Hizi zifuatazo ni takwimu zilizojitokeza kwenye michezo ya juzi ya FIFA Confederation Cup baina ya Spain vs Tahiti na Uruguay vs Nigeria.
- Diego Lugano alimaliza ukame wa goli ambao umedumu kwa miezi 18 - mara ya mwisho kufunga ilikuwa kwenye kombe la Ufaransa akiwa na PSG mwezi January 2012.
- Diego Forlan pia nae alimaliza ukame wa mabao, juzi alifunga bao kwa upande wa Uruguay kwa mara ya kwanza tangu alipofunga dhidi ya Venezuela tarehe 2 June 2012.
- Kipigo walichopata Nigeria kutoka kwa Uruguay kinamaanisha kwamba wamepoteza rekodi yao ya kutowahi kufungwa kwenye michuano hii. Denmark sasa ndio inabaki kuwa timu pekee kutowahi kufungwa kwenye historia ya michuano hii.
- Ushindi wa mabao 10-0 wa Spain dhidi ya Tahiti ulikuwa ndio mkubwa kuliko wowote uliowahi kutokea kwenye historia ya michuano ya mabara - ukivunja rekodi ya ushindi wa Brazil 6-0 Australia mwaka 1997 na
Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999.
- Pia ushindi wa Spain wa 10-0 ulifikia rekodi ya uwepo wa mabao mengi katika mechi moja (Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999)
- Fernando Torres aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat tricks mara mbili katika kombe la mabara - mara ya kwanza alifunga hat trick kwenye mchezo dhidi ya New Zealand mwaka 2009.
- Torres ni mchezaji wa tatu kufunga mabao manne katika mechi moja - wa kwanza Marzouk Al Otaibi na wapili ni Cuauhtemoc Blanco
- Tahiti wamefikia rekodi ya kuruhusu mabao mengi kwenye kombe la mabara - wamefungwa jumla ya mabao 16 - rekodi hii iliwekwa na Saudi Arabia Saudi Arabia mwaka 1999
CEO wa klabu ya Sunderland, Margaret Byrne, ameusifia ushirikiano na Tanzania kwamba ni hatua kubwa kuendelea mbele.
The Black Cats wameingia mkataba na kampuni ya nishati ya Power kujenga cademy kubwa ya soka nchini, ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Raisi Jakaya Kikwete alitembelea makao makuu ya klabu ya Sunderland huko Wearside siku ya jumapili katika kukata rasmi utepe wa kuanza kwa project hiyo.
“Ni siku muhimu kwa klabu na klabu na mji wetu,” Byrne alisema.
“Kutembelewa na mheshimiwa Raisi hapa wakati akiwa UK kuhudhuria mkutano wa viongozi wa G8 ni jambo kubwa kutoka kwake na mawaziri wake. Ni zuri sana kwetu.”
Hatua za mwanzo kwa ajili ya Academy zilizinduliwa siku hiyo ya jumapili, kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short.
Project hiyo itaisaidia Tanzania katika kukuza soka lake pia kuwapa nafasi kubwa vijana wadogo kabisa kuweza kuendeleza vipaji vyao kwenye academy hiyo.
Sunderland watajenga majengo pamoja na kutoa makocha wa kufundisha.
“Hatua ya kwanza itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion Power kujenga academy ya kijamii, tukiruhusu watoto wengi kuja na kufurahia kucheza mchezo wa soka,” Byrne alielezea.
“Hatua ya pili itatuhusisha sisi kufanya kazi na Symbion labda ikiwezekana na taasisi nyingine kujenga kituo cha kisasa cha kufundishia soka.
“Tutoa usaidizi mkubwa wa vifaa vingi tunavyotumia kwenye academy yetu ya Academy of Light na pia na maarifa tuliyoyapata na tunayoyapata kutoka kwenye project ya EPPP (Elite Player Performance Plan).