Search This Blog

Saturday, August 24, 2013

PICHA: HARUNA MOSHI BOBAN - KADO WANG'ARA COASTAL UNION IKIWAUA OLJORO 2-0 ARUSHA

 Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' akisalimiana na Yayo Kato, kabla ya mpira kuanza.

                                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Oljoro JKT.




                         Yayo Kato akituliza mpira mbele ya Majaliwa Mbaga wa JKT Oljoro.

 Mashabiki wa Coastal Union waliuteka uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo. Watu wote mazungumzo ni kigoma hiki.

 Yusuf Machogote wa JKT Oljoro akijaribu kukimbilia mpira na Suleiman Selembe leo.

 Hiki ni kipindi cha pili Selembe alikosa bao la wazi yeye na golikipa. Na hili lilikuwa bao la pili kukosa baada ya kipindi cha kwanza kupewa pasi murua na Yayo akabaki na golikipa akapiga kichwa mpira ukatoka nje.

 Uhuru Suleiman akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Oljoro leo.

 Selembe akimpongeza Abdi Banda baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya dakika 16 ya mchezo.

 Hapa Banda akiwa anarudi kutoka kufurahia na mashabiki wa Coastal Union waliofurika uwanjani leo.

 Mwamuzi wa leo kutoka Mwanza Jacob Adengo akimwonyesha kadi ya Njano Banda kwa kutoka nje ya uwanja wakati mpira ukiendelea.

 Shaaban Kado leo alikuwa nyota ya mchezo baada ya kuopoa michomo mingi ambayo iliyawacha watu mdomo wazi.

 Hapa mashabiki wa Oljoro wakiingia uwanjani kipindi cha pili baada ya kupigiwa simu waje kuongeza nguvu maana kigoma cha Wagosi kiliwazidi nguvu.

                                                 Morocco akisisitiza jambo uwanjani.



               Haruna Moshi Boban leo alivutia watu wengi kutokana na style yake ya kucheza.

 Hamad 'Basmat' akikokota mpira bila wasiwasi wowote, leo alipiga beki nzuri hakuna mchezji aliyethubutu kumsogelea.

                                                Selembe akituliza mpira kwa ufundi mkubwa.

                         Haruna Moshi 'Boban' akituliza mpira mbele ya wachezaji wawili wa Oljoro.


              Mashabiki wa Coastal Union baada ya mpira kuisha ilikuwa raha tu mwanzo mwisho.

Nassor Binslum, Akida Machai na Heme Hilal wakiwa katika viunga vya jiji la Arusha baada ya mechi kuisha kwa ushindi 2-0.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://coastalunionsc.blogspot.com

MATOKEO KAMILI YA LIGI KUU YA VODACOM: SIMBA YAVUTWA SHARUBU - YANGA YAUA, AZAM NA MTIBWA NGOMA DROO

Matokeo kamili ya Ligi Kuu Tanzania

Mtibwa Sugar 1 - 1 Azam FC
Rhino Rangers 2 - 2 Simba SC
Coastal Union 2 - 0 JKT Oljoro
Mbeya City 0 - 0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 3 - 0 Tanzania Prisons
Young Africans 5 - 1 Ashanti Unite

LIGI KUU YA VODACOM LIVE SCORE: YANGA VS ASHANTI, SIMBA VS RHINO, MTIBWA VS AZAM




Mbeya City 0-0 Kagera Sugar 

FT: JKT Oljoro 0-2 Coastal Union

FT Rhino Rangers 2-2 Simba wafungaji Imani Noel, Kipanga, Jonas Mkude 2

Dk 43 Simba 2-2 Rhino

Dakika 25 kipindi cha pili Rhino wanasawazisha. Simba 2-2 Rhino. 

Ashanti wanapata bao la kufutua machozi: Full Time Young Africans 5-1 Ashanti United 

 Full Time; Mtibwa Sugar 1-1 Azam Fc 

Dakika 90' Young Africans 5-0 Ashanti United Tegete 10' 58' Msuva 48' Niyonzima 74' Khalfan 90' 

Dakika ya 82, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Jerson Tegete

Kutoka Tabora mpira ni mapumziko Simba 2-1 Rhino

Dakika 74' Young Africans 4-0 Ashanti United Tegete 10' 68' Msuva 48 Niyonzima 74' 

Jonas Mkude tena anaiandikia Simba bao la pili - Rhino Rangers 1-2 Simba Sc Jonas Mkude 11' 38'Penati

Dakika 36' Rhino Rangers 1-1 Simba Sc 

Dakika ya 68, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Hussein Javu kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu

Dakika ya 58, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la tatu

Dakika 49' Mtibwa Sugar 1-1 Azam Fc Luizio 4' Morris 33' Mabadiliko anatoka MCha Khamis aingia Kipre Bolou 

Dakika ya 50' JKT Ruvu  2-0 Prisons mfungaji Elias 46' 

Jonas Mkude anaiandikia Simba la kuongoza dhidi ya Rhino 

Yanga 2-0 Ashanti (Msuva dk 47)

Kipindi cha pili kinaanza uwanja wa Taifa Dsm - Yanga vs Ashanti.

Updates: Mpira ni Mapumziko
Yanga 1 Ashant 0
Oljoro 0 Coastzl 2
Mtibwa 1 Azam 1
Ruvu 1 Prisons 0

Rhino 0 Simba 0 (Mechi inaendelea)

Mechi kati ya Simba vs Rhino inaanza sasa katika dimba la Al Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza mchezo wa Yanga vs Ashanti zimemalizika. Yanga 1-0 Ashanti

 DK 35 - JKT Oljoro 0-2 Coastal Union Mfungaji Abdi Banda 10' lingine Oljoro wamejifunga dakika 29.

Yanga 1 Ashant 0
Mtibwa 1 Azam 1
Oljoro 0 Coastal 1

Tabora mechi bado haijaanza

Kutoka Morogoro Mtibwa 1-1 Azam - Dakika ya 34
 
 Taarifa ya mwisho kutoka Tabora kwenye mechi kati ya Simba vs Rhino - mechi imechelewa kuanza kutokana na wachezaji kadhaa kutokamilisha leseni zao.

Dakika ya 18, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Frank Domayo kuchukua nafasi ya Athuman Idd 'Chuji' aliyeumuia
Dakika ya 15, Young fricans 1- 0 Ashanti United

Dakika ya 10, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la kwanza

Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Young Africans Vs Ashanti United

ROBERT LEWANDOSKI: "KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA MAN UNITED, REAL MADRID NA CHELSEA.'


On target: Lewandowski scored the winner for Dortmund in a 1-0 victory over Werder Bremen on Friday night


Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amefunguka na kusema kwamba amekataa kujiunga na vilabu vya  Manchester United, Chelsea na Real Madrid ili aendelee kucheza kwenye Bundesliga.
Baada ya tetesi za usajili kumhusisha na vilabu kadhaa barani ulaya, ikiwemo klabu hasimu ya Dortmund - Bayern Munich, Lewandowski sasa amesuluhisha tofauti zake na Dortmund na ameripotiwa kwamba tayari ameongezea marat tatu mshahara wake.a

Na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amezungumza na kusema alifuatwa na vilabu kadhaa, pamoja kuzungumza binafsi na kocha Jose Mourinho.

Baada ya kufunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa raundi ya kwanza wa nusu fainali ya Champions League, Mpoland huyo alipokea ujumbe wa simu kutoka Mourinho: 'Nataka uungane nami katika klabu yoyote nitakayoenda.'
Lewandowski aliiambia The Sun: 'Naweza kuthibitisha kwamba niliongea na Mourinho. Tulikuwa na mazungumzo mara kadhaa huko nyuma. Nina namba yake ya simu kwenye simu yangu. Ninahisi fahari kuwa kocha mwenye jina kubwa kama lake kunihitaji.
'Mwaka mmoja uliopita niliongea na Sir Alex Ferguson na kwa kweli lilikuwa jambo kubwa na muhimu kwangu.
Quadruple: Lewandowski scored four against Real Madrid in the first leg of the Champions League semi-finals



'Kustaafu kwa Sir Alex hakukubadilisha maamuzi yangu ya kutokwenda England. Aliongea nami mwaka mmoja uliopita, lakini haukuwa muda sahihi kuondoka. 

'Premier League ni kubwa sana, kama ilivyo La Liga. Lakini  Bundesliga ni kila kitu cha kuifanya kutawala kwa miaka mitano ijayo.'
Lewandowski pia alithibitisha kwamba alikutana na raisi wa Real Madrid Florentino Perez kwenye dimba la uwanja wa Bernabeu muda mfupi baada ya Dortmund kuweza kufuzu kucheza fainali ya Champions League.

USAJILI SIMBA MAJANGA: ABEL DHAIRA NA OWINO HAWANA VIBALI VYA KUFANYA KAZI NCHINI - AMISI TAMBWE NA GILBERT KAZE HAWAJAPATA ITC, MOMBEKI NAE ATAKIWA KUKAMILISHA UHAMISHO KUTOKA PAMBA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.

Klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja mbalimbali nchini.

Klabu ya Simba inatakiwa kumfanyia uhamisho Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Mchezaji Joseph Owino tayari ITC imepatikana lakini hana kibali cha kufanya kazi nchini. Pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha kufanya kazi nchini.

Vilevile Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim kutoka Coastal Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20). 

Nayo Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.

JKT Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans). Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto (Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata (African Lyon).

Pia Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.

Tanzania Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro.


Kagera Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto Africans).

Pia Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work permit).

Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif (African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).

Oljoro JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.

 Nayo Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif (Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20.

Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz Chibwabwa (Villa Squad).

Wachezaji waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na ITC.
Kwa mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
Pia TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru (free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.

KOCHA PATRICK LEIWIG: SHOMARY KAPOMBE ANAPOTEZA MUDA AS CANNES - HASTAHILI KUICHEZEA TIMU YA DARAJA LA NNE

KIRAKA wa Tanzania, Shomari Kapombe ametambulishwa juzi Ahamisi kwenye mazoezi ya klabu ya AS Cannes ya Ufaransa, lakini Kocha Mfaransa aliyetimuliwa Simba, Patrick Liewig amesema timu hiyo haina hadhi ya Kapombe.
Hata hivyo, Simba imemjibu Liewig kuwa asiwe na wasiwasi kwani tayari Kapombe anatakiwa na timu ya daraja la pili ya Ufaransa.
Liewig aliiambia Mwanaspoti kwa simu kutoka jijini Paris, Ufaransa jana Ijumaa kwamba klabu hiyo ya daraja la nne ni ya hadhi ya chini sana kulinganisha na ubora wa Kapombe ambaye alipaswa kuchezea madaraja ya juu hivyo Simba imempeleka sehemu anakokwenda kupoteza muda wake.
Liewig alisema; “Naijua Cannes ni timu ndogo sana, inashiriki daraja la nne ni ya chini sana kulinganisha na ubora wa Kapombe niliyemfundisha hapo Simba. Yeye hadhi yake ni daraja la kwanza au la pili, na zipo klabu nyingi tu ambazo angeweza kupata nafasi.”
“Simba na huyo wakala wanampotezea Kapombe muda wake, wachezaji wakubwa wa Tanzania wanapaswa kukaa chini na kujipanga. Klabu zikae na watu wa maana zifanye mambo kwa kufuata weledi, mimi najuana na watu wengi sana kuanzia makocha na viongozi ambao naweza kuwaunganishia wachezaji wa Tanzania na wakacheza soka daraja la kwanza.
“Mchezaji mwenyewe ajipange anifuate aonyeshe nia ya kweli mimi nitashirikiana na viongozi nitamsaidia, lakini huko alikokwenda Kapombe sijapaafiki,” alisisitiza kocha huyo ambaye bado hajapata dili mpya.
Katika klabu hiyo, Kapombe atajumuika na ‘Waswahili’ wanne kutoka Burundi, Uganda, Senegal na Togo.
Kapombe atakuwa katika klabu hiyo na iwapo atauzwa ndio Simba itapata mgawo wake.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe aliliambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa hawana wasiwasi na suala hilo kwani tayari Kapombe ameivutia timu ya daraja la pili.
“Sisi tunajiamini na mambo tunayoyafanya, hapo nazungumza na wewe nilikuwa napata mawasiliano kutoka Ufaransa kuwa kuna timu ya daraja la pili inamhitaji Kapombe. Hao AS Cannes wakimuuza Kapombe sisi tunapata asilimia 40,” alisema Hanspoppe.

SOURCE: MWANASPOTI

USAJILI WA BALE: BAADA YA JANA KUANZA KUUZA JEZI ZAKE - LEO HII REAL MADRID WAANZA KUTENGENEZA JUKWAA LA KUMTAMBULISHA MCHEZAJI MPYA

Gareth Bale anakaribia kutua Real Madrid

BSW25jqIgAAKTWM {Pictures} Real Madrid preparing stage for tomorrows presentation of Gareth Bale [AS]
Ujeniz wa jukwaa kubwa la kutambulishia wachezaji wakubwa wanaosajiliwa na Real Madrid ukiendelea mapema jana mchana. Inaaminika Real Madrid wapo katika hatua za mwisho za kumsajili Gareth Bale kwa ada ya uhamisho wa £94m ambayo itakuwa rekodi mpya ya dunia baada ya ile £80m waliyolipa Madrid kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United miaka minne iliyopita.
Miaka minne iliyopita Cristiano Ronaldo alikuwa mtu wa mwisho kupita juu ya jukwaa hili - na kama habari zilizopo ni za kuaminika basi Gareth Bale akiwa na jezi yake namba 11 atakuwa mchezaji mwingine kutoka ligi kuu ya Uingereza kupanda kwenye jukwaa ndani ya uwanja wa Santiago Bernabeu ndani ya siku chache zijazo

BSW3fY9CcAE8LT0 {Pictures} Real Madrid preparing stage for tomorrows presentation of Gareth Bale [AS]

EXCLUSIVE: HIVI NDIVYO UWANJA WA NAMFUA ULIOPO SINGIDA ULIVYO - UPO KATIKA MAZINGIRA MABOVU MNO

Hii ndio hali halisi ilivyo katika uwanja mkongwe na wa kipekee ambao unafaa kuchezewa mechi za ligi wa Namfua uliopo mjini Singida.


Nje ya uwanja kulivyo

Hali ya mazingira ya uwanja ni mbaya sana - kuna uchafuzi wa mazingira wa hali ya juu




Uwanja huu kuta zote zipo katika hali mbaya ya kimazingira kutokana na kujaa vinyesi na mikojo

Friday, August 23, 2013

DIAMOND PLATNUMZ, MRISHO MPOTO NA WASANII WENGINE WALIVYOSHIRIKI KATIKA SEMINA YA 'KAMATA FURSA TWENZETU'

Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa  Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na wengineo.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 

 Baadhi ya Wakazi wa Tabora wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiliamali iliyokuwa ikiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo
Picha ya pamoja,kiukumbusho zaidi,Msanii Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond,akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye  ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora,kushoto kwake ni Bwa.Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. .
 Mmoja wa akina Mama wajasiliamali kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria akiwa na bidhaa zake alizozitengeneza yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza ndani ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo imewahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi mbalimbali wa mji wa Tabora,Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
 Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga ( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora),Mh. Elibariki Kingu wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil
 Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.

 Baadhi ya wakazi wa Tabora wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi  Student's Center mkoani  Tabora mapema leo,ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa,ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,mikopo,akiba sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.