Nahodha wa zamani wa Yanga Shedrack Nsajigwa akiwa na Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili. |
Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini. |
Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo |
Kozi hiyo
ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini
ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake
‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza
kushiriki.
Ofisa Habari wa
DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia
makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika
kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.
“Hadi sasa
tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho
wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini haya ya
kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa
katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri
yanafuata,” alisema Mharizo.
Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA
tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya
Mwenyekiti wake Almas Kassongo.
No comments:
Post a Comment