Search This Blog

Saturday, February 25, 2012

MSUMBIJI KUTUA NCHINI FEBRUARI 26

Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) itawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya South African Airways. Ndege hiyo yenye mruko namba SA 186 inatarajia kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.55 mchana. Msafara wa Mambas kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano (Februari 29 mwaka huu) saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa na watu 29. Kati ya hao, 19 ni wachezaji wakati waliobaki ni maofisa wa timu hiyo. Mwamuzi wa mechi hiyo Farouk Mohamed na wasaidizi wake Ayman Degaish, B.T Abo El Sadat na Gihed Greisha kutoka Misri watawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya Egypt Air. Kamishna ni Loed Mc Ian kutoka Afrika Kusini. Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa Jumanne (Februari 28 mwaka huu) katika vituo vya vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.

YANGA WATAKIWA 40 TU UWANJANI

Kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yaliyotumwa jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ni idadi hiyo tu inayotakiwa kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila washabiki. Adhabu ya Zamalek kutocheza mechi mbili za nyumbani za michuano hiyo bila washabiki ilitolewa Aprili 20 mwaka jana na Bodi ya Nidhamu ya CAF iliyokutana jijini Johannesburg, Afrika Kusini.  Mechi dhidi ya Yanga ndiyo itakayokuwa ya kwanza kwa Zamalek kuanza kutumikia adhabu hiyo iliyotakana na washabiki wake kufanya fujo kwenye mechi ya michuano hiyo mwaka jana ilipocheza dhidi ya Club Africain ya Tunisia.  Hivyo kila timu (Yanga na Zamalek) katika mechi hiyo inatakiwa kuwa na wachezaji ambao wana leseni za CAF kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa 2012. Pia benchi la ufundi katika kila timu linatakiwa kuwa na watu watano. Kwa klabu zote mbili, kila moja imeruhusiwa kuingia na wajumbe wake wa Kamati ya Utendaji wasiozidi kumi. Mbali ya klabu hizo mbili, wengine waliotajwa kuruhusiwa kuingia uwanjani ni vijana 20 watakaofanya kazi ya kuokota mipira (ball-boys). Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia.

MBWANA SAMATTA AKATAA KUTOKUA NA MAPENZI NA TAIFA STARS!




































Poulsen anasema hajakuita National Team kwa kuwa huna mapenz na timu ya taifa imekaaje hii?
Mbwana Samatta Kwa kweli aijanifuraisha ila siamini kama ni kweli sina moyo na taifa langu.

Ronaldo na Messi watakavyokuwa mwaka 2040

HATIMAYE ARSHAVIN AONDOKA ARSENAL - ARUDI ZENIT KWA MKOPO


Andrey Arshavin hatimaye amekuwa chanzo cha habari nzuri kwa mashabiki wa Arsenal jana Ijumaa baada ya kuondoka Gunners kwa mkopo.

Mchezaji huyo aliye na rekodi ya kununuliwa kwa fedha nyingi kuliko wote katika historia ya klabu  amerudi katika klabu ya Zenit St Petersburg baada ya klabu hiy ya Russia kukubali kulipa ada ya mkopo ya  £1million na pia kulipa mishahara ya mshambuliaji huyo mpaka mwishoni mwa msimu.

Arshavin ambaye aliigharimu Arsenal £15million alipojiunga na klabu hiyo kutoka Zenit in 2009, alisema kupitia Twitter account : “Limeisha”

Baadae kupitia Sport-Express in Russia alisema: “Ijumaa ilikuwa siku ngumu sana, hakuna kilichokuwa kimeamuliwa mpaka dakika ya mwisho. Lakini naamini kutoka sasa kila kitu kitaenda vizuri. Nataka kucheza na nitafanya yote niyawezayo kuisadia Zenit kushinda taji la ligi.”

EXCLUSIVE: NAFASI YA NGASSA SEATTLE SOUNDERS YACHUKULIWA NA MKONGO - AAMBIWA AENDELEE KUSUBIRI.

Ngassa akiwa na kocha wa Seattle Sounders alipoenda kufanya majaribio nchini Marekani.


Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Mrisho Ngassa kwenda kujiunga na timu ya Seattle Sounders imejulikana leo baada ya blog hii kuongea na Rahim Zamunda mmiliki wa African Lyon na mtu aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Ngassa kwenda kufanya majaribio nchini Marekani mwaka Uliopita.


Imefahamika kwamba Ngassa ambaye ilisemekana amefanya vizuri katika majaribio yake nchini Marekani hivyo angejiunga na Seattle Sounders mwezi January mwaka huu, hatoweza tena kujiunga na timu hiyo baada ya nafasi yake kujazwa na mchezaji mwingine kutoka nchini Congo.

Rahim Zamunda akiwa na kiongozi wa Seattle Sounders alipompeleka Ngassa kwenda kufanya majaribio mwaka jana.



"Ni kweli Ngassa hakuweza kujiunga na Seattle Sounders kwa sasa baada ya nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine ambaye anacheza nafasi kama ya Ngassa uwanjani. Mcongo huyo nae alifanya majaribio na Seattle akafanya vizuri na kocha akapendekeza yeye ndio achukuliwe kwanza kabla ya Ngassa, ambaye ataendelea kuangaliwa kwa ukaribu na itakapotokea nafasi nyingine atachukuliwa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Marekani. Hiyo ndio hali halisi ya mambo yalivyo katika sakata la Ngassa kwenda kucheza Seattle Sounders." - Alimaliza Zamunda.

Christopher Samba ajiunga na Anzhi Makhachkala

Blackburn wamethibitisha Christopher Samba amejiunga na Anzhi Makhachkala.

Dirisha la usajili la Russia lilikuwa halijafungwa mpaka usiku wa leo na warusi hao ambao hivi karibuni walimtangaza Guus Hiddink kama kocha wao mkuu, na sasa wamemsaini Samba ambaye aliomba kuondoka Blackburn tangu mwezi January lakini ombi lake likapigwa chini.

MAENDELEO YA UTENGENEZWAJI WA UWANJA WA STADE TP MAZEMBE YANAVYOENDELEA










Friday, February 24, 2012

VIINGILIO STARS VS MSUMBIJI


Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
 
Jumla viti 36,693 (rangi ya bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa kiingilio hicho katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wameketi.  
 
Viingilio vingine ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 15,000 kwa VIP B wakati kwa watakaokuwa miongoni mwa watakaokaa katika viti VIP A ambavyo viko 748 tu watalazimika kulipa sh. 20,000 kwa kila mmoja.
 
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.
 

BAADA YA KUTOKUFUNGA BAO KATIKA MECHI 20 - HATIMAYE FLOP TORRES APIGWA CHINI SPAIN


Matumaini ya Fernando Torres  kucheza at Euro 2012 yameanza kushuka baada ya kutemwa katika kikosi cha  Spain kwa ajili ya mechi ya wiki ijayo dhidi ya Venezuela.

Spain, ambao watatea ubingwa wao wa ulaya baadae mwaka huu, wanakutana na wasouth America mjini Malaga wiki ijayo Jumatano huku Del Bosque akisema kunaweza kuwa na mabadiliko katika kikosi kabla ya michuano ya ulaya nchini Ukraine na Poland, na Torres anaonekana yupo mbali katika kuipata nafasi ya kuwemo ndani ya kikosi cha watu 23.

Del Bosque anasema anataka kuwazadia wachezaji ambao wamekuwa wakifanya vizuri. Torres amekuwa hafanyi chochote kwa zaidi ya mwaka sasa.

“Torres ni mchezaji ambao ninaheshimu sana mchango wake na inaniuma kumuacha nje ya kikosi lakini nataka kuwa fair,” Del Bosque aliwaambia waandishi.

Torres amekuwa na wakati mbaya kuliko wowote katika maisha yake ya soka tangu ajiunge na Chelsea  kutoka Liverpool na ada iliyoweka rekodi £50million mwanzoni mwa mwaka uliopita. Amefunga goli tu katika mechi 18 msimu uliopita huku msimu huu katika mechi 29 akiwa amefunga magoli 5, na sasa hajafunga goli tangu October 19 alipofunga dhidi ya Genk katika UCL.
Enzi Hizo Torres akifunga goli la ushindi dhidi ya Ujerumani in Euro 2008 final.

Mara ya mwisho kufunga katika premier league ilikuwa dhidi ya Swansea mwezi September last year.
Pia mara ya mwisho kuifungia Spain ilikuwa katika kufuzu kmbe la euro dhidi ya Liechtenstein waliposhinda 4-0 in septmber 2010.

Sina deni Prime Time wala Yanga- Mohamed Bhinda

MWANACHAMA na mjumbe wa kamati ya utendaji wa siku nyingi wa klabu ya Yanga, Mohamed Bhinda amekanusha kuchukua fedha za mapato za mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kati ya timu yake na klabu ya Zamalek Spoting ya Misri.
Hivi karibuni kulikuwa na habari tofauti zikimuhusisha Bhinda kuwa amechukua baadhi ya fedha zilizotokana na kiingilio huku wengine wakidai kuwa mwanachama huyo anatarajiwa kuhojiwa hivi karibuni na kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Bhinda alisema kuwa mbali ya kufanya kazi kama kiongozi wa Yanga, pia alipewa jukumu la kutafuta wauzaji tiketi ambao aliwasisimia yeye ili kufanikisha zoezi hilo gumu kwa maeneo ya Kariakoo na Temeke.
Alisema kuwa alipewa kazi hiyo na kampuni ya Prime Time Promotions ambao walikuwa wasimamizi wakuu wa mechi hiyo. Alifafanua kuwa kutokana na utaratibu mpya wa tiketi za ki-elotroniki, zpezi la kuhakiki tiketi lilikuwa gumu sana kwani uwanja wa Taifa unaingiza watu 60,000.
“Kutokana na zoezi la kuhakiki tiketi kuwa gumu, uuzaji ukachelewa, hivi mimi nilipewa tiketi kwa ajili ya wauzaji wa Temeke na nilichukua dhamana yao baada ya kuwapa najira ya uuzaji huo,” alisema Bhinda.
Alisema kuwa anashangazwa na taarifa kuwa ameingia mitini na fedha za malipo ya tiketi wakati malipo yote alikabidhi Prime Time Promotion chini ya uangalizi wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security. “Sina deni Prime Time wala Yanga, sasa haya majungu yanatoka wapi, naamini kuna watu ambao hawataki sisi kufanya kazi hizi, baada ya kupongeza wanatoa tuhuma ambazo si za msingi,” alisema.
Alisema kuwa Wanayanga wanatikiwa kuipongeza kampuni ya Prime Time kwa kufanikisha zoezi hilo na kuipatia mapato Yanga ya kihistoria. Mara ya mwisho Yanga ilipata jumla ya Shs milioni 100.5 baada ya kucheza mechi na timu ya Al Ahly  ya Misri.
Alisema kuwa hamasa ya mchezo huo ilikuwa kubwa sana na Prime Time imefanya kazi ya kupongezwa katika kufanikisha hayo. Yanga ilipata mgawo wa zaidi ya shs milioni 170 baada ya mechi hiyo.

SIMBA NA AZAM KUCHUANA CHAMAZI WIKIENDI HII



Kikosi cha Simba kinataraji kushuka dimbani kesho kuvaana na Azam Fc katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Chamazi ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao.

Akizungumza jijini jana Katibu mkuu wa Simba Evodius Mtawala alisema mbali na mchezo huo wanaamini mechi kati ya  Taifa Stars na Msumbiji pia itakuwa kipimo tosha kwa wachezaji wao kabla ya kuivaa Kiyovu siku mbili baadae.

Simba itaingia uwanjani kuivaa Azam bila ya nyota wake walioitwa kwenye kikosi cha Stars, imefufua matumaini baada ya majeruhi wake Amir Maftah, Ulimboka Mwakingwe pamoja na Haruna Moshi kupona na kucheza katika pambano hilo.

Mtawala alisema timu hiyo inaendelea na mazoezi chini ya kocha Milovan tayari kwa pambano hilo na wamepani kuendeleza heshima nyumbani na kuhakikisha wanatoka na ushindi.

"Jumamosi hii tutacheza na Azam asubuhi katika pambano la kirafiki, tunaendelea vyema na maandalizi ya mchezo wetu wa marudio ambao utachezwa hapa nyumbani wikiijayo na kila kitu kinakwenda vizuri," alisema Mtawala.

MECHI YA MARUDIANO YA YANGA NA ZAMALEK KUPIGWA JESHINI

Uwanja wa soka unaomilikiwa na Jeshi la Misri, uliopo jijini Cairo, Misri ndiyo utakaochezwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa kati ya Zamalek na Yanga ya Tanzania.

Maofisa wa uwanja huo, ambao pia ni chuo maalumu cha masuala ya kijeshi walisema juzi kuwa tayari wameshapata taarifa kuhusiana na suala la mechi hiyo.

Lakini maofisa hao ambao hawakutajwa majina, walikaririwa na mtandao wa Misri wa Ahram Online, wakisema wana asilimia kubwa kwamba mechi hiyo itachezwa jeshini.

Kulikuwa na hofu kama mchezo huo ungeweza kufanyika Cairo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia maafa ya mashabiki 74 yalitokea kwenye Uwanja wa Port Said wakati wa Mechi ya Al Ahly na Al Masry.

Zamalek imepewa ruhusa ya kucheza kwenye uwanja huo wa kijeshi na itachezwa bila ya mashabiki kufuatia kufungiwa kwa timu hiyo kucheza mechi zake za Ligi ya Mabingwa bila ya mashabiki na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufuatia vurugu za mashabiki wa timu hiyo kwenye mechi dhidi ya Club Africain ya Tunisia msimu uliopita.

Zamalek, ambayo ilichukua taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya mwisho mwaka 2002, ilitoka sare ya bao 1-1 na Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Jumamosi iliyopita na sasa zitarudiana Jumamosi wiki ijayo.

NIZAR KHALFANI HATIHATI KUIKWAA MSUMBIJI!

Timu ya Philadelphia Union imemuacha kiungo Mtanzania Nizar Khalfan ikiwa ni wiki chache baada ya klabu hiyo kuwa imemsajili toka Vancouver Whitecaps. Philadelphia Union ilimsajili Nizar kwenye mchakato wakubadilishana wachezaji uliofanyika November 23 mwaka jana baada ya Vancouver Whitecaps kumpeleka Philadelphia siku moja kabla. Kuachwa kwa Nizar kunaacha wazi nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa kwenye timu hiyo huku ikisaliwa na wachezaji saba tu wa kimataifa kati ya nafasi tisa zinazoruhusiwa na MLS kwa wachezaji wa kimataifa toka nchi nyingine .
Khalfan ambaye ni mzaliwa wa Mtwara , aliichezea Vancouver mechi 22 za msimu wa Ligi ya marekaniikiwemo michezo 9 ambayo alikuwemo kwenye kikosi cha kwanza . Katika muda wa dakika       1, 066, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23 alifanikiwa kufunga bao moja huku akitoa pasi nne za mwisho . Khalfan Alijiunga na Vancouver mwaka 2009 wakati timu hiyo ilipokuwa kwenye ligi daraja la kwanza ambapo alicheza michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029.
Taarifa ambazo nimezipata hivi punde Nizar huenda asije nchini kujiunga na kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Msumbiji.
Nizar yupo bize akitafuta timu ya kujiunga nayo kabla ya ligi kuu ya Marekani maarufu kama MLS kuanza hapo mnamo mwanzoni mwa mwezi wa tatu.

BAADA YA KUFUNGWA 3-1 NA NAPOLI: ABRAMOVICH ATAKA MAELEZO KWANINI AVB ALIWAPIGA BENCHI AKINA LAMPARD.

Imefahamika Roman Abramovich alitaka maelezo ya kutosha kwanini Andre Villas-Boas aliwapiga benchi Ashley Cole, Frank Lampard na Micheal Essien.

AVB aliwaacha watatu hao katika kikosi kilichoanza katika mechi waliyofungwa 3-1 na Napoli in Champions league jumanne iliyopita.
Kutokana na hali ya hiyo mmiliki wa timu hiyo Abramovich alisisitiza kupewa maelezo ya kutosha kuhusu sakata la kutemwa wachezaji hao ambao siku mbili kabla waliponda mbinu za ufundishaji wa mreno huyo hadharani.

Mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Micheal Emenalo alimbana Villas-Boas kuhusu uchaguzi wake wa kikosi siku na akapeleka majibu kwa aliyemtuma, Roman Abramovich.

AVB alikiri: “Sikuongea na mmiliki mwenyewe badala yake nilipeleka taarifa kwa watu wa karibu yake kama vile Emenalo na wengine ili kupeleka majibu kwa mwenyewe Roman.

“Walitumwa kuniuliza. Hii ndio njia ya kawaida kuwasiliana na mmiliki. Naona kawaida tu. Alikuwa anataka kujua mawazo yangu juu ya uchaguzi wa kikosi ninaoufanya.

“Mmiliki alikasirishwa  na matokeo na aliuliza maswali kuhusu timu na mimi nikapeleka majibu.”
Lampard na Cole pamoja na Essien walimtolea uvivu manager wao walipopigwa benchi nchini Italy.
Pamoja na kufungwa na Napoli lakini AVB anasema alichagua kikosi sahihi.
“Ilikuwa ndio timu sahihi kucheza, japo tulifungwa lakini sina majuto. Uchaguzi wa kikosi ulikuwa sahihi.
“Nina mahusiano mazuri na Cole na Lampard lakini muda pekee unaokuwa ukisapotiwa na wachezaji ni pale na wenyewe wanapokuwa kwenye kikosi cha kwanza.
“Kitu muhimu kwa Chelsea ni kanuni na taratibu. Klabu ni muhimu kuliko mtu yoyote binafsi.”

“Nitafanya kila kitu ninavyoona mimi, na mtu yoyote hatakiwi kuwalaumu wachezaji kwa chochote.” Alimaliza AVB.  

EUROPA LEAGUE HATUA YA 16 BORA: MAN U KUANZIA OLD TRAFFORD DHIDI YA BILBAO, CITY WARUDISHWA URENO KUKIPIGA NA SPORTIN LISBON.


AZ Alkmaar v Udinese Calcio

Club Atlético de Madrid v Beşiktaş JK

FC Metalist Kharkiv v Olympiacos FC

FC Twente v FC Schalke 04

Manchester United FC v Athletic Club

R. Standard de Liège v Hannover 96

Sporting Clube de Portugal v Manchester City FC

Valencia CF v PSV Eindhoven
 
Mechi kuchezwa tarehe 8 na 15 Mwezi wa Tatu.

MATOKEO YA JUMLA YA UEFA EUROPE LEAGUE HATUA YA 32 BORA







               Man. City4-0Porto
Aggregate: 6-1
Referee: Wolfgang Stark (GER) – Stadium: City of Manchester Stadium, Manchester (ENG)
23 February 2012


Valencia1-0Stoke
Aggregate: 2-0
Referee: Markus Strömbergsson (SWE) – Stadium: Estadi de Mestalla, Valencia (ESP)


Athletic1-0Lokomotiv Moskva
Aggregate: 2-2 Athletic win on away goals
Referee: Pawel Gil (POL) – Stadium: San Mamés, Bilbao (ESP)


Twente1-0Steaua
Aggregate: 2-0
Referee: Robert Schörgenhofer (AUT) – Stadium: FC Twente Stadion, Enschede (NED)


PAOK0-3Udinese
Aggregate: 0-3
Referee: Tom Harald Hagen (NOR) – Stadium: Stadio Toumba, Salonika (GRE)


PSV4-1Trabzonspor
Aggregate: 6-2
Referee: Tony Chapron (FRA) – Stadium: PSV Stadion, Eindhoven (NED)

Club Brugge0-1Hannover
Aggregate: 1-3
Referee: William Collum (SCO) – Stadium: Jan Breydelstadion, Bruges (BEL)

Standard Liège0-0Wisła
Aggregate: 1-1 Standard Liège win on away goals
Referee: Milorad Mažić (SRB) – Stadium: Stade Maurice Dufrasne, Liege (BEL)


BeÅŸiktaÅŸ0-1Braga
Aggregate: 2-1
Referee: István Vad (HUN) – Stadium: BJK Ä°nönü Stadyumu, Istanbul (TUR)


Sporting1-0Legia
Aggregate: 3-2
Referee: Vladislav Bezborodov (RUS) – Stadium: José Alvalade, Lisbon (POR)

Schalke3-1Plzeň
Aggregate: 4-2 Schalke win after extra time
Referee: Alan Kelly (IRL) – Stadium: Arena AufSchalke, Gelsenkirchen (GER)


Metalist4-1Salzburg
Aggregate: 8-1
Referee: Antony Gautier (FRA) – Stadium: Metalist Stadium, Kharkiv (UKR)

Olympiacos1-0Rubin
Aggregate: 2-0
Referee: Stefan Johannesson (SWE) – Stadium: Georgios Karaiskakis Stadium, Piraeus (GRE)


Anderlecht0-1AZ
Aggregate: 0-2
Referee: Pedro Proença (POR) – Stadium: Constant Vanden Stock Stadium, Brussels (BEL)


Atlético1-0Lazio
Aggregate: 4-1
Referee: Martin Atkinson (ENG) – Stadium: Estadio Vicente Calderón, Madrid (ESP)


Man. United1-2Ajax
Aggregate: 3-2