Siku ya leo ndio siku ambayo ilitakiwa fomu za kugombea uchaguzi wa mkuu wa TFF zilipaswa ziwe zimeanza kutolewa lakini mpaka sasa hakujawepo na tangazo lolote kutoka TFF kuhusu uchukuaji fomu kwa wagombea watakaopendelea kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
Mtandao huu ulijaribu kufanya uchunguzi kufuatilia nini tatizo nyuma ya uchelewaji huu wa kuanza mchakato wa uchaguzi, tukaja kugundua kwamba tatizo ni kwamba katiba iliyofanyiwa marekebisho na mkutano mkuu wa TFF hivi karibuni imekataliwa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu katiba ya TFF imekataliwa kusajiliwa na msajili kutoka na kutokidhi vigezo vilivyowekwa kwa ajili ya katiba kuwa halali kusajiliwa.
Kisheria ili katiba ipate uhalali wa kusajiliwa na msajili inabidi ufanyike utaratibu wa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na baada ya hapo 2/3 ya wajumbe wapitishe mabadikiko ya katiba hiyo ndipo itakapopata uhalali wa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.
Kingine kilichokwamisha usajili ni kitendo cha TFF kuteua kamati mbali mbali mpya kabla ya katiba kusajiliwa. Sasa waliteua kamati kwa kutumia uhalali wa kamati gani?
tayari gogoro lishaingia bora tufungiwe tukae na kujipanga upya timu yenyewe majanga kila kitu mashaka
ReplyDeleteKwa kweli ngoja leo niseme jambo hakuna kitu kinanikera kama uongozi wa TFF,sijawahi kuona wala ksikia hata siku 1 hao jamaa wakifanya jambo likaeleweka kila siku utasikia kwa mujibu wa sheria wameona sheria ni ngao yao ya kfanya maovu kwenye Soccer letu,tusidanganyane now tunaona Soccer linachezwa na watz sasa wao wapo pale kwa manufaa zaid sio kupandisha kiwango cha Soccer la Taifa letu inaniuma saaana kuona mtu kama Tenga nae anayumba yumba kwenywe Soccer while amecheza sasa leo kioa siku ubabaishaji tuu
ReplyDeleteMwalubadu Oslo
Mdau
ukweli ulo wazi tff ni wababajshaji ni kitengo maalum cha watu kuja nakuneemesha matumbo yao na si kwa faida ya soka la tanzania na kama ni laana basi itakuwa laana ya mzee almaamriy maana tangu yeye kuondoka hapana lolote japo kuwa hata nae hakuweza kukidhi haja ya matakwa ya watanzania lakini kulikuwa na uhai wa chama tafauti na sasa.fat ilijiendssha yenyewe bila wadhamini lakini mabus ya fat tuliyaona na yakitumika kuwahudumia wadau wa soka lakini tangu watu wenye kujua fitina wakamtoa mpaka leo hakuna lolote.na wamepita wengi hapana lolote zaidi yaufujaji wa mali na soka letu kurudi nyuma siku hadi siku watanzania hatuwezi kwenda mbele kama hatubadiliki na mabadiliko yaanze kwenye vilabu yainhie tff na tuwe na viongozi wa maendeleo na si viongozi wa maslaji yao
ReplyDeleteNakumbuka rais aliepo madarakani alijijengea jina zuri wakati ule akiwa katibu mkuu wa kamati ya muda ya FAT akaonekana ni kiongozi wa mfano katika soka la bongo sasa sijui tatizo na wasaidizi wake au ni nini maana badala ya kuokoka tunazidi kudidimizwa sijui tufanyeje
ReplyDeleteTff wanajua walifanyalo, muda wao umekwisha lakini hawataki kuondoka ndiyo mana tenga Anabariki ubabaishaji ili waendelee kuwepo! Na kwakua wizara imezoea kuwabeba hata hili mwisho wa siku watalifumbia macho, mwanzo waliidanganya wizara kuwa wamefanya mkutano wakati hawakufanya, wizara ikajifanya kupiga mikwara mbuzi mwisho hakuna kilichoendelea yakaisha, kwanini wasirudie tena uozo wao?
ReplyDeleteKwa kawaida kibaka akijua nyumba ina mbwa koko wala haingii pressure, atakata tu nyavu za madirisha aibe cm.