ben Paul akionesha kipaji chake ch a kuimba.
 Palikuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.
 Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku
 Mbunge wa Tabora Mjini,Mh Afeni Rage akisoma moja ya namba ya aliyebahatika kuibuka na bajaji,kulia kwake ni Mkuu wa utafiti wa Clouds .TV,Bwa.Ruge Mutahaba.
 NI full mzuka mwanzo mwisho kwa mashabiki.

Watu walikuwa kibao.
Hamza Balla na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.

BAADA YA KUWEKEA INI JIPYA MADAKTARI WAMPA RUKSA KWA ABIDAL KURUDI UWANJANI

Mlinzi wa Barcelona Eric Abidal ameambiwa na madaktari ambao walimfanyia upasuaji wa upandikizaji wa ini kwamba hakuna sababu itakayomfanya asiendelee kucheza soka.

Mfaransa huyo aligundulika kuwa na uvimbe kwenye ini lake mwezi March 2011 na akaenda kufanyiwa upasuaji muda mfupi baadae, lakini yakatokea matatizo kidogo ya kiafya ambayo yalimlazimu awekewe ini jipya mapema mwaka huu.

"Siku zote amekuwa akiniambia anajisikia vizuri," anasema daktari Garcia Valdecasas.

"Hakuna sababu itakayomfanya asicheze tena soka, lakini kitu muhimu kabisa ni kwamba yupo hai na ana afya nzuri kabisa."

Kilichobaki sasa kwa Abidal ni kujitahidi kupunguza uzito uliotokana na kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu kiasi cha kumfanya apate kilo 6 za ziada, lakini ili kuweza kurudi uwanjani mapema Abidal amepewa vipindi vinne vya kufanya mazoezi ya gym kwa siku, hivyo anaweza kurejea uwanjani muda wowote kutoka sasa.

MSAADA TUTANI: WASHABIKI WA UKWELI WA CHELSEA HUYU NI NANI?

SIRI YA NAPOLI KUTOKUWA NA MAJERUHI WENGI KWENYE KIKOSI CHAO - NI SHERIA YA KUKATA TENDO LA NDOA KWA WACHEZAJI

Timu za soka siku zote zinatafuta njia mpya za kuzuia au kupunguza namba za majeruhi kwenye timu zao ambazo haziepukiki kila msimu na Napoli wameweka sheria moja ambayo ni mahususi kupunguza majeruhi wa misuli. Hakuna kufanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya mechi.

Kwa mujibu wa Football Italia

"Kutofanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya mechi njia nzuri ya kuzuia maumivu ya misuli," Proffesa Alfonso De Nicola ambaye ni daktari mkuu wa Napoli ameliambia gazeti la Corriere del Mezzogiorno.

"Ni sheria ya kikosi chetu. Pia kuna kazi maalum inayofanywa na wafanyazi walio chini yangu na kocha wa fitness ambayo inalenga zaidi katika kuzuia kuliko kutibu."

Kutokana na njia hii inaoneka kuwa nzuri kwa Napoli, kwa sababu timu hiyo imekuwa namba ya chini ya majeruhi wa misuli kwenye kikosi, lakini taarifa zinasema wachezaji wanaona sheria hiyo ni kali dhidi yao na inawakera wachezaji matajiri.

Friday, September 7, 2012

GOLI LA SIKU: LIPI NI BAO NZURI KATI YA HAYA MAWILI

CLOUDS MEDIA NA WASANII WA BONGO FLEVA WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA TABORA

 
 Sehemu ya nje ya kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kama kionekanavyo kwe mbele jioni ya leo,kituo hicho kipo nje kidogo ya mji wa Tabora,chenye jumla ya watoto wapatao 30 wanaolelewa na kituo hicho.
Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mh.Aden Rage sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya wakiwa katika picha ya pamoja na uwakilishi wa kampuni ya Clouds Media Group sambamba na baadhi ya Wasanii wa muziki wa Bongofleva ambao usiku huu wanatumbuiza ndani ya uwanja wa mpira wa Ally Hassan Mwinyi,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu  mbalimbali wa vyakukula walioutoa kwenye kituo hicho cha ST.Francis
Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya sehemu ya msaada wa vyakula uliotolewa na kampuni hiyo kwa kituo cha ST.Francis kilichopo maeneo ya Ipuli nje kidogo ya mji wa Tabora mjini,anaeshuhudia kulia ni Mlezi wa kituo hicho  Father Anthony Rajesta pia akipokea msaada huo  kwa niaba kutoka kwa mkuu wa Wilaya,Shoto nyuma ya Mkuu wa Wilaya ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage ambaye pia alijitolea mipira ya mitano kwa ajili ya michezo ya kituo hicho. 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya akizungumza machache ikiwemo na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group na wasanii waliojumuika kwa pamoja katika tukio hilo jioni ya leo,katika suala zima la kujitolea kuisadia sehemu ya jamii kwa namna moja ama nyingine.
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage nae akitoa shukurani zake za ujumla kwa Clouds Media Group na Wasanii wenyewe kwa kuwa na moyo wa upendo na kujitolea katika mambo mbalimbali ya kuisaidia jamii isiyojiweza kwa namna moja ama nyingine. 
Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group akizunguma machache ikiwemo na kufanya utambulisho mfupi kwa baadhi ya viongo husika na wasanii wenyewe kwa ujumla.
Msanii mkongwe katika kafika anga ya muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.
Juu ni baadhi ya wasanii waliojitokeza kushiriki katika suala zima la kuisaidia jamii isiyojiweza kwa namna moja ama nyingine.
Pichani juu ya chini ni sehemuya watoto wanaolelewa na kituo hicho wakiwa na baadhi ya walezi wao.Picha na michuzijr.blogspot.com
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage akiwa na  Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya wakiwasili kwenye kituo cha watoto yatima,St Francis kilichopo maeneo ya Ipuli,nje kidogo ya Tabora mjini.

KALI YA LEO: NAHODHA WA MANCHESTER UNITED AKAMATWA KWA KUFANYA MAPENZI HADHARANI

Star anayechipukia wa klabu ya Manchester United ya Uingereza  amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuonekana akifanya tendo la ndoa na mpenzi wake hadharani.

Luke McCullough, 18, ambaye msimu uliopita alikuwa nahodha wa Academy ya United, alionekana kwenye kamera za CCTV akiwa na mwanamke wakifanya mapenzi saa 11 asubuhi baada ya kukesha usiku mzima klabu.

Mchezaji huyo raia wa Ireland amekuwa akitajwa na mabosi wa Old Trafford kama Jonny Evans mpya.

Tukio hilo lilotokea eneo la Concert Square, kwenye bar maarufu katika wilaya ya Liverpool, litamuudhi sana kocha wake Sir Alex Ferguson.

Fergie huwa na mkali sana kwa vijana wake hasa wachanga, na wiki iliyopita aliwakataza wachezaji wadogo wote chini ya umri wa miaka 23 kuendesha magari ya kifahari yanayogawiwa na mdhamani mpya wa klabu Chevrolet.

Imetaarifiwa kwamba Luke akiwa na demu wake walionekana wakiwa wapo nusu uchi huku wakifanya mapenzi, na ndipo polisi wakaenda eneo la tukio na kuwakamata.

Wapenzi hao walishatuliwa na polisi na kuonywa kisha wakaachiwa, na walipoondoka na kufika mbele kidogo wakarudia tena mchezo wao, polisi wanasema.

Maofisa wa polisi walienda tena mpaka kwenye eneo lile na kuwakamata kisha kuwapeleka kituoni na sasa wanakabiliwa na kesi ya kufanya mapenzi hadharani.

SIMBA NA AZAM KUICHANGIA FEDHA HOSPITALI YA TEMEKE MECHI YA NGAO YA HISANI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Uganda (The Cranes) katika raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2014.
 
Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana (Septemba 7 mwaka huu) makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Cairo, Tanzania imeingia moja kwa moja raundi ya kwanza ambapo itacheza na Uganda.
 
Mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kati ya Juni 21,22 na 23, 2013 wakati ya marudiano itakuwa Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala kati ya Julai 5,6 na 7, 2013.
 
Nchi 38 zinashiriki katika mechi hizo za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya awali itakayochezwa kati ya Novemba 30 na Desemba 1 na 2 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Desemba 14,15 na 16 mwaka huu.
 
Ratiba imepangwa kwa makundi ya kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza fainali hizo nchini Afrika Kusini. Kanda hizo ni Kaskazini itakayopeleka timu mbili katika fainali, Magharibi A (timu mbili), Magharibi B (timu tatu), Kati (timu tatu), Kati Mashariki (timu tatu), Kusini (timu tatu akiwemo mwenyeji Afrika Kusini).
 
Kwa upande wa kanda ya Tanzania (Kati Mashariki), timu zinazoanzia raundi ya awali ni Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya.
 
Fainali za Kwanza za CHAN zilifanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast ambapo Tanzania ilishiriki huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ikiibuka bingwa. Fainali za Pili zilichezwa mwaka 2011 nchini Sudan ambapo Tunisia ilitwaa ubingwa. Fainali za Kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.

TAIFA STARS YAPANGWA KUCHEZA NA UGANDA KUWANIA TIKETI YA CHAN 2012

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Uganda (The Cranes) katika raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2014.
 
Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana (Septemba 7 mwaka huu) makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Cairo, Tanzania imeingia moja kwa moja raundi ya kwanza ambapo itacheza na Uganda.
 
Mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kati ya Juni 21,22 na 23, 2013 wakati ya marudiano itakuwa Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala kati ya Julai 5,6 na 7, 2013.
 
Nchi 38 zinashiriki katika mechi hizo za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya awali itakayochezwa kati ya Novemba 30 na Desemba 1 na 2 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Desemba 14,15 na 16 mwaka huu.
 
Ratiba imepangwa kwa makundi ya kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza fainali hizo nchini Afrika Kusini. Kanda hizo ni Kaskazini itakayopeleka timu mbili katika fainali, Magharibi A (timu mbili), Magharibi B (timu tatu), Kati (timu tatu), Kati Mashariki (timu tatu), Kusini (timu tatu akiwemo mwenyeji Afrika Kusini).
 
Kwa upande wa kanda ya Tanzania (Kati Mashariki), timu zinazoanzia raundi ya awali ni Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya.
 
Fainali za Kwanza za CHAN zilifanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast ambapo Tanzania ilishiriki huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ikiibuka bingwa. Fainali za Pili zilichezwa mwaka 2011 nchini Sudan ambapo Tunisia ilitwaa ubingwa. Fainali za Kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.

MSIKILIZE HUYU MDAU WA SOKA MKOANI TABORA!

MBWIGA NA SHAFFIH WASHINDWA KUTAMBIANA MJINI TABORA.

Mchezo maalum wa kuzipatanisha timu za Rhino Rangers na Police za hapa mjini Tabora umemalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1.
Mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Clouds Media Group ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za tamasha la Fiesta linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
lengo la kuzikutanisha timu hizo lilikua ni kuondoa uhasama uliokuwepo hapo awali baina ya timu hizo mbili uliokuwa umedumu kwa muda sasa,watangazaji wa vipindi vya michezo vya Clouds Media Group bwana Shaffih Dauda (Polisi ) na Mbwiga Mbwiguke (Rhino Rangers ) walizichezea timu hizo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kwamba upinzani kwenye mchezo wa soka huwa ni uwanjani na mara baada ya hapo maisha mengine huendelea kama kawaida.
Lengo lingine la mchezo huu lilikua pia kuzichangia timu hizi pesa kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la kwanza inayotaraji kuanza siku chache zijazo,o.
mapato ya mchezo huo yalikuwa ni Tsh 1,2170,000 kutokana na kiingilio cha tsh 1,000 kwa wakubwa na 500 kwa watoto.

    Dauda na Mbwiga wakisalimiana kabla ya mchezo.

   Hapa huyu jamaa alijipendekeza nikampiga kikoi kwa kutumia guu langu la dhahabu kama unavyoona hapo.
    Mbwiga kama anapigaaaaaaaaaa, anafinyaaaaaaaaaaaa
    sehemu ya mashabiki waliohudhulia mpambano huo.


   Bonge nae alikuepo kushow luv na wadau wake.
    Mgeni wa heshima akiikagua Rhino Rangers




 Hapa nilikua nawaeleza wachezaji wa timu zote mbili dhumuni hasa la mchezo huu!
 Kikosi cha Shaffih (POLICE TABORA )
Kikosi cha Mbwiga ( RHINO RANGERS )