Search This Blog

Saturday, January 25, 2014

YANGA YAANZA MZUNGUKO WA PILI KWA KUTOA KIPIGO - YAICHAPA ASHANTI 2-1

 Raha ya ushindi.....Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti United.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti United, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-1. Kutoka kushoto ni Frank Domayo, Simon Msuva na David Luhende. Yanga imeshinda 2-1.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la ushindi wa timu yao dhidi ya Ashanti United. 
 Idd Seleman wa Ashanti United akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Yanga, Simon Msuva.
 Davidi Luhende wa Yanga akiipangua ngome ya Ashanti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo.
 David Luhende akimtoka Hussein Mkongo wa Ashanti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
 David Luhende wa Yanga, akipiga mpira uliozaa bao la pili la timu yake. Huku Hussein Mkongo (kulia), akiwa hana la kufanya.
Benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na  Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm (kulia), Kocha Msaidizi, Charles Boniface na Kocha wa Makipa Juma Pondamali.
Moja ya heka heka zilizotokea katika lango la Yanga.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
 Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibaden akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akibadilishana mawazo na David Luhende wakati wa mapumziko.
Francis Dande

BREAKING NEWS: JUAN MATA AWASILI MANCHESTER - AKUTANA NA DAVID MOYES TAYARI KUFANYIWA VIPIMO





MANCHESTER UNITED WATHIBITISHA RASMI KUMSAJILI JUAN MATA

Thursday, January 23, 2014

KUUMIA KWA FALCAO NI PIGO KWA COLOMBIA & KOMBE LA DUNIA.



Habari mbaya leo kwenye michezo ni kuhusu majeraha ya mshambuliaji  Radamel Falcao aliyoyapata jana usiku kwenye mchezo kati ya timu yake ya Monaco dhidi ya timu ya ligi daraja la nne ya Chasselay kwenye kombe la Ufaransa.

Kwenye mchezo huo Falcao alifungia bao la kuongoza wakati timu yake ya Monaco ilipopata ushindi wa mabao 3-0 kabla ya kuumia, taarifa zilizotoka leo baada ya vipimo zinasema jeraha hilo litamuweka nje kwa kipindi cha miezi sita na kupelekea kuzikosa  fainali za kombe la dunia baadae mwezi wa sita nchini Brazil.

Kukosekana kwa Falcao kwenye mashindano hayo sit u pigo kwa nchi yake ya Colomboa bali litakuwa pigo kwa mashindano hayo kumkosa mshambuliaji huyo.

CHELSEA YATHIBITISHA KUFIKIA MAKUBALIANO NA FC BASEL JUU YA UHAMISHO WA MOHAMED SALAH.



EXCLUSIVE: CHELSEA YAIPIGA CHINI LIVERPOOL NA KUFANIKIWA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI WA FC BASLE MOHAMMED SALAH.



Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuipiku Liverpool na kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Fc Basle ya nchini Uswizi raia wa Misri,Mohammed Salah kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 1.
Salah maarufu kama Messi wa Misri kwa muda mrefu alikuwa akiwaniwa na Liverpool.

TANZIA: FUNDI WA VIFAA VYA TENNIS GYNKHANA CLUB NDUGU CHARLES KIANDO AFARIKI DUNIA



Siku chache baada ya kumazilika kwa Mashindano ya vijana ya Tennis ukanda wa Afrika Mashariki Kati,kwenye viwanja vya GhymKhana Jijini Dar-es-salaam,Tasnia hiyo imepata pigo baada ya Fundi Mkuu wa vifaa vya Tennis Kutoka Klabu ya Gymkhana Charles Kiando kufariki Dunia.
Charles Kiando Maarufu kama Tola,amefariki Dunia Alfajiri ya Leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa baada ya kuzidiwa Ghafla,na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mwananyamala Kwa Ali Maua Jijini Dar-es-salaam.
Clouds TV ilifanya nae mazungumzo enzi za Uhai wake,ili kuufahamisha UMMA wa Tanzania juu ya umuhimu wa Fundi huyo Mkongwe mkongwe kwa takribani miaka ishirini sasa.
Clouds Media Group,inaungana na wadau wote wa Michezo Tanzania,kutoa pole kwa familia ya Marehemu kwenye kipindi hiki kigumu,Mungu Amlaze mahala Pema Peponi Amin.