Arsene Wenger amefanikiwa kuiwezesha timu yake kupata nafasi ya kushiriki klabu ya ulaya msimu huu.
Sasa ufuatao ni muda muafaka ambao utaamua hatma ya Gunners msimu huu na nini wat-achive kwa msimu wote wa 2011-2012.
Akifanyiwa mahojiano ya TV baada ya ushindi dhidi ya Udinese, nahodha mpya wa Arsenal aliweka wazi kuwa anataka timu yake kufungua akaunti na kuleta wachezaji wa ukweli kuimarisha kikosi kabla halijafungwa dirisha la usajili.
Ni usajili mzuri pekee utakaotoa taswira ya Gunners msimu huu whether itagombea nafasi ya nne kwenye ligi au itagombea makombe makubwa yakiwemo Premier league.
Gunners walikuwa na bajeti ya kutosha hata kabla ya kuuzwa Cesc Fabregas na Samir Nasri, ushamisho ambao umeleta zaidi ya £60m kwenye akaunti ya klabu hiyo huku wakitarajiwa kuzidi kutunisha mfuko kwa mapato makubwa ya kushiriki Champions League.
Hivyo, Arsene Wenger hana tena visingizio.Wengi wa mashabiki wa Gunners bado wanataka kuona mzee Wenger anaijenga upya Arsenal na kufanikiwa, lakini inabidi awashawishi kwamba mataji makubwa yapo njiani.
Sio tu mashabiki, pia itawashawishi watu kama Van Persie na Bacary Sagna kwamba Arsenal bado shauku na hamu ya mafanikio kwa kutaka kunyakua makombe.Hivi ndivyo Wenger anavyohitaji na atapata line up na kikosi kitakuwa imara zaidi ifikapo September 1.
Wachezaji wote hapa chini wamekuwa katika rada ya Arsenal na wengine Wenger ameshajaribu kutuma ofa though hajafanikiwa bado, ama kwa hakika wataibadilisha Gunners.
1: YANN M’VILA – (£22m)
Wenger amaeshatuma ofa mbili kwa ajili ya kiungo huyu wa Rennes, na bid mpya ya Arsenal ya £20m inaonyesha wapo serious na biashara hii.
M’Vila ambaye ni mfaransa ana nguvu, ufundi na uwezo mkubwa wa kuweza kucheza kama kiungo mkabaji mbele ya mabeki, kitu ambacho kitampa Wenger option ya kumruhusu Jack Wilshare asogee mbele.
Wilshare anaweza kuwa ndio future ya timu ya taifa ya England katika eneo la kiungo, pia ana uwezo na nafasi ya hata kuja kumzidi Cesc Fabregas.M’Vila anabakia ndio chaguo sahihi kwa upande wa kiungo cha Arsenal – ikiwa Rennes watakubali kumuuza.
EDEN HAZARD (£25M)
Wenger amekuwa akimfuatilia mshambuliaji huyu wa klabu ya Lille raia wa Ubelgiji kwa zaidi ya miaka miwili.Hazard ni mchezaji ambaye ni versatile yaani ana machaguo mengi ya kucheza dimbani, ni mchezaji anayewindwa na almost vilabu vikubwa vyote na kama Arsenal wakimpata atawasaidia sana.
Lille wanatambua kwamba Arsenal wanamuhitaji Hazard, lakini hawataki kumuuza ingawa inawezekana kufanyika biashara kwa kiasi ambacho hakitokuwa chini ya £25m.
Arsenal tayari walishajaribu kumsajili, lakini waligonga ukuta ingawa bado wanaweza kutuma ofa nzuri ambayo itakuwa ngumu kwa mchezaji na klabu kukataa.Mchezaji mwezie wa Lille, Gervinho tayari ameshaanza kuilipa fadhila Gunners.
3: PHIL JAGIELKA NA LEIGHTON BAINES (£30M)
Gary Cahill ni mdogo zaidi na mzuri kuliko Jagielka lakini Wenger anamtaka Jagielka na Arsenal hawataki kulipa £17m kwa ajili ya mchezaji huyo wa Bolton.
Jagielka anapapenda sana Goodson Park na amezoeana na wachezaji wenzake, hivyo kumfanya acheze vizuri itabidi Leighton Baines nae ajiunge na Gunners.
Arsenal pia wamekuwa wakimfuatilia sana Baines tangu msimu uliopita na sasa wakiwa na beki wa kushoto ambaye anaandamwa na majeruhi akiwa bado mchanga Kieran Gibbs, wanahitaji guality player kama Baines kuisadia ngome dhaifu ya timu yao.
Hii ndio dream timu ya Arsenal ambayo inaweza kuwashawishi na kuwafanya mashabiki kurudisha imani iliyoanza kupotea kwa timu yao.
Pia usajili wa wachezaji hawa utakuwa upo katika mipaka ya matumzi ya Arsenal baada ya kupata fedha walizowauzia Fabregas na Nasri zinzofikia £60m, za Gael Clichy £7m na zile ambazo Wenger alipewa kwa ajili ya usajili msimu £35m bila kusahau mapato yanayofikia £25m kwenye Champions League.