Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana jana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Short alisema ushawishi wa Malkia wa Nyuki umechangia yeye kutoa mwaliko huo na anaamini timu zote zitafaidika.
"Mazungumzo yetu na Rahma yalikuwa mazuri sana, nimefarijika na ninaamini mwaliko niliotoa utakuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kwa kuwa mwanamama huyu amenishawishi," alisema.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu.
Awali Simba, ilijulikana kwa jina la Sunderland.
YeboYebo mpoooooo
ReplyDeleteNaamini huu ni mwanzo mzuri mengi yanakuja nawatakieni kila la kheri simba
ReplyDeleteMbele twasonga tuweke tofauti zetu pembeni.....Simba imara
ReplyDeletewazee wa ndala sijui wanajisikiaje, kwa pamoja simba kanyaca twende ila tuweke siasa pembeni tuijenge simba ya kisasa
ReplyDeleteTUKAJIFUNZE KWA AZAM FC HAPA HAPA DSM KABLA YA KWENDA ENGLAND AMBAKO NI MBALI SANA
ReplyDeletetumkabidhi malkia wa nyuki timu,rage aendelee na siasa kwa kuwatumikia wana tabora!
ReplyDelete