Huu ni mwaka
2013,ukirudi nyuma kwa miezi minne yaani mwezi wa 11 mwaka 2012,yalifanyika
mashindano ya Soka kwa Timu za Taifa kutoka Ukanda wa Africa Mashariki na
Kati,maarufu kama Challenge.
Mmoja wa
washiriki wa michuano hiyo iliyomalizika kwa wenyeji Uganda kuitwaa,ni Timu ya
Taifa ya Tanzania Bara,ambao walitolewa katika hatua ya nusu fainali na ndugu
zao Tanzania Visiwani.
Kitendo cha
Timu Zote mbili yaani Tanzania Bara na Visiwani kufika nusu fainali,kilikuwa
furaha tosha kwa Watanzania wote kwa ujumla katika kipindi cha mashindano hayo.
Pia,Timu ya
Taifa ya Tanzania Taifa Stars,hivi karibuni imecheza mechi tatu za
kirafiki,ambapo mchezo wa kwanza imeshinda bao 1-0 dhidi Zambia,mechi ya pili
ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Ethiopia wakati wiki mbili zilizopita
imeshinda goli moja kwa bila dhidi ya Mabingwa wazamani wa Africa Cameroon.
Matokeo ya
mechi hizi ukijumuisha na hatua zilipofikia timu za Taifa za Tanzania Bara na
Visiwani,yamekuwa tumaini jipya la kufufuka kwa soka la Tanzania na hatimaye
kufanya vyema katika michezo tofauti ikiwemo ya kufuzu Mataifa ya Africa.
Wakati
Watanzania wakiunganisha Sara zao kuliombea Soka la nyumbani,Kamati ya uchaguzi
na kamati ya Rufani ya uchaguzi mkuu wa TFF na Bodi ya Ligi wameibuka na jambo
jipya lakukatisha tamaa juu ya mafanikio ya Soka la Bongo.
Kamati
hizo zimetumia sababu dhaifu,kuwaengua
baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika
Mwezi Feb 22 na 24,akiwemo mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo la
Soka Nchini Jamal Malinzi,kwa kukataa kusaini katiba ya mabadiliko ya leseni ya
Ligi na kutokuwa na uzoefu wa uongozi
kwa miaka 5
Maamuzi haya
yanaonesha wazi nia ya kuwabeba baadhi ya wagombea kwa kuwatengenezea mazingira
ya kushinda uchaguzi bila kupingwa,hii ni aibu kwa wadau husika hasa katika
wakati huu ambapo kila mtu anafahamu kinachoendelea kutokana na kuwepo kwa
uwazi na ukweli.
Aidha Maamuzi
haya yanalenga kurudisha nyuma maendeleo ya Soka la Bongo,kwa kuwa baadhi ya
wagombea walioenguliwa,pengine walikuwa na mipango thabiti ya kuliinua Soka
hili na kulifikisha mbali zaidi ya hapa.
Katika
kuonesha kuwa kitendo hiki si haki na sio cha kiungwana,Naibu Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makala,ametoa tamko kali la kuitaka kamati ya
Uchaguzi ya TFF kusimamisha shughuli za
uchaguzi huo adi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi,ikiwa pamoja na kuwarudisha
wagombea walioenguliwa kimakosa.
Kama
ninafikiria vyema,basi ninaamini kuwa maamuzi ya kamati hii yaliyomshangaza
kila mpenda Soka na kuwavunja moyo waliokuwa njiani kupenda Soka,ni msukumo
kutoka kwa baadhi ya wagombea wanaotaka madaraka kwa hali na mali.
Hii ni hali
ya hatari kwa hatma ya Soka la bongo ambalo lilianza kuchanua,kwa kuwa uzoefu
unaonesha kuwa mtu anayetumia nguvu ya ziada kupata uongozi,huwa hayupo kwa
maslahi ya Taifa isipokuwa maslahi yake binfasi kama ilivyo kwa baadhi ya
Viongozi wa Siasa Nchini na nchi za jirani.
Mimi binafsi
ninaamini wakati muafaka na sahihi kwa Watanzania kukemea mambo haya yaliyopitwa
na wakati ni sasa,na sio baada ya maamuzi na mbinu za ya kurudisha nyuma Soka
kufanikiwa.
Sote
tunafahamu kuwa Mpira wa Miguu ni Mchezo unaoongoza kwa kupendwa Duniani
kote,na pia ni mchezo unaotoa ajira nyingi kwa Vijana wenye kipaji cha Mchezo
huo kiasi cha wachezaji wengine kuingia kwenye orodha ya watu matajiri.
Kutokana na
hilo,Wadau wote wa Soka na Michezo kwa ujumla nchini,tuungane kuhakikisha
jitahada za kukuza Soka la Bongo lenye vijana wenye ndoto za kufanikiwa kitaifa
na kimataifa na hatimaye kuitangaza Nchi zinafanikiwa kwa kuwa na uzalendo.
========
========
Huo ndo ushabiki wa kijinga, huvi Malinzi ndo kaonewa tu?
ReplyDelete