Search This Blog
Saturday, August 3, 2013
VIDEO: HUYU NDIO MOSES OLOYA ANAYEZITOA UDENDA SIMBA NA YANGA KWENYE USAJILI MSIMU HUU - AKIRI TIMU ZOTE ZINAMTAKA
HAYA NI MAHOJIANO BAINA YA OLOYA NA GAZETI LA MWANASPOTI
MCHEZAJI wa Xi Mang Saigon ya Vietnam, Moses Oloya amekiri kupokea tiketi ya ndege aliyotumiwa na Yanga, lakini akasema hajachagua timu ya kuichezea kati ya Simba na Yanga. Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Vietnam jana Ijumaa, mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda alisema amefanya mazungumzo na klabu zote mbili; Simba na Yanga lakini atafanya uamuzi wa mwisho Agosti 31 baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Vietnam. “Mkataba wangu unakwisha mwishoni mwa Oktoba, lakini mechi za Ligi Kuu Vietnam tunamaliza Agosti 31,” alisema. Haya ndiyo mahojiano ya Mwanaspoti na Oloya yaliyofanyika jana Ijumaa saa 9:15 alasiri kwa dakika 12.
Mwanaspoti: Kuna utata hapa Tanzania, ni timu gani unakuja kuichezea msimu ujao?
Oloya: Ngoja nikuambie ukweli, mpaka sasa sijaamua kati ya Simba na Yanga.
Mwanaspoti: Kwani umefanya mazungumzo na timu zote mbili?
Oloya: Ndiyo karibu kila siku ninazungumza na watu wa Simba na Yanga.
Mwanaspoti: Umewaambia nini?
Oloya: Nimewaambia wasubiri nimalizane na timu yangu ya Saigon.
Mwanaspoti: Utamalizana lini na timu yako ya Saigon?
Oloya: Tutamaliza mechi ya mwisho ya ligi Agosti 31, lakini mkataba wangu unakwisha Oktoba mwishoni.
Mwanaspoti: Mbona tunasikia upo Dar es Salaam?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam.
Mwanaspoti: Kwa mara ya mwisho umekuja lini Dar es Salaam?
Oloya: Kwa mara ya mwisho nimekuja Dar es Salaam Kombe la Chalenji mwaka jana.
Mwanaspoti: Mbona tunasikia umekuja Dar es Salaam wiki hii?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam, tena nipo na Geoffrey Kizito hapa tunakwenda kupata chakula cha jioni (Namsalimu Kizito).
Mwanaspoti: Lakini moyoni unaijua timu utakayochezea msimu ujao?
Oloya: Zipo timu tatu, timu yangu
(Saigon) bado wapo fifte fifte, halafu kuna hizo Simba na Yanga. Bado
sijajua timu ambayo nitaichezea. Itategemeana na makubaliano.
Mwanaspoti: Mbona tumeambiwa Yanga wamekutumia tiketi ya ndege?
Oloya: Ni kweli, Yanga walinitumia tiketi ya ndege, ambayo ilitakiwa niwe Dar es Salaam Alhamisi na kurudi Ijumaa wiki hii.
Mwanaspoti: Mbona umeshindwa kuja Dar wakati tayari ulitumiwa tiketi na Yanga?
Oloya: Klabu yangu imekataa kuniruhusu, kwa sababu tuna mechi muhimu kesho (leo Jumamosi) dhidi ya Da Nang.
Mwanaspoti: Hiyo tiketi ilikuwa ni ya ndege gani?
Oloya: Qatar Airways
Mwanaspoti: Kwa hiyo ulitaka kuja kusaini mkataba Yanga?
Oloya: Nilitaka kuja kuwasikiliza.
Mwanaspoti: Kwa hiyo mpango wako ni upi kwa Yanga na Simba?
Oloya: Wameniambia nimalizane na
klabu yangu (Saigon) na hicho ndicho ninachokifanya, ingawa pia timu
yangu bado haijawa wazi kama itanipa mkataba mpya au la.
Maelezo ya ziada
Baada ya mechi ya leo Jumamosi, Saigon itakuwa
imebakiza mechi nne dhidi ya Kien Giang, Song Lam Nghe An, Hoang Anh Gia
Lai na Long An.
Saigon inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 23 katika msimamo wa Ligi Kuu Vietnam yenye timu 12.
Usajili wa awali wa Ligi Kuu Bara msimu ujao
unafungwa Jumatatu saa 6.00 usiku lakini utafungulia tena kwa muda wa
wiki mbili kuanzia Agosti 15 na kwamba hadi jana Ijumaa jioni Simba na
Yanga zilikuwa na wachezaji wanne wa kigeni kila moja na wanamsubiri
mchezaji huyo kujazia orodha yao.
MAKALA: USAJILI WA GARETH BALE UNAASHIRIA SIKU ZA CRISTIANO RONALDO KUBAKI SANTIAGO BERNABEU ZIPO SHAKANI
Wakati Real Madrid wakiwa kwenye harakati za kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili winga wa Tottenham Gareth Bale, uhamisho ambao unatoa ishara kwamba mwisho wa mchezaji waliyemlipia fedha nyingi zilizovunja rekodi ya dunia Cristiano Ronaldo unakaribia? Imekuwa ikiaminika kwamba Madrid wangeenda kumnunua Bale msimu huu ikiwa tu Ronaldo atataka kuondoka. Kwa sasa, mreno huyo anabaki kuwa mchezaji wa Real Madrid kwa asilimia mia, lakini kwa namna Madrid inavyoonesha kumhitaji Bale inaonekana siku za Ronaldo Bernabeu ni za kuhesabika.
Wakati tetesi za Ronaldo kurudi Manchester United ambazo zilitikisa sana mwanzoni mwa dirisha la usajili, sasa zinaonekana zimepoa, bado hatma yake ndani ya Madrid ipo shakani. Sababu kuu la hilo ni kwamba winga huyo mwenye miaka 28 anaingia kwenye miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake, hatua ambayo thamani ya mchezaji huanza kushuka, na ameonyesha hana nia ya kusaini mkataba mpya. Mara ya mwisho Ronaldo kuzungumzia mkataba wake na Madrid alisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba 'taarifa zote za kusaini mkataba mpya ni za uongo'.
Huko nyuma, Ronaldo alizipa tetesi za kutaka kuondoka baada ya kusema kwamba hakuwa na furaha kwa sababu za kikazi ndani ya Madrid, kitu kilichotafsiriwa kwamba alikuwa akihitaji mashahara mkubwa na sapoti kubwa kutoka viongozi wa juu wa klabu. Mtu mmoja ambaye haamini kama suala hilo lilishaisha ni raisi wa zamani wa Madrid Ramon Calderon.
"Nafahamu kwamba hana furaha kabisa kwasababu ya tabia za Raisi," aliiambia Talksport Jumatano iliyopita. “Anataka mshahara wa €20 million kwa msimu jambo ambalo litakuwa gumu kwa Real kukubali.”
Na Calderon pia anaamini kwamba uhamisho wa kumleta Bale umechangiwa sana na sintofahamu ya hatma ya Ronaldo. “Nadhani raisi amejiandaa kwa kila kitu ikiwa atashindwa kumshawishi Ronaldo asaini dili jipya. Hivyo ndivyo ninavyoona. Anaogopa utafikia wakati Cristiano atasema 'sitaki kuendelea kuwa hapa'. Hiyo itakuwa habari mbaya kwa Madrid. Ningependa aendelee kuwa pale na kustaafu soka akiwa Bernabeu lakini kwa sasa hali ilivyo ni vigumu. Ngoja tuone wiki kadhaa zijazo mambo yatakavyokuwa.”
Maoni ya Calderon ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa kumleta Ronaldo Madrid - na amekuwa akimtuhumu Perez kwamba kutokana hakuhusika katika kumleta mchezaji huyo ndio sababu ya kutompa sapoti mchezaji anayohitaji tofauti na ilivyo kwa wachezaji ambao alihusika na kuwanunua moja kwa moja, kitu ambacho kimewahi kumtokea hata Gonzalo Higuain.
Perez amekuwa akitaka kuonekana kwamba yupo nyuma ya Ronaldo kwa asilimia 100, na amekuwa akikaririwa akisema kwamba mchezaji huyo ataendelea kuwa Bernabeu na atamalizia mpira katika klabu hiyo - lakini nyuma ya kauli zake hizo ambazo zimekuwa zikitafsiriwa kuwa za kisiasa haswa hivi karibuni wakati ulipofanyika uchaguzi wa Madrid.
Wakati wakijiandaa kutoa fedha nyingi kuhakikisha wanamsajili Bale, inaonekana kama ni jambo la kamari kumfanya mchezaji ambaye ana uzoefu wa msimu mmoja wa champions league kuwa ndio star wa kikosi kinachotaka kubeba ubingwa wa ulaya kwa mara 10.
lakini pia uharaka wa kumleta Bale Bernabeu unatokana na hisia kwamba Ronaldo anaweza asiwe jijini Madrid kwa muda mrefu. Suala la Ronaldo kutokusaini mkataba mpya mpaka sasa haliwezi kuwa suala la Madrid kulichukulia poa. Kwa mchezaji hili suala ni faida kwake kwasababu mkataba unapokuwa unaelekea kuisha yeye anazidi kupata nguvu ya maamuzi dhidi ya hatma yake, wakati kwa upande wa Madrid wanajua wanapaswa kufanya wafanyalo kipindi hiki cha kiangazi walimalize suala la Ronaldo ikiwa wanataka kurudisha fedha zao walizolipa kumnunua la sivyo wanaweza kumuuza kwa kiasi kidogo au wakakosa kabisa ikiwa atabaki mpaka mkataba wake utakapoisha.
Friday, August 2, 2013
REAL MADRID NA MANCHESTER UNITED KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFORD
Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda Manchester United mwezi huu baada ya nahodha huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.
Gazeti la Daily Star limesema United na Real Madrid wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada ya uhamisho ya paundi millioni 80 - na mabingwa wa Premier League wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha kipenzi chao Old Trafford.
Raisi wa Real Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini mkataba mpya - na alishangazwa kwamba mchezaji kuwa alikuwa tayari kurudi United.
Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.
Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye tayari wameshatoa ofa ya £85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth Bale kutoka Tottenham.
Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa. Pia Wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'.

DIRISHA LA USAJILI TANZANIA KUFUNGWA JUMATATU IJAYO - AUGUST 5
Usajili
wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa
Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama
ilivyokuwa imepangwa awali.
Uamuzi
wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu
ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa
wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na
kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.
Kutokana
na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6
na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana
Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa
wachezaji wenye matatizo.
Hatua
ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha
wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu
huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza
nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia
Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.
Pia
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa
kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za
bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa
kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa
kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Rwiza
atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha
mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola
itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa
na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.
Matemera
atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa
mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi
namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.
QUOTE OF THE DAY: '' SIMBA HAINA HAJA YA KUJUA KILICHOMO KWENYE MKATABA '' - MH ISMAIL ADEN RAGE.
Hii ni kauli aliyoitoa mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Aden Rage awakati akizungumzia mkataba wa uuzwaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za Ligi kuu ya Tanzania, baina ya kamati ya ligi/TFF na Azam Media
BASKETBALL ALL STARS BONANZA:
BASKETBALL ALL STARS BONANZA:
Kama wasemavyo watoto wa Mjini kuwa Habari YA MUJINI kwa sasa Ni Bonanza la mastar wote wa mpira wa Kikapu Dar es salaam na Tanzania kwa Ujumla.Vijana basketball Club imeandaa bonanza maalumu la mchezo wa Kikapu litakalo shirikisha wachezaji mbali mbali kutoka pande za jiji la Dar es salaam .Bonanza Hilo Litakalofanyika jumamosi hii(August 3) katika viwanja vya LEADERS CLUB KINONDONI ,kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa Kumi na Moja jioni.Litashirikisha Wachezaji wakali (mastar) katika mpira wa kikapu kwa ngazi Tofauti.Kutakuwa na Timu mbili pinzani katika kila Ngazi.Ngazi ya Kwanza Itakuwa ni ya VIJANA WADOGO(watoto) ambao watatengezeza timu mbili zitakazo chuana kuonyesha Hazina ya mpira wa kikapu kwa Miaka ya Baadae.Ngazi ya pili itakuwa ni ya wechazaji wakali(Bora) wa basketball wenye jinsi ya Kike(wanawake),ambao nao watafanya yao mapema kabla ya ngazi ya Tatu ya wakongwe wa Zamani Kuchukua uwanja.Wakongwe hao(VETERANS) nao wataonyeshana Ubavu kukumbushia enzi zao na kuonyesha ramani kwa chipukizi jinsi kikapu cha zamani kilivyokuwa.Katika kile kinachoaminika kusubiriwa na wengi Mjini,ni pale VIJANA waliopevuka,wakali na wanaosifika Tanzania Kwa mchezo wa Kikapu watakapo funga pazia la bonanza hili linalosubiriwa na wengi jijini Dar es salaam.
Bonanza hili litasindikizwa na Burudani Mbali mbali zikiwemo Element za HIP HOP (DJ,DANCING(B-BOY),FREE STYLE),Haitaishia Hapo watakao bahatika kufika watashuhudia burudani kutoka wasanii mbali mbali wa mziki wa Kizazi kipya na stand up comedies wakifanya yao kuongeza Radha.Wakishirikiana na mabingwa wa Burudani Tanzania CLOUDS ENTERTAINMENT watasimamia mpango mzima wa Burudani na mziki mzito eneo la Tukio.
Pia bonanza hili litapambwa na mashindano ya mchezaji mmoja mmoja katika vipengele Tofauti.Kutakuwa na mashindano ya kumtafuta mkali wa Kupiga DUNK,(slam dunk contests),mkali wa 3 points(3 points shoot outs),na mengine mengi ya ziada yatakayo fanywa kama Suprize.
Kiingilio katika Bonanza hili itakuwa ni shilingi elf kumi(10,000) tu kwa wakubwa na elfu tano(5,000) kwa watoto.Burudani na michezo weekend hii ni katika Bonanza la mpira wa Kikapu pale Viwanja vya leaders club.
LIGI KUU YA SIERRA LEONE - VILABU VYAGOMA KUCHEZA MPAKA MSHAMBULIAJI WA SIERRA LEONE ARUDISHWE KUGOMBEA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CHAMA CHA SOKA CHA NCHI HIYO
Ligi kuu ya Sierra Leone imesimamishwa kwa muda usiojulikana kufuatiwa azimio lilosainiwa na vilabu 10 kati ya 14 vinavyoshiriki ligi kuamua kususiwa ligi hiyo jumatatu iliyopita.
Vilabu vilivyosusiwa ligi ni Diamond Stars, Gem Stars, Kambui Eagles, Old Edwardians FC, FC Kallon, Bo Rangers, Ports Authority FC, Mighty Blackpool, Central Parade FC, na Freetown City FC.
Vilabu hivyo vilichukua uamuzi huo katika kupinga kuondolewa kwa Mohamed Kallon na wagombea wengine wa uongozi katika uchaguzi mkuu wa chama cha soka Sierra Leone Football Association (SLFA), ambao utafanyika jijini Freetown siku ya jumamosi.
Meseji iliyotumwa kwenye vyombo vya habari badi inayoendesha ligi ilisomeka: "Katika kuamini usawa na kwa hatma ya mchezo tumeamua kuwasiliana na na mwenyekiti wa kamati ya haki na sheria ya SLFA baada ya kupokea barua iliyosainiwa na vilabu 10 vikielezea uamuzi wao wa kususa kushiriki kwenye ligi.
"Wote - kamati ya ligi na SLFA wameamua kwa haraka kusimamisha ligi inayoendelea mpaka uamuzi mwingine utakapochukuliwa wakati mazungumzo ya utatuzi wa suala ukiendelea."
Mchezaji wa zamani wa Inter Milan na AS Monaco Mohamed Kallon aliondolewa katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi zikitolewa sababu kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo hajakidhi vigezo vya andiko la 32 (4) la katiba ya SLFA.
Andiko hilo linasema: "Wanachama wa kamati kuu wote ni lazima wawe raia wa Sierra Leone na inabidi wawe wameishi Sierra Leone kwa kipindi kisichopungua miaka mitano ili waweze kuwa halali kugombea nafasi ya kuchaguliwa."
Lakini, Kallon alikataa kukubaliana na uamuzi hupo, akisisitiza ni uamuzi wa kisiasa uliopelekea jina lake kukatwa .
Wagombea wengine wawili waliondolewa kwenye uchaguzi wa uraisi ni Rodney Michael na Foday Turay, wote kwa sababu wote wapo kinyume na andiko la 25 za maadili ya FIFA ambalo linadili na uchezaji wa kamari na mambo mengine yanayohusiana na kamari kwenye mchezo wa soka.
Lakini wakati huo huo, Raisi wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ameingilia kati suala hilo na anajaribu kulitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Mashabiki wanaomsapoti Kallon walifanya maandamano ya amani mbele ya ikulu ya nchi siku ya Jumatatu kuelezea kutoridhiswa kwao na uamuzi wa kuondowa wagombea kwenye uchaguzi isivyo sahihi. Mpaka sasa Raisi

Koroma ameshafanya mikutano miwili na viongozi wa SLFA na wagombea walioenguliwa, wakati huo waziri wa michezo wa nchi hiyo kwa pamoja na wagombea, SLFA na FIFA watafanya mkutano wa mwisho wa pamoja siku ya leo.
.
Mpaka sasa kwenye uchaguzi huo amebakia mgombea mmoja tu kwenye nafasi ya uraisi Isha Johansen na kama mambo yataendelea kama yalivyo basi mwanamke huyo atapita bila kupingwa.
SAKATA LA GARETH BALE; TOTTENHAM INAPASWA KUMUUZA BALE ILI KUWA TIMU IMARA ZAIDI
Ikiwa umekaa sana kwenye dunia ya biashara, kuna kundi la maneno mawili lazima uyazoee: "Fedha ni nguvu" na "kila mtu ana bei yake." Barclays Premier League ni biashara kubwa sana, hasa kwa vilabu vikubwa vya juu, mahala ambapo Tottenham inapataka kwa hali na mali - kuwa miongoni mwa vilabu vinne vya juu na kujijengea uhakika wa kucheza champions league kila mwaka. Baada ya msimu miwili kuikosa michuano hiyo kwa pointi chache tu, sasa swali ni namna gani wanaweza kutimiza lengo, na huku Real Madrid wakiripotiwa kumtaka Gareth Bale, Tottenham sasa wanaanza kuona nguvu ya maneno ya "Fedha ni nguvu" na "kila mtu ana bei yake."
Kama taarifa za vyombo vya habari ni zakuaminika, Real Madrid wapo tayari kuvunja rekodi ya muda wote ya uhamisho ili kumpata Bale, kwa kulipa kiasi cha £86 million ($135 million U.S.). Bei hiyo ni zaidi paundi millioni 6 zaidi ya zile alizonunuliwa Cristiano Ronaldo mwaka 2009 akiwa na miaka 24 kama ilivyo kwa Bale sasa.
Kwa vyovyote vila ambavyo Bale alivyokuwa kwenye kiwango kikubwa, na kuwa na msaada mkubwa kwa Spurs kiasi cha kukaribia kuiondoa Arsenal kwenye Top 4, lakini Bale hajafikia kiwango cha Ronaldo wakati akinunuliwa na Madrid, na kwa hakika sio mchezaji mwenye kiwango kikubwa mara tatu zaidi ya wachezaji wengine wa EPL. Kuna ubishi wenye maana umetengenezwa kwamba Luis Suarez ni mchezaji mzuri aliyekamilka kuliko Bale kwa sasa, na bei yake inaweza kuwa kuanzia 30-40 million pounds ikiwa atauzwa kwenda Arsenal akitokea Liverpool.
Hii ni kama kusema kwamba: Hakuna namna ambayo unaweza kusema Gareth Bale ana thamani kubwa kama inavyotajwa, lakini pamoja na yote haya, sioni sababu kwanini Spurs wasimuuze kijana huyu.
Kama Spurs watang'ang'ania kubaki na Bale White Hart Lane utakuwa ni uamuzi ambao umetokana na kujijenga kuwa klabu yenye wachezaji wakubwa - ambapo klabu inayojitutumua kama Tottenham haitaki kupewa jina la 'muuzaji' kwa klabu tajiri. Madrid tayari ilishamnyakua Luka Modric kutoka Spurs msimu uliopita, na inaonekana ndivyo itakavyokuwa siku kadhaa zijazo kwa Gareth Bale.
Katika cheni ya chakula ambayo ndio hatua ya juu ya soka barani ulaya, kama hauli, then unaliwa, na hii ndio hali ilivyo kwa sakata la uhamisho wa Bale baada ya Modric kuchukuliwa kwa Spurs bila wao kupenda kutokana na misuli ya kifedha ya Madrid.
Mashabiki wa Spurs wana haki kuamini wana timu yenye nguvu ya kutosha kuweza kuingia kwenye top 4 ikiwa wataweza kumbakiza Bale. Klabu ilimaliza nafasi ya nne misimu miwili iliyopita (huku Bale akiwa hana kiwango alichokuwa nacho msimu uliopita), lakini walinyimwa nafasi yao ya kushiriki Champions League baada ya Chelsea kushinda ubingwa huo wakati wakiwa wamekosa nafasi kwenye ligi - wakimaliza nafasi ya sita.
Msimu uliopita, Tottenham walimaliza pointi moja nyuma ya mahasimu wao Arsenal. Ukiwaongeza wachezaji wapya Paulinho na Nacer Chadli kwa pamoja Soldado, then kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba Spurs wana timu nzuri kufanikisha ndoto yao wakiendelea kuwa na Bale.
Lakini itakuwa jambo la maana kiuchumi kumbakiza Bale? Sawa, watashika nafasi ya nne kwenye ligi (na labda wataingia kwenye hatuya ya makundi ya Champions League ikiwa watashinda kwenye mechi za awali) then watakuwa wameingiza kiasi cha chini sana £13 million kupitia mapato ya haki za matangazo ya TV na bonasi, na kiwango hico kinaweza kuongezeka kutokea hapo.
Mara ya mwisho Tottenham kucheza Champions League msimu wa 2010-11, klabu iliingiza kiasi cha millioni £27, baada ya kucheza mpaka robo fainali na kutokana na mapato ya haki za matangazo ya TV. Wakati Manchester United ilipofungwa na Barcelona katika fainali msimu huo huo, klabu hiyo ilitengeneza kiasi cha £45million, ukiangalia na kiasi walichoingiza mwaka mmoja kabla waliposhika nafasi ya katika ligi kupitia mapato ya TV ya mechi za Premier League. Hivyo ukifananisha na walichopata kwenye Uefa Champions League unakuja kugundua vilabu vya England vinatengeneza fedha nyingi kwenye EPL kuliko barani ulaya.
Hivyo, kwa misingi ya kibiashara iliyopo, ikiwa Danie Levy (mwenyekiti wa Spurs) na wenzie, wakiweza kumbakiza then wanaweza kucheza Champions League msimu wa 2014-15, na kwa kufanikisha hilo litawasogeza juu kwenye msimamo wa EPL hivyo kuweza kujihakikishia ushiriki wa michuano ya ulaya - hivyo wakiingiza fedha nyingi zaidi za matangazo ya TV na bonasi kutoka kwenye UCL na EPL, kwa jambo hili unaweza kutetea uamuzi wa Spurs kutaka kumbakiza Bale angalau kwa msimu mmoja. Akiepukana na majeruhi, atakuwa kwenye kiwango kilichoimarika zaidi na thamani yake itakuwa juu sana, hata kama Madrid hawatokuwa tayari kulipa fedha nyingi kumsajili. Lakini hili litawezekana ikiwa kama Bale atakuwa sawa kisaikolojia baada ya kufeli kwa uhamisho huu - na kuweza ubora ule ule aliokuwa nao msimu uliopita uwanjani, jambo ambalo ni kama kucheza kamari - ukizingatia mchezaji mwenyewe amesharipotiwa kwamba anataka kuondoka Spurs na ameshamwambia kocha wake kwamba akili ipo Madrid. Huu ni ushahidi tosha mchezaji anaweza akavurugwa kiakili ni jambi hili la usajili kama halitoenda kama nafsi yake inavyotaka.
Ndio, japokuwa kuna uwezekano wa Spurs kufuzu kucheza Champions League, lakini kukataa kiasi cha £85 million ni ujinga ukiangalia na thamani halisi ya mchezaji, tena kama habari za vyombo ni za kuaminika kwenye dili hilo bado Spurs watapewa na Angel Di Maria - utakuwa ni ujinga kukataa ofa ya namna hiyo. Kwenye hiyo Millioni 85 wanaweza wakalipia uhamisho wa Soldado kwa £25m, pia wanaweza wakamsajili mchezaji mwingine mwenye thamani ya £30m na bado wakabikia na chenji ambayo wanaweza wakanunua wachezaji wengine kadhaa kukiongezea uimara kikosi chao.
Chadli ni mchezaji mzuri sana ambaye anaweza akaleta ubora mwingine kwenye kikosi, aliigharimu Spurs £7 million.
Ukiangalia kikosi cha sasa Spurs, hakuna ubishi wa maana unaoweza kuuleta kwa kusema kwamba Di Maria, Soldado, Lennon, na mtu Julian Draxler wa Schalke itakuwa sio timu nzuri kama akiwemo Bale pekee yake.
Watu wengi wanakisia kwamba kuuzwa kwa Bale hivi sasa kutakuwa sawa na Spurs kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi za kucheza Champions League, wakati kuuzwa kwa Bale kutawapa uwezo Spurs kutengeneza timu nzuri zaidi kwa fedha nyingi watakazopata.
Kwa vyovyote itakavyokuwa Spurs hawawezi kupata dili zuri zaidi hili ambalo Madrid wanaripotiwa kutoa, kuendelea kukaa na Bale na kamari, anaweza akaisaidia timu au akashindwa. Fikiria akiumia na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu Spurs watakuwa kwenye hali gani? Maoni yangu ni bora auzwe - ili timu isijengwe kumtegemea yeye tu - auzwe timu ipate fedha nyingi za kuweza kutengeneza kikosi bora na cha ushindani kuliko cha sasa.

Thursday, August 1, 2013
MASHINDANO YA SUPER 8 MWAKA HUU VIPI?
Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah wakibadilishana mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wa mashindano ya mpira wa miguu utakaotambulika kama BancABC SUP8R katika Ukumbi wa TFF Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah (kulia) akisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa BancABC wa mashindano ya SUP8R yanayotarajiwa kuanza rasmi 4Julay2012.Mkataba huo ulifanyika TFF Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni
Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni (kushoto) akisaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa BancABC wa mashindano ya SUP8R yanayotarajiwa kuanza rasmi 4Julay2012.Mkataba huo ulifanyika TFF Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Angetile Hoseah.
Katibu Mkuu wa TFF akizungumza na waandishi wa habari
EXCLUSIVE: UCHAGUZI MKUU WA TFF HATARINI KUFANYIKA TENA - KISA KATIBA IMEKATALIWA NA MSAJILI
Siku ya leo ndio siku ambayo ilitakiwa fomu za kugombea uchaguzi wa mkuu wa TFF zilipaswa ziwe zimeanza kutolewa lakini mpaka sasa hakujawepo na tangazo lolote kutoka TFF kuhusu uchukuaji fomu kwa wagombea watakaopendelea kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
Mtandao huu ulijaribu kufanya uchunguzi kufuatilia nini tatizo nyuma ya uchelewaji huu wa kuanza mchakato wa uchaguzi, tukaja kugundua kwamba tatizo ni kwamba katiba iliyofanyiwa marekebisho na mkutano mkuu wa TFF hivi karibuni imekataliwa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu katiba ya TFF imekataliwa kusajiliwa na msajili kutoka na kutokidhi vigezo vilivyowekwa kwa ajili ya katiba kuwa halali kusajiliwa.
Kisheria ili katiba ipate uhalali wa kusajiliwa na msajili inabidi ufanyike utaratibu wa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na baada ya hapo 2/3 ya wajumbe wapitishe mabadikiko ya katiba hiyo ndipo itakapopata uhalali wa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.
Kingine kilichokwamisha usajili ni kitendo cha TFF kuteua kamati mbali mbali mpya kabla ya katiba kusajiliwa. Sasa waliteua kamati kwa kutumia uhalali wa kamati gani?

BRUNO METSU: KOCHA ALIYEFIKISHA SENEGAL ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA APIGANIA MAISHA YAKE DHIDI YA KANSA
Kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu amekiri kwamba aliwahi kuwaambia wachezaji wake kwamba wacheze mechi kama wanapigania maisha yao - ikiwa ni njia ya kuwahamasisha, lakini sasa kocha huyo mwenye miaka 59 anapigania maisha lakini sio kwenye soka bali ni dhidi ya ugonjwa wa kansa.
Wakati alipoiongoza Senegal kwenye kombe la dunia 2002 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa, wachache wangeweza kutabiri kilichokuja kutokea baadae. Goli la ushindi wa Papa Bouba Diop liliwapa ushindi Sengal dhidi ya mabingwa wa dunia, lakini kocha huyo mwenye nywele ndefu aliiwezesha timu ya Simba wa Teranga kucheza robo fainali ambapo wakaja kutolewa kwa ushindi mwembamba na Uturuki katika dakika za nyongeza.
Miaka 10 baadae Oktoba 2012, baada ya kuanza kuumwa akiwa Dubai na kukimbizwa hosptiali, Metsu aliambiwa alikuwa ameanza kuugua ugonjwa wa kansa ambao ulikuwa unashambulia ini lake na mapafu.
"Ilikuwa ni habari iliyonistua sana. Nilikuwa na Viviane, mke wangu na tulikuwa tunalia tu. Unaanza kufikiria kuhusu watoto wako na kila anayekuzunguka na kukutegemea. Nilianza matibabu ya chemotherapy mara moja na nilipoenda hospitali nilikuwa nipo kwenye kiti cha wagonjwa wasiweza kutembea, nilikuwa mdhaifu sana lakini hakujawahi kutokea muda nikakata tamaa.
"Mara nyingi kama kocha, ni kawaida kuwaambia wachezaji wako 'leo chezeni kama mnapigani maisha yenu'. Lakini sasa na mie nacheza mechi ya maisha yangu. Nilipomuona Eric Abidal na kipindi chake cha TV, nilipata hamasa na nguvu kupigania maisha yangu," alisema Metsu akizungumzia namna alivyohamasisha na Abidal ambaye hivi karibuni alishinda vita yake na ugonjwa ulikuwa uliokuwa unashambulia ini lake.
Metsu aliwahi kucheza soka lakini kwa muda mfupi kabla ya kuamua kuingia kwenye maisha ya ukocha lakini alikuja kupata mafanikio wakati alipoanza kufundisha soka barani Afrika mnamo mwaka 2000 wakati alipoanza kuifundisha Guinea kabla ya kuhamia Senegal. Aliiongoza nchi hiyo kucheza fainali ya kwanza na pekee ya kombe la mataifa huru ya Afrika nchini Mali walipofungwa katika mikwaju ya penati na Cameroon, miezi sita kabla ya kuiongoza nchi hiyo kucheza kombe la dunia enjoyed a modest playing career before an equally unspectacular start to life as a coach until his African adventure began in 2000 when he took over the Guinea helm for two years before moving to Senegal.
Sasa baada ya kushindwa kubeba makombe huko nyuma, sasa Bruno Metsu anataka ushindi wake dhid ya magonjwa ili aweze kupata zwadi ya kuendelea kuishi. Mwenyezi mungu atamsaidia kushinda vita hii. Ameen

Wednesday, July 31, 2013
MCHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU LIGI YA MAREKANI(NBA),STEPHEN CURRY KUENDESHA CLINIC MAALUM YA BASKETBALL TANZANIA KESHO KWENYE VIWANJA VYA DON BOSCO OYSTERBAY
WARDELL STEPHEN "STEPH" CURRY II.
Akiripoti kupitia account yake ya Facebook, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) PHARES MAGESA alisema mkali huyo kutoka timu kali Inayoshiriki Ligi kuu ya kikapu Marekani GOLDEN STATE WARRIORS(GSW), Amekuja nchini Tanzania kupitia mpango wa Malaria wa UN FOUNDATION.
Ukiachana na shughuli hizo za Kijamii za vita Dhidi ya Malaria,CURRY atatumia muda huo kufanya Clinic fupi itakayoshirikisha vijana 100 wakitazania wenye umri kati ya miaka 14-18.Vijana hao ni pamoja na watakaotoka katika mashule na vilabu mbali mbali vya kikapu jijini Dar es salaam. Akitaja mgawanyiko wa vijana watakaoshiriki ni pamoja na MABIBO(5), MONTFORT(5), POLIS(5), STREET WORRIES(5), CHUI(5), CHANG'OMBE(6),OUTSIDERS(5),VIJANA(7), AIRWINGS(5),TUSIIME(8),LORD BADEN(5),DON BOSCO UPANGA(7), JKT MGULANI(5), HEROIS(5), ALI HASSANI MWINYI(5), DON BOSCO OYSTERBAY (11).
Pia clinic hiyo itahudhuliwa na Makocha wa Wazawa akiwemo SAJDA AHMED NA AGNELA SEMWAIKO(SAVIO), JEVERINO PEMBE(MABIBO),KABLOLA SHOMARI(VIJANA), MOHAMMED MBWANA(CHANG'OMBE),WILLIAM MZIRAY (OILERS), na ROBERT MANYERERE (UDSM OUTSIDERS).
Wasimamizi wa shughuli nzima uwanjani watakuwa ni BAHATI MGUNDA(VIJANA) NA EVARIST MAPUNDA(PAZI). Wadau wote wa Basketball wanakaribishwa kuhudhulia clinic hii ili kuweza kujifunza kitu kutoka kwa Stephen Curry.
SAKATA LA YANGA KUPINGA MECHI ZAO KUONYESHWA AZAM TV - WANACHAMA WA KLABU HIYO WAUNGA MKONO UONGOZI
Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo
umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha
kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi
(kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye
luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja.

XAVI: "BALE HANA THAMANI YA MILLIONI 90 - CESC FABREGAS BADO ANA FURAHA CAMP NOU"
GARETH BALE hana thamani ya £90million, hii ni kwa mujibu wa kiungo wa FC Barcelona Xavi.
Kiungo huyo wa Hispania amenukuliwa akisema kwamba bado hajamuangalia vizuri nyota huyo wa Spurs kiasi cha kumfanya kutoa maoni yake kuhusu kutakiwa kwake na Real Madrid.Alisema: “Sidhani kama Bale ana thamani ya fedha hizo zinazotajwa.
“Kiukweli kabisa sijawahi kumuona akicheza dakika 90 zote.”
Xavi pia alisisitiza Cesc Fabregas ana furaha kuwepo ndani ya Barcelona, pamoja na kutakiwa na Manchester United.
Kiungo huyo alisema: “Anaonekana kutulia, ana mkataba hapa. Anajituma mazoezini na anacheza vizuri.
"Kuhusu kuondoka, nadhani ni tetesi tu. Tutaona kitakachotokea lakini kwa sasa anaonekana kutulia na tayari kwa msimu mpya na Barcelona.”
BAADA YA LIONE MESSI - SASA RAISI WA BAYERN MUNICH ASHTAKIWA KUKWEPA KODI
Wiki kadhaa baada ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi kutuhumiwa kukwepa kulipa kodi, sasa raisi wa mabingwa wa ulaya Bayern Munich Uli Hoeness ameshatakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi, mwendesha mashtaka wa Ujerumani amethibitisha.
Imegundulika kwamba mnamo April mwaka huu, Uli, 61, alishindwa kulipa kodi ya kodi akaunti yake iliyopo nchini Switzerland mnamo mwezi January, na sasa imethibitika ameshtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi.
"Mwendesha mashataka wa jiji la Munich II amekamilisha uchunguzi," taarifa rasmi ilisema.
"Mahakama ya makosa ya jinai ya mkoa wa Munich II sasa inasubiriwa kuamua kukubali au kukataa mashtaka hayo."
Msemaji wa klabu ya Bayern Markus Horwick aliiambia SZ kuhusu issue hiyo: "Hatutosema kitu chochote kuhusu suala hili."

MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUCHEZA MECHI NYINGI ZA KIMATAIFA - AHMED HASSAN AGHAIRI KUSTAAFU
Mchezaji mwenye rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kimataifa. Ahmed Hassan, ameamua kutostaafu kwa kuongeza msimu mmoja wa kuichezea klabu ya Misri Zamalek.
Kiungo huyo mwenye miaka 38, ambaye kwa sasa amejiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Misri, atacheza kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika nchini, klabu ya Cairo ilisema kupitia taarifa yake rasmi.
Huu ni msimu wake wa pili akiwa na Zamalek, ambaye alijiunga nayo akitokea kwa mahasimu wao Al Ahly mwaka jana.
Hassan anatambuliwa na shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuwa ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi za kimataifa, akiwa ameiwakilisha Misri mara 184 kuanzia 1995 mpaka 2012.
Hassan, ambaye ana rekodi ya kushinda kombe la mataifa huru ya Afrika mara nne, lakini hajawahi kucheza kwenye michuano ya kombe la dunia, pia aliwahi kucheza soka nje ya nchi katika klabu ya Anderlecht ya Belgium na Besiktas iya Uturuki.

VIDEO: ANGALIA NEYMAR AKIWAOMBA MAKOCHA WA BARCA WAMUINGIZE ACHEZE MECHI YAKE YA KWANZA
Bila kuona aibu kwa camera za TV zilizokuwa zinammulika, mchezaji mpya wa FC Barcelona Neymar alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa Barca akiingia kutoka benchi katika dakika 78 ya mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya kipoland Lechia Gdansk. Aliingia badala ya Alexis
Sanchez katika mchezo ambao ulienda kuisha kwa sare ya 2-2, lakini wakati mchezo huo unaingia kwenye kipindi cha pili mwanzoni, Neymar alionekana akiwa anawaomba makocha wasaidizi wa Barca wampe nafasi aingie atimize ndoto yake ya kuichezea Barcelona.
MAKALA: DILI LA AZAM MEDIA NA LIGI YA TANZANIA - SUPERSPORT NA ASILI YA SOKO LETU.
Wiki iliyopita kamati ya ligi ya VPL na TFF ziliingia mkataba na kampuni ya Azam Media Group kwa kuwauzia haki za matangazo ya Television kwa ajili ya kuonyesha ligi kuu ya Tanzania bara.
Pia zilitoka ripoti kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari kwamba kampuni nyingine kutoka nje ya Supersport ilionyesha kuvutiwa na dili hilo lakini ikashindwa na Azam Media ambao walitoa ofa kubwa zaidi. Hii ni habari ngumu kuiamini kwa kuzingatia hakuna mtu yoyote anahusika aliyethibitisha kama kweli SuperSport walitoa ofa rasmi ambayo ilizidiwa na wapinzani wao.
Tena ukiangalia uzoefu na ubavu wao wa kifedha na teknolojia katika uonyeshwaji wa michezo kwenye upande wa kusini mwa jangwa la Sahara, ni vigumu kuamini wangeweza kushindwa kirahisi kama kweli walikuwa wanahitaji kwa nia ya dhati kuonyesha ligi ya Tanzania. ukiliangalia Hili kwa mtazamo wa kibiashara zaidi utagundua kuwa kwenye nchi za Kenya na Uganda wana watumiaji wengi wa DSTV, Kenya wakiwa na asilimia 44 na Uganda 28, ukilinganisha na asilimia 12 ya Tanzania.
Kwa maana hiyo Tanzania imekuwa na wateja wachache wa huduma za DSTV, na wengi wao wanatumia kwa kuangalia mchezo wa soka, tofauti na nchi za Uganda na Kenya.
Kenya na Uganda wote wanashiriki kwenye michezo tofauti, rugby na riadha ambayo yote inaonyeshwa. Tanzania mchezo wetu mkuu ni soka, na michezo mengine hata kama ipo lakini haina dili kubwa kwenye masuala ya kuuza haki za matangazo ya TV. DSTV kama wangeamua kuja kuonyesha soka hapa Tanzania, basi uwekezaji wao mkubwa wa vifaa ungewagharimu zaidi ikizingatiwa ni soka tu ambalo wangeonyesha kwa maana kipindi kingine wakati ligi imesimama mitambo yao isingekuwa inatengeneza fedha za ziada - tofauti na nchi za Uganda na Kenya ambao muda wote inakuwa inafanya kazi kutoka na wingi wa michezo tofauti inayoonyeshwa kutoka kwenye nchi hizo.
Azam Media wanaweza kuwa wametoa ofa nzuri ya kifedha lakini kama Supersport wangetaka kweli kuonyesha umwamba wao wa kiuchumi, basi ingekuwa vita nzuri ya kibiashara - ambayo ingeviacha vilabu vyetu vikienda benki huku vinatabasamu.
Wakati GTV ilipotaka kuchukua haki za matangazo ya Kenya Premier league, SuperSport waligundua walikuwa wanapoteza kitu kikubwa sana kibiashara. GTV tayari walikuwa wameshakamata haki za matangazo ya ligi za Uganda na Tanzania na walikuwa wakitaka kumalizia na Kenya. Hivyo Supersport wakalazimika kuja na ofa nzuri zaidi na mwishowe wakafanikiwa kushinda tenda ya haki za matangazo za KPL. Hivyo ndivyo ushindani wa kibiashara ulivyo.
Ingekuwa SuperSport wanataka kweli na kuona kuna fursa ya kibiashara kuja kuwekeza kwenye ligi ya Tanzania basi wangeweza kutoa ofa nzuri zaidi waliyotoa Azam Media Limited. Lakini pia, kamati ya ligi ingeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangetangaza tenda ambayo ingevutia media tofauti kuja kushindana kwa kutoa ofa tofauti.
Ni vigumu kupata dili zuri zaidi ya walilitoa Azam Media limited ukiangalia na asili ya soko letu. Ambalo ni dogo na limejitenga kiasi kuwa na uwezo mdogo wa kuvutia Media kubwa kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza kama ambavyo Azam wameweza.
Pia kama taratibu zote zingefuatwa, labda klabu zetu zingeweza kupata fedha nyingi zaidi kutokana na ushindani wa makampuni ambao ungekuwepo kugombea tenda hiyo. Lakini katikati ya maneno maneno yaliyojitokeza katika dili hili - tusisahau kwamba Azam wametoa nafasi kwenye mkataba kwa media nyingine kushirikiana nayo.
Azam kwa kutokuwa wabinafsi inasemekana waliamua kisiwepo kipengele ambacho kingefunga njia kwa wawekazaji wengine ambao wangetaka kushirikiana nao. Kwa mfano Zuku , StarTimes au SuperSport kirahisi tu wanaweza kushirikiana kibiashara na Azam katika kurusha matangazo hayo ya mechi za ligi kuu. Kwa kifupi, Azam TV hawajabana milango kwa wengine kwa maana ya 'exclusive rights', kuna nafasi kubwa ya Media nyingine zitakazojisikia kushirikiana nao kwa makubalianao watakayokubaliana.
Japokuwa dili bado dogo kwa baadhi ya vilabu vyenye bajeti kubwa, lakini bado ni tamu kwa vilabu vyenye bajeti ndogo japokuwa ni vigumu kuacha kuyasemea makosa yaliyofanywa na kamati ya ligi pamoja na TFF ya kutaka kulazimisha kusainisha mkataba na Azam Media.
Story hii imeandikwa na ALLEN MICHAEL wa lonestrikertz.blogspot.com
BAADA YA KUSHINDWA KUNG'ARA REAL MADRID NA VALENCIA - FERNANDO GAGO ARUDI KWAO ARGENTINA
Kiungo wa kiargentina Fernando Gago
amekamilisha usajili wake wa kurudi kwenye klabu ya nyumbani kwao ya Boca Juniors akitokea Valencia baada ya kufaulu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitatu juzi jumatatu.
Gago tayari alishacheza kwa miezi Boca akitokea Valencia lakini Boca waliamua kumrudisha moja kwa moja kiungo huyo ambaye alianza kucheza soka la ushindani mnamo mwaka 2004 akiwa na klabu hiyo.
Gago alijiunga na Real Madrid mnamo mwaka 2007 na kusiadia klabu hiyo kushinda ubingwa wa La Liga mara mbili kabla ya kuhamia Valencia msimu uliopita akitokea AS Roma alipopelekwa kwa mkopo na Madrid baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
KALI YA LEO: JOSE MOURINHO AJICHORA TATTOO YA JINA LA MKE WAKE MKONONI MWAKE
Boss wa CHELSEA Jose Mourinho amefanya kitendo ambacho sio watu wengi wenye umri wake wanaweza kufanya - mreno huyo amechora tattoo yenye la mkewe kwenye mkono wake.
Mourinho, mwenye miaka 50, alijichora tattoo hiyo baada ya kurejea na timu yake kutoka mashariki ya mbali. Alilipa kiasi cha £80 ili kuchora jina la mkewe 'Matilde Faria' baada ya kuvutiwa na michoro aliyoiona kwa mmoja wa wafanyakazi wa klabu ya Chelsea.Kocha huyo mwenye majivuno alitumia saa nzima kutulia na kuchorwa tattoo hiyo ambayo ndio ya kwanza kwa mchoraji anayefanya shughuli zake karibu na uwanja wa Chelsea uliopo magharibi mwa London.
Mtu aliyemshuhudia kocha alikaririwa akisema kwamba: “Jose alionekana mtu mwenye furaha baada ya kuchora tattoo hiyo.”
Subscribe to:
Posts (Atom)