Search This Blog

Saturday, November 19, 2011

GOLI LA TICK TAK LA ROONEY VS MAN CITY KUGOMBANIA TUZO YA FIFA

Goli la mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney alilolifunga dhidi ya Manchester City msimu uliopita limewekwa katika orodha ya magoli yanayoshindania tuzo ya goli la mwaka la FIFA.

Goli la Rooney ambalo lilitokana na krosi kutoka kwa Nani katika mechi ambayo United waliwafunga mahasimu wao City, lilimuacha Joe Hart akiwa hana la kufanya wakati mpira ukiingia pembeni mwa nyavu.

Mchezaji wa Tottenham Giovan dos Santos, Barcelona star Lionel Messi na mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic na mshambuliji wa Santos kinda Neymar, wote wametajwa katika kugombea tuzo hiyo maarufu kwa jina la Puskas award.

Dos Santos alifunga goli lake katika mechi kati ya Mexico dhidi ya United States, Messi na goli lake la kwanza dhidi ya Arsenal katika Champions league, Ibrahimovic akifunga katika mechi kati AC Milan vs Lecce, huku Neymar akiingia na goli alilofunga katika mpambano kati ya Santos na Flamengo.

FIFA 2011 Puskas award, ambayo hutolewa kwa heshima ya mchezaji wa Hungary Puskas, itatolewa mwezi January tarehe 9, na mchezaji aliyeshinda mwaka jana alikuwa Hamit Altintop

HAYA NDIO MAGOLI YALISHINDANA MWAKA JANA.

GIGGS, ZIDANE, MESSI, GERRARD WATAJWA KAMA WACHEZAJI BORA WA HISTORIA YA CHAMPIONS LEAGUE

Welsh wizard: Giggs is the best British player to feature in the tournament

Winga wa Manchester United Ryan Giggs ametajwa kama mchezaji aliyeshika nafasi ya 6 katika listi ya wachezaji bora wa muda wote ligi ya mabingwa wa ulaya, kutokana na jarida rasmi la michuano hiyo.

The Welshman ndio muingereza aliyeshika nafasi ya juu katika listi hiyo inaundwa na wachezaji 50 ambayo Steven Gerrard nae amaeshika nafasi ya 10, huku wachezaji wengine wa United Paul Scholes na David Beckham wakiwemo katika 20 bora.

Giggs ambaye amelibeba kombe la ulaya mwaka 1999 na 2008 ndio mchezaji mwenye umri mkubwa kufunga bao katika michuano hiyo na maefunga katika misimu mingi zaidi kuliko mchezaji yoyote.

Mchezaji aliyeshika nafasi ya kwanza ni Zinedine Zidane ambaye goli lake kwa Madrid dhidi ya Bayern Leverkusen katika fainali ya 2002 litakumbukwa kama bao bora katika historia ya michuano hiyo.

Lionel Messi mshindi wa mara mbili wa kombe hilo akiwa na Barcelona, anafuatia katika nafasi ya pili, huku Paolo Maldini, Xavi na Raul - mfungaji bora anayeongoza akiwa na magoli 71 wakikamilisha top 5.

LISTI KAMILI IPO KAMA IFUATAVYO.

1. Zinedine Zidane
2. Lionel Messi
3. Paolo Maldini
4. Xavi
5. Raul
6. Ryan Giggs
7. Clarence Seedorf
8. Luis Figo
9. Samuel Eto'o
10. Steven Gerrard
11. Andres Iniesta
12. Oliver Kahn
13. Andriy Shevchenko
14. Paul Scholes
15. Javier Zanetti
16. Alessandro Del Piero
17. Iker Casillas
18. David Beckham
19. Thierry Henry
20. Ronaldo
21. Carlos Puyol
22. Edwin van der Sar
23. Andrea Pirlo
24. Didier Deschamps
25. Alessandro Nesta


26. Fernando Redondo
27. Wayne Rooney
28. Frank Rijkaard
29. Kaka
30. Cristiano Ronaldo
31. Ruud van Nistelrooy
32. Roberto Carlos
33. Marcel Desailly
34. Jari Litmanen
35. Peter Schmeichel
36. Flippo Inzaghi
37. Dejan Savicevic
38. Gaizka Mendieta
39. Roy Keane
40. Claude Makelele
41. Fernando Hierro
42. Edgar Davids
43. Gianluigi Buffon
44. Stefan Effenberg
45. Ronaldinho
46. Deco
47. Lothar Matthaus
48. Frank Lampard
49. Fernando Morientes
50. Paulo Sousa



Friday, November 18, 2011

FERGIE: SIMUUZI BERBATOV, ATAENDELEA KUWA HAPA MWAKA 1 ZAIDI.


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema anataka kuendelea kumfundisha Berbatov at Carrington atleast kwa mwaka mmoja zaidi.

Berbatov ambaye alinunuliwa kwa ada iliyoweka rekodi kwa klabu hiyo ya £30.75million amejikuta akipoteza namba kwa makinda Javier Hernandez na Danny Welbeck katika msimu huu unaoendelea.

Hali hii imepelekea kuzuka kwa minong’ono kuwa Ferguson anatarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo wakati wa dirisha dogo mwezi January.

Ingawa, United Boss amesisitiza hilo halitotokea.

Badala yakeinaonekana Fergie anataka kumuongezea mkataba Mbulgaria huyo kwa msimu mmoja zaidi.

“Dimitar yupo katika mipango yangu, Nimekuwa nikisoma baadhi ya magazeti kuwa nitamuuza lakini siioni sababu yoyote kwangu mimi kumuachia aondoke.

“Ni mchezaji mzuri na nitamuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Ni bahati mbaya kwamba form ya Hernandez kuanzia last year imekuwa nzuri sana lakini anacheza vizuri na anajituma mazoezini.

“Hana manung’uniko yoyote. Huyu ni professional wa kweli na tuna furaha yupo hapa. Unahitaji washambuliaji wengi wazuri siku hizi. Kama utakumbuka mwaka 1999, tulikuwa na washambuliaji wanne wazuri na wote walitumika ipasavyo, ni hivyo ndivyo hali ya sasa.” –Alisema Ferguson.

MAN CITY YAVUNJA REKODI KWA HASARA YA £195 MILLION.


Klabu ya Manchester City imetangaza imepata hasara ya kiasi cha £195.9 million.

Hasara hii imevunja rekodi kwa kuwa kubwa kuwahi kutokea kwa vilabu vya premier league, ikionyesha namna ya uwekezaji mkubwa wa Sheikh Mansour katika kuitoa City kuwa kuwa klabu ya kawaida in 2008 mpaka kuwa viongozi wa EPL kwa msimu huu.

City hawana budi kushukuru mungu, kwa kuwa figures hizi hazitokuweza kuguswa na sheria mpya ya UEFA juu ya matumizi ya pesa kwasababu matumizi haya yalifanyika kabla ya kupitishwa kwa sheria hii ambayo itaanza kutumika kwa vilabu vyote vinavyoshiriki michuano ya ulaya kuanzia msimu wa 2014-15.

UEFA wata-monitor akaunti za vilabu katika miaka mitatu kuelekea msimu huo wa 2014-15 – ukianza na msimu huu unaoendelea.

Katika sheria hiyo, vilabu vinaruhusiwa kupata hasara isiyozidi £38.5m kwa jumla ndani ya miaka 3. Hii ni moja ya njia ya UEFA kuweza kupunguza matumizi katika ada za usajili na mishahara ambayo imekuwa ikitolewa na vilabu.

City chini ya Billionea wa biashara ya mafuta kutoka Uarabuni Sheikh Mansour wameoata hasara ambayo imeweza kuifunika ya Roman Abromavich ya £141 in 2005, mwaka wa pili tangu ainunue Chelsea.

Hasara ya City imetokana na kuwekeza fedha nyingi katika kununua wachezaji wa daraja la dunia kama Edin Dzeko £27m, David Silva £26m, Yaya Toure £24m, Kolarov £19m, Mario Balotelli £24 na James Milner £26m, jumla ya fedha zilizotumika kwa wachezaji hawa ni £156m.

SIMBA KUTIMIZA MIAKA 75, ASANTE KOTOKO YAALIKWA KATIKA SHEREHE


Klabu ya Simba inatarajia kufanya sherehe za kutimiza miaka75 ya klabu hiyo mapema mwezi ujao na itazialika klabu mashuhuri kwa ajili ya maadhimisho hayo baada ya kumalizika michuano ya Chalenji.

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa shughuli hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam ikiambatana na kusoma dua kwa wale waliotangulia mbele za haki walioitumikia Simba kwa njia moja ama nyingine.

Alisema kuwa wamekwishatuma mialiko mbalimbali kwa timu watakazoalika ikiwamo Asante Kotoko ya Ghana..

Hata hivyo, Kamwaga alisema kuwa ni mapema kufahamu ni timu zipi watazialika lakini wanatarajia kuanza mchakato wa kutuma barua za mialiko kwa baadhi ya timu hasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Wakati huo huo klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana imethibitisha kucheza mchezo wa kirafiki na klabu za Simba na Yanga katika kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

Thursday, November 17, 2011

CAPELLO: PHIL JONES ANANIKUMBUSHA FRANCO BARESI


Kocha wa England Fabio Capello ameonekana kuridhika sana na kiwango cha Phil Jones baada ya kumfananisha kinda huyo wa Manchester United na moja ya wachezaji bora wa muda wote Franco Baresi.

Jones alicheza mechi yake ya 3 kwa England katika nafasi 3 tofauti baada ya kucheza kama holding midfielder katika mechi dhidi ya Sweden katika uwanja wa Wembley.

Teeneger huyo ambaye anakiri kuwa nafasi yake halisi kiwanjani ni beki wa kati, alicheza mechi yake ya kwanza kama beki wa kulia in Montenengro mwezi uliopita kabla ya kucheza kiungo cha bele katika mechi dhidi ya Spain wiki iliyopita.

“Ni vigumu sana kupata mchezaji kama Phil Jones, vigumu sana,” alikaririwa Capello.

“Katika career yangu labda nimeshakutana na aina ya wachezaji wa namna hiyo wawili tu. Naongea kuhusu Franco Baresi akiwa Milan na Fernando Hierro at Real Madrid. Walikuwa wachezaji wazuri, ambao waliweza kucheza kama kiungo na vilevile kama beki wa kati.

“Phil anaweza kucheza katika sehemu tofauti na katika kiwango cha juu. Hii inaonyesha ana kipaji kikubwa sana.”

“Kitu kizuri kuhusu Jones anapopokea mpira anatulia na kucheza vizuri bila woga,” aliongeza Capello.

“Anatoa pasi nzuri na kuzuia vizuri sana, kumuona akicheza mbele ya ukuta wa nyuma katika mechi dhdi ya Sweden kilikuwa kitu muhimu sana kwangu, kwa sababu sasa kama Parker akiwa hayupo fiti, then ninaye mbadala wake, nae ni Jones.” Alimaliza Fabio Capello.

LUCAS MOURA: MBRAZIL MWENYE KIPAJI ANAYEZIGOMBANISHA MAN UTD NA LIVERPOLL.


Kiungo anayechipukia wa kibrazili anayewania na klabu mbili mahasimu wa ligi kuu ya England Lucas Moura ameambiwa na klabu yake ya Sao Paulo kuwa ataweza kuuzwa mwezi January ikiwa klabu inayomtaka itatoa ofa ambayo watashindwa kuikataa.



Kiungo huyo ambaye amekuwa akizizvutia klabu nyingi barani ulaya baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika ligi ya nchini kwao, lakini klabu yake ya Sao Paulo wamekuwa wagumu kumuachia kiungo huyo.

“Wazo letu ni kutokumuuza kabisa katika dirisha dogo la usajili mwezi January, lakini kama kuna timu kati nyingi zinazomuwania itatoa ofa ambayo ni nzuri tutashindwa kumzuia kuondoka.” Alisema mwakilishi wa klabu hiyo ya Brazil.

KOCHA KENNY MWAISABULA ATAJA KIKOSI CHA RAUNDI YA KWANZA YA VPL.

MZUNGUKO WA KWANZA WA LIGI KUU YA VODACOM UMEMALIZIKA HIVI KARIBUNI, KOCHA MAHILI HAPA NCHINI KENNY MWAISABULA ( MZAZI ) AMEKITAJA KIKOSI CHA WACHEZAJI WALIOFANYA VIZURI KWENYE HUO MZUNGUKO WA KWANZA.

Kenny Mwaisabula.






1- Mwadini mwalimu [Azam]
2- Hamis Mapande [JKT]
3- Waziri Ally [Azamu]
4- Shabani Aboma [Afikan Lyon]
5- Juma Nyoso [Simba]
6- Ibrahimu Masawe [Polisi ]
7- Nurdin Bakari [Yanga]
8- Haruna Niyonzima [Yanga]
9- Said Rashid [Mtibwa]
10- Haruna Moshi [Simba]
11- Ramadhani Chombo[Azam]

RESERVES

12- Juma Kaseja [simba]
13- Mohamedy Binsulum [villa]
14- Sabri Ramadhani [Coastal]
15- Shaban Ibrahimu[Ruvu]

16- Malegesi Mwangwa [Kagera]
17- Mohamedy Soud [Toto]
18- Andrew Basembe[Moro]
19- Ally Hamza [Oljoro]
20- Sunday Mussa [oljoro]
Hao ni wachezaji ambao binafsi niliona wanastahili kuwepo katika kikosi cha TAIFA STARS hawa ndo wachezaji waliocheza kwa kiwango kizuri mno na ushahidi pia utaupata TFF kupita kwa wataalamu wao, Wengi wa wachezaji hawa wamekuwa kwenye tuzo za wachezaji bora wa mwezi na hilo ndo uthibitisho kuwa ni wazuri

SUAREZ ASHTAKIWA NA FA KWA KUTOA MANENO YA KIBAGUZI DHIDI YA EVRA


Mshambuliaji wa ki-uruguay Luis Suarez anayeichezea klabu ya Liverpool ameshtakiwa na FA kwa tuhuma za kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra.

Mshambuliaji alishutumiwa na mlinzi wa Manchester United mara tu baada ya mchezo dhidi ya timu zao ulioisha kwa matokeo ya sare ya 1-1 mwezi uliopita.

Akiongea baada ya mchezo , Evra aliiambia kituo cha matangazo cha kifaransa: “Kuna camera. Unaweza kuona Suarez akiniambia neno la kibaguzi zaidi ya mara 10.”

Lakini Suarez alipinga madai hayo ya Evra, akisema: “Nimekasirishwa sana na shutuma hizi za ubaguzi wa rangi. Ninachoweza kusema kwamba siku zote nimekuwa nikiheshimu kila mtu. Wote tupo sawa. Naenda uwanjani kucheza mchezo ninaofurahia na sio kuleta mitafaruku.”

Hata baada ya kujitetea chama cha soka cha FA kimeona kuna kesi ya kujibu kwa Suarez, ikiwa ni muda mchache tangu Raisi ya FIFA Sepp Blatter kukaririwa akisema hakuna ubaguzi wa rangi ndani ya dimba la soka.

BOBAN AITWA KWENYE KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS


28 WAITWA KILIMANJARO STARSK

ocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu. Wachezaji walioteuliwa ni Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba) na Paul Ngelema (Ruvu Shooting). Mabeki wa kati ni Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Salum Telela (Moro United). Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mwaipopo (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Haruna Moshi (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Rashid Yusuf (Coastal Union), Jimmy Shogi (JKT Ruvu Stars) na Mohamed Soud (Toto Africans). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Gaudence Mwaikimba (Moro United), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Daniel Reuben (Coastal Union) na Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada).

MAPATO STARS v CHAD

Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil- raundi ya mtoano kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Chad lililochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 78,389,000. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,111. Viti vya kijani na bluu ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 2,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo walikuwa 23,748 ikiwa ni zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo. VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 20,000, jumla ya mashabiki 187 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. VIP B ambapo kiingilio kilikuwa sh. 10,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa 1,181. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 5,000 kwa VIP C ambapo waliingia mashabiki 1,678 wakati mashabiki 2,319 walikata tiketi kwa viti vya rangi ya chungwa ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA KUONGOZA FAM

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya. Uchaguzi huo uliendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya FAM chini ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Viongozi waliochaguliwa kwa kuzingatia Katiba ya FAM na Kanuni za Uchagzui za wanachama wa TFF ni wafuatao; Fabian Samo amefanikiwa kutetea wadhifa wake wa Mwenyekiti huku Deogratius Rwechungura akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa ni Mugisha Galibona (Katibu Mkuu), Samwel Silasi (Katibu Msaidizi), Evans Liganga (Mhazini), David Sungura (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), William Chibura (Mwakilishi wa Klabu) na Valerian Goroba (Mjumbe).

Binafsi sina lengo la kuwa mwanasiasa- Aboutraika..


Number 10-Unaelezeaje historia yako kifamilia na ulianzaje soka lako?

Aboutraika-Kiukweli mimi nimetokea kwenye familia masikini , kama ilivyo kwa familia nyingi Misri, nilipata tabu sana utotoni , niliwahi kufanya kazi kwenye kiwanda cha matofali nikiwa na umri wa miaka 12 ili kuisadia familia yangu katika kulipa ada ya shule na pia nilianza kujitegemea nikiwa na umri mdogo sana .Wazazi wangu walifanya juhudi kubwa sana kunikuza na kunilea na tabu tulizopata utotoni zimenisaidia san kufika hapa nilipo leo.Nilianza kucheza soka mitaani na vijana wenzangu nikiwa mdogo hadi hapo jirani yetu mmoja aliponiona na kunipeleka timu inayoitwa Tersana huko Misri kwa ajili ya majaribio , nilicheza huko kwa miaka 12 hadi hapo nilisajili El Ahly ambao nimekuwa nao kwa miaka nane sasa.

Number 10-Siku zote umekuwa ukifunga mabao muhimu kwenye nyakati muhimu za mechi,unawezaje kufanya hivyo?

Aboutraika
-Ni zawadi toka kwa Mungu kusaema kweli, kwa yote ninayofanya siwezi kuamua kufunga bao la ushindi au la kusawazisha au kufunga kwenye dakika za majeruhi , ni zawadi toka kwa Mungu na natumaini zawadi hii ntaendelea kuwa nayo.

Number 10-Ulicheza dhidi ya Brazil na Italia mwaka 2009.Ulijisikiaje kucheza kwenye kiwango cha juu kama hivyo?
Aboutraika
-Ilikuwa kitu kizuri sana kwangu.Kiwango ambacho unajihisi upo ukiwa unacheza kwenye michuano kama ile ni kikubwa sana na unaona mwenyewe unapokuwa uwanjani, ni kiwango cha juu sana ambacho kilitupa nafasi ya kuonekana dunia nzima kama timu na kama nchi, nadhani Misri ina vipaji vya kutosha kupambana na timu kama Brazil na Italia .

Number 10-Ulikuwa unawaza nini ulipokuwa unacheza mechi hizi?

Aboutraika-Tulifikiri kuwa hatuna chochote cha kupoteza kama timu,sio kama tunacheza mechi hizi kila siku hivyo nafasi zote chache tunazopatra tunazitendea haki kadri tuwezavyo, ilikuwa nafasi ya kuonyesha uwezo wetu, hakuna aliyetaraji kutuona tukiwa washindi ila tulitumai kuonyesha dunia nzima sisi ni kina nani na soka letu lilipo.

Number 10-Misri haijacheza kombe la dunia tangu mwaka 1990, unaweza kutueleza kwanini?

Aboutraika-Wapinzani wetu wanasema kuwa tunacheza soka zuri na bora kuliko timu nyingi Afrika , lakini huwa tunafanya hivyo pale tunapokuwa pamoja kwa muda mrefu kitu ambacho ni cha kweli, kwa mfano kwenye kombe la mataifa ya Afrika ambako tunakaa pamoja kwa muda mwingi lakini huwa tunakaa kambini kwa siku tatu tu kabla ya mechi za kufuzu kombe la dunia na umeona tofauti ilipo kwenye mataifa ya afrika tumefanyaje na kwenye kombe la dunia tumefanyaje.

Number 10-Umewahi kupoteza matumaini juu ya kucheza kombe la dunia katika maisha yako?


Aboutraika-Inakuwa vigumu sana kwangu kushiriki kombe la dunia , kwanza kwa sababu ya umri wangu, lakini nadhani kwa kila mafanikio yanapokosekana uzoefu unaongezeka , inabidi tujikakamue na na kupigana huku tukiwa na matumaini kuwa siku yetu itakuja na sisi tutacheza .

Number 10-Bado una mawazo kuwa mchezo wa soka unaunganisha watu?

Aboutraika-Hakika , mchezo wa soka unaunganisha watu na unasaidia kwenye vita dhidi ya umasikini. Mbali na kucheza soka na kufunga magoli mchezo huu unajenga maadili ya watu , sisi tunawapelekea watu ujumbe na misingi ya kimaisha kwa watu , huu ni mchezo ambao unapeleka ujumbe wa masuala ya biashara na hata siasa ni mchezo ambao unavuka zaidi ya uwanja.

Number 10-Imani yako ina umuhimu gani kwako?

Aboutraika-Mimi ni muislamu na ninaona sifa kuwa muislamu .Unapata nguvu za mwili kutokana na kufanya mazoezi lakini nguvu ya kiimani inatoka kwa Mungu, Mungu anakupa nguvu ya maisha,uhusiano wako na Mungu ndio unaokupa maisha na ndio kitu cha muhimu kuliko kila kitu katika maisha, ni mahesabu rahisi sana Mungu alituumba na roho na mwili lakini roho haiwezi kuwa na nguvu bila ya kupewa nguvu hiyo na Mungu, nadhani Mungu anapaswa kutafutwa na kila mtu ulimwenguni.

Number 10-Kuna picha inakuonyesha wewe ukipiga magoti kuswali kwenye mahali Fulani pale Tahrir siku ambayo Hosni Mubarak aliachia ngazi, kuna kitu chochote hapa?

Aboutraika-Hakuna chochote pale ambacho kina maana kubwa , nilikuzwa kwa kuelekezwa kuwa kuna mabaya na mema,nimepewa zawadi na Mungu na siku zote naunga mkono kilicho sahihi.Unaweza kuwa kwenye baya au kwenye jema au unaweza kuwa katikati ya mambo yote yanayotokea au unaweza kuunga mkono yanayotokea . Baada ya hotuba ya mwisho ya Mubarak, siku moja kabla ya kuachia ngazi,nilihisi kuwa kuna hisia kubwa za hasira na kukata tama miongoni mwa watu wote hasa wale waliokuwepo pale Tahrir Square,nilikuwa na lengo la kuwanyanyua watu wangu na kuwapa moyo kuwa kuna mema yanakuja.

Number 10-Unadhani ungeweza kujiunga na na waandamanaji wakati vugu vugu lilipoanza ?

Aboutraika-Nadhani ningejiunga na waandamanaji mwanzoni kama ningepata nafasi ya kufanya hivyo , niliwahi kufikiri kujiunga na waandamanaji mwanzoni na siku zote nilipowaza nilipata wazo ambalo lilinipa sababu ya kungoja .

Number 10-Uliwahi kuwaza kuwa ungeunga mkono mapinduzi halafu inatokea yakafeli ungejiweka kwenye wakati mgumu katika maisha yako ya soka?

Aboutraika-Hapana , sijawahi kufikiria hivyo hata siku moja . Ninaaamini kuwa maishani kuna wakati unapaswa kuwa na msimamo na unachotaka na hupaswi kufanya mahesabu kwenye msimamo huo na hupaswi kuwaza matokeo mabaya akilini mwako , kaka unaamini kuwa unachounga mkono ni sahjihi basi kifanye pasipo woga.
Number 10-Ulijisikiaje kuona Mubaraka akiachia ngazi mwisho wa siku ?

Aboutraika-Kama mtu yoyote wa Misri nilipata tabu kutokana na rushwa ambayo imepoteza maisha ya watu wengi na rasilimali pia, nilipoteza haki zangu kwa kiasi kikubwa kutokana na rushwa.

Number 10-Je una malengo ya kujiunga na siasa?

Aboutraika-Hapana mimi ni mtu wa vyama vyote , naamini mtu yoyte anaweza kuitumikia nchi yake na mtu yoyote mwenye malengo mazuri na nchi yangu nitamuunga mkono ila binafsi sina lengo la kuwa mwanasiasa.

NAMIBIA YAINGIA MICHUANO YA CHALENJI



Release No. 116

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Novemba 16, 2011

Namibia itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Hivyo Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti. Pia ratiba ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Tusker imetangazwa rasmi leo (Novemba 16 mwaka huu) ambapo mechi zote zitachezwa Dar es Salaam baada ya Mkoa wa Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa ili nayo iwe kituo cha michuano hiyo. Mechi mbili zitachezwa kwa siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo kutafanyika uzinduzi rasmi saa 10 jioni kwa mechi kati ya Tanzania Bara na Rwanda. Novemba 25 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Burundi na Somalia (saa 8 mchana) na Uganda na Zanzibar itakayoanza saa 10 jioni. (Ratiba yote ya mashindano imeambatanishwa)


MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI


Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro), Charles Boniface Mkwasa kesho (Novemba 17 mwaka huu) saa 6 mchana atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika ofisi za TFF ambapo pamoja na mambo mengine atatangaza kikosi kitakachotetea Kombe la Chalenji.


Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, November 15, 2011

FINAL SCORE: MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014:TANZANIA 0-1 CHAD

DK 90: Mpira umemalizika Stars 0-1 Chad, TANZANIA imefuzu hatua ya makundi kwa sheria ya goli la ugenini.


DK 82: Machupa anafunga bao kutokana na pasi ya Samata lakini mwamuzi anakataa kwa kusema mfungaji ameotea.

DK 80: Chad wanamtoa Mahamat Habib aliyefunga bao na anaingia Dany Karl Max.

DK 75: Chad wanalishambulia kwa kasi sana lango la Stars, wanakosa bao la wazi baada ya Aggrey Morris kuondoa hatari langoni mwa Stars.

DK 70: Taifa Stars inafanya mabadiliko anatoka Henry Joseph, anaingia Abdi Kassim.

DK 68: Chad wanafanya mabadiliko anatoka Yaya Karim anaingia Appolinare.

DK 61: Stars wanalishambulia kwa nguvu sana lango la Chad.

DK 58: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka Nizar Khalfan anaingia Nurdin Bakary.

DK 54: Tanzania inapata kona 3 na kushindwa kuzitumia vizuri.

DK 53: Thomas Ulimwengu anakosa bao la wazi hapa.

DK 49: Goaaaaaaaaaaaaal, Chad wanapata bao la kuongoza hapa.

DK 46: Kipindi cha pili kinaanza na Samta anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa tu.

DK 45: Mpira ni mapumziko, Stars 0-0 Chad.

DK 38: Juma Nyosso anaokoa hatari hapa langoni mwa Stars.

DK 35: Jves Maldjilam wa Chad anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Shomari Kapombe.

DK 30: Nditi anakosa bao la wazi kutokana na krosi nzuri ya Ngassa.

DK 25: Chad wanafanya shambulizi kali lakini wanashindwa kulenga lango. Chad wanacheza mchezo wa counter attack huku wakipiga mashuti kila wanapopata nafasi.

DK 20 : Ngassa anaangushwa ndani ya eneo la hatari na mpira unatoka nje mwamuzi anaamuru kona, ambayo Stars wanashindwa kuitumia vizuri.

DK 15: Mahmat Habib wa Chad anapiga shuti kali na Kaseja anapangua inakuwa kona,

DK 12: Samatta anakosa bao la wazi akishindwa kuunganisha krosi nzuri ya Ulimwengu thomas.

DK 9: Stars wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia.

DK 5: Nizar Khalfan anagongeana vizuri na Thomas Ulimwengu lakini anakosa bao hapa.

DK 1: Mpira umeanza na Chad wameanza kwa kasi sana. mwamuzi ni kutoka Madascar, Andraza Hamada.

9:45: Timu zinaingia uwanjani na nyimbo za taifa zinaanza kupigwa lakini cha ajabu hakuna hata bendera ya taifa inayopepea hapa uwanjani

Taifa Stars:

Juma Kaseja (1)

Shomari Kapombe (2)

Idrissa Rajab (15)

Juma Nyosso (4)

Aggrey Morris (6)

Shabani Nditi (19)

Thomas Ulimwengu (20)

Henry Joseph (17)

Mbwana Samata (10)

Nizar Khalfan (16)

Mrisho Ngassa (8)

Subs:

Mwadini Ally (18)

Erasto Nyoni (12)

Hussein Javu (23)

Mohamed Rajab (11)

Ramadhan Chombo (21)

Abdi Kassim (13)

Nurdin Bakari (5)

John Bocco (9)

Juma Jabu (3)

Godfrey Taita (7)

Chad (tentatively line up)

Brice Mabaya (1)

Sylvain Doubam (5)

Massama Asselmo (15)

Armand Djerabe (4)

Yaya Karim (2)

Herman Doumnan (6)

Ferdinand Gassina (17)

Ahmat Mahamat Labo (10)

Ezechiel Ndouassel (11)

Hassan Hissen Hassan (7)

Dany Karl Marx (9)

Subs:

Cesar Abaya (12)

Wadar Igor (13)

David Mbaihouloum (8)

Dillah Mbairamadji (16)

Djingabeye Appolinare (3)

Rodrigue Casmir Ninga (18)

Mahamat Habib (14)

Marius Mbaiam (

Abakar Adoum (

Jules Hamidou (


Ekiang Moumine (


BRAZIL WAENDELEZA UBABE AFRIKA

KELVIN YONDAN AWASILISHA UTETEZI WAKE SIMBA, KUJUA HATMA YAKE LEO.


Mlinzi wa kati klabu ya wa Simba, Kelvin Yondan amewasilisha utetezi wake kwa uongozi wa klabu hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo kutokana na kuondoka kambini bila taarifa yoyote.

Beki huyo ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Simba, hivi karibuni alitoweka kambini bila taarifa yoyote kwa uongozi kitu kilichosababisha kukosa michezo kadhaa ya Ligi Kuu raundi ya kwanza.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alithibitisha uongozi kupokea barua hiyo ya utetezi kutoka kwa mchezaji huyo lakini akasema kuwa wataweka wazi kila kitu siku ya leo.

''Ni kweli mchezaji huyo ametuandikia barua baada ya kukaa kimya muda mrefu pamoja na uongozi kumtaka kujitete kwa barua lakini kiutendaji ni lazima Mwenyekiti aipitie barua hiyo ndipo nami niitangaze,'' alisema Kamwaga.

Uongozi wa klabu hiyo ulimpa nafasi mbili mchezaji kuandika barua ya kujitetea au kukatisha mkataba kama hatakuwa hataki kuitumikia klabu hiyo..

Monday, November 14, 2011

BECKHAM NA MWANAE: LIKE FATHER LIKE SON



Anaweza kuwa na miaka 6 tu lakini Cruz Beckham tayari ameshaanza kufuata nyayo za baba yake.

Cruz tayari ameshaanza kucheza soka lakini inaonekana tayari ameshaanza kufuata mitindo ya nywele ya zamani ya mzazi wake.

Cruz alionekana jana akiwa anacheza soka huku kichwani akiwa kanyoa mtindo wa “kiduku” ambao Beckham alinyoa miaka 10 iliyopita

Mtoto huyo mdogo kabisa wa kiume wa Beckham, pia style yake ya nywele imeonekana kufanana na na style ya Roberto De Niro katika filamu ya Taxi Driver.

Cruz pia anajulikana kwa kupenda kuchora temporarly tattos – kitu kingine ambacho amekiiga kutoka baba yake.

Alionekana na baba yake mjini LA akiwa anachorwa katika painting session at Color Me Mine – sehemu ambayo watoto wanajifunza kuchora kwa ubunifu wao wenyewe.

BREAKING NEWS: CHUJI ARUDI YANGA.




Dirisha la usajili nchini limefunguliwa na taarifa zilizothibitishwa kutoka klabu ya Jangwani zinasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo kiungo Athumani Idd Chuji ameongezwa katika kikosi cha Yanga.


Chuji ambaye aliondoka Yanga baada ya msimu uliopita na kujiunga na Simba kabla ya kuondoka na kutaka kujiunga Villa lakini akakosa nafasi, sasa amejiunga na klabu yake ya zamani baada ya kocha Kostadin Papic kutoa mapendekezo hayo.


Pia kocha huyo wa Yanga inasemekana amewapa ruhusa ya kuondoka wachezaji Fred Mbuna na Godfrey Bonny kwa kuwa hawapo katika mipango yake ya baadae ndani ya timu hiyo.


ULIKUWA MCHEZO WA KIRAFIKI, LAKINI SASA NI DHAHIRI SPAIN WANAHITAJI "PLAN B" ILI KUENDELEZA UTAWALA WAO KWENYE SOKA.


Timu ya taifa ya Hispania ni ndio timu inayocheza mchezo mzuri kuliko timu ulimwengu kwa sasa. Hata waanzalishi wa mpira wa miguu wakicheza katika dimba lao la nyumbani Wembley, walijikuta wakicheza ndani ya nusu yao ya uwanja ili kujihakikishia japo nafasi finyu ya kupata matokeo chanya dhidi ya vijana wa Vicente Del Bosque. “Ilikuwa ndio njia pekee ya kushindana nao,” alisema kocha Fabio Capello.

Alikuwa sahihi kabisa.

Spain waliutawala mchezo sana na walitengeneza nafasi na kufanya mashambulizi mengi katika mchezo wao dhidi ya England. Kitu pekee kilichokosekana kwa upande wao, ni goli.

England nao walikuwa na bahati baada ya Davidi Villa kugongesha mwamba, Cesc Fabregas nae alipiga shuti ambalo lilitoka nje kidogo ya goli katika dakika ya mwisho, hizi ni baadhi ya nafasi nyingi Spain walizopoteza. Ndio, Spain walistahili kushinda, lakini tatizo ni nini?

NOT-SO-FRIENDLY MATCHES | Spain's defeats since winning the World Cup

RivalPlayed in
Date
Result
Argentina
Buenos Aires07/09/2010Lost 4-1
Portugal
Lisbon17/11/2010Lost 4-0
Italy
Bari
10/08/2011Lost 2-1
England
London12/11/2011Lost 1-0

Rekodi za hivi karibuni za Spain katika mechi za kirafiki zinaonyesha hali ni mbaya sana kwa vijana wa Del Bosque. Tangu washinde World Cup, ‘La Roja’ wamekuwa na matokeo mabaya katika mechi zisizo za mashindano. Vicente Del Bosque’s men walihangaika kupata droo na Mexico, kabla ya kufungwa 4-1 na Argentina mjini Buenos Aires na baadae kutandikwa 4-0 na Ureno.

Pengine walijitahidi kushinda 4-0 dhidi ya Marekani na 3-0 dhidi ya Venezuela lakini ilikuwa wakicheza na timu ambazo ni dhaifu kwa upande wao, lakini wakicheza dhidi ya wapinzani wa levo zao wanakuwa wana-struggle sana, hasa wakiwa timu inayocheza mchezo wa kuzuia zadi.

Hali hii ilionekana zaidi katika World Cup katika mchezo wa kwanza wa dhidi ya Switzerland ambao walifungwa, kabla ya kuwafunga Portugal, Paraguay, Germany na kumaliza kwa Uholanzi katika mechi ngumu ambayo iliamuliwa kwa ushindi wa goli moja tu. Spain walistahili kushinda mechi hizi, lakini walipata shida, na bahati inaweza isiwe upande wao kama ilivyokuwa jumamosi iliyopita @ Wembley.

Muda huu , wakiwa wanaonekana kama timu bora ulimwenguni, Spain wanaonekana kujua kucheza aina moja tu ya mchezo, ambayo mara nyingi imekuwa ikiwapa matokeo mazuri, lakini mbinu mbadala zinahitajika ili kujihakikishia ushindi katika mechi ngumu. Ndio maana Del Bosque ni mpenzi mkubwa wa mchezaji wa Athletic Bilbao Fernando Llorente, ni sababu mojawapo kwanini bado ana imani kubwa na uvumilivu kwa mchezaji wa Chelsea Fernando Torres: wanatoa mchango tofauti timu inapokabiliana na wapinzani wagumu. Pia Fabregas akicheza kama namba tisa wa uongo, huku David aki-operate kama Lionel Messi na Del Bosque anaweza kuunda ukuta wa watu watatu dhidi ya timu isiyoshambulia sana, kama ambavyo Barcelona wamekuwa msimu huu.

Japokuwa mafanikio ya Euro na World Cup, Spain ni hatari wanapokuwa wametanguliwa kufungwa. Comebacks dhidi ya Chile na Czech Republic zilithibitisha wanaweza, lakini michezo yote miwili walitegemea kushinda, Anyway. Kutanguliwa kufungwa na moja ya timu kubwa barani ulaya mara zote umekuwa ni mtihani mgumu kwa upande wao, na hii ndivyo ilivyotokea katika mechi nyingine ya kirafiki waliyofungwa na Italy 2-1 mwezi August. Afadhali Spain walisawazisha ikawa 1-1 kwenye mechi hiyo, lakini walishindwa kufanya hivyo katika mechi dhidi ya Switzerland au katika mechi nyingine zote za kirafiki walizofungwa.

Hizo ndio zilikuwa mechi za kirafiki na ni fair kusema Spain watacheza vizuri katika mechi za mashindano – kama ilivyo kwa timu nyingine. Kwa sasa timu nyingi barani ulaya ambazo Spain ni wapinzani wao watakuwa wameshajizatiti namna ya kucheza dhidi ya mbinu ya uchezaji ya La Roja. Hivyo Spain aka La Roja ili kuweza kuwa timu ya kwanza kushinda Euro, then World Cup na baadae kufuatiwa na ushindi wa kombe lingine la bara mfululizo, then a “Plan B” Inahitajika ili kuweza kuitimiza ndoto hiyo.