Search This Blog

Friday, August 5, 2011

XAVI HERNANDEZ: MCHEZAJI KAMA MIMI NI HATARI NA NAJIFANANISHA NA UKUTA ULIOJENGWA KUZUIA MAFURIKO

XAVI Hernandez anazungumza kwa tabasamu la furaha na kujiamini yeye ni wa kipekee. Anapenda mpira ndiyo maana wikendi moja alikwenda Italia kushuhudia mechi ya Sampdoria na Juventus ingawa hakufurahishwa na mchezo uliochezwa.
Lakini Xavi ambaye ni mchezaji miongoni mwa wachezaji watatu bora wa Dunia, anaamini kuwa aina ya mchezo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ndiyo bora zaidi duniani kwa sasa.
Lakini ni mchezaji anayetoa heshima kwa wenzake. Xavi anasema kuwa nyota kama Paul Ince, Paul Scholes, Michael Carrick, Roy Keane, John Terry na Jammie Carragher ni bora na anawaheshimu sana.
NINI SIRI YA MAFANIKIO YAKO?
“Kujiamini, kufanya mazoezi ya kutosha, kupokea ushauri, kupumzika pia kupokea mafundisho sababu nina ‘enjoy’ mpira kote Barcelona hadi katika timu ya taifa. Pia nidhamu ni jambo la msingi. Pia naamini kuwa makocha wote wa Hispania wana falsafa moja ya mchezo (kucheza kwa tabasamu)”

JE UNA NAFASI YA KUCHEZA ENGLAND?
“Mchezaji huweza kucheza mahali kokote, ila inategemea na kuzoea aina ya mchezo wa sehemu husika. Xabi Alonso na Mikel Arteta wanaweza kuwa mfano mzuri wamefanikiwa kucheza England na wamefanya vizuri”


UNAZUNGUMZIAJE TUZO ZILIZOPITA ZA MCHEZAJI BORA WA DUNIA?
“Ninasikitika sikushinda lakini sikuwa wa kwanza mimi kushindwa. Naheshimu maamuzi ya majaji”

UNAFIKIRIA KUACHA KUICHEZEA BARCELONA?
“Hapana, navutiwa sana na soka la Barca ila pia napenda changamoto ya kucheza mazingira tofauti tofauti”

HATA KUCHEZA ENGLAND?
“Ndiyo, sipendi soka la Italia ila napenda soka la England na naipenda Manchester United kwani ina soka la ‘ajabu’ pia navutiwa na mashabiki wa England ambao wanashangilia kwa nguvu ukilinganisha na vilabu vya Hispania, kwani mashabiki kama wa Espanyol, Atletico Madrid na Sevilla huwa wanashangilia kwa kupiga sana kelele”
UNAHISI NINI KUHUSU UMAARUFU WAKO?
“Najisikia faraja kujulikana duniani kote kama mastaa wengine waliopita, na najivunia kuwepo Barcelona, watu wananichukulia mimi kama mfano hapa Catalunya na La Masia. Pia kocha Vicent Del Bosque anavutiwa na tabia yangu ya kutozungumza na vyombo vya habari, Frank Benckerbeur na Michael Platini (Rais wa Uefa) wanapenda nidhamu yangu”

UNAMZUNGUMZIAJE PEP GUARDIOLA?
“Umesema Guardiola?...Pep ni kocha mwenye msimamo ana miaka mitatu tangu awepo hapa kama kocha na wakati anasaini mkataba alisema amekuja kuipaisha Barcelona. Pep ni kocha mwenye kutaka kazi yake ikamilike pia anachukia mtu mzembe na anataka utimamu wa mwili na akili kwa kila mchezaji”

UNADHANI PEP ATAFANIKIWA AKIPEWA TIMU ENGLAND?
“Ndiyo, sababu Pep ana kipaji cha kufundisha timu yoyote atakayopewa”

NI KWELI UJUZI WA PEP NA SAPOTI YA MASHABIKI WENU NDIYO INAFANYA MUONEKANE BORA?
“Ni kwamba kuwa bora hutambulishwa na matokeo bora KWAMBA KUWA BORA, fikiria kuwa Guardiola asingekuwa na matokeo bora basi na wapenzi wasingemuona bora ….Mchezaji bora ni yule anayefanya kazi na kocha bora”







UNAZUNGUMZIAJE LA MASIA?
“Wachezaji wote wa Catalunya lazima wapitie La Masia kwani shule hii huzalisha aina bora ya soka Duniani—mfano mzuri ni Sergio Busquets ambaye ni kiungo bora katika pasi za one-two na ni kinda mwenye rekodi za ajabu kutoka La Masia…..La Masia ni chuo bora zaidi ya kile cha Ajax Amsterdam ambacho kiliwaibua nyota kama Johan Cruffy”

KUNA CHANGAMOTO GANI CAMP NOU?
“Changamoto zipo na uwepo wangu tu na uwezo wangu uwanjani unanipa mataji nikishirikiana na David Villa, Leo Messi, Busquets, Inesta na timu nzima ya Barcelona, kwa sasa sina wasiwasi sana na nafasi yangu labda vijana wa kutoka La Masia watakapokuja hapo baadae, lakini si kwa wachezaji wa sasa wa Barcelona”

No comments:

Post a Comment