Kocha
wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young
Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza
kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla
ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa
Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa
Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.
Amesema
timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya
Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na
wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia
Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
“Timu
hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa
vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia
uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu
hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo
wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali
Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa
Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail
Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed
Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily
Mgeta (Simba).
Viungo
ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya
(Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga
(Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba),
Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa
Sugar).
Washambuliaji
ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro
Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam)
na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).
AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT
Ruvu.
Mechi
hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya
usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi
hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari
Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.