JERRY SANTO ANAFUNGA GOLI LA KUONGOZA
Search This Blog
Saturday, October 22, 2011
LIVE MATCH CENTRE: FULL TIME - SIMBA 2-0 JKT RUVU
JERRY SANTO ANAFUNGA GOLI LA KUONGOZA
YANGA WAOMBA ARDHI KWA SERIKALI - KUJENGA UWANJA MPYA WA KISASA
Uongozi wa mabingwa soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, umeiandikia barua Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuomba kiwanja ambacho wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Celestine Mwesiga, alisema, wameiandikia barua wizara hiyo, kutaka kupewa kiwanja cha hekari 20 katika Manispaa ya Kinondoni au Ilala, ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutaka kumiliki kiwanja hicho cha kisasa kama ilivyo kwa klabu mbalimbali duniani.
“Tumeishafanya mawasiliano na wenzetu wa Wizara ya Ardhi kuomba kupatiwa kiwanja hicho na wameonyesha wapo tayari kutufanikishia lengo letu, hivyo tunasubiri wakati wowote watujulishe wapi wametupata,” alisema Mwesiga.
Alisema uongozi wake umejipanga kuhakikisha unajenga uwanja huo, ili Yanga iweze kupunguza gharama mbalimbali zinazolipwa kupitia viwanja wanavyochezea sasa, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.
Akifafanua kuhusu uwanja huo, Mwesiga alisema utakuwa na bwawa la kuogelea, uwanja wa tenisi, mpira wa mikono, sambamba na hosteli kwa ajili ya wachezaji wa klabu hiyo.
Hivi karibuni, watani zao Simba walitangaza mikakati mbalimbali kujenga vitega uchumi ikiwamo kujenga jengo la ghorofa 12 yalipo makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi sambamba na uwanja wa kisasa ‘Simba Sports Arena, huko Bunju nje kidogo ya jiji.
YANGA: HATUNA MPANGO NA PAPIC
Mabingwa wa Tanzania bara na Afrika mashariki na kati klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imezima uvumi kwamba imemtema kocha wake raia wa Uganda, Sam Timbe, kwa kile kilichodaiwa kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu nchini, na badala yake imemrejesha kocha wake wa zamani Costadin Papic.
Uvumi huo uliongezwa nguvu zaidi hasa baada ya Timbe kutokuwepo kwenye benchi la la Yanga katika mechi ya ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Toto African iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Kufuatia ujio wa Papic, uvumi ulienea kwamba kocha huyo amerudi kuchukua nafasi ya Timbe.
Lakini Katibu mkuu wa Yanga, Selestin Mwesigwa alisema klabu yake haijawahi kuwa na mpango kama huo, na kwamba wanamtambua Timbe kama kocha wao mkuu mpaka sasa.
Mwesigwa alisema, si kweli kwamba kutokuwepo kwa Timbe kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Toto, kulikuwa na maana ya kwamba ametimuliwa.
"Hakuna kweli wa taarifa hizi, Timbe bado ni kocha wetu isipokuwa tu alishindwa kutokea katika mechi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya," alisema Mwasigwa.
Kuhusiana na ujio wa Papic aliyetua nchini Jumatano iliyopita Mwesigwa alisema kuwa kocha huyo amekuja nchini kwa shughuli zake binafsi.
Alisema kuonekana uwanjani Papic katika mechi yao dhidi ya Toto ni moja ya mapenzi yake kwa Yanga kwa sababu alishawai kuifundisha kwa mafanikio makubwa.
PHOTOS: KIKAO CHA VILABU 14 KILICHOAMUA LIGI KUU KUENDESHWA NA KAMPUNI.
Baada ya kikao cha karibia masaa 4 au zaidi viongozi wa vilabu 14 vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara walifikia maamuzi ya kuanzishwa kwa kampuni itayoendesha ligi kuanzia msimu ujao.
Kikao hicho kilichofanyika katika hoteli ya JB Del-monte (zamani Paradise) @ Benjamin Mkapa Tower kilihudhuriwa na viongozi 13 kati ya 14 wa vilabu vya ligi kuu isipokuwa Kagera Sugar waliotoa udhuru lakini wakisema wataunga mkono maamuzi yatakayotolewa
Katika kikao hicho maamuzi yaliyotolewa ni kwamba uanzishwe mchakato wa kuwezesha usajili wa kampuni ambayo itaendesha ligi hiyo, huku Makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Celestine Mwesiga katibu mkuu Yanga-Makamu mwenyekiti, Meja Ruta wa Ruvu Shooting- akiteuliwa Katibu wa hiyo kamati, na Shani wa Azam FC na Evadius Mtawala wa Simba wakiwa wajumbe, ambao wote kwa pamoja watashugulikia mchakato wa kupatikana kwa usajili wa kampuni hiyo.
“Dauda nilialikwa na viongozi wa vilabu kutoa mawazo yangu juu mchakato mzima wa kuundwa kwa kampuni itayoendesha ligi kuu.”
Friday, October 21, 2011
BREAKING NEWS: HATIMAYE LIGI KUU YA TZ BARA KUENDESHWA NA KAMPUNI.
Taarifa za kuaminika za hivi sasa zinasema kuwa mkutano wa vilabu vyote vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara vimeamua kwa pamoja kuanzia msimu ujao ligi kuu ya Tz bara itaendeshwa na kampuni itakayoundwa na muunganiko wa vilabu vishiriki katika premier league, hivyo kuanzia msimu ujao T.F.F wataicha ligi hiyo kuendeshwa na kampuni.
Kwa maelezo zaidi endelea kutembelea blog yako namba ya michezo na burudani.
NICO NYAGAWA MENEJA MPYA WA SIMBA SC
Uongozi wa klabu ya Simba umemteua, nahodha wake wa zamani, Nico Nyagawa, kuwa meneja mpya wa timu hiyo inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Nyagawa ambaye aliachwa katika usajili wa msimu huu, aliahidiwa kupewa ajira nyingine kutokana na mkataba wake kuendelea kuwepo na alikaa kimya tofauti na wachezaji wenzake ambao walipewa taarifa za kutemwa katika kipindi ambacho hawakuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine.
Kiungo huyo ambaye alisajiliwa Simba mwaka 2005 akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro, alianza kazi yake hiyo mpya jana asubuhi na alipewa mikoba hiyo baada ya aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo, Abdallah Kibaden 'King' kuwa safarini kwenye ibada ya Hijja mjini Makka.
Akizungumza na blog hii jana mchana, Nyagawa alithibitisha kurejea kundini na kuahidi kutumia uzoefu aliokuwa nao kuisaidia Simba ili ifikie malengo yake.
"Ni kweli nimeitwa na nitaanza kazi rasmi leo (jana) jioni," alisema Nyagawa ambaye msimu huohuo wa mwaka 2005/2006, Simba ikitumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, aliifungia mabao mawili katika mchezo uliomalizika kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga.
Wekundu wa Msimbazi hawakuwa na meneja wa kudumu tangu Innocent Njovu alipoondolewa baada ya mabadiliko yaliyofanywa na uongozi wa sasa wa Simba kufuatia kuondoka kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri.
Nyagawa anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kwa mara ya kwanza kesho wakati watakapoivaa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba wanaongoza kwenye msimamo wa ligi ya Bara baada ya kushuka dimbani mara 10 na kufikisha pointi 24 huku wakifuatiwa na ‘maafande’ JKT Oljoro waliocheza mechi za idadi sawa na Simba na kufikisha pointi 19.
CHANZO CHA UHASAMA NA UADUI MKUBWA KATI YA JIJILA MARSEILLE DHIDI YA ARSENE WENGER
JAPO ARSENE WENGER AMEKUWA AKICHUKIWA NA MASHABIKI WA TIMU PINZANI ZA ENGLISH PREMIER LEAGUE KUTOKANA NA KIBURI CHAKE NA KWA BAADHI YA MASHABIKI WA KLABU YAKE YA ARSENAL KUTOKANA NA UWEZO MDOGO WA KUSOMA ALAMA MUHIMU ZA NYAKATI , CHUKI HIZI SI CHOCHOTE UKIFANANISHA NA CHUKI ILIYOKO DHIDI YA WENGER KWENYE JIJI LA MARSEILE .SABABU KUU YA CHUKI HII NI KWAMBA WENGER ALIKUWA MOJA YA SABABU KUU ZILIZOUMALIZA UFALME WA MARSEILE KWENYE SOKA LA UFARANSA MIAKA 20 ILIYOPITA .
MAPEMA MWANZONI MWA MIAKA YA 90 , MARSEILE WALIKUWA TIMU KUBWA BARANI ULAYA , KAMA ILIVYO BARCELONA AU MANCHESTER UNITED KWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI.TIMU HII ILIKUWA IMETWAA UBINGWA WA LIGI YA UFARANSA MARA TANO MFULULIZO NA MSIMU WA MWAKA 1992-93 WALITWAA UBINGWA WA ULAYA WAKIIFUNGA AC MILAN BAO MOJA BILA.
UTAMU WA USHINDI HUU WA KIHISTORIA HATA HIVYO ULIGEUKA NA KUWA SHUBIRI CHUNGU KWA MASHABIKI WA MARSEILE NA WAFARANSA WOTE BAADA YA KUGUBIKWA NA KASHFA YA RUSHWA AMBAYO ILILILAZIMU SHIRIKISHO LA VYAMA VYA SOKA BARANI ULAYA UEFA KUWAVUA MARSEILE UBINGWA .
KASHFA HII ILIIBUKA BAADA YA BEKI WA KLABU YA VALENCIENNE JACQUES GLASSMAN KUFICHUA SIRI JUU YA JINSI MARSEILE KUPITIA KWA RAIS WAKE BERNARD TAPIE WALIVYOKUWA WAKIPANGA MATOKEO KWA KUWAHONGA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TIMU NDOGO .
UPANDE WA PILI ARSENE WENGER ALIKUWA AKIIJENGA KLABU MOJA YA MONACO HUKU AKIWA NA WACHEZAJI HATARI KAMA KINA GEORGE WEAH NA GLENN HODDLE , MONACO ILITWAA UBINGWA WA UAFARANSA MWAKA 88 NA WAKATI MARSEILE WAKIWA MABINGWA MONACO NDIO WALIKUWA WAPINZANI WAKE WAKUBWA . ARSENE WENGER ALIAMINI KUWA MONACO NDIO WALIOSTAHILI MAFANIKIO WALIYOKUWA WAKIYAPATA MARSEILE LAKINI HAIKUWA HIVYO KWA KUWA TIMU YAKE HAIKUWA NA MSULI WA KIFEDHA HIVYO WALIKUWA WAKICHEZA MECHI UWANJANI PEKE YAKE TOFAUTI NA WENZAO WALIOKUWA WAKICHEZA NDANI NA NJE YA UWANJA .
MAWAZO YA WENGER YALIUNGWA MKONO NA ALIYEKUWA KOCHA WA KLABU YA VALENCIENNE BORO PRIMORAC AMBAKO MCHEZAJI WAKE ALIFICHUA JANJA YA MARSEILE . KWA SASA PRIMORAC NI KOCHA MSAIDIZI WA ARSENAL CHINI YA WENGER . PRIMORAC ALIFICHUA SIRI KUWA RAIS WA MARSEILE ALIMFUATA NA KUMPA HONGO ILI APINDISHE USHAHIDI NA KUMLINDA LAKINBI HAKUFANYA HIVYO NA MATOKEO YAKE YALIKUWA KUVULIWA KWA TAJI LA MARSEILE .
KWA MASHABIKI WA MONACO WENGER ALIKUWA SHUJAA KAMA ALIVYOKUWA BEKI WA VALENCIENNE GLASSMAN NA KOCHA WAKE PRIMORAC MBELE MASHABIKI WAO , LAKINI UKITOKA NJE YA VILABU VYAO WATU HAWA WATATU WALICHUKIWA NA UFARANSA NZIMA KWA KULIAIBISHA SOKA LA NCHI YAO NA KWA MASHABIKI WA MARSEILE WATU HAWA WALIONEKANA ZAIDI YA WASALITI . UAMUZI WA GLASSMAN WA KUZUNGUMZA WAZI JUU YA MAOVU YA MARSEILE ULIMFANYA APEWE TUZO YA FAIR PLAY YA FIFA MWAKA 1995 WAKATI HUO HUO AMBAO ARSENE WENGER ALIFUKUZWA KAZI NA MONACO KWA MASHANGAO WA WENGI NA ALITIMKIA HUKO JAPAN KUFUNDISHA KLABU YA GRAMPUS 8.
HADITHI YA MARSEILE ILIISHIA HAPO KWANI WALIVULIWA TAJI LA ULAYA NA TAJI LA UBINGWA WA UFARANSA PIA NA HAIKUISHIA HAPO KWANI WALISHUSHWA DARAJA HUKU RAIS BERNARD TAPIE AKIFUNGWA GEREZANI . TANGU MIAKA HIYO HAWAKUREJEA KUWA TIMU KUBWA KAMA ILIVYOKUWA ENZI HIZO NA NI UJIO WA NAHODHA WA ZAMANI DIDIER DESCHAMPS NDIO ULIOREJESHA HADI YA MARSEILE KAMA TIMU YA KUOGOPWA UAFARANSA KWANI CHINI YAKE WALITWAA UBINGWA WA MWAKA 2009/ 2010 .
WAZIRI: ZANZIBAR HAIWEZI KUWA MWANACHAMA WA FIFA
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameambiwa kwamba Zanzibar imepoteza hadhi ya utaifa wake Aprili 26, mwaka 1964 ilipojiunga na Tanganyika na kuzaliwa kwa taifa jipya la Tanzania na hivyo haina sifa ya dola na haiwezi kuwa mwanachama wa FIFA.
Waziri wa Habari, Utangazaji, Michezo na Utalii, Abdillahi Jihadi Hassan alisema hayo katika Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali aliloulizwa na mwakilishi wa jimbo la RAHALEO Nassor Salim Ali aliyetaka kujua hatma ya Zanzibar katika kujiunga na shirikisho la soka la kimataifa FIFA.
“Suala la Zanzibar kupata uanachama wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa sasa limegonga mwamba....naomba wajumbe mfahamu hivyo kwa sababu Zanzibar imepoteza hadhi ya utaifa wake katika mwaka 1964 April 26 ilipojiunga na Tanganyika na kuzaliwa kwa taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Jihadi.
Alisema njia pekee ya kujaribu tena kujiunga na FIFA ni kutumia mchakato unaokuja wa marekebisho ya katiba kulielezea suala hilo kwa umakini zaidi.
Jihadi alisema suala la uanachama wa Fifa linaonekana zaidi kuwa na sura ya kisiasa kuliko michezo.
Alisema juhudi mbali mbali zilifanyika ikiwemo vyama vya soka nchini pamoja na Baraza la michezo la Taifa kutoa baraka zake kwa Zanzibar kupata uanachama wa FIFA lakini ilishindikana.
Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi zaidi baada ya kikao kilichopita cha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011-2012 kuwaambia wajumbe kwamba yapo matumaini makubwa ya Zanzibar kupata uanachama wa FIFA huku akijitayarisha kufanya safari kuonana na rais wa FIFA Sept Blatter.
BASENA: T.F.F BADILISHENI MFUMO WA RATIBA YA LIGI -INACHOSHA
Kocha wa wekundu wa msimbazi Simba, Mganda Moses Basena amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), kuangalia upya upangaji wa ratiba za mechi za Ligi Kuu kwa madai kuwa inawachosha na kuwaumiza wachezaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Basena alisema, TFF inapaswa kupanga ratiba itakayotoa nafasi kwa timu kucheza mechi moja kisha ikapata muda wa kupumzika kabla ya kucheza mechi nyingine.
Alisema kama hilo litazingatiwa, kutasaidia timu kuepuka tatizo la majeruhi mfululizo kama ambavyo imetokea kwenye kikosi chake siku za karibuni.
"Sioni sababu ya kucheza mechi mfululizo tena za ligi tu, mimi nafikiri shirikisho linapaswa kuliangalia hili kwa umakini vinginevyo tutakuwa tunawaumiza wachezaji kila kukicha.
"Ebu angalia, mfano tumecheza mechi ngumu leo, na baada ya siku tatu tunacheza mechi nyingine. Hii ni sahihi kweli," alihoji Basena.
Basena kocha msaidizi wa zamani timu ya taifa Uganda, The Cranes, alisema ni makosa kulinganisha mazingira ya ligi ya Tanzania na zile za Ulaya.
"Ligi za Ulaya ni za kulipwa, pia klabu zinashiriki mashindano tofauti na si ligi pekee.
"Mazingira yao ni tofauti na sisi, hivyo ni makosa kulinganisha ligi za kule na huku,"alisema Basena.
Akizungumzia suala hilo, Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema: "Hilo ni suala la kiufundi zaidi na wahusika ni Idara ya Ufundi ambao wana mamlaka ya kupanga ratiba."
Mkurugenzi wa ufundi wa T.F.F Sunday Kayuni was nowhere to be found kuelezea kuhusu shutuma za Basena.
DANNY MRWANDA: T.F.F IACHE UBABAISHAJI
Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars, na klabu ya DT Long An, Vietnam, Danny Mrwanda, amelitaka Shirikisho la soka Nchini (TFF) kuwa makini linapofanya mawasiliano ya kuwaita wachezaji wanaocheza soka nje kuja kujiunga na Stars.
Lakini kauli yake ilipingwa na TFF kupitia msemaji wake, Boniface Wambura alipokuwa akiongeaa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Mrwanda alishutumiwa na TFF kwa kitendo cha kuchelewa kuripoti kambi ya Stars ilipokuwa ikijiandaa kucheza na Morocco mechi ya mwisho kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.
Akiongea juzi, Mrwanda alisema wakati TFF ikituma taarifa kwenye klabu yake kumtaka kuja nchini, yeye wakati huo tayari alikuwa nchini kwa shughuli zake binafsi.
"Nilipewa taarifa na uongozi wa klabu (DT Long An, Vietnam) nikiwa nchini kwamba natakiwa nijiunge na wenzangu kwenye timu ya Taifa," alisema Mrwanda.
Mrwanda anasema alishangazwa na TFF kutompa taarifa za kuitwa kwake Stars, kwani mbali na kutoa taarifa kwa mwajiri wake pia, TFF ilikuwa na kujumu la kumfahamisha na yeye.
Mrwanda alisema kinachotakiwa kufanywa na TFF ni kuhakikisha mchezaji anapata taarifa mara tu wanapowasiliana mwajiri wake, na si tu kusubiri klabu ndio impe taarifa.
Aidha Mrwanda aliilalamikia TFF kwa kushindwa kumsaidia kupata visa kama ambavyo aliahidiwa na Mkurugenzi wa mashindano ambaye hakumtaja jina.
"Tangu turudi toka Morocco sijaondoka kwa vile visa yangu imeisha. Waliahidi wangenisaidi lakini mpaka sasa kimya," alisema Mrwanda.Kwa upande wake, Wake Wambura alisema walipeleka taarifa mapema kwenye klabu yake wakiwa na imani kwamba, pia taarifa hizo zitamfikia Mrwanda.
"Taarifa zilikwenda, na kweli huenda hakuwepo Vietnam wakati huo, lakini uongozi wa klabu yake haukutupa taarifa," alisema Wambura.
Akiongea kuhusu suala la visa, Wambura alisema suala hilo si jukumu lao kama TFF.
"Hatuhusiki kwenye hilo, ni jukumu la mchezaji mwenyewe kutafuta visa, labda kama anataka kusaidiwa nyaraka na si vinginevyo."
<!--[if !supportLineBreakNewLine]-->
<!--[endif]-->
TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 131 KWA UBORA WA SOKA DUNIANI
TANZANIA imezidi kuporomoka katika viwango vya kila mwezi vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Katika orodha ya Oktoba iliyotolewa jana na shirikisho hilo, Tanzania imeshuka kwa nafasi nne kutoka ya 127 hadi 131 duniani. Kwa upande wa Afrika imeshuka kutoka nafasi ya 32 hadi 34.
Kuporomoka huko kunatokana na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kuchapwa mabao 3-1 na Morocco katika mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika mwezi uliopita ambapo kwa mara nyingine Tanzania imeshindwa kufuzu.
Hali hiyo inazidi kukatisha tamaa pamoja na nguvu nyingi ambazo serikali na wafadhili wameelekeza kwenye soka kwa sasa.
Katika nchi za Afrika Mashariki Uganda wanashika nafasi ya 88 duniani na 22 Afrika, wakati Kenya wapo nafasi ya 135 duniani na 36 Afrika.
Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast bado wameendelea kutamba kileleni pamoja na kushuka kwa nafasi tatu katika viwango vipya vya Fifa.
Rwanda wamekuwa nchi ya Afrika ambayo imepanda kwa nafasi nyingi Oktoba. Nchi hiyo imepanda kwa nafasi 31 na kushika nafasi ya 29 Afrika na 112 duniani.
Nafasi tatu za juu Afrika hakuna mabadiliko baada ya Misri na Ghana kuendelea kubaki kwenye nafasi ya pili na tatu.
Vijana wa Pharao wameendelea kubaki nafasi ya pili kutokana na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Niger kwenye mechi za kufuzu Mataifa ya Afrika mwezi uliopita.
Benin wamekuwa timu iliyoshuka kwa nafasi nyingi 27 na kushika nafasi ya 199 baada ya kipigo cha bao 1-0 nyumbani kutoka kwa Rwanda mwezi uliopita.
Nchi zinazoshika nafasi 10 bora Afrika na nafasi zao duniani kwenye mabano ni Ivory Coast (19), Misri (29), Ghana (33), Algeria (35), Senegal (42), Nigeria (44), Cameroon (47), Afrika Kusini (49), Burkina Faso (54) na Morocco (56).
Mabingwa wa Dunia Hispania wameendelea kupanda kwa kuongoza katika orodha ya viwango duniani.
Mbali na Hispania nchi zilizo kwenye 10 bora duniani nyingine ni Uholanzi (2), Ujerumani (3), Uruguay (4), Brazil (5), Italia (6), England (7), Ugiriki na Ureno (8), Argentina na Denmark (10).
Thursday, October 20, 2011
MAONI YA MPANGO WA MAENDELEO TFF
Kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia Novemba 7 hadi 20 mwaka huu. Makocha 30 wameteuliwa na TFF kwa ajili ya kushiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne, mmoja wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wawili wa CAF na mmoja wa Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU). Mkufunzi wa FIFA atakuwa Jan Poulsen, kutoka CAF ni Sunday Kayuni (Tanzania), Kasimawo Laloko (Nigeria) wakati kutoka Denmark ni Kim Poulsen. Makocha walioteuliwa kushiriki kozi hiyo ni Christopher Eliakim, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Mussa Furutuni, Mecky Maxime, Gideon Kolongo, Maka Mwalwisi, Haji Amir, Tiba Mlesa, Stephen Matata, Wane Mkisi, Edward Hiza, Leonard Jima na Ahmed Mumba. Wengine ni Peter Mhina, Absolom Mwakyonde, Maarufu Yassin, Mussa Kamtande, Wilfred Kidau, Eliasa Thabit, Dismas Haonga, Fulgence Novatus, Juma Mgunda, Hassan Banyai, Mohamed Tajdin, Sebastian Nkoma, Emmanuel Massawe, Gabriel Gunda, Abdul Nyumba na Richard Kabudi. Pia kutakuwa na kozi nyingine ya juu ya leseni za daraja B ambayo inatarajia kufanyika baadaye Desemba mwaka huu.
NAULI LIGI KUU YA VODACOMM
dhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom tayari imeshatoa hundi ya nauli kwa ajili ya klabu ambazo timu zake zinashiriki ligi hiyo. Mgawo uliotolewa ni kwa ajili ya mwezi Septemba na Oktoba. Tayari klabu husika zimeanza kuchukua hundi zao kutoka TFF. Kwa mwezi Septemba kila klabu imepata sh. 4,732,142 wakati Oktoba ni sh. 5,622,321. Hivyo kwa miezi hiyo miwili kila klabu imepata sh. 10,354,463.
SIMBA, SHOOTING ZAINGIZA MIL 14.7
Mechi namba 66 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Oktoba 19 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 14,755,000. Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,794 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa mzunguko na sh. 10,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za VIP walikuwa 157. Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,180,763 kila timu ilipata sh. 3,172,271.19. Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,057,423.70), TFF (sh. 1,057,423.70), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 528,711.86), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 422,969.49) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 105,742.37).
MAONI YA MPANGO WA MAENDELEO TFF
iko katika mchakato wa kutengeneza mpango wa maendeleo wa muda mrefu. Ni nia ya TFF kufanyia kazi maoni ya wadau ili kuhakikisha yanaingia katika mpango huo. Hivyo wadau wanakaribishwa kutuma maoni yao kupitia email- tfftz@yahoo.com au sanduku la barua 1574 Dar es Salaam. Maoni yawe yametumwa kufikia mwishoni mwa Novemba mwaka huu. Pia TFF kupitia Kurugenzi ya Ufundi itakutana na makundi mbalimbali kusikiliza maoni yao. Novemba 2 mwaka huu imepanga kukutana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na pia waandishi wa habari.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
NIGERIA NA CAMEROON ZAJITOA CECAFA CHALLENGE CUP 2011
Timu za soka za mataifa ya Cameroon na Nigeria yametangaza kujitoa katika kinyang'anyiro cha michuano ya Baraza la Vyama vya Soka la Nchi za Afrika Mashariki na Kati(CECAFA)iliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 10.
Jumla nchi 11 wanachama wa baraza hilo zinatarajia kushiriki katika patashika hiyo ikiwemo Sudan, Ethiopia, Uganda, Kenya, Eritrea, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Djibouti, Somalia na wenyeji Tanzania.
Kabla ya kutangaza kujitoa, Cameroon na Nigeria zilikuwa miongoni mwa nchi tano kutoka nje ya ukanda huo zilizowasilisha maombi zikitaka kushiriki michuano hiyo ambayo itafanyika kwa mara ya pili mfululizo katika ardhi ya Tanzania.
Nchi nyingine zilizowasilisha maombi hayo ni pamoja na Malawi, Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia na Ivory Coast ambayo pia ilishiriki kama nchi mwalikwa katika michuano iliyopita iliyofanyika pia nchini.
Akizungumza kwa simu kutoka Naironi jana, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye alisema kuwa ofisi yake imepokea taarifa za kujitoa kwa nchi hizo pasipo maelezo mengine ya ziada kuhusu sababu za kujitoa kwao.
"Kwa ujumla sisi tunaendelea na maandalizi kama kawaida labda tu jambo jipya ni kwamba Cameroon na Nigeria ambazo awali ziliomba kushiriki zimetoa taarifa ya kujiondoa,"alisema Musonye.
Hata hivyo Musonye alisema kuwa ni nchi mbili tu kati ya tatu zilizosalia ndizo zinazoweza kupewa nafasi ya kushiriki michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Kilimanjaro Stars.
"Kimsingi tuna nafasi mbili tu kwa nchi waalikwa na hii ni kutokana na suala zima la bajeti iliyopo hii ina maananisha si nchi zote zilizoomba zitakubaliwa,"alisema Musonye.
Alisema kuwa viongozi wa baraza lake wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam wiki ijayo na kuchagua timu zitakazoalikwa kushiriki michuano hiyo.
Kwa upande mwingine kujitoa kwa Cameroon na Nigeria kunaweza kukawa na uhusiano na matokeo mabaya iliyokutana nayo nchi hizo ambapo hazikufanikiwa kufuzu kushiriki katika fainali zijazo za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon.
Wednesday, October 19, 2011
NGORONGORO HEROES YAPANGWA NA SOUTH AFRICA COSAFA CUP
Timu ya taifa chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes ipangwa kundi C pamoja na South Africa katika michuano ya vijana ya COSAFA itakayofanyika nchini Botswana.
Ngorongoro heroes itashiriki kama timu mualikwa katika mashindano hayo yanayohusisha timu za Taifa za vijana chini ya miaka 20 kwa mataifa ya kusini mwaafrica.
Ngorongoro wamepangwa kundi C pamoja na South Africa, Zambia, na Mauritius, wakati kundi A lina timu za Botswana, Comores, Swaziland na Mozambique.
Kundi B lina timu toka Seychelles, Malawi, Lesotho na Zambia na Kundi D lina timu za Angola, Madagascar, Namibia na Zimbabwe.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza december 01 mwaka huu kwa mchezo kati ya Botswana na Comores, wakati Swaziland ikiwakabili Mozambique siku hiyo ya ufunguzi.
Ngorongoro watafungua kwa kucheza na Zambia december 2 wakati Angola wakicheza na Madagascar, Namibia na Zimbabwe, South Africa na Mauritius, Seychelles na Malawi siku hiyo.
RATIBA YA MICHEZO MENGINE.
4/12/2011
Malawi vs Lesotho
Comores vs Swaziland
Mozambique vs Botswana
Tanzania vs South Africa
Mauritius vs Zambia
05/12/2011
Madagascar vs Namibia
Zimbabwe vs Angola
Lesotho vs Seychelles
06/12/2011
Madagascar vs Zimbabwe
Tanzania vs Mauritius
Comores vs Mozambique
Namibia vs Angola
South Africa vs Zambia
Swaziland vs Botswana
08/12/2011: SEMI FINALS
Winner A vs Winner C
Winner B vs Winner D
10/12/2011:
FINAL
ROONEY AVUNJA REKODI YA MABAO KWENYE CHAMPIONS LEAGUE
Magoli mawili aliyoifungia klabu yake ya Manchester United dhidi ya klabu Otelul Galati ya Romania jana usiku, yamemfanya mshambuliaji Wayne Rooney kuwa ndio mchezaji wa kiingereza mwenye mabao mengi katika Champions League history.
Wayne Rooney ametupia jumla ya mabao 26 katika UEFA CL, akiwaacha nyuma Paul Scholes mwenye mabao 24, Frank Lampard mabao 20, na Steven Gerrard aliyetupia nyavuni mabao 19.
WAYNE ROONEY CL DEBUT AND EXCLUSIVE INTERVIEW
CHELSEA VS GENK: DE BRUYNE – NITAWAONYESHA CHELSEA WANACHOKIKOSA LEO USIKU.
Kevin De Bruyne anajipanga leo usiku kuwaonyesha Chelsea wanachokikosa kutoka kwake.
Mchezaji huyo wa Genk alikuwa kati ya moja ya wachezaji waliofuatiliwa sana na The Blues katika kipindi cha usajili kilichopita lakini ilishindikana kwenda Stamford Bridge.
De Bruyne, 20, alisema: “Nilikuwa disappointed sana wakati uhamisho wangu kwenda Chelsea ulipokwama.Nilidhani kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri lakini haikuwa hivyo, bado nina miaka 4 katika mkataba wangu na Genk wanataka pesa nyingi kwa ajili ya uhamisho wangu.Bado naamini, labda mwakani naweza kwenda Chelsea, au timu nyingine.Sidhani kama nahitaji ku-provekila kitu katika mchezo huu mmoja.Chelsea wataniangalia hata mara 20 au 30 ili kujiridhisha.”
De Bruyne atakuwa akiangaliwa na familia yake yote at Stamford Bridge leo usiku atakapokuwa akichuana na akina Lampard.
“Kuna watu zaidi ya 12 wa familia yangu na marafiki 10 wanakuja kuniangalia nikicheza leo. Nitacheza kwa uwezo wote kuiwezesha timu kushinda na kuwafurahisha ndugu na rafiki, na mashabiki wa timu yangu.”
SIMBA KUCHEZA NA RUVU SHOOTING LEO, YANGA DIMBANI NA TOTO LAKE KESHO
SIMBA ya Dar es Salaam leo ina nafasi kubwa ya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakati itakapocheza na Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Azam Chamazi Mbagala.
Hadi sasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi tisa na kushinda sita na kutoka sare tatu, ikifuatiwa na JKT Oljoro ya Arusha iliyocheza mechi 10 na kujikusanyia pointi 19 hadi sasa.
Pamoja na Simba kucheza na Ruvu Shooting iliyopo katika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14, isitarajie mteremko kwani wapinzani wao hao sio wa kubeza kwani nao wanaweza kusimama kidete na kuizuia Simba, iliyopania kumaliza duru la kwanza bila ya kufungwa hata mechi moja.
Simba katika mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya African Lyon na kuirejesha timu hiyo kileleni baada ya uongozi wa ligi hiyo kushikiliwa kwa siku kadhaa na JKT Oljoro yenye pointi 19 baada ya kucheza mechi 10 hadi sasa.
Timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa leo, itakuwa imebakiza mechi tatu kabla ya kukamilisha duru la kwanza la ligi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo namba 66 ni sh. 10,000 kwa VIP n ash. 5,000 kwa mzunguko.
Tiketi za mechi hiyo zitauzwa uwanjani Chamazi katika magari maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo.
Wakati huo huo mahasimu wa Simba, Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kucheza na Toto Africa ya Mwanza katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.