Search This Blog

Saturday, November 16, 2013

MIEZI KADHAA BAADA YA KUMPONDA - JOSE MOURINHO ASEMA CRISTIANO RONALDO NDIYE MCHEZAJI BORA KULIKO WOTE ALIOWAHI KUWAFUNDISHA'


Jose Mourinho amesema kwamba kumfundisha Cristiano Ronaldo walipokuwa Real Madrid kinabakia kuwa kitu muhimu na kizuri katika maisha yake.

Wawili hao walikaa pamoja kwa miaka mitatu ndani ya Santiago Bernabeu, huku Ronaldo akifunga jumla ya mabao 168 katika mechi 164 wakati Mourinho akiwa katika benchi la Bernabeu. 


Na japokuwa imewahi kuripotiwa kwamba hawakuwa wakielewana walipokuwa Madrid, lakini kocha wa sasa wa Chelsea amemsifia sana mshambuliaji huyo mwenye miaka 28. 


"Kumfundisha Ronaldo kilikuwa kitu kikubwa sana kwenye maisha yangu ya ufundishaji," Mourinho aliiambia France Football.

"Ndio mchezaji mweledi zaidi ambaye nimewahai kumuona.

"Kocha na mchezaji wanaweza kuwa na tofauti zao kwa muda fulani, lakini inashiia pale pale, sina tatizo nae.

"Kuwa na Ronaldo katika klabu moja ni kitu bora kabisa kilichowahi kunitokea kwenye soka. "

Ronaldo mpaka sasa ameshafunga mabao 24 katika mechi 17 alizocheza msimu huu katika mashindano yote, na jana usiku aliingiza mguu mmoja timu ya Ureno katika mashindano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Sweden 1-0 katika mechi ya kufuzu kucheza World Cup 2014. 

MALINZI KUFUNGUA MICHUANO YA UHAI 2013


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.

Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika kesho (Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.

Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa Karume).

Kundi C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, na kwenye uwanja huo huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania Prisons.
RAMBIRAMBI MSIBA WA NYOTA COPA COCA-COLA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Sayari, Fatuma Bahau ‘Crouch’ kilichotokea jana (Novemba 15 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika mpira wa miguu kwani Fatuma ndiyo kwanza alikuwa anachipukia katika mpira wa miguu wa wanawake ambapo alikuwa mfungaji bora wa michuano ya U15 Copa Coca-Cola ya mwaka huu akichezea timu ya Ilala, hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

Kwa mujibu wa mlezi wa mchezaji huyo, Stephania Kabumba, marehemu anasafirishwa kesho kwenda kwao Mwanza kwa ajili ya maziko ambapo kifo chake kimesababishwa na ugonjwa wa malaria.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bahau, klabu ya Sayari, Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Fatuma mahali pema peponi. Amina

Friday, November 15, 2013

CECAFA CHALLENGE CUP DRAW

This is to inform you that the draw for the CECAFA Challenge cup 2013 in Kenya was held today in Nairobi. And the drawing of lots are as follows:-
 
GROUP A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
 
GROUP B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia
 
GROUP C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.
 
The fixtures will be released next week.

RONALDO VS ZLATAN: JOHAN CRUYFF ATAJA ANAYETAKA AMUONE AKIFUZU KWENDA KOMBE LA DUNIA

Gwiji wa soka wa Uholanzi Johan Cruyff angependa kuona  Cristiano Ronaldo akienda kucheza kombe la dunia 2014 mbele ya   Zlatan Ibrahimovic.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona amesema kwamba ni jambo baya kuona aidha Ronaldo au Ibrahimovic wakikosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa ya dunia, lakini angependa zaidi kumuona staa wa Ureno Cristiano Ronaldo akifuzu na timu yake mbele ya Sweden ya akina Ibrahimovic.

"Ni jambo baya kwa kombe la dunia kwamba mmoja kati  ya washambuliaji bora duniani hatoweza kucheza michuano hiyo. Ni ni jambo la kuhuzunisha," Cruyff aliiambia Algemeen Dagblad.

"Sina yoyote ninayempendelea kati ya hawa wawili, lakini nikitakiwa kuchagua mmoja kati yao yupi  ningependa kumuona akiingia World Cup na timu yake, basi ningependa kumuona Ronaldo akifuzu." 

MAKALA: THAMANI YA JEZI YA TAIFA, NA UCHAGUZI WETU WA WACHEZAJI


Na Baraka Mbolembole

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza na timu ya
Taifa ya Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu baadae wiki ijayo. Kwa sasa timu hiyo ipo kambini pamoja na ile inayofahamika kama ' Future Young Taifa Stars', zikijiwinda na mchezo huo sambamba na michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, Tusker Challenge Cup ambayo itapigwa baadae mwezi huu hadi mwanzoni mwa mwezi ujao nchini
Kenya.

Timu hizo mbili juzi zilicheza mchezo wa wao kwa wao na ile ' YoungTaifa Stars' kuitambia, Stars na kuichapa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Karume, zilipo ofisi za  shirikisho la soka nchini, TFF, na hatimaye jana kutangazwa rasmi kwa timu ya Taifa ambayo itacheza michuani ijayo ya Challenge.
  ILIPOTOKA STARS, INAPOKWENDA.....
Tanzania ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kundi la kufuzu kwa
fainali za Brazil, wakiwa wamepata ushindi mara mbili na kufungwa maranne . Chini ya kocha Kim Poulsen timu hiyo ilitolewa katika harakati za kufuzu kwa AFCON 2013 na timu ya Msumbiji, na ilishika nafasi ya nne katika michuano iliyopita ya Challenge, 2012, nchini Uganda.

Makocha wa zamani wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo, na Mdenish, Jan Borge Poulsen walikuwa wakilaumiwa sana na mashabiki wa soka kwa kushindwa kuleta mabadiliko katika timu hiyo. Jukumu hilo akapewa KIM.

 KIM, aliamua kubadili mfumo wa kiuchezaji, kutoka ule wa kutumia nguvu na kuanza kutumia wachezaji wenye vipaji zaidi na wanaojituma.
Alitarajia mpango wake huo ungeweza kumpatia mafanikio, lakini
haukufanya kazi hata pale Stars ilipokabiliana na timu ya Taifa ya
Uganda katika kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani. Stars iliyotimia ilifungwa katika michezo yote miwili ya mtoano dhidi ya ' The Crannes' ambayo ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kikosi halisi cha nchi hiyo.

Mfumo huo mwanzoni haukuonekana kuwakera wengi, ila katika siku za karibuni umekuwa ukiwaudhi mashabiki wengi ambao wanaona jambo analofanya NI gumu kwa Tanzania na haliwezi kutoka matunda yoyote

Mabadiliko makubwa ambayo KIM, ameyafanya tangu mwezi, machi, 2012 alipokabidhiwa timu hiyo ni kumpandisha kiungo, Salum Abubakary ambaye hakupewa nafasi wakati wa utawala wa Maximo na Jan. Kuwa na majukumu ya kuinoa timu ya Taifa siyo kazi ya kuwa na moyo wa kubabaika. Wakati mwingine mwalimu unatakiwa kujenga imani kwa wachezaji vijana, pengine imani ya Kim kwa wachezaji vijana imekuwa ni sababu ya uwepo wake hadi sasa, ila hata Maximo na Jan walijaribui jambo hilo ila waliishia kupigiwa kelele za kuondoka, na wakaondoka wakliwa hawajafikia hata nusu ya matarajio yao.

 Huwa kuna ukiritimba mkubwa katika timu yetu ya Taifa. Kuna mapendekezo mengine yanakuwa katika hali ya haki na usawa, ila yapo mapendekezo mengine ya wachezaji huwa ni ya kipuuzi sana. Kujihusisha katika mambo hayo ni sawa na KIM kujiondoa mwenyewe katika taaluma ya ukocha.

Lakini pamoja na kuwa na kazi ya kuchagua wachezaji kama mwalimu, pia KIM, anatakiwa kuangalia anavyoweza kuisadia Tanzania kupiga hatua ya kiuchezaji ndani ya uwanja na si kupanda katika renki za FIFA ambazo wakati mwingine haziendani na uhalisia wa mchezo wetu.

KIM, amekuwa mtu wa mipango ambayo itakuwa muhimili wa kuwa na kikosi imara cha timu ya Taifa. Ili kupata wachezaji wanaoweza kuishawishi jamii imuamini, ila kama kocha ambaye anaweza kuwajibishwa jambo hilo linaweza kuwa hatari sana. Pamoja na kazi ya kuchagua wachezaji kama mwalimu, pia kazi ya kocha ni kuangalia mfumo wa uchezaji, mbinu na ufundi, na moja ya nguzo muhimu kama mwalimu pia ni kuweka umoja katika timu na hilo limekuwa likioneshwa na KIM.
    
 KIM, AMEFELI AU AMEFAULU?
Bila shaka hata KIM mwenyewe atakuwa anatambua kuwa kipindi cha yeye kuwa kocha wa timu hiyo kinaweza kuamuliwa na matokeo ya Nairobi, Kenya katika michuano ijayo ya Challenge. Watu wengi wamekubali kushindwa katika harakati za kufuzu kwa AFCON 2013, kushindwa kutwaa Challenge, 2012, kushindwa kufuzu au kumaliza nafasi ya pili kwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa kanda ya Afrika, kushindwa kufuzu kwa CHAN 2014, Ila sifikirii kama ataendelea kuwa mtu sahihi endapo atashindwa kufika walau fainali katika michuano ijayo ya Challenge. Timu bora hujijenga huku zikipiga hatua katika michuano ya kimataifa. Hivyo itakuwa haina maana kusema tunawaendeleza yosso wetu kama kina Salum huku wakishindwa hata kucheza fainali ya michuano ya ukanda wetu.
Tunatakiwa kupigania mataji katika kila michuano ya ukanda huu, huku tukiwa na lengo la kuwandeleza vijana wetu wenye vipaji katika timu ya taifa, hali ya mazoea ya ushindi huwa ni kitu kizuri. Iitazame Uganda, utawala wao wa soka la kanda ya CECAFA, umewafanya kuwa na timu kali na wamejaribu mara nne mfululizo kufuzu kwa michuano mikubwa ya Afrika na ile ya kidunia, ila hawakuwa na vitu vingine vya ziada. UDHAMINI, kama ambao upo nchini kwetu.
   LA KUJIULIZA....
 Je, Stars itajijenga kwa mfumo wa sasa ambao hata wachezaji wasio na nafasi katika klabu zao
huchaguliwa?. Inakuwaje kuwa na wachezaji zaidi ya 40 ambao kwa pamoja wana sifa za kuiwakilisha nchi?. Ndiyo tunao wachezaji wenye vipaji lakini hata Brazil haina rundo la wachezaji bora zaidi ya 40 kwa
wakati mmoja, ambao wanaweza kuiwakilisha timu yao ya Taifa. Kwa uwepo wa timu ya pili ya Taifa, KIM ameshindwa kuwa na mtazamo mzuri katika hili kwa kuwa wachezaji hao wengi ni vijana, ambao wangeweza kukua vizuri wakiwa timu za vijana ambako wangeweza kucheza mashindano na kupata uzoefu huko. Na, wapo ambao hawachezi katika klabu zao ila hupewa nafasi,.

Wachezaji kama Miraj Adam, Adam Ramadhani, Amri Kiemba, Haji Nu hu, ni baadhi ya wachezaji ambao kimsingi hawakuwa na sifa za kuitwa kikosini kwa sasa. Wapo chini ya utaratibu wa machaguo ya timu ya Taifa. Timu ya Taifa ni muhimu kuliko matakwa binafsi ya Mtu.
 Kim, anatakiwa kupewa nafasi ya mwisho sasa. Baada ya kutolewa katika AFCON, kushindwa kutwaa taji la Challenge, kushindwa walau kumaliza katika nafasi pili katika kundi la kufuzu kwa kombe la dunia, kushindwa kufuzu kwa CHAN, CHALLENGE YA NAIROBI, Iwe nafasi ya mwisho kwa KIM.


 TIMU YA TAIFA IMARA, LIGI IWE IMARA PIA
Kuitwa kwa mshambuliaji, Elius Maguli wa klabu ya Ruvu Shooting ni moja ya machaguo ambayo yalitarajiwa na wengi. Amefanikiwa kufunga mabao tisa katika duru la kwanza la ligi kuu, Pia uchaguzi wa mara nyingine wa Juma Luizio wa Mtibwa Sugar umekuwa ni sahihi kwa kuwa amefanikiwa kufunga mabao tisa katika ligi kuu iliyosimama.
Mshambuliaji wa Azam, John Bocco amekuwa na miezi isiyovutia,
ameshuka sana kiwango, pengine naye alistahili kuwa kundi la kina
Kiemba. Hasingeitwa, timu ya Taifa ni orodha ya wachezaji bora wa nchi katika wakati husika. Bocco ni kielelezo kingene kuwa KIM, hatakiwi kuwa na timu mbili za Taifa, bali kuhakikisha anakuwa na timu moja imara ya Taifa ambayo itajumuhisha wachezaji bora waliofanya vizuri katika ligi ya ndani ambayo ndiyo pekeeinayoweza kutoa wachezaji wa kikosi hicho, au wale wachezaji bora wanaopata nafasi katika klabu za ng'ambo na kufunya vizuri. Huku akihakikisha wachezaji vijana kama Aishi Munula wakipata nafasi ya kukua vizuri kiumri na kimchezo katika timu za vijana.

Ni kama kwa David De Gea, kipa namba moja wa Manchester United kwa misimu mitatu sasa ila hana nafasi katika timu ya Taifa ya Hispania kutoka na uwepo wa makipa Iker Cassilas, Victor Valdes, na Pepe Reina. De Gea, amebaki kuwa chaguo sahihi namba moja katika timu za taifa za vijana. Si, kila mchaji '  yosso' anaweza kuingia moja kwa moja katika timu ya Taifa na kufanya vizuri. Pele' ' Mfalme wa kandanda' duniani alianza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 16, na mwaka mmoja baadae akafunga mabao sita katika fainali za kombe la dunia akiwa na miaka 17.
Ila, bado tunawataza wachezaji kama Xavi Hernandez,. Andrea Pirlo, Frank Lampard, Steven Gerrard wakiwa nguzo kubwa ya timu zao za Taifa huku wakiwa juu ya miaka 33. Ila Ujerumani ina makinda wengi na hufanya vizuri, ila Kina Ozil Mesut, Sami Khedira, Jereome Boateng, Org Bardistuber, Marko Marin, Mario Gotze wameshatwaa taji la vijana la Ulaya, watakapo pevuka wanaweza kuvunja mwiko wa kuishia nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia mara mbili na mara moja wakifungwa katika nusu fainali ya Euro.
 WACHEZAJI WETU WANAWAZA NINI?
Nafikiri kwa mchezaji ambaye hufikia kuitwa wa hadhi ya kimataifa, ni lazima ajitahidi kuonesha vitu tofauti katika uchezaji wake. Kila namba ya mchezo inapoongezeka kwa mchezaji kucheza mechi za kimataifa ni muhimu akijitambua kuwa anatakiwa kupiga hatua zaidi kiuchezaji, kiuzoefu, umakini, huku akiona fahali kuiwakilisha nchini yake katika michezo ya kimataifa. Wanatakiwa kuziheshimu timu zao na kuhakikisha kila mara wanacheza katika kiwango cha juu ili kulinda nafasi yake katika timu ya Taifa. Ni fahali kuchezea timu ya taifa, wajibu ni kitu muhimu na huanzia katika  moyo wa mtu mwenyewe, na si wa kulazimishwa.
 0714 08 43 08

Thursday, November 14, 2013

BAADA YA KASEJA - HUYU NDIO MCHEZAJI MWINGINE ALIYESAJILIWA NA YANGA



RAISI WA BAYERN MUNICH AMWAGA CHOZI AKITANGAZA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA ZAIDI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 113



Raisi wa Bayern Munich Uli Hoeness, anakabiriwa na kesi ya kukwepa kodi itakasomwa mwakani, jana alitokwa na machozi wakati akitangaza klabu yake kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa katika cha 113 years.
Katika mkutano wa mkuu wa klabu, Hoeness, ambaye alipokewa kwa shangwe, alishindwa kujizuia na kuanza kulia baada ya mabosi wenzie kumsifia kuiongoza vizuri timu hiyo na kupata mafanikio ya kushinda makombe matatu msimu uliopita. 
Hoeness, ambaye anashtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye fedha zake zilizopo katika moja ya benki huko Uswis.
 
Hoeness, amekuwa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 40 kama mchezaji, kocha na saa raisi, alizungumzia matatizo yake ya kisheria, akisema kwamba alifanya makosa na kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye akaunti yake ya nje.
'Nilifanya makosa kutokulipa kodi katika uwekezaji kutoka nje. Sikuchukua mamilioni ya fedha na kuyatoa nje ya nchi," alisema Hoeness, baada ya kujifuta machozi.  'Nitapambana na matatizo.'

'Nina imani kubwa na utawala wa kisheria wa Bavarian.
'Ninatumaini kwamba story hii itakuwa na mwisho mzuri mpaka kufikia mwezi  March. Na kama mpaka wakati huo nitaruhusiwa kuendelea kuwa hapa naahidi kuitumikia klabu hii mpaka pumzi yangu ya mwisho.'

MEXICO YAITANDIKA NEW ZEALAND MABAO 5-1 NA KUKARIBIA KUKATA TIKETI YA BRAZIL.






Mexico imeitandika New Zealand mabao 5-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano na kufanikiwa kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.

NANI MTANI JEMBE YAELEKEA KWA MASHABIKI WA TUNDUMA NA MOROGORO



Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye miji ya Tunduma na Morogoro nao watapata fursa ya kuburudika katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Mwaka mjini Tunduma na Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza litakalofanyika Tunduma zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya High Class pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Mbeya.

Kwa Mkoa wa Morogoro bendi maarufu mkoani humo ya Beacon Sound itatoa burudani kabambe kwa mashabiki watakaojumuika kushiriki bonanza hilo huku wasanii wa kundi maarufu la dansi GYT wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia Nani Mtani Jembe.

Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa Oktoba 2 na  inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.

Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.

Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.

Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.

Kwa mujibu wa matokeo kama ilivyotangazwa kwenye https://cms.rasello.com/kili  tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe timu ya Yanga inaongoza kwa kuwa na kiasi cha shilingi 55,600,000 huku Simba ikiwa na shilingi 44,400,000 hii ikiwa ni baada ya Simba kuongoza kwa takribani wiki mbili sasa hatimaye Yanga wamewapita.

KIM ATEUA 32 KUIKABILI KENYA



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.

Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).

Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).

Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

MANCHESTER UNITED YAVUNJA REKODI YA MAPATO - YAINGIZA £98.5m NDANI YA MIEZI MITATU TU

Manchester United imevunja rekodi ya makusanyo ya mapato baada ya kuingiza kiasi cha  £98.5m katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka wa fedha. 
Ukuaji wa asilimia 29% wa mapato unakuja baada ya ukuaji wa  63% pato linalotokana na udhamini na pia kutoka kwenye dili za kuuza haki za matangazo ya TV.  
Kulikuwepo na mikataba mipya 12 ya udhamini iliyosainiwa, ukiwemo na shirika la ndege la Urusi Aeroflot.
Klabu hiyo inategemea kwa mawaka mzima itaingiza kiasi cha  £420-430m, wakiwazidi kuwakaribia matajiri wenzao wa , Real Madrid and Barcelona.

USHIRIKINA KATIKA SOKA UPO HATA ULAYA ?



HEBU msomaji cheki jinsi wenzetu wa Ulaya wanavyofanya mambo yao ya kiufundi kistaili!
10. Paul Ince
Mtaalamu huyu wa zamani wa Man united, Liverpool na timu kadhaa nyinginezo alikuwa anahakikisha anakuwa wa mwisho kutoka katika chumba cha kubadilishia nguo katika kila mechi aliyocheza. Si hapo tu bali angesubiria hadi sekunde ya mwisho kabla mchezo kuanza ndipo angevaa jezi yake. Wadau hatujui hii ilimsaidia nini!
9. Laurent Blanc
Nani anakumbuka fainali za kombe la dunia mwaka 1998? Kama una kumbukumbu nzuri utajua kwamba beki wa zamani wa Ufaransa na kocha wa sasa wa timu hiyo hiyo laurent Blanc, alikuwa na utaratibu wa kubusu kipara cha kipa wao Fabien Barthez kabla ya kuanza kwa kila mechi. Sasa sijui alikuwa akionesha mapenzi yake kwa Barthez ama ilikuwa kwa ajili ya kupata bahati, ukweli ni kwamba ilisaidia kwani Ufaransa waliibuka mabingwa mwaka huo!
8. Steven Pienaar
Kila timu huwa na sala zao kabla ya mechi lakini mwaka huu timu ya taifa ya Sauzi Bafana Bafana ilitoa mpya pale wachezaji wote walipokuwa wakishika kichwa cha Steven Pienaar na kupeana maneno ya kutia moyo kabla ya kila mechi.
7. David James
Walinda milango huwa wanajulikana kwa kuwa watu wa ajabu. Kipa wa Uingereza David James ni mmojawapo wa watu hawa. lakini mwaka huu alizidi kipimo kwani alikuja na staili ya kujitupa na kudaka hewa kabla ya kila mechi akidai kwamba hii inamsaidia kujiweka fiti kabla mechi. Sisi tunajiuliza kwa nini adake hewa na asitumie mpira wa ukweli?
6. Johan Cruyff
Sasa hii hadi najisikia kucheka! Nguli huyu wa soka wa Uholanzi alikuwa mmojawapo wa wachezaji bora, kama si mchezaji bora kupata kutokea katika nchi ya Uholanzi. Lakini yaelekea ubora huo ulichangiwa na kitu fulani kwani jamaa huyu alikuwa ana tabia ya kumchapa bonge la kibao cha tumbo kipa wake na baadae kwenda kutema bigijii yake katika lango la timu pinzani kabla ya kila mchezo. Usiniulize maumivu aliyokuwa akipata kipa wake, si bora angembusu tu!
5. Bobby Moore
Nahodha wa timu ya Uingereza iliyokuwa mabingwa wa dunia mwaka 1966 alikuwa na katabia kamoja kakushangaza sana. Jamaa huyu alikuwa anahakikisha anakuwa wa mwisho kuvaa kaptula yake kabla ya mchezo. Na iwapo kama kuna mchezaji mwingine ataamua kubadilisha kaptula yake katikati ya mchezo, mtaalamu Bobby More atahakikisha anavua ya kwake na kuvaa tena.
4. Gary Lineker
Mmojawapo wa wafumania nyavu wakali kupata tokea katika timu ya Uingereza alikuwa akiwashangaza wengi pale alipokuwa akiepuka kabisa kufanya mazoezi ya kupiga mashuti kabla ya mechi. Alisema kwamba huwa hafanyi mazoezi ya kupiga mashuti sabau alikuwa hataki kupoteza magoli yake bure na alikuwa akiyahifadhi kwa ajili ya mechi. Hakuishia hapo tu mzee mzima kama hakupata bao katika dakika 45 za mwanzo alikuwa akihakisha anabadili jezi yake na kuvaa nyingine kuondoa nuksi.
3. Raymond Domenech
Kocha asiyeeleweka wa Ufaransa, Domenech alikuwa ana tabia ya kuchangua wachezaji kutokana na nyota zao. Kuna wakati kiungo Robert Pires aliachwa katika timu sababu alikuwa ana nyota ya Scorpio ama nge. Kajaribu vyote lakini kashindwa kusafisha nyota yake mwenyewe kwani hivi sasa anahaha kutafuta kibarua.
2. Adrian Mutu
Inasikitisha kuwa Mutu hatopata tena nafasi ya kufanya mambo yake ya kishirikina hivi karibuni sababu ya adhabu ya kisoka anayotumikia kwa ajili ya matumizi ya dawa za kulevya. Lakini enzi zake mtu huyu alikuwa akihakikisha anavaa chupi yake nje ndani katika mechi yoyote ile anayocheza. Alipoulizwa kwanini anafanya hivyo, Mutu alijibu kuwa kama hainiumizi kwanini nisifanye!
1. Shay Given
Kutakuwa kuna kitu tu nyuma ya magolikipa wa nchi ya Ireland, tukiangalia kipa wao wa zamani Pattie Booner ambaye alikuwa ana tabia ya kubeba kipande cha udongo katika mkoba wake wa glovu za kipa. Tukija kwa kipa wa sasa Shay Given ambaye huwa anahakikisha ana chupa ya maji matakatifu” nyuma ya goli lake kila wakati. Given alikuwa hachezi mechi bila chupa yake ya maji!Wabongo mpo hapo?