Search This Blog

Saturday, May 14, 2011

KIUNGO WA BARCELONA SERGIO BUSQUETS HATARINI KUIKOSA LIGI YA MABINGWA ULAYA.



BARCELONA IKO HATARINI KUMKOSA KIUNGO WAKE SERGIO BUSQUETS KWENYE MCHEZO WA FAINALI YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA. BUSQUETS YU HATARINI KUFUNGIWA MECHI KADHAA KWA KOSA LA KUMDHIHAKI NA KUMDHALILISHA KIBAGUZI BEKI WA REAL MADRID MARCELO WAKATI TIMU HIZO MBILI ZILIPOKUTANA KWENYE NUSU FAINALI YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA . MIKANDA YA TELEVISHENI ILIMUONYESHA BUSQUETS AKIMTAMKIA MARCELO NENO MONO AMBALO LINAMAANISHA NYANI HUKU AKIWA AMEFUNIKA MDOMO WAKE KWA MIKONO YAKE .

AC MILAN NA CHELSEA ZAMWANIA KAKA.



KLABU YA A C MILAN IMEPANGA KUTIBUA MIPANGO YA CHELSEA MBAYO INADAIWA KUWA MBIONI KUMSAJILI KIUNGO MBRAZIL RICARDO KAKA. KAKA AMBAYE NI MCHEZAJI WA REAL MADRID AMEONEKANA KUTOKUWA KWENYE MIPANGO YA MUDA MREFU YA KOCHA JOSE MOURINHO NA KOCHA HUYO ANAHUSISHWA NA MPANGO WA KUMBADILI KAKA NA KIUNGO MWINGINE TOKA CHELSEA YA ENGLAND FRANK LAMPARD . A C MILAN NDIYO KLABU AMBAYO KAKA ALITOKA KABLA YA KUSAJILIWA NA MADRID.

SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA ZANZIBAR.



Real madrid watepeta mapema leo chelsea wapigwa nusu fainali sasa hivi ni fainali kati ya ARSENAL VS BARCELONA KATIKA VIWANJA VYA MAO TSE TUNG VISIWANI ZANZIBAR.

YANGA YAKATAA UJIO WA BIRMINGHAM.



Klabu ya yanga ya Dar es salaam imesema haitaki kuhusishwa katika maandalizi ya kuileta timu ya BIRMINGHAM CITY ya uingereza lakinai itakua tayari kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu hiyo endapo itafanikiwa kufanya ziara yake yakuja nchini mapema mwezi ujao.

Mwenyekiti wa yanga Lloyd Nchunga alisema jana kwamba klabu yake imefikia maamuzi hayo baada ya kuona kwamba ni kiasi kikubwa mno cha fedha (sh.bilioni 2.7)kinahitajika ilikuileta timu hiyo,jambo ambalo ni ndoto kwa yanga na simba kumudu gharama hizo zilizoelezwa.

UNITED WANATAKA HESHIMA-FERGUSON


Man United manager amekasirika kufuatia maoni ya wachambuzi mbalimbali wa soka kusema kikosi chake cha sasa sio kizuri kama cha mwaka 1999.
Old Trafford chief amezungumza na kusema na kujivunia rekodi ya kikosi chake cha sasa, wingi wa magoli ya kufunga, rekodi kucheza vizuri nyumbani, na sasa wanakaribia kuchukua makombe mawili ndani ya msimu mmoja.
“Tumekuwa na performance nzuri sana mwaka huu, wachezaji wamejituma sana hakuna atakayebisha juu ya rekodi nzuri tuliyonayo kwa michezo ya nyumbani”.
“Tumepoteza pointi mbili tu @ Old Trafford msimu mzima na sifikirii kuna timu yoyote yenye rekodi kama hiyo ndani Europe, ingawa tumepoteza some points kwa team zilizo chini kwenye msimamo kama Birmigham, Wolves, West Brom, Aston Villa, and Newcastle nah ii inathibitisha kwamba hii ni ligi ngumu kushinda, so kushinda taji hili inabidi my players wapewe heshima wanayostahili ”. said Ferguson

BARCELONA WAKISHANGILIA UBINGWA WA LA LIGA






KOCHA WA TIMU YA TAIFA STARS AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA BAFANA BAFANA LEO.


Mchezo utakua mgumu kwasababu wachezaji wa timu zote watataka kuonyesha viwango vya juu ili wasake nafasi katika vikosi vya kwanza baada ya nyota wanaocheza soka la kulipwa kutokuwepo
Poulsen alisema wachezaji wake wamemaliza ligi tangu Aprili 10 wamefanya mazoezi ya kujijenga stamina kwa muda mrefu ili kukabiliana na bafana na anaamini kwamba wataonesha kiwango bora na hatimaye kupata matokeo mazuri.

KUELEKEA MECHI KALI YA LEO ITAKAYOPIGWA UWANJA WA TAIFA KATI YA TAIFA STARS NA BAFANA BAFANA MAKOCHA WATOA TAMBO ZAO.


Kocha wa timu ya bafana bafana PITSO MOSIMANE akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu mechi yao ya leo dhidi ya TAIFA STARS.
Aidha kocha wa wa bafana bafana PITSO MOSIMAME kikosi chake kitashuka dimbani bila nyota wake 14 wanaocheza soka la kulipwa ulaya huku pia ikiwakosa nyota wake wengine nane wanaochezea klabu za Ajax Cape town,Orlando pirates na Kaizer Chiefs zilizokataa kuwaruhusu kutokana na kukabiliwa na mechi muhimu za ligi kuu ya kwao,kombe la shirikisho na ligi ya klabu bingwa afrika"ukicheza siku ambayo haitambiliwi na FIFA ni tatizo, ila wachezaji nilionao watatumia nafasi hii kunionesha kwamba wanaweza alisema Mosimane. Aliwataka wachezaji wake ambao wako kwenye kikosi cha kwanza na leo watashuka dimbani kuwa ni pamoja na Itumeleng Khune (kipa) Reneilwe Letsholonyane na mfungaji wa bao la kwanza kwenye fainali za kombe la dunia zilizopita Siphiwe Tshabalala ambaye ndiye aliechaguliwa kuwa nahoza wa timu hiyo.Mosimame alisema kuwa wakali anaowakubali zaidi ndani ya kikosi cha stars ni winga Mrisho Ngassa n, Shadrack Nsajigwa na kipa juma kaseja aliowahi kuwaona katika mechi tofauti zilizowahi kuoneshwa na televisheni ya super sports.

HATIMAYE KLABU YA YANGA YAPANDA DAU KWAJILI YA KUMRUDISHA NGASSA JANGWANI.


Baada ya juhudi za viongozi wa yanga kumrudisha Mrisho ngassa katika klabu ya yanga ya jijini Dar es salaam sasa imeamua kumpandia dau na inamtaka kwa sh.milioni 50.

SIKUMTUKANA MARCELO-BUSQUETS.


Kiungo wa mabingwa wa La Liga, Sergio Busquets amejitokeza hadharani na kupinga madai ya kwamba alimtukana beki wa Real Madrid Marcelo kwa kumuita nyani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kwanza ya Champions League iliyozikutanisha Barcelona na Real Madrid kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Spanish Midfielder amepinga madai baada ya kutangaza kwamba wamefungua kesi ya nidhamu dhidi yake.
Real Madrid walalamika kwa UEFA kwamba Busquets alimwita Marcelo “MONO” (nyani), na kutoa video ambayo inamuonyesha Barcelona midfielder akiongea huku akiwa ame-cover mdomo wake na kiganja cha mkono.
Msemaji wa Barcelona pia amepinga madai hayo ya Real Madrid akisema ni madai hayo ni ya uongo na Madrid wana nia mbaya dhidi ya timu na mchezaji wao.
Barcelona wanatarajiwa kuwasilisha utetezi wao Leo (Ijumaa) na kama Busquets atapatikana na hatia aanaweza kusimamishwa hivyo kukosa fainali ya Champions League dhidi ya Manchester United tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa Wembley-Uingereza.

TEVEZ AONDOKE KAMA HANA FURAHA-MANCINI


Kocha wa Manchesterb City Roberto Mancini amemwambia mshambuliaji wa timu Carlos Tevez hiyo acheze kwa kujituma kwa asilimia 100 au aondoke Eastlands.
Tevez ambaye aliomba kuondoka Man City earlier this season kabla hajabadili mawazo na kuamua kubaki, amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamishia huduma zake nchini Italia katika klabu ya Inter Milan.
Akiongea na vyombo vya habari Mancini amesema kama the Aegentian Striker hana amani ndani ya Man City basi aondoke, “Tevez ana mkataba wa miaka mitano hapa lakini kwa maoni kama mchezaji anataka kukaa hapa inabidi ajitume kwa 100% na awe na furaha lakini kama hana furaha na amani ni aondoke.”
Hata hivyo Carlos Tevez ambaye alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya bega, amepona na leo anatarajiwa kuanza katika mechi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya Stoke City.

CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI REAL MADRID.


Baada ya Juzi kufunga mabao 3 katika mechi dhidi ya Getafe, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa miaka 50 iliyopita na Hungarian footballer Ferenc Puskas kwa kufunga mabao mengi zaidi ndani ya msimu mmoja katika klabu ya Real Madrid.
Puskas ambaye alifunga mabao 47 ndani ya msimu mmoja(1959/60) alikuwa ndio Real Madrid all time top scorer in one season mpaka kufikia jana ambapo CR7 alipovunja rekodi hiyo kwa kutimiza mabao 49 in a single season na ligi ikiwa bado inaendelea.
2008 FIFA Ballon d'Or winner ameshatia kambani goli 36 kwenye La Liga, 6 goals in Champions League na 7 goals in Copa De Rey.

Wednesday, May 11, 2011

TERRY-IT'S ALL OVER NOW


Baada ya jumapili kupokea kipigo kutoka kwa Man UTD, England and Chelsea captain John amesema ni vigumu kukubali ukweli lakini ubingwa wameshaukosa.

Chelsea ambayo jana ilienda Old Trafford ikijua ushindi pekee ndio ungeweka hai matumaini ya kuutetea ubingwa wao lakini magoli ya mapema kabisa ya Javier Hernandez "Chicharito" na Nemanja Vidic yalizima ndoto za watoto wa Abromavich.

Akiongea baada ya mechi John Terry alisema, "Sijui nini kilitokea, tulienda Old Trafford na matumaini na kuomba tuuanze mchezo vizuri lakini haikuwa hivyo.United walianza vizuri na kupata magoli ya mapema ambayo yaliwasaidia kujipanga vyema.Kipindi cha kwanza hatustahili chochote kwenye mchezo ule second half tulijitahidi tukacheza vizuri na kufanikiwa kupata goli moja lakini halikutosha kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wetu."

NIPENI LAMPARD MCHUKUENI KAKA.


Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anaripotiwa kuvutiwa na huduma za Chelsea and England international football player, Frank Lampard na anafikiria kumtumia Ricardo Kaka katika kufanikisha deal hilo.
Frank Lampard alihusishwa sana na kujiunga na Inter Milan kipindi Mourinho alipojiunga na klabu hiyo ya Italia, lakini uhamisho huo haukufanikiwa na Lampard akabaki darajani.
Now the news has that the Special One anafikiria kumtoa Kaka ambaye ameshindwa kung'ara ndani ya kikosi cha Madrid ili apate discount from the expected £ 40 million asking price ili aweze kumleta Frank Lampard Santiago Bernrbeu

TEAM YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI BAFANA BAFANA YATARAJIA KUSHUKA NCHINI.


Kikosi cha timu ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) kikiongozwa na kiungo wa Kaizer
Chiefs, Siphiwe Tshabalala kitawasili nchini Mei 12 mwaka huu saa 1.30 jioni kwa
ndege ya South African Airways kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars
itakayochezwa Mei 14 mwaka huu saa 12 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.


Wachezaji wengine kwenye kikosi hicho kinachofundishwa na Pitso Mosimane ni
makipa: Itumeleng Khune na Wayne Sandilands. Mabeki ni Morgan Gould, Siyanda
Xulu, Eric Matoho, Mzivukile Tom, Prince Hlela, Siyabonga Sangweni, Tefu
Mashamaite na Siyanda Zwane.


Viungo ni Hlompho Kekana, Thanduyise Khuboni, Reneilwe Letsholonyane, Thandani
Ntshumayelo,Thabo Matlaba, Erwin Isaacs na Sifiso Myeni wakati washambuliaji ni
Bernard Parker, Vuyisile Wana, Lehlohonolo Majoro na Katlego Mphela.


WACHEZAJI WA STARS KUTOKA NJE
Klabu ya Vancouver Whitecaps imemnyima ruhusa Nizar Khalfan kwa vile Mei 15
mwaka huu itakuwa na mechi muhimu ya ligi. Ujio wa wachezaji Idrissa Rajab,
Henry Joseph, Abdi Kassim, Dan Mrwanda na Athuman Machupa bado tunafuatilia
majibu katika klabu zao.


Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa Alhamisi (Mei 12 mwaka huu)
katika vituo vya Premier Betting (Kariakoo- Mtaa wa Sukuma, Buguruni Sokoni,
Manzese Midizini, JM Mall na Tandale kwa Mtogole), Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Big Bon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa
Uhuru.

REAL MARDID WAMEFANIKIWA KUMSAJILI NURI.


Real Madrid wamefanikiwa kumsajili Borussia Dortmund midfielder Nuri Sahin jana jumatatu mtandao wa klabu hiyo unaripoti.
The German-born Turkish player amesaini mkataba wa kuichezea Real Madrid kwa misimu sita for €10 millions.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Real Madrid sports director Miguel Pardeza alisema "Sahin ni mchezaji mzuri na alikuwa moja ya viungo bora kwenye Bundesliga msimu huu, ni mdogo kiumri na ni mchezaji bora vitu vinavyomfanya kuwa a good signing".
Pia Nuri Sahin aliuzungumzia uhamisho wake kwenda Santiago Bernebeu, "Haukuwa uamuzi rahisi kuondoka Borussia, naipenda klabu na kocha na nilikuwa najisikia furaha sana nikiwa pale lakini Real Madrid ni moja ya timu bora duniani hivyo kujiunga nayo ni hatua kubwa katika maisha yangu."
"Sikuichagua Real kwasababu ya pesa.Nimechagua kwasababu hii ni timu kubwa ulimwenguni, ni vigumu kukataa kujiunga na timu hii.Jose Mourinho ni kocha bora duniani, nafuraha sana kufanya nae kazi".

MESSI NA RONALDO-NA​NI KUCHUKUA PICHICHI?


Cristiano Ronaldo and Lionel Messi are no strangers katika kuvunja records.Tarehe 23 April, Messi alijiwekea rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka la Hispania kwa kutia kambani magoli 50 (31 goals in La Liga alone) ndani ya msimu mmoja, and last saturday night, Ronaldo aliivunja rekodi yake binafsi baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Sevilla na kufikisha mabao 46 in this season, magoli 36 akiwa amefunga kwenye La liga pekee.


Zikiwa zimebakia mechi tatu msimu wa ligi kumalizika wadau wa soka duniani wanajiuliza nani between the two best players in the world ataibuka La liga top scorer na kuchukua tuzo ya mfungaji bora inayotolewa na gazeti la michezo la Marca maarufu kama "PACHICHI" pamoja na kuingia katika orodha ya La liga top scorer of all time.

BADO NIPO UNITED-FER​GUSON.


Muda mrefu baada ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kuondoka Old Trafford msimu ujao, Sir Alex Ferguson amezungumza na kuthibitisha kwamba ataendelea kuwa kocha wa Man United hata kama akifanikiwa kuwapita Liverpool na kuweka rekodi kwa kuchukua ubingwa wa Uingereza msimu huu.
The Scottish coach ambaye amekuwa in charge of the club tangu 1986, msimu huu ametimiza miaka 25 na kuweka rekodi ya kuwa the longest serving boss in United’s history and the longest serving currently working in EPL.
SAF ambaye wakati akiingia Old Trafford, alisema anataka kuangusha utawala wa Liverpool kwa kuchukua makombe mengi zaidi, now he has taken the club level on 18 top flight championships with their Merseyside rivals.
Na sasa akiwa katika nafasi nzuri kuchukua ubingwa wa 19 wa ligi kuu ya England, the news doing the rounds zinasema ikiwa United watachukua ubingwa msimu huu then Ferguson ataachia ngazi kwa kuwa malengo yake yatakuwa yametimia lakini 69-year old coach ameongea na gazeti la “The Mirror” and he said “I’ll be here next year”.

MICHUANO YA KILI TAIFA CUP YAFIKIA HATUA YA ROBO FAINAL.


Michuano ya KILI TAIFA CUP yaliyokua yakiendelea sasa yafikia katika hatua ya ROBO FAINALI Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni MBEYA,RUVUNA,MWANZA,ARUSHA,SINGIDA,ILALA,KAGERA na U23 kama BEST LOSERS michezo ya robo fainali itafanyika katika jiji la ARUSHA Tarehe 22 mwezi huu.

BREAKING NEWS KWA MASHABIKI WA YANGA

‎'Baada ya AZAM kufungwa na yanga mashabiki walidai nimeihujumu timu,viongozi wa Yanga wakamalizane na wa Azam ili nirudi Yanga sasa '- MRISHO NGASA.

ULIMBOKA MWAKINGWE.

Mchezaji wa zamani wa club ya SIMBA SPORTS CLUB ULIMBOKA anatarajia kurudi kundini mda si mrefu akitokea club yake ya sasa ya MAJI MAJI FC.

AZAM FC NDANI YA JEZI MPYA KWAJILI YA MSIMU UJAO.

JEZI YA UGENINI AMBAVYO ITAKAVYOONEKANA.

JEZI YA NYUMBANI AMBAVYO ITAKAVYOONEKANA.

VIONGOZI WA BIRMINGHAM WARIDHISHWA NA UWANJA WA TAIFA.


kocha msaidizi wa BIRMINGHAM na mkuu wa idara ya afya wameridhishwa na na uwanja wa taifa pamoja na sehemu mbali mbali walizotembelea katika ziara yao nchini tanzania ambapo team hiyo itacheza mechi za kirafiki na vilabu vikubwa vya Tanzania ambavyo ni SIMBA na YANGA.


KOCHA MSAIDIZI WA BIGMINGHAM ANDY WATSON.



MKUU WA IDARA YA AFYA LAN MCGVINESS.

VITU VYA KIPRE TCHETCHE KABLA HAJATUA AZAM FC.

KUTOKA AZAM FC KUHUSIANA NA SAKATA LA MRISHO NGASSA



Azam FC haiwezi taja dau la kumuuza Ngasa kwa kuwa HAUZWI, kwa klabu za ndani isipokuwa nje ya nchi. Azam FC inawataka Yanga waache kuzungumza na Ngasa. Ngasa siyo mchezaji wao na wala siyo mchezaji huru, Ngasa ana mkataba na Azam FC. ambao Azam FC haina nia ya kuuvunja isipokuwa kuuboresha.

Tuesday, May 10, 2011

CECAFA YAHAIRISHA DRAW YA KAGAME CUP


Chama cha soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kimeharisha upangaji wa ratiba wa kombe la Kagame Cup iliyopangwa kufanyika jumapili.
Hali hiyo ilijitokeza ili kuweza kusubiri uthibitisho wa ushiriki wa timu za Al-Ahly kutoka Egypt na Liberty Professionals kutoka Ghana.
"Kutokea mwanzo timu za Al-Ahly na Liberty zilionyesha kuvutiwa na kushiriki katika mashindano haya, lakini mpaka sasa bado hawajathibitisha ushiriki wao"-alisema Nicholas Musonye, Katibu Mkuu wa CECAFA.
Mashindano hayo ambayo mwaka huu yatafanyika jijini Khartoum-Sudan kuanzia tarehe 5 July yatajumuisha timu za Bunnamwaya-Uganda, Ulinzi-Kenya, St.George-Ethiopia, El-Merreikh and Al Hilal-Sudan, Ocean View-Zanzibar, Vital'O-Burundi, Port Of Djibouti, Red Sea-Eritrea, Elman-Somalia, Etincelles and APR-Rwanda.
Ikiwa tofauti na miaka iliyopita mwaka huu mashindano hayo yatakuwa co-sponsored na Rwandan President Paul Kagame atakayetoa $60,000 na El Muriate Group watatoa $40,000.
APR ya Rwanda ndio mabingwa watetezi wa kombe baada ya mwaka jana kuwafunga St.George ya Ethiopia kwa mabao 2-0.

TERRY - IT'S ALL OVER NOW


Baada ya juzi kupokea kipigo kutoka kwa Man UTD, England and Chelsea captain John amesema ni vigumu kukubali ukweli lakini ubingwa wameshaukosa.
Chelsea ambayo jana ilienda Old Trafford ikijua ushindi pekee ndio ungeweka hai matumaini ya kuutetea ubingwa wao lakini magoli ya mapema kabisa ya Javier Hernandez "Chicharito" na Nemanja Vidic yalizima ndoto za watoto wa Abromavich.
Akiongea baada ya mechi John Terry alisema, "Sijui nini kilitokea, tulienda Old Trafford na matumaini na kuomba tuuanze mchezo vizuri lakini haikuwa hivyo.United walianza vizuri na kupata magoli ya mapema ambayo yaliwasaidia kujipanga vyema.Kipindi cha kwanza hatustahili chochote kwenye mchezo ule second half tulijitahidi tukacheza vizuri na kufanikiwa kupata goli moja lakini halikutosha kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wetu."