Search This Blog

Saturday, August 6, 2011

OFFICIAL: PASTORE AKAMILISHA UHAMISHO WA PSG


Paris Saint –Germain wamekamilisha usajili wa Javier Pastore kutoka Palermo kwa dili lenye thamani ya €42million, klabu hiyo ya Ufaransa wamethibitisha kupitia mtandao wao rasmi.

Pastore amesaini mkataba wa miaka 5 na klabu hiyo iliyonunuliwa na Qatar Investment Authority.

Taarifa kutoka kwenye mtandao huo ilisema: “Javier Pastore amesaini mkataba wa miaka 5 na PSG.Atavaa jezi namba 27.Muargentina huyo atatambulishwa kwa waandishi wa habari Jumatatu jioni @ the Parc des Princes.”

MAMELODI: BOTSWANA INAPIGA HATUA BAADA YA KUWEKEZA KATIKA SOKA LA VIJANA


ASHFORD Mamelodi ni Ofisa Maendeleo wa FIFA kwenye Kanda ya Kusini mwa bara la Afrika. Nilikutana naye tukazungumza mambo mengi yanayohusu mchezo wa soka na namna unavyowezeshwa na FIFA, Serikali na shirikisho la soka la nchi husika. Mazungumzo yetu yalikuwa hivi:

Ashford wewe unatoka Botswana tungependa utufahamishe jinsi ligi ya huko inavyoendeshwa.
Ashford: Ligi ya Botswana bado sio ya kulipwa lakini lengo ni kujaribu na kuifanya iwe hivyo. Cha ziada ni kwamba ni ligi huru ambapo klabu zinaendesha ligi zenyewe na zinasaidiwa na shirikisho la soka kwenye mambo ya kiutendaji.

Klabu zinaendeshaje ligi zenyewe?
Kwa kila namna, zinatafuta wadhamini zenyewe, zinapanga ratiba zenyewe, kanuni na taratibu za mashindano; na sio vilabu vyote, vilabu vimejiwekea utaratibu ambapo ligi inaongozwa katika utaratibu unaoeleweka, kikubwa ni kwamba vilabu vinajengewa uwezo ambapo vyote vinapaswa kuwa vinajitegemea .

Kwa kutazama jinsi michuano ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Botswana iko kwenye nafasi nzuri na hii inaonyesha mmepiga hatua kisoka.
Naweza kusema kuwa Botswana imeendelea sana baada ya kuwa tumewekeza kwa vijana kwa miaka mingi. Nakumbuka kuwa tulimleta jamaa mmoja toka Ghana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi na katika kipindi hiki kulikuwa na mipango ya makusudi kabisa ya kuendeleza vipaji vichanga, kuwaendeleza makocha na mipango mingine mingi thabiti ambayo naweza kusema imesaidia sana.

Kwa hapa Tanzania tuna Mkururgenzi wa Ufundi ambaye machoni kwa wengi hafanyi wajibu wake ipasavyo, je, kwenu Botswana Mkurugenzi wa Ufundi ana majukumu gani?

Majukumu ya Mkurugenzi wa Ufundi ni rahisi sana; nayo ni kutekeleza mipango ya maendeleo; maendeleo ya soka kwa upande wa vijana, soka la wanawake na pia maendeleo ya makocha na anapaswa kuzingatia eneo hilo tu na si vinginevyo. Anahusika na kuunda au kubuni mifumo ambayo timu za taifa zitafaidika na jinsi wachezaji wapya wanavyopatikana lakini hiyo haimaanishi kuwa anahusika moja kwa moja na timu za taifa. Hiyo ni kwa sababu timu za taifa ni taasisi huru ambazo zinajiendesha zenyewe na makocha wake .

Wewe ni Ofisa Maendeleo wa FIFA, kuna huu mradi wa GOAL, unaweza kutueleza kuwa huu ni mradi gani?
Mradi wa GOAL ni moja ya mambo mengi ambayo yanafanywa na FIFA, GOAL ni mradi ambao FIFA imeuanzisha makusudi kabisa ili kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kwa mfano kuanzia mwaka jana FIFA imekuwa ikitoa miundombinu mbalimbali kama vile fedha taslimu Dola Laki Tano, ambazo kama shirikisho husika la nchi wanapaswa watoe maelezo juu ya matumizi ya fedha na miundombinu ambayo inatolewa na FIFA pamoja na kuonyesha jinsi nchi iliyopewa msaada inavyofaidika na miundombinu ya FIFA.

Je, nchi yako Botswana imefaidika kwa chochote kile na huu mradi wa GOAL.
Kabisa, kabisa. Botswana hivi tunavyozungumza imekamilisha kituo cha ufundi ambacho kina sehemu kama vile ofisi, sehemu kwa ajili ya masuala ya ufundi na tulikuwa na bahati kwa sababu kwenye mradi wa mwanzoni FIFA ilitoa Dola laki Nne ambazo serikali iliongeza fedha nyingine kiasi hicho na kufanya kiasi kuwa Dola laki Nane ambazo Botswana imefaidika nazo sana. Pamoja na fedha, serikali pia ilitoa ardhi ambayo ndio ilitumika kujengea jengo ambalo ndio makao makuu ya BFA yalipo, kumbi za mikutano pamoja na kituo ambacho kina viwanja pamoja na sehemu za kulala. Na kwenye mradi wa pili BFA ilijenga jengo ambalo liko kama hoteli ya kitalii ambalo linaweza kutumika hata na timu ya taifa pale inapoweka kambi.
Kwenye swali la awali ulitueleza kuwa mradi wa GOAL ni moja kati ya miradi mingi, unaweza kutueleza chochote kuhusu miradi mingine pembeni na huo?
Kuna maafisa 12 wa maendeleo ya soka ulimwenguni kote na wote hawa wana eneo la kijiografia ambalo wanafanya kazi na sisi ni mawakala wa FIFA linapokuja suala la maendeleo na hii inamaanisha kuwa pale ambapo FIFA inataka kuingilia kati mradi wa maendeleo kwa kawaida inakuwa jukumu letu kuhakikisha mradi huu unasimama. Kazi yetu ni kuhakikisha kuwa misaada yote inakuwa sawa pamoja na miundo mbinu yote inayohusika. Kwa ujumla tuna jukumu la kusaidia vyama husika vya soka kuendeleza mchezo huu lakini vyama ndio vinakuwa mstari wa mbele, vinatakiwa kuwa na falsafa ambayo inalenga kwenda mbele na sisi tunakuja kama wasaidizi wawezeshaji.

Kombe la Dunia lililochezwa Afrika Kusini mwaka jana lilikuwa kama baraka kwa mchezo wa soka barani Afrika, nchi yako Botswana imefaidika vipi na Kombe la Dunia la kwanza barani Afrika?
Ashford: Ni vigumu kueleza moja kwa moja jinsi nchi ilivyofaidika lakini nadhani kwa Waafrika wote ambao walikuwepo watashuhudia kuwa kila Mwafrika alifaidika na Kombe la Dunia lakini kwa upande wa FIFA tulikuwa na kaulimbiu ambayo inasema ‘WIN IN AFRICA WITH AFRICA’ yaani ‘SHINDA AFRIKA NA AFRIKA’ ambapo FIFA ilitenga kitita cha fedha kiasi cha Dola milioni 7 za Kimarekani ambazo zilililega kuendeleza soka barani Afrika baada ya Kombe la Dunia kwa kuwa hili ni Kombe la Dunia la kwanza Afrika na wazo lilikuwa kuacha kumbukumbu ya tukio hili. Fedha hizi zilitumika katika vitu mbalimbali kwa mfano viwanja ambapo kila moja kati ya nchi 53 za Afrika zilisaidiwa kuendeleza viwanja husika ambapo kila kiwanja kiligharimu Dola Laki Saba. Hii ilikuwa moja; pia tulikuwa na issue ya uongozi wa vilabu, tumefanya semina mbalimbali ambapo tuliweka azimio ambapo tumemua kuwa ni lazima ligi mbalimbali barani Afrika ziendeshwe kwa mfumo wa professional. Kimsingi ni kwamba fedha hizi ni nyingi sana na bara la Afrika limefaidika na fedha hizi na Kombe la Dunia kwa ujumla.

FIFA wana sera ambayo inapiga marufuku serikali kuingilia masuala ya soka, sera ambayo imekuwa ngumu kidogo kwa Afrika kuzingatia, vipi kwa Botswana imekuwa vigumu kama sehemu zingine au imekuwaje?

Ashford: Bostwana wamejitahidi sana kuzingatia kanuni hii na FIFA haina huruma katika suala hili, kumbuka kuwa serikali si mwanachama wa FIFA, mwanachama ni shirikisho ama chama, tumejaribu kuhakikisha kuwa shirikisho liko huru kujiendesha lenyewe kwa uhuru, japo kwetu serikali ni mdau mkubwa wa masuala ya michezo, hivyo ule mwingiliano ambao ni wa hasi, yaani mzuri haukatazwi lakini si mwingiliano chanya, huo ndio FIFA inaupinga.

Unazungumziaje mchango wa rais wa FIFA Sepp Blatter kwa mchezo wa soka barani Afrika.
Sepp Blatter amekuwa na baraka kwa soka letu, amekuwa msaada mkubwa sana, kumbuka kuwa haya maendeleo yote tunayozungumza, ‘goal project’ na mengineyo ni mawazo yake, ni yeye aliyeanzisha, ametuunga mkono sana, ni yeye alihakikisha kuwa Kombe la Dunia linakuja Afrika kwa mara ya kwanza na bado anaendelea, nadhani tuna deni la shukrani kwa mtu huyu kusema kweli.

JUMA JABU AITWA STARS, 37 SERENGETI BOYS WAITWA MAZOEZINI

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaita kwenye kikosi hicho wachezaji Juma Jabu kutoka Simba na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ wa Azam kwa ajili ya mechi ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wachezaji hao wameitwa kuchukua nafasi za Amir Maftah wa Simba na Nurdin Bakari wa Yanga ambao ni majeruhi. Mechi ya FIFA dhidi ya Sudan ‘Nile Crocodile’ itafanyika Agosti 10 mwaka huu jijini Khartoum na timu inatarajiwa kuondoka Agosti 8 mwaka huu kwenda huko.

Stars hivi sasa inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo ni moja ya maandalizi kabla ya Septemba 3 mwaka huu kuivaa Algeria ‘Desert Warriors’ jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya mchujo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Gabon na Guinea ya Ikweta.

37 SERENGETI BOYS WAITWA MAZOEZINI
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Kim Poulsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo wameita wachezaji 37 kwa ajili ya mazoezi kujiandaa kwa michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Michuano hiyo imepengwa kufanyika Nairobi, Kenya mwishoni mwa mwezi huu ingawa bado CECAFA haijatoa uthibitisho wa kuwepo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuanza mazoezi ya asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam siku ya Jumatatu (Agosti 8 mwaka huu).
Walioitwa ni Hamad Hamad (Skaba FC), Aishi Manula (Serengeti Boys), Mwalo Ilunga (Saigon), Mgaya Jafari (Sifa United), Ismail Gambo (Kioma United), Miraji Selemani (Mwere Kids), Mohamed Mohamed (Moro United), Pascal Matagi (Agram), Hussein Ibrahim (Moro), Selemani Bofu (Makongo Sekondari) na Mudathiri Abbas (Orange Academy).
Maulid Mwishere (Kombora), Clever Mkini (Matembe), James Mganda (Morogoro), Mohamed Kharabu (Avizona), Faridi Shah (Amani Centre), Mbwana Hassan
Champion), Idrissa Said (Amana), Michael Mpesa (Nyanda), Awadh Rashid (Alkadir), Joseph Lubasha (Villa Squad), Salvatory Nkulula (Red Star), Godson Naftal (Visanakabulu), Ismail Moshi (Orange Academy), Basil Seif (Kinondoni), Mustafa Rashid (Ruvuma), Thabit Kinyunyi (Ruvuma), Seleman Jumanne (Mara), Hassan Ally (Mara), Peter Manyika (Jitegemee), Mohamed Hassan (Mbande), Joseph Seleman (Jitegemee), Rajab Mwalimu (Kinyerezi), Bakari Ally (Twiga), Hassan Twiga (Twiga),

MATCH CENTER: ITALY SUPER CUP MILAN 2 - 1 INTER

WESLEY SNEIJDER AWATANGULIZA INTER - ITALY SUPERCUP

Kikao cha vilabu na tff chashindwa kufanyika ...

Leo kulikuwa na kikao kati ya TFF na Vilabu 14 vitakavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom Msimu ujao,
Cha kustaajabisha kikao hicho kimeshindwa kufanyika baada ya viongozi wa vilabu vinane kushindwa kuudhulia kikao hicho.
Viongozi waliohudhulia wametoka vilabu vifuatavyo:
African Lyon,Mtibwa Sugar,Kagera Sugar,Jkt Ruvu,Ruvu Shooting na Moro UTD.
Kikao hicho kilikuwa ni kwa ajili ya kuzungumzia namna ligi ya msimu ujao itakavyoendeshwa.

BORA TFF MUENDELEE NA LIGI YENU INAVYOONEKANA VILABU VYENYEWE HAVIJAWA TAYARI KUENDESHA LIGI YAO.

BUNDESLIGA 2011/12 YAANZA RASMI: Dortmund yaanza vyema kuutetea ubingwa wake













Mabingwa watetezi wa taji la BUNDESLIGA timu ya Borussia Dortmund imeanza vizuri kampeni yake ya kuutetea ubingwa wake baada ya kuifunga Hamburg mabao 3-1 hapo jana usiku.



Kevin Grosskreutz akifunga bao la kwanza la msimu wa 49 wa Bundesliga dakika ya 17 pia akaongeza la pili dakika ya 48 na Mario Goetze akifunga lingine dakika ya 28 na kukamilisha ushindi huo mnono.

OBERTAN KUJIUNGA NA NEWCASTLE JUMATATU


Winga wa kifaransa anaichezea Manchester United Gabriel Obertan amekubali dili la mkataba wa miaka 5 wa kujiunga na Newcastle United kwa ada ya uhamisho wa unaofikia £3million.

Obertan ambaye tangu January mwaka huu alikuwa yupo sokoni atajiunga na Newcastle United Jumatatu ijayo, baada ya kukamilika kwa mazungumzo binafsi kati yake na Newcastle.

SCHOLES AWAAGA UNITED NA BAO

Kiungo wa kimataifa wa England Paul Scholes jana usiku alicheza yake ya mwisho akiwa kama mchezaji wa Man United dhidi ya New York Cosmos.United walishinda kwa mabao 6-0, huku Scholes akifunga moja kati ya mabao hayo katika mechi hiyo iliyochezwa @ theatre of dreams Old Trafford.
DESPIDIDA(GOODBYE) THE LEGEND, WE WILL BE MISSING U.








Friday, August 5, 2011

ratiba ya raundi ya tatu uefa champions league yatoka..




League route

Odense v Villarreal
Twente v Benfica
Arsenal v Udinese
Lyon v Rubin Kazan

Bayern Munich v Zurich

Champions Route
Wisla Krakow v APOEL
Maccabi Haifa v Genk
Dinamo Zagreb v Malmo
BATE v Sturm Graz
Copenhagen v Viktoria Plzen

AZAM YAILIPA TP MAZEMBE KWA KUWA NA GYM YA KISASA....

Huyu ni mtaalam wa mazoezi ya gym wa Azam. Huyu jamaa anatokea nchini Finland ameletwa kwa kazi maalum ya kuwajenga wachezaji wa Azam



hiki ni kikosi cha vijana cha Azam mara baada ya mazoezi magumu.


vyumba vya kulala



Kiungo wa Azam Fc Abdulhalim Humoud akiwa kwenye kiwanja cha Azam,


































CRISTIANO RONALDO AMAZING GOAL

INTER VS MILAN

MMEPENDEZA SANA !!!


mmmhhhh haya MAZOEZI ni ya kujiandaa na nini ?
hawa ni wachezaji wa AC Milan wakiwa mazoezini kujiandaa na msimu ujao..


ENZI HIZO!!!

PIGA MAKOFI TAFADHALI-METHOD MOGELLA ' FUNDI', ABEID MZIBA,SAID MWAMBA 'KIZOTA' HAMIS TOBIAS GAGA ( kwanza kushoto )....tusaidiane kuwatambua wengine hapo..



Haidary Abeid Akiwatambulisha wachezaji wa Simba kwa Mgeni wa heshima.

msaada wa majina mengine jamani.....



XAVI HERNANDEZ: MCHEZAJI KAMA MIMI NI HATARI NA NAJIFANANISHA NA UKUTA ULIOJENGWA KUZUIA MAFURIKO

XAVI Hernandez anazungumza kwa tabasamu la furaha na kujiamini yeye ni wa kipekee. Anapenda mpira ndiyo maana wikendi moja alikwenda Italia kushuhudia mechi ya Sampdoria na Juventus ingawa hakufurahishwa na mchezo uliochezwa.
Lakini Xavi ambaye ni mchezaji miongoni mwa wachezaji watatu bora wa Dunia, anaamini kuwa aina ya mchezo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ndiyo bora zaidi duniani kwa sasa.
Lakini ni mchezaji anayetoa heshima kwa wenzake. Xavi anasema kuwa nyota kama Paul Ince, Paul Scholes, Michael Carrick, Roy Keane, John Terry na Jammie Carragher ni bora na anawaheshimu sana.
NINI SIRI YA MAFANIKIO YAKO?
“Kujiamini, kufanya mazoezi ya kutosha, kupokea ushauri, kupumzika pia kupokea mafundisho sababu nina ‘enjoy’ mpira kote Barcelona hadi katika timu ya taifa. Pia nidhamu ni jambo la msingi. Pia naamini kuwa makocha wote wa Hispania wana falsafa moja ya mchezo (kucheza kwa tabasamu)”

JE UNA NAFASI YA KUCHEZA ENGLAND?
“Mchezaji huweza kucheza mahali kokote, ila inategemea na kuzoea aina ya mchezo wa sehemu husika. Xabi Alonso na Mikel Arteta wanaweza kuwa mfano mzuri wamefanikiwa kucheza England na wamefanya vizuri”


UNAZUNGUMZIAJE TUZO ZILIZOPITA ZA MCHEZAJI BORA WA DUNIA?
“Ninasikitika sikushinda lakini sikuwa wa kwanza mimi kushindwa. Naheshimu maamuzi ya majaji”

UNAFIKIRIA KUACHA KUICHEZEA BARCELONA?
“Hapana, navutiwa sana na soka la Barca ila pia napenda changamoto ya kucheza mazingira tofauti tofauti”

HATA KUCHEZA ENGLAND?
“Ndiyo, sipendi soka la Italia ila napenda soka la England na naipenda Manchester United kwani ina soka la ‘ajabu’ pia navutiwa na mashabiki wa England ambao wanashangilia kwa nguvu ukilinganisha na vilabu vya Hispania, kwani mashabiki kama wa Espanyol, Atletico Madrid na Sevilla huwa wanashangilia kwa kupiga sana kelele”
UNAHISI NINI KUHUSU UMAARUFU WAKO?
“Najisikia faraja kujulikana duniani kote kama mastaa wengine waliopita, na najivunia kuwepo Barcelona, watu wananichukulia mimi kama mfano hapa Catalunya na La Masia. Pia kocha Vicent Del Bosque anavutiwa na tabia yangu ya kutozungumza na vyombo vya habari, Frank Benckerbeur na Michael Platini (Rais wa Uefa) wanapenda nidhamu yangu”

UNAMZUNGUMZIAJE PEP GUARDIOLA?
“Umesema Guardiola?...Pep ni kocha mwenye msimamo ana miaka mitatu tangu awepo hapa kama kocha na wakati anasaini mkataba alisema amekuja kuipaisha Barcelona. Pep ni kocha mwenye kutaka kazi yake ikamilike pia anachukia mtu mzembe na anataka utimamu wa mwili na akili kwa kila mchezaji”

UNADHANI PEP ATAFANIKIWA AKIPEWA TIMU ENGLAND?
“Ndiyo, sababu Pep ana kipaji cha kufundisha timu yoyote atakayopewa”

NI KWELI UJUZI WA PEP NA SAPOTI YA MASHABIKI WENU NDIYO INAFANYA MUONEKANE BORA?
“Ni kwamba kuwa bora hutambulishwa na matokeo bora KWAMBA KUWA BORA, fikiria kuwa Guardiola asingekuwa na matokeo bora basi na wapenzi wasingemuona bora ….Mchezaji bora ni yule anayefanya kazi na kocha bora”







UNAZUNGUMZIAJE LA MASIA?
“Wachezaji wote wa Catalunya lazima wapitie La Masia kwani shule hii huzalisha aina bora ya soka Duniani—mfano mzuri ni Sergio Busquets ambaye ni kiungo bora katika pasi za one-two na ni kinda mwenye rekodi za ajabu kutoka La Masia…..La Masia ni chuo bora zaidi ya kile cha Ajax Amsterdam ambacho kiliwaibua nyota kama Johan Cruffy”

KUNA CHANGAMOTO GANI CAMP NOU?
“Changamoto zipo na uwepo wangu tu na uwezo wangu uwanjani unanipa mataji nikishirikiana na David Villa, Leo Messi, Busquets, Inesta na timu nzima ya Barcelona, kwa sasa sina wasiwasi sana na nafasi yangu labda vijana wa kutoka La Masia watakapokuja hapo baadae, lakini si kwa wachezaji wa sasa wa Barcelona”

Thursday, August 4, 2011

FINALLY DADDY IS AT HOME




Steven Gerrard ameruhusiwa kutoka leo jioni na amepokelewa na mkewe Alex ambaye ni mjamzito pamoja na watoto wake wawili wa kike.


Gerrard alilazwa hospital toka last weekend baada ya kupata infection katika korodani, sehemu ya mwili ambayo alifanyiwa operation last year.





Gerrard ambaye hajaichezea timu yake ya Liverpool toka mwishoni mwa msimu uliopita, anatarajiwa kurudi dimbani mwezi September, miezi miwili kabla ya mkewe kujifungua mtoto wa 3.


Welcome Home Kapteiiiiiiiiiiiiiiin.


UNAWAKUMBUKA HAWA JAMAAA ,KAMA UNAWEZA ORODHESHA MAJINA YAO...








ARSENAL KUWEKA USAJILI WA FABREGAS BARCA SHAKANI


Arsenal wanaweza kuuweka hatarini usajili wa Cesc Fabregas kwenda Barcelona kwa kutaka kumchezesha nahodha wao katika Champions League play offs.

Mabingwa wa ulaya ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimtaka Fabregas lakini wamekuwa wakishindwana na Arsenal katika ada ya uhamisho, na sasa mambo yanaonekana kuzidi kuwa magumu baada ya Arsenal kuanza kufikiria kumtumia Cesc katika hatua za mwanzo za ligi ya mabingwa, hatua ambayo itamuweka Fabregas nje ya michuano hiyo ikiwa atajiunga na Barcelona kutokana na sheria ya kukataza kuchezea timu mbili tofauti katika msimu mmoja wa Champions League.

Gunners watafahamu ni wachezaji gani watakaoshiriki katika play offs kesho ijumaa, huku Samir Nasri, mchezaji mwingine anayetaka kuondoka Emirates na Robin Van Persie wakiwa wamesimamishwa na UEFA.

MBWANA SAMATTA AKIFANYA MAMBO YAKE.

MBWANA SAMATTA AZIDI KUNG`ARA TP MAZEMBE.

Amini usiamini ‘MISUMARI’ kwenye mchezo wa soka ipo!

Hizi ni malighafi zinatumika kutengenezea dawa...

suala la misumari limehalalishwa na viongozi wa soka hapa nchini..hayo ni maneno ya mganga maarufu hapa jijini Dar es Salaam kwa kuucheza mchezo nje ya uwanja, amejitambulisha kwa jina la sheikh Omary Alhad amefunguka na kulielezea suala hili kwa kina.
Sheikh Omary emezicheza mechi nyingi sana na amezifanyia kazi karibia timu zote za Dar Es Salaam.
Kila msimu huwa na timu moja ambayo husafiri nayo kila mahala iendako kucheza mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara au Visiwani.
Akafunguka kwa kusema yeye ni shabiki wa kutupwa kabisa wa klabu ya Yanga, na akasema kuwa suala la yeye kuwa shabiki wa Yanga halimzuii kuifanyia kazi timu pinzani.
‘’huwa naumia sana roho pindi napoishuhudia Yanga inafungwa tena na timu niliyoifanyia kazi ‘’.
Mechi ambayo hawezi kuisahau miongoni mwa mechi zote alizowahi kuzicheza ni mechi baina ya timu moja kutoka mkoani Mbeya ambayo imeshuka mwaka mmoja au miwili iliyopita dhidi ya timu moja ambayo HAIPENDI kabisa kutoka Dar es salaam,mechi hiyo ilikuwa ngumu kwasababu timu iyo ya Dar kila mara ilipoenda Mbeya ilikuwa ikichezea vichapo,mazingira ya utendaji yalikuwa magumu kwasababu kila upande ulifanya maandalizi kabambe,mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.



Sheikh Omary Alhad akifanya mahojiano na Issa Maeda




Sheikh omary anasisitiza huwa hapendi kushirikiana na mtu pindi anapokuwa kazini,Kila mtu ana kanuni zake za utendaji, mimi kanuni yangu nataka nikiwa napiga ‘misumari’ niwe peke yangu sipendi kuchanganya utendaji wangu na wengine, nikichanganya mkono na mtu huwa sipati mafanikio nakumbuka miaka minne iliyopita timu moja kutoka kisiwani Pemba iliyopanda kwa kasi sana ila kwasasa imepotea, watu wa michezo mtaikumbuka na pemba inasifika kwa mambo haya, nilipelekwa kisiwani pemba niisaidie timu hiyo kupanda daraja kitu tulichogombana ni hicho cha kuchanganya madawa.
Kwani viongozi wa timu hiyo walitaka nishirikiane na wataalam kutoka Pemba kitendo ambacho binafsi sikuwa tayari.
ITAENDELEA….
Sikiliza pia Sports Xtra ya CLOUDS FM kila siku kuanzia saa tatu kamili usiku ili umsikie Sheikh Omary Alhad akiizungumzia ‘misumali’ michezoni.
NB
Misumari ni neno maarufu kwenye mchezo wa soka hapa nchini Tanzania likimaanisha KUROGANA.

CANTONA: SNEIJDER NI ERIC MPYA


Manchester United icon Eric Cantona amemsisitiza Sir Alex Ferguson kumleta Wesley Sneijder Old Trafford huku amkisifia kiungo huyo wa Inter Milan kwa kusema, “Sneijder ni Eric Cantona mpya”.

Mfaransa huyo ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa soka katika klabu ya New York Cosmos, yupo jijini Manchester kushiriki katika mechi ya kumuaga Paul Scholes kesho Ijumaa, na sasa anaungana na Scholes ambaye juzi alimsifia Sneijder kama mchezaji sahihi kumrithi kutokana na mchezo wake wenye akili na maarifa.King Eric alikaririwa akisema: “Sneijder ni mtu ambaye Manchester United inahitaji.Hakuna mchezaji kama yeye kwa sasa, ana nguvu, muda mwingine ananikumbusha kuhusu Eric wa zamani.”

UJUMBE TOKA KWA MDAU Patrick Semiono

Salaam mkuu,,
Pole na majukumu na hongera sana katika suala zima la kusogeza gurudumu la tasnia ya michezo hapa nchini mahususi soka kama mchezo wenye mashabiki wengi.
Natumai jina ni geni kwako lakini mie na wewe tunajuana sana haswa leaders club kwenye mabonanza ya kusukuma gurudumu la afya za wanamichezo wa zamani kabla sjahamia Loliondo kimajukumu.

Kusudio haswa la kukuandikia barua pepe hii ni kutaka kuchukua hatua za ulazima katika suala lilitokea jana la TBL kudhamini Klabu kongwe za Simba na Yanga.
Soka la sasa ni kweli laendeshwa kifedha zaidi lakini nataka niende juu ya upeo wa fikra za kawaida(beyond normal thinking) katika kuona hasara za udhamini wa TBL katika kuua soka la Tanzania.
Klabu za Simba na Yanga ni moja ya vilabu vilivyokaa mda mrefu bila mafanikio kuliko vilabu vyovyote katika Afrika Mashariki na Kati kulingana na umri ulionao.Klabu zenye umri sawa nazo ni El marrek na El hilal ya Sudan ambazo zimefanya mambo mengi nchini mwao na Afrika kwa ujumla.
Pamoja na udhamini kadha wa kadha (vodacom,kilimanjaro,magazeti) klabu za Simba na Yanga zimekuwa zikifanya vibaya kwenye mashindano makubwa na mbaya zaidi wadau(mashabiki na viongozi)wanadhani ni bahati mbaya kumbe ni uhalisia vilabu hivyo haviwezi kuleta medali zaidi ni majungu ya soka.

Arsenal ni klabu ambayo haijachukua kombe lolote zaidi ya miaka sita lakini kwenye viwango vya Fifa ni klabu ya 5 kwa ubora,unajua ni kwanini!?ni uwezo wa klabu husika kushiriki katika michuano,wanachama,malengo,uwezo wa uwanjani katika uchezaji na faida inayopatikana.Hata nchi ya Holland haijawahi kuchukua kombe la dunia ila uwezo wa kuushiriki unaifanya nchi hiyo isitoke 5 bora kwa mlongo mzima sasa.
Kumbe kuchukua kombe si silaha pekee ya mafanikio hata uwezo waushiriki hufanya klabu kuwa bora.Kwa mlongo sasa klabu za SImba na Yanga ni klabu za hatua za mwanzo katika michuano ya kimataifa.Na hamna mwaka tunaokosa visingizio achana na ndoto za kombe.

kuwalundikia vilabu hivi udhamini ili viongozi wao watajrike ni kuua Klabu nyingine kutokana na sababu zifuatazo:-
1.Kila mchezaji nchi hii atakuwa na malengo ya kucheza Simba au Yanga kwa sababu ndio klabu zenye uwezo wakati wanaenda kuua vipaji vyao.kumbuka wachezaji wa timu za mikoani wanashindwa kukaa katika vilabu vyao ugumu wa maisha,mfn AFC Arusha

2.Wimbi la uongezekaji wa rushwa lazima liongezeke kwani tofauti ya klabu za Vilabu hivyo na vilabu kama Villa Squad,Toto Africa utakuwa mkubwa na hamna mchezaji atakayekataa hongo nzuri kwa mapenzi ya soka wakati hana hela mfukoni.Mfn Siang'a alishairi hajui uwezo wa wachezaji wake kutokana na ununuzi wa mechi.

3.TFF ilishakiri haina uwezo wa kupandisha timu nyingi ligi kuu kwani nyingi hazina uwezo kiuchumi,kwahiyo tutabakia kuona klabu tajiri na si vilabu vyenye uwezo wa soka

Wasiwasi wangu ni kuwa fedha hizo ni asilimia 10% zitanufaisha wachezaji zilizobakia ni wajanja wa vilabu,kama huamini kawaulize wachezaji wa simba walipata Tshs ngapi baada ya mechi na TP Mazembe wakati klabu llilingiza mil 202 baada ya mgao.Je ni Kaburu na Rage walijaza mashabiki lukuki Taifa!? sjui

Sina nia mbaya na TBL ila kuna ulazima TFF kusimammia udhamini ili tuone vipaji vingine,angalia JKT ruvu na Mtibwa zilivvyolisha Simba na Yanga mafundi,lakini zisipopewa udhamini klabu hizo zitakufa na tutakosa mafundi kama ilivyokufa prosons na hatuoni tena Primus Kasonzo,Oswald Morris na Henry Morris,Godfrey Bonny'Ndanje'.

Mbona Zanzibar huwezi sikia Safari lager inadhamini michuano?ni sheria zinalinda,basi hata udhamini nao ungelenga na gaiwo kwa vilabu vingine tuone ushindani wa kweli kama msimu wa ligi ya 2010/2011

Kuna ulazima ya kikao cha wanahabari wa tasnia ya michezo kutoka vyombo tofauti kuufacha kikao na TFF,kam watafunga masikio ni sawa ila ujumbe ufike

Mtiifu wa soka bongo,
Patrick Semiono

Vita , Amani na Kombe la Dunia.


Kikosi cha sasa cha Ethiopia...
Hakuna kinachovutia vyombo vya habari kama habari zenye zengwe ndani yake , hakuna , ni zengwe mwanzo mwisho . Chochote kinachohusu eneo linalofahamika kijiografia kama pembe ya Afrika kwa wiki chache zilizopita kimetawaliwa na ishu ya janga la njaa linaloikabili sehemu hiyo . Janga hili linasemekana kuwa kubwa kuliko yote yaliyowahi kuikumba Afrika kwa takribani miaka 60 iliyopita . Eneo la mashariki mwa Ethiopia lina wakazi wengi ambao wana asili ya kisomali na watu hawa wamejenga uhasama kama si utani wa soka ambao umekuwa upinzani mkubwa na wenyeji wao ambao ni waethiopia . Hili ni jambo geni kidogo na ilipofanyika ‘draw’ ya michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 upinzani huu ulichagizwa pale ambapo Ethiopia na Somalia walipojikuta wakikutana . Hakika wapangaji wa ratiba hiyo hawakuwa wanajua ni uhasama wa aina gani umefufuliwa kwa draw ile ya kuwaweka wasomali na waethiopia kwenye mchezo mmoja .

kikosi cha kale cha Ethiopia
Somalia si mpinzani mkubwa wa Ethiopia kwenye soka , wapinzani wa Ethiopia kwa miaka mingi wamekuwa Sudan , Uganda na hivi karibuni Rwanda. Ila wasilojua wengi ni takwimu isemayo kuwa Ethiopia haijawahi kuwafunga wapinzani wao toka mashariki mwa nchi yao Somalia tangu mwaka 2004 na waethiopia siku zote wamekuwa fasta kutoa sababu ya kutowafunga wasomali wakisema kuwa timu yao ( Ethiopia) imekuwa haina umoja na sio kwa sababu Somalia ni timu bora kuliko Ethiopia .



Kikosi cha sasa cha Somalia..

Timu ya taifa ya Ethiopia maarufu kama Waliyas iliwahi kutwaa ubingwa wa CECAFA CHALLENGE mwaka 2003 . Katika mafanikio hayo waliongozwa na Asrat Haile kocha mwenye mafanikio kuliko wote kwenye soka la nchini Ethiopia . Mwaka mmoja baada ya kutwaa ubingwa wa CECAFA Asrat aliondolewa kama kocha mkuu na kupewa jukumu la kuwa msaidizi wa kocha wa Kijerumani Johan Figge. Asrat aliweka wazi kuwa asingeweza kufanya kazi chini ya Mjerumani huyo na ‘beef’ hili lilihamia kwa wachezaji ambao wengi wao walichukua upande wa Asrat .
Katika kipindi cha ugomvi huu baina ya Asrat na Johan ikaja mechi dhidi ya Somali na athari zake zilionekana kwani Ethiopia walifungwa na hii ilikuwa ishu kubwa kwenye nchi zote mbili .


Kikosi cha kale cha Somalia
Somalia na Ethiopia wamepigana vita kuu mbili katika historia yao kwenye miaka 1964 na mwaka 1977 na kwa sababu hiyo wamekuwa na uhusiano mbaya kweli kweli . Miaka miwili baada ya Somalia kuwafunga Ethiopia wasomali waliingia kwenye vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe . Majeshi ya Ethiopia yalivuka mpaka wa Somalia na ugomvi baina ya nchi hizo mbili ukaibuka tena . Tangu mchezo wa mwisho ambao Somalia ilishinda timu hizi hazijakutana tena kwenye mechi ya soka na watakapokutana kwenye mechi ya kufuzu kombe la nyasi zitawaka moto .

Roberto Baggio: Na.10 bora kutokea Italia

HII ILIKUWA NI BAADA YA KUPAISHA PENALTI KWENYE MCHEZO WA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 1994 DHIDI YA BRAZIL.

KWA watu wengi, anaonekana kuwa mtu wa ajabu kwa jinsi alivyoishika dini yake ya Budha, katika taifa la Kikatoliki, lakini kwa Wataliano, huwaambii kitu kwa shujaa wao huyu wa kombe la Dunia.

Roberto Baggio, alikuwa mtu tofauti; siyo tuu mchezaji aliyejaaliwa kipaji cha hali ya juu, lakini pia mtu wa mikasa. Maisha yake kama mwanasoka yalikuwa ya kushangaza sana.

Tunamzungumzia mchezaji ambaye uhamisho wake toka klabu moja kwenda nyingine ulikuwa ukigubikwa na migomo na vurugu toka kwa mashabiki wake waliokuwa hawaambiwi kitu juu ya mwanandinga huyo aliyependa sana wanyama.

Alikuwa hatulii kwenye timu moja, lakini ukizungumzia maisha yake ya kiimani, alikuwa na msimamo usiobadilika. Alijiunga na imani yake ya Kibudha tokea akiwa na miaka 15.

Kati ya mwaka 1982 na 2004, Baggio alifunga mabao 317 katika michezo 697, mengine akifunga toka katikati ya kiwanja kama alivyowafanya Czechoslovakia kwenye fainali za kombe la Dunia za mwaka 1990 ambayo yanabaki kuwa alama ya matukio ya kuvutia kati ya mchezo wa mpira wa miguu duniani.

Lakini mikasa yake ya kuvutia haikuwa kwenye mafanikio pekee, bali hata katika maanguko, kama pale alipokosa penati wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya Brazil mwaka 1994. Historia inatuambia kwamba ilikuwa ni penati ile iliyoikosesha Italia kikombe, ingawa Franco Baresi na Daniele Massaro walipoteza mikwaju yao hapo awali.

Taswira ya Baggio akiwa ameweka mikono yake kiunoni na kichwa chini, wakati huohuo akionekana mlinda mlango wa Brazil, Claudio Tafarel akiwa amepiga magoti akinyoosha mikono juu kumshukuru Mungu; ni mojawapo ya taswira za kukumbukwa katika historia ya soka.

Taswira hii inaonyesha tofauti kati ya mafanikio na kushindwa, ushindi na kukata tama. Hii ni taswira ambayo Baggio ametumia maisha yake yote akijaribu kuifuta.

Lakini katika wakati huo wa upweke na mazingira magumu, baada ya mashindano ambayo twaweza kusema kuwa Baggio alitoa mchango mkubwa sana kuwafikisha fainali, kuna mengi ambayo yalikuwa yanavutia kuhusu Baggio.

Uchezaji wake mahiri, usiohitaji kutumia nguvu kama wachezaji wengi kipindi hicho, ndio uliokuwa ukiwavutia watu kwake. Alikuwa na uwezo wa kuwachezea mabeki wa timu pinzani kwa jinsi anavyotaka yeye. Hata ilifikia kipindi kuna waandishi wa vitabu nchini Italia walitunga vitabu vinavyoelezea nywele za Baggio kuwa ni “nywele zenye utukufu”.

Katika miaka yake 22 ya kisoka, Baggio alichezea timu ya taifa ya Italia mara 56 akipachika mabao nyavuni katika fainali tatu mfululizo za kombe la Dunia. Aliwahi kuchezea vilabu saba: Vicenza, Fiorentina, Juventus, AC Milan, Bologna, Inter Milan na Brescia.

Alifanikiwa kubeba vikombe viwili vya ubingwa wa ligi ya Italia, kombe moja la UEFA na kombe moja la ligi nchini Italia. Kuna wachezaji wengi wa Kiitaliano wenye CV kali kupita hii, lakini wako wachache waliopendwa kama Baggio.

Muulize Muitaliano yoyote kuchagua mchezaji wa Kiitaliano mwenye kipaji kuliko wote na wengi watakwambia kuwa ni Baggio. Wazee wa zamani wachache watamchagua kiungo wa zamani wa Kiitaliano aliyecheza soka huko miaka ya sitini aitwaye Gianni Rivera. Wale waliokula chumvi zaidi watakwambia Giuseppe Meazza mtaalamu wa miaka ya 30 an 40 huko. Lakini kuna mwandishi mmoja wa soka ambaye alipata bahati ya kuwaona wachezaji wote hawa watatu wakisakata kabumbu na yeye alikubali kuwa Baggio yuko mstari mmoja na kina Rivera na Meazza.


Katika misimu yake mitano akichezea Juventus, kuanzia mwaka 1990 hadi 95, Baggio alikuwa akifananishwa na Michel Platini kila mara. Ingawa ufananisho huu haukukubalika na Platini mwenyewe. Baggio naye alikuwa akivaa jezi namba kumi mgongoni kama Platini na mastaa wengine wa soka.

Lakini cha kufurahisha, Platini alinukuliwa akisema, Baggio si namba kumi halisi bali ni namba tisa na nusu. Platini anasema hakutamka hivyo kumkashifu Baggio bali alikuwa akijaribu kuelezea staili ya uchezaji wa Baggio ambayo alikuwa akicheza kama namba tisa lakini mwenye uwezo wa kutafuta kumiliki mpira kitu ambacho alikuwa sahihi.

Katika historia yake ya maisha, Baggio alitamka kuwa anajiweka katika orodha moja na Pele na Maradona, lakini akisisitiza kuwa Pele na Maradona wako katika dunia nyingine, ila yeye yuko katika mstari unaowafuatia.

Na hii ilithibitishwa mnamo mwaka 2000 wakati FIFA walipoendesha zoezi la mtandaoni la kupata maoni kuhusu nani mchezaji bora wa karne ya 20; Baggio alikamata nafasi ya nne nyuma ya Maradona, Pele na Eusebio.

Mwaka 1993 wakati akichezea Juventus, Baggio alifanikiwa kuwa mchezaji wa Kiitaliano wa tatu, baada ya Rivera na Paolo Rossi, kupata tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya; na baada ya hapo Waitaliano ilibidi wasubiri miaka 13 baadae ndipo Muitaliano mwingine aitwaye Fabio Cannavaro, alipochukua tuzo hiyo baada ya kuiongoza timu yake kubeba kombe la Dunia mwaka 2006.

Ila kitu kinachowauma wapenzi wa mchezaji huyu zaidi, ni kuwa hawakuweza kujua fika kiwango cha juu zaidi anachoweza kufikia jamaa huyu, kwani alikuwa akipata majeraha mara kwa mara. Unaweza kusema kuwa maisha ya kisoka ya Baggio yaliisha kabla hata hayajaanza.

Wakati Fiorentina walipomnasa mwaka 1985 tayari alikuwa akichukuliwa na wengi kama nyota wa miaka ya mbele. Vilabu vya Italia vilikuwa vikimvizia toka akiwa na miaka 11 akichezea timu ya kijijini kwao katika mji wa Vicenza.

Akiwa na miaka 13 alijiunga na klabu ya Vicenza katika ligi ya vijana ambapo alifanikiwa kufumania nyavu mara 110 katika mechi 120. Baada ya hapo alihamia timu ya wakubwa, lakini hata kabla hajakaa vizuri, Fiorentina waliwapiku Juventus, kupata saini ya kijana huyu baada ya kumwaga dau lililokuwa na thamani ya paundi milioni 1.5.

Hata hivyo, siku mbili tu kabla mkataba haujasainiwa, Baggio alichanika msuli katika mguu wake wa kulia akiwa katika mechi dhidi ya Rimini, maumivu ambayo yalilazimu madaktari kumfuma na nyuzi 220 ili aweze kupona.

Kwa bahati nzuri, Fiorentina waliheshimu mkataba na kumsajili akiwa majeruhi, hali ambayo ilimuweka nje kwa takriban kipindi cha misimu miwili; na hata baada ya hapo aliendelea kupata maumivu ya goti mara kwa mara.


Baggio alitambulishwa katika dini ya Kibudha na rafiki yake wa Kiitaliano Mbudha aitwaye Maurizio Boldrini. Katika dini hii ndipo Baggio alipofanikiwa kupata maana ya mateso ambayo alikuwa akiyapata.

Baada ya kupona, Baggio alikjikita katika timu ya Fiorentina kama mmojawapo wa wachezaji bora katika timu hiyo haswa katika msimu wa mwaka 1987 -88 ambapo alicheza mechi 27 akifunga mabao 6. Katika msimu uliofuata alifanikiwa kufumania nyavu mara 15 katika michezo 30 aliyocheza. Kilichokuwa kikiwagusa watu wengi ni kuwa si idadi ya mabao tu bali ubora wa mabao aliyokuwa akifunga.

Mnamo mwezi wa tano mwaka 1990, Fiorentina walimuuza Baggio kwa mahasimu wao wa jadi Juventus. Habari za kuuzwa kwa Baggio zilipotoka, mashabiki walianzisha vurugu na balaa mji mzima wakivunja vioo, maduka na magari. Ilichukua idadi ya askari wa kutuliza ghasia 350 kuwatuliza mashabiki hawa waliokuwa na hasira.
Baggio alicheza chini ya makocha 18 tofauti katika maisha yake ya kisoka. Hadi leo hii jamaa huyu ana maneno mazuri ya kuzumgumza juu ya makocha hawa wakiwemo kina Carlo Mazzone (Brescia), Gigi Maifredi (Juventus) na Sven Goran Erricson (Fiorentina).

Lakini katika makocha wote, Baggio hatokuja kumsahau Marcelo Lippi, kwani huyu alikuja kuwa kocha aliyemchukia kuliko wote. Akiwa katika msimu wake wa pili katika timu ya Inter Milan Baggio anaelezea kuwa Lippi alikuwa akijaribu kila aliloweza kummaliza mwanasoka huyu sababu ya kupendwa kwake na mashabiki tofauti na Lippi ambaye hakuwa kipenzi cha mashabiki nchini Italia.

Baggio anakumbuka siku moja akiwa mazoezini na timu ya Inter alicheza pasi moja ndefu iliyomkuta Bobo Vieri, ambaye aliutia mpira kimiani. Baada ya hapo kila mchezaji alimpongeza kwa kupiga makofi akiwemo Cristian Panucci. Lakini Lippi alipandisha mashetani na kuwafokea Pannucci na Vieri huku akiwaambia kwa lugha ya Kiitaliano, “Nyie washenzi mnafanya nini? Hapa hatuko maonyeshoni, hapa tuko kufanya kazi!”
Ndio maana hakuna aliyeshangaa wakati Lippi alipokuja kufukuzwa kazi miezi kadha baadae.

Baggio alistaafu kucheza soka katika msimu wa 2003 -2004 na kwa asilimia kubwa akapotea kabisa katika rada ya soka. Siku hizi hutoa ‘intavyuu’ kwa waandishi mara chache sana na huonekana mitaani kwa nadra.

Siku hizi, Baggio hutumia muda wake mwingi akiwinda katika ranchi yake nchini Ajentina na kusafiri nchi moja hadi nyingine ‘akipromoti’ masuala ya kibinadamu huku akiwa mfuasi thabiti wa dini yake ya Kibudha. Anatumia muda wake mwingi zaidi kusaidia kupigana na umasikini duniani akiwa kama balozi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, (FAO).

Nywele zake ndefu nyeusi zimeshabadilika rangi na kuwa na mvi nyeupe. Anaonekana mzee zaidi kuliko miaka 41 aliyonayo hivi sasa; na soka pekee analocheza ni akiwa na watoto wake nyumbani.

DVD yampatia nafasi ya kufanya majaribio Max Lonsdale Manchester United


Wakati Max Lonsdale alipotupiwa vilago na timu ya Macclesfield Town inayoshiriki ligi daraja la 3 nchini England msimu uliopita hakuna aliyedhani angefika hapa alipo.
Lonsdale mwenye umri wa miaka 18 alitengeneza DVD na kuipeleka kwa kocha wa Manchester Utd,Sir Alex Ferguson,
Baada ya Lonsdale kutemwa na timu yake aliamua kumtafuta Ferguson na alipompata akampatia hiyo DVD na Ferguson akampatia jukumu kocha wa timu ya wachezaji wa akiba ambaye alimpatia wiki moja ya majaribio na baadae yakawa majuma mawili.

sasa anasubiria kuona kama atapata mkataba wa kudumu.
...binafsi nimemkubali huyu dogo hakuna mafanikio yanayopatikana kwa njia nyepesi...SAFI SAANA DOGO KOMAA MPAKA KIELEWEKE..



VILLA SQUARD YA MAGOMENI ILIANZIA HUKU.....ENTEBE FC







Wednesday, August 3, 2011

RAISI WA MATEJA LANGA SHABIKI WA BARCELONA


Msanii maarufu wa muziki wa bongo flava aliyekuwa akiunda kundi la Cocacola Pop Star kwa pamoja na Shaa na Witness, Langa a.k.a Raisi wa Mateja amesema kama kama asingekuwa mwanamuziki basi angechagua soka kama kazi yake.

Langa ambaye recently alijitangaza kuwa ameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya baada ya kutumia kwa zaidi ya miaka 5, amesema kabla hajawa mwanamuziki alikuwa anapiga soka vibaya mno katika timu ya mtaani kwao ya Regent Football club lakini kutokana na muziki kuonyesha mwelekeo zaidi wa kimafanikio zaidi ya soka akaamua kuachana na soka na kujikita katika music business.

“Kiukweli nina mapenzi makubwa sana na mchezo wa soka, na kama nisingekuwa rapper basi now ningekuwa dimbani nazungusha tu.Kwa sasa nimebaki kama mshabiki na timu ninazozishabikia ni Barcelona kwa Spain, Juventus in Serie A na Liverpool in England.”-Langa.