Hivi karibuni kumetokea hali ya Sintofahamu kuhusiana na Uchaguzi kuu wa TFF uliopangwa kufanyika Tarehe 24/2/2013, mimi nilikuwa mmoja kati ya watanzania wengi waliojitokeza kuomba nafasi mbali mbali nikiwa nawania nafasi ya makamu wa Rais, matarajio yangu ya kuwania nafasi hiyo yalianza kuingia dosari kwa mara ya Nne(4) tangu 2008 katika chaguzi mbalimbali ambazo TFF ina maslahi nazo.
Kamati ya Uchaguzi ililiondoa jina langu kwa sababu mbili.
- Kamati inaheshimu maamuzi ya Kamati ya Jaji Mkwawa ya 2008 yaliyoniondoa katika kinyang’anyiro hicho.
- Sababu ya pili ni kuwa niliipeleka Simba mahakamani.
Katika kujaribu kutekeleza na kulinda maslahi yao kwa kuitumia kamati ya Rufaa za Uchaguzi, kwa ulafi wa kamati hiyo imejikuta ina kula mpaka vidole vyake, huku ikisema kuwa kuhusu wambura wanaheshimu maamuzi ya kamati ya Jaji mkwawa, ni kwa nini hawakuheshimu maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya prof FIMBO yaliyonisafisha wakati wa uchaguzi wa MARA? hivi tujiulize Kamati ile ilinifungia maisha nisigombee tena uongozi wa Mpira wa Miguu.
Kama kwenda mahakamani ni Kosa ni vipi leo Sunday Kayuni anakuwa mkurugenzi wa Ufundi wa TFF wakati aliwahi kuishitaki TFF katika mahakama ya Hakimu mkazi ya KISUTU kesi na 21 ya 2004. Kamati ya Uchaguzi ya Lyatto pia Imempitisha Stanley lugenge kugombea ujumbe wa kamati ya Utendaji kanda ya Njombe na Songea huku kamati ikijua wazi alishirikiana na Sunday Kayuni kuishitaki TFF mahakamani inachoonekana kwenda mahakamani ni dhambi kwa Wambura tu.
Kamati ya Jaji mkwawa iliyotengua maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF 2008 baada ya kuliondoa Jina la Jamal Malinzi kwenye orodha ya wagombea Uraisi wa TFF, ni kwanini Kamati ya Mtinginjola haikuliona hilo katika mazingira hayo ninaamini TFF na Raisi wake kwa njia moja au nyingine wana mkono kwenye hili la kuondoa jina la MALINZI Kwa sabau zifuatazo,
- 2008 Jamali malinzi aligombea Urais wa TFF wakichuana na Tenga, katika hatua za awali za Mchakato Jina la Malinzi liliondolewa(kukatwa) kwenye orodha ya wagombea na kamati ya Uchaguzi iliyokuwa chini ya Tandau kwa sababu hizi hizi zilizo tolewa sasa na mtu wa kufikirika anayeitwa AGAPE FUE. Malinzi alikata rufaa kwenye kamati ya Rufaa chini ya Jaji Mkwakwa, kwa mbinde jina lake likarudishwa kugombea, Katika Uchaguzi ule Kura hazikutosha kwa Malinzi, Tenga akachaguliwa kwa mara ya Pili.
Mara baada ya Uchaguzi, TFF alitoa shukurani na kuipongeza iliyokuwa Kamati ya Uchaguzi kwa kazi nzuri kwa na kwateua katika kamati mbali mbali za TFF na wengine kuingia katika Kamati ya Utendaji.
Kamati ya Rufaa ya Jaji Mkwawa iliondolewa kwani wajumbe waliokuwa wameonekana walikuwa na nguvu na ushawishi kwenye kamati ile waliondolewa bila hata kushukuriwa wala kuteuliwa katika kamati pamoja na kwa nzuri mbalimbali walizokuwa wameifanyia TFF kwa kuwa tu walishiriki kulirudisha jina la Jamal Malinzi agombee Urais wa TFF kumpambana na TENGA wajumbe wa kamati ile walikuwemo DR Dau-Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mwanasheria William Urio- mkurugenzi Mkuu PPF, Marehemu Gratian Matovo wote hao hawakuteuliwa tena kwenye kamati ndogo ndogo za TFF.
- Mwaka 2012 TFF akijua wazi FIFA haikuiagiza TFF kuunda kamati ya rufaa ya uchaguzi ila ilishauri kuwa sio vyema kamati ya uchaguzi ikwa ndio ya mwisho kwenye maamuzi ya Uchaguzi kwani yenyewe pia ndio inasimamia chaguzi hizo ili haki itendeke kutokana na ukweli wa Suala langu,TFF iliamua kuunda kamati nyingine kusikiliza rufaa za uchaguzi.
TFF ilikuwa inafahamu fika Kanuni za uchaguzi mkuu wa TFF zilikuwa zinaelekeza masuala ya rufaa za Uchaguzi wa TFF yatashughulikiwa na Kamati ya Rufaa ya TFF, lakini kwa jinsi Kamati ya Rufaa ya TFF inayoongozwa na Prof Fimbo ilivyo shughulikia suala langu katika Rufaa ya FAM(Mara) na kunipa Ushindi, TFF Hakufurahishwa na ilihisi katika uchaguzi huu isingeweza kuishawishi kamati Prof Fimbo iwakate au kuwapitisha watu inaoataka wao.
Ili kutimiza matakwa yake Tff ikaamua kuvunja na kuisigina Katiba ya TFF kwa kutoa waraka wa kubadili katiba kinyume na katiba ya TFF Ibara 22(1), 24(1)(l),27(1) ili aweze kuunda kamati zenye hila ambazo zitatekeleza amri zao, ambazo kwa kiwango kikubwa amefanikiwa kwa muda tu. TFF hakumtaka malinzi mwaka 2008 na haimtaki 2012 hainiingii akilini kuamini TFF haina mkono katika hili la kukatwa malinzi.
Nina hakika Jamal Kupitishwa na Kugombea Kagera ilikuwa ni kwa mbinde, kila njia na mbinu za kuondoa jina lake kupitia kamati ya Uchaguzi Kagera zilifanyika zikashindikana, nina hakika kama TFF hii ingeendelea kuwa madarakani au wakaingia vibaraka waao basi Malinzi na watu wengine wenye uwezo na nia njema na mpira wa miguu wa Tanzania wangeondolewa kwa kutumia Kamati zenye Hila na Majungu za TFF.
Mpango wa Kuondolewa kwa Jina la Malinzi kwenye uchaguzi zilianza mapema na zilifanywa na watu wa kambi ya Mgombea Urais mmoja ambaye kwa kiasi kikubwa alishirikiana na Tenga kusigina katiba na Kuunda kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ambayo sehemu kubwa imejaa marafaiki wa mgombea huyo, baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wenye heshima zao katika jamii Kama Prof Madundo Mtambo, Kamanda Mpinga wamejikuta katikati ya watu waliokuwa tayari wana hila na maamuzi yao kabla ya kikao.Pamoja ya kuwa na Mjumbe kutoka mahakama kuu (FRANCIS KEBWE) tulipata imani ya kuwa atasaidia kamati kuelewa kuwa kwa kuwa Kamati ya Juu yaani Rufaani ya Jaji Mkwawa 2008 iliisha toa uamuzi wa Uzoefu wa Malinzi na kwa kuwa hakuna chombo chochote kilicho wahi kuutengua basi walipaswa kuuheshimu na kuutumia kwenye maamuzi ya Kesi zinazo fanana za aina hiyo (PRECEDENCE) isipokuwa alikumbuka principle hiyo wakati anajadili rufaa ya wambura akasahau wakati wa rufani dhidi ya MALINZI, inawezekana ilikuwa ni bahati mbaya au ilipangwa na yeye alishiriki kujisahaulisha? Hiyo tunaiachia jammi ihukumu pamoja na kwamba kuna tetesi za ukaribu wake na mgombea mmoja wa Uraisi wa TFF na ameahidi kuwa atatumia kofia yake mahakamani kuhakikisha kama kuna mtu atataka kufungua shauri Mahakamani basi yeye atadhibiti kwa uwezo wake, ninapenda kumtahadharisha kutochanganya kazi na mambo ya jamii.
Mwenyekitiki wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi Ng Mtinginjola ni mwanasheria ninamfahamu , aliwahi kuwa kwenye kamati moja za DRFA wakati Nd Athmani Nyamlani akiwa katibu wa DRFA, na baadaye alihamishwa TFF kwenye kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, hakuna ubishi anafahamiana vizuri na mgombea Nyamlani, Kisheria Mtinginjola alipaswa kujiondoa wakati wa rufaa ya Malinzi kwa kuwa asingeweza kuwa na mikono misafi ya kutekelaza haki ya msingi ya Natural Justice kwani sheria inataka “ Si tu haki itendeke lakini ionekane kutendeka” kuna wanao sema Mtinginjola na Nyamlani waliwahi kufanya Kazi pamoja Katika Mahakama Temeke mmoja akiwa hakimu mwingine Karani wake, hivyo ni wazi Kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kwenye Uamuzi juu ya rufani ya Malinzi, Katiba ya TFF (2006)ibara ya 36(3) inamtaka “mjumbe wa kamati ya Utendaji kutoa tamko kama ana maslahi na mjadala wowote na kujiondoa kwenye mjadala kama kushirki kwake kuteleta mgongano wa kimaslahi”hivi ni kweli Mtinginjole na wenzake hawakulijua hili au uwepo wao katika kamati hii ulikuwa wa kimkakati zaidi huku wakisimamiwa na TFF ili majina ya MALINZI na WAMBURA yaondolewe? Kanuni za Uchaguzi Ibara 2(1) inazungumzia democrasia ya Mgawanyo wa madaraka katika Uwazi bila kuacha kitu katika mchakato wa Uchaguzi wa TFF, swali je Urafiki, Hila, Ghilba ndio uwazi huo.
UVUNJIFU WA KATIBA YA TFF
Mpango huu wa kuondoa majina ya wagombea ulirasimiwa rasmi kwa nguvu ya kubadili katiba kwa njia ya waraka ukilenga kuunda chombo dhalili chenye mlengo wa kusaidia wagombea Fulani washinde uchaguzi.
Hivi sasa kuna njama zinafanyika ili uchaguzi usifanyike /Uharibike ili walioko madarakani waeendelee kuwapo nina kila sababu ya kuamini hiyo kwa sababu zifiatazo;
- Katiba iliyotumika kuitisha uchaguzi huu ni batili kwa kuwa mabadiliko ya katiba hayakufuata utaratibu wa Kikatiba Kwani hakuna mkutano Mkuu wowote wa TFF uliokaa kupitisha mabadiliko hayo. TFF imempotosha Msajili wa vyama kupitia Ibara ya 76 ya katiba ya TFF ya kuwa Mkutano Mkuu wa TFF ulikutana Tarehe 15th December 2012 kufanya mabadiliko hayo huku ikijua sio kweli, nina penda kuitahadhalisha TFF hili sio swala michezo ni swala la Kisheria, hivyo kwa mujibu wa sheria za nchi mwenye mamlaka ya kutafsiri sheria(Katiba) ni mahakama hivo ni Ushauri wangu kwa TFF ili kuondoa uwezekano wa mkono wa sheria kuingia yafanyike yafuatayo,
i) kusimamisha Matumizi ya Katiba hiyo mara moja kwani sio halali ili kuondoa uwezekano wa kutafutwa haki kwenye Mahakama za Kiraia.
ii) Kuyafuta maamuzi yote na kuivunja Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inayoongozwa na Nd Mtinginjola, na ili matakwa ya kikatiba ya Uchaguzi yatimie rufani zote zirudishwe kwenye Kamati ya Rufaa kama katiba halali inavyotaka ili kukamilisha Mchakato wa uchaguzi.
iii) Maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Uchaguzi chini ya Lyatto yaheshimiwe na kama kuna wasio ridhika wakate rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya TFF.pamoja na kuwa maamuzi wa Lyatto hyana faida ya moja kwa moja na mimi lakini utaweka misingi bora ya kikatiba.
- Kwa mujibu wa katiba mpya ambayo mie naaita sio halali ibara ya 76 katiba hiyo imeeanza kutumika tarehe 15/12/2012 na Kanuni za Uchaguzi zimeanza kutumika tarehe 7/jan/2013 kanuni hizi na katiba yake ndio zilizotumika kuitisha uchaguzi huu.
Baada ya kupitisha katiba na kuanza kutumika TFF ilipaswa kuunda Kamati Mpya ya uchaguzi, Kwa mujibu wa Katiba ya TFF ibara 49(4) Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi anapashwa kuwa na taaluma ya Sheria(mwanasheria) sifa ambayo mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Bw Deogratius Lyatto hana sifa hiyo na hivyo ushiriki wake kuwa kinyume cha katiba ya TFF, kwa maana hiyo kuufanya mchakato wote wa uchaguzi kuwa batili na unapaswa kufutwa na kuteua kamati mpya ili mchakato uanze upya hivyo kuchelewesha kupatikana kwa viongozi wapya wa TFF.
- Kanuni hutengenezwa ili kuwezesha utekelezaji wa Katiba husika. Hivyo katiba hupitishwa na kusajiliwa kwanza na baadae hutungwa kanuni, cha kushangaza Kanuni za uchaguzi za tff zilipitishwa na kusainiwa Tarehe 7/jan/2013 wakati katiba TFF ilisajiliwa na kugongwa mhuri wa msajili Tarehe 10/jan/2013 siku tatu (3) baada ya kanuni kusainiwa. Swali linakuja kanuni hizi zilitungwa kwa mujibu wa katiba gani? Kwa maana hiyo kanuni za uchaguzi ni batili na katiba ni batili kisheria. Ninaishauri TFF ili kuondoa uwezekano wa kuingiza tff kwenye mgogoro wa kisheria uamuzi wa busara wa kuachana na Katiba batili ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania kwa kusimamisha matumizi ya katiba mpya batili ya TFF na matokeo ya maamuzi yote yanayotokana na katiba hiyo.
………………………………….
MICHAEL RICHARD WAMBURA
February 14, 2013