Search This Blog
Saturday, October 8, 2011
HUYU NDIYE MBWIGA WA SPORTS XTRA...
TAIFA STARS NDANI YA MARRAKESH
Kutoka Casablanca hadi Marrakech ambapo ni umbali wa kilometa 230, wenyeji Morocco waliisafirisha Stars kwa basi ambao ni mwendo wa saa tatu hadi kufika hapa. Baada ya kuwasili na kuingia hotelini, timu ilifanya mazoezi jana jioni, na leo usiku (kwa muda ule ule wa mechi) itafanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa mechi (the Great Stadium). Kocha Jan Poulsen leo amemtaja kiungo Henry Joseph kuwa kapteni kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 43,000.
Mitaani hapa Marrakech mashabiki wa Morocco wamekuwa wakiizungumzia mechi hiyo, na wana imani kuwa timu yao itaibuka na ushindi, hivyo kufuzu kwa ajili ya fainali za AFCON zitakazochezwa mwakani katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon. Morali kwa upande wa wachezaji wa Stars iko juu, na hadi sasa hakuna majeruhi kwa wachezaji wote 20 waliokuja na Stars hapa kupeperusha bendera ya Tanzania. Poulsen amesema atatangaza kikosi kitakachoanza baada ya mazoezi ya leo usiku.
HII NDO HOTEL WALIYOFIKIA INAITWA DU GOLF....
THOMAS ULIMWENGU AIFUNGIA TP MAZEMBE BAO LAKE LA KWANZA.
Friday, October 7, 2011
TWIGA STARS KUANZA NA NAMIBIA MATAIFA HURU YA AFRIKA
Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imepangwa kucheza na Namibia katika mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za nane za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani wakati mechi ya marudiano ya raundi hiyo ya awali itachezwa Dar es Salaam kati ya Januari 27, 28 na 29 mwakani.
Alisema iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Namibia, katika raundi ya kwanza itacheza na mshindi wa mechi kati ya Ethiopia na Misri ambazo pia zinaanzia raundi ya awali.
Mechi ya awali ya raundi ya kwanza itachezwa ugenini kati ya Mei 25, 26 na 27 mwakani.
Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Juni 15, 16 na 17 mwakani. Timu ambazo zinaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza kutokana na kuwa juu katika viwango vya ubora ni Afrika
Kusini, Cameroon, Equatorial Guinea na Nigeria.
Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ni Guinea, Ivory Coast, Kenya, Msumbiji, Zambia, Malawi, Morocco, Tunisia, Senegal, Burundi, Botswana, Zimbabwe, Uganda,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali na Ghana.
KOCHA MOSES BASENA KUMPA SOMO BOBAN
Kocha wa klabu ya Simba Mganda Moses Basena amesema kuwa anatambua matatizo ya mchezaji Haruna Moshi Boban na sasa anajipanga vizuri ili kuweza kuyashughulikia kwa faida ya timu yake kufanya vizuri katika mashindano inayoshiriki.
Kauli hii ya Basena inakuja siku moja tangu zitoke taarifa kuwa uongozi wa klabu hiyo unajipanga kumfungia boban na wenzie ambao ni wategaji wa mazoezi katika klabu hiyo.
Akizungumza na blog hii Basena alisema “"Nitakaa na Boban niongee naye, nitaendelea kumshawishi apende mazoezi, Boban namkubali ni mchezaji mzuri, lakini huwezi kuwa mzuri uwanjani halafu mazoezi ukazembea, ni lazima afuate programu yangu,"alisema.
KASEBA AMTAKA TENA CHEKA
Wiki moja baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Maneno Osward bondia Japhet Kaseba amesema kwa sasa yupo tayari kurudiana na Francis Cheka muda wowote.
Kaseba ameliambia gazeti hili kuwa kipindi alipopigana na Cheka na akapigwa kwa KnockOut alikuwa hana uzoefu, lakini sasa amejipanga na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
Alisema alikuwa akicheza ngumi, kisha akahamia katika Kickboxing, alipoamua kurudi katika ngumi ndipo muda mfupi akapangwa kucheza na Cheka hivyo hakuweza kumhimili.
Alisema kwa sasa amejiimarisha zaidi na yupo tayari kupigana na bondia yeyote yule.
Alisema ushindi alioupata mwishoni mwa wiki, alipocheza na Maneno Oswald ni ushahidi tosha kuwa anaweza kupambana na hivyo atamkabili Cheka bila matatizo.
“Mimi kwa sasa ninahitaji kukutana na yeyote yule na nina uhakika kuwa nitashinda kwa KO ni suala la kutafuta promota tu,” alisema Kaseba.
Cheka mwenye maskani yake mkoani Morogoro amekuwa tishio katika mchezo wa ngumi na kuibuka na ushindi katika kila pambano analocheza.
TAIFA STARS YAONDOKA, KADO ATEMWA
Siku chache baada ya kocha wake Sam Timbe kusema anacheza chini, golikipa Shaaban Kado na ameachwa katika katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 21 waliokuwemo katika msafara wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwenda Morocco kwa mchezo wa mwisho kuwania kufuzu fainali za Afrika.
Kado ambaye aliitwa na kocha Jan Poulsen katika kikosi cha mwanzo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wadau wa soka kwa madai hakuwa kwenye kiwango kizuri kama ilivyo kwa Mwadini Ally wa Azam, ameshindwa kupita katika chujio la wachezaji 21 waliotakiwa kwenda Morroco.
Nae ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa Taifa Stars ilitarajiwa kuondoka jana jioni kwa ndege ya Qatar Airways kwenda Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya wenyeji ambayo itachezwa Jumapili wiki hii.
Alisema msafara wa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Wallace Karia na una wachezaji 20, benchi la ufundi lina watu sita chini ya Kocha Mkuu Jan Poulsen.
“Naibu Mkuu wa Msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Alhaj Haji Ameir.
“Wachezaji ni Juma Kaseja, Shabani Dihile, Erasto Nyoni, Idrisa Rajab, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Nadir Haroub, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Shabani Nditi, Jabir Aziz, Mrisho Ngasa, Ramadhan Chombo, Abdi Kassim, Mbwana Samata, Dan Mrwanda, Mohamed Rajab, John Bocco, Hussein Javu na Nassoro Cholo.
“Mbali ya Poulsen, wengine kwenye Benchi la Ufundi ni Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Juma Mwankemwa (Daktari wa Timu), Alfred Chimela
(Meneja Vifaa) na Leopold Mukebezi (Meneja wa Timu).
Kwa mujibu wa Wambura, Stars itarejea Oktoba 11 mwaka huu saa mbili asubuhi.
YANGA YASAJILI NEMBO, YATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA
Uongozi wa Yanga umewataka wafanyabiashara wote ambao wanamiliki bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo kujisalimisha kabla ya Novemba.
Kauli hiyo ya Yanga imekuja kufuatia kuzagaa kwa vifaa vyenye nembo ya klabu hiyo ambavyo vinauzwa kiholela na wafanyabiashara na kuchapishwa au kutengenezwa bila idhini ya klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Celestin Mwesigwa alisema kuwa ni bora wafanyabiashara hao wakajisalimisha wenyewe kwenye klabu ili kujua wafanye nini ili kuepuka usumbufu.
“Kuna wafanyabiashara ambao wana makontena ya bidhaa zenye nembo ya klabu yetu au wameagiza kutoka China na sehemu nyingine duniani, tunawaomba wavisalimishe klabuni ili kuepuka usumbufu wa kisheria,”alisema Mwesigwa.
Alisema wameshafuata taratibu za kisheria ikiwamo kwenda kusajili nembo ya klabu yao kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni za Biashara (Brela), zoezi ambalo limewagharimu zaidi ya shilingi milioni 10 ili iwe rahisi kwao kufanya wenyewe biashara ya vifaa vyenye nembo ya klabu hiyo.
Katibu huyo alisema kuwa mwanzoni kulikuwa na tatizo kwamba mahitaji ya vifaa hivyo vyenye nembo ya klabu yalikuwa makubwa kwa wanachama na wapenzi wa klabu hiyo na usambazi ulikuwa hakuna kwa klabu ndio maana wafanyabiashara wakajipa jukumu la kutengeneza na kusambaza bila makubaliano na wahusika, lakini klabu haikuwa na uwezo wa kudhibiti waagizaji wake.
Alieleza kuwa wameshafuata taratibu za kisheria na wanaye mshauri wa kisheria ambaye ni Kampuni ya AlexGlobes kwa ajili ya kuhakikisha analisimamia jambo hilo kwa umakini ingawa hakuwa tayari kueleza nani atasimamia zoezi la kukamata wafanyabiashara watakaokiuka ifikapo Novemba.
“Itakapofika Novemba tutajua nani atasimamia zoezi hilo bado kuna vitu tunakamilisha na huu ni wito kwa kila anayehusika hatutaki kuleta usumbufu kwa jamii kwa kuwa Yanga ni sehemu ya jamii pia,”alisema.
Aliongeza kuwa katika zoezi hilo la kuuza na kisambaza bidhaa zenye nembo yao, klabu hiyo inategemea kukusanya Shilingi 300 milioni hadi hadi 400 kwa mwaka.
Thursday, October 6, 2011
FUNDI WA FREE-KICK HAKAN YAKIN AASTAFU SOKA
Mshambuliaji mwenye kipaji cha hali juu raia wa Switzerland Hakan Yakin ametangaza kustaafu soka la kimataifa leo Alhamisi.
Yakin ambaye ana umri wa miaka 34, ameshiriki mara katika EURO na mara mbili katika Kombe la dunia, hivyo anaamini huu ni muda sahihi kuacha kucheza soka la kimataifa.
Hakan ameichezea Uswis mechi 87 na kufanikiwa kufunga magoli 20 kwa timu yake ya taifa kuanzia mwaka 2000-11.
BABA YAKE ROONEY MBARONI KWA KUCHEZA KAMARI
BABA MZAZI WA MSHAMBULIAJI WA MAN UNITED NA KIUNGO WA TIMU YA SOKA YA MOTHERWELL INAYOSHIRIKI LIGI KUU YA NCHINI SCOTLAND STEVE JENNINGS WAMETIWA MBARONI KUFUATIA TUHUMA ZA KUSHIRIKIANA NA WACHEZESHA KAMARI .
MR.WAYNE Snr. ANATAJWA KUSHIRIKIANA NA WATU WENGINE NANE KWA KUSHIRIKI KATIKA KITENDO HICHO.
KWA UPANDE WA JENNINGS AMEKAMATWA KUFUATIA UCHUNGUZI UNAOFANYWA KWENYE MCHEZO WA TIMU YAKE DHIDI YA HEARTS ULIOCHEZWA MWEZI DESEMBA AMBAPO TIMU YAKE ILIFUNGWA MABAO MAWILI KWA MOJA . KATIKA MCHEZO HUO JENNINGS ALIONYESHWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUWA AMEONYESHWA KADI MBILI ZA NJANO NA TUKIO HILO LA KUONYESHWA KADI NYEKUNDU NI MOJA YA MATUKIO AMBAYO YANATAZAMWA KWA MASHAKA NA KAMISHENI MAALUM YA KUZUIA KAMARI MICHEZONI NCHINI SCOTLAND .
SHAKIRA AKANUSHA KUACHANA NA PIQUE
Siku chache baada ya taarifa kuenea katika vyombo vya habari mbalimbali kuwa mapenzi kati ya Gerard Pique na mwanamuziki Shakira yamefikia tamati, leo mwanadada huyo kutoka nchini Colombia amekanusha kuachana na beki huyo wa kati wa klabu bingwa ya ulaya na timu ya taifa ya Spain.
The WakaWaka superstar alimtumia msemaji wake rasmi kutoa taarifa kuwa wawili hao bado wapo pamoja na taarifa kuwa wameachana ni uongo.
“Bado wapo pamoja na wanaendelea vizuri,” alisema msemaji huyo wa Shakira, bwana Rodrigo Beltran.
Mwanadada Shakira pia nae alitumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kumtakia heri mpenzi wake na timu ya taifa ya Spain katika mchezo wao kugombea nafasi kucheza michuano ya ulaya dhidi ya Czech Republic.
Aliandika “Good luck to the Spanish team this week and to my No. 3, muah! @3gerardpique.”
SIMBA DIMBANI NA PRISONS JUMAMOSI
Siku ya jumamosi ya wiki hii, vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayohangaika kusaka nafasi ya kurejea ligi kuu Tanzania Prisons ya Mbeya.
Mchezo huo wakirafiki utachezwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Prisons ilishuka daraja katika msimu wa 2009/2010, baada ya kupata mafanikio katika msimu wa 2007/2008 kwa kushika nafasi ya pili na hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Kagame na Kombe La Shirikisho, ambapo hawakufua dafu baada ya kutolewa katika hatua za awali.
Prisons inajianda na michezo ya ligi daraja la kwanza ambao inatarajiwa kuanza kutimua vumbi oktober 15, wakati Simba wanajianda na muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom.
KOCHA WA AZAM AOMBA KUIFUNDISHA MALAWI
Kocha wa Azam FC na timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', Stewart Hall ametuma maombi ya kwa shirikisho la mpira nchini Malawi ya kuifundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Kocha huyo toka Uingeleza aliyejiunga na Azam FC january mwaka huu, baada ya kufanya kazi nzuri na Zanzibar Heroes katika michuano ya Challenge mwaka jana mwishoni. Ametuma maombi nchini Malawi ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi.
Hall ambaye aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes, na Chama Cha Mpira wa miguu Zanzibar 'ZFA' katika michuano ya Challenge yatakayofanyika nchini mwezi wa kumi na mbili, amepata ridhaa ya viongozi wa Azam FC, katika suala zima la kutuma maombi ya kuifundisha timu ya taifa ya Malawi kama ilivyo kwa Zanzibar Heroes.
VICTOR COSTA AACHWA STARS-CANNAVARO ACHUKUA NAFASI YAKE
Beki wa kutumainiwa wa klabu ya Simba Victor Costa “Nyumba” ameachwa katika kikosi cha timu a Taifa baada ya kupata maumivu ya nyonga.
Kutokana na Costa kuumia kocha Jan Poulsen jana alimuita kikosini beki wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na Costa.
Taifa Stars imeondoka leo kuelea Morocco kwa ajili ya mechi ya mwisho ya kundi linalozihusisha timu za Algeria, Morocco, Afrika ya Kati na Tanzania katika kugombania nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la mataifa huru ya Afrika litakalofanyika mwakani nchini Gabon na Equatorial Guinea.
BOBAN, YONDANI, OKWI NA MWAKINGWE HATARINI KUFUNGIWA SIMBA
Taarifa ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa klabu ya Simba zinasema kuwa wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’, Kelvin Yondani, Emmanuel Okwi na Ulimboka Mwakingwe wapo katika hatari ya kufungiwa ama kusimamishwa na klabu hiyo kutokana utovu wa nidhamu.
Taarifa kutoka moja ya chanzo cha habari kilicho karibu na uongozi wa timu hiyo kinasema kuwa wachezaji hao wote wana makosa yanayofanana ya kutofika mazoezini huku wengine wakitoa sababu zisizo za kweli na wengine wakiwa kimya tu, wanatarajiwa kujadiliwa na uongozi wa timu pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo kabla ya maamuzi ya kuwapa adhabu kali kutolewa.
BREAKING NEWS: WHITECAPS YAMZUIA NIZAR KUJIUNGA NA STARS-KUKOSA MCHEZO WA MOROCCO
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Nizar Khalfan hatokuwemo katika kikosi cha Taifa Stars kitakachokwenda Morocco kwa ajili ya mechi ya mwisho na muhimu ya michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika litakalofanyika mwakani nchini Gabon na Equatorial Guinea.
Nizar amezuiliwa na klabu yake ya Vancouver Whitecaps kujiunga na Taifa Stars baada ya shirikisho la soka nchini TFF kuchelewa kupeleka barua kwa klabu hiyo kumuombea ruhusa kiungo huyo kuja nchini kujiunga na timu ya taifa.
Kwa mujibu kwa Vancouver Whitecaps ni kwamba barua ambayo ilitumwa na TFF ilichelewa kufika hivyo timu hiyo imegoma kumruhusu Nizar kuja Bongo.
Tanzania inakabiliwa na mtihani mgumu wa kuhakikisha inaifunga Morocco nyumbani kwa idadi ya mabao yasiyopungua 3-0 ili kujihakikishia walau nafasi moja ya kushiriki AFCON 2013.
Wednesday, October 5, 2011
VIDIC NA SABABU TANO KWANINI ANA UMUHIMU KATIKA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL
Nemanja Vidic ni mapigo ya moyo katika safu ya ulinzi ya Manchester United, na sasa United wakiwa wanaeleka kucheza mahasimu wao wa jadi Liverpool F.C ndani ya siku 14 zijazo, uwepo wake katika mechi hiyo utaleta utofauti mkubwa sana kati ya kushinda na kufngwa.
Vidic amekuwa nje ya uwanja kwa maumivu ya misuli ya nyuma ya mguu tangu katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya West Bromwich Albion ambapo aliweza kucheza kwa dk 45 za mchezo.
Ilifikiriwa kwa mara kwanza kwamba majeruhi ya Vidic ni madogo, lakini baada ya vipimo kufanyika vizuri ilionekana kuwa serious.
Vidic sasa amekuwa nje kwa takribani wiki 5-akikosa michezo dhidi ya Tottenham Hotspur, Arsenal, Bolton, Chelsea, Stoke City na Norwich.
Pamoja na kutokuwepo kwa Vidic, United wamefanikiwa kushinda mechi zao zote za EPL msimu huu kasoro mechi dhidi ya Stoke City.
Japokuwa, uwepo wa Vidic kwa mchezo wao wa ugenini dhidi ya Liverpool siku zote ni muhimu sana, na hata kocha wa United Sir Alex Ferguson amedhihirisha juu ya hili juzi, akisema Vidic inabidi afanye kazi kuhakikisha anakuwepo fiti kwa ajili ya kuwakabili majogoo wa jiji.
Hizi hapa ni sababu kwanini United wanamuhitaji Vidic kwa ajili ya mechi hiyo.
1: UONGOZI
Vidic alichaguliwa kuwa nahodha wa kudumu wa United katika msimu wa 2010-11.
Kitambaa cha unahodha hakijabadilisha chochote kwa Vidic, kwani siku zote amekuwa kiongozi shupavu uwanjani bila kitambaa hicho.Lakini kitambaa hicho kinaonyesha imani ya Ferguson kwake Vidic.
Kama Vidic atakuwa fiti kucheza dhidi ya Liverpool, anaweza kujikuta yupo kwenye bench kama sub kwa sababu kadhaa.
Kwanza manager anaweza kutotaka kumuhatarisha kutonesha au kupata majeraha mengine, ingawa kwa sababu ya ubora wa uongozi wake awapo dimbani, Fergie anaweza kumpa nafasi kuongoza safu ya ulinzi.Na kama itakuwa hivyo basi United watakuwa imara zaidi.
Vidic ni mchezaji influence kubwa dimbani, na wachezaji wenzie wanajua wanaweza kumtegemea-especially kwa mabeki ambao ni wadogo kiumri kama vile Chris Smalling, Phil Jones, Jonny Evans na mapacha Rafael na Fabio Da Silva.
2: UWEZO WA KUZUIA
Vidic anajulikana kwa uwezo na ubora wake kuzuia kwa staili yake kucheza soka la kutumia nguvu na akili.
Aina hii ya mentality ni nzuri na bora, tena zaidi ukiwa unaichezea United dhidi ya mahasimu wao Anfield.
Vidic alitajwa kama mchezaji bora wa mwaka wa Barclays Premier League na defenda bora wa msimu wa 2010-11.
3: MFUNGAJI WA MABAO
Hata kama kuna watu kama Wayne Rooney, Nani, na Danny Welbeck wamekuwa waking’ara kwa kufunga mabao msimu huu lakini katika mechi dhidi ya Liverpool wanaweza wakawa kwenye hali ngumu kutupia kambani.
Vidic ambaye amefunga mabao 18 katika mechi zote alizoichezea United.Hii ni idadi ambayo watu wanaweza kuibeza lakini kuna mabeki wengine wanamaliza muda wao wa kucheza bila hata kufunga bao.
Vidic ni hatari sana kwa set-pieces, Liverpool wanafahamu hili na watakuwa makini kumlinda ili asiwadhuru ndani 18.
4: MCHEZAJI WA MECHI KUBWA
Hii mechi ni moja ya mechi kubwa sana duniani.Hii ndio mechi ambayo kila kocha anategemea wachezaji kujituma na kucheza vizuri zaidi.Kama kuna mchezaji mwenye sifa hizi basi anaweza kuwa Vidic.
5: LIVERPOOL F.C
Hakunaga mechi ambayo haisisimui wanapokutana na Man United na Liver na Vidic akiwemo uwanjani.Ameshawahi kupewa red card katika mechi tatu dhidi ya majogoo wa jiji, na mara zote alizotolewa nje Liverpool walishinda.
Ingawa, katika mechi mbili kati ya 3 zilizopita dhdi ya Liver, Vidic alifanikiwa kucheza kwa dk zote 90, na kama hiyo haitoshi United walishinda mechi hizo.
MAGOLI YA HATARI KUWAHI KUFUNGWA KWENYE KOMBE LA DUNIA.
WORLD CUP NA MAGOLI MAKALI
10: Pele (Brazil) vs Sweden @Sweden 58
Goli la Gazza dhidi ya Scotland sio kali kihivyo.Imekuja kufahamika amelikopi kutoka Pele ambaye alifunga goli kama hilo katika fainali za kombe la dunia nchini Sweden mwaka 1958.
9:Diego Maradona (Argentina) vs Greece @USA 94
Maradona aliushangaza ulimwenguni alipoondolewa katika mashindano ya mwaka 1994 baada ya kufeli vipimo vya madawa.Lakini baada ya kuangalia uwezo wake dhidi ya Greece, unaweza kuelewa kwanini kikosi cha kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya walienda kumgongea hodi kwenye chumba cha hotel mara tu baada ya mchezo.
8: Manuel Negrete (Mexico) vs Bulgaria, @Mexico 86
Unakumbuka hili jina? Inawezekana hukumbuki.Ingawa ni mtu anayehusika na kufunga moja ya magoli mazuri katika historia ya kombe la dunia.Kiungo huyu wa Mexico alitumia muda wake wa mwingi kucheza soka nyumbani kwao akiichezea timu ya Pumas zaidi ya michezo 400.
7: Carlos Alberto (Brazil) vs Italy, Mexico 70
Goli la nne na la mwisho kwa Brazil katika fainali ya World Cup ya kukumbukwa.
6: Roberto Baggio (Italy) vs Czechoslovakia, @iTALY 90.
Timu zote zilikuwa zimeshafuzu kwa hatua ya mtoano ya michuano hiyo, lakini taifa mwenyeji walitaka kushinda na kuwa kileleni mwa kundi, walifanikiwa na shukrani kwa goli la Roberto Baggio.
5: Archie Gemmill (Scotland) vs Holland, @Argentina 78.
Miaka 33 iliyopita “Tartan Army” walikuwa na timu ambayo ilikuwa hatari.Graeme Souness, Kenny Dalglish, Joe Jordan, John Robertson na Archie Gemmill yalikuwa majina ya wakali wa timu hiyo, na matarajio ya World Cup yalikuwa juu.Lakini baada ya kufungwa na Peru na kutoa sare na Iran, The Scots walihitaji kuwafunga Holland kwa magoli 3 ili wafuzu.Ilionekana ni vigumu na haiwezekani mpaka wakati walipokuwa mbele kwa 2-1, wakafunga goli ambalo litaishi milele katika kumbukumbu za Tartan, asante kwa Archie Gemmill.
4: Saeed Al-Owairan (Saudi Arabia) vs Belgium @USA 94
Kombe la dunia halikuwa jombe la dunia bila mtu Fulani kufanya tukio kama la huyu jamaa, kufunga goli la uwezo binafsi kama hili.
3: Dario Rodriguez (Uruguay) vs Denmark, Japan/Korea 2002
Hii listi inaonyesha kwamba wachezaji kutoka Amerika ya kusini ndio uwezo zaidi ya kufanya ya hatari dimbani, na hili la Dane lilidhihirisha vipaji walivyo watu kutoka S.A, likiwa goli la michuano hiyo.
2: Diego Maradona (Argentina) vs England, Mexico 86
Baada ya bao “Mkono wa Mungu” kulikuwa nanjia moja tu ya kuwanyamazisha mashabiki wa England, na ndipo Diego Maradona alipofunga goli bora la michuano, dakika nne baadae.
1: Dennis Bergkamp (Holland) vs Argentina, France 98
Watu wengi waliomo kwenye hii listi wametokea South America, lakini “Ice Man” ndio kinara wao akiwa anatokea barani ulaya.Halikuwa tu goli bora kiufundi pia lilikuwa ni goli muhimu sana kutofautisha na mengine kwenye hii listi.
BECKHAM, SHEIKH MANSOUR, CAPELLO, NA WACHEZAJI WA MAN U WATAWALA LISTI YA WATU MATAJIRI NCHINI ENGLAND KWENYE MICHEZO
WANASOKA TAJIRI NCHINI ENGLAND 2011/12
1: David Beckham £135m
2: Micheal Owen £40m
3: Rio Ferdinand £36m
4: Ryan Giggs £30m
5: Wayne Rooney £30m
6: Steven Gerrard £27m
7: Frank Lampard £26m
8: John Terry £22m
9: Didier Drogba £19m
10: Fernando Torres £18m
LIST YA MAKOCHA TAJIRI UINGEREZA 2011/12
1: FABIO CAPELLO - £38M
2: SIR ALEX FERGUSON £27m
3: ARSENE WENGER £20m
4: ROBERTO MANCINI £19m
5: SVEN-GORAN ERIKSSON £15m
6: HARRY REDKNAPP £10m
7: STEVE BRUCE £9m
8: KENNY DALGLISH £8m
9: ANDRE VILLAS-BOAS £7m
10: ALEX McLEISH £6m
WAMILIKI WA VILABU TAJIRI ENGLAND
1: Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan £20bn (Manchester City)
2: Alisher Usmanov £12.4bn (Arsenal)
3: Lakshmi Mittal £11.8bn (QPR)
4: Roman Abromovich £10.3bn (Chelsea)
5: The Liebherr Family £3bn (Southampton)
6: Joe Lewis £2.8bn (Tottenham Hotspur)
7: Denis O’Brien £2.517bn (Celtic, Doncaster Rovers)
8: Stanley Kroenke £1.8bn (Arsenal)
9: Malcom Glazer & family £1.64bn (Manchester United)
10: Mike Ashley £1.37bn (Newcastle United)
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa jarida la michezo la fourfourTWO
MKOSI WA MECHI 50 KWA JURGEN KLOPP NA UBINGWA WA DORTMUND
Kama vile mambo hayajaharibika vya kutosha kwa muda huu, Jurgen Klopp atakutana na mbaya @ Coface – Arena jumamosi jioni: Stephan Mai.
Mai sio mchezaji wala kocha ila ni TV reporter anayefanya kazi katika channel ya kusini magharibi mwa Ujerumani.Kutokana na gazeti la Ujerumani la “WAZ”, Mai ameudhuria michezo 50 ambayo imemuhusisha Klopp aidha kama mchezaji au kocha (akiwa na Mainz na Dortmund) tangu mwaka 1993 na cha ajabu Klopp hajawahi kushinda hata mchezo mmoja kati ya 50 aliyoudhuria mwandishi huyo wa habari.
The 43-year old manager anafahamu sana juu ya mksi huu na Stephen Mai.Wakati timu yake ya Borussia iliporudishiwa goli la kusawazisha mwishoni mwa mchezo dhidi ya Kaiserslautern mwezi February, Klopp kwa hasira alikataa kufanya interview na Mai baada ya mechi hiyo, akimwita Stephen “Ndege mwenye ugonjwa mbaya wa kuambukiza”.
Mai hakutaka kujibizana nae, badala yake bila majivuno alihaidi kutokwenda tena katika mchezo wa ugenini wowote wa Borussia msimu ule.Lakini kwa bahati mbaya kwa kocha kocha huyo wa Dortmund, repota Mai anategemea kuhudhuria mchezo wa ugenini wa mabingwa watetezi wa Bundesliga @Mainz wikiendi hii, mchezo ambao Dortmund wanahitaji sana kushinda ili kuondoa fikra mbaya juu yao.
Point saba kutoka katika michezo 6 ya ufunguzi inaashiria mwanzo mbovu wa kwa mabingwa watetezi wa Bundesliga.Borussia wapo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.Wanaongoza ligi Bayern Munich wapo 8 mbele lakini hiyo sio mbaya sana, Dortmund sasa tayari wameshapoteza michezo mingi (mechi 3).”Presha sasa ipo juu” alisema Klopp baada ya kufungwa 2-1 na Hannover, mechi ambayo walianza kufunga na ku-dominate mchezo kabla ya kufungwa mabao mawili katika dk 4 za mwisho na kurudi nyumbani mikono mitupu.
Recently historia inaonyesha kwamba matokeo mabovu ya Black n Yellow Team hayaji kama surprise.Stuttgart (Mabingwa wa 2007) na Wolfsburg (mabingwa wa 2009), ambao wote walishinda ligi bila kutegemea, wote walihangaika sana msimu uliofuatia, wakati michezo ya champions league ilipowaongezea mzigo na changamoto mpya.So far mchezo bora kwa Dortmund, ukiondoa wa ushindi wao wa 3-1 dhidi ya timu ambayo haipo kwenye kiwango kabisa Hamburger SV katika siku ya ufunguzi, ulikuwa mchezo dhidi ya Arsenal waliopata matokeo ya 1-1.Dortmund wamecheza vizuri mara chache san asana, lakini ni sawa kusema kwamaba vijana wa Klopp wame-struggle to kufikia levo yao yenye ubora iliyowafanya wachukue ubingwa msimu wa 2010/2011.
NINI TATIZO?
Klopp anasema kuwa tatizo ni saikolojia. “Tunakosa consistency na tama ya mafanikio,” alisema baada ya mchezo dhidi ya Hannover.Beki wa kushoto Marcel Schmelzer anakubaliana na hili, “Inaonekana kama hutukuupigania vizuri mpaka mwisho.Kila mtu alikuwa ana matumaini hakuna kitakachotokea.Wote tunahitaji kugundua kwamba tunatakiwa kuweka 100% kwa dakika 95.” Hii inaonyesha kwa timu nzima ilikuwa kama wamechoka, lakini data rasmi zinaonyesha Dortmund hawana tofauti sana na msimu uliopita.Labda shida kubwa ni kuweka ukali ule ule ukicheza mchezo mgumu unaohitaji nguvu kwa kipindi kirefu cha muda. “Staili yetu ni ‘very demanding’,” anakiri beki wa kati Mats Hummels. “Lakini hali hiyo unaiona wakati mambo yanapokuendea kombo.Unapofanikiwa, huioni hali hiyo kwa sana.”
Kukosekana kwa umakini ni jambo lingine, kama ushahisi unavyoonesha namba ya magoli ya magoli waliyofungwa kutokana na mipira iliyokufa.Mara tatu Dortmund wamefungwa kwa aina ya mipira hii. “Hii haikubaliki” alisema Klopp. “Tunatakiwa kuwaweka watu warefu ambao wataweza kuondoa mipira ya adhabu pembeni mwa goli letu.” Suala pia ilnaweza kufananishwa kuhusu uwezo wa wao kufunga magoli msimu pia.
Takwimu za wastani wa kumiliki mpira kwa Dortmund ni asilimia 56, ni Bayern pekee ambao wameweza kumiliki vizuri kiasi hicho.Timu imetengeneza nafasi za wazi 34 za kufunga mabao, takwimu inayoonyesha ni timu 5 pekee kwenye ligi waliyoizidi rekodi hii, lakini kiwango chao cha ufunguji ni kidogo mno, aslimia 20, wastani mbaya kuliko wote katika timu 18 za top flight. “Tunakosa kujiamini”, alisema tena Hummels.Inawezekana mchezo wa kutumia nguvu na kasi unachosa akili za wachezaji lakini hawakuwa na tatizo hili msimu uliopita.Tofauti kubwa pekee inawezekana kutokuwepo kwa mshambuliaji wa ki-paraguay Lucas Barrios, ambaye alifunga mabao 16 na akatoa assists 6 msimu uliopita, Dortmund wanamtegemea Polish forward Robert Lewandowski. The 23 year-old Lewandowski ni mchezaji mzuri sana lakini anaonekana kutokuwa sawa kuongoza mashambulizi mwenyewe kama ilivyokuwa kwa Barrios.Hafichi mipira na matokeo yake, Dortmund inabidi wahangaike sana kuingia ndani ya box.
Watu wengine wenye uzoefu nchini Ujerumani wanasema tatizo ni mabadiliko katika kiungo cha kati. Nahodha wa Dortmund Nuri Sahin amehamia Real Madrid kipindi cha kiangazi na mbadala wake Ilkay Gundogan, bado anahitaji uzoefu wa kuichezea timu kubwa.Anajua na ni mchezaji mzuri lakini hana ‘strategic vision’ kama ya Nuri Sahin.Dortmund wamepoteza ya silaha zake katikati mwa kiwanja.
Kama utaangalia mchezaji muhimu Mari Gotze amesimamishwa na si Shiji Kagawa wala Kevin Großkreutz ambaye ameweza kurejesha fomu waliyokuwa nayo msimu uliopita, hivyo haishangazi kuona kuna ukame wa magoli.
Habari nzuri ni kwamba Barrios amerudi kwenye mazoezi baada ya kuwa nje kwa maumivu ya misuli lakini si rahisi kumuona tena uwanjani mpaka baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kuisha.Mshambuliaji wa Egypt Mohamed Zidan hayupo hata katika kikosi cha kwanza.
Ni muda pekee pekee ndio utakaotoa majibu kwamba Dortmund wanaweza ku-regroup na kuzichaji upya betri zao katika kipindi hiki muhimu.Kama watashindwa, tegemea kuona sera ya uhamisho ya klabu kubadilika sana.