Juma Kaseja akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mbele ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Bin Kleb, nyuma Abdulfatah. Kaseja amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.
|
Search This Blog
Saturday, November 9, 2013
PICHA: JUMA KASEJA AKISAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA YANGA SC
TUZO ZA MWANASOKA BORA WA TANZANIA: HARUNA NIYONZIMA AIBUKA KIDEDEA, AWABWAGA KIEMBA NA YONDANI
Hii ndio ilikuwa kamati iliyoratibu tuzo hizo :Zamoyoni Mogella ( Mwenyekiti ), Kenny Mwaisabula ( Kaimu katibu ), na wajumbe Shaffih Dauda, Boniface Wambura,Edo Kumwembe na Doris Malyaga. |
Godfrey Nyange akimkabidhi tuzo mwaamuzi bora Oden Mbaga.
Ezekiel Kamwaga akipokea tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa niaba ya Abdallah Kibadeni.
Zamoyoni Mogella akitoa tuzo ya bao la mwaka kwa mwakilishi wa Thomas Ulimwengu.
Kiungo wa Simba Amri Kiemba akipokea tuzo ya 11 Bora |
Niyonzima akikabidhiwa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka.
Haruna Niyonzima akikabidhiwa zawadi yake ya kuwa mwanasoka bora wa Tanzania |
Haruna Shamte ( kushoto ),Ramadhani Singano pamoja na mdau.
Joseph Kimwaga wa Azam Fc ndiye alichukua tuzo ya mwanasoka chipukizi.
Rais wa zamani wa SAFA,Kirsten Nematandani akimpatia tuzo Haruna Niyonzima ya mwanaoka bora wa kigeni wa mwaka.
Juma Nature Kibla akitumbuiza kwenye tuzo hizo |
|
Friday, November 8, 2013
TAARIFA KUTOKA TFF,MECHI YA JKT RUVU, COASTAL YAINGIZA LAKI 2/-
UHAI CUP KUANZA
KUTIMUA VUMBI NOV 17
Michuano
ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa
klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya
Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
Droo
ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8 mwaka
huu) mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu.
Kundi
A linaundwa na timu za Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City na
Yanga, wakati kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT na Ruvu
Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania Prisons ndizo
zinazounda kundi C.
Mechi
za ufunguzi kundi A Novemba 17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal Union (saa
2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Karume). Kundi B ni Ruvu
Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10
jioni- Karume).
Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na Tanzania
Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za ufunguzi Novemba 17
mwaka huu katika kundi C.
Robo
fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati nusu
fainali itapigwa Novemba 26 na 27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu
na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.
TANZANITE
YATUA SALAMA MAPUTO
Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake
chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili salama jijini Maputo, Msumbiji tayari
kwa mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia itakayochezwa
kesho (Novemba 9 mwaka huu).
Kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa
Tanzanite, Kidao Wilfred ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), timu hiyo chini ya Kocha wake
Rogasian Kaijage ilifanya mazoezi yake ya kwanza jana asubuhi.
Tanzanite itafanya mazoezi yake ya
mwisho leo (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo
utakaotumika kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa
za Msumbiji.
Nao wachezaji waliobaki kumalizia
mtihani yao ya kidato cha nne wameondoka leo saa 11 jioni kwa ndege ya LAM
wakiongozwa na naibu kiongozi wa msafara, Khadija Abdallah Nuhu ambaye ni
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).
KESSY
KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya
Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya
Afrika Kusini na Botswana.
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Afrika Kusini, Novemba 9
mwaka huu. Waamuzi kutoka Zambia ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba kumi.
Waamuzi
hao wataongozwa na Glads lengwe atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi
namba moja ni Bernadette Kwimbira kutoka Malawi, namba mbili ni Mercy Zulu na
mezani atakuwepo Sarah Ramadhani, wote wa Zambia.
Afrika
Kusini ilishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 5-2. Mshindi wa mechi hiyo
atacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Tanzania na Msumbiji.
MECHI YA JKT
RUVU, COASTAL YAINGIZA LAKI 2/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji JKT Ruvu na Coastal Union ya Tanga
iliyochezwa juzi (Novemba 6 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam
imeingiza sh. 201,000.
JKT
Ruvu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 85 na kushuhudiwa
na watazamaji 67 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 3,000 na 10,000.
Kila
klabu ilipata mgawo wa sh. 39,010 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 30,661.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 19,835, tiketi sh. 38,100,
gharama za mechi sh. 11,901, Bodi ya Ligi sh. 11,901, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,950 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 4,628.
Nayo
mechi kati ya Ashanti United na Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa
imeingiza sh. 24,931,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 5,333,590.
Wakati
huo huo, mechi za jana (Novemba 7 mwaka huu) kati ya Yanga na Oljoro imeingiza
sh. 34,902,000 kutokana na watazamaji 6,045 ambapo kila klabu imepata sh.
7,812,477.95. Mechi ya Azam na Mbeya City iliyochezwa Azam Complex yenyewe
imeingiza sh. 15,973,000 kwa watazamaji 4,857 na kila klabu imepata sh.
3,953,162.
WATATU WAOMBEWA ITC KUCHEZA UJERUMANI
Watanzania watatu wameombewa Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) ili
wacheze mpira wa miguu nchini humo.
Wachezaji hao ni Charles Mishetto na
David Sondo wanaombewa hati hiyo ili waweze kujiunga na timu ya SpVgg 1914
Selbitz, wakati Eric Magesa ameombewa kibali hicho ili achezee timu ya klabu ya
SC Morslingen.
Hata hivyo, katika maombi hayo DFB
haikuleza hapa nchini walikuwa wakicheza katika klabu zipi. Wachezaji wote
wameombewa hati hiyo kama wachezaji wa ridhaa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
NUKUU YA LEO!
“Nilikuwa
namdai fedha zangu Chang’walu na wala sikumkimbiza kwa ajili ya kumpiga”
-Kauli ya
kiungo wa Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’ alipohojiwa kwa madai ya kutaka kuwapiga
waamuzi katika pambano la Yanga dhidi ya African Lyon.
MASHABIKI WA MBEYA CITY WATOA MISAADA HOSPITALI YA AMANA
Mwenyekiti wa
Mashabiki wa Mbeya City, Wille Mastala akikabidhi Msaada wa Sabuni Sukar na
Poda kwa Muunguzi Mkuu Agnes Mwanga (kulia) kwa ajili ya akina mama
kwenye Hosptali Amana jijini Dar es Salaam jana. Picha na John Dande
Baadhi ya mashabiki wa Timu ya Mbeya City wakiwa wamebeba Baadhi ya Vitu kwa ajili ya Msaada wa wagonjwa wa kina mama wa Amana Hosptali jijini Dar es Salaa jana
Baadhi ya mashabiki wa Timu ya Mbeya City wakiwa wamebeba Baadhi ya Vitu kwa ajili ya Msaada wa wagonjwa wa kina mama wa Amana Hosptali jijini Dar es Salaa jana
Thursday, November 7, 2013
NYOTA WA CHELSEA WALIPOKUTANA NA RAFAEL NADAL.
Rafael Nadal akiwa kwenye picha na Willian, Oscar na Ramires.
Hapo jana usiku mara tu baada ya mchezo baina ya Chelsea na Schalke mchezaji nyota wa mchezo wa Tenisi toka nchini Hispania Rafael Nadal aliingia ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na kupiga picha na baadhi ya wachezaji wa Chelsea.
Subscribe to:
Posts (Atom)