Umeshawahi kumshuhudia mchezaji mpya wa Yanga kutoka Uganda Hamis Kiiza akiwajibika uwanjani?
Anacheza kwa kasi, yupo kila sehemu huku akikaba kwa nguvu na kusaidia kupeleka mashambulizi mbele.
Je unaijua siri ya uchezaji wa namna ile wa Hamis Kiiza?Blog yako bora ya michezo inakuletea exclusive story ya Ugandan Golden Boy.
“Kiukweli naichezea Yanga kutokana na mapenzi makubwa niliyonayo kwa klabu hii, lakni sababu kubwa iliyonifanya nijiunge na Yanga mara tu walipoonyesha nia ya kunitaka ni kwamba marehemu baba yangu Mzee Kiiza wakati wa uhai wake alikuwa ni shabiki mkubwa wa Yanga, na kipindi nakuwa alikuwa akinunulia jezi za Yanga huku akinisisitiza nikifanikiwa kucheza soka la ushindani ukubwani nije niicheze klabu hii ya Jangwani, hivyo kujiunga kwangu na Yanga ni kufanikiwa kutimiza ndoto ya marehemu baba.
“Mzee Kiiza alikuwa ni mtanzania kabisa, lakini mwaka 1974 ilipotokea vita ya Uganda na Tz, alijiunga na jeshi la Tanzania kupigana na Iddi Amini, waliposhinda na kuingia Uganda, Baba alibaki Kampala na huko ndipo alipokutana na mama yangu,” alisema Hamis Kiiza ambaye kwa sasa yupo Uganda akiangalia familia yake baada ya mkewe kujifungua wiki iliyopita.