HEBU msomaji cheki jinsi wenzetu wa Ulaya
wanavyofanya mambo yao ya kiufundi kistaili!
10. Paul
Ince
Mtaalamu huyu wa zamani wa Man united, Liverpool
na timu kadhaa nyinginezo alikuwa anahakikisha anakuwa wa mwisho kutoka katika
chumba cha kubadilishia nguo katika kila mechi aliyocheza. Si hapo tu bali
angesubiria hadi sekunde ya mwisho kabla mchezo kuanza ndipo angevaa jezi yake.
Wadau hatujui hii ilimsaidia nini!
9. Laurent
Blanc
Nani anakumbuka fainali za kombe la dunia mwaka
1998? Kama una kumbukumbu nzuri utajua kwamba beki wa zamani wa Ufaransa na
kocha wa sasa wa timu hiyo hiyo laurent Blanc, alikuwa na utaratibu wa kubusu
kipara cha kipa wao Fabien Barthez kabla ya kuanza kwa kila mechi. Sasa sijui
alikuwa akionesha mapenzi yake kwa Barthez ama ilikuwa kwa ajili ya kupata
bahati, ukweli ni kwamba ilisaidia kwani Ufaransa waliibuka mabingwa mwaka huo!
8. Steven
Pienaar
Kila timu huwa na sala zao kabla ya mechi lakini
mwaka huu timu ya taifa ya Sauzi Bafana Bafana ilitoa mpya pale wachezaji wote
walipokuwa wakishika kichwa cha Steven Pienaar na kupeana maneno ya kutia moyo
kabla ya kila mechi.
7. David
James
Walinda milango huwa wanajulikana kwa kuwa watu wa
ajabu. Kipa wa Uingereza David James ni mmojawapo wa watu hawa. lakini mwaka
huu alizidi kipimo kwani alikuja na staili ya kujitupa na kudaka hewa kabla ya
kila mechi akidai kwamba hii inamsaidia kujiweka fiti kabla mechi. Sisi tunajiuliza
kwa nini adake hewa na asitumie mpira wa ukweli?
6. Johan
Cruyff
Sasa hii hadi najisikia kucheka! Nguli huyu wa
soka wa Uholanzi alikuwa mmojawapo wa wachezaji bora, kama si mchezaji bora
kupata kutokea katika nchi ya Uholanzi. Lakini yaelekea ubora huo ulichangiwa
na kitu fulani kwani jamaa huyu alikuwa ana tabia ya kumchapa bonge la kibao
cha tumbo kipa wake na baadae kwenda kutema bigijii yake katika lango la timu
pinzani kabla ya kila mchezo. Usiniulize maumivu aliyokuwa akipata kipa wake, si
bora angembusu tu!
5. Bobby
Moore
Nahodha wa timu ya Uingereza iliyokuwa mabingwa wa
dunia mwaka 1966 alikuwa na katabia kamoja kakushangaza sana. Jamaa huyu
alikuwa anahakikisha anakuwa wa mwisho kuvaa kaptula yake kabla ya mchezo. Na
iwapo kama kuna mchezaji mwingine ataamua kubadilisha kaptula yake katikati ya
mchezo, mtaalamu Bobby More atahakikisha anavua ya kwake na kuvaa tena.
4. Gary
Lineker
Mmojawapo wa wafumania nyavu wakali kupata tokea
katika timu ya Uingereza alikuwa akiwashangaza wengi pale alipokuwa akiepuka
kabisa kufanya mazoezi ya kupiga mashuti kabla ya mechi. Alisema kwamba huwa
hafanyi mazoezi ya kupiga mashuti sabau alikuwa hataki kupoteza magoli yake
bure na alikuwa akiyahifadhi kwa ajili ya mechi. Hakuishia hapo tu mzee mzima
kama hakupata bao katika dakika 45 za mwanzo alikuwa akihakisha anabadili jezi
yake na kuvaa nyingine kuondoa nuksi.
3. Raymond
Domenech
Kocha asiyeeleweka wa Ufaransa, Domenech alikuwa
ana tabia ya kuchangua wachezaji kutokana na nyota zao. Kuna wakati kiungo
Robert Pires aliachwa katika timu sababu alikuwa ana nyota ya Scorpio ama nge. Kajaribu
vyote lakini kashindwa kusafisha nyota yake mwenyewe kwani hivi sasa anahaha
kutafuta kibarua.
2. Adrian
Mutu
Inasikitisha kuwa Mutu hatopata tena nafasi ya
kufanya mambo yake ya kishirikina hivi karibuni sababu ya adhabu ya kisoka
anayotumikia kwa ajili ya matumizi ya dawa za kulevya. Lakini enzi zake mtu
huyu alikuwa akihakikisha anavaa chupi yake nje ndani katika mechi yoyote ile
anayocheza. Alipoulizwa kwanini anafanya hivyo, Mutu alijibu kuwa kama
hainiumizi kwanini nisifanye!
1. Shay
Given
Kutakuwa kuna kitu tu nyuma ya magolikipa wa nchi
ya Ireland, tukiangalia kipa wao wa zamani Pattie Booner ambaye alikuwa ana
tabia ya kubeba kipande cha udongo katika mkoba wake wa glovu za kipa. Tukija
kwa kipa wa sasa Shay Given ambaye huwa anahakikisha ana chupa ya maji
matakatifu” nyuma ya goli lake kila wakati. Given alikuwa hachezi mechi bila
chupa yake ya maji!Wabongo mpo hapo?
hayo mambo ya kawaida 2 ktk soka hmna jambo la ajabu kusema inahusiana na ushirikina, na kuhusu Blanc na Barthez hpo umechemka, Blanc alikua ana busu upara wa Brthez pindi atkapokua ameokoa mchomo hatari na c kua kabla ya mechi kuanza.
ReplyDeletejipange mjomba uckurupuke
hayo mambo ya kawaida 2 ktk soka hmna jambo la ajabu kusema inahusiana na ushirikina, na kuhusu Blanc na Barthez hpo umechemka, Blanc alikua ana busu upara wa Brthez pindi atkapokua ameokoa mchomo hatari na c kua kabla ya mechi kuanza.
ReplyDeletejipange mjomba uckurupuke
hata mbele yapo sio
ReplyDelete